MY STORY | MKE WANGU NA MMUDU MWENYEWE NDIYO MAANA NILIMUOA! | BongoLife

MY STORY | MKE WANGU NA MMUDU MWENYEWE NDIYO MAANA NILIMUOA!

MKE WANGU NA MMUDU

Ghafla mke wangu alikua hana amani, kila nikirudi nyumbani anakua kachoka, anakua kugugumia maumivu lakini hasemi. Ndiyo kwanza alikua ametoka kujifungua mtoto wetu wa kwanza, tena kwa kisu, binti wa kazi alikua kaondoka kama wiki moja kabla. Madai yake ni kwamba Mama yake alikua anaumwa, kwakua nilikua naishi na dada yangu, mtoto wake pamoja na mdogo wangu wa kike basi niliona hakuna shida, watamsaidia wifi yao.
Lakini wiki baada ya biti wa kazi kuondoka mke wangu alikua kama kituko, kachoka, mgongo unauma, ndani ukiingia kuchafu kuchafu, chakula kinapikwa ili mradi tu. Nilimuangalia na kusema hapana, huyu si mke wangu, kuna nini? Siku moja nilirudi nyumbani mapema, nilimkuta mke wangu yuko jikoni anasonga ugali, anasonga ugalli huku kampakata mtoto mchanga wa miezi miwili, mtoto analia lakini mke wangu anahangaika peke yake.
Kwa kawaida kutokana na kazi zangu narudi nyumbani saa tatu sa anne, inajulikana hivyo kwakua mimi ni msimamizi hivyo lazima mahesabu yakae sawa, ila siku hiyo nilirudi saa moja jioni, Derava alinishusha nnje, sikumbua mtu nikaingia ndani na kumkuta mke wangu katika hali hiyo. Nilimuuliza kwa hasira huku nikimchukua mwanangu ni wkanini anapika na mtoto wakati hatakiwi hata kunyanyuka na kufanya chochote.
“Yaani umejifungua kw aupasuaji, una mshono unahangaika na magali, unampikia nani ugali unajisahau wewe na mtoto….” Nilimfokea, lakini kama kawada aliniambia kaamua ili asikae sana,a lilala sana. Wakati nimemshika mtoto ndiyo dada yangu, mtu mzima tu alikuja na kutaka kumchukua, akajifanya hakumsikia mtoto akilia, nilimuuliza ni kwanini wifi yao anapika wakati wao wapo, hawajui kuwa katoka kujifungua kwa upasuaji,a liniambia kuwa yeye ndiyo kang’ang’ania.
“Alitaka kukupikia kwakau unapenda ugali wake!” nilimuangalia dada yangu na kutamani ni mtandike makofi, mke wangu hawezi kusema upuuzi huo, kwanza anajua kuwa mimi sipendi ugali, yaani ni kama mfungwa na gereza si upendi, yeye hapendi sasa anampikia nani kama si wao. Lakini nilijizuia, niliacha mambo yapite, usiku nilimuuliza mke wangu kuna tatizo gani,a kanyamaza, hakunaimbia kitu, akaniambia tuyaache lakini aakaniomba nimtafutie mfanyakazi.
Nilijua kuna kitu, na kwakua najua mambo ya ndugu, ukizingatia mimi kwetu ndiyo mwenye pesa nilijua washaanza kuniharibia ndoa yangu. Nilimuangalia mke wangu na kuwaza “Hivu mke wangua livyo mtamu hivi wanataka kuniharibia, yaani mtoto mwenyewe wa wkanza, hata sijamfaidi, washaanza kulete kisirani, ndugu wenyewe nimewachukua kwa muda kwani mimi si mtu wa kukaa na ndugu, sio kwamba si wapendi ila najua ndoa haina utamu, hawa watu hawanijui.
Nilinyamaza, sikusema chochote, asubuhi nilimpigia yule binti wa kazi kumuulizia hali ya nyumbani kwao na kuwa anarudi lini. Alinipa ahadi ahadi nikajua anadanganya, nikamaua kumbana miwsho akanaiambia ukweli kuwa harudi kwani Dada zangu ndiyo wamemuambia aondoke ili kumkomoa mke wangu, kwamba wanataka ateseka na mtoto kwani kazi zote anafanya yeye, alinaimbia wanamtumia mpaka msahara mara mbili ya niliokua nampa ili tu abaki kulekule na yeye asirudi tena.
