NILIOA NYOKA | BongoLife

NILIOA NYOKA

Simulizi:NILIOA NYOKA.

MTUNZI: Samwel Emmanuel.
Contact:0745165106.
Madhari :Dar es salaam.

NILIOA NYOKA SEHEMU YA KWANZA (01).

Kila nikikaa na kuanza kuyatafakari mapito magumu niliyowahi kuyapitia katika maisha yangu huwa naishia kulia tu na kumshukuru Mungu kwa kunivusha salama maana hii dunia kama jambo bado halijakupata unaweza kudhani ni maigizo au mzaha,lakini huo ndo ukweli.Wahenga wanasema ni kheri ukosee kununua nguo kama suruali au sketi kuliko kukosea kuoa au kuolewa maana majuto utakayoyapata yatakuwa na maumivu yasiyoelezeka.Pesa si kitu endapo utaoa au kuolewa na mtu kicheche kwani utatamani kufa lakini haitowezekana.Nimejitokeza mbele yenu nikiwa na makala yangu hii ya kusisimua,simulizi inayoyahusu maisha yangu miaka kumi na tano iliyopita.Ni makala ya kutisha kidogo lakini iliyosheheni mafunzo mengi katika maisha yako hasa kwa vijana ambao wanajiandaa kuoa ama kuolewa.Kabla hujaoa au kuolewa nipende kukushauli neno moja tu ,mshirikishe Mungu katika hili kwani ukidhubutu kukurupuka tu basi utajuta maishani.Mimi nilikurupuka ila baadae ndo nikaja kujua kumbe si kila king'aacho ni dhahabu zingine ni nyembe . Tafadhari ifuatilie simulizi hii yenye sehemu ishirini na tano kwa makini ili ujifunze.ASANTE.
*********************************
Mwaka 2004 nikiwa kijijini kwetu Isagang'wale Simiyu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu nilianza kujishughulisha na kazi mbali mbali ikiwemo kilimo na biashara za hapa na pale.Kazi kama kulima mpunga,pamba ndizo zilinivutia zaidi kiasi kwamba nguvu zote nikawa nazimalizia huko kila iitwapo leo .Sasa baada ya kufanya kazi hizo kwa muda wa miezi kadhaa na kuona nimekipata nilichokuwa nikikitafuta niliamua kufunga safari kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kufungua biashara zangu huko.Hapa unaweza kujiuliza ni kwa nini niliamua kuelekea Dar es salaam na si kwingineko,jibu ni fupi tu,moyo wangu uliridhia maana Mimi nilikuwa na desturi ya kuyaheshimu maamuzi ya roho yangu kuliko kitu chochote kile.Nakumbuka wakati Safari yangu ya kuelekea huko inawadia sikuwaaga wazazi kwamba nina mpango wa kwenda Dar kwani pale kijijini kwetu kulikuwa na mambo ya ovyo sana yanayohusiana na ushirikina,ukiaga tu na ukawa umejichanganya kuisema hadi siku ya wewe kuondoka jua maisha yako yapo hatarini.Siyo kwamba nilipanga kutoroka lahasha,mpango wangu ulikuwa ni hivi,nilipanga endapo nitafika jijini Dar es salaam basi nitawapigia simu mama na baba na kuwataarifu moja kwa moja kwamba wasihangaike kunitafuta nipo Dar nahangaikia maisha.Nakumbuka yalikuwa ni majira ya asubuhi sana kama kwenye saa kumi kasoro hivi siku ya juma mosi niliamka nikajiandaa haraka haraka ili niondoke bila kupoteza muda,hilo wala halikushindikana maana nilikuwa nikilala kwenye gheto langu la nje mbali kidogo na wazazi wangu.Basi nikawa nimeamka maandalizi nikayafanya hatimaye yakawa yamemalizika.Ni
lichukua begi langu dogo nikalivaa na jingine kubwa nikalibeba kwenye mkono wa kulia,safari ya kuelekea stendi ya mabasi ikaanza.Nilimpigia simu rafiki yangu mmoja mwedesha bodaboda akaja na kunichukua kuniwahisha stendi kwani pale kijijini kwetu hakukuwa na stendi yoyote ile,na kutoka hapo kwenda kwenye ile stendi ya mabasi,umbali wake ulikuwa ni kama kilomita tatu na nusu hivi.Basi jamaa akanichukua akawa ameniwahisha huko na kunifikisha salama saliminii inshallah kama ndugu zangu waislam wanavyoshukuru au kutakiana jema katika jambo furani.Sasa wakati ananifikisha huko,nilimuona kama ana jambo la kuniuliza maana macho yake yaliashiria hivyo japo hakuniuliza.
"Luka ngoja Mimi niwahi nyumbani kwani kuna jamaa zangu watano niliwaalika jana kwa ajili ya kunisaidia kwenye zoezi la mavuno ya pamba,wasije wakafika na kukuta sipo,ngoja niwahi,aisee tutawasiliana".Alisema jamaa angu huyo kisha akaiwasha pikipiki yake na kujiandaa ili aondoke.
"Sawa,mimi nawahi Bariadi tu hapa,kesho ama kesho kutwa nitarudi,nyumbani wakikuuliza waambie mimi nipo nimetoka kidogo kuangalia upepo wa biashara zangu".Nilisema ,nae akaitikia kwa ishara ya kutikisa kichwa akawa ameondoka.Kwa bahati nzuri tiketi tayari nilikuwa nimeshakata,nilikata jana yake kimya kimya kabla ya safari maana Mabasi ya kwenda jijini humo kwa kipindi hicho yalikuwa ni machache sana hivyo kuwahi kukata tiketi lilikuwa ni suruhisho.Basi nikasogea kwenye gogo moja nikakaa hapo ili nilisubiri Basi langu lifike nipande niondoke.Nilikaa kwa muda wa lisaa limoja,kwenye saa kumi na mbili hivi,Basi lilikuja nikapanda haraka,safari ikaanza mara moja.Kiukweli safari hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani niliifurahia mno.Mwanzo mwisho matumaini yangu yalikuwa ni makubwa kwamba nikifika tu huko basi mambo yangu niliyokuwa nikiyapanga yatatimia.Dar es salaam pamoja na viunga vyake tulifika usiku.....ulikuwa ni Usiku majira ya saa tano kwa mjibu wa saa yangu ya mkononi.Sikupat
a tabu baada ya kufika kwani huko nilikuwa mwenyeji,nimepata degree yangu ya uchumi nikiwa huko huko Dar es salaam hivyo sehemu zote nilikuwa nikizifahamu vyema na isitoshe nilikuwa na marafiki zangu wa kutosha tu.Usiku huo huo niliamua kufunga safari ya kuelekea ghetoni kwa jamaa angu wa kuitwa Gerard ili kwa Usiku huo nikajihifadhi huko,kukikucha niendelee na mambo yangu.Basi sikupoteza muda nilianza kwenda huko nikatumia dakika chache tu nikawa nimefika.Usiku huo nililala huko huko hadi kulipopambazuka,na kulipopambazuka
,Gerard nae sikumuaga naelekea wapi zaidi niliondoka kimya kimya tu,natokea siku hiyo sikuweza kuwasiliana nae hadi nayaanza maisha mpaka kufanikiwa kimaisha.
Miaka kadhaa baadae nilifanikiwa kuanzisha biashara zangu kwa kufungua maduka makubwa ya jumla jumla pamoja na kujenga machine mbali mbali za kusaga na kukoboa,nikaajiri watu hatimaye nami nikaanza kuitwa Boss.Sikuishia hapo,kiu yangu ya kusonga mbele kimaendeleo ilizidi kuutamanisha moyo wangu mpaka likaja wazo la kufungua kampuni langu binafsi la kutengeneza majembe ya kilimo na pambajeo mbali mbali za kilimo,kampuni hilo nikalipa jina la IGEMBE SABO kama Mila na desturi ya kukuza lugha yangu mama ya kisukuma.Maisha yalizidi kuendelea nikanunua kiwanja na hatimaye kujenga nyumba yangu binafsi ili kuepusha changamoto za kodi na usumbufu mwingine usiokuwa wa lazima.Nilijenga nyumba moja kubwa ya kutosha tu na kila kitu kikawa kimekamilika,ki
kabaki kitu kimoja tu yaani mke.Hapo ndo nikawa naumiza kichwa changu kwa sana,,,niliamua kuituliza akili yangu nikaja na jibu la maana ambalo nililiamini kwa asilimia zote kwamba halitafeli.Kwa kujiangalia tayari nilikuwa na mali na pesa pia,sasa ili nisipate mke wa kuja kunisaliti hapo baadae sikutaka kujionyesha kwamba nina pesa yaani kutafuta mke kwa kigezo cha kuwa na pesa yasije yakanitokea puani.
"Haaa!! Boss unaenda wapi na huo mkokoteni ni wa nini Boss?" Ni swali ambalo liliulizwa na mmoja wa wafanyakazi wangu wa ndani,ajulikanaye kwa jina la Mtashobya,,,,Wakati huo nilikuwa nimevaa kama najiandaa kwenda majerubani sikutaka kuvaa tai wala nini,lengo la kutafuta mke mwema lilikuwa limejikita moyoni,yaani nilidhamiria na sikuwa mtu wa kukubali kushindwa."Mtashobya,nadhani huu ni muda wangu wa kumtafuta mwenzangu,na ndio maana nipo katika hii hali......nikisema nitafute mke kwa njia ya pesa hatokuwa na upendo wa dhati kwangu".Nilimjibu kijana huyo,nikamuona akitikisa kichwa chake kwa mshangao nikashindwa kumuelewa kabisa.Alinitazama sana baadae akasema "Boss,sidhani kama hiyo ni njia sahihi ya kumpata mke mwema,,,,wewe ni mkristo mzuri tu na unamuamini Mungu ,cha msingi ni wewe kumshirikisha Mungu tu kwani kila kitu kitakuwa vizuri".Alisema Mtashobya lakini kwa hapo kimoyo moyo nikampinga kwa kumwambia moyo wangu umeridhia na hilo wala halitokuwa jambo baya.Sikuwa na maneno mengi,niliagana nae nikaondoka niingie mjini nizunguke huku na huko kama mzoa taka kwenye mkokoteni nione kazi hiyo itaniletea majibu gani.Nakumbuka siku hiyo nilizunguka sana mpaka basi,nikachoka nikaamua kwenda kujipumzisha chini ya mtu mmoja mkubwa wa Mbuyu,lengo la kwenda hapo lilikuwa ni kwenda kupumzika tu na si vinginevyo.Nikaenda hapo nikaupaki pembeni mkokoteni wangu nikakaa,usingizi nao ukawa umenipitia nikalala kana kwamba nipo kitandani .
**************************
Ghafla nikiwa nimelala nilianza kuhisi kama kuna mikono ya mtu tena milaini ikikipapasa kifua changu,Nikakurupuka na kukuta hakuna kitu nikajua labda hiyo ilikuwa ni ndoto tu,nikaachana na kitu kama hicho nikawa naendelea na usingizi.Nililala sana,usingizi ukawa umeisha ikanibidi niamke hapo nirudi nyumbani kupumzika zaidi maana kama ni kuchoka tu ,kwa kweli nilikuwa nimechoka sana.Nilitoka hapo nikaikamata barabara ya kuelekea kwangu,nikawa najivuta vuta kuusukuma mkokoteni wangu kwa tabu kwani hata nguvu zilikuwa zimeniishia.Nilitembea hatua chache tu,nikajikwaa nikaanguka chini.....wakati najikakamua kusimama,nilimuona mdada mmoja mweupe kiasi amevaa nguo za heshima na Biblia mkononi mwake akija kwa mwendo wa kukimbia kimbia hadi eneo nililokuwa nimedondokea bila kuyapepesa macho yake akanishika mkono kunisaidia kusimama.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA PILI (02).

Nilisimama,nikawa najitazama kama nimeumia au sijaumia,kwa bahati nzuri sikuwa nimeumia ina maana nilikuwa poa tu.Sasa yule dada ambaye alinisaidia kusimama bado sikuwa nimepata nguvu za kumuuliza hata jina lake tu na kila nikiwaza kufanya hivyo niliona kama moyo wangu unasita.Sijui yeye alijiongeza kwani baada ya kunikodolea macho vya kutosha aliyasema maneno haya "Samahani Kaka,kwanza pole sana,kama hautojali ninaweza kukufahamu?" Aliuliza nikabaki najikuna kuna kichwani,,,,nilimkazia macho usoni nikakutana na uso wenye huba,uso wenye kila ishara ama dalili za upole maana binti kwa kumtazama tu ilionyesha dhahiri alikuwa ni mcha Mungu sana tu ukiachilia mbali ile Biblia yake aliyokuwa ameishikilia kwenye mkono wake wa kulia,,,sikuishia hapo nilizidi kumtazama kimya kimya maeneo mengine hasa kwenye hips na umbo napo nikakutana na vitu vizuri aise!!! Nikabadiri gia angani na badala ya hofu nikawa nammezea mate yule binti mpaka nikaanza kujipigilizia mahesabu kwamba huyu nikimpata basi hata kama shetani atatumia siraha zake zote kunishambulia kunishinikiza niachane nae sitokubali hata kidogo.Niliyamng'unya maneno yangu kimya kimya,,,nikayacheuwa nikaona yapo tayari kuyatoa "Dada mimi kwa majina yangu naitwa Luka Mangangarasi,naishi mitaa ya Kariakoo ,sijui mwenzangu unaitwa nani?" Nilisema kisha nikamuuliza jina lake ili nione atanijibuje maana kama nilikuwa nishampenda ghafla hivi .....Baada ya kumuuliza swali hilo hakutaka kunijibu papo kwa hapo alitulia kwanza ,,,alitulia kama dakika tatu au mbili hivi na wakati ametulia sikujua kama alikuwa akinichunguza au alikuwa akifanya kitu gani,hiyo ilikuwa ni siri ya moyo wake."Kaka Luka mimi naitwa Athumta,naishi mitaa ya Jangwani na pia ni muumini wa kanisa moja la Pentecost nje kidogo ya mitaa hiyo ya Twiga,nampenda sana Mungu".Alisema kwa sauti ya upole,japo ni sauti ya upole lakini nilihisi kama ikiutingisha moyo wangu kwani ilikuwa ni sauti nyororo sana yenye uwezo wa kuvuruga mipango yote na kuiweka sawa muda huo huo."Haya Kaka,muda naona unawahi sana acha niwahi nyumbani maana nyumbani huwa naishi na mama pekee hivyo inatakiwa nikamsaidie kazi mama yangu".Alisema kisha akageuka ili aanze kuondoka!! Na kweli akafanya hivyo ila kabla hajaondoka nilimsimamisha ili angarau nimuombe namba ya simu kwa mawasiliano zaidi maana nilivutiwa sana na miondoko yake siyo kwamba nilivutiwa kwa umbo lake pekee aisee hapana bali japo kwa muda huo mfupi niliozungumza nae nilimbaini huyo atakuwa ni binti mwema na mwenye tabia njema.
"Dada samahani naomba unisubiri japo kidogo tu".Nilisema mara hii nikiutua chini mkokoteni wangu maana msichana huyo tayari alikuwa ameshajongea mbele na kuziacha nyuma hatua kadhaa.Binti alinisikiliza na akawa amesimama ili kunisubiri,nilitembea haraka haraka kumsogelea,asante miguu nikawa nimemfikia.Uzuri mimi kwenye mambo kama hayo sikuwa na aibu wala kuwa na mizunguko mingi mingi.
"Dada Athumta naomba kama hautojali sana unipatie namba yako ya simu,tafadhari usiniambie kwamba hutaki kunipatia,tafadhari sana Athumta".Nilijitahidi kuyazungumza hayo kwa upole mno ili tu binti huyo aweze kunipatia namba yake.Athumta alianza kunitazama kuanzia juu ya kichwa changu hadi chini ya miguu yangu,nikamshuhudia akitabasamu huku ile Biblia aliyokuwa ameishika akizidi kuipakata vizuri Biblia yake hiyo."Kaka Luka,kwa bahati mbaya maskini wa Mungu wala sina simu mimi,maisha ya nyumbani kwetu ni magumu sana,sina simu Kaka". Aliongea na kuzidi kuninyong'onyesha vya kutosha nikawa najiuliza nifanyaje maana nilijua endapo ningemwachia aende zake kwenda kuonana tena ingekuwa ni ngumu sana.Cha kufanya ilibidi nimuulizie nyumbani kwao,kwamba yeye na mama yake wanaishi wapi na nyumba aina gani ili iwe virahisi kwangu kumpata.
"Tafadhari kwa mara nyingine tena,naomba angarau unielekeze nyumbani kwenu ili nije kukutembelea ikiwezekana kesho mapema".Nilisema nikamuona yupo tayari kunielekeza."Mimi na mama yangu kama ambavyo nilikuambia ,tunaishi mitaa ya Jangwani nyumba namba kumi,ukifika ulizia kwa mama Jema watakuelekeza vizuri tu".Alisema na hapo sasa kidogo amani ikarejea moyoni mwangu.Baada ya mambo yote hayo kumalizika tuliagana kwa wema,Athumta akaendelea na safari yake na mimi nikaurudia mkokoteni wangu nikaondoka maana jua lilishaanza kuwa kali na masaa yalikuwa yamesogea.Niliondoka pale nikiwa nimechoka lakini nikiwa na furaha ya hali ya juu isiyokuwa na mfano.Njia nzima wakati nikitembea nilikuwa nikijiongelesha peke yangu na wakati mwingine kucheka peke yangu kama mwendawazimu vile.Nyumbani nilifika kwenye mishale ya saa nane na robo hivi,nikafika,w
atumishi wangu wakaniandalia maji nikaoga baadae chakula nikala,mambo sasa yakawa yamekaa vizuri.Masaa yaliyoyoma hatimaye usiku ukaanza kuingia.....vya kuandaliwa viliandaliwa mwisho wasaa wa kwenda kulala nao ukafika.Kila mtu akaelekea anako lala,mimi nikaelekea chumbani kwangu,nikafika na kukaa kitandani kuwaza mambo mawili matatu.
"Athumta....Athumta!! Huyu binti atanifaa,,sasa nifanyaje ili nimpate? Je ninunue simu nimpelekee au nifanyaje....ah!! Itabidi kesho niamke mapema sana niende kwenye moja la maduka yangu ya simu nikachukue simu najua ataifurahia tu".Nilijisemesha nikaona wazo hilo limekaa vyema nikalipitisha,nikalala.Asikwambie mtu,usiku huo sikuweza kupata usingizi wa moja kwa moja zaidi ya usingizi wa kuunga unga tu maana kila nikijaribu kuyafumba macho yangu kuusaka usingizi nilihisi kama masikioni mwangu kunajipenyeza sauti nyororo ya Athumta.Ikafiki
a hatua nikawa naombea kupambazuke haraka.Basi nililala hivyo hivyo,Mungu saidia hatimaye kukawa kumepambazuka.Siku hiyo ya Alhamis niliamua kuahirisha kila kitu nikajiandaa vizuri ili niende dukani nikachukue simu .Nilioga nikamaliza,nikatafuta suruali moja ya dark bluu nikavaa pamoja ya shati jeupe la kung'aa nikajiona kwa hapo nimependeza hivyo endapo nitafika nyumbani kwa kina Athumta basi nitakuwa na mvuto sana,,,mambo ya mkokoteni na nini kwa wakati huo niliyaweka kando.Nilitafut
a viatu vyangu vya maana vizuri tu nikavivaa baadae nikatoka nje.Wakati natoka hakuna ambaye aliniulizia kwamba naenda wapi zaidi walijua nitakuwa naelekea kazini maana ule muonekano wangu ulitosha kabisa kulidhihirisha hilo.Niliitazama saa yangu ya mkononi,nikakuta ni saa mbili za asubuhi,nikaanza kuondoka.Sasa wakati nalikaribia geti la kutokea nje......nilisikia sauti "Boss.....Boss....Boss".Niligeuka,nikamuona Mtashobya akinikimbilia kuashiria kwamba alikuwa na shida ya kuniambia,,,nilisimama kumsubiri nae akawa amenifikia.
"Samahani Boss,sijui leo utakula chakula gani maana mpishi amenituma nije nikuulizie kabla hujaondoka".Alisema nikamjibu hapo hapo "Kwa leo mtanipikia michembe maana nimeikumbuka sana".Nilisema,Mtashobya akakubali na kuondoka,mimi nikatoka na kwenda zangu .Sikutaka kutumia gari nilitembea kwa miguu tu.......Kwa mwendo huo wa miguu nilifika dukani yaani moja ya maduka yangu ya simu nikamkuta mfanyakazi wangu Juliana.
"Karibu Boss".Alinikaribisha huku akisimama kwa heshima kama zote."Habari za asubuhi Juliana?" Nilimpa salamu hiyo "Nzuri tu boss,shikamoo?" Nae aliitikia na kunisalimia."Marahaba,sasa naomba unipatie simu iPhone aina yoyote ile nina shida nayo".Nilisema akafanya haraka kunichagulia simu ya iPhone ya maana na kisha akanipatia."Okey Juliana kazi njema na asubuhi njema pia".Nilimuaga lakini akawa kama kuna jambo anataka kuniambia japo alikuwa na aibu sana na isitoshe alikuwa akiniogopa."Sawa boss na kwako pia". Alizungumza nikampa mkono wa kwa kheri nikaondoka hapo ili niwahi haraka nyumbani kwa kina Athumta.Nilitembea kwa umakini mkubwa ili nihakikishe sipitilizi kwenye nyumba ile ambayo binti Athumta alinielekeza.Ni
kiwa natembea yale maeneo ya mtaa wa Jangwani nilianza kuyafikia,,,macho yangu yalikuwa makini kuitizama kila nyumba.....nilitembea nikawa nimezipita kama nyumba tano hivi ,, hatimaye ile nyumba namba kumi nikaifikia,Nili
poiona tu nilianza kujiuliza mara tatu tatu,hapa ndo nyumbani kwa kina Athumta au naona maruweruwe? Ile nyumba ilikuwa ni nzuri na kubwa na kwa kuitazama tu haikuwa nyumba ya wapangaji bali ni nyumba ya familia kama familia.Nyumba hiyo iliyokuwa imepakwa rangi ya brown na kijani kwa chini ilikuwa na uzio wa maana,na kwa haraka haraka kwa muonekano wa nyumba hiyo hapo ilionyesha dhahiri ni kwa matajiri na si vinginevyo.Nilijikaza nikawa nalisogelea geti,nikalifikia na kuanza kubisha hodi.
***********************************
Alitoka jamaa mmoja kauzu sana,akasimama mbele yangu na kuanza kunikazia macho "Vipi sijui nikusaidie nini?" Aliniuliza huku akizidi kunitazama,sema uzuri nilikuwa nimevaa vizuri laiti kama ningekuwa shagala bagala kwa jinsi jamaa yule alivyokuwa angenitimua kama mbwa."Bila shaka hapa ndo nyumbani kwa kina Athumta".Nilisema akaitikia kwa ishara ya kutikisa kichwa."Yeah!! Hapa ndo nyumbani kwao,ndo nyumbani kwa mama Jema,vipi unafahamiana na huyo binti ?" Aliuliza nikamjibu "Ndio binti huyo nafahamiana nae na ni rafiki yangu pia".Nilimjibu huku nikiitengeneza vizuri tai yangu."Sawa!! Sasa ingia zunguka nyuma ya jengo lile,utamkuta binti huyo ila uwe makini nimemaliza".Alisema,nikashtuka kidogo aliponiambia niwe makini ila nikachukulia poa tu.Niliachana na mlinzi huyo wa getini nikaanza kutembea kuelekea sehemu ile ambayo nilielekezwa.Nilizunguka kama kawaida hatimaye nikafika nyuma ya jumba hilo.Kwa mbali niliona kiti cha plastic bila kumuona mtu,nikakitazama kwa makini nikagundua juu yake kulikuwa na Biblia.Nilianza kusogea huku mapigo ya moyo yakienda mbio maana nilikuwa nikipangilia mistari ya kwenda kuanza nayo .Sasa ile nimezibakiza hatua chache kukifikia kile kiti juu ya ile Biblia nilimuona nyoka amekaa akiwa amekinyanyua juu kichwa chake,akikizungusha huku na huko.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA TATU (03)...

Yule nyoka kusema ukweli aliniogopesha sana ila kwa vile hiyo haikuwa mara yangu ya kwanza kukabiliana na majoka sikuona kama hilo lingekuwa ni tatizo la kutisha kivile kwani kule kijijini kwetu ni mara nyingi tu nimeshawahi kupambana na majoka makubwa makubwa majerubani na nikayashinda.Niliupiga konde moyo wangu nikaamua kuendelea kukisogelea kile kiti.Wakati nakikaribia tu,Athumta nae alionekana akija kwa kasi ikaonekana alikuwa akitokea uani....akafika pale na kwa bahati hata yeye yule nyoka alimuona hivyo aliruka na kuanza kupiga kelele.....kelele zile zilimshtua hadi mlinzi wa getini,jamaa akatokea akiwa na bonge la rungu."Kuna nini hapa,kuna nini?" Aliuliza Mlinzi ,Athumta akamuonyesha kwa kutumia kidole chake akimsihi atizame kitini,mlinzi alitazama akamuona yule nyoka."Muue haraka,muue!!".Aliagiza Athumta ,haraka mlinzi akasogea pale kwa mwendo wa pole pole akakifikia kile kiti na kisha kuanza kupambana na nyoka huyo ,akampiga rungu moja ya kichwani,nyoka akaanguka chini na kufa hapo hapo.Baada ya kumaliza kulifanya hilo,mlinzi aliaga akaondoka pale kwenda kuendelea na majukumu yake pale getini.
"Karibu kiti Kaka Luka mbona umesimama tu".Aliniambia Athumta huku yeye akikaa chini ya zile nyasi za kijani....nilisogea kwenye kiti hicho nikakaa ile Biblia nikaibeba na kisha kumpatia Athumta,binti akaichukua na kuanza kuifunua funua huku akitabasamu na wakati mwingine kunitizama kwa macho ya kuibia."Halafu hujaniambia Kaka Luka,hivi huwa una sali kanisa gani?" Aliniuliza swali hilo likawa gumu kwangu maana Mimi pamoja na kuwa na jina la Kikristo lakini nilikuwa mpagani yaani kanisani nilikuwa sikanyagi kabisa.Nilimtazama usoni nikamkazia macho na kumjibu "Hapana mimi sina dini yaani sisali kwani hapa nilipo mimi ni mpagani ".Nilimjibu akanishangaa sana."Mh!! Wewe ni mpagani? Mbona una jina zuri tu la Kikristo? Haiwezekani bwana siamini kama wewe ni mpagani".Alitamka Athumta nikamuona kama bado kuna maneno anatamani kuendelea kuyatamka."Huo ndo ukweli wangu,mimi ni mpagani sina dini wala sijawahi kusali maana ukoo wetu huwa tunaamini sana mambo ya Mila kama kutambika na kadharika".Nili
zungumza,kisha binti huyo akanisihi kama sitojali nishuke chini nikae mbele yake kwenye zile nyasi azungumze na mimi vizuri.Nilimsikiliza nikashuka nikakaa kwa kutazamana nae.Athumta alinishika mabegani akanitingisha mara tatu mfululizo akanitazama kwa macho malegevu usoni mwangu mpaka nikapatwa na kiwewe duuh!!,sasa akisha kunifanyia hivyo alitabasamu kwa kuachia tabasamu nono usoni mwake,tabasamu la haja ambalo kwa upande wangu liliweza kunichanganya sana nikawa natamani masaa yasiende ili mradi tu niendelee kuufurahia uwepo wa Athumta pale.
"Luka?" Aliita Athumta."Naam,dada Athumta".Niliitikia huku nikiwa na hamu ya kutaka kujua ni kipi ama neno lipi ataniambia."Nikuambie kitu Luka?" Aliniuliza nikaitikia kwa ishara ya kutikisa kichwa."Okoka Kaka yangu maana hii dunia kwa sasa haieleweki,Yesu yupo karibu kurudi asije akakukuta ukiwa hujaokoka maana utaenda motoni".Alisema Athumta nikawa kama nimemuelewa vile japo kiutimilifu sikuweza kumuelewa moja kwa moja."Sawa nimekuelewa Athumta nitajitahidi kufanya hivyo".Nilimjibu lakini mwenyewe nikajua hayo maneno nimeyatoa mdomoni tu wala siyo moyoni."Waooo!! Ngoja nikusomee neno la Mungu kutoka katika maandiko Matakatifu,,,Neno la Mungu linatoka katika kitabu cha Mathayo Mtakatifu sura ya saba mstari wa saba.Ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona,bisheni nanyi mtafunguliwa.Sasa Kaka Luka mpaka hapa umechagua fungu lililo jema kwani ukiokoka tu,endapo utamuomba Mungu kitu chochote kile atakupatia".Nilimsikiliza kwa umakini mkubwa mno Athumta japo macho yake yaliyokuwa yametua usoni mwangu yalikuwa hayatikisiki wala kupepesuka na yalikuwa yakionekana kuwa ni meupe sana.Nilijibalaguza balaguza,mwisho nikaona kumuachia Athumta azungumze kila kitu yeye nitakuwa mwanaume suruali.Cha kufanya niliunyoosha mkono wangu wa kulia nikaichomoa ile simu ili nimpatie kwani lengo langu kubwa lilikuwa ni ili niweze kuwa nawasiliana nae vizuri.Niliitoa simu nikaishikilia kwenye mkono wangu wa kulia nikawa naitazama tazama huku nikiigeuza geuza.Nilimkazia macho nikamtazama weee baadae kama kwenye dakika moja hivi nikaamua kufunguka,
"Athumta hivi hii ndo nyumba yenu ama?" Nilianza kwa kumuuliza hilo swali akakubali kuwa ile ni nyumba yao."Yeah!! Hii ndo nyumba yetu,mama amehangaika sana mpaka kuusimamisha huu mjengo". Alizungumza Athumta ikanibidi nimuelewe hivyo hivyo japo mwanzo alinidanganya kuwa yeye na mamaye maisha yao ni magumu,wanakula kwa shida na kulala kwa tabu.Niliitizama ile simu nikampa akakataa."Hii simu mbona ni ya gharama sana,wala mimi siitaki labda ungekuwa umeninunulia simu ndogo aina hata ya Nokia na siyo hii".Alisema Athumta nikashindwa kabisa kumuelewa .....Nikajua labda binti huyu huwa anaishi maisha ya kawaida yasiyo na complication."Poa Luka acha mimi nikuache hapa nikaandae chakula cha mchana,vipi nikuachie hii Biblia ukutwe unasoma?" Aliniuliza nikamjibu poa.Binti akasimama na akisha kusimama alianza kutembea haraka haraka kuondoka maeneo hayo.Aliondoka akawa ameingia ndani sikujua alienda kuandaa chakula au laa,mimi nikabaki nimekaa zangu pale beach ndogo.
Nilikaa pale kwa muda mrefu kidogo,dakika zikawa zinaenda tu bila kumuona Athumta akija kunikaribisha au kunijurisha kama amemaliza kuandaa chakula au laa.Ghafla nikapitiwa na usingizi nikalala pale pale juu ya zile nyasi.Mwanzo niliufurahia sana usingizi lakini baadae kama usingizi wangu ulianza kuingiliwa na doa hivi.Ilikuwa hivi,,,wakati nikiwa nimelala juu ya tumbo langu nilianza kuhisi kama kuna kitu cha baridi kimenilalia,nikaamua kunyanyuka na kuona hakuna kitu,nikaendelea na usingizi.Niliku
ja kukurupushwa na kelele za Athumta za "Nyoka!! Nyoka!! Nyoka jamani".Niliamka fasta nikamuona nyoka mwingine amekaa juu ya kile kiti akiwa amenyanyua juu kichwa chake.Nilisimama kama nimevutwa na winchi vile nikasogea pembeni na kuanza kutafuta fimbo nimshambulie yule nyoka .Wakati huo bado Athumta alikuwa akiendelea kupiga kelele huku akijisogeza sogeza nyuma ya mgongo wangu.Kwa bahati nzuri niliupata ukuni mmoja nikaanza kumshambulia yule nyoka mpaka akafa,,,nikambeba na kumtupilia mbali."Asante Luka,mi huwa nawaogopa sana nyoka na huwa sitaki hata kuwaona maana wanatisha".Alisema Athumta."Usiwe muoga kiasi hicho Athumta,nyoka ni viumbe wa kawaida tu".Nilimwambia akacheka kidogo na akawa ameliegemea bega langu moja,nikajua huyu mtoto ameshajinasa kwenye nyavu zangu."Twende tukale sasa Luka au vipi".Alisema,nami sikukataa,nilikubali tukawa tunazipiga hatua kuelekea ndani tukapate chakula cha mchana.Tuliingia humo ndani,Athumta akachukua maji akaanza kuninawisha wakati huo nikiwa nimekaa juu ya sofa.Sasa ile anamaliza kuninawisha tu ,mara aliliachia lile jagi la maji."Nyoka!! Nyoka!! Nyoka".Alipayuka nikasimama haraka,nilipoya
geuza macho yangu tu,kumbe kwenye lile sofa ambalo nilikuwa nimelikalia kulikuwa na bonge la joka.Alikuwa ni nyoka mrefu mweusi.Nilitoka nje haraka nikaja na mpini,cha kushangaza yule nyoka sikumuona tena na sikujua alipotelea wapi,sikujua alishuka chini ya lile sofa au alikimbilia wapi.
"Athumta yule nyoka yupo wapi,ameenda wapi?" Nilimuuliza Athumta kwani yeye ndo nilimuacha humo ndani wakati nikitoka nje kwenda kutafuta cha kuja kumpigia nyoka yule.
"Wala sifahamu Luka,mimi nilimuona ameshuka chini akaingia muleee".Alisema huku akinyoosha kidole cha mkono wake kunionyesha sehemu ile ambayo nyoka alipitia.Nilisogea hapo nikaanza kulisogeza lile sofa mpaka nikafanikiwa kuliweka pembeni,yule nyoka sikumuona,nikamtafuta sana lakini wapi,ikabidi nimuache tu.Nilikaa tukaendelea kula.Baada ya chakula nilimshukuru sana kwa chakula chake kizuri wakati wangu wa kuondoka ukawadia nikamuaga ili niondoke lakini yeye akanisihi tuondoke nae,na kama haitoshi akaniambia tuelekee kwa mangi akaninunulie soda tuagane kwa wema.Nilikubali tukaambatana wote kuondoka maeneo hayo.Tulifika kwa mangi baada ya dakika kadhaa kupita,mangi akatukaribisha vizuri tu,nasi tukakaa.
"Niletee Pepsi nyeusi tafadhari".Nili
agiza,Athumta yeye akaagiza maji.Tukaanza kunywa huku tukiendelea kupiga story za hapa na pale.
*****************************
"Athumta kiukweli yaani acha tu ukweli ni useme".Nilizungumza nikajisachi mfukoni,kumbe nilikuwa na simu ndogo tena aina ile ile ya Nokia.....nilifurahi sana nikaona hii simu ninatakiwa nimpatie Athumta."Ukweli gani unataka kuniambia Kaka Luka?" Nae aliamua kuniuliza baada ya kuniona nimebaki kimya."Subiri kidogo,simu aina ya Nokia hii hapa Athumta naomba uipokee".Nilimpa napo akakataa.
"Hapana,mimi tangu nizaliwe sijazoea kutumia simu na sitaki kutumia simu Luka,mimi mazungumzo yangu huwa ni ya ana kwa ana".Alisema Athumta,ile simu nikairudishia mfukoni."Athumta,kiukweli nimetokea kukupenda sana tafadhari naomba uwe mke wangu".Niliamua kumfungukia mpaka akawa ananitazama na kuishia kucheka tu."Wewe ni tajiri Luka na mimi ni maskini tutawezaje kuoana?" Aliuliza,swali hilo likawa na utata mkubwa sana kwangu ."Una maanisha nini kusema hivyo Athumta?" Nilimuuliza akaigeuza geuza shingo yake."Namaanisha hivi,wewe una pesa halafu mimi sina,okey tuachane na hilo,mimi nimekubali uwe mume wangu ila ni lazima ukubali kuokoka kwanza,maa....?" Kabla hajamalizia sentensi yake hiyo mara........


