Zifahamu tiba ya muwasho Sehemu za siri

Wanaume wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri :-
– Kuosha vizuri uume, na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
– Ziweke sehemu zako za siri kutia ndani makalio katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi. Matumizi ya poda ya Cornstarch yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali.
– Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani (chupi) angalau kila siku.
– Vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya kiujumla.
Wanawake wanapaswa kufuata hatua zifuatazo ili kusaidia kuepuka kuwashwa sehemu za siri:-
– Baada ya kukojoa au kujisaidia, osha sehemu zako za siri kuanzia mbele(ukeni) kwenda nyuma(matakoni) ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.