Baada ya kumsikiliza nilimuambia kwa heri, huyo binti nilimchukulia kama mwanangu, mke wangu alikua anampenda anampa kila kitu na mwisho kaamua kuungana na ndugu zangu kumyanyasa mke wangu, nilimuambia kwa heri na asitegemee pesa nyingine kwani ndugu wote wananitegemea mimi na muda si muda wataanza kuisoma namba. Siku hiyo niliamua kurudi mchana, nilimkuta mke wangu kainana amapiga deki, Mdogo wangu alikua katoka na Dada yangu alikua chumbani Kalala, nilimchukua mke wangu mpaka chumbani, nikamuambia kuwa siwezi lazimisha ndugu zangu kumhudumia kwani yeye ni mke wangu na ahwahusu ila siwezi kumuona Mama wa mtoto wangu anateseka wakati nipo. Nilimuambia kuwa kazi yake ni kupumzika kwajaili ya mtoto wetu.
“Umehangaika miezi tisa nishindwa kukuhudumia, nilivua nguo za kazini, nikainama na kuanza kupiga deki mwenyewe, wakati nafanya hivyo Dada yangu alitoka, alikua anaulizia chakula, hakujua kama nimerudi, aliona aibu kuona kuwa nimeinama napiga deki, alitaka kunisaidia nikamuambia hapana, hapa ni kwangu sitaki yeye kugusa chochote kila kitu nitafanya mimi.
Nilimalzia kudeki, nikaingia jikoni na kupika chakula cha mchana, nikaenda chumbani nikamuita Dada yangu na kumuambia ni muda wa kula. Yaani huwezi amini alishindwa hata kutoka chumbani, alikua anatetemeka kwa uoga, nikala mimi na mke wangu, nikatenga chakula mezani kisha nikamuambia Dada yangu kuwa sitaki mtu aguse kitu changu tena, wao wamakuja kwangu kula na kulala basi kila kitu nitafanya mimi na mke wangu. Jioni saa kumi na mbili nilikua nyumbani, nilimuachia ofisi mtu, basi nikarudi nyumbani, mke wangu nilimuambia asiotoke nnje na wala asifanye chochote.
Nilikuta mdogo wangu na Dada yangu wapo jikoni, niliwaambia warudi chumbani kama kawaida yao mimi nitapika, kwanza wlaijua kama ni utani, lakini niliwakazia macho nikaingia jikoni nikapiga, yes, mimi nafanya kila kitu nyumbani, mke wangu wakati wa ujauzito ulimsumbua sana, binti wa kazi alikua anaumwa nilikua naamka nafanya kila kitu, ndani, kupika na kila kitu najua, nafanya mwenyewe hivyo haikua shida, nilipika chakula cha usiku nikawaita kula, waligoma ila niliwalazimisha, tukakaa mezani na kula wote.
Nilipomaliza walipotaka kuondoa vyombo nilikataa, nikachukua vyombo vyangu nakwenda kuosha mwenyewe. Asubuhi niliamka na kufanya usafi nyumba nzima, kisha niakenda kazini. Kwenye sa atano hivi Mama yangua linipigia simu, alianza kuwaka kuniambia ni kwanini nawanyanyasa ndugu zangu, sijui nafanya kila kitu mwenyewe, akaanza mambo ya sijui mke wako akakukalia, mke wako sijuia nakuambia uongo, aliongea mambo mengi sana mimi namsikiliza tu. Mwisho nikamuambia Mama aongee na watoto wake vizuri, awaambie kuwa wana machaguo mawili, wamuambie ukweli au mimi nikirudi nitawafanyia kweli, sikutaka kujibishana na Mama yangu, nilikata simu.
Baada ya kukata simu Mama alinipigia tena, niliacha kupokea, akatuma meseji nyingi za kunilaumu, nikaamua kumpigia Mama na kumuambia.