NILIOA NYOKA SEHEMU YA NNE (04).

Nilimuona binti furani hivi amevaa gauni la bluu akikatiza karibu na eneo lile tulilokuwa tumekaa kwani lilikuwa ni eneo lenye uwazi na isitoshe ilikuwa ni nje.Nilimtazama sana yule binti nikawa namfananisha huku nikijiuliza huyu dada mbona namfahamu? Nikaona kuendelea kubaki kimya haiwezekani acha nimuite......nilipaza sauti hatimaye dada yule nikawa nimemuita akaja pale na kusimama."Samahani dada,mbona kama nakufahamu?" Nilimuuliza akatikisa kichwa kuashiria kwamba sina nina chokifahamu yaani sieleweki."Umeshawahi kuniona sehemu gani,kwani wewe unaitwa nani kwanza?" Nae alizungumza ikanibidi nimuambie jina langu labda atanitambua maana Mimi nilikuwa namfahamu kabisa kuwa ni dada yangu tena tumezaliwa tumbo moja,mama mmoja na baba mmoja pia."Mimi naitwa Lukas Majaba,wewe si ni dada angu tena unaitwa Milembe,ina maana dada umenisahau?" Nilimuuliza akakataa kuwa wala hanifahamu.Hakuendelea kubaki eneo lile aliondoka muda huo huo akaendelea na safari yake.Kiukweli nilianza kuchanganyikiwa sana nikadhani labda akili yangu imevurugika au macho yananidanganya.Ila kwa pale sidhani kama macho yangu yalikuwa yakinidanganya kwani yule dada alikuwa ni yeye kabisa....ni dada angu kabisa niliyezaliwa nae tumbo moja.Nilikataa katakata kukubali kama akili yangu au macho yangu yalikuwa yameingiliwa na mawenge.Nilikaa kimya mpaka Athumta akanishtukia na kuamua kuniuliza swali,,
"Ina maana ,Luka hufahamiani na ndugu zako?" Aliniuliza swali hilo rahisi tu lakini nikachukua dakika kumi kumjibu."Hata sielewi Athumta,yule ni dada angu,anaitwa Milembe halafu nashangaa jana tu niliongea nae kwenye simu akasema yupo Mwanza anashughulikia biashara zake,sasa nashangaa kumuona huku Dar es salaam sijui amekuja lini hata sijui kwa kweli".Nilizungumza....Athumta akanikazia macho usoni,,alinishika begani akawa anatikisa kichwa chake."Una uhakika kwa hicho unachokizungumza Luka? Inawezekana vipi dada yako akukatae aseme hakufahamu?" Aliniuliza nikampa jibu lile lile la kwamba sielewi,,,akapata oni la kunishauri "Luka sasa hapa tufanye hivi hebu toa simu yako ya mkononi jaribu kumpigia simu sasa hivi tuone itakuaje ". Aliongea Athumta nikawa nimemuelewa sana.Cha kufanya sikutaka kuanza kujihoji maswali yasiyokuwa na msingi.....nilitoa simu nikazitafuta namba za dada Milembe nikapiga,simu ikaanza kuita.Iliita kama mara mbili hivi ikapokelewa."Haloo Kaka Luka vipi mzima wewe?" Sauti ile ile ya dada ilisikika nikamjibu "Nipo poa tu,hivi dada kwa sasa upo wapi?" Nilimuuliza."Kwa sasa si bado nipo Mwanza jamani isitoshe jana tu nilikuambia umeshasahau Kaka ?" Aliniuliza nikawa namng'unya mung'unya tu maneno."Aha poa dada sema nilisahau ,samahani sana".Niliona yaishie hapo sikutaka kusema nimemuona Dar kwani angesema nimechanganyikiwa au nimerogwa."Haya poa Kaka angu,mchana mwema". Aliongea nikawa na mimi nimemtakia mchana mwema nikakata na simu.Kiukweli hali ile ilinichanganya sana nikawa najiuliza maswali kadha wa kadha ambayo sikuweza kuyapatia ufumbuzi wala majibu ila nikawa najikaza hivyo hivyo tu.Nilitulia kwa muda na sikuwa na hamu tena ya kuendelea kuzungumza.
"Luka vipi,huyo uliyezungumza nae si ndiye dada yako Milembe au?" Athumta aliniuliza,nika
mtazama na kisha kumjibu "Ndio niliyemaliza kuzungumza nae ndo dada angu Milembe ila sielewi huyu niliyemuona ni nani na kwa nini anafanana sana na dada angu,sielewi".Nilimjibu nikabaki nikiwa nimeyainamisha chini macho yangu.
"Usiwaze sana Luka,unajua katika hii dunia tupo wawili wawili unaweza kufanana na mtu anayeishi hata America na mkawa hamna uhusiano wowote ule wa kindugu hivyo mambo kama hayo ni kawaida tu,tuachane nayo na tuliza akili yako tuendelee kupata kinywaji".Alinipa moyo binti huyo nikamuelewa nikaamua kuachana na hayo mawazo tukaendelea kupata kinywaji......t
ulikunywa huku tukipiga story za hapa na pale mpaka tukamaliza .Tulisimama tukaagana kila mmoja akaondoka.Athumta alirudi kwao na mimi nikawa nimerudi kwangu kwenda kupumzika.Basi masaa yaliendelea mpaka jioni yake ikawa imefika,,,,Kutokana na joto kali la siku hiyo nilienda kwenye beach yangu yaani Garden nikapungwe na upepo kidogo.Nilielekea hapo na hiyo Garden ilikuwa ipo upande wa nyuma wa jengo langu la Kalakana.Nilikaa sana ndani ya hiyo Garden dakika kumi zikawa zimekatika baada ya mishale ya saa kumi na mbili kuwadia.Ikiwa inaelekea dakika ya kumi na moja..... Mfanyakazi wangu mmoja wa kike alikuja akasimama mbele yangu kuashiria alikuwa na jambo la kuniambia.
"Vipi Dayana?" Nilimuuliza ."Poa tu Boss,,,,ila samahani boss,,,kuna mgeni wako anakuhitaji ".Alisema binti huyo na mimi haraka nikasimama nikaongozana nae huko,,,kufika kumbe mgeni mwenyewe ni Athumta.Nilimkaribisha nikarudi nae hadi kwenye ile Garden tukafika na kuketi....."Kumbe Luka una nyumba nzuri kiasi hiki yaani nimeipenda".Aliyasema hayo ila mimi swali langu likawa amepajuaje kwangu maana sikuwa nimemuambia namba ya nyumba yangu ila pamoja na kujiuliza hivyo ,swali hilo niliamua kulipotezea kwa kudhani atakuwa aliulizia kwa watu akaelekezwa.Hilo nikawa nimeliamini kwa asilimia zote."Athumta hivi unajua kama wewe ni mrembo?" Nilimuuliza akacheka huku akiving'ata ng'ata vidole vyake."Ah!! Wapi,ila na wewe ni bonge la handsome....Yaani kwa ulivyo kila msichana ni lazima atamani kuwa na wewe kimapenzi".Alisema Athumta nikafurahi sana maana maneno kama hayo tena kutoka kinywani mwa binti mrembo kama Athumta hilo lisingekuwa na kipingamizi."Luka mimi sikai sana ila ningependa siku ya juma pili nikuone kanisani nitafurahi na hapo ndo nitakuwa tayari asilimia mia kuolewa na wewe tuyaanze maisha yenye amani ndani yake". Aliongea Athumta nami nikamhakikishia kwamba kuanzia juma pili hiyo ijayo nitaanza kusali .Alisimama akanisimamisha na mimi kisha akanikumbatia na kunibusu akaanza kuzipiga hatua kuondoka,nilimsindikiza kwa macho hadi alipotoweka kwenye mboni hizo za macho yangu.Sasa baada ya Athumta kuondoka tayari giza lilikuwa limeshaingia hivyo sikuendelea kukaa ndani ya ile Garden,nilitoka hapo nikawa nimeingia moja kwa moja ndani ya nyumba yangu.
Giza likatanda kila sehemu na kwa muda huo mishale ya saa mbili za usiku ilikuwa imeshawadia.Waliandaa chakula tukala tukawa tumeshiba.Kwa vile sikuwa nimeokoka kipindi hicho wala sikuwa na muda wa kusema tusali kabla ya kwenda kulala....kwa hapo kila mmoja aliondoka kimya kimya kuelekea anako lala,na mimi nikaelekea kule ninako lala.Niliingia chumbani kwa ajili ya kulala.Sikulala moja kwa moja bali nilikaa kwanza kitandani kutafakari mambo mawili matatu kama ambavyo ilikuwa kawaida yangu.Niliwaza jambo moja nikalimaliza,nikatafakari jingine nalo nikawa nimelimaliza nikaona sasa acha nipumzike kwa ajili ya kesho.Tayari saa tatu ilikuwa imeshakaribia kwani kwa hapo ilikuwa ni saa mbili na dakika hamsini na nane ina maana zilikuwa zimebaki dakika mbili tu.Nilipanda kitandani nikajinyoosha nilale,,,,Kabla hata sijajinyoosha vizuri simu yangu ilianza kuita nikaichukua,kui
tazama juu ya kioo chake nikaona namba mpya ya simu....nikaitazama mpaka simu ikakatika.Dakika moja tu,simu yangu ilianza kulia kwa mara nyingine tena,kwa hapo nikaamua kuipokea.
"Haloo!! Luka mimi Athumta".Sauti hiyo ya Athumta ilinifanya nitabasamu nikasahau hadi kumuulizia namba yangu aliipata wapi."Vipi Athumta kwema lakini?" Nilimuuliza,aka
cheka."Kwema mpenzi wangu ila hapa nilipo nawashwa sana natamani uje unikune".Alisema nikashindwa kutambua anawashwa kwa namna gani au ni wapi anapowashwa."Unawashwa nini Athumta?" Nilimuuliza."We niruhusu nije tu nitakuelekeza kwa vitendo pale ninapowashwa".A
lisema nikamwambia haina shida aje tu."Poa Athumta we njoo,mimi kwa sasa natoka nje kukusubiria".Niliyaongea hayo kisha nikakata simu,haraka haraka nikatoka pale kitandani nikaufungua mlango wa chumba changu nikawa nimetoka nje.
Nikaanza kumsubiria Athumta kwa hamu zote kwani niliwaza endapo akija tu basi kamwe siwezi kumuachia aondoke hivi hivi.....wakubwa wenzangu nadhani kwa hapa mtakuwa mnenielewa namaanisha nini,watoto hawawezi elewa.Basi nilitafuta kiti nikakaa tayari kabisa kwa kuendelea kumsubiria mrembo huyo.Nusu saa ilikatika bila Athumta kuja,,,nikawa najipa matumaini tu kwamba atakuja wacha niendelee kumsubiria.Mpaka lisaa limoja linakatika bado Athumta hakuwa amefika.Nilianza kuachia miayo nikaisogeza simu yangu na kisha kuamua kuitafuta namba ya Athumta,,,kwa vile nilikuwa bado sijaisave nilianza kuitafuta kwenye Received calls.Niliingia kwenye kipengele hicho kuitafuta lakini nikakuta hakuna namba yoyote kwenye hicho kipengele zaidi ya kukutana na neno la "NO ITEMS".Nikajiuliza nimezifuta saa ngapi namba nilizokuwa zimezipokea ili hali baada tu ya kumaliza kuongea na Athumta simu yangu niliiweka pembeni,nilijiuliza sana ila ikabidi nikubaliane na hali kuwa namba hizo hazipo.Nilisimama ili nianze kuondoka pale,,, nilianza kuzipiga hatua kuelekea ndani,sasa ile naziacha hatua chache tu nyuma mara simu yangu ilianza kuita nikaipokea."Haloo Luka,mimi Athumta,samahani nimeshindwa kufika maana mama yangu amenikataza kwa kuniambia sasa hivi ni Usiku mno ,,,tukutane kesho mpenzi wangu". Aliongea nikashindwa kumjibu hadi akamaliza na kukata simu yake.Haraka baada ya kuikata hiyo simu nilitamani namba ile niisave lakini baada tu ya kuingia kwenye kipengele cha Received calls sikuiona wala sikuona namba yoyote ile nikajua labda simu yangu imepatwa na tatizo.
*******************************
Niliendelea na safari yangu ya kuelekea ndani ili nikalale maana muda ulikuwa umeenda sana,saa tano ilikuwa inakaribia karibia.Nilipoufikia tu mlango wa kuingilia sebuleni nilihisi haja,nikageuza ili nielekee uani,choo cha nje .Niliingia humo nikawa najisaidia hadi nikamaliza,,,,haraka nikatoka humo ili nianze kurudi ndani .Nilitembea hatua tano tu nikahisi haja tena,nikageuka na kurudi ili nikajisaidie.Sa
sa ile naingia tu chooni,,,haja ilitoweka na tumbo likatulia,,,
Nilisimama nitoke humo,nikatoka na kuanza kutembea kuelekea ndani.Nilitembea mpaka nikaufikia mlango.Ghafla tumbo langu likaunguruma tena ,nikageuza nirudi tena chooni..Nilipoingia tu humo,tumbo lilitulia na hakukuwa na haja yoyote ile ambayo ilikuwa ikidai kutolewa.Amani ikawa inatoweka moyoni mwangu.Nilibaki nimekaa mule chooni huku hofu ikiwa kubwa moyoni mwangu.Nilijikaza lolote na liwe nikatoka humo chooni kwa mwendo wa kukimbia.Nilitoka mbio nikaenda kuufungua mlango wa sebuleni nikaingia ndani nikanyoosha kuelekea chumbani kwangu .Niliufikia mlango wa chumba hicho na kwa bahati nzuri lile tumbo lilikuwa limetulia.Nikakikamata kitasa cha huo mlango ili niufungue,,,,nilipoufungua tu,nilimuona dada angu Milembe amekaa hapo kitandani huku akiwa amejifunika shuka jeupe kiunoni.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA TANO (05)

Niliweza kumuona kwa uzuri kabisa dada Milembe bila chenga yoyote maana taa zote ndani ya hicho chumba changu zilikuwa zikiwaka.Nilish
indwa hata nifanyeje....niingie tu,nisimame ama nikimbie nikawa kama nimepigwa shoti ya umeme.Sikujua kile ambacho kiliendelea baada ya hapo kwani nilidondoka chini na fahamu zangu nazo zikawa zimekatikia hapo.Nilipokuja kuzinduka tena,yule dada sikumuona na sikujua alipotelewa wapi.Mapigo ya moyo wangu yaliishia kwenda mbio nikaghaili hadi kuingia humo chumbani nikarudi sebuleni na kuamua kabisa sitorudi tena humo chumbani hadi kutakapopambazuka.Nilipanda juu ya sofa langu jeusi nikawa nimelala hapo.....Sasa wakati naendelea kupiga usingizi niliota ndoto moja ya kutisha na kusononesha mno.Niliota nikiwa nimeketi sehemu ya nyuma kanisani siku ya juma pili,mara upande wangu wa kulia nikahisi kama nimeguswa na mikono ya binti,nilipogeuka kumtazama msichana huyo sikuamini kwa kile ambacho nilikuwa nimekiona.Msichana huyo wala hakuwa Athumta alikuwa ni msichana mwingine mwingine tu.Wakati namtazama kumbe nae alinishtukia macho yetu yakaja kugongana tukawa tunatazamana.Binti alitabasamu akayageuza pembeni macho yake ......mimi sikuchoka niliendelea kumtazama kila sehemu japo hakujua kama nilikuwa nikimchunguza kimya kimya.Nyuma yaani sehemu ya makalio yake nilishuhudia kitu kama mkia nikijitokeza kidogo kidogo ,kitu hicho ghafla kikawa mkia kamili,nikashtuka baada ya kuugundua mkia huo ni wa nyoka,ghafla ile sura yake ikabadirika na kuwa ya Athumta machale yakanicheza na hapo ndo nikaanza kuyalinganisha matukio yote ya nyuma nikaja kugundua kumbe Athumta ndiye anayenifanyia hayo yote......nilitambua moja kwa moja kuwa Athumta siyo binadamu wa kawaida bali ni jini hivyo nikakata shauri ya kuachana nae kuanzia muda huo huo .Nilikurupuka pale kwenye sofa nikawa najiuliza hii ni ndoto ya namna gani hii,,,Nilishindwa kabisa kuamini kama Athumta ni jini na sikuwa tayari kuachana nae iwe jua ama mvua.Niliitupil
ia mbali ndoto ile nikaendelea na usingizi wangu.Nililala hadi asubuhi ,mapema baada ya kuamka.....nikaanza kujiandaa mapema mapema nielekee nyumbani kwa mganga nikaangaliwe ni nani ambaye alikuwa akinisumbua,sikuamini kabisa kama Athumta ndiye aliyekuwa akinifanyia maruweruwe na ile ndoto sijui ya kuachana na dada huyo niliitupilia mbali kwa kuamini ni ndoto ya uwongo haiwezi kuwa na ukweli wowote ule.Sikuwa na imani kwenye masuala ya dini imani yangu ilikuwa ni kwa waganga tu.Mpenzi msomaji,,,kwa kweli ukiwa haumjui Mungu katika maisha yako na haujawa tayari kumpokea awe Bwana na mwokozi wa maisha yako utahangaishwa sana na shetani na haya yote ndo yaliyokuwa yakinikabili.Ni
limaliza kujiandaa nikaanza safari ya kwenda nyumbani kwa mganga shida yangu ikatatuliwe.Nil
itumia usafiri wa gari yangu aina ya Land Rover nyeusi ili niokoe muda.Basi kwa mganga nilifika baada ya nusu saa kumalizika,,,,kwa bahati nzuri wakati nafika hapo,mganga nilimkuta na akanikaribisha vizuri tu.Alianza kunihudumia na mwisho wa siku akaniambia anayenifanyia hayo ni binti mmoja maji ya kunde ajulikanae kwa jina la Lilian Mshobyee tena nina sali nae kanisa moja ."Luka......Narudia tena kukuita Lukaa!! "....."Naam mganga wangu"......"Huyo binti aitwaye Lilian unatakiwa umuepuke kama ukoma,huyo binti ni nyoka na ndiye anayekusumbua kwani anaigiza kukupenda ili ukija kumuoa tu aanze kukutesa jumla jumla.Muogope sana na unatakiwa ukae nae mbali".Sikuweza kumuelewa mganga kuhusiana na maeneo yake hayo kwani huyo Lilian mimi sikuwa namfahamu.Basi ilinibidi maneno hayo niyachukue kama yalivyo nikayafanyie kazi na ikibidi binti huyo nimfahamu.Nilimpa pesa kama malipo yake nikawa nimetoka hapo na kisha kurudi tena nyumbani kwangu huku jua likiwa nimeshakuwa kali.
Nyumbani napo sikukaa sana niliondoka kuelekea nyumbani kwa kina Athumta,binti niliyekuwa nimetokea kumpenda kwa dhati kutoka ndani kabisa ya roho yangu.Nilifika huko,nikamkuta mtoto amejiachia ndani ya Garden nikaenda kuungana nae tukawa tunafurahi sana pamoja na kuyafurahia maisha.
"Luka nikuambie kitu?" Sauti nyororo na laini ya binti Athumta ilisikika ikiliuliza swali hilo mpaka nikahisi kama moyo wangu umeingiwa na hali ya mtetemo."Niambie tu wala usiwe na hofu kabisa Athumta".Nilimjibu akaachia kicheko cha haja na chenye uwezo wa kumtoa nyoka wa aina yoyote ile pangoni."Hivi ni lini utanioa my?" Aliniuliza Athumta huku akiniegemea begani."Nitakuoa baadae Athumta yaani miezi hii mitatu ikipita basi ni lazima niwe na wewe kama mke wangu tena kwa kufunga ndoa".Nilimjibu tukasimama pale na kisha kuelekea ndani,,,,chakula kiliandaliwa tukala tukashiba baadae kwenye saa tisa hivi niliagana na mke wangu mtarajiwa Athumta nikawa nimenyoosha moja kwa moja nyumbani kwenda kujipumzisha.
Zilipita siku tatu hatimaye siku ya kumwabudu Mungu katika roho na kweli ikawa imefika .Siku hiyo nilikuwa nimeamua kwenda kanisani kama ambavyo Athumta alinisihi japo sikuwa na lengo la kwenda kumwabudu Mungu kiukweli ukweli ila nilipanga kufanya hivyo kwa lengo la kumfurahisha Athumta tu ambaye niliamini ndiye atakaye kuja kuwa mke wangu wa milele kabla mambo hayajaharibika na kuwa magumu kwangu.Saa moja na nusu asubuhi,Athumta alikuja pale nyumbani kwangu akaja na kunywa chai kabisa,chai ambayo iliandaliwa na moja ya wafanyakazi wangu mahili pale nyumbani.Saa mbili ilipotimia,tuliongozana kwa pamoja kwenda kanisani huku tukiwa na furaha isiyokuwa na kifani.Huko tulienda kwa kutumia gari yangu,dakika chache tu tukafika huko na kwa bahati ibaada bado ilikuwa haijaanza kwani ilitaraji kuanza kwenye mishale ya saa mbili na nusu hivi na kwa muda huo bado ilikuwa ni saa mbili na dakika kama kumi na tano tu.Tulikaa sana tukiisubiria ibaada hiyo kwa hamu,ibaada ikaanza mnamo saa hiyo saa mbili na nusu,,,,watu wakamsifu Mungu kwa nguvu zao zote huku mimi nikiufurahia uwepo wa mpenzi wangu Athumta tu pamoja na kuombea muda wa kuondoka ufike.Kwenye ile sehemu ambayo nilikuwa nimekaa tangu ibaada ianze sikuwa nimetazama kulia ama kushoto zaidi macho yangu yalikuwa yametazama mbele tu .Sasa sijui ilitokeaje ama ilikuaje tu hadi macho yangu yakageukia kunako upande wa kushoto.....Nil
ijikuta tu upande huo nikiugeukia,nilipougeukia upande huo nilimuona binti mmoja mzuri sana amekaa,na baada ya kumuangalia sijui na yeye alikuwa akinitazama kwa kuibia ibia.Sasa nilijifanya kama simtazami tena nikawa bize kutizama mbele.Ghafla nikaja kumshtukiza kumtazama,nikakutana nae macho kwa macho tukawa tunatazamana .Kwa jinsi macho ya binti huyo yalivyokuwa yakionekana ilijidhihirisha msichana huyo alikuwa akinifahamu sema tu mimi sikuwa nikimfahamu na kulikuwa na kificho furani hivi ndani ya hayo macho.Niliachana nae nikawa bize kumsikiliza mtumishi aliyekuwepo pale mbele akizungumza.
******************
Muda wa ibaada ulimalizika ,watu wakaanza kutawanyika kuelekea makwao. Wakati wakitawanyika,mimi sikuanza moja kwa moja Safari ya kuondoka kwani nilikuwa nikimsubiria Athumta atoke tuondoke wote kwani kwa kipindi hicho yeye na mchungaji Samba walikuwa ndani ya kanisa wakihesabu sadaka.Nilielekea kwenye mti mmoja hivi nikasimama ili nimngojee hadi atakapotoka.Sikuyapepesa macho yangu pande yoyote ile bali kwa kipindi hicho nilikuwa nimejiinamia.Ghafla nikasikia sauti ya msichana ikiniita....nikageuka na kumuona yule binti niliyekuwa nimekaa nae kanisani benchi moja akiniita nikaamua kumsogelea muda huo huo.
"Luka.....Umechagua fungu ambalo litayagharimu maisha yako".Aliyasema hayo nikamshangaa mno."Una maana gani,halafu mbona dada mimi sikufahamu,kwani wewe ni nani?" Nilimuuliza."Mi
mi ni Lilian sa....?" Kabla hajalimalizia neno hilo,upande wake wa nyuma niliuona mkia mrefu kama wa nyoka ukiishia ishia ndani,sijakaa sawa,Athumta nae huyu hapa.......


NILIOA NYOKA SEHEMU YA SITA (06).

Sijui kama macho yangu nilikuwa nimeyafumba ama nini ,maana sikuwa namuona Athumta wakati akija na sikujua alipitia mlango upi kunijia pale.Nilibaki nikimeza mafundo ya mate tu bila kumuongelesha chochote msichana huyo ambaye ninaweza sema ndiye niliyekuwa nimempanga aje kuwa mke wangu wa ndoa.Sasa mara baada ya binti Athumta kunijia ,alianza kunitazama usoni kwa muda kidogo kisha akanipa ishara ya mkono kwamba tuondoke.Kabla hatujaanza kuondoka,Lilian nae nilimuona kama kuna maneno mengine anatamani aniambie ila sikuwa na haja nae kwani niligundua nyuma yake kuna kitu mithili ya mkia wa nyoka nilikuwa nimekiona .Kwa kumtazama tu yeye hilo jambo hakuwa akilifahamu zaidi ya kujiona yupo poa tu."Luka,naomba uyazingatie maneno yangu ukiyapuuza utajuta".Alisema binti huyo kisha akageuka ili aanze kuondoka .....Aligeuka nikawa namuona vizuri upande wa nyuma lakini cha kushangaza ule mkia sikuuona tena na sikujua mkia huo ulipotelea wapi.Ghafla moyo ukaanza kunisukuma kumfuata Lilian lakini hapo hapo kuna kitu kingine kikaibuka kunishinikiza nisimfuate .Bila kutarajia nikawa nimemfuata Lilian tena kwa kumkimbilia kabisa.Nilimfikia nikawa namuita,akageuka nakuamua kunisubiri muda huo mikono yake akiwa ameiweka kiunoni."Samahani Lilian....nil.?" Sikuimalizia sentensi yangu ule mkia nikaanza kuuona tena.Niligeuka kimya kimya kumtazama Athumta nikamuona anatabasamu,nikaguna mwanamke wa aina gani huyu hana wivu kwani nilitaraji kumuona akiwa na hali ya wasiwasi lakini kitu hicho Athumta hakuwa nacho."Vipi Kaka Luka nasubiri uongee maana nahisi njaa".Alisema Lilian,binafsi nikahisi kama sentensi zangu zote zimevurugika.....sikumwambia chochote msichana huyo niligeuka nikaanza kuondoka .Nilitembea bila kuyapepesa macho kumtazama,nikajisemea acha nigeuke nimtazame,kugeuka kumtazama nikamkuta pale alipokuwa amesimamia bado hajadhubutu kuunyanyua hata mguu wake mmoja ina maana alikuwa akinitazama tena kwa macho yasiyokuwa ya Kawaida,sikuelewa lengo lake hasa lilikuwa ni lipi nikaamua nimpotezee tu nikanyoosha zangu kumfuata Athumta ili tuanze kuondoka.
Hatukupoteza muda tuliiendea gari tukapanda kisha safari ya kurejea nyumbani ikaanza.Basi baada ya kuondoka ndani ya maeneo ya kanisa tulifanikiwa kufika nyumbani kwa kina Athumta kwanza baada ya dakika kumi na tano kama kumbukumbu zangu hazijanidaganya.Maisha yalizidi kuwa mazuri sana kwa upande wangu,ujio wa binti Athumta kama mpenzi na mke wangu mtarajiwa ulionekana kuja na baraka za aina yake,kamwe baraka hizo sikujua kama zilikuwa zimetoka kwa Mungu kupitia Athumta ama kwa shetani ila kadri siku zilipokuwa zikisogea hapo ndo nilipokuja kubaini kumbe hayo yote yalikuwa hayaji bure bure bali yalikuwa na malengo yake maalumu kabisa.Takribani wiki mbili zilikatika Athumta kama ni kumchunguza kitabia nilimchunguza kwa akili yangu bila kushikiliwa na mtu nikadhamiria kumuoa Athumta pamoja na kwamba Lilian alikuwa akinisumbua na kunisihi nisifanye makosa au kudhubutu kumuoa binti huyo.....mie Lilian nilimuona kama msichana wa ajabu tu tena mchawi au jini nikayapuuza mashauli yake yote ili tu Athumta awe wangu wa maisha,sikujua kama walimwengu waliniroga ama nilijiroga mwenyewe kwani sikuwa tayari kumsikiliza yeyote yule atakaye nikalisha chini kwa kuniambia ubaya wa Athumta au madhaifu yake.Ilikuwa ni tarehe 10/7/2010 niliamua kumchukua Athumta na kusafiri nae hadi mkoani Shinyanga,kwa sasa mkoani Simiyu wilaya ya Bariadi kwa kipindi hicho ,wilaya ya Itilima kwa kipindi hiki kijijini kwetu Isagangw'ale kwa ajili ya kwenda kumtambulisha ili mipango ya harusi na nini ianze kufanyika.Huko nikaenda kuwakuta baba na mama wakiwa salama kabisa ila kwa maneno haya ambayo mama aliniambia sikumuelewa na nilimpinga kama sina akili nzuri vile.
"Mwanangu hivi kweli umekosa mwanamke wa kuoa unatuletea huyu? Hapana Luka huyu mwanamke sidhani kama anakufaa,achana nae".Hayo maneno,mama aliyazungumza hadharani mbele yangu mara baada ya kuniita pembeni."Mama,ila mimi huyu msichana ndo chaguo langu,kumuacha itakuwa ni vigumu mno mama angu labda nife lakini nikiwa hai kumuacha hivi hivi haitowezekana mama".Nilikataa katakata kabisa,kwani Athumta kwa kipindi hicho nilikuwa nikimuona kama Malkia machoni kwangu hivyo sikuwa tayari kumuacha kwani kama ni kufa nilikuwa nimekufa kwake tena na kuoza kabisa."Sawa wanasema mapenzi hayalazimishwi,sawa nimekuelewa Luka na hapo nilikuwa nataka kukupa ushauli wa bure tu......kama umemchagua huyo umuoe,sawa lakini....,acha nikomee hapo nisiongee sana".Mama aliyazungumza hayo huku akiipiga piga mikono yake mithili ya mtu anayepiga makofi nikampa moyo kuwa nimechagua fungu bora na Athumta wala asimuelewe vibaya atakuwa ni mke mwema na ndoa yetu itadumu milele na milele.Alinikubalia japo kwa shingo upande .Hilo likawa limemalizika,,,,Tuliondoka nyumbani kurejea Dar es salaam wiki moja baadae na kwa kipindi chote hicho tukiwa kijijini Athumta alikuwa akifanya shughuli zote zipasavyo kufanywa na Wanawake,kama ni kuchota maji visimani alifanya hivyo,kama ni kupika na kula mboga za majani za kienyeji mfano mrenda napo hakubaki nyuma.Kuosha vyombo na hata kujihusisha na masuala ya mavuno yaliyokuwa yakiendelea kwa wakati huo napo tulikuwa tukienda nae yaani kwa ufupi yale maruweruwe sikuwahi kuyaona tena nikaamini asilimia mia kuwa Athumta ni binti anayefaa kuolewa na kuwekwa ndani kama mke bora na mwema.Basi tukawa tumerejea Dar es salaam na maandalizi kwa ajili ya harusi yetu yakaanza kufanyika ......Hakika kwa maandalizi hayo ingekuwa ni harusi kubwa ya kutisha.Siku nne kabla ya harusi yetu kufanyika,mama Athumta alitoa ushauli na wosia wake kama mama .....Na inasemekana yeye hakuwa akimfahamu mwanae kiundani zaidi pamoja na kwamba alimzaa.
"Wanangu,,,,kabla hamjafunga pingu za maisha napenda niwaachie maneno haya.Ndoa ni zawadi kubwa sana kutoka kwa Mungu,,,Mkiwa ndani ya ndoa hamna budi kuheshimiana kwani bila heshima hakuna kitakachofanyika zaidi ya ndoa kuvunjika.....pendaneni na mshirikiane kwa moyo na mshikamano ili ndoa yenu ipate kudumu".
Hayo ndo maneno kutoka kwa mama Athumta,mama mwenye hekima zake.Kila mmoja wetu aliapa kutoyaacha maneno hayo ......Kila kitu kikawa sawa na hatimaye tukafunga ndoa yetu takatifu mbele ya mchungaji Samba mnamo siku ya tarehe kumi na nne mwezi wa nane,saa nne asubuhi mwaka huo wa 2010.
SIKU MBILI BAADA YA NDOA.
Nilianza kutomuelewa mke wangu Athumta kwani siku zote hizo tukiwa kitandani alikuwa akipenda kulala akiwa amevaa nguo .Yaani endapo asubuhi atavaa dera basi usiku atalala na dera lake hilo hilo,,,,kingine nikimgusia kuhusu suala la kuoga kwa pamoja ili kuinogesha ndoa yetu napo alikuwa akikataa na kunipinga kwa nguvu zake zote.
"Mume wangu,mimi sioni maana ya kuoga pamoja huo ni kama ushamba tu na ulimbukeni usiokuwa na maana yoyote ile,kwani kuna ubaya gani kila mmoja kwenda bafuni kuoga kivyake?"
"Hapana mke wangu,kumbuka hii ndo fungate yetu,sasa unapokataa kila nikuambiacho unaniumiza sana,,,unaniumiza mno Athumta mke wangu .Halafu jana na juzi ulikataa kufanya mapenzi kwa madai ya kwamba unaumwa,leo bila shaka utakuwa tayari ".Niliyasema hayo baada ya uvumilivu kunishinda kwani siku zote hizo mbili sikuwa nimewahi kumuona Athumta akivua nguo zake.Nilibaki kimya siku hiyo ya tatu yake nikawa namsikilizia tu kwamba ataniambiaje."Mume wangu naomba unipe angarau siku mbili mbeleni,tutafanya tu hicho unachokihitaji kwa sasa hivi sipo vizuri nina mambo mengi mazito yanayonisibu". Aliongea maneno hayo akazidi kuninyong'onyesha sana,,,mpaka nikawa najuta huyu mwanamke na urembo wake kwa nini ananihangaisha kiasi hiki? Nikajisemea poa nitajua cha kufanya.Wakati tukiwa na maongezi hayo kwa muda huo yalikuwa ni majira ya saa mchana kwenye saa saba hivi.Basi masaa yakawa yanasogea japo taratibu hatimaye usiku nao ukawa umewadia.Bado sikukata tamaa kumsihi mke wangu Athumta maana niliamini siku zote uvumilivu ndo nguzo na kukata tamaa upesi ni sawa na kuubomoa msingi wa nyumba.
"Mke wangu Athumta basi japo dakika moja tu nakuomba niuone mwili wako ukiwa hauna nguo nikiwa nazisubiri siku hizo mbili zimalizike".Nil
imsihi napo akanikatalia nikasema kwa leo sikubali hata kwa nguvu lazima nifanye nae mapenzi haiwezekani mimi nioe mke awe kama gogo au sanamu.Nilijiandaa vyema nikawa nimekamilika kila idara kuanzia nguvu pamoja na kiakili.Kwanza nilipanga akisema anaenda kuoga nitammendea kwa nyuma na hata kumchungulia kwa Siri humo bafuni lengo langu nipate kujua ni kitu gani anachoumwa au kinachomtatiza mpaka asivue nguo mbele ya macho yangu .Aliandaa chakula kama ilivyo ada,tukala kisha tukaelekea chumbani.
******************************
"Mume wangu nataka nikaoge sasa si unaujua vyema muda wangu wa kuoga ?" Aliuliza,nikamk
azia jicho la chini chini na kumjibu hapo hapo "Haina shida wewe nenda kaoge".Nilimjibu akaamua kusimama ili aanze kuelekea huko .....dakika tano baada ya Athumta kuondoka kwenda bafuni niliamua na mimi kutoka mule chumbani ili nimfuate huko kimya kimya bila ya yeye kujua wala kunishtukia.Niliufikia mlango wa pale bafuni nikasimama ili niangalie ni wapi napata mwanya wa kuchungulia.Nilihangaika sana kuutafuta huo mwanya mwisho nikaupata....ila sikuweza kumuona Athumta zaidi ya kusikia kiumbe kikubwa mithili ya samaki kikiyapiga piga maji,nacho sikuweza kukiona kwa macho.NILIOA NYOKA SEHEMU YA SABA (07)

Hofu ilizidi kutanda moyoni mwangu na amani nayo ikawa inatoweka,sikujua ni kitu gani hicho nikabaki naogopa tu.Niliwaza au kuna kiumbe cha kutisha kimemvamia Athumta na kummeza,mawazo yangu hayo yakaendelea kubaki kuwa kama kitendawili kigumu sana kukitatua.Niliondoka mbele ya mlango huo nikiwa nimenyong'onyea vya kutosha akili ikiwa imefeli na mapigo ya moyo yakienda mbio.Nilitembea nikiwa nimejiinamia hadi sebuleni nikafika hapo na kukaa,,huku mkono wangu mmoja nikiuweka shavuni.Sikukaa sana hapo,nilisimama nikaelekea chumbani nikaingia na kujitupa kitandani kiunyonge nikajaribu kulala ikashindikana.Niliwaza labda Athumta siyo binadamu wa kawaida nimeoa jini au jinamizi wazo hilo nikalifanyia uchunguzi nikaliona halina ukweli wowote nikaachana nalo.Nikakaa kitandani,kitanda pamoja na ukubwa wake na godoro lake zuri lakini nilihisi kama vile nimekalia misumari,nilisimama nikaanza kuzunguka zunguka,nikatoka tena humo hadi sebuleni.Nilifi
ka nikakaa chini baadae nikasimama na kukaa juu ya kochi dogo nikawa naendelea kuwaza.Mawazo yangu yalikuja kukatishwa na Athumta mara baada ya kumuona akija akitokea bafuni.Kwa wakati huo alikuwa amejifunga kanga moja kiunoni mwake huku mapaja yake meupe yakiwa nje nje.Kufumba na kufumbua mawazo yote yakatoweka ,furaha ikawika hapo hapo maana Athumta tangia nimuoe yapata siku tatu sasa sikuwahi kuuona mwili wake wa ndani zaidi ya kumuona akiwa amevaa madera tu au sketi usiku na mchana.Kitendo cha kumuona katika hali hiyo kikanipa matumaini huenda ameamua kubadiri msimamo wake wa awali na atanipatia penzi nililokuwa likiliwinda kwa udi na uvumba maana kwa kipindi hicho nilikuwa na hamu ya kufa mtu.Basi,Athumta akawa anasogea mbele,mara akaja kwangu na kisha kuunyoosha mkono wake wa kulia akanishika mkono wangu wa kulia pia akaninyanyua bila kuniongelesha chochote tukatembea kuelekea chumbani.Tuliingia chumbani,mke wangu Athumta akanisukumizia kitandani na kisha akaja juu ya kifua changu akiyarembua na kuyakodoa kodo macho yake utadhani ametafuna kungu.Alinibusu akaninyanyua juu na kunikumbatia......joto tamu kutoka kwake nikahisi likipenya hadi chini ya unyayo wangu nikawa naishia kujilamba lamba tu kwa haja na hamu kubwa."Leo nataka nikupe surprise mume wangu".Alisema Athumta nikatengeneza maswali mia ya kumuuliza hapo hapo ila swali moja tu ndo likapata nafasi "Surprise gani hiyo mke wangu Athumta?" Nilimuuliza akacheka na kutabasamu."Nipo tayari kufanya mapenzi na wewe muda huu".Aliponiambia tu hivyo,mzunguko wa damu ukawa kama umechochewa,rungu langu likadinda na kuchachamaa kama linataka kuvunjika.Nilimbeba Athumta nikamzungusha mara mbili kisha nikambwaga kitandani,tukaa
nza kubusiana hapo kwa muda huku tukigeuzana geuzana.Nilimchezea kwa pupa Athumta mpaka binti akaanza kulegea na kulainika mithili ya mboga ya bamia.Athumta akasanua kila kitu ikabaki kazi kwangu kama waswahili wasemavyo umetengewa chakula mezani ushindwe wewe tu.Akiwa anaachia sauti ya kugugumia ,nilichomoa nguo zangu zote nikamweka sawa baadae tukawa tumeufanya ule mchezo.Sikuamin
i kama Athumta angekuwa na tunda zuri na tamu kiasi hicho,utamu wa penzi nililolipata hapo haukuwa wa nchi hii ,nikatambua huenda alipokuwa akikataa kufanya tendo hilo kuna kitu kizuri alikuwa akiniandalia ambacho ndio hicho.Ya nyuma yote nikayasahau,mawazo mabaya juu ya mke wangu Athumta kwamba si binadamu wa kawaida niliyatupilia mbali nikawa namfikiria yeye tu kila dakika.Na hapo nikatambua huenda anayenifanyia maruweruwe hayo ni Lilian wala si mke wangu wa ndoa Athumta.Nilijaribu kuulinganisha utamu nilioupata na kitu chochote kile chenye utamu kama mapapai,ndizi nikakosa cha kuulinganisha kwani hata asali yenyewe ilikuwa haijafikia hata nusu.Kutokana na hamu niliyokuwa nayo........usi
ku huo nilipiga mabao matano mazito yote yakaishia ndani nikaridhika na hapo sasa nikawa sina kinyongo na mke wangu zaidi ya kuyaacha maisha yaendelee.Tulilala usingizi mnono sana mimi na mke wangu Athumta,na mpaka kunapambazuka hakuna kitu hata kimoja ambacho kilituharibikia.Asubuhi na mapema nikaamka ili nielekee chooni,choo cha ndani.Nilitembea haraka haraka kwenda humo chooni,,nikafika na kuingia maana mlango ulikuwa wazi.Sasa ile naingia tu humo ndani ghafla juu ya lile sinki jeupe nikaona vitu mithili ya magamba ya nyoka vimevunjika na kugawanyika gawanyika nikashtuka sana.Nikajaribu kuchungulia kwenye tundu nikaishia kuona maji tu."Mh? Nyoka ? Nyoka ametokea wapi tena?" Nilijiuliza nikapokelewa na ukimya,nikaamua kumuita Athumta ili na yeye aje ajionee.Athumta alipoingia tu,yale magamba ya nyoka hayakuonekana tena.
"Luka sasa hayo magamba ya nyoka yapo wapi?" Aliuliza Athumta nikawa nayapepesa macho huku na huko nisione hata lile doa moja la gamba."Mke wangu magamba menyewe yalikuwa hapa hapa,tena juu ya hili sinki".Nilimjibu akanipangusa usoni na kuniambia "Punguza mawazo mume wangu na uzikatae kabisa ndoto mbaya maana zitakuja kukuathiri kisaikolojia".A
lisema na akawa ametoka akaniacha mwenyewe mule chooni.Lakini mimi wala sikuwa naota wala nini bali madude hayo niliyaona kwa macho kabisa ila ikanibidi nimuelewe hivyo hivyo Athumta.Nilichuchumaa tayari kwa kujisaidia na sikuwa nimeyainua juu macho yangu,,,,kama nimeambiwa na mtu vile,nikayainua macho juu .Nilipoyainua tu kwenye lile dirisha la pembeni niliona kidude kimoja kinachofanana na uke ,nikasimama ili nikitazame vizuri,ile nasimama tu,kidude kile kikapotea katika mazingira ya kutatanisha.Nilishindwa nikimbie au nifanyaje nikabaki napua haraka haraka tu,,,,Vitisho kama hivyo nikavichukulia kama vitu vya kawaida maana Mimi tangu nikue nimelelewa kwenye Kijiji cha wachawi wadogo,wakubwa na hata wale wa kimataifa.Nilimaliza kujisaidia nikatoka kimya kimya mule chooni nikazipiga hatua hadi chumbani.
"Luka,humo chooni hujaona saa yangu?" Aliuliza Athumta nikamjibu sijaona saa yoyote ile hata ule mkanda wake tu nao sijauona,jibu hilo kwake likawa halijaeleweka akaamua kuniuliza kwa mara ya pili."Luka huko chooni hujaona saa yangu?" Aliuliza nikamjibu vile vile akaamua kusimama mwenyewe kuifuata saa hiyo.Dakika mbili tu nikamuona akiingia huku akiwa na saa kwenye mkono wake wa kushoto."Na hii? Mbona mimi nimeiona tena ilikuwa juu ya dirisha,macho yako mume wangu bila shaka yatakuwa na matatizo". Aliongea nikabaki kimya tu maana sikuona cha kumjibu nikajua labda macho yangu yana mawenge ukizingatia nilikuwa naamka kutoka usingizini.
"Haya mume wangu naomba uvae ili twende kwenye maombi". Aliongea na jambo hilo likawa geni kwangu kwani kitu maombi hata kukisikia tu nilikuwa sijakisikia."Maombi ya namna gani hayo mke wangu?" Nilimuuliza akatabasamu huku akiitizama saa yake aliyokuwa ameivaa."Ina maana maombi huyajui wewe? Tunaenda huko kwa ajili ya kumuomba Mungu atusaidie katika mahitaji yetu pamoja na mambo mbalimbali yanayotukabili".Alinijibu nikamuelewa tukaamua kutoka ili tuanze kuelekea kanisani kwa ajili ya hayo maombi.....Tulitumia gari ili tuwahi tusipoteze sana muda.Na kweli tukawa tumefika kanisani baada ya dakika kumi kumalizika yaani saa kumi na mbili na dakika kumi mara baada ya kuondoka pale nyumbani mishale ya saa kumi na mbili kamili.Huko tuliwakuta watu wengine kadha wa kadha akiwemo mchungaji Samba,Lilian pamoja na wengine lakini wakiwa wa kike wote ukimweka kando Mchungaji Samba.Tukaingia ndani na kisha kuenda kukaa.Nilianza kuyapepesa macho yangu huku na huko yakaja kutua juu ya meza moja hivi ndogo,juu ya hiyo meza nikaona Biblia kubwa imewekwa katikati huku ikiwa imezungushiwa vitu kama majivu hivi.Ila nikawa sina uhakika kama hayo yalikuwa ni majivu kweli au maua ya kawaida yanayofanana na majivu.Nikayatoa macho hapo nikawa naendelea kumtazama mchungaji Samba aliyekuwa akiendelea na taratibu za maombi.Dakika thelasini baadae,maombi yalimalizika watu tukatoka nje ili tuondoke zetu.Nikiwa nimeshikana mikono na mke wangu Athumta mara sauti ya kike nikasikia ikiniita,kugeuka nikamuona Lilian akija."Waooo!! Kama mapacha vile,hongereni,ni hayo tu nilitamani niwaambie hasa wewe Luka". Alizungumza Lilian kisha akageuka na kuondoka akatuacha tukimkodolea macho.
"Luka hivi huyu binti ni nani kwako maana ni muda sasa amekuwa akikuzoea sana ila omba nisijue kinachoendelea kwake yeye na wewe maana sitokuelewa na huo ndo utakuwa mwisho wa ndoa hii". Alisema Athumta nikamhakikishia sitofanya hivyo na huyo Lilian mimi simfahamu kiundani namchukulia kama mchawi furani tu asiyekuwa na lolote lile.Tulipanda gari tukawa tumerejea nyumbani."Mume wangu kaa unisubiri kidogo nikakuandalie maji ya kuoga".Alisema Athumta."Lakini mke wangu mbona humu ndani tuna wafanyakazi kwa nini ujisumbue kiasi hicho? Hata hivyo sioni haja ya mimi kuandaliwa maji nitaenda kutumia maji ya humo humo kwenye lile bomba la juu". Nilisema akakataa "Wewe ni mume wangu na kukuandalia maji ya kuoga ni wajibu wangu na siyo tatizo niache nikakuandalie maji ya kuoga". Aliongea nikaona nimkubalie tu hamna namna.Alielekea huko akawa amerudi baada ya dakika kadhaa kupita akanikaribisha vizuri kwa heshima zote nikaenda bafuni kuoga.Baada ya kuoga na kuwa nimemaliza nilitoka humo,,,,sasa wakati napita pale sebuleni nilishangaa mno kuona mazaga zaga juu ya meza kama chapati,chai ,mikate na vitu vingine nikajiuliza vitu hivi vimeandaliwa muda gani,,,nikakosa jibu .........niliyageuza kulia macho yangu nikamuona mke wangu Athumta akija na jagi la maji ,nikamngoja ili nimuulize maana ule muda niliokuwa nimeutumia bafuni haukutosha kuyakuta hayo yote ni dakika tano tu nilizitumia wakati naoga.
**************************
Na kuhusiana na maandalizi ya zile chapati napo nilikuwa na mashaka kwani wale wafanyakazi wangu sidhani kama walikuwa wameziandaa chapati hizo.
"Mke wangu Athumta!! Chai hii umeiandaa wewe au kina Mtashobya?" Niliamua kumuuliza ili anipe ukweli na kuniondolea utata kuhusiana na hilo."Ndio nimeziandaa mimi kulikoni?" Alijibu nikawa najihoji sana moyoni mwangu.Nilijihoji kwa sababu kitu hicho kwa hali ya kawaida kilikuwa hakiwezekani na hata angesema zile chapati alienda kuzinunua napo bado haikuwa ikiwezekana kwani umbali wa kutoka pale nyumbani kwangu kwenda madukani au migahawani ulikuwa ni wa dakika kumi mpaka kumi na tano."Mbona hivyo mume wangu kulikoni?".Alinishtua baada ya kuniuliza swali hilo."Poa tu mke wangu nilikuwa nawaza namna ya kukutunza mke wangu".Nilijibu nisichokijua yaani kwa maneno hayo nilijikuta nikiyatamka bila kutarajia.Basi nikaamua kuachana na mawazo hayo nikawa napigia mahesabu huenda Athumta alitumia gari kwenda kununua mazaga zaga hayo.Mke wangu sasa akaninawisha nikaanza kuinywa ile chai ,,,nilipomaliza kikombe kimoja tu mara mdomoni karibu na koo nikawa nawashwa na vitu vichungu,dawa si dawa,pilipili si pili pili.NILIOA NYOKA SEHEMU YA NANE (08).

Sijui vilikuwa ni vitu gani hivyo sikuvielewa kwa kweli,,,,sikuendelea kulikalia sofa langu niliinuka haraka nikawa nakimbilia nje kwenda kuitema chai nyingine iliyokuwa imesalia kinywani ili nisitaabike.Nilifanya hivyo baadae nikachukua maji nikawa najisafisha sana mpaka ule mwasho ukatoweka,baada ya mwasho huo kutoweka nilirudi ndani nikaenda kuketi pale pale nilipokuwa nimeketi.Mara nikageuka na kumuona Athumta akinitazama kwa macho ya tofauti yenye kuashiria lile jambo hakulifurahia na isitoshe alionekana kununa.Niliacha kumtazama nikainuka taratibu nielekee chumbani,nilitembea nikaufikia mlango ila nikasita kuingia nikabaki nimesimama tu kana kwamba nimewekewa kizingiti miguuni.Niligeuka kurudi tena sebuleni nikawa nimeghaili kuingia humo chumbani kwani niliamini mke wangu atakuwa amechukia au amekasirishwa na kitendo ambacho nilikifanya hivyo kumuacha hivyo hivyo bila kumuondoa katika hali hiyo amani itapungua,basi nikawa nimerudi na kisha kwenda kukaa karibu nae .....Nilimtazama usoni kwa muda,akayachengesha macho yake na kuuvuta mdomo."Mke wangu,samahani ndani ya chai niliyokuwa nikiinywa nilihisi kuwashwa mdomoni na ndio maana ukaniona nimefanya hivyo samahani sana".Niliongea lakini Athumta akaonekana kutonielewa hata kidogo,hakuendelea kukaa pale alisimama akatoka nje.Nilishindwa kuamini kama kitendo cha mimi kuitema ile chai ndo kimemchukiza kiasi hicho ama kuna jambo jingine chini ya kapeti lilikuwa limejificha.....kwa vile nilikuwa nikimpenda niliamua kukubaliana na hali halisi,kama nikumbembeleza nilikuwa radhi kufanya hivyo na hata kumsikiliza tena kwa chochote kile atakachonisihi.Nilimfuata huko nikamkuta amekaa chini nyuma ya lile jengo akilia."Mke wangu ina maana ndo umekasirika kiasi hiki,basi kama nimekukwaza naomba unisamehe kwani nilipitiwa tu nikaamua kufanya jambo hilo,nisamehe mke wangu".Nilianza kumuomba msamaha akawa haongei chochote zaidi ya kuendelea kulia tu.Aliponyamaza kidogo alinitizama kwenye paji la uso wangu akatikisa kichwa chake "Luka leo ndio nimeamini kumbe wewe hunipendi,hunipendi Luka na sijui ni kwa nini niliamua kuolewa na wewe bora nirudi kwetu tu". Aliongea hayo kwa sauti ya kwikwi akanichanganya mno mpaka nikawa naongea visivyoongeleka kumbembeleza,,nilimbembeleza kwa kadri ya uwezo wangu kwa bahati nzuri akanielewa ila akanisihi ile chai ni lazima nikaendelee kuinywa.Niliamua kumkubalia tu sikuwa na jinsi kwani kama ni maji tayari nilikuwa nimeshayavulia nguo.Tulishikana mikono,tukawa tumerudi ndani...... Athumta akakaa pembeni kunitazama jinsi ninavyohangaika kuinywa ile chai.Kwa mara hii chai haikuwa na mwasho tena badala yake ikawa chungu kama imewekewa panado.Yaani sijui ni nani tu ambaye alikuwa ameniroga kwani kwa jinsi nilivyokuwa nikimsikiliza mwanamke huyo hata kama angeniambia ninywe maji ya upupu sidhani kama ningekataa,kwa kifupi nilikuwa limbukeni wa mapenzi kwa binti Athumta.Basi chai nikainywa kwa kujikaza mpaka nikawa nimefanikiwa kuimaliza.
"Asante kwa chai mke wangu".Nilimshukuru akawa amefurahi mno maana mara hii tabasamu lilikuwa likimtoka ."Asante nawe mume wangu wa ndoa hakika wewe ni mume bora na ndio maana huwa sichoki kukupenda".Alisema Athumta na baada ya mambo yote kumalizika niliagana nae nikafunga safari ya kuwahi kazini.Kutokana na muda kuendelea sana ,niliona ni bora nitumie gari,nikaichukua gari yangu nikawa nimeondoka pale nyumbani.Nilikuja kufika kazini baada ya dakika zipatazo kumi kukatika nikaipaki gari kisha kushuka na kuanza kuelekea ofisini kwangu .Sasa nilipoufikia mlango wa kuingilia,nilisimama ili niufungue,kawaida yangu ya siku zote ilikuwa ni hii......kila nikifika hapo kabla sijaufungua huo mlango huwa nalitaja jina la Marehemu Babu yangu Madiro mara tatu,,,cha ajabu kwa siku hiyo sijui nilisahau sijui nilipitiwa kwani nilijikuta nikiufungua mlango bila kulitamka jina hilo la Marehemu Babu yangu kama Mila na Desturi za ukoo wetu pindi tunapotaka kufanya kazi yoyote ile.Mpendwa msomaji kwa muda huo bado sikuwa nimeokoka hata ile robo tu pamoja na mke wangu Athumta kunishawishi mpaka nikashawishika walau hata kwa kwenda kanisani.Basi mule ndani ya ofisi nikawa nimeingia,nilipokikalia tu kiti cha humo ofisini,nilishtuka baada ya kukumbuka nimeingia bila kulitaja jina la Babu nikatoka haraka na kuufunga mlango ili nilitaje.....Ni
lilitaja mara tatu nikaufungua mlango nakujifakamia jumla jumla ndani nikakaa.Nilipokaa tu ghafla nikaanza kuhisi hali ya uchovu kila kazi ambayo nilipanga kuifanya niliiona ngumu kinoma.Hata ile ya kupanga mafaili na kuyapangua nayo niliiona ni kazi moja ngumu sana.Nikajiuliza ni kipi kimenipata tena au nimechoka baada ya kudrive gari kutoka nyumbani kuja hapo ofisini,daah!! Hali hiyo ikawa na utata usiojulikana.Mara usingizi nao ukaanza kuninyemelea nikasema hebu ngoja nilale huenda ni uchovu wa kawaida tu nikiamka kila kitu kitakuwa vizuri.Nilikisogeza pembeni kiti changu karibu kabisa na ukutani nikakiegemea nikalala fofofo.Nikiwa ndani ya usingizi mzito wa kifo kama ndoto vile nilianza kuhisi pale mlangoni kuna kiumbe kikubwa kinautikisa maana vishindo vilikuwa vikisikika.Nikakurupuka na kuyafumbua macho.....Niliyafumbua kwa hali ya uhiari kabisa lakini kwa kile ambacho nilikiona pale mlangoni nilitamani nizimie au nife kabisa kabla hakijaanza kunisogelea.Nilihisi kama nipo ndotoni kwani katika maisha yangu yote sikuwahi kumuona nyoka yoyote yule mwenye uwezo wa kusimama kama kiumbe mwenye miguu tena miwili.Ni aina furani ya nyoka mkubwa sana ,mnene mithili ya Kobra nilimuona amesimama pale mlangoni huku akiwa ameachama akinitishia kunimeza.Uvumilivu kwa hapo ulinishinda uoga ukaniingia nikaamua kupitia dirishani nikawa napiga makelele ya nguvu .
"Boss,simama tafadhari,kuna nini boss mbona una kimbia?" Ni sauti ya mfanyakazi wangu mmoja ilisikika kwa nyuma ikiyatamka hayo baada ya Mimi kuonekana nikitimua mbio.Nilisimama umbali wa mita ishirini huku nikiwa nahema juu juu."Boss kulikoni tena?" Aliuliza mfanyakazi huyo baada tu ya kunikaribia,,kabla sijamjibu kumbe kuna wafanyakazi wengine waliyasikia makelele yangu na wote wakaamua kutoka maofisini kwao na kunijia pale nilipokuwa nimesimama."Boss kulikoni.....Nini kimekupata boss?" Kila mmoja akawa ananiuliza swali lile lile la nini kimetokea.Nilivuta pumzi ndefu nikazishusha kwa nguvu "Jamani siyo kwamba mimi ni kichaa,hapana jamani bali kuna kiumbe cha ajabu nimekiona ofisini kwangu,kiumbe ambacho tangu nizaliwe sijawahi kukiona popote pale".Niliwaambia huku nikitetemeka ndani kwa ndani hofu ikiwa imeuteka moyo wangu."Boss kiumbe gani hicho?" Waliniuliza."Sijui ni nyoka sijui ni kitu gani hata hakieleweki isitoshe kina miguu,twendeni mkajionee wenyewe".Nilipo
yazungumza hayo muda huo huo tuliongozana kuelekea huko.....Cha kushangaza baada ya kuingia ndani ya hiyo ofisi yangu kile kiumbe hakikuonekana na haikujulikana kilipotelea wapi.
"Boss mbona hicho kiumbe hakionekani kipo wapi boss?" Waliniuliza baada ya kukitafuta kiumbe hicho bila mafanikio."Kilikuwa hapa hapa.... kilikuwa hapa hapa".Niliwajibu ikabidi wanitulize maana walinisoma kisaikolojia."Boss tulia wala usiwe na mawazo,mimi nadhani achana na mawazo ya kuwaza sana.....sijui kuwawaza wachawi sijui walozi hayo yatapunguza utendaji kazi wako,humu hakuna nyoka wala nini bali ni mawazo yako boss uliwaza hivyo mwisho ikajitengeneza picha isiyokuwa na uhalisia". Alizungumza mmoja wa wafanyakazi wangu ikabidi nitulie.Waliondoka humo wakawa wameniacha peke yangu,nilijikaza nikayapotezea mawazo hayo nikaendelea na kazi.Masaa yalisogea mpaka muda wa jioni ukafika.......Saa kumi na moja kamili ilipotimia nilirudi nyumbani.Huko nikamkuta mke wangu Athumta anaosha vyombo huku wale wafanyakazi wa ndani wakiwa wanasukana,kitendo hicho kikanikwaza sana,nikaamua kuwafuata ili wakaniambie vizuri ni kwa nini wamekaa tu hawafanyi kazi,kazi zote wamemuachia mke wangu ili hali wanalipwa.
"Viviana ,sasa kwa nini mmekaa hamfanyi kazi? Mnataka niwaeleweje mimi,,,,kila mwisho wa mwezi nawalipeni mishahara tena bila kuwacheleweshea,,,sasa iweje kazi zote mpaka za kuosha vyombo mmuachie mke wangu?" Niliyasema hayo wakawa wananitazama kwa huruma ."Ni kweli boss lakini wifi hapendi sisi tuzifanye hizo kazi......kila tukimwambia aachane nazo anakataa na kusema hakuja hapa kukaa bali kufanya kazi kwa ajili ya mumewe ambaye ni wewe .Na isitoshe hata kupika ametukataza kwa kutuambia hiyo kazi ya kuandaa chakula cha mume wake aachiwe yeye kazi hiyo isiguswe na mtu yeyote yule".Alisema mmoja wao nikawa nimewaelewa kwani mke wangu akili zake za ubishi nilikuwa nikizijua mwenyewe tu .Niliamua kumfuata Athumta sehemu ambako alikuwa akioshea vyombo,,Nikasalimiana nae kwa ufupi kisha baada ya hapo nikaingia ndani kwenda kupumzika.
Masaa ya usiku yaliwadia,kabla ya kulala mara baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku nilimshirikisha mke wangu kuhusiana na kile kiumbe cha ajabu ambacho nilikiona kazini hadi kupelekea kunitoa katika hali ya kawaida ya ufanisi wa utendaji kazi.
************************
"Mke wangu leo asubuhi kule kazini niliona kiumbe cha ajabu sana tena kikiwa kimesimama wima kama binadamu hivi,yaani kinafanana kama nyoka mmoja mkubwa aina ya Kobra , kiukweli mpaka sasa nikikitafakari naishia kutetemeka".Niliongea,Athumta akawa ananishangaa."Hivi mume wangu ni lini utaacha fikra zako hizo potofu?". Aliuliza Athumta.
"Siyo fikra potofu mke wangu Athumta,ni kweli nilimuona huyo kiumbe na alikuwa akitisha mno unaweza usiamini ila huo ndo ukweli halisia,yaani kwa yule kiumbe hata wewe ungemuona usiku wa leo usingelala".Nilimjibu lakini bado akawa anaona kama namtania vile."Achana na mawazo hayo Luka,unajua sisi ni wakristo na tunamjua Mungu,sasa mambo kama hayo ambayo hata hayawezekaniki ni ya kuyatupilia mbali tu hakuna haja ya kuumiza akili......Hebu tulale mume wangu,mengine ni ya kuyaacha tu". Aliongea nikaona kuendelea kumgusia jambo asiloliamini ni kupoteza muda,niliachana na jambo hilo tukawa tumelala.Mwanzo tulilala vizuri tu lakini kadri masaa ya usiku yalivyokuwa yakizidi kusogea ndipo hali ya hewa ilivyoanza kuharibika.
Kwenye saa saba za usiku mara nje nilianza kusikia kama kuna mtu ananiita tena kwa sauti nzito ya kiume."Luka.....Lukaaaa!! Huu siyo muda wa kuendelea kulala ,amka.....amka.
....amkaaa!!!".


NILIOA NYOKA SEHEMU YA TISA (09).