“Ongea na watoto wako, ni wanao, mimi wao kukaa wkangu ni hisani, ni wanao, ni jukumu lako kuwasaidia, mimi jukumu langu ni kwa Mwanangu, sasa kama hawawezi kuishi vizuri na Mama wa mtoto wangu basi wanatakiwa kwenda kwa Mama yao!” nilimaliza nikakata simu na kuizima kabisa, nilirudi nyumbani mchana na kukuta dada zangu eti wamekusanya vitu vyao, wana hasira wanataka kuondoka, niliwauliza sbabau wakaniambia kuwa mke wangu hawataki hivyo hawawezi kuendelea kushi kwangu.
Niliwaangalia nikajikuta nacheka, nilimuita mke wangu, nakumbuka tulikua tumekaa sebuleni, wakati namuita walianza kuonge amammbo mabaya kuhusu mke wangu, kuwa ana wanayanaysa, sijui hawataki, ananiloga, mke wangu alikuja na kuniambia kuwa yeye hataki ugomvi wasameheane warudi. Nilimuangalia mke wangu nikajikuta nawaza hivi nimefanya nini kupata mke mzuri namna hiyo.
“Sikukuita kwajaili ya kuongea, nimekuita kwakua ndugu zangu wanaondoka, sas anataka ukague mabegi yao kuona kama hawajaiba kitu.” Kila mtu alishangaa, dada zangu walidhani ni utani na mke wangu aligoma kufanya hivyo.
Mimi nilianza kufungua mabegi ya dada zangu, niliangalia kila kitu, kila nguo na muonyesha Mke wangu kumuuliza kama ni yake, nilikua nafanya hivyo kwa hasira ili kuwaonyesha ndugu zangu kuwa sitishiki lakini huwezi amini, wkaati nakagua nilikuta kwenye bagi wana chupi tatu za mke wangu tena zilizotumika, niliwauliza kwanini wana chupi za mke wangu wakaanza kujifanya kuwa labda walichukua vibaya kwenye kamba wakasahau, kamba gani wakati mke wangu chupi zake haaniki nnje, anaandika bafuni, walibaki kimya.
Niliingia mfukoni, nikatoa nauli, nikaita Bajaji, ikaja kuwachukua, hawkauamini, mpaka wanafika nyumbani Morogoro walikua hawaamini, mimi hata sikujali, nilimuambie mke wangu hatuna mfanyakazi ila nitafanya kila kitu mpaka nimpate ila sitaki kuishi tena na ndugu, kama ni kuwasaidia nitawasaidia huko huko walipo. Walipofika Mama alinipigai simu,a kilalamika kuwa nimewaita ndugu zangu wachawi wkasababu ya Mke wangu, nilizidi kumsisitiza kuwa awaambie waongee ukweli sla sivyo wataona rangi yangu.
Hawakuongea, waliendelea kunilaumu na kumchukia mke wangu, ila baada ya kuona kuwa nina msimamo walifuata mke wangu, wakamuomba awasaidie kuaomba msamaha niliwaambia nilishawasamehe, nikarudisha huduma ila niliwambia kwangu nitaishi na mke wangu tu na binti wa kazi ambaye akinishinda nafukuza, Mama yangu akitaka aje wakati wowote kisirani chake nakiweza ila ndugu nitawasaidia kwa chochote ila kwa mbali, sihitaji kuwa na mke ambaye ana stress za watu amabo nao ipo siku watakua na familia zao.
MWISHO

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MY STORY | MKE WANGU NA MMUDU MWENYEWE NDIYO MAANA NILIMUOA!
MY STORY | MKE WANGU NA MMUDU MWENYEWE NDIYO MAANA NILIMUOA!
https://1.bp.blogspot.com/-zPQX7ijrOjU/XqbB56KLUcI/AAAAAAAADRc/_7Y9sa3_Txkv_OQsnNlchtqvDMyxaG4eQCLcBGAsYHQ/s400/MKE%2BWANGU%2BNAMMUDU.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-zPQX7ijrOjU/XqbB56KLUcI/AAAAAAAADRc/_7Y9sa3_Txkv_OQsnNlchtqvDMyxaG4eQCLcBGAsYHQ/s72-c/MKE%2BWANGU%2BNAMMUDU.jpg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2020/04/my-story-mke-wangu-na-mmudu-mwenyewe.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2020/04/my-story-mke-wangu-na-mmudu-mwenyewe.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content