"Ukidhubutu kuendelea kulala hakika kifo chako kinakaribia na utakufa kifo kibaya sana".Hiyo sauti ya mwangwi na nzito kupita kawaida iliniogopesha mno mpaka nikawa natetemeka kwa kuyagongesha meno yangu.Usingizi ulikatika wote nikawa naishia kujiuliza ni nani huyo anayeniita na kuniambia maneno makali na ya kutisha kiasi hicho,akili ikanituma ,moja kwa moja nikajua hilo ni jinamizi limekuja kwa ajili ya kunitisha.Niliamua kukaa kitandani na sikuwa na hamu tena ya kuendelea kulala kwani akili yangu yote ilihama harufu ya hofu ikawa inauzunguka moyo wangu.Nikawaza ni wapi nilipokwama? Au ni nani ambaye nimemkosea hadi nikawa nayapata hayo? Hakika nilikosa majibu.... yote kwa yote nikabaki kusubiri ni nini kitatokea maana hata nguvu nazo zilikuwa zimeshaanza kuniishia tena kwa kasi ya ajabu.Niliendelea kutetemeka nikajikaza nikasimama......niliposimama tu,ghafla nikaanza kuumwa tumbo yaani kwa jinsi tumbo lilivyokuwa linajisakama kwa ndani maumivu yake utadhani kulikuwa na mtu alikuwa akiuchinja au kuunyonga utumbo.Kwa maumivu hayo nilishindwa kupumua vizuri nikawa nalia tu tena kwa sauti ,na kitendo hicho kikamuamsha hadi mke wangu Athumta.Akaamka na kunikuta nikilia,akanikazia macho "Mume wangu vipi,kwa nini unalia?" Aliuliza hilo swali ,nikamtazama kwa huruma "Tumbo mke wangu,tumboo".N
ilimjibu nae bila kunirudishia neno lolote akaamua kuunyosha mkono wake wa kulia akalipapasa papasa tumbo kwa muda wa dakika tano hivi.Mara yale maumivu yakatoweka nikaanza kuhisi raha na msisimko .Tabasamu likanijaa usoni mwangu."Tuendelee kulala mume wangu,vitu hivyo ni vya kawaida sana,tumbo ni ugonjwa mmoja wa kawaida mno na dawa yake ni hii lakini siku nyingine ukihisi unaumwa tumbo usimuambie mtu mwingine akupapase mwenye hiyo dawa ni mimi pekee hivyo unatakiwa ulizingatie hilo na usilipuuze,sawa Luka?" Alisema Athumta na mimi kama bendera fata upepo nikamkubalia kwa hicho ambacho alikizungumza.Basi tukalala.......Nusu saa baadae ghafla hali ya hewa mule chumbani ikaanza kubadirika kwa mara nyingine tena.Mara hii nilianza kuhisi kama kuna watu wakanong'onezana karibu na kona ya mlango,,,,nikayafumbua macho lakini wala hakukuwa na chochote nilichokiona zaidi ya taa tu ambazo kwa muda huo zilikuwa zikiwaka.Nikahi
si labda nilikuwa naota hivyo hilo jambo nikaachana nalo nikaendelea kulala.Nililala sijui yalikatika masaa mangapi,ghafla ile sauti ya mwanzo nikawa naisikia ikiniita.
"Luka....Lukaa....Luka,,,huu siyo muda wa kuendelea kulala....amka....amkaa...amka
aa,ukidhubutu kuyapuuza maneno haya hakika kifo chako kitakuwa ni kibaya sana.....narudia tena kifo chako kitakuwa ni kibaya sana".Aisee nilitamani niombe yaani nianze kukemea lakini uwezo huo sikuwa nao kwani bado nilikuwa sijampokea Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yangu.Imani pekee ambayo nilikuwa nayo iliwategemea waganga na mababu kwa kipindi hicho .Sasa ile sauti ilipomalizika sikujua ambacho kiliendelea maana fahamu nilipoteza nikawa kama mfu vile.Katikati ya giza nene nilikuja kuzinduka nikiwa na shuka jeupe na sikujua ni nani alinifunika shuka hilo halafu mwili wangu wote ulikuwa ukitoa harufu kali mithili ya kiumbe aliyeoza.Nikajaribu kuyaangaza macho yangu kuitambua ile sehemu lakini hakuna nilichoambulia maana sehemu hiyo haikuwa na mwangaza wowote na hata mbingu nayo haikuwa ikionekana macho yalikuwa yakiona kwa hisia hisia tu,,,Mzunguko wa giza jeusi ndo uliokuwa umetamalaki eneo hilo.Nilikaa nikajaribu kupiga kelele lakini kelele hizo hazikufika popote."Nipo wapi hapa jamani? Nipo wapi ?" Nilijiuliza maswali hayo nikaja kujibiwa na sauti kali ya kike ila mtu mwenyewe hakuwa akionekana "Upo ndani ya himaya ya watu wa nyoka ,,, kwa sababu umemuoa Malkia wa Majoka duniani" ilisikika sauti hiyo nikawa natetemeka kama kinda la ndege lililo nyeshewa mvua.Lile shuka nalo likaanza kuwa mzigo kwangu kwani ile harufu ilikuwa ikiongezeka maradufu kila baada ya muda mfupi tu.Sijakaa vizuri nilianza kuvutwa kwa nguvu na kitu kisichoonekana yaani kama vile napeperushwa na upepo nikaenda kutupiwa ndani ya matope meusi yenye harufu kali ya kinyesi nikazama humo mzima mzima.Kiukweli kwa eneo hilo nilijua sitapona nitakufa tu, nikiwa natapatapa kujaribu kujiokoa ,,,Kilikuja kijidubwana nisichokijua ndani ya hayo hayo matope kikapanda kifuani kwangu na kupotea,,,nilikihisi tu kwani sikuwa naona kutokana na macho yangu kuzibwa na yale matope.Sasa kile kijidubwana kilipotoweka,ni
lijikuta nimerudishwa eneo lile la awali lililokuwa na giza lakini mara hii likiwa na kijimwangaza hafifu kisicho cha mbingu kwani mbingu au mawingu yalikuwa hayaonekani bado,,, Sasa kwenda kujitazama mikononi mwangu tayari rundo la funza waliokuwa wakizunguka zunguka niliwaona wametapakaa mikononi mwangu.Nikajaribu kuwatoa ikashindikana..
......Ghafla funza hao wakaanza kukua huku wakibadirika,na hazikupita hata dakika mbili wakawa nyoka wengi wadogo wadogo.Sikuwa na nguvu za kulia wala kupiga kelele kwa muda huo zaidi nilibaki nikiwatazama tu jinsi nyoka hao walivyokuwa wakiuzunguka zunguka mwili wangu.
"Luka kurudi tena duniani sahau kesho utapelekwa rasmi kwenye ulimwengu wa majoka watu kwani kile ambacho nilikuwa nikikitafuta nimeshakipata".Sauti hiyo niliisikia vizuri na nikaitambua vyema kama ndo sauti ya Athumta,nikaogopa mno.....macho yangu yakawa kama yamefumbuliwa,kumbe eneo hilo lilikuwa limezungukwa na majoka watu.Yaani maana halisi ya majoka watu ilikuwa ni hii......Majoka watu walikuwa na maumbo ya aina tatu,,,maumbo ya watu,maumbo ya nyoka wenyewe na maumbo ya samaki.Basi wale majoka sasa nikawa nawaona kwa uzuri.....Kuanzia chini hadi kiunoni walikuwa na muonekano wa binadamu wa kawaida lakini wakiwa uchi ,juu kuanzia kifuani hadi kichwani walikuwa na muundo wa nyoka....walivyokuwa wanatisha hakika ndugu yangu ungewaona ungekufa hata kabla ya muda wenyewe wa kufa.Niliyazungusha macho nikamuona Athumta kama alivyo tena akiwa na mwili wake wa kibinadamu nikashtuka.
"Athumta...... Athumta!! Ina maana kumbe wewe ni joka?" Sikujua ujasiri wa kuliuliza hilo swali niliutoa wapi ukizingatia sehemu hiyo ilikuwa ikitisha na mambo yalikuwa hayaeleweki."Un
auliza!! Mimi siyo binadamu wa kawaida bali mimi ni joka mtu ukoo wangu umetokana na majoka na ndio maana nipo hapa".Nilitamani nimwambie ayarudie maneno hayo ila nikakosa ujasiri wa kumwambia afanye hivyo.
Kwa mbali lilionekana joka mtu moja likinijia kwa mwendo wa haraka na kadri lilivyokuwa likinisogelea na ndivyo ule mwonekano ulivyokuwa ukibadirika.Mara akawa binadamu....nik
amtazama vizuri binadamu huyo nikamtambua kuwa ndiye yule mchungaji ambaye alinifungisha ndoa mimi na Athumta wiki nne zilizopita na kwa jina lake watu walimfahamu kama mchungaji Samba.
"Hahahaha!! Kunguru siku zote huwa hanaga uwezo wa kutua juu ya kinyesi bali uwezo wake ni kutua nchi kavu kwenye neema......Luka kule duniani mpaka sasa umeshamaliza mwaka mmoja haupo,na watu wanatambua wewe umeshafariki mali zako zimeshachukuliwa na nduguzo na isitoshe umeshasahaurika sasa kaa ukilijua hilo.Wahenga wanasema ukilipenda uwa penda na boga lake,,,,Bila shaka kwa hapo wewe unajua umelala,ila haujalala bali umekufa,ulikufa kwa ajali mbaya ya gari".Jamaa huyo alizungumza nikawa nalia kwa uchungu ...
*************************
"Haa nimeota ndoto gani hii,ndoto gani hii jamani?" Nilijiuliza maswali hayo baada ya kuzinduka pale chini karibu na mlango wa chumba changu nilipokuwa nimezimia mara baada ya kuisikia sauti ile.Nilisimama taratibu nikaufungua huo mlango na kutoka kwa mwendo wa kunyata kuelekea sebuleni huku mapigo yangu ya moyo yakienda kasi kwani ile ndoto ya kutisha ilinivuruga mno,,,,nilizunguka zunguka pale sebuleni kwa muda baadae nikarudi chumbani.Nikayainua juu macho yangu kumtazama Athumta pale kitandani.Nikamuona yupo hoi anakoroma mimi hofu ikawa ni kubwa na kiukweli nikaogopa hata kulala nae kitanda kimoja.Sikukaa humo chumbani nilichukua shuka langu nikatoka kuja sebuleni ili nilale hapo.Kabla sijalala,niliusikia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa nikageuka kuutazama nikamuona Athumta akitoka huku akiwa amejifunika kanga moja.....Mimi nikaanza kurudi rudi nyuma maana nilianza kumuogopa kutokana na ile ndoto maana ndoto hiyo haikuwa na fumbo wala chenga,ilielezea watu wale wale na sauti zao zile zile.Ile hali ya mimi kusogea sogea nyuma ilimshtua Athumta."Mume wangu vipi,mbona sikuelewi?" Aliuliza Athumta lakini sikumjibu kwani kama ni ukweli nilishaanza kuuelewa kuwa binti huyo huenda si wa kawaida tena.
"Mume wangu vipi mbona sikuelewi? Nimekuja kukuambia hivi ,nina...nina"...Kabla hajamaliza kuyaongea hayo, hapo hapo alianguka chini akafumka na kuwa chatu mkubwa.Nililikanyaga sofa la pembeni ili nikimbilie nje lakini pale mlangoni nilimuona Athumta amesimama akinicheka kwa nguvu,nikageuka nirudi nyuma napo nikamuona akinijia huku yule chatu nae akijiburuza kwa kasi kunisogelea..


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI (10).

Nilishindwa nikimbilie wapi au nielekee wapi ....Nilibaki nimesimama pale Pale nisiyaangaze macho yangu kulia ama kushoto,yule Athumta wa pale mlangoni nae akawa ananifuata kwa mwendo wa kunyata huku akitema mate yenye mchanganyiko wa damu,,,Meno yake nayo yalikuwa yakitisha mno kwani yalikuwa ni marefu mithili ya misumari ya nchi tano.Athumta wa nyuma nae alianza kufanya hivyo hivyo ina maana wote wawili wakawa wananifuata kwa pamoja.Nililegea ,miguu yangu ikawa inatetemeka kwa kugongana nikajikuta nakaa kwenye kochi moja bila kutegemea,nikajisemea kama nikufa acha tu nife kwani sikuwa na namna ya kufanya.Nilimuacha yule chatu nae kama anafanya yake basi afanye ,yaani kwa kifupi nilijikatia tamaa.Sasa baada ya hao viumbe wa ajabu kunikaribia huku wakinitishia niliamua kuyafumba macho yangu.Nikiwa nasubiria muujiza usiojulikana mara nafsi ikaniambia niyafumbue macho nitazame kunako upande wangu wa kushoto.Nilisita sita kidogo kwa woga baadae ikabidi niyafumbue tu macho yangu,ile nayafumbua Athumta tayari alikuwa amebakiza hatua chache kunifikia na kwa jinsi alivyokuwa akionekana alidhamiria kuniangamiza pale pale kwa kuivunja vunja mifupa yangu.Ghafla moyo ukapata ujasiri,nikageuka kushoto kwangu nikakiona kitabu kimoja chenye kasha jeusi nikakitambua huenda hicho kikasha kimebeba Biblia, maswala ya kuanza kujiuliza hicho kitu kimetoka wapi niliyaweka kando kwanza .Kwa nguvu ya ajabu nilisimama nikamkamata Athumta Joka wa mbele nikamkaza kwa nguvu ,hapo hapo kikasikika kilio kikali akatoweka na kuniachia alama ya damu mikononi mwangu.Athumta wa nyuma nae nilimsikia ameangua kilio nilipomgeukia sikumuona na sikujua alitowekea wapi.Joka nalo katika mazingira ya kutatanisha niliripuka na kusambaa likakombwa na upepo wa kisurisuri usiokuwa na chanzo maalumu likatoweka,hali ya hewa ikarudi kama ilivyokuwa hapo awali.Nilishusha pumzi za haja na hapo ndo ikawa mara yangu ya kwanza kumshukuru Mungu pamoja na kuujua ukuu wake kwani kwa hali ilivyokuwa tayari ningeshakuwa marehemu au kupotezwa na hao mashetani katika mazingira ya kutatanisha.Nilitembea taratibu nikawa nimekifikia kile kikasha nikakibeba bila woga na kisha kukikumbatia kifuani.Nilipokishusha na kukiweka kwenye kochi kumbe ilikuwa ni Biblia na niliiona vizuri kwa mara hii.Sikuwaza sana nikaibeba tena na kuamua kuelekea chumbani.Mara hii sikuwa na hofu yaani nilikuwa siogopi na sikujua ule ujasiri niliupatia wapi.....Basi nikiwa na ile Biblia yangu ya maajabu nilianza kuzipiga hatua kuelekea huko chumbani.Nikaufungua mlango niingie.Niliufu
ngua nao ukafunguka nikawa nimeingia humo,,cha kushangaza pale kitandani sikumuona tena Athumta zaidi ya kuona damu damu tu kitandani zikiwa zimetapakaa kila mahali .Nilijitoa ufahamu yale mashuka nikayavuta na kisha kuyashusha chini nikakaa pale kitandani.Usingizi wote uliyeyuka nikawa nimebaki nimekaa tu bila kazi ya kufanya .Nilitoka humo chumbani nikaelekea sebuleni na huko ndiko nilikopata usingizi hadi kukapambazuka.Mapema sana baada ya kupambazuka sikuwa na amani wala raha hata hamu ya kwenda kazini nayo ilikuwa imekatika nikaamua nibaki tu nyumbani niangalie cha kufanya maana sasa Athumta si mke wala si binadamu wa kawaida na isitoshe ametoweka kimiujiza.Nilitaka hilo libaki kuwa siri yangu asiijue mwingine.....Nilipanga kutomuambia mwanadamu yeyote yule kwamba Athumta ni jini yaani joka .Saa moja na nusu mishale ya asubuhi niliingia bafuni kuoga,,,nikaoga japo kwa mawazo nikawa nimemaliza kuoga.Nilitoka bafuni nikitikisa kichwa njia nzima hadi chumbani."Hivi ni kweli Athumta ni jini au naota?" Nilijiuliza swali hilo nikaona hakuna atakaye nipatia jibu nikaamua kubaki kimya mithili ya maji ya mtungini.Mawazo mfululizo yasiyokoma yakaanza kuniandama kila dakika.Sikujipaka mafuta wala nini,nilivaa hivyo hivyo nikatoka humo na kurejea sebuleni nikakaa hapo kimya,mkono wangu mmoja ukiwa shavuni.Sikujua ilienda endaje tu kwani katika mazingira nisiyoyatarajia nilisinzia nikaja kukurupusha na sauti ya kike ikiniita,
"Boss....Boss....Boss?" Baada ya kuyanyanyua macho yangu juu nilimuona Nancy mfanyakazi wangu wa ndani akiwa amesimama huku akinitizama kwa macho ya huruma,nikaguna kidogo na kisha kumkazia macho,nikavuta pumzi "Niambie Nancy!!".Nilizungumza kwa sauti yenye mkwaruzo.
"Boss chai tayari".Alisema Nancy."Daah!! Chai?" Nilimuuliza."Ndio boss,chai tayari".Alijibu."Kwa sasa mbona sina hamu ya kunywa chai?" Nilimuuliza kana kwamba sijui kinachoendelea tumboni kwangu."Kwa hiyo boss una maanisha hunywi chai leo au?" . Aliuliza Nancy."Ndio kwa leo sinywi chai naomba mniache kidogo". Nilizungumza kisha Nancy akageuka ili aondoke mbele yangu,alifanya hivyo haraka akawa ameondoka .Nilibaki peke yangu pale nikiwaza mwisho nikaamua kuelekea nje nikaone cha kufanya.Mpaka inatimia mishale ya saa saba za mchana bado sikuwa nimekula chochote hadi wafanyakazi wangu pale nyumbani wakaanza kunishangaa huku wakijiuliza ni kipi kimenipata lakini pamoja na hayo hakuna hata mmoja ambaye nilimuambia ukweli.Katikati ya jua kali la utosini niliamua kwenda kujipumzisha ndani ya bustani yangu ya maua ......nikafika hapo na kujilaza chini dakika zikapita usingizi usiokuwa na kipimo ukaniijia.Sasa baada ya usingizi huo kunipitia niliota ndoto moja ya kusisimua ambayo nilishindwa kabisa kuitafsiri.
Niliota nikiwa nimesimama karibu na mto mmoja wenye maji ya mawimbi na maporomoko mazito huku kunako sehemu ya mkono wangu wa kulia na kushoto nikiwa nimefungwa kamba furani hivi nyeupe zinazofanana na mikufu.Kila nikijaribu kuzifungua hizo kamba zilikuwa hazifunguki na wakati mwingine hata kama zitafunguka basi zinajifunga zenyewe.Nikajaribu kutazama pande zote kuona kama kutakuwa na mtu wa kunisaidia pale kwani hata miguuni nako nilikuwa nimefungwa na kwa eneo hilo nililokuwa nimesimamia lilibaki suala la muda tu niweze kudumbukia mtoni kwani lilikuwa limemeguka mno na maji nayo yalikuwa yakizidi kulipiga kwa nguvu huku mengine yakiruka hadi juu ya uso wangu.Kupiga kelele nako sikuwa na uwezo huo maana sauti yote ilikuwa imekatika.Ghafla nyuma yangu nikaanza kusikia vishindo vya watu wanaokimbia,nikaigeuza shingo nione ni kina nani hao.Kuja kugeuka niliwaona watu wa ajabu ajabu warefu wenye sura za kutisha na wanao vuja damu kila sehemu ya miili yao,nikaogopa na kuanza kutetemeka.Ile naanza kutetemeka tu mara ardhi nilipokuwa nimesimamia ilivunjika nikaangukia majini.Cha kushangaza baada ya kuangukia majini yale maji yalitoweka yote na haikujulikana yamepotelea wapi.Kuja kujiangalia miguuni na mikononi ile minyororo nayo sikuiona,ila vile vishindo vya watu wale wa ajabu vikaendelea kusikika.Sasa ghafla watu wale wakaonekana waziwazi mbele ya mboni za macho yangu na kwa mara hii walikuwa wameshikilia mataya matatu matatu ya punda,,,,wakawa wanachomoka kwa kasi ya ajabu kunifuata......Kabla hata hawajanifikia ule mto ulijitokeza tena na wote kwa pamoja wakadumbukia mtoni baadae kama kwenye dakika mbili hivi,miili yao ikaibukia juu ya maji ikiwa imeoza kabisa.Yaani kwa hapo ilikuwa ni kama maajabu yasiyowezekanika kwa akili za kawaida au kwa ufahamu wa kawaida kwani mimi nilikuwa nipo eneo hilo hilo lenye mto lakini sikuwa nimekanyaga maji wala nini nilikuwa nimekanyaga ardhi tu ya kawaida ila wale watu wa ajabu wenyewe walikuwa majini na walikuwa tayari wameshakufa.Sasa nikiwa kwenye mshangao ,mara nikasikia sauti ya muungurumo ikiniita nikaamua kuifuata kule iliponiitia.Nil
ikifuata kinjia kimoja chembamba nikawa nimefika karibu na pango la mawe lenye muonekana kama msalaba hivi,,,, mbele yangu nikaona taa ya mshumaa inawaka huku karibu na taa hiyo kukiwa kumelazwa kitu kinyoofu nisichokijua kwani kilikuwa kimefunikwa kwa sanda nyeupe.Ghafla kitu hicho kama kufumba na kufumbua kikaanza kutikisika.....kikatikisika sana baadae akaibuka mtu mwenye sura kali ya jua akaniambia nitazame kuume kwangu ,nikatazama nikaona ufunguo mmoja mkubwa na wa ajabu,akaniambia niuchukue ufunguo huo nami nikauchukua kama ambavyo aliniambia.Yule mtu akaniambia tena kwamba nigeuke kushoto kwangu,nikageuka na kuiona Biblia kubwa imewekwa hapo,yule mtu akaniambia niichukue nikaichukua.Baada ya kuichukua mtu huyo akaniambia kwa mara nyingine tena kwamba nigeuke nyuma yangu,nikageuka na kukiona kijikaratasi chekundu chenye maandishi ya damu akaniambia nikitwae kisha nianze kuyasoma maandishi hayo,sasa nilipokichukua nilijaribu kuyasoma yale maandishi nikayashindwa kwani yalikuwa hayaeleweki na isitoshe yalikuwa hayasomeki.Yule mtu akaniambia nitazame usoni mara tatu nikamtazama baadae akaniambia nianze kuyasoma sasa hayo maneno,,,kumbe yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya kiyunani na yalikuwa yakisomeka hivi;
"Luka,una Vita vikali sana mbele yako ,una maadui wengi mno wanaokuwinda mchana na usiku,sasa fanya hima ukimbie hapa uende kwenye mji mdogo wa MASHINO MASHINO,ukifika huko nenda kaingie kwenye kijumba chochote kidogo unachokifahamu humo utamkuta Mzee wa makamo atakuambia kila kitu upasacho kukifanya".Maneno hayo yalisomeka hivyo ila mimi nikawa nashindwa kulielewa lile neno MASHINO MASHINO ikabidi nivunje ukimya kwa kuamua kumuuliza,nilimuuliza yule mtu akaniambia maana ya mji wa MASHINO MASHINO,ni sehemu kutoka mkoani Mbeya wilaya ya Mbeya kijijini kwa lugha ya Kiyunani kwa hapo nikamuelewa.Sasa baada ya kumuelewa aliniruhusu nianze kuondoka,,,,Nikaanza kuondoka,niliziacha hatua chache tu nyuma nikaliona kundi moja kubwa sana la majoka aina ya Sawaka yameiziba njia yote,,,,roho yangu ikaniambia niendelee mbele,nami nikakaza mwendo kuendelea mbele.Ghafla lile kundi la majoka likatoweka,,,likaja kuonekana kwa mbele umbali wa mita mia mbili,,,nikawa natembea bila kuogopa huku zile funguo nikiwa nimezishikilia kwa kuzining'iniza.Nilipotazama kulia kwangu nilisikia sauti ya kilio cha mtoto ,roho ikaniambia nisigeuka kuyaelekeza macho yangu huko nikifanya hivyo sina maisha.Basi nikawa najikaza kusogea mbele,,,,Mara upande wa mbele yangu nikamuona binti mzuri yupo uchi ananiijia,,,,,Kabla sijamtazama vizuri ni nani huyo Ghafla nikasikia sauti ikiniita pale chini ya nyasi ndogo za Garden yangu.
"Boss.....Boss....Boss".Niliamka huku mapigo yangu ya moyo yakienda mbio kutokana na ile ndoto nikayaangaza macho huku na huko nikawa nimemuona Mtashobya amesimama mbele yangu huku akiwa ameikusanya mikono yake .
"Samahani Boss wife anakuita chumbani ameniambia nikuletee pete hii". Aliongea Mtashobya nikashtuka na kuanza kujiuliza kimoyo moyo ,ina maana Athumta amerudi tena? Huyu ananitafuta nini huyu? Daah!! Kwa hali hii sijui.Nilijiuliza baadae nikamkazia macho Mtashobya na kumwambia "Nenda kamwambie kwa sasa nimechoka aniache nipumzike hapa hapa na hii pete mrudishie siihitaji kwa sasa".Nilisema,Mtashobya akakubali akawa ameondoka pale kuingia ndani.Baadae dakika moja tu alikuja tena.
*****************************
"Boss amesema ukamuone maana ana shida ya mhimu pia ameniambia uwahi haraka".Alisema Mtashobya ."Nenda kamwambie kwa sasa nimechoka aniache nipumzike".Nilimjibu , Mtashobya akaondoka kuelekea ndani hakuja tena eneo hilo .Ghafla nyuma yangu nikahisi kama kuna mtu ananitekenya,nikageuka na kukutana na sura ya Athumta bila kujua alifika fikaje pale,,,,mara hii akiwa uchi wa mnyama.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11).

Ule uchi ulikuwa ukionekana waziwazi machoni kwangu bila chenga yoyote.....Sasa kwa vile akili yangu ilikuwa ikiwaza ya mbali,uwepo wa Athumta eneo hilo na muonekano wake huo wala haukuweza kunitisha.Nilimgeukia ,kwa hasira nikawa namtazama.....nikamuona anayachezea chezea maziwa yake kana kwamba anajiandaa kufanya jambo mimi nikawa nazidi kumtazama tu baadae nikasimama,niliposimama na yeye alisimama tukawa tunatazamana uso kwa uso."We jini umeijia nini nyumbani kwangu?" Niliamua kumuuliza muda huo nikijiandaa kuondoka hapo,sasa mara baada ya kumaliza kumuuliza hilo swali alianza kunitumbulia macho kuanzia chini ya unyayo wa miguu yangu hadi kichwani baadae akaanza kucheka kicheko kikali chenye mwangwi.Alipotulia ghafla nikawa namuona ameanza kubadirika na hazikupita hata dakika tano akawa na muonekano wa nyoka akajiburuza chini ya zile nyasi akapotelea vichakani,ndani ya vichaka vidogo vidogo vilivyokuwa vikipatikana karibu na usawa wa uzio.Nilishusha pumzi ndefu nikayaangaza macho huku na huko sikumuona mtu yeyote akija wala kujipitisha maeneo yale.....Nikataka kukaa ila moyo ukasita ukiniambia niondoke hapo haraka iwezekanavyo,sikuupinga moyo wangu nilianza kuzipiga hatua kuondoka maeneo hayo nikawa naelekea ndani.Nilifanikiwa kufika sebuleni nikaenda kukaa karibu na screen nikachukua remote ili angarau akili yangu niipoze kwa kutazama runinga hiyo.Niliikamata vizuri tu hiyo remote ila nilipotaka kuibofya nilisita nikaiweka kando.Nilisogea nyuma nikakiegemea kiti nilichokuwa nimekikalia nikatulia.Sasa nilipotulia tu na zikaja kumalizika dakika kadhaa ghafla niliisikia sauti ya Athumta ikiniita ."Mume wangu Luka,jamani mume wangu,,,Luka mume wangu".Sikuitika nilibaki kimya kana kwamba siisikii.Kwenda kutazama mbele kunako mlangoni yaani kwenye malango ya kuingilia ndani nilimuona binti mmoja akija ila kwa bahati mbaya sikuweza kumtambua......alitembea hatua chache tu akapotea,nikahisi labda macho yangu yana mawenge nikaachana nalo hilo nikawa naendelea kukaa pale.Baada ya kukaa sana,Nancy alikuja pale sebuleni akiwa na hotpot mbili za chakula akafika na kuziweka mezani akachukua na maji akasogea ili aninawishe."Una
enda wapi Nancy?" Nilimuuliza baada ya kumuona akinisogelea."Nakuja kukunawisha boss ili ule maana nakuonea huruma sana tangu asubuhi hujanywa chai wala kutia kitu chochote tumboni,tafadhari boss naomba ule walau kidogo tu". Aliongea Nancy muda huo akiwa amepiga magoti chini kana kwamba ananiomba msamaha."Nancy sina hamu ya chakula dada angu hapa nilipo naona kama nimeshakwama sina amani wala furaha,pesa kwa sasa naziona kama makaratasi tu hazina thamani kabisa". Nilizungumza waziwazi bila kutegemea kama maneno hayo ningeweza kuyazungumza.Nancy alinitazama kwa macho ya uwoga kidogo baadae akajitia ujasiri akaamua kukaa karibu yangu."Boss,niambie kinachokufanya uwe katika hali hii,niambie boss wangu huenda nikawa na cha kukusaidia".Kwa sauti ya upole Nancy alizungumza nikamtazama bila kumuongelesha nikatikisa kichwa nikawa nimejiinamia maana moyo wangu ulikuwa umeshaanza kugubikwa na uchungu usiokuwa wa kawaida.Nikamtazama tena Nancy."Nimeoa nyoka dada Nancy,yaani sina,sina ...? furaha....na na na...Na sijui nitaishije tu mpaka najuta ni kwa nini nilimpenda,ama kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza".Niliongea maneno hayo mbele ya Nancy mfanyakazi wangu wa kike niliyekuwa nikimwamini kuliko wafanyakazi wangu wote .Sasa baada ya kuyazungumza hayo,Nancy aliona nimemuacha njia panda akawa kama hajanielewa kwa kile ambacho nilikizungumza.
"Una maanisha nini boss unaposema kwamba umeoa nyoka,tafadhari niambie boss".Alisema Nancy ikabidi nianze kufunguka tu.
"Nancy..... Athumta siyo binadamu wa kawaida bali ni joka yaani ni nyoka na amekuwa akinisumbua kila kuitwapo leo mpaka nimekosa furaha katika maisha yangu na amani pia,mwanzo nilidhani nimepata mke bora na mke mwema kumbe nilikuwa nimejikaanga mwenyewe ndani ya mafuta yangu mwenyewe najuta Nancy,,najuta mie na laiti kama ningemsikiliza mama haya yote yasingenipata,usiku silali kabisa,mara Athumta atokee mbele yangu kama joka,mara kitandani nikute damu mara niote nakula nyama za watu mara niote nimedumbukia kwenye shimo refu la majoka yaani nateseka sana Nancy".Niliyasema hayo,binti akaanza kunipa moyo ."Boss pole sana hayo huwa yapo tu hapa duniani na wala yasikukatishe tamaa au kukusononesha kiasi hicho cha msingi ni wewe kumkabidhi Yesu maisha yako ili uwe huru,yote Mungu atakuzidishia na mke mwema,mcha Mungu ,mzuri atakupatia mbele ya safari". Aliongea Nancy maneno yake nikayatia moyoni nikaapa kuyafanyia kazi .Tuliongea mambo mengi sana mpaka nikapata na hamu ya kula chakula,Nancy nae akaungana na mimi katika kukila hicho chakula.Na kuanzia wakati huo urafiki wa karibu kati yangu na Nancy ukaanzia hapo.Kwa ufupi tu,Nancy alikuwa ni binti mmoja mrembo sana ila urembo wake ulikuwa ni asilia pamoja na umbo zuri la kuvutia,sema utofauti wake na Athumta,Athumta alikuwa mwembamba kiasi mwenye makalio makubwa na yeye alikuwa mnene kiasi mwenye makalio makubwa kiasi na kwa kumtazama tu alikuwa ni binti mbichi kuashiria hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ,na jambo alilokuwa akilithamini kwake yeye ni kumcha Mungu.Basi ile siku ilimalizika salama na cha kushukuru Athumta kwa Usiku wa siku hiyo hakuweza kunitokea nilala usingizi mnono.
Kesho yake kulipopambazuka tayari ilikuwa ni siku ya juma nne.Asabuhi na mapema nikiwa nahangaika kulikumbatia shuka langu la kimaasai kujikinga na kijibaridi cha asubuhi asubuhi,niliusikia mlango wangu ukigongwa,nikat
oka haraka pale kitandani ili niusogelee niweze kuufungua,,,niliufikia nikawa nimeufungua nikamkuta Nancy amesimama pembezoni mwa mlango huo.
"Boss shikamoo?" Alisalimia Nancy."Marahaba dada Nancy,habari za asubuhi?" Niliitikia kisha na mimi nikaamua nimjulie hali."Boss nimeshakuandalia maji ya kuoga". Alizungumza Nancy huku akiviminya minya vidole vyake."Asante Nancy".Nilimshukuru kwa hilo baadae akawa ameondoka mimi nikaelekea bafuni kwenda kuoga.Huko sikukawia sana bali nilitumia dakika chache nikawa nimemaliza.....
...nilirudi chumbani nikajiandaa haraka haraka mwisho ule muda wa kwenda kazini ukafika nikaondoka mapema kuwahi huko ofisi Siku hiyo nilifanya kazi zangu kwa ufanisi wa hali ya juu na furaha yangu ikawa imerejea huku nikijitahidi kumsahau Athumta ambaye kwa kipindi hicho alikuwa kashaingia mtini kunitokea hovyo ovyo.Jioni yake ilipofika nilirudi salama nyumbani Nancy kama mfanyakazi wangu alinipokea akanivulisha ule mkoti wa suti niliokuwa nimeuvaa akauweka kando."Boss unataka nikuandalie chakula gani leo yaani usiku wa leo?" Aliuliza Nancy nikapata kigugumizi kumjibu nitakula chakula gani."Niandalie chakula chochote kile kizuri".Nilimjibu hivyo baada ya kuona nimekosa cha kuchagua,,,Sasa baada ya kumjibu Nancy na yeye akawa amesimama alianza kunitazama usoni akageuka ili aanze kuondoka pale,akatembea hatua chache akageuka kunitazama kwa mara nyingine tena nikamuona akitabasamu akaendelea mbeleni mpaka akatoweka mbele ya mboni za macho yangu.Dakika kumi baadae nilimuona akirudi tena akafika na kisha kusimama mbele."Kuna kitu kimepungua Nancy?" Nilimuuliza akakataa kwa ishara ya kutikisa kichwa huku akiwa ameyainamisha chini macho yake ."Ka....ka daah?" Alijaribu kuzungumza akashindwa aongee nini akaendelea kubaki kimya akijinyonga nyonga mbele yangu,baadae akaanza tena kunitazama usoni macho yake mawili akiyagandisha usoni mwangu."Bo.....
Ka...ka,,,Boss naomba uniangalie usoni nina zawadi yako".Aliamua kuyasema hayo huku akizidi kuyalegeza macho yake."Zawadi gani hiyo Nancy?" Nilimuuliza."Naomba unitazame tu utaielewa".Baada ya kuyazungumza hayo niliamua kumtazama ila yeye akayakwepesha macho yake na kuanza kucheka kimya kimya huku akiuziba mdomo wake
"Boss,yaani uwepo wako tu huwa unanifurahisha sana,ukienda kazini najihisi mpweke mimi". Aliongea Nancy na kunifanya nicheke kidogo."Sawa boss ngoja Mimi nikakuandalie chakula kitamu ule na ushibe maana....Maana,
,,basi sawa boss ngoja mi niende". Aliongea Nancy muda huo huo akaanza kuzipiga hatua kuondoka pale,alipoufikia tu mlango wa kutokea aligeuka na kunirushia jicho moja ambalo mpaka sasa nikilitafutia tafsiri yake huwa naishia kuguna na kucheka mwenyewe.
Baada ya lisaa limoja kumalizika chakula cha usiku kilikuwa tayari,Nancy akanitengea chakula hicho tukala na kushiba .Kabla hatujaelekea kulala Nancy alinisihi tusali kabla ya kulala nami nikamkubalia tukaanza kusali tukaja kumaliza nusu saa baadae kwani huyo binti kwenye masuala ya kuomba tu alikuwa ni moto wa kuotea mbali."Boss yaani mimi ningekuwa mkeo ningeinjoy sana sema basi tu".Maneno hayo aliyaongea Nancy mara baada ya kumaliza kusali ."Hahaha!! Acha utani basi Nancy ".Nilisema akaniangalia usoni kisha akatabasamu."Ni kweli boss maana wewe ni mpole,mcheshi na isitoshe una roho nzuri yaani we acha tu,ningeinjoy sana,halafu boss umependeza sana". Aliongea kwa kunipa sifa hizo."Asante Nancy kwani wewe kwa sasa huna boyfriend?" Nilimuuliza akakataa kwa ishara ya kutikisa kichwa."Wala....akhaa!! Sina boyfriend mimi jamani halafu boss kesho nikusindikize kazini eti?" Aliongea Nancy huku akiwa hana dalili za kuondoka pale sebuleni kuelekea chumbani kwake.
"Unisindikize kazini?" Nilimuuliza na mimi."Ndio boss wangu".Alijibu mara hii macho yake yakiwa yametulia usoni mwangu."Tutaangalia Nancy wala usiwe na shida,cha msingi tumuombe Mungu tu atulinde kesho atuamshe tukiwa wazima,basi mimi nikutakie usiku mwema Nancy". Niliongea lakini akawa kama hajalizishwa na jibu langu hilo."Mmh? Boss mbona bado mapema jamani!!".Alisema Nancy huku akisimama."Usij
ali Nancy kesho na yenyewe ni siku tutaonana". Niliongea akawa amenielewa baadae akaenda chumbani kwake kwa ajili ya kulala.Mimi nikabaki nimekaa hapo nikayazungusha macho huku na huko.Nilitulia kidogo kisha nikasimama ili nianze kuondoka pale kuelekea chumbani kwangu,sasa kabla sijaanza kuondoka hapo,mara nikauona mlango wa sebuleni ukifunguliwa nikashtuka kwani mlango huo ulikuwa umefungwa vizuri tena kwa komeo la ndani,,,,nikajitoa ufahamu nikausogelea nione ni nani ameufungua,,,,n
ilikitoa nje kichwa changu nikaanza kuchungulia nisione chochote zaidi ya mwangaza wa taa za hapo nje.Nikakirudisha ndani kichwa changu nikawa nimeufunga mlango huo.
********************
Nikazipiga hatua za mwendo wa taratibu kulisogelea sofa moja nililokuwa nikitazamana nalo,,,,ile nageuka nyuma nikauona ule mlango upo wazi kwa mara nyingine tena.Nikauacha ukiwa wazi nikakaa kwa kuutazama,niliutazama mpaka ukajifunga.Baada ya mlango huo kujifunga wenyewe niliamua kusimama tayari kabisa kwa kuelekea chumbani kuangalia utaratibu wa kulala..Nikawa nimeingia na kabla sijajinyoosha kitandani nilikaa juu ya hicho kitanda.Ghafla juu ya bati nilianza kusikia vishindo vya watu wakifukuzana baadae vishindo hivyo vikatoweka.
Kwa hapa nikapanda kitandani ili nilale......Baa
da ya kujifunika shuka mwili mzima,shuka hilo ambalo nilijifunika lilipeperushwa sijui na nini likadondoka chini,nikainama ili nilichukue ila nikawa silioni tena.Sasa nikiwa kwenye hali ya mshangao na hofu ya hapa na pale mara kwenye kona ya mlango walitokea wasichana wawili ambao siwafahamu......Ghafla zile sura zao nazo kama kufumba na kufumbua hivi zikaanza kubadirika mara hii nikazitambua,,,mmoja alikuwa ni Lilian na mwingine ni Athumta na wote kwa pamoja walikuwa uchi.Walianza kucheka kwa nguvu,nikatamani niwakemee ila koo langu likagoma kutoa sauti,nikasema niwakemee kimoyo moyo napo nikashindwa nianzie wapi.Ghafla ile sura ya Lilian ikabadirika akawa Nancy mwenyewe.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12).

Mh! Nancy tena? Kwa hapa hapana ni lazima kutakuwa na kitu hapa,haiwezekani na siwezi kuamini kama huyu aliyejitokeza ni Nancy.Nilijiongelesha maneno hayo kimya kimya huku nikijikaza kuyazuia mapigo ya moyo wangu yasiende kasi.Niliendelea kumtazama yule jini aliyekuwa amejigeuza kuwa Nancy baadae akadondoka chini ,hapo hapo akaanza kubadirika na punde si punde akawa nyoka.Sasa baada ya kuwa nyoka wa kutisha alisimama nyoka huyo wima akawa anaachama mdomo wake kujaribu kunitisha kama anataka kunimeza vile lakini mimi nikasimama pale pale pasipo kuusogeza mguu wangu kulia ama kushoto.Nyoka huyo wa ajabu alipoona siteteleki alianza kutema mate lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mate hayo yalikuwa yakimrudia kwa kasi kila ajaribupo kunitemea.Alishindwa akaanguka tena chini akaja kusimama akiwa yeye kama yeye.....mara hii hakuwa Nancy tena bali Pasto Samba.Kwa hapo ilinishtua kidogo hali hiyo nikajikaza kwa nguvu huku nikisogea sogea nyuma.Niliyazungusha macho kunako upande wa kusini mwa kile chumba nikaiona ile Biblia niliyokuwa nimepewa katika ulimwengu wa kimiujiza nikaitwaa na kuanza kuinyoosha kuwaelekeza mashetani hao......Sasa mara baada ya kuinyoosha Biblia hiyo kuwaelekeza walianza kuweweseka mithili ya watu waliomaliza kunywa pombe.....wakasogea ukutani na kisha hapo hapo wakatoweka.Nilishusha pumzi ndefu za haja nikasogea kitandani na kumshukuru Mungu.Nilipohakikisha nimemshukuru Mungu vya kutosha nilipanda hapo kitandani nikawa nimelala......muda mfupi tu tayari usingizi mzito ulinipitia nikawa nimelala kama mfu kwani hata kuchoka napo nilikuwa nimechoka mno ukijumlisha na yale majukumu ya kutwa nzima.Cha kushukuru usiku huo baada ya Mimi kulala sikuweza kusumbuliwa na viumbe hao wa ajabu hadi kunapambazuka.
Asubuhi na mapema ndani ya siku hiyo mpya kabisa ya Ijumaa,niliendelea na majukumu yangu ya siku zote na kazi zote hizo zikawa zinaenda vizuri tu.Sijui tayari Mungu alianza kuwa na makusudi na mimi kwani kila kazi ambayo niliifanya kwa siku hiyo ilifanikiwa zaidi ya asilimia mia moja.Basi maisha yakaendelea na siku nazo zikawa zinazidi kukatika moja baada ya nyingine.Wiki moja ilipokatika,Nancy alijikuta akianza kuvutiwa na mimi huku akijiweka karibu yangu katika kunitia moyo na hata kunifariji kwa kila jambo au pale panapohitajika.Ilikuwa ni mishale ya saa kumi na moja za jioni siku ya juma tano ambapo ndo kwanza nimeshatoka kazini na kuamua kujipumzisha ndani ya Bustani ya maua nikiwa napitia mistari kadha wa kadha ya Biblia...... Alionekana Nancy akija kwa mwendo wa kujificha ficha ukutani......kwa jinsi alivyokuwa akija alidhani simuoni lakini mie nilikuwa nikimuona vizuri tu.Alitembea akafanikiwa kunifikia,akasimama mbele yangu huku akiachia mfululizo wa matabasamu yasiyokuwa na idadi maalumu ,alinitazama baadae nae akaketi ila alipoketi tu hakuweza kuniambia neno lolote au shida yoyote iliyomfanya anifuate pale na hata nilipomuuliza anahitaji nini au ana shida gani au kuna jambo gani limejitokeza tulitatue napo hakusema zaidi ya kuniambia yupo poa tu,,,, mengine sasa ilibidi nianze kujiongeza mwenyewe,,,Niliiweka kando Biblia yangu nikaanza kumtazama usoni binti huyo,,Wakati namtazama kuna kipindi macho yake aliyakwepesha huku akicheka kimya kimya bila kunitazama.
"Nancy?" Nilimuita kimtego."Abeee!! Boss !!".Aliitika na akawa makini sana kusikia ni neno lipi nitamuambia."Wewe ni mrembo yaani kama nikuumbika tu kwa kweli umeumbika mimi kukuona tu nipo hoi taabani,kiukweli Nancy mpaka hapa wewe ndo unayefaa kuwa wangu wa maisha.......nimevutiwa na wewe Nancy na nimetokea kukupenda sana".Wakati nikiyaongea hayo,Nancy alikuwa ameshayafumba macho yake huku akionekana dhahiri mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio.Yaani kwa hapo ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko kwani mimi saikolojia ya kuwatambua wasichana waliopenda ila wakawa waoga wa kufunguka nilijaliwa kuwa nayo na ndicho nilichokuwa nikijivunia kwa upande mwingine.Sasa Nancy macho yake akawa ameyafumbua,,,nikamshika mikono yake na kumsogeza karibu yangu na kweli nikagundua binti alikuwa akitetemeka hakuamini kama ningeweza kumtamkia maneno kama hayo,siyo kwamba nilimtamkia kwa kumtega,hapana tena hapana bali nilifanya hivyo kwa sababu hata Mimi nilitokea kuvutiwa sana na msichana huyo.
"Nilaze kifuani kwako baby...... hatimaye leo furaha ya moyo wangu imechipuka upya,,,,nimempata kipenzi wangu niliyekuwa nikimpenda tena kwa dhati.Luka ni siku nyingi sana nilikuwa nikikupenda ,nilikupenda hata kabla hujamuoa huyo Athumta na kiukweli siku ile unafunga ndoa niliumia sana na hata kubaki nikiyauguza majeraha yangu ya moyo.Ila sikukulaumu kwa vile nilikuwa nimechelewa kwa kuogopa kukutamkia waziwazi kuwa nakupenda usije ukanielewa vibaya, nikawa najipa matumaini tu kwamba ipo siku Luka atakuja kuwa wangu wa maisha,wa kufa na kuzikana na hatimaye imekuwa......Nitakupenda Luka na nitakupa kila kitu utakachokihitaji kutoka kwangu na nitasex na wewe tu maishani kwani wewe ni mwanaume wangu wa pekee hakuna mwingine". Aliongea Nancy na baada ya kumaliza tu kuyaongea hayo...Nilimbeba juu juu tukaingia ndani ,baadhi ya wafanyakazi wangu wa ndani waliotuona waliishia kutikisa vichwa vyao wasijue ni nini hicho.Mapenzi baina yangu na Nancy yakawa yameanzia hapo.Mpendwa msomaji na mfatiliaji wa mkasa huu wa kusisimua ngoja nikudokezee mambo machache tu kama ulikuwa huyafahamu.Kwa sasa yaani muda huu ninapokuletea kisa hiki kilichowahi kunipata kwenye maisha yangu,mimi ni mchungaji wa kanisa moja la KKKT hapa Ilemela Mwanza,sina mali,magari na hata majumba ya kisasa ila naishi maisha ya furaha sana zaidi ya yale maisha yangu ya zamani miaka kumi iliyopita.Kama ni kula nakula vizuri tu na nina amani kwani kule Mungu alikonitoa ni mbali mno na ndio maana niliamua kujitoa kumtumaini na kumtumikia yeye.Nina watoto wanne wa kike watatu na wa kiume mmoja na wote walizaliwa na mke wangu kipenzi Nancy.
Basi tuendelee......Sasa baada ya kumbeba Nancy niliingia nae ndani nikaenda kumshusha juu ya sofa moja nikawa namchezea kwa jinsi nipendavyo mpaka binti akaanza kulegea .Japo bado alikuwa ni bikra lakini kwa namna ile alivyokuwa amelegea usingeweza kupata tabu kutambua ni kipi anakihitaji.Niliyaangaza macho yangu kulia,kushoto,mbele nikamalizia nyuma baadae nikambeba hadi chumbani .Nikaanza upya kumchezea huku nikiwa nimedhamiria kabisa kulionja penzi lake jipya kabisa yaani kuutoa ule usichana wake.Nilipomchezea na kuhakikisha amelainika nilianza kuvua nguo zangu .Nilianza na shati baadae nikamalizia na suruali.Sasa ile najaribu kumpanda msichana huyo Ghafla nikaanza kuhisi maumivu ya tumbo,nikarudi nyuma huku nikigugumia kwa uchungu.Pale kitandani Nancy alikuwa ameniachia kila kitu nishindwe mimi tu,na kwa wakati huo macho yake legevu yalikuwa yakinitazama kwa huba na mapenzi moto moto .Sasa wakati nikiwa nahangaika mara msichana huyo akagundua kwamba sipo sawa,akaamua kushuka pale kitandani na kisha kuanza kunisogelea pale ukutani akanifikia akawa ananitazama kwa macho ya upole..
"Mpenzi vipi tena?" Aliniuliza Nancy nikawa naishia kumtumbulia macho tu."Tumbo limeanza kuniuma Nancy,tumbo linaniuma sana".Nilimjibu akahuzunika kana kwamba ni yeye anayeyapata hayo maumivu."Pole Luka ila litapoa tu,naomba japo kidogo unikumbatie na mimi nihisi raha moyoni na msisimko pia".Alisema Nancy huku akinivuta taratibu kunielekeza kifuani kwake."Naumwa tumbo mpenzi kama hautojali naomba hili tendo tulifanye kesho ". Niliongea kwa uchungu sana huku mkono wangu mmoja nikiwa nimeugusisha tumboni ."Sawa mpenzi mimi nipo kwa ajili yako,na hilo tumbo litapoa tu". Alizungumza Nancy baadae akavaa nguo zake na mimi akanivalisha nguo zangu tukawa tumetoka humo chumbani bila kufanya chochote.
Kesho yake ikawadia.........Nayo ilikuwa ni siku ya juma mosi,siku ya mapumziko,hivyo mimi na wafanyakazi wangu wote hatukwenda kazini Sasa siku hiyo niliipanga kuitumia kwa ajili ya kumpendezesha Nancy......Tulisubiri jioni ifike ili tufunge safari ya kuelekea supermarket.Tul
iisubiri kwa hamu sana jioni hiyo hatimaye sasa ikawa imewadia,,,,Mnamo majira ya saa kumi na robo tulipanda ndani ya gari yetu aina ya Hammer tukaanza kuondoka pale nyumbani ili tuwahi huko,tukachukue vya kuchukua tuwahi pia kurudi.
Safari ya kuelekea supermarket kubwa jijini humo ilikuwa ni nzuri tu haikuwa na dosari kabisa......tulifanikiwa kufika baada ya robo saa kupita.Tukashuka kwenye gari tukiwa tumeshikana mikono tukaanza kuzipiga hatua kuingia ndani ya jumba moja kubwa wanakouza nguo mbali mbali pamoja na viatu vya kike vya maana.Sasa wakati tukiingia mara msichana mmoja hivi aliniita sikumuitikia pamoja na kwamba nilimsikia vizuri nikawa nipo bize na Nancy tu kuelekea mbele.Hatimaye tukawa tumemfikia mhudumu mkuu wa humo ndani.
Kiukweli huyo mhudumu sijui alikuwa ni mcheshi,sijui muongeaji sijui alikuwa akinifahamu yaani sikumwelewa kwani kila nikitaka kuzungumza nahitaji nini ananikatiza kwa kuniletea habari zingine tofauti kabisa na zisizokuwa na maana yoyote."Mhudumu aise tuna mambo mengi mno ya kufanya kama vipi acha kwanza tufanye yetu story zipo tu".Niliamua kumwambia maneno hayo baada ya kumuona anazidi kunipigiza story zisizoeleweka."Haa!! Yamekuwa hayo tena,haya bwana ila ukirudi huko nyumbani usisahau kwenda kumsalimia mke wako". Aliongea maneno yake nikayachukua juu juu tu baadae nikayatupilia mbali.Nilimsaidia Nancy kuchagua nguo,tukanunua nguo za kutosha na za maana,tukaja kuagana na mhudumu baada ya dakika arobaini na tano.Tulipotoka nje tayari jua lilikuwa limeshaanza kuzama kwani mishale ya saa kumi na moja na dakika za kutosha ilikuwa imeshawadia.Tukapanda gari na hapo hapo tukawa tumeondoka.Niliikamata barabara ya kuelekea nyumbani kwangu nikatembea umbali wa mita mia,kufumba na kufumbua mbele ya usawa wa gari nikaanza kuona kama kuna kiumbe kirefu kimesimama,,,nikikaribia kukisogelea tu nacho kinasogea mbele zaidi.Kile kiumbe nikashindwa kukitambua kwamba ni aina gani ya kiumbe maana kilikuwa hakionekani waziwazi na hata kichwa cha kiumbe hicho nacho kilikuwa hakionekani vizuri.Nikasema potelea mbali nikazidi kuidrive gari kwa kasi.......Nilipokikaribia tu nacho kikasogea tena mbele,ukimya ukanishinda nikaona nimshirikishe na Nancy.
"Nancy hivi mbele unaona nini?" Nilimuuliza swali hilo akatikisa kichwa "Hapana sioni chochote". Alijibu nikamtazama sana hatimaye nikashusha pumzi."Mbona naona kama kuna jitu limesimama?" Nilisema akawa ananishangaa tu."Mbona sikuelewi Luka? Jitu gani hilo sasa?" Aliuliza nikamwambia hilo tuachane nalo.Safari ikaendelea,yule jitu akawa anajitokeza hivyo hivyo bila kumuogopa mpaka akatoweka mwenyewe.Nyumbani tulifika kwenye mida ya jioni sana saa kumi na mbili na nusu ,giza totoro nalo lilikuwa limeshaanza kuingia .Tukakuta chakula kimeshaandaliwa ,,,,tukasubiri hadi ule muda wa kula,tukausubiri nao ukawa umewadia tukala chakula na kukimaliza.
"Baby nakutakia usiku mwema,lala salama".Ni maneno matamu ya Nancy yalisikika mara baada ya kila kitu kumalizika pale sebuleni,mimi nami sikubaki nyuma nilimtakia na yeye usiku mwema,,,,kila mmoja akawa ameelekea chumbani kwake.Sikwenda kukaa mule chumbani wala kupoteza muda niliamua kwenda kulala moja kwa moja.Nililala sana nikaja kuamka kwenye mishale ya saa saba za usiku kwani nilihisi haja ndogo na ilikuwa ni lazima nitoke tu humo chumbani kwani choo kilikuwa kikipakana na sebule.
***********************
Niliufungua mlango ili nitoke,nikaufunga tena baada ya kugundua nimesahau kitu cha kwenda nacho huko chooni .Baada ya kukichukua kitu hicho niliufungua mlango kwa mara nyingine tena nikawa nimetoka ,nikaja kutokelezea sebuleni.Nilipita pale sebuleni nikashangaa kumuona Nancy amelala kwa kujinyoosha kwenye kochi huku akihema juu juu,nikajisemea ngoja kwanza niende chooni,nikirudi nitakuja kumuamsha na kumuuliza ni kwa nini amelala hapo na alirudi mida gani kwani kipindi tunaagana kwa kutakiana usiku mwema kila mmoja alielekea chumbani kwake .Hivyo nikapitiliza moja kwa moja hadi chooni,,,,nikar
udi na kumkuta bado amelala nikaenda kukaa nae ili nianze kumuamsha..
"Nancy......Nancy...... Nancy?" Nilimuamsha huku nikimtingisha lakini hakuamka,nikarudia tena kumuamsha kwa mara ya pili."Nancy....
..Nancy.....Nancy?" Alikuja kuamka akawa ananitazama tu asiongee neno lolote.Sasa kabla sijamuongelesha tena,mara kunako upande wa chumba cha Nancy nilianza kusikia vishindo vya mtu anayekuja.Ghafla Nancy huyu hapa akaonekana akija akitokea chumbani akafika na kuanza kunishangaa mno na kwa hapo bila shaka alikuwa akielekea uani,nilimtazama yule Nancy niliyekuwa nimekaa karibu nae nikamtazama na yule aliyekuwa amesimama nikashindwa kuwatofautisha."Luka mbona umelala hapo,kwa nini?" Aliuliza Nancy aliyesimama nikamshangaa maana Mimi wala sikuwa nimelala bali nilikuwa nimekaa.
..............


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA TATU (13).

Nikajiuliza ni kwa nini Nancy aniulize swali kama hili ili hali ananiona kabisa nimekaa,nikawaza kivingine tena kwa kuusemea moyo wangu huenda yeye alikuwa ananiona nimelala.Nilimtazama yule Nancy wa pale kwenye kochi nae akanitazama pasipo kuzungumza neno lolote zuri au baya.Ghafla Nancy huyo akaanza kufifia mithili ya ukungu baadae akapotea kabisa .Nilishtuka kisha nikayainua macho kumtazama Nancy aliyekuwa amesimama na hapo ndo nikaelewa kwamba yule Nancy aliyekuwa amekaa hakuwa Nancy wa ukweli bali jini."Luka nenda kalale mwaya maisha pamoja na majukumu yasikukoseshe usingizi namna hiyo". Aliongea Nancy wa ukweli nikasimama na kuanza kumsogelea ......wakati nikimsogelea nilimuona akiguna tu kana kwamba kuna kitu au jambo alikuwa akiliona kwangu."Mpenzi na hicho kidonda umekipata wapi tena?" Swali hilo kutoka kwa Nancy lilinifikirisha sana kwani nilianza kujihoji kidonda nimekipatia wapi na kipo sehemu gani,ikabidi kwa hapo nimuulize tu."Nancy mbona Mimi sina kidonda,kidonda hicho kipo wapi?" Nilimuuliza akabaki akinishangaa asinielewe."Hicho hapo karibu na pua tena kinatokwa na damu".Alinijibu nikajaribu kuunyoosha mkono wangu kuuelekeza kwenye pua lakini baada ya kuushusha na kuutizama kwa makini sikuweza kuona damu hata lile tone lake tu."Nancy mpaka hapa nipo kwenye wakati mgumu sana,kwanza naomba uanze kuomba hapa hapa,naamini hicho unachosema kuwa ni kidonda sicho bali ni maruweruwe tu ya kiibirisi".Baada ya kumwambia maneno hayo, Nancy hakupoteza muda alianza kuomba kwa nguvu sana alipomaliza tu ,hapo hapo nae akatambua kuwa kile hakikuwa kidonda bali alikuwa akiona kiini macho.Alinishika mkono akanisindikiza chumbani kwangu kwenda kulala.Basi nikawa nimelala , usingizi ukaniijia hadi asubuhi kulipopambazuka.Maisha yakaendelea.......zilikatika siku mbili hatimaye siku ya juma pili ikawadia.Siku hiyo niliamka mapema sana ili nianze maandalizi ya kuelekea mkoani Mbeya kwenye kile Kijiji nilichoelekwezwa na yule mtu siku kadhaa zilizopita kwenye maono na siku hiyo ndo ilikuwa ya mwisho kati ya zile ambazo nilipewa.
Kuondoka hivi hivi bila kumuaga Nancy wangu niliona haitakuwa vizuri ,nilijiandaa upesi baadae nikaelekea sehemu ile aliyokuwa akifanyia kazi Nancy hapo nyumbani ili nikamuage niondoke haraka .Basi nikawa nimemfuata huko."Mh? Luka vipi tena ndo kusema unawahi kanisani au?" Aliuliza Nancy muda huo akinitazama kwa makini ,nilimkazia macho kisha nikamjibu "Hapana Nancy bali muda huu nataka niwakimbie kidogo nielekee mkoani Mbeya kuna kitu cha thamani sana kimenifanya niende huko,hivyo Nancy mimi nakuaga ubaki salama na kama Mungu atapenda basi tutakuja kuonana".Niliyazungumza hayo maneno huku nikiwa nimejikaza kwani machozi mepesi tayari yalikuwa yameshaanza kuninyemelea."Basi Luka mi nikutakie safari njema na Mungu akuongoze urudi salama". Aliongea Nancy baadae akanisogelea na kunikumbatia akanibusu akawa ameniachia nikasogea nyuma kidogo .Mpendwa msomaji cha kukukumbusha tu,muda wote huo naanza uhusiano wa kimapenzi na Nancy tangu nigundue kuwa nilipotea njia kwa kuoa nyoka yaani mwanamke mwenye asili ya nyoka nyumbani sikuwa nimewaambia kama nishaachana na huyo Athumta.Basi nikawa nimesogea nyuma nikaziacha hatua kama tano hivi nikasimama.Nancy nae akakiweka kikombe kimoja alichokuwa amekishikilia mkononi akikiosha akanisogelea na kisha kunikumbatia tena mara hii hata yeye machozi yalikuwa yakimtoka japo ya matone matone."Luka mpenzi wangu kwa mara nyingine nakutakia safari njema Mungu akulinde na kukupigania urudi salama". Aliongea maneno hayo muda huo akiwa amenikumbatia,kwa kumbatio la dhati kabisa."Amen Nancy,Mungu hatoniacha katika safari hii, najua yeye ni Dereva na atanifikisha ninakoenda nikiwa salama na pia nitarudi nikiwa salama,hii nyumba nakuachia wewe uitunze uwe boss wao humu ndani maana nakuamini". Niliyazungumza hayo kisha nikamuachia msichana huyo nikawa nazipiga hatua kuisogelea gari yangu.Niliifikia nikapanda nikaiwasha na kuanza kuiendesha kuitoa ndani ya geti .Nilitoka nayo nje nikaenda kuipaki karibu na barabara moja ya lami,,,nikawaza mambo mawili matatu,,,,nikamaliza na safari sasa ya kuelekea Mbeya ikaanza.Safari yangu ilikuwa na matumaini makubwa sana ya kufika salama mkoani Mbeya huku nikijipa moyo hata nikirudi nitamkuta Nancy pamoja na wafanyakazi wangu wote wakiwa salama......si hapo tu pia nilikuwa na matarajio makubwa mno ya kwamba nikifika kwenye kile Kijiji basi shida zangu zote zilizokuwa zikinikabili zitakwisha.Niliikamata rasmi barabara ya kuelekea Mbeya mnamo majira ya saa moja na nusu nikawa nadrive gari kwa mwendo wa kawaida tu.Nilianza kwa kuziacha hatua kadhaa,baadae mita kadhaa baadae tena kilomita kadhaa nikaanza kuingia kwenye barabara nyingine iliyokuwa imezungukwa na misitu yenye miti mikubwa na midogo kwenye kingo zake .Saa nane majira ya mchana ikawadia nikazidi kuongeza mwendo.Ilikuwa ni saa nane za mchana baadae ikafika saa kumi za jioni bila ya kufika huko.Nikawa bize na gia tu japo hofu nayo ilianza kunizonga huku nikiwaza nitafika fikaje huko.Sasa cha kushangaza masaa yalikuwa yakipita tu bila ya mimi kufika huko Mbeya,saa moja kwa hapo tayari ilikuwa imeshafika huku kwenye ile barabara niliyokuwa nikienda nayo nikijiona kama ndo kwanza naanza safari.
"Mh!! Yaani kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya kwa gari hii ya Hammer nitumie masaa kumi na mbili kweli ? Aisee hapana".Nilijisemesha ikabidi niisimamishe gari nishuke.Niliisogeza pembezoni mwa barabara nikashuka,,,baada ya kushuka nilisogea nikaenda kusimama karibu kabisa na nguzo ya umeme isiyokuwa na nyanya,nikashtuka tangu lini nguzo hizo zimetolewa nyanya zake wakati juzi juzi tu zote zilikuwa zina nyanya.Nikawaza labda nimekosea njia lakini akili yangu ikakataa kuwa sikuwa nimekosea njia,,,njia ni yenyewe kabisa.Nilianza kuichunguza barabara hiyo kwa umakini kujiridhisha kama ni yenyewe nikakubaliana na mawazo yangu ile barabara ni yenyewe wala sijakosea njia."Mh? Sasa kwa nini sifiki?" Nilijiuliza huku nikianza kuisogelea gari yangu.Nilitazama saa yangu ya mkononi nikakuta tayari saa mbili ilikuwa imeshafika.Nikasogea zaidi na zaidi nikaifikia gari na kuufungua mlango ukabaki wazi.Nikiwa nawaza cha kufanya,mara ilipita gari moja nyeusi kwa kasi nikaifuatilia kwa macho sikuiona kama iliishia wapi au ilikata sehemu gani maana lile barabara halikuwa na kona wala mteremko.Dakika mbili tena ile gari ikarudi kwa speed yake ile ile nikaifuatilia kwa macho sikubaini ilipotelea wapi,,,Kwa hapo nikajua tayari Vita imeshaanza,maruweruwe ya ajabu yameshaanza.Nikaanza na mimi kujipanga nione ni kwa namna gani nakabiliana na vitisho hivyo.Niliendelea kusimama kama sanamu maeneo hayo,baadae muda mfupi baadae akapita jamaa furani hivi anaendesha baiskeli nikamsimamisha na kisha kumfuata ili nikamuulizie.
"Kaka samahani,hivi hapa ni wapi?" Nilimuuliza,akanitizama kidogo akatabasamu."Kwani wewe umetokea wapi?" Aliuliza huku akishuka kwenye ile baiskeli."Natok
ea Dar es salaam Kaka naenda Mbeya ila cha kushangaza sifiki na sijui kama nimekosea njia ama laa". Niliongea muda huo nikiyageuza geuza macho yangu."Brother mbona hapa ndo Mbeya brother,sasa unaposema hufiki una maana gani ?" Aliuliza,na kweli nikayabaini maeneo yale kuwa ndo ya Mbeya."Kaka,cha kukusaidia ni hiki,naomba tuongozane hadi nyumbani kwangu tukishafika huko nitakuelekeza vizuri kwani mimi ni mwenyeji wa maeneo haya". Aliongea yule jamaa."Samahani brother kwa jina wewe unaitwa nani? Mimi naitwa Luka na kama nilivyokuambia nimetokea Dar es salaam".Nilisema."Kwa jina mimi naitwa Mwakitimbile Mwakalebya Tuntufye,au we niite tu Mwakitimbile inatosha". Alizungumza baadae ile baiskeli yake tukaifunga juu ya gari tukaondoka eneo lile kuelekea nyumbani kwake.
Tulitumia dakika tano tu tukawa tumefika,Mwakitimbile akanikaribisha malangoni mwake ndani ya jumba lake kubwa la maana tu japo lilikuwa limezungukwa na miti mingi mingi."Luka hapa ndo nyumbani kwangu karibu sana na ujisikie upo nyumbani kwenu au nyumbani kwako".Alisema Mwakitimbile."Dah! Shukrani sana jamaa angu nimeshakaribia". Niliongea Mwakitimbile akasimama na kuingia chumbani punde si punde akatoka akiwa amebeba chupa mbili za plastic ambazo zote kwa pamoja zilikuwa tupu akafika na kisha kukaa.
"Vipi Luka Dar es salaam wanasemaje?" Aliuliza huku akinitazama kila sehemu ya mwili wangu."Dar es salaam wapo tu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida jamaa angu Mwakitimbile". Niliongea,Mwakitimbile akatabasamu."Sawa sasa unaweza kuniambia unaenda sehemu gani ili nikuelekeze vizuri kesho usije ukahangaika!!".Alisema jamaa huyo huku akisimama tena......Kabla sijaanza kumwambia alizipiga hatua akaingia chumbani kwa mara nyingine akatoka akiwa amebeba chupa zingine mbili tofauti na zile za mwanzo alizokuwa nazo akafika na kukaa kwenye kiti chake."Ehe unaweza kuniambia Luka?" Aliuliza mara hii macho yake yakiwa yameganda kifuani kwangu.Nilitamani sana kumwambia sehemu ile ninayoelekea ila moyo ulikuwa ukisita huku nafsi ikiniambia kimya kimya hiyo ni siri yangu sipaswi kumwambia mtu yeyote yule."Ah!! Brother bila shaka nipo nipo tu ila kesho ikifika nitakuambia vizuri".Nilisema baadae Mwakitimbile akakubali kwa ishara ya kutikisa kichwa."Poa Luka nimekuelewa". Alisema Mwakitimbile huku akisimama,aliposimama alitembea kuelekea chumbani,muda mfupi tu akatoka akiwa na chupa zingine mbili tofauti na zile za mwanzo,nikawaza huyu jamaa vipi ? Ni mganga wa kienyeji nini? Huenda huyu ni mganga wa kienyeji".Niliwaza hivyo maana kwa ule mtindo wake wa kutoka anarudi akiwa na chupa tofauti tofauti ulinishangaza na sikuelewa alikuwa na maana gani kufanya hivyo.
"Luka?" Aliita."Naam Kaka".Niliitika tayari kwa kumsikiliza."Hivi umeoa kweli na mke wako bado unae?" Aliuliza."Nilioa ila baada ya kugundua yule mke niliyemuoa ni nyoka niliachana nae".Nilimjibu akanitazama tena kifuani."Unaposema ulioa nyoka una maana gani,na uliwezaje kumuoa nyoka jamaa angu maana hao viumbe wanatisha jamaa angu".Alisema huku akisimama...... akazipiga hatua akawa ameingia tena chumbani.Alikuja akiwa ameshikilia chupa mbili kubwa za plastic tofauti na zile za mwanzo.
***************************
"Ehe Luka,unaweza kuniambia ni sababu ipi ilikushawishi mpaka ukamuoa huyo binti mwenye asili za nyoka?" Aliuliza tena."Ni kutokujua tu Kaka,huyo binti mwanzo nilijua ni binti mmoja mzuri tu ,mrembo,mcha Mungu sikuwaza kama angekuwa jini.Kumbe nilikuwa ndani ya usiku mnene wa giza kama ambavyo wahenga wasemavyo jambo usilolijua ni kama usiku wa giza".
"Duuh!! Pole sana brother,unatumiaga kinywaji gani nikuletee?" Aliuliza Mwakitimbile."Niletee milinda nyeusi kama unayo".Nilimjibu akasimama na kuingia chumbani akatoka humo akiwa amebeba ndoo moja Lita kumi pamoja na kikombe akafika na kisha kuiweka hiyo ndoo mbele yangu.Mwanzo sikutambua ndani ya hiyo ndoo kulikuwa na nini,kulikuwa na ile milinda mieusi ama kitu gani,kwa hapo sikujua.
"Luka karibu,chukua hiki kikombe uanze kujichotea maana hii ndo milinda nyeusi".Alisema ikabidi nichungulie ndani ya ile ndoo.Ile nachungulia tu nilikutana na kichwa cha binadamu pamoja na damu nzito iliyokuwa imegandamana .
................................


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA NNE (14).

Aisee asikwambie mtu na omba sana ndugu yangu usije ukayapitia haya kwani utaiona dunia chungu utaiona dunia haina huruma na pia unaweza ombea ufe ili tu hayo magumu yasikupate.Ile damu ilinivuruga kabisa nikawa nahisi kama nipo ndotoni nisiamini kama ni kweli na ni ukweli mtupu lakini wala haikuwa ndoto bali uhalisia,nilipoyanyayua juu macho yangu kumtazama Mwakitimbile tayari hakuwa Mwakitimbile tena bali alikuwa amebadirika na kuwa jitu la ajabu ajabu tu.Jitu lenye muonekano kama wa zombi,macho ya kutisha makubwa yasiyokuwa na mfano halafu mwili mzima lilikuwa likitokwa na damu na halikuwa limevaa nguo yoyote ile."Hohohohooo!! Ohohohohooo!!".Lilicheka sana baadae katika mazingira ya kutatanisha likatoweka.Ile nyumba nayo ikawa haionekani nikabaki nje waziwazi kabisa.Nilisimama huku nikitetemeka mwili wote unatokwa na jasho nikajiuliza kumbe ukiambiwa dunia ndo hii na ina maajabu yake basi usipinge bali umuombe tu Mungu akuepushie hayo maana ni hatari sana,kwa hapa najaribu kukuelezea jinsi Mungu alivyonitoa shimoni na jinsi alivyonitoa mbali katika safari yangu ya maisha maana laiti kama asingekuwa yeye basi leo hii mimi ingebaki historia tu kwamba kulikuwako na mtu anayeitwa Luka na ndio maana nikaamua kumtumikia kwa nguvu zangu zote.Ndugu yangu kama umeokoka au kama wewe ni Muislam unamjua Allah basi shikilia sana imani yako kwani dunia hii amini ipo katika nyakati za mwisho ukiteleza kidogo tu umepotea.Basi tuendelee.....Sasa nilipojikuta nipo nje huku nikitetemeka nilijaribu kusimama ili niondoke ndani ya maeneo hayo ya kutisha lakini cha ajabu kila nikisimama tu nilijikuta nikidondoka chini yaani magoti yangu yote yalikuwa yakiuma mithili ya mtu aliyepigwa mawe au virungu.Nilifan
ya hivyo kama mara tatu nikaishia kushindwa nikaona bora nilale tu kama ni kifo acha kinipate maana sikuwa na ujanja.Nililala nikawa nimeyafumba macho yangu ,Nikiwa nahangaika hangaika,ghafla mbele yangu nikasikia vishindo vikumbwa vikubwa kana kwamba kuna tembo ananiijia,kwa taabu nikayafumbua macho,nilipoyafumbua tu nililiona jitu refu lenye kichwa kidogo cha chatu na mkia likiwa limesimama mbele,na lilikuwa likitoa harufu kali ya uozo.Nikaogopa mno nikawa najivuta vuta nyuma huku nikigugumia kwa maumivu.Sasa lile jitu baada ya kugundua nasogea sogea nyuma kwa kujiburuza nalo likaanza kunifuata taratibu taratibu huku likinusa nusa hewani.Likanifikia na kisha kunikanyaga ubavuni yaani ubavu wangu wa kulia.Nililipo nikanyaga tu huku nguvu za kusema nianze kulikemea zikiwa hazipo kinywani mwangu wala moyoni mwangu nilijibangaiza nikalishika mguuni,nilipolishika tu niling'atwa na kitu kama ng'e hivi kwenye huo mguu nikagundua hiyo miguu haikuwa ya kawaida nikauachia haraka maumivu makali yakaanza kuzunguka kwa kasi kila sehemu ya mwili wangu,nikajua kwa hapa muda wangu wa kufa umekaribia.Nikiwa naendelea kutaabika sijui iliniijia nguvu gani tu kwa kweli sijui na mpaka leo huwa naitafakari sana nguvu hiyo nisiipatie majibu wala ufumbuzi .Nguvu hiyo ya ajabu ilinifanya nisimame kwa miguu yangu miwili nikaanza kutimua mbio kuelekea kwenye mapori yaliyokuwa yamelizunguka eneo lile nikatokomea na kuja kutokelezea kwenye ile barabara ya lami yenye zile nguzo za umeme zisizokuwa na nyama.Nilisimama nikawa nahema juu juu,mbavu zote zikiuma,wakati huo nahema kichwa nilikuwa nimekiinamisha chini.Sasa nilipokinyanyua tu,macho yangu yaliliona kundi kubwa la wanawake waliokuwa wamejitwisha mapipa ya moto uliokuwa ukiwaka wakija mbele yangu muda huo wakipiga kelele,vigeregere pamoja na kuimba nyimbo kadha wa kadha zisizoeleweka.Nikajitazama mikononi kumbe hata ile Biblia yangu nayo niliisahau huko kwenye lile jumba la ajabu,nikaumia mno kwani kwa hapo nilijua ndo nimeshaipoteza Biblia yangu na kuipata siwezi kuipata tena,,,kutazama mbele napo wale wanawake waliokuwa wakionekana ni wachawi wa kutupwa nao walizidi kunisogelea .Waliponifikia ,walinizunguka ndani ya dakika moja wakawa wananicheka baadae wakatulia,mkuu wao akatamka maneno ya kuwafurahisha kwa kusema miungu imesikiliza dua zao hatimaye wamefanikiwa kupata kitoweo.Sikuwa na jinsi nilitulia kimya na hata kuwatazama usoni Wanawake hao sikuweza.Nikiwa nasubiria nikamatwe na hao wanawake......Mara sauti kali ya kilio ikasikika,wote wakayatupa chini yale mapipa yao wakaanza kutimua mbio kuondoka mbele yangu asisalie hata mmoja.Nilipowaona wametokomea mbali,nilianza kuondoka nisirudi tena kule kwenye lile jumba nikawa nakaza mwendo kwenda mbele......mara hii safari yangu ikawa haina matumaini tena,yaani nikawa naenda enda tu,wallet yangu nayo nilikuwa nimeipoteza ilipotelea huko huko kwenye lile jumba yaani acha tu ndugu yangu, kwa hapo nilibaki Luka kama Luka,milioni tano zangu ndani ya Wallet zikawa ndo zimepotea hivyo .Nilizidi kusogea mbele,nikaziacha hatua kama tano au nne hivi nikasimama na kuwaza jambo....Jambo hilo lilihusiana na mimi kurudi kuifuata gari yangu,Biblia yangu pamoja na wallet kama tu nitakuwa nimezisahau kama zimepotea basi.Nikiwa nawaza hivyo moyoni nikasikia sauti ikiniambia nisiende huko kuna majinamizi ya ajabu yametapakaa kila sehemu yataenda kuniangamiza nikaamua kutokurudi,potelea mbali kama ni gari,pesa acha zipotee tu hilo ndo likawa wazo langu la mwisho nikaamua kuendelea kutembea nisiyageuze macho yangu kulia ama kushoto.Sasa wakati naendelea mbele,katika hali isiyokuwa ya kawaida mikononi mwangu nilijikuta nimeishikilia ile Biblia bila kujua ilikuja yenyewe ama ililetwa na nguvu gani .Ni hiyo tu ambayo iliniijia,Gari pamoja na pesa ndo zikawa zimepotea hivyo.Moyo ukaniambia nikisha zikamilisha hatua tatu mbele nikate kulia baadae kushoto kisha ninyooshe kwenye kinjia kimoja chembamba chenye miinuko mirefu nikakubali,safari ikawa inaendelea.Nilitembea sana nikazimaliza hizo hatua nikakata kulia baadae kushoto kisha nikakifikia kile kinjia,aise hatari sana,kwa kukiangalia hakikuwa na uafadhari kabisa kwa kukipitia maana kilikuwa juu sana tena milimani,kwa haraka haraka urefu wake nina weza kusema kilikuwa na urefu usiopungua kilomita elfu moja au mia tisa hivi kwa wenzangu na mimi tuliosoma Geography pindi tukiwa O level na A Level tutakubaliana kwa hili.Kwa vile nilikuwa nimedhamiria nilikipanda kijimuinuko hicho nikawa natembea kwa kuinama inama hivyo hivyo.Nilitembea mpaka nikachoka nikaamua kuipakata ile Biblia yangu kifuani."Luka usisimame hapa panatisha,utapo
tea endelea na safari jikaze hivyo hivyo".Sauti ilinijia moyoni ikiniambia hayo nikawa sina jinsi zaidi ya kujikaza kutembea hatimaye mbele yangu nikaanza kukiona kijumba cha nyasi kikiwa kimezungukwa na taa za kila aina ndogo ndogo,nikashusha pumzi huku nikiombea kwa hapo nisije tu nikakutana na yale maruweruwe ya majoka na majitu ya ajabu ajabu.Nilianza kukifuata kijumba hicho baadae nikawa nimekifikia,,,,kufika tu sikuyaamini macho yangu maana pale nje niliiona gari yangu ,,,Nikiwa na hali ya tabasamu usoni,mara alitoka Mzee mmoja aliyekula chumvi za kutosha,mzee mwenye mvi nyingi akanipokea kwa kunikumbatia baadae akanishika mkono na kuniongoza hadi ndani,akanisogezea na kiti nikaketi,,,Mzee nae akaketi akaanza kunitazama huku akitabasamu,,,akasimama akawa ameingia chumbani,punde akatoka humo akiwa amebeba Biblia kubwa mbili pamoja na magombo makubwa mawili ya kale.Akafika na kukaa kwenye kiti chake.
"Luka una kitu gani mkononi mwako?" Aliuliza huku akilitaja jana langu mpaka nikashtuka kidogo maana nilijiuliza ni wapi alipolifahamia hilo jina."Mzee nina Biblia mkononi mwangu".Nilimjibu huku nikiwa nimekuzia macho usoni mwake."Aha! Sawa,kwanza nikupe pole kwa yale yote ambayo yamekupata ukiwa njiani,hii ndo maana halisi ya wokovu ulivyo ,ukitaka kumuona Bwana katika maisha yako ni lazima upitie magumu na hata katika mafanikio ili uweze kufanikiwa ni lazima upitie changamoto.Kwa sasa wewe hizo changamoto ndo kwanza umezianza bado zipo nyingi sana unatakiwa uzivumilie pamoja na kwamba zinakatisha tamaa". Aliongea Mzee huyo kisha akavuta pumzi na kuendelea "Usiwaze sana kuhusiana na zile pesa zako jua tu zipo salama na gari yako nayo ipo salama usiwaze ...... usiwaze!!".Alipomaliza kuyatamka hayo alisimama akazipiga hatua kuelekea chumbani humo akaja kutoka akiwa amebeba kichupa kidogo akafika na kukifungua kumbe kilikuwa na mafuta laini ya kimiminika ambayo sikuyatambua ni aina ipi ya mafuta.Mzee bila kuniongelesha chochote alikishika kichwa changu yale mafuta akayamimina yote kichwani yakasambaa huku yale mengine yakinifikia hadi shingoni,alipomaliza alianza kuimba wimbo huku akiruka ruka kama kijana mdogo akamaliza akakaa baadae akasimama na kuninyanyua na mimi akanikumbatia,baada ya kuniachia alisogea nyuma kidogo.
"Kwa sasa wewe utaitwa Lukas Mathew kuanzia leo na kuendelea......Mungu amenipa kibali cha kukutia mafuta kwani kuna kitu amekiona kwako kwamba kuna siku yaja utakuja kuwa fimbo kwa watu wake.Utarudi nyumbani usiku huu huu,ila angalizo,uwe makini sana njiani kwani kuna maajabu ya kutisha yatakupata huko,,,gari utaiacha hapa hapa,ukifanikiwa kufika salama utaiijia siku nyingine,,,,hizi pesa nazo utaziacha utaziijia baadae na utazikuta kama zilivyo,mimi nikutakie safari njema".Yule Mzee alitamka kisha akanishika mkono nikatoka nae nje tukaanza kutembea......akanisindikiza kidogo baadae akaniaga kwamba arudi mimi niendelee na safari yangu,,,,Kabla hajaondoka alivua pete yake moja aliyokuwa ameivaa kwenye kidole cha chanda mkono wa kushoto akanivisha,akavua na lile kanzu lake moja akanivisha akawa ameniaga.Mzee alitembea taratibu mpaka akaja kutoweka machoni mwangu,eneo lile nikabaki peke yangu pamoja na kijiupepo cha baridi kilichokuwa kikinipiga.Nikaishikilia Biblia yangu vizuri nikauinua mguu wa kushoto baadae wa kulia nikaanza kujongea mbele.Ile nasogea hatua chache tu,mbele niliona bahari kubwa imetulia ikiningoja nikasimama,nikageuka kulia nikaona kuna milima mirefu ya kutisha,,nyuma napo katika mazingira nisiyoyatarajia ,wale wanawake wa ajabu nikawaona tena wakiniijia huku wakiwa wameyabeba yale mapipa yao ya moto kulia kwangu nako kulikuwa na milima ile ile kama iliyopo kushoto kwangu.Sikuogopa nilisema lolote na liwe nikakaza mwendo mbele kuifuata ile Bahari,,,,ile najitoa kujirusha majini ,kumbe wala haikuwa Bahari kwani kama kufumba na kufumbua ilitoweka nikawa napita nchi kavu bila hata tone moja la maji .Kule nyuma nako wale wanawake wakazidi kunifuata mpaka wakaingia ndani ya lile eneo ambalo lilikuwa na Bahari kabla..
************************
Nilipotoka ndani ya eneo hilo,ile Bahari ya ajabu ilirudi na wale wanawake sikuwaona na sikujua kama walifunikwa na yale maji ama ilienda endaje mpaka wakapotea.Nikaachana na wazo hilo,safari ikaendelea.Nilitembea mpaka nikaimaliza kilomita moja......Mbele yangu nikawa nakutana na Mzee mmoja.Kumuangalia vizuri nikamtambua kuwa ni yule Mzee aliyenitia mafuta ndani ya kile kijumba cha nyasi milimani pamoja na kunipatia lile kanzu na ile Pete .Kimya kimya tukawa tunakaribiana.
"Ooooh!! Luka unaenda wapi?" Aliuliza yule Mzee."Naenda nyumbani".Nilimjibu lakini nikawa simuelewi kabisa."Usiogope...... Usiogope Luka,nasema hivi usiogope!!!".Alisema huku akinisogelea,mimi nikawa nasogea nyuma maana sikuwa nikimuamini."Luka,nasema usiogopee!! Mimi ni wakili wa Mungu.......Mimi ni wakili wa Mungu nipo hapa kwa ajili ya kukusaidia".


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA TANO (15).

Huyo Mzee pamoja na kuyazungumza hayo huku akionekana kama ni mtu wa hekima sana bado sikuwa na imani nae kwa kifupi sikumwamini nikajua ni wale wale tu mashetani wanaoniwinda na kujaribu kunizibia njia yangu nisiweze kupita na kufika kule ninapoenda.Nilijiuliza sana majibu ya maswali yangu nikakosa nikabaki namtazama tu Mzee huyo mwenye mvi zake na ndevu zake ndefu.Moyo ukaniambia nisiendelee kusimama kumngoja Mzee huyo azungumze neno jingine,nikawaza au niiache hiyo njia nipite njia nyingine nikasema hapana acha niinyooshe njia hiyo hiyo liwalo na liwe .Niliachana na yule Mzee nikawa nimempuuza nikaamua kuondoka kuendelea na safari yangu.Nilipozipiga hatua za kutosha nilisimama kisha nikageuka kumtazama yule Mzee kama bado yupo pale au ameondoka,cha kushangaza baada ya kugeuka sikumuona tena yule Mzee ina maana alitoweka kimiujiza eneo lile kwani kama sijasahau ile barabara haikuwa na kona wala mikato mingi mingi ilikuwa imenyooka vizuri tu.Jambo hilo kama ambavyo moyo wangu ulizoea nililichukulia poa nikageuza shingo yangu,safari ikaendelea.Nili
tembea weee!! Baadae nikawa nimefika sehemu moja yenye vinjia vitatu vyembamba vyembamba .Ikanibidi nisimame hapo nijue napita wapi maana nisingeweza kukurupuka tu yakanitokee ya kunitokea.Sasa nikiwa naifikirisha akili muda huo macho yangu nikiyaangaza huku na huko......Ghafla mbele nikawa naona kama kuna taa nyekundu zinamlika kwa mwanga mkali sana,nikayakwepesha macho nikawa sitazami mbele bali kwa mara hii nikawa natazama pembeni yaani upande wangu wa kushoto huku nikijitahidi kuyaziba macho kwani ule mwanga haukuwa wa kawaida."Mh!! Nani tena anayekuja?" Nikajiuliza nikakosa jibu.Mara ule mwanga ukaanza kujiviringisha viringisha mithili ya ule upepo wa kisulisuli ukafanya hivyo kwa muda mfupi tu baadae ukatoweka giza likarejea katika hali yake ya kawaida.Mimi nikaendelea na safari nilitakiwa kwa namna yoyote ile nifike Dar tena kwa miguu kama ambavyo nilielekezwa ,kutumia gari au kupanda chombo chochote kile nisingeweza au yote kwa yote bado nilikuwa nikimsubiri Mungu anifunulie kwa hilo hapo baadae kama ni kweli nitafika Dar es salaam kwa miguu nikitokea mkoani Mbeya au itakuaje!! Hilo likawa ni fumbo gumu sana kwangu.Nilitembea hatimaye uchovu ukaanza kuninyemelea kwa kasi,miguu yote ikaanza kuishiwa nguvu kwani tokea asubuhi sikuwa nimekula chochote wala kunywa chochote zaidi ya ile hewa ambayo nilikuwa nikiivuta.Kuna kipindi roho ilikuwa radhi kabisa kuendelea kutembea lakini mwili ukawa dhaifu mpaka ukapelekea kuchoka na kuamua kutafuta sehemu ya kukaa ili nipumzike.Sikus
ogea mbali wala wapi nilikaa pembezoni kidogo tu mwa kile kinjia nikaikunja miguu yangu na hapo sasa nikahisi kama ndo nimepata ahueni.Nikiwa nakifurahia kijiupepo cha hapo,Ghafla kwa mara nyingine tena,yule Mzee akatokea mara hii akiwa amevaa kanzu jekundu,kibaragashia cheusi mkononi kwenye mkono wake wa kulia akiwa amejifunga kitambaa chekundu na miguuni akiwa hajavaa chochote,Mzee akaanza kunicheka kwa nguvu,akacheka kisha akapotea,akaja kutokea tena.
"Hahahahaha!! Ahahahahaha!! Wewe kijana,naona wewe umeuchoka ugari,yaani mimi nimekuijia kwa amani halafu wewe unaniletea jeuri,sasa ngoja nikuonyeshe". Alizungumza Mzee yule kwa sauti nzito yenye mkoromo wa kutisha akaanza kujiviringisha mikono yake.....haraka nikasimama maana nilijua hapa kama ni Vita imeanza,,,nilisimama nikaikumbatia kwa nguvu Biblia yangu.Nikawa namtazama yule Mzee anavyonyumbulika.Mzee alinyumbulika sana bin vuu akajibadirisha akawa chatu mkubwa wa kijani akaanza kunifuata .Kuona hivyo niliinyoosha Biblia yangu kuielekeza kwa huyo chatu,ikapeperushwa juu juu na kwenda kudondoka mbali,mikononi nikabakiwa na pete tu.Muda huo huo Biblia baada ya kupeperushwa na hizo nguvu za giza niliiona ikinirudia kwa mwendo huo huo wa kupepea ikaja na kutua tena mikononi mwangu.Yule chatu badala ya kunisogelea akaanza kurudi rudi nyuma akakigeuza kichwa chake kilichokuwa kimepondeka akakimbilia vichakani akiacha nyasi zikisikika kwa ule mwendo aliokuwa akiondoka nao.Baada ya yule chatu mnene na mkubwa kukimbia nilipumua huku nikitetemeka nikakaza msuli kuendelea na safari maana safari yangu ilikuwa ni ndefu mno na isitoshe kwa hapo ndo kwanza safari nilikuwa ndo nimeianza .Nilitembea kidogo tu mambo yakaanza kuvurugika tena......Ule mwanga wa awali ulijitokeza vile vile na punde si punde yule Mzee akaonekana tena akija mbele yangu.Sijakaa sawa nikajikuta nimesimama katikati ya msitu mnene ......Chini ya miguu yangu nikawa naona vitu vyeusi sana vikizunguka na sikuweza kuvitambua.Nilibaki najikaza tu,nikajaribu kutembea angarau kusogea mbele ikashindikana,nikajaribu kurudi nyuma napo ikashindikana.Nikaanguka chini na kupoteza fahamu.Nilikuja kuzinduka nikaona nimezungukwa na kundi kubwa sana la watu wa ajabu ajabu mwenye sura zisizoeleweka.N
ikakaa,kumbe pale nilipokaa kulikuwa na shimo refu sana lisiloonekana,nilidumbukia mzima mzima ndani ya hilo shimo la kutisha,nikapaa hewani hewani bila kufika chini.Nilipokuja kufika huko chini tayari sikujua ambacho kiliendelea.Kiu
kweli ndugu yangu nazidi kukukumbusha kama una imani yako basi endelea kuishikilia usiyumbishwe na chochote maana mambo yanayo fanyika katika hii dunia hayaeleweki.Nilikuja kuzinduka nikajikuta nimelala pembezoni mwa mto mmoja mishale ya jioni jioni nguo zangu zote zikiwa zimelowana sana,mwili wote ukiwa umejaa utelezi kuashiria kuna kitu kama siyo mnyama au samaki kilinimeza na kunitema maeneo hayo,kwa kweli hilo lilikuwa ni jambo la kushangaza sana.Niliinuka japo kwa taabu nikawa najivuta vuta nisijue hata pa kuanzia maana hapo sikupaelewa na sikutambua ni wapi.Kwa ufupi nilipotea,,,nilianza kutembea kwa mwendo wa taratibu kujaribu kusogea mbele nione nafanyaje.Nilijongea nikaziacha kama hatua tano hivi za miguu ya mtu mzima nikachoka nikaamua kukaa,,,nilipiga magoti nikaanza kulia sana huku nikijilaani ni kwa nini nilizaliwa na hayo yananipata kwa sababu ipi au kosa langu hapo ni lipi maana kama ni kuchoka nilikuwa nimeshachoka na nilikuwa nishaanza pia kujikatia tamaa."Mungu baba upo wapi baba? Kwa nini niteseke namna hii,ni kwa nini Baba umeniacha mithili ya vifaranga waliofiwa na mama yao,kwa nini Baba?" Niliyatamka hayo kwa uchungu huku machozi yakinitoka,nika
jikakamua kusimama,lakini magoti hayakuwa na nguvu hivyo nikaishia kudondoka tu.Mara nikasikia sauti moyoni mwangu ikiniambia nisimame nisonge mbele majaribu hayana budi kunipata .Nikajikaza hivyo hivyo nikawa nimesimama .....nikaanza kutembea taratibu kutafuta angarau upenyo wa kutokea eneo hilo.Nilitembea kwa mwendo huo huo hatimaye nikawa nimeiona barabara moja pana ya lami nikaamua kuifuata ili kama nitamuona mtu nimuulizie hapo ni wapi.Nilitembea sana bila ya kumuona mtu yeyote yule akija,matumaini ya kuendelea na safari yakazidi kufifia huku nikibakiza wazo moja tu la kuondoka duniani thamani yangu haipo tena.Nilijilaza katikati ya Barabara ili endapo itapita gari hapo basi inigonge tu nife.Sikulala vizuri moyoni nikasikia sauti ikiniambia nisimame niendelee na safari majaribu hayana budi kunipata,,,nika
simama.Sasa kabla hata sijauinua mguu wangu kusogea walau hata hatua moja,,,,Nilidondoka chini bila kutarajia nikaanza kuvutwa na kitu kisichoonekana nikaenda kudumbukia ndani ya Bwawa la matope yaliyokuwa na harufu kali nikazama.Nikiwa natapatapa nisijue kama ile Biblia ninayo ama laa,,,kifuani nilianza kuhisi kama kuna kitu kinatembea.Ghafla nikasukumwa na nguvu ya ajabu kinyume nyuma mithili ya volcano nikarushwa pembeni kutoka kwenye yale matope,,,nikaanguka hapo na kisha kuanza kuhangaika kukaa nikakaa.Nikajitazama kifuani kwangu nikaiona ile Biblia imejishikiza yenyewe hapo huku ikiwa haina hata doa moja la matope.Nikasimama hivyo hivyo,Nikiwa bado nipo ndani ya dimbwi zito la mawazo,mara gari moja ikapita,,,moyo wangu ukaniambia nipande ndani ya hiyo gari,gari ikanifikia nikapanda tukaanza kuondoka.Sasa cha ajabu sijui shetani alijidhihirisha tena humo ndani ya gari,,,,maana katika mazingira nisiyoyatarajia ile gari nilianza kuiona ni gari yangu kabisa,viti ni vyenyewe,kila kitu nichenyewe ndani ya gari hiyo.Sijui Dereva sikuwa nimemtazama vizuri sijui.......Kama nimefumbuliwa macho vile......
Yule Dereva nikamtazama,nikabaki mdomo wazi ."Haa Mtashobya?" Niliita kwa sauti ya kupayuka,jamaa hakuitika.Ghafla akaanza kubadirika ,akabadirika hapo hapo akaonekana nyoka amekaa kwenye kiti hicho maajabu ya mwaka akiendesha gari. Niliyafumba macho yangu nikaufungua kwa kasi mlango nikajirusha nje nikaenda kudondoka vibaya sana.....Na kuanzia wakati huo sikuelewa ni kipi kimeendelea hapo.Nikaja kuzinduka ,nikashangaa kujikuta nikiwa wodini tena Jijini Dar es salaam nimetundikiwa dripu mbali mbali za maji na damu pamoja na bandage maeneo kadha wa kadha ya mwili wangu.Nikayaangaza macho huku na huko,cha kwanza kukiulizia ikawa ni ile Biblia yangu.
"Jamani Biblia yangu ipo wapi na hapa nimefikaje?" Nilisema Daktari mmoja akanitoa hofu kwa kuniambia Biblia ipo na wameihifadhi salama.Pia akaja kuniambia "Luka kwa mjibu wa wasamalia wema uliokotwa ukiwa umeanguka pembezoni mwa Barabara kuu ya kutoka jijini Mbeya kuja huku Dar es salaam ukiwa umevunjika mguu wa kushoto pamoja na mkono wa kulia na majeraha mengineyo maeneo ya shingoni tena ukiwa hujitambui kabisa.Mpaka leo umezinduka imepita takribani miezi miwili mizima na kiukweli tulijikatia tamaa tukawa tunajua utakufa tu na wala hautapona ,yaani kuzinduka kwako hapa ni kwa neema tu ". Aliongea Daktari nikaona kama ananitania vile lakini huo ukawa ndo ukweli wenyewe.Na nilipokuja kuutazama mguu wangu wa kushoto niliuona umefungwa piopi nyeupe na mkono wa kulia pia , machozi yakawa yananitoka kwa uchungu yakaishia kifuani kwangu.Niliendelea kuyaangaza macho huku na huko nikamuona mama pamoja na Nancy wamesimama huku Nancy akiwa ameliegemea bega moja la mama angu,kwa kumtazama tu alikuwa akilia.Dokta akasema hiyo siku ndo ambayo mama pamoja na Nancy walikuwa wamekuja kunichukua.Kikaletwa kile kijibaskeli cha mataili matatu wakanibeba na kunipandisha hapo,Nancy akaanza kukisukuma tukawa tumetoka nje.Nancy akawa anakisukuma huku mama akimfuata kwa nyuma tukajongea mbele hatimaye tukawa tumefika kwenye nyumba moja hivi iliyokuwa imeezekwa kwa nyasi.
*********************
Nikashtuka na kubaki nikishangaa tu ni kwa nini tumeenda hapo tusiende kwenye lile jumba langu la Kifahali,,,,Ikabidi nimuulize Nancy.
"Nancy hapa ni kwa nani,kwa nini tusiende moja kwa moja nyumbani kwetu?" Nilimuuliza swali hilo likawa kama nimemuibulia machungu kwani alianza kulia tena kwa sauti mithili ya mtoto mdogo. ....Alipotulia,alianza kunisimulia kwa sauti ya uchungu kuniambia ukweli wa yale yaliyotokea miezi miwili iliyopita.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA SITA (16).

Nilitamani sijui asiniambie tu kwa yale yaliyotokea nyumbani kwangu kwani kila nikimtazama nilihisi kama amechanganyikiwa furaha haipo tena.Lakini yote kwa yote nikaona ni bora tisa kuliko kumi nenda.Basi Nancy akaanza kunisimulia na haya ndo maneno aliyoniambia "Luka,miezi miwili iliyopita baada ya wewe kusafiri kwenda mkoani Mbeya ukakaa huko kwa siku nyingi kidogo za miezi hiyo kabla haya hayajakukuta,nyumbani kulitokea tukio moja la kuhuzunisha sana...... Ilikuwa ni majira ya saa mbili za usiku siku ya Alhamis mwezi uliopita ilitokea shoti ya umeme ikazua moto mkali sana ukaunguza nyumba pamoja na mali zote zilizokuwemo humo na kwa bahati mbaya zaidi hakuna hata kitu kimoja ambacho tulifanikiwa kukiokoa maana vyote kwa pamoja viliteketea na kuharibika vibaya.Nashukuru Mungu hakuna ambaye alipoteza maisha kwenye ajali hiyo ya moto zaidi ya hizo mali pamoja na nyumba". Aliongea Nancy akatulia mimi nikashindwa hata cha kufanya.Nikawaza nilie au nifanyaje napo nikashindwa nikabaki nikiumia tu ndani ya moyo wangu.Ilinibidi nijikaze kiume kwani hata kama ningelia isingesaidia chochote maana siku zote maji yakisha mwagika huwa ni vigumu sana kwa maji hayo kuzoleka.Nilipatwa na kigugumizi nikawa namtumbulia macho Nancy nisijue nianzie wapi na niishie wapi.Sikuelewa ni kwa sababu ipi hilo tukio lilitokea na ni kwa nini ila nilimwachia Mungu tu hata kama Mungu aliniadhibu kwa namna hiyo nilimwachia yeye tu kwani yeye ndiye ajuaye na kila ridhiki atupayo ni kwa mipango yake na Makusudi yake pia."Nancy vipi kuhusiana na biashara zangu na makampuni yangu?" Nilijikaza nikamuuliza swali hilo ili apate kuniambia pia kuhusiana na mali zangu kwamba zipo wapi kama nazo zilipotea au zilienda wapi basi nipate kujua ili kama ni kujipanga au kuanza upya nianze upya.Basi baada ya kumuuliza swali hilo,Nancy aliniangalia sana usoni akatikisa kichwa chake kabla ya kulijibu swali langu.
"Makampuni yote ndani ya mwezi huo huo kama wiki moja baada ya nyumba kuteketea nayo yaliteketea kwa moto huo huo wa umeme". Kiukweli hakuna siku ambayo iliniumiza kama hiyo,moja kwa moja nikajua tayari nimesharudishwa tena shimoni yaani kule nilikotoka!!!! Vyeti vyangu navyo viliteketea kwa moto nikabaki mimi kama mimi.Nancy akamalizia pia kwa kuniambia wale wafanyakazi wangu wote walihama na kuna baadhi tena wengi tu walianza kunidhihaki pamoja na kunicheka kwamba iko wapi jeuri yangu, dunia imenipiga sina ujanja tena na wala sitokuja kufanikiwa maishani.Basi mambo yakawa yameenda kama hivyo,tukafarij
iana nami nikawa na neno moja tu la kwamba siku zote penye magumu na majaribu ,,mbele yake huwa kunakuwaga na ridhiki kubwa sana.Hilo mimi nililikubali nikakubali kuanza upya ili mradi tu uhai ninao maana ndo jambo la kujivunia.Baadae tukawa tumeingia ndani ya hicho kijumba cha nyasi,Humo Nancy akaandaa chakula tukala baadae kwenye mishale ya jioni hivi nikamwambia Nancy anisukume kwenye kibaiskeli changu anipeleke kanisani nikaokoke rasmi.Safari ya kuelekea huko kanisani ikaanza.......Na kwa wakati huo yaani ule muda tunaondoka tayari saa kumi na nusu jioni ilikuwa imeshawadia.Nikamuuliza Nancy kama tutapita kwa kutumia barabara kuu akasema haina haja ya kutumia barabara kuu kwenda huko bali tutatumia njia za mkato ili tuwahi tusichelewe sana.Kwa hilo tukawa tumekubaliana tukaanza kuondoka.Nancy alikuwa akiisukuma taratibu baiskeli yangu ya mataili matatu muda huo macho yake akiyaangaza huku na huko.Tulitembea na baada ya kukamilika dakika kadhaa tulianza kuwasiri maeneo ya kanisani,kanisa moja la T.A.G Tabata .Na siku hiyo ilikuwa ni ya maombi,tukaingia kanisani tukaungana na baadhi ya wana maombi mambo yakawa yanaenda vizuri tu,,,baadae nikaziungama dhimbi zangu zote nikatubu maisha mapya nikayaanza siku hiyo hiyo.Mpendwa naendelea kukukumbusha kwamba shikilia sana imani yako kwani duniani tunao maadui wengi mno ambao hawapendi kutuona tukidhubutu kusonga mbele wakati mwingine maadui wako wakubwa wanaweza kuwa ni nduguzo amini hivyo na hilo uliweke moyoni.Kwa upande wangu baada ya kumwamini Yesu na kumpa maisha yangu nilijua sasa maisha yangu yatarudi kuwa katika hali ya kawaida,majaribu hayatanipata tena wala magumu hayatanipata tena kumbe ndo kwanza yaliongezeka maradufu na maisha yangu sasa yakawa ni magumu zaidi na yenye vitisho vya kufisha.
Wakati tunaondoka kanisani kwenye mishale ya saa kumi na mbili za jioni,,,,tulifika nyumbani tukamkuta mama amebadirika sana tofauti na vile ambavyo tulimuacha hadi tukawa tunamshangaa sana ni kwa nini amekuwa hivyo .Kwanza ilikuwa ni hivi,kabla hatujaingia ndani alianza kwa kutuzuia akituambia ni marufuku kuingia ndani iwe jua iwe mvua huku akitutukana sana .
"Leo mnalala nje majibwa nyie ,,,na kabla sijaamua maamzi magumu naomba mniambie kwa nini mliondoka kwenda huko.....eee huko sijui wapi,sijui kwenye mazindiko ya kimuzimu,,,Na kama hamtaniambia basi leo ni lazima mlale nje ". Kiukweli sikuamini kama maneno hayo ameyazungumza mama,ikabidi nimuombe Nancy anifuatie Biblia yangu ya kimaajabu hata kwa nguvu pamoja na kwamba mama alikuwa amejinyoosha mlangoni kutuzuia tusipite.Nancy akakiachia kijibaskeli changu akawa anazipiga hatua kuusogelea mlango......Ile anaukaribia tu huo mlango,ghafla mama nilianza kumuona akijiviringisha mithili ya joka ,,, hazikupita hata dakika tatu akaanguka chini hapo hapo akabadirika na kuwa joka aina ya chatu nene na refu lenye rangi kama magwanda ya kijeshi.Nancy akaruka pembeni..... akaanza kulikemea joka hilo akalikemea sana mwisho likatoweka pale mlangoni katika mazingira ya kutatanisha.Nancy akaingia humo ndani kwa mwendo wa umakini.....Alikuja kutoka akiwa ameshikilia Biblia yangu mkononi mwake akanipa nikaikumbatia kifuani.Na hapo ndipo nilipokuja kutambua kumbe siku zote hizo tangu nikiwa hospitalini na hapo nyumbani nilikuwa nikiishi na joka nikitambua ni mama yangu kumbe sivyo .Na hii ilionekana baada ya joka hilo kujitokeza wazi wazi likakemewa na kupotea jumla bila kuacha chochote kwa muda huo kwani ingekuwa labda lilikuwa limemwingia mama basi mama angeonekana hapo akiwa yeye kama yeye mara baada ya jenyewe kutoweka.Basi Nancy baada tu ya kunipa Biblia yangu alitoa na kiti akakaa karibu yangu tukawa tunashauriana nini cha kufanya maana kama ni mambo yalikuwa yameshaanza kuwa magumu kwetu.Tuliongea mambo kadha wa kadha tukawa tumemaliza tukaingia ndani maana giza nalo lilikuwa limeshaanza kuingia.Kama kawaida Nancy akaandaa chakula cha usiku na kilipokuwa tayari tulikula,,,,kabla ya kwenda kulala tulisali tukaingia chumbani ili tulale sasa.
Nakumbuka ule muda tunaondoka kwenda kulala ilikuwa ni saa tatu na dakika kumi na tano kama kumbukumbu yangu inasoma vizuri na bila shaka ni hivyo.Ile tunapanda kitandani tu tulale kwenye kile kitanda kidogo cha chuma.....Mimi nilianza kusikia kama kuna mkoromo wa mtu amelala sebuleni nikaamua kuupuuza mkoromo huo nikajifunika shuka lile lile alilokuwa amejifunika Nancy maana tulikuwa tukilala ndani ya chumba kimoja kitanda kimoja ila hatukuwa tunafanya chochote yaani kugusana kimwili au kufanya ngono kwani tulikuwa na hofu ya Mungu na tuliahidiana kufanya hivyo tukishafunga ndoa.Ule mkoromo ukawa unaongezeka maradufu mpaka ukawa unazitikisa hadi nyasi pamoja na ule ukuta kama tetemeko vile,,,, nilijifunua nikakiinua kichwa changu nikamtazama Nancy nikamuona amelala fofofo na bila shaka kwa upande wake alikuwa hasikii chochote.
Ghafla miguu yangu nikawa nahisi kama kuna kitu kinaifunga ,kinaifungua na kuikaza,,,kufum
ba na kufumbua wazo likaniijia na kuniambia nishuke pale kitandani nitembee kwani nimepona si mlemavu tena,ile na utazama na mkono wangu uliokuwa umefungwa piopi nao niliuona hauna piopi upo katika hali yake ya kawaida.Nikajua kwa hapo Mungu ametenda miujiza ameniponya.....wazo la kufikiria zile piopi zilielekea wapi liliyeyuka nikawa nawaza tu kwamba Mungu ameniponya.Basi nikawa nimeshuka kitandani,nikasimama na kuanza kujitizama huku nikitabasamu na kucheka mwenyewe nikawa nahisi kama naota lakini kila nikijiangalia kwa makini wala sikuwa naota bali huo ulikuwa ndo uhalisia.Nilizunguka zunguka humo chumbani kama mwendawazimu bila ya Nancy kunisikia baadae nikatoka chumbani nikawa nimeingia sebuleni.Nilipofika tu hapo sebuleni,kwenye ule mlango wa kuingilia ndani ukitokea nje nilisikia unagongwa kumaanisha kuna mtu hapo anaugonga nikataka niufungue ila moyo ukagoma nikaahirisha kuufungua.Nilikaa juu ya kigoda kimoja kirefu nikaanza kuyazungusha macho yangu nikasimama tena na kisha kurudi tena chumbani kuendelea kulala.
Nilipoingia tu humo,nilimkuta Nancy ameamka tena amekaa kitandani amejifunua yupo kama alivyozaliwa,,mwili wangu wote ukaanza kusisimka huku hisia zikinizidi mapigo.Nikajiuliza nimwambie Nancy ajifunike nisiuone mwili wake au tufanye tu yale mambo ya kikubwa nikashindwa niamue vipi.Nikiwa bado nimesimama,mapigo ya moyo yakienda kasi huku nikitetemeka kwa hisia kali.Nancy alianza kusimama huku akijichekesha chekesha......a
kaanza kunisogelea.
Niliingiwa sijui na ujasiri wa kutoka wapi maana nilikuwa kama nimefumbuliwa macho ,kile kitendo cha zinaa ambacho nilipanga kukifanya nilikighaili nikasimama imara.
***************************
"Nancy.....Nancy tafadhari nakuomba ujifunike nguo ". Nilizungumza,Nancy akaanza kurudi rudi nyuma huku akiendelea kunirembulia."Wewe Luka acha utoto mpenzi wangu.....Yaani umetengewa chakula mezani umeshindwa kujihudumia unasubiri upakuliwe,hebu acha mambo yako bwana ". Aliongea Nancy mashaka yakaanza kuniingia nikajisemea huenda huyo nae siyo Nancy amejibadirisha tu kuwa Nancy ili aniteke.Nikasema hapana.Nilijipanga nikaanza kukemea.....Sasa wakati nikikemea cha ajabu na yeye alikuwa akikemea tena kwa nguvu na sauti ya ajabu.
Nikipunguza kasi ya kukemea nae anapunguza.Dakika tano tu mara baada ya Mimi kupunguza ile kasi ya kukemea nilirushwa kwa speed kinyume nyume nikaenda kuangukia sebuleni nikasimama na kutembea kwa kasi kuelekea chumbani.Nikafika na kumkuta Nancy bado yupo katika ile ile hali ya utupu mara hii akiwa amepandisha na mapepo akitamka kila aina ya lugha zisizoeleweka.Nikaanza tena kukemea na yeye akaanza kukemea!!! Nilipoona kama nimeanza kuchoka niliifuata ile Biblia ili niichukue,,,,Nilipoifikia tu na kunyoosha mkono wangu wa kulia niitie viganjani,ilipotea hapo ikaja kuonekana kitandani.Niligeuka niifuate pale kitandani,sijakaa sawa macho yangu yakatua mlangoni.Pale mlangoni nilimuona Athumta amesimama akicheka kicheko kikali huku akiinyoosha mikono yake yenye vidole vyenye makucha marefu.Nikayepepesa kushoto macho yangu,pale dirishani napo nikaona kama kuna sura inanichungulia huku dirisha likiwa wazi bila kujulikana ni nani aliyelifungua.Katikati ya miguu yangu napo niliona mkia wa nyoka ukiishia ishia uvunguni.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA SABA (17).

Mkia huo mrefu na wa kutisha ulinifanya nibaki nikiwa nimesimama pale pale nisisogee mbele wala nyuma kwani wakati mkia huo unaonekana ilijionyesha dhahiri ulipita katikati ya miguu yangu.Athumta sasa akawa anazidi kunifuata,,,ila kabla hata hajanifikia kilionekana kitu mithili ya radi kikampiga shingoni akatoweka muda huo huo.Kwenda kutazama dirishani yale macho yaliyokuwa yakinichungulia nayo hayakuonekana tena......Hali ya utulivu ikarejea na Nancy fake akaanguka chini na kisha kutoweka,Nancy wa ukweli akawa anaonekana amelala pale kitandani ,yaani ilikuwa ni kama nimefumbwa macho vile.Basi huku nikihema juu juu nilishusha pumzi ndefu za haja nikazipiga hatua kukisogelea kitanda nikapanda na kulala.Japo niliutafuta usingizi wangu kwa taabu lakini hivyo hivyo nilifanikiwa kulala hatimaye kukaja kupambazuka.Asubuhi na mapema nikaamka na kukuta Nancy hayupo pale kitandani,nikajiuliza ameenda wapi lakini nikajua tu kwamba huenda yupo nje anaosha vyombo au anafagia uwanja wa nje.Sikuendelea kukaa hapo kitandani nilishuka nikawa natembea kwa miguu yangu mwenyewe kuelekea sebuleni maana kile chumba kilikuwa kikipakana na sebule kama mdomo na pua.Sasa baada ya kufika sebuleni niliufuata taratibu mlango wa kutokea nje ila nilipoufikia sikutoka nje moja kwa moja bali nilisimama pembeni nikawa nachungulia ,,,baada ya kujiridhisha zaidi nilitoka nje nikamuona Nancy anafagia uwanja,, mwenyewe baada ya kuniona hakukaa kuyaamini macho yake kwa kumtazama tu alionekana kupigwa na butwaa ama mshangao wa hali ya juu.Hakuweza kujizuia aliutupa pembeni mfagio wake akawa ananikimbilia akanifikia na kujirusha nikambeba kwa kumkumbatia,,,tukazungushana hapo kwa dakika kama mbili hivi baadae nikamshusha nikagundua mapigo yake ya moyo yanaenda mbio sana.
"Luka hivi naota au macho yangu yananidanganya?" Ilimbidi aniulize ili aupate ukweli.....Swali hilo wala sikulifikiria sana nilitabasamu kidogo tu kisha papo kwa hapo nikamjibu "Huoti Nancy,,huu ni uharisia kabisa kwamba kwa sasa mimi si mremavu wala nini,,kwa kusudi na uwezo wa Mungu siwezi kuitwa mlemavu mimi ".Nilimjibu Nancy akafurahi sana maana huo ulikuwa ni muujiza tena wa ajabu.Basi tuliongea mambo mengine mawili matatu,mimi nikamuaga Nancy nikawa nimerejea ndani kwenda kujipumzisha.Masaa mawili yalikatika saa nne majira ya asubuhi yakawa yamewadia.Nikiwa bado natafakari ndani nijue naanza wapi kwa maisha haya mapya,mara Nancy aliyekuwako huko nje akaniijia ndani akionekana kuwa na jambo la kuniambia.
"Vipi Nancy kuna shida?" Nilimuuliza akakaa kimya kwa muda.....baada ya kuonekana yupo tayari kunijibu alizungumza "Hapana wala sina shida ila nje kuna mgeni wako anakusubiria". Aliongea ikanibidi nisimame muda huo huo niongozane nae huko nje......Tulifika nje mgeni mwenyewe nikamtambua kuwa ndiye rafiki yangu Gerald,kwa wakati huo alikuwa amekaa kwenye kigoda huku kushoto kwake ikionekana gari moja nyeusi aina ya Range Rover imepakiwa akili yangu ikanituma nikatambua moja kwa moja kwamba gari ile ndo yake,nikabaki kimya kwa hilo nisimuulize ili kujihakikishia kwa kile nilichokuwa nikikiwaza.Nilimkaribisha nae akakubali nikakaa chini mazungumzo yetu yakaanza......Nancy yeye ili kutupisha ilimbidi aondoke hapo aingie ndani na akawa amefanya hivyo,pale nikabaki mimi na rafiki yangu wa siku nyingi Gerard.
"Ah!! Luka kwanza nipende kukupa pole kwa mahasibu yaliyokupata,pole sana ila kwa sasa nina swali moja nataka nikuulize kama hautojali".Alisema Gerard,nikamkazia macho usoni kisha nikawa nimetikisa kichwa changu kama ishara ya kukubaliana nae."Unaweza kuuliza tu wala haina shida".Niliongea nikamuona amejikuna kichwani mara tatu."Kwa sasa utaishije jamaa angu,makampuni yako yote yameteketea,wafanyakazi wako nao wamekukimbia,,,nyumba na mali zako nazo zimeteketea!!! Luka utaishije?" Aliuliza nikacheka kama mazuri vile japo kwa mtindo wa kutabasamu."Sikiliza Gerard!! Neno la Mungu linasema pesa,dhahabu pamoja na mali zote zilizomo duniani ni mali za Bwana,hivyo wala hilo haliniteteleshi mimi kwani najua nitaishi tu na hakuna kitakachoshindikana".Nilimjibu kwa ujasiri sana mpaka akanishangaa kwani hakutegemea kama nitayaongea hayo.
"Luka wewe na ulokole wapi na wapi ndugu yangu!!! Na tangu lini wewe ukamtegemea Mungu ili hali kila siku tulikuwa tukipishana kwenda kwa waganga wa kienyeji!!". Aliongea Gerard huku akiwa haamini kabisa."Kwa sasa mimi nimeokoka nampenda Yesu,kwa hiyo mambo ya kwenda kwa waganga wa kienyeji nimeshayatupilia mbali na wala sitaki hata kuyasikia". Nilizungumza akazidi kunishangaa.
"Duuh!! Ahaa!! Ahaa!! Ngoja nikuambie kitu rafiki yangu Luka,kwa hicho ulichoamua kukichagua hakika utakufa maskini,,,Walokole wangapi wanaopayuka kila siku tunawaona wakilala njaa bila ya kuwa hata na mia mfukoni,Luka achana na hayo mambo na ndio maana hata mali zako zimeyeyuka maana mali huwa hazikai kwa walokole wapoteza muda,mali huwa zinakaa kwa watu watafutaji,achana na ulokole ndugu yangu utapotea". Aliongea Gerard akawa kama anatwanga maji kwenye kinu kwani msimamo wangu sikutaka kuupindisha ya dunia niliyaona hayanifai tena zaidi ya kusonga mbele kiimani nisirudi nyuma.
"Gerard!! Hakuna jipya litakalo nifanya niyumbe hata siku moja,kama ni mali acha zinipite kushoto ili niweze kuurithi ule uzima wa milele nilioandaliwa na Baba,,,mali,wanawake warembo na wazuri wote hao nishawahi kuwa nao hivyo hawanitishi,,nimekata shauli ya kumtumikia Mungu acha nionekane mjinga au Mpumbavu ila baadae nitaeleweka kama nilichagua fungu bovu au nilichagua fungu jema". Niliongea nikamuona amekasirika sana akasimama kwa hasira,
"Tangu niijue hii dunia sijawahi kuona mtu Mpumbavu kama wewe,,amini nakuambia utakufa maskini na kuanzia leo mimi na wewe urafiki wetu unaishia hapa tusijuane,kwa kheri!!".Baada ya Gerard kumaliza kuyazungumza maneno hayo aliondoka kwa kasi mbele yangu akaiendea ile gari akafungua mlango akapanda na kisha kuondoka,akaenda zake.
Nikabaki pale natikisa kichwa changu tu......Basi Gerard akawa ameondoka,Nancy nae akaja na kukaa kwenye kile kigoda alichokuwa amekikalia Gerard."Mh!! Luka nakupenda sana yaani,acha tu kwa huo msimamo wako Mhuuuuuu siyo wa nchi hii". Aliongea Nancy huku mkono wake wa kulia akiwa ameuzungusha shingoni kwangu."Hata mimi nakupenda sana Nancy naamini kwako wewe nimempata mke mwema kwani kwa sasa wewe ni mama yangu,rafiki yangu na ndugu yangu pia maana huchagui kwa kuishi pamoja na kwamba wewe ni mrembo tena umeumbika lakini umeyaacha hayo ukaamua kuwa na mimi hata katika hali hii niliyonayo kwa sasa". Niliongea kwa sauti ya chini kidogo.
"Usijali Luka,amini nakuhakikishia wewe utakuwa mume wangu labda Mungu anichukue,lakini kama nipo hai nitakuwa tayari kuishi na wewe popote pale kwani moyo wangu umekuchagua wewe kukuacha itakuwa ni sawa na kujiwekea kisu shingoni". Aliongea Nancy baadae tukasimama na kisha kukumbatiana,,,Saa tano ilipotimia Nancy aliniaga kwamba anaenda sokoni kuhemea mahitaji kadha wa kadha ya ndani,nikamuaga nae akawa ameondoka.Sasa mara baada ya Nancy kuondoka,,,,Nikiwa nimekaa pale ghafla pasipo kutarajia usingizi ulianza kunikamata nikashindwa kujizuia na nikawa nimesinzia moja kwa moja.Usingizi ulipokolea,masikioni mwangu nilianza kuhisi kama kuna sauti ya mtu inaninong'oneza.....kwa bahati mbaya sauti hiyo ilikuwa haieleweki kwani ilikuwa na mkoromo mzito nikaipuuza nikawa najikakamua nikawa nimeyafumbua macho yangu nisione mtu yeyote yule amesimama nyuma wala mbele yangu.Dakika kadhaa zilimalizika hatimaye Nancy akawa amerudi kutoka sokoni akafika na kupitiliza ndani moja kwa moja.
Amani kwa upande wangu kwa wakati huo nikawa naiona inajaa tu moyoni mwangu,,,,Sasa katika wakati nisioutarajia,, mbele yangu ilionekana gari ya maaskari ikija ikafika na kusimama,wakashuka maaskari wapatao watano wote wakiwa na siraha za moto yaani bunduki aina ya SMG wakaanza kunizunguka nisiwaelewe......Nikiwa natetemeka nisijue ni kipi kilichowafanya waje kwangu nilisimama nikawa naipandisha juu kaptura yangu chakavu ya kaki pamoja na kulitizama shati langu jeusi lililokuwa limetoboka mgongoni.
"We boya muuaji usiyekuwa na chembe ya huruma kuanzia leo utajuta kuzaliwa,yaani unamuua mkeo Athumta unaamua kuoa mke mwingine asiyekuwa na kichwa wala miguu? Sasa utajuta kuzaliwa".Sauti hiyo niliisikia waziwazi nisimuone anayeitoa,nikageuka kulia kwangu nikamuona pasto Samba akija huku akiwa amevaa suti nyeusi gari nyeupe ndogo akiiacha kwa nyuma......Sijakaa sawa Gerard nae akaja pale na kuisimamisha gari yake akashuka wakawa wanaongozana na pasto Samba kuniijia wakafika na kusimama nyuma ya wale maaskari.Wakati huo Nancy zile purukushani za hapa na pale alizisikia akawa ametoka.Baada ya Nancy kutoka nilimuona ameiinua juu mikono yake na kisha kuiweka kichwani.
"Jamani kwani amekosea nini Luka? Ni kosa gani alilolifanya Luka?" Aliuliza Nancy huku akionekana dhahiri kuwa akitetemeka akajibiwa kwa tusi zito la nguoni ambalo siwezi hata kuliandika hapa.Mimi nikabaki njia panda tu nisijue hata cha kufanya.Nikiwa nayasikiliza kwa makini mapigo ya moyo wangu.....Ghafla nilipigwa mtama wa nguvu nikaanguka chini,wakaninya
nyua tena....Askari mmoja akanipiga kwa kiwiko cha bunduki mdomoni kwangu,damu ikawa inanitoka na tayari meno yangu mawili yalivunjika.
************************
Nancy alipatwa na uchungu akawa anaruka ruka huku akilia,machozi mengi kama maji yakimtoka.
"Niambieni basi,kwa nini mnampiga Luka jamani?" Aliuliza Nancy mara hii akajibiwa na askari mmoja aliyekuwa amejazia kifuani."We malaya haya mambo wala hayakuhusu ni bora ungekaa kimya tu".Alijibiwa Nancy akashindwa hata cha kufanya zaidi ya kubaki akilia tu."Kijana utaenda kufia gerezani,umemuua mkeo tambua hivyo na hatutaki utuulize tena". Aliongea askari mwingine.
"Sawa a....a....Afande ila ngoja niwaambie jambo moja tu,siku zote uthamani wa paka huwa unaonekana akifa na kuwaacha panya ndani wakijitawala watakavyo,ila akiwa hai unaweza kumdharau kwa kumpiga kisa tu amejisaidia ndani".Niliongea maneno hayo huku machozi yakinitoka,damu nayo ikiendelea kunitoka.Nikaji
kaza nikawa nimegeuka nyuma nikamuona Athumta akiwa katika umbo la nyoka,,,yaani kichwa cha binadamu umbo la nyoka,nae akatoweka tena.

NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA NANE (18).

Alitoweka katika mazingira ya kutatanisha mno na hakuweza kuonekana tena.Basi wale maaskari wakawa wamenikamata na mimi nikawa tayari tu kwa hilo kwani nilijua ni jaribu halina budi kunipata,,,Mungu atanipigania na kunivusha.Niliamini pia katika hii safari ya kiimani niliyonayo napita katikati ya bonde la uvuli wa mauti,njia imejawa na vitisho vya kila aina ila ipo siku na mimi nitaipata tena amani.Nilimsihi Nancy asilie bali anyamaze tu zaidi nikamkumbusha hata habari za mtumishi wa Mungu Ayubu ......Nilimwambia naenda kufungwa gerezani kwa kosa nisilolijua ila Mungu atanitoa katika kipindi asichokitarajia.
"Baki salama Nancy.....najua moyo wako unaumia mno kwa hili lililonipata ila tambua Mungu hajanifanyia hivi kwa makusudi ipo siku tu,kwa kheri"..
Ni maneno ya uchungu na yaliyojaa simanzi niliyazungumza mbele ya Nancy huku nikijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuyazuia machozi yaliyokuwa yakininyemelea yasinitoke kwani ningemfanya Nancy aumie maradufu na hata kukosa matumaini ya kuendelea kuishi.Nilimpa mkono wa kwa kheri Nancy nae akanipungia mkono nikatupwa ndani ya ile Defender safari ya kuelekea mahakamani ikaanza.Sikuamini kama ndo naenda kufungwa lakini moyoni nikawa na amani pamoja na furaha tu ,sikujua kama Mungu alikuwa na makusudi gani na maisha yangu,sikujua.Nilifikishwa mahakamani mnamo majira ya saa nane za mchana nikaenda kuwekwa rumande muda huo huo.Basi kwa siku hiyo nililala mbu wakining'ata usiku kucha,hatimaye kunapambazuka nikamshukuru Mungu kwa kusema yeye ni Bwana na siku zote atabaki kuwa Mungu tu,kila jambo,au gumu huwa halikosi mlango wa kutokea,niliamini hivyo na kila wakati sikuchoka kumtukuza yeye aliyeniumba.
Baada ya siku tatu kupita nilihukumiwa moja kwa moja kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumuua Athumta,maadui zangu wote wakafurahi mno.....nikatengwa na wengi ,wakiwemo ndugu zangu wa damu maana hata babaangu nae alinikataa.Unaweza kujiuliza haya yalifanyika vipi..... ilikuwa ni hivi,,,wakati nasomewa mashtaka bila ya kupewa muda wa kujitetea,hao wote walikuwepo maana baadhi ya ndugu zangu mara baada ya kusikia nimekamatwa kwa hilo kosa,walikuja ili kushuhudia na miongoni mwao alikuwa ni Kaka yangu mkubwa Matiku.Siku hiyo sikuamini kama hata Mtashobya niliyekuwa nikimsaidia katika shida mbali mbali kwa kunigeuka na kuanza kunidhihaki wakati nikipelekwa gerezani na hapo ndipo nilipotambua kumbe hapa duniani hata umsaidieje mwanadamu atakudhihaki na kukusema tu.Mtashobya mpaka sasa huwa najiuliza yupo wapi na ana kazi gani nashindwa kuelewa,na sijui kama bado yupo hai ama amekufa maana hawa wengine walionicheka na kunidharau kipindi hicho kwa sasa wananipigia saluti,na cha kushukuru hata huyu Athumta alikuja kuokoka katika mazingira ya kutatanisha na akawa si jinamizi tena,akawa binadamu tena maana ilikuja kujulikana kwa kipindi hicho chote kumbe alikuwa akitumiwa na nguvu za giza.Tutaona ni kwa kijinsi gani Athumta alibadirika na kuokoka,tutaona,cha msingi ni wewe ndugu msomaji kuendelea kunifuatilia na kukifuatilia kisa hiki bila kukubali kupitwa.Basi ngoja nikuwekee maneno ambayo Mtashobya aliniambia,maneno ambayo yaliniumiza mno mpaka nikashindwa kujizuia nikawa nalia kama vile mtoto aliyenyimwa ziwa na mama yake.Mtashobya alisema;
"Hahahaha!! Wazinzi bana,tangu lini mzinzi,mwasherati,mchawi na Mwizi akapata neema duniani? Hilo haliwezekani!! Luka nilikuwa nikimuona mtu mmoja mzuri tu,kumbe jamaa ni nyoka mkali,kumbe jamaa hafai,mzinzi,mu
uaji,mwasherati na bila shaka hata zile mali zake alizipata kwa njia haramu na ndio maana Mungu kampiga!!! Hahaha!! Jeuri yake kwishine,kwisha habari yake,wacha akafie gerezani ili akili imkae vizuri". Kiukweli kwa hayo maneno ninaweza sema sitoyasahau japo Mtashobya nishamsamehe,tena sina kinyongo nae kabisa pamoja na kwamba hakuja kuniomba msamaha.Vile vile hata Juliana,binti aliyekuwa akisimamia maduka yangu,nae hakubaki nyuma alinisemea maneno yale yale ya dhihaka kwa kuniita mimi ni muuaji tena malaya mwenye tamaa afadhari ya fisi.Basi Luka mimi nikawa nimetupwa gerezani na maisha mapya ya jela nikayaanza.Siku ya kwanza nikiwa gerezani ilimalizika salama ikaja siku ya pili yake nayo ikapita,hatimaye wiki moja ikapita wakati huo nilikuwa sipo tayari kula chochote wala kunywa chochote kwani sikuwa na hamu hata ya chakula pamoja na kwamba maaskari Magereza walikuwa wakinilazimisha kwa nguvu kula.Basi baada ya wiki hiyo ya kwanza kabisa kwa mimi kuwa gerezani,wiki ya pili yake ikaanza,,,siku ya kwanza ndani ya hiyo wiki ikawa imepita.Sasa siku ya pili yake ilipofika......nakumbuka ilikuwa ni mishale ya jioni kama kwenye saa kumi na mbili hivi,tukiwa tunafanya kazi tunamalizia malizia kazi za siku hiyo nje kidogo ya maeneo ya gereza,niliona gari mbili nyeupe aina ya Land cruiser zikija mbele yetu,wafungwa wote tukasimama tukawa tunazitizama zile gari tusijue ni za kina nani na zimekuja kufanya nini pale,tukasubiri ili tuone.Mara zile gari zikasimama.....Wakashuka wanaume wawili mmoja akiwa ni waziri wa ulinzi kwani nilimtambua,halafu yule mwingine alikuwa ni mzungu na sikumtambua ila nikajua tu kuwa huyo ni mchungaji maana shingoni alikuwa na kola nyeupe ya kichungaji.Wote walishuka kwenye gari moja...... Kwenye ile gari nyingine alishuka hakimu na wakili mmoja,wote wakatembea kusogea mbele kidogo wakawa wamesimama.Baad
a ya hapo akaitwa askari Magereza mmoja aliyekuwa akitusimamia.Akaenda baadae kama kwenye dakika tano hivi,akaja na kuita kwa jina,
"Lukas Mathew Madango".Nikaitika nikawa najipenyeza kwenye ule umati wa wafungwa mpaka nikamfikia akanishika mkono na bila kupoteza muda nikaongozana nae hadi kwa hao wakuu.Baada ya kuwafikia na kusikia ni kipi ambacho waliniitia sikukaa kuyaamini masikio yangu kabisa.Niliambiwa sina hatia,wala kosa uchunguzi umefanywa kwa kina hivyo wakanisihi yale mavazi niyavue kisha maaskari Magereza wafanye mambo kadha wa kadha niweze kuachiwa huru.
Mpaka inatimia saa mbili mishale ya usiku niliruhusiwa moja kwa moja kwenda nyumbani,nikawa huru kuanzia siku hiyo.Na hapo nikaamini kumbe Mungu huwa hamtupi mja wake,sikujua huo uchunguzi waliufanyia wapi nikabaki namshangaa Mungu tu.
Nilirejea nyumbani nikamkuta Nancy amejikunyata nje,Machozi yakimtoka .Sasa baada ya binti huyo kuniona hakuyaamini macho yake akawa anaona kama anaota vile lakini huo ndo ukawa ukweli wenyewe.Alinyanyuka akaja na kunikumbatia kwa nguvu,wote kwa pamoja tukalia huku tukimshukuru Mungu kwa wema na fadhiri zake.Basi tuliingia ndani,tukala kile ambacho Nancy alikiandaa ,maisha yakazidi kusonga .Takribani miezi miwili ilipita bila ya Athumta wala mchungaji Samba kunisumbua,amani ikatawala na kila kitu kikawa kinaenda vizuri tu.Tulianzisha biashara moja ndogo tu lakini ikawa inatosha kutupatia mahitaji ya hapa na pale.Maisha yakawa yanasonga kama kawaida.
BAADA YA MWAKA MMOJA.
Nilifunga ndoa takatifu na Nancy,akawa mke wangu rasmi.Nakumbuka harusi yetu ilifanyika mnamo siku ya juma mosi mwezi wa nane mwaka 2011.Siku hiyo tulikuwa na furaha isiyokuwa na kifani na kila mmoja wetu alikuwa na amani tu huku nyuso zetu zikiwa na matabasamu yasiyo fifia.Ndoa yetu tuliifunga ndani ya kanisa la T.A.G.T Tabata Dar es salaam na kwa hapa unaweza kumshangaa sana Mungu.Mimi na Nancy mke wangu hatukuwa na kipato cha kutosha kwa wakati huo lakini ili kudhihirisha ya kwamba Mungu ni tajiri kwa wote wanaomtumaini,aliibua watu sijui kutoka wapi tu wakaighalimia harusi yetu ikawa kubwa kuliko hata unavyofikiria.K
wanza ile kamati iliyokuwa imeundwa ikiongozwa na hakimu yule ambaye alinihukumu mwanzo ilikuwa si mchezo ndugu yangu,na huyo hakimu alikuja kuwa rafiki yangu mkubwa wa chanda na pete.Watu kwenye harusi yetu walikula hadi wakasaza.Jioni yake ilipofika tulipelekwa kwenye ukumbi wa maana huko tukaenda kuzawadiwa zawadi za kutosha huku tukiahidiwa ahadi kede kede.Basi mambo yote yakawa yamemalizika,tu
kachukuliwa na gari hadi hotelini......hoteli ya kifahali ambayo iliandaliwa kwa ajili yetu.
Sasa ile tunaingia ndani ya chumba maalumu kwa ajili ya kuianza rasmi fungate yetu ilitulazimu kwanza tukaiandae miili yetu ikae sawa.Hivyo tukaingia bafuni tukaoga tukamaliza,kwa pamoja tukarudi tena chumbani kwa ajili ya kuifurahia ndoa yetu maana kwa kipindi hicho tulikuwa huru kufanya chochote hata kukutana kimwili kwani tayari tulikuwa tumeshaunganishwa kuwa mwili mmoja.
Tulipakana mafuta mazuri yenye harufu ya kuvutia tukamaliza na hapo sasa ile shughuli tukaianza.Kwanza tulipanda kitandani tukawa tunacheza ile michezo ya kitoto ya kurushiana mito baadae tukasogeleana tukawa tunabusiana huku tukiwa tumekumbatiana.Nilimsukuma Nancy mke wangu akalala chali mimi nikapanda juu yake nikawa namtomasa taratibu huku nikimgusa kila sehemu ya mwili wake kwani kwa wakati huo wote tulikuwa hatuna nguo mwilini mwetu.Wakati nikimtomasa mke wangu,kama kwenye dakika tano hivi alianza kuhema juu juu kama ishara ya raha alizokuwa akizipata maana pamoja na kuhema kiasi hicho pia alikuwa akiguna ile miguno ya taratibu taratibu.Nilipohakikisha nimemwandaa vya kutosha huku jogoo wangu akiwa amesimama vizuri,Nancy alianza kudai kwamba nimpe maana mabao ya nje alikuwa ameyafunga vya kutosha tu hivyo binti alikuwa tayari ameshalainika na kuuachia mwili wake wote yaani niufanye nitakavyo.Sasa nikiwa najiandaa kuanza kumwingilia huku jogoo wangu nikiwa nimemshika nimuweke kunako ndani ya kitumbua kizuri cha mke wangu......Ghafla nikalisikia tumbo langu likiunguruma.Li
liunguruma kwa mara ya kwanza likatulia.
**************************
Likaunguruma kwa mara ya pili napo likatulia mimi nikawa sijali zaidi ya kumsogeza jogoo wangu kunako kitumbuani kwa mke wangu,kitumbua ambacho kilikuwa kimejaa bluu band za kutosha.Sasa wakati nahangaika kukichomeka huku Nancy akijigeuza geuza,tumbo langu likaunguruma kwa mara ya tatu.Nikahisi maumivu makali ya kutisha chini kabisa ya tumbo langu,,,,Nikahisi kama kuna mlio umesikika "KAT-A" jogoo akalala na hakuweza kuamka tena.Hisia zote zikakata maumivu ndo yakachukua nafasi mpaka yakawa yanauzunguka mwili wangu wote.Nilimtazama Nancy kwa huruma akiwa ameipanua miguu yake nikatamani nimwambie lakini nikashindwa nimwambieje maana kwa hali aliyokuwa nayo pale ilikuwa ni afadhari ya mtu aliyesukumwa kutoka ndani ya gari lenye mwendo kasi speed mia na ishirini.Mke wangu alikuwa akiyafumba fumba tu macho yake.
"Mume wangu nini jamani ,mbona umetulia tu jamani,tuendelee basi".Ilisikika sauti nyororo ya Nancy ikiyaongea hayo,mimi nikashindwa hata nimjibuje maana nilikuwa nikihangaika na maumivu tu.
Ghafla nikasikia sauti ya kicheko kikali sana cha kike kikipenyeza masikioni mwangu baadae kikatulia ......kwenda kujiangalia kwenye nyeti yangu tayari damu nyingi ilikuwa ikinitoka.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA KUMI NA TISA (19).

Nilianza kujibangaiza nisipate hata nguvu za kuamua chochote,,,,ghafla nikakumbuka ninae mumeza anayenipigania nikajikaza kiume nikawa naomba kimoyo moyo kwa nguvu sana,,kama kwenye muda wa dakika tatu hivi ile damu ilitoweka,,,nyeti yangu hapo hapo ikawa sawa na ikasimama tena.Nilifurahi mno nikaendelea kumshughulikia mke wangu na tukawa tumefanikiwa kufanya tendo la ndoa salama salimini na wote tukalifurahia mno kwani tulipata raha.Basi hilo likawa limemalizika,tukalala kwa ajili ya kuiaga siku hiyo.Masaa ya usiku yakawa yanasogea kama kawaida hatimaye kukapambazuka,maisha yakaendelea.Siku hiyo nilikaa na mke wangu tukaanza kupanga mambo mengi sana ya mhimu yanayohusiana na maisha yetu kwamba tufanye nini ili maisha yasonge."Mke wangu nimepata wito wa kwenda kusomea Uinjilisti kwani nahisi kabisa hiyo ndo kazi niliyoitiwa na Baba".Maneno hayo niliyatamka mbele ya Nancy mke wangu wakati huo nikiwa nimeuzungusha mkono wangu wa kulia shingoni mwake."Mimi nakusikiliza wewe tu mume wangu,na kama Mungu kakupangia uifanye kazi yake hakuna haja ya kuipinga".Alisema Nancy muda huo akiwa amenikazia macho usoni.Tulielewana vizuri na kwa pamoja tukawa tumekata shauli ya kumtumikia Mungu katika maisha yetu.Basi mipango ya kutafuta chuo cha Biblia ikawa imeanzia hapo.Sikutaka kungoja katika wakati unaofaa bali nilisimama muda huo huo unaofaa kwa ajili ya kutafuta chuo nianze mara Moja kujifunza neno la Mungu.Kesho yake mambo yalienda vizuri na Mungu saidia nilifanikiwa kupata chuo cha Biblia maeneo ya Mwanza huko ,nikatakiwa kuripoti masomoni baada ya miezi mitatu maana kwa kipindi hicho ulikuwa ni mwezi wa nane 2011,ina maana kwenye mwezi wa kumi na mbili tarehe za mwanzoni mwanzoni ndo zingekuwa za mimi kusafiri hadi jijini Mwanza kwa ajili ya kuyaanza masomo ya Biblia..... degree yangu ya uchumi kwa kipindi hicho ilinibidi niiweke kando kwanza kwani kwa jinsi Mungu alivyokuwa akinipitisha kwenye tundu la sindano ningekuwa mjinga sana endapo ningekataa kumtumikia , mathalani hata leo hii nisingekuwepo kwani ningeshakufa zamani sana.
Basi hilo likawa limekaa hivyo likabaki suala la muda tu.......Ilipita wiki moja bila ya kusumbuliwa na Athumta huku amani ikirejea kwa kasi,nikasubiri siku ya juma tano ya wiki hiyo ya tatu ya mwezi iwadie niangalie utaratibu wa kwenda mkoani Mbeya kwa yule Mzee ili kama inawezekana niifuate gari yangu pamoja na ile wallet kwani Mzee alishaniambia hivyo kwamba mambo yangu yakikaa sawa basi ni lazima niifuate .Basi siku moja yaani juma tatu ikawa imepita,,,siku inayofuata nayo ambayo ilikuwa ni ya juma nne ikawa imetoweka.Kesho yake sasa ndo ilikuwa ni siku ya juma tano......Siku hiyo ilipambazuka vizuri tu ,hali ya hewa ikiwa imetulia.Nilidamka mapema kwenye saa kumi alfajili nikamuamsha na mke wangu tukasali mpaka kwenye saa kumi na mbili hivi.Jua lilipoanza kuchomoza nilianza kujiandaa tayari kabisa kwa safari ya kwenda Mbeya.Nilimaliza maandalizi yangu baada ya dakika kumi hivi,,,nikaichukua na ile Biblia yangu nikaagana na Nancy kwamba naenda nitarudi nae akanitakia safari njema,nikawa nimetoka humo ndani.Sikutafuta bodaboda kunipeleka stend ya mabasi bali nilitembea kwa mguu kutoka pale nilipokuwa nikiishi na mke wangu hadi stendi ya mabasi ya kwenda mikoani.Kama sijasahau,wakati nafika huko nililikuta Basi moja aina ya Sheraton la kuelekea Mbeya likiwa tayari tayari nikakatiwa haraka tiketi nikapanda ndani,,,,safari ya kwenda Mbeya ikawa imeanza.Njia nzima nilikuwa nikiimba kimoyo moyo huku nikimuomba Mungu anifikishe salama niendako aniepushie ajali na mambo mengine ya ajabu ajabu huko niendako.Kweli Mungu kwa upendo na neema yake ya ajabu akawa amenifikisha jijini Mbeya nikiwa salama kabisa.Mbeya tulifika baada ya masaa machache tu tofauti na mwanzo wakati ule naenda na gari yangu .Basi nikawa nimefika jijini Mbeya,nikashuka na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee maana kutoka stend ya Mabasi hadi huko,umbali wake ulikuwa ni wa kilomita tano maana Mzee alikuwa akiishi milimani milimani na alikuwa amejitenga sana na miji ya watu.Nilitafuta bodaboda ya kuniwahisha huko.Tayari kwa mjibu wa saa za Africa ya Mashariki saa sita majira ya mchana yalikuwa yameshawadia.
Nilifika nyumbani kwa yule Mzee kwenye mishale ya saa saba kamili mchana,Mzee akanikaribisha vizuri akaniandalia chakula kwa upendo wake nikala na nafsi yangu ikawa imeridhika .......Kabla hajanikabidhi ile gari yangu pamoja na wallet ambayo imekaa kwake kwa muda wa mwaka mmoja na nusu,,,aliniambia maneno haya.
"Mwanangu.....Najua umepitia magumu mengi sana hadi unafika hapa ulipo,Mungu hajakuacha wala hajakutupa kwani bado ana makusudi na wewe hivyo inakupasa uendelee kuupiga konde moyo wako maana safari bado ni ndefu sana na iliyojaa kila aina ya majaribu na magumu ya kutisha,vumilia na jitahidi upambane ili uweze kuyashinda majaribu yote yatakayokupata"
.Alizungumza huyo mzee na akisha kumaliza alinikabidhi moja kwa moja ile wallet pamoja na ufunguo wa gari nikasimama ili nimuage niondoke kwani hata muda ulikuwa umeendelea sana na ilinipasa nirudi siku hiyo hiyo bila kungoja kesho .Basi nikawa nimepanda ndani ya gari yangu ambayo ilikuwa na mafuta ya kutosha.....nikawa naiendesha kwa mwendo wa taratibu ili nishuke kwenye kile kinjia chembamba chenye mteremko wa kutisha!! Nilishuka na gari pole pole hatimaye nikafanikiwa kutoka.Niliikamata njia moja ya lami nikaongeza kasi ya kudrive maana sikutaka kupoteza muda,nilitamani niwahi mapema nyumbani nikaonane na mke wangu Nancy.Nilizidi kuchanja mbuga,nikasogea mbele zaidi nikawa nimeziacha takribani kilomita kumi.Sasa baada ya kuziacha hizo kilomita ,,,mara mbele yangu nikawa naona kama kuna mtu amesimama,kwa bahati nzuri muda huo speed nilikuwa nimepunguza hivyo ikawa virahisi kwa mimi kuisimamisha gari.Nilipoisimamisha tu,cha ajabu mtu huyo hakuonekana tena.Nikawaza,huenda Athumta yale mambo yake ameyaanza tena,,,,Niliwaza kidogo tu,jambo hilo nikawa nimelitupilia mbali nikakamata usukani niendelee na safari yangu.
Nilidrive gari kwa muda mfupi tu mbele tayari yule mtu niliyekuwa nimemuona awali akajitokeza kwa mara nyingine tena.Mara hii akawa ananiijia yaani tukawa tunakutana kati yake yeye na mimi pamoja na kwamba yeye alikuwa akiniijia kwa miguu.Alipozidi kunikaribia tu kwa mbele alitoweka tena,,,baada ya kuona hivyo sikubaki kimya nilianza kukemea,nikakemea mpaka kikaeleweka kabisa na mambo yote yakawa sawa,hali ya hewa ikawa imerudi katika hali yake ya kawaida.
Nikazidi kusonga mbele kuendelea na safari.....Nilitembea mwendo mrefu nikawa nimeziacha hatua za kutosha nyuma hatimaye nikaifikia barabara nyingine yenye mikato mikato .Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya kuikamata hiyo njia na kujiona kama ndo nimeshayamaliza matatizo yote nilikuja kukata kona yenye mteremko mkali gari yangu ikafeli break ikapinduka kama mara tatu hivi ilipokuja kutulia tayari ilikuwa chini ya mtaro pembezoni kidogo mwa ile barabara huku mataili yote yakiwa juu .Nilipoteza fahamu pale pale nikawa sijui chochote kinachoendelea.
BAADA YA WIKI MOJA .
Nilikuja kuzinduka nikiwa hospitalini nimelazwa kwenye kifaa maalumu kuashiria mgongo wangu ulikuwa umeumia vibaya sana.Watu niliowaona humo ndani akiwemo mke wangu Nancy niliishia kuwakodolea macho tu kwani ule uwezo wa kuzungumza sikuwa nao,yaani ninaweza kusema niligeuka kuwa bubu kwa muda.Nilimtizama Nancy nikamuona analia machozi yakimtoka baadae akaanza kuzungumza kwa uchungu.
"Mungu kwa nini? Kwa nini kila siku ni sisi tu,mume wangu amekuwa bubu? Haya mateso yatakwisha lini? Hizi tabu zitaisha lini?".Alilia sana Nancy mpaka baadhi ya wauguzi wakamshikilia na kutoka nae nje kwenda kumtuliza zaidi .Yaani ilikuwa ni zaidi ya uchungu ndugu yangu!!! Kwa magumu ambayo niliyapitia acha tu Mungu niendelee kumtumikia maana amenitoa mbali sana.Sasa kwa mujibu wa maelezo niliyoyasikia kutoka kwa Daktari akimwambia rafiki yangu hakimu yalikuwa ni maneno ya masononeko mno,maneno mazito na ya kukatisha tamaa.
"Luka mpaka hapa tumejitahidi kwa kadri ya uwezo wetu ila....ila kwa kweli acha tu niseme ukweli maana tukiendelea kupeana matumaini tutakuja kuchukiana bure tu.Luka uti wake wa mgongo umevunjika mara saba ina maana mpaka hapa alipo mwili wake hauna mawasiliano na miguu.Kiuno nacho kama unavyomuona kimevunjika mara tatu na hapa tumekiwekea hichi chuma kama egesha tu .Na kama atafanikiwa kupona basi hatakuwa na uwezo wa kukaa wala kutembea".NILIOA NYOKA SEHEMU YA ISHIRINI (20).

Maneno hayo baada ya Daktari kumaliza kuyazungumza huku akimtazama rafiki yangu hakimu usoni alitikisa kichwa akawa anazunguka zunguka wodini mara ajishike kiunoni kama ishara tu za kuchanganyikiwa.Mimi kwa huo muda sikuwa na uwezo kabisa wa kuzungumza pamoja na kwamba yale maongezi yao nilikuwa nikiyasikia .Sasa wakati Daktari anahangaika kuzunguka zunguka hana mbinu tena.....Ghafla moyoni mwangu nikawa nahisi kama kuna msukumo unaniambia niinuke nikaupuuza kwa mara ya kwanza,zikapita dakika tano nikausikia tena ule msukumo moyoni mwangu na hapo ndipo nilipoanza kujaribu kuinuka .Kumbuka kwa wakati huo nilikuwa nimelazwa ndani ya kifaa maalumu kwani mgongo wangu ulikuwa umefungwa kwa vyuma kutokana na kwamba uti wa mgongo ulikuwa hauna kazi.Nilijaribu kwa mara ya kwanza kuinuka.....Nikamuona Daktari akinijia kwa kasi kunituliza kwa ishara nisifanye ninachotaka kufanya,lakini mimi nikawa simuelewi nikawa nazidi kujilazimisha tu kuinuka maana sauti ya kunisihi nifanye hivyo ilikuwa ikizidi kuchipuka kwa kasi ya ajabu moyoni.Daktari alichanganyikiwa zaidi,akamuita Hakimu nae ajaribu kunituliza nae akashindwa ikambidi awakimbilie madaktari wenzake ili ikiwezekana wanishikilie kwa nguvu.Alitoka mbio hadi nje na punde si punde akaja akiwa ameambatana na madaktari kama kumi hivi wakaniijia na kunikamata,nikamuona mke wangu Nancy akija huku akiwa ameshikiliwa na wauguzi wapatao wawili maana alionekana kama nguvu zimemwishia na kwa haraka haraka alionekana kujikatia tamaa na mimi.Sasa wakati lile jopo la madaktari wakihangaika kunituliza pamoja na kunishikilia kwa bidii na juhudi zao,,,,nilianza kulia kwa nguvu tena kwa sauti ya juu.Nguvu ya ajabu ikaniijia uwezo wa kuzungumza nao ukanijia nikawaambia hapo hapo,,
"Vyuma mlivyonifunga mgongoni pamoja na Vifaa vyenu vyote naomba mviondoe sivihitaji,naomba mviondoe kwa jina la Yesu ,,viondoeni kwa jina la Yesu maana nitaishi wala sitakufa kama ambavyo nyinyi mnadhani kwani ile kazi aliyoniitia baba bado sijaikamilisha,
niondoleeni vyuma vyenuu".Niliyatamka hayo kwa sauti ya nguvu mpaka nikahisi ukuta ukitingishika.Madaktari wakaanza kunong'onezana wao kwa wao nisiwasikie wazungumzacho,mara wakanikaribia madaktari watatu wakanigeuza na kuanza kuniondolea vile vyuma walivyokuwa wamenifunga.Sasa walipoviondoa tu,ghafla Daktari mmoja kati ya wale watatu akapayuka "NO.....NO....NO!! Haiwezekani nasema haiwezekani huyu shetani hapaswi kuishi,kwa nini amepona ili hali mkuu wetu alituambia mwisho wake umewadia? No......noooo!!".Alitamka yule Daktari wenzake wote wakashtuka wakaanza kutazamana wasiweze kumuelewa kabisa,wasielewe ana maanisha nini kuyatamka hayo.Wakiwa bado wanaendelea kumshangaa ghafla yule Daktari alidondoka chini na hakuongea tena,,, madaktari wenzake wakambeba juu juu wakatoka nae nje sikufahamu walimpeleka wapi alipona au alikufa.Mwanaume nikashuka pale kitandani nikiwa na nguvu za ajabu nikamfuata mke wangu nikamfikia na kumshika mkono tuondoke mara Moja humo ndani,Hakimu nae nikampa ishara kwamba tuondoke kimya kimya tukawa tumetoka tukazipiga hatua tukawa tumelifikia geti la kutokea nje tukasimama hapo .Daah!! Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni ya maajabu sana,siku ya Mungu kulipiza kisasi kwa maadui zangu wote waliokuwa wakinitakia mabaya.Sasa tukiwa tumesimama hapo niliingiliwa na nguvu ya ajabu nikageuka nyuma nikawaona wale madaktari wamesimama huku wakiwa wamepigwa na butwaa wasiamini kwa kile wakionacho.....yamkini waliamini mimi siyo binadamu wa kawaida mimi ni mchawi kumbe mchawi wangu ni Yesu ndiye anayenitia jeuri pamoja na nguvu.Ghafla nikaanza kuwatazama Nancy na rafiki yangu kwa zamu nikameza fundo zito la mate nikawa nimeyainua juu macho yangu.
"Zamu ya maadui zangu kupigwa kama ambavyo walikuwa wakinipiga mimi imewadia...... siwezi kurudi nyumbani mpaka nione maadui zangu wote wamepigwa". Nilizungumza nikawa nimetulia kidogo."Mume wangu basi itatubidi twende nyumbani kwanza angarau ukapumzike mume wangu".Alisema Nancy nikamkazia macho usoni "No....nitarudi endapo hili litafanikiwa lisipofanikiwa nikafie huko huko nisirudi tena". Nilizungumza wote wakawa wananishangaa mno.
"Lakini Kaka ni bora turudi kwanza nyumbani angarau ukapate hata juisi maana humu ndani yaani hospitalini umekaa kwa siku nyingi sana hivyo itakuwa vyema sana tukiambatana kwanza kwenda nyumbani".Alisema hakimu huku akinishika begani kwenye bega langu la kulia."No....siwezi kurudi nyumbani,muda wa Baba yangu wa kuwapiga maadui wote waliokuwa wakinitakia mabaya umewadia !! Nitarudi nyumbani endapo hili litafanikiwa na kama halitafanikiwa sirudi hadi mwisho wa dunia".Niliongea wakawa wananong'onezan
a"Naenda msituni kupambana na maadui zangu,nyie tangulieni tu huko nyumbani mimi nitarudi baadae maana masaa yamewadia".Baada ya kumaliza kuyazungumza hayo nilichomoka mbio za ajabu,nikawa nakimbia bila kugeuka nyuma huku nikiwa peku peku watu wakinishangaa na bukta yangu nyekundu nisiwajali......nikatoka mbio mbio hadi kwenye moja ya misitu ndani ya maeneo hayo nikazama humo.Nikawa nimesimama!!! Sasa baada ya Mimi kusimama,kama kuna kitu furani hivi kiliniambia nitazame chini,nikayashusha macho yangu nikawa nimetizama chini.Kutazama kwa makini niliyaona majoka makubwa manne yamenizunguka huku yakiwa yameviinua juu vichwa,ndimi zikiwa nje nje maana yalikuwa yameachama na midomo kiukweli ilikuwa ikitisha sana.Ghafla Majoka matatu yakapotea kimiujiza,pale likawa limebaki joka moja ambalo lilionekana kuwa dogo kiasi ukilinganisha na yale ambayo yalitoweka!!.Nilibaki nimesimama pale pale nisisogee kulia wala kushoto.Sasa lile joka nalo likaanza kuniijia usawa wa kifua changu,,,likaniijia nikaliona likinyanyuka juu kama hua au ndege likapaa kukifuata kifua changu...Sasa mimi kuona hivyo niliinyanyua mikono yangu yote nikawa natazamana na joka hilo likiwa na kasi ya ajabu katika kupaa.Niliirush
a mikono yangu kwa nguvu nikatamka "Kwa jina la Yesu nakupigaaa!!".Joka likarudi rudi nyuma likawa limedondoka chini likagaa gaa kidogo lilipokuja kukaa sawa halikuwa joka tena bali binadamu tena mwenye mwonekano kama wa dada yangu Milembe."Hahahaha!! Luka tangu lini wewe ukawa na uwezo wa kupigana na mapepo ili hali wewe nakufahamu hata kabla haujakua!! Hahaha kimbia watakumalizaa!!".Niliyasikia maneno yale nikasema hapana,nikayatamka maneno haya kwa nguvu ile ile "Kwa jina la Yesu nakupigaaa.....nakupigaaa!!".Likadondoka chini,lilipokuja kusimama lilikuwa na muonekano wa uhalisia yaani binti ninayemfahamu,L
ilian,,mara hii akiwa na sura ya kutisha!! Lilian akaanza kunisogelea huku akicheka kicheko kikali cha kutisha!!! Alipozidi kunisogelea ulishuka moto ukasimama katikati ukinitenganisha mimi na huyo Lilian,,,ghafla katika mazingira ya kutatanisha ule moto kwa macho yangu nikauona ukitembea kumfuata!! Badala ya kuendelea kucheka,mara hii akaanza kulia,kilio kikali chenye uchungu mzito.Akajaribu kuanza kukimbia ,kule alipogeukia ili akimbilie ule moto wa ajabu ulimtokea mbele yake ukawa unamrudisha,akageuka akimbilie kwangu napo ule moto ukajitokeza ukamrudisha,akaishiwa nguvu,bin vuu akaanguka chini ule moto ukamfikia na kumdonoa kidogo tu akalia mara Moja akatulia kimya.Moto ukatoweka!!!.
Nilimfuata Lilian pale chini nikawa nimemfikia nikamgusa kifuani kwake mara tatu akazinduka na kukaa akawa anayaangaza macho yake huku na huko."Haa!! Nipo wapi hapa? Nipo wapi jamaniii? Haa!! Kaka Luka hapa nipo wapiii? Bibi.....Bibi.....Bibi .... Bibi ananiijia ,,,,naona kitu......naona kitu cha ajabuuu kinaniijia,kina miguu ya pundaa". Lilian akawa analia huku akiyatamka hayo maneno .....mimi nikausikiliza moyo wangu utaniambia nini!! Moyo ukaja kuniambia nimshike mkono binti huyo nimsimamishe halafu niweke mikono yangu juu ya kichwa chake.Nilipokuja kufanya hivyo.....Lilian aliinama akawa anatapika upupu pamoja na vitu vyeusi vingi vingi nguvu zikamwishia akazimia kwa mara ya pili.Moyo ukaniambia nisogee nyuma muda wa wengine kufunguliwa na muda wa ukombozi umewadia.Nilisogea nyuma nikamuacha Lilian akiwa amelala pale chini.Bin vuuu,likatokea joka jingine likamzungukia Lilian pale chini likawa linatoa sauti ya muungurumo wa hasira likajaribu kummeza Lilian likaambulia kurushwa mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme likaanguka chini,lilipokuja kusimama liliyeyuka,hapo hapo kwenye eneo hilo hilo akaibuka Simba akijaribu kuja kwa kasi,,,,kasi yake haikufika popote kwani alipigwa vibaya sana mnyama huyo wa ajabu na akawa ametoweka kimiujiza.Punde si punde akaonekana mwenyewe kwenye uhalisia wake na huyo hakuwa mwingine bali ni aliyekuwa rafiki yangu Gerard ila kwa wakati huo alikuwa na sura ya kutisha yaani sura ya kuogopesha!! Ile anainyoosha tu mikono yake yenye makucha marefu.Ule moto wa ajabu ukatokea ukasimama mithili ya binadamu.Sasa hali ile ilimchanganya Gerard akaishusha mikono yake ili akimbie lakini wapi,,,,alipojaribu tu kugeuka akimbie!! Alidondoka chini.Ule moto ukamfikia na kumdonoa mara mbili kama kuku adonoavyo punje,Gerard akatulia kimya huku akiwa amelala chali ,ule moto ukatoweka.Hazik
upita hata sekunde tano
******************************
Likaja kutokea joka la tatu nalo likajaribu kupaa kunifuata kikaonekana kitu mithili ya radi kikalipiga likaanguka chini ,,,cha ajabu baada ya joka hilo kuanguka lilianza kulia kama binadamu tena kwa sauti ya kike.Likatulia likaanza kunyanyuka tena.Likafanikiwa kukiinua juu kichwa,,,sasa baada ya kuwa limefanikiwa kukiinua juu kichwa cha lenyewe liliachama likaanza kutema mate ovyo hovyo nguvu zikaliishia likaanguka chini kwa kishindo likatulia kimya.Mimi kwa wakati huo nilikuwa nimetulia zangu nikitazama jinsi Mungu anavyofanya maajabu kwa hayo majinamizi.Sasa lile joka baada ya kuwa limedondoka chini na kutulia lilitoweka!! Kwa mbali nikamuona Athumta akija kwa kasi huku akilia,kwa muda huo damu nyingi sana ilikuwa ikimtoka puani pamoja na mdomoni,,,,aliponikaribia tu alianguka chini akaanza kugaa gaa huku akiendelea kulia kwa uchungu.Moyo ukaniambia nimsogelee nikafanya hivyo,,,kabla hata sijatamka neno lolote Athumta alichuchumaa bila kutegemea akakohoa kikohozi cha ajabu,kikohozi cha kutisha!!! Muda huo huo akaanza kutapika damu yenye mchanganyiko wa magamba ya nyoka.Nilipoyai
nua macho yangu mbele ,nilimuona mtu mmoja wa ajabu amesimama mgongoni mwa Athumta akiwa amenyoosha upanga unaong'aa kama umeme.


NILIOA NYOKA SEHEMU YA MWISHO (21).

Sikuweza kujua yule mtu alikuwa na lengo gani maana kila baada ya dakika moja alionekana akiurusha upanga wake wa ajabu juu chini kisha anaganda.Nilibaki kimya kumtazama wakati huo huo Athumta akiendelea kulia kwa uchungu mara hii akiwa hatapiki tena..... Athumta alilia sana mwisho akaanguka na kupoteza fahamu.Sasa baada ya Athumta kupoteza fahamu yule mtu hakuonekana tena ina maana alipotea katika mazingira ya kutatanisha.Ukimya ulitanda kwa muda nikasogea nyuma umbali kama wa mita ishirini hivi nikasimama wima ,nikawa nawatizama wale watu yaani Athumta na wenzake wawili wakiwa bado wapo chini wamelala na hawajitambui tena,moyo wangu ukasoneneka mno yaani ukawa unaumia kupita kawaida.Nilianza kujongea mbele nikazipiga hatua nikawa nimefanikiwa kumfikia Athumta nikamtikisa kidogo akawa ameamka na kisha kukaa hapo hapo.Baada ya kunitazama kwa makini ikawa kama amefumbuliwa macho maana alistaajabu sana.
"Luka?.....Luka hapa ni wapi na ni nani aliyenileta hapa?" Aliuliza Athumta,nikatab
asamu kidogo baadae nikamjibu."Hapa ni msituni Mungu amekuleta hapa baada ya kugundua ulikuwa ukitumikishwa na shetani ila kwa sasa upo huru".Nilimwambia akawa kama haamini amini maana binti hakuwa akifahamu wala kuelewa chochote."Shetani? Shetani alikuwa akinitumikisha kivipi wakati mimi ni mkristo na nimeokoka?" Aliuliza Athumta."Okey dada Athumta hii ni story ndefu sana nitakuja kukukumbusha baadae".Nilimjibu baadae nikamsimamisha nikamkumbatia nikawa nimemketisha tena chini.Nilimuacha hapo nikazipiga hatua kumfuata mwingine ambaye ni Lilian nikamfikia na kumgusa kifuani akainuka na kisha kukaa chini akawa ananitazama sana usoni."Kaka Luka hapa tupo wapi na ni lini mimi nimerudi nchini wakati nilikuwa India kimasomo na nilienda miaka miwili iliyopita?" Aliuliza Lilian akanishangaza mno ila nikaja kutambua hakuwa yeye kwa wakati huo bali ibirisi alikuwa ameuvaa uhalisia wake yaani muonekano wake kwa lengo moja la kumwangamiza kwa kumtumikisha kwa mambo machafu na haya yote Mungu mwenyewe alikuwa amenifunulia kabla."Hapa tupo kwenye msitu wa Mungu,tukirudi mjini nitakwambia vizuri na wewe mwenyewe utajua".Nilimjibu Lilian baadae nikamuacha nikamfuata Gerard pale chini na yeye nikaenda nikamgusa kifuani akanyanyuka akawa ananikazia macho usoni na mimi nikawa namkazia macho vile vile."Mh! Luka !! Hapa nipo wapi na hizi nguo nimezivaa saa ngapi wakati asubuhi tu nilikuwa na suti nyeusi ofisini kwangu...Kaka Luka hapa ni wapii?" Aliuliza Gerard sikumjibu bali nilimshika mkono nikamnyanyua juu kwa pamoja tukaanza kuzipiga hatua kuwasogelea kina Athumta.....Sas
a wakati tukiendelea kuwasogelea ghafla mgongoni mwangu nilihisi kama nimepigwa na kitu kizito mithili ya chuma nikaanguka chini uso wangu wote ukatapakaa mavumbi.Nikiwa nawaza nimepatwa na nini......Ghafla sauti nzito ya kutisha mithili ya baragumu ikasikika ikisema "We-we....We-We!! Umeamua kunichokoza kwa kuwatwaa watu wangu si ndio?" Sauti hiyo ya kutisha ilisika namna hiyo nikageuza uso wangu chini kwa chini nikakutana na jitu la ajabu refu jembamba lenye sura isiyoonekana limevaa kanzu nyeusi ndefu yenye marinda mekundu likiwa limesimama karibu kabisa na ubavu wangu wa kulia likajaribu kunikanyaga kichwani likaghaili likawa limebaki likinitizama tu.Ghafla mwanga mkali sana ukaonekana radi ya ajabu ikashuka ikalipiga jitu lile likaanguka pale pale likaanza kutokota kama mboga ya maharage likawa limetulia.Niliposimama kulitazama nililiona limeteketea na kuwa na muonekano mweusi kama oili kumaanisha kwamba tayari lilikuwa limeshakufa.Nilichuchuma ili nilichunguze nikawa nayaangaza macho yangu nikakutana na kidude furani hivi chenye chapa ya jina linalosomeka "THE GREATER PASTO SAMBA".Nikalitafakari sana hilo jina baadae nikaja kulielewa,ila hilo jinamizi bado niliendelea kulishangaa sana kwani sikuwa nikilielewa nikahisi kama ndo hivyo basi pasto Samba ndo aliyekuwa mkuu wa majini pale mtaani na kama limekufa basi hata yeye katika ule uhalisia wake wa kawaida kesho ama kesho kutwa muda wowote ule atakufa.
Sikuwa na muda wa kupoteza niliwakusanya kina Athumta nikawashika mikononi tukawa tunatembea taratibu kuelekea nyumbani.Nyumba
ni kwangu ndipo ambapo tulielekea yaani kwenye ile nyumba ya nyasi niliyokuwa nikiishi,huko nilimkuta mke wangu Nancy,hakimu pamoja na watu kadha wa kadha akiwemo mchungaji wangu mlezi mshauli wangu kutoka katika kanisa hilo la T.A.G.T Tabata.Mkeka ulitolewa,wote tukawa tumekaa pale ,maongezi yale ya kawaida yakaisha zikiwemo salamu na nini na nini,baadae mazungumzo mazito yenye ushuhuda ndani yake yakaanza.Kiukweli tangu niokoke katika maisha yangu sikuwahi hata siku moja kupata nguvu ya kuomba kama ambayo niliipata siku hiyo,haikuwa ya kawaida kabisa ilikuwa na msukumo wa ajabu yaani nilijikuta nimesimama tu bila kutarajia nikaanza kuomba,nikaomba jamani,nikaomba tena kwa nguvu ya kutisha.Sasa ile namaliza tu kuomba!! Athumta,Lilian,Nancy mke wangu,Gerard pamoja na Hakimu wote walikuwa wamelala juu ya ule mkeka kama ishara ya kupoteza fahamu isipokuwa mchungaji pekee.Mchungaji nae alisimama nikaungana nae tukawa tunawaombea baadae wakainuka na kuketi,kila mmoja akaanza kutoa ushuhuda wake ila ule ushuhuda wa Athumta ndo ulikuwa ukitisha sana.Athumta kabla ya kuanza kuutoa ushuhuda wake alianza kwa kulia kwanza huku machozi mengi kama maji yakimtoka bila kumhurumia.
"Mimi Athumta....Jamani mimi Athumta!! Asante Mungu kwa kuniokoa.Nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa 2006 mara baada ya Mimi kuingia kidato cha pili,siku moja nikiwa naelekea shuleni asubuhi kwenye majira ya saa moja njiani nilikutana na Mzee mmoja hivi amevaa kanzu nyeupe,koti jeusi na kibalakuitikiagashia cheupe na mkongojo wake akitembea kuelekea kusini mwa ile barabara ya mikato mikato niliyokuwa nikienda nayo.Sasa baada ya kuwa tunakaribiana nae zaidi nilimsalimia akaitikia vizuri tu.Sasa baada ya huyo mzee  alianza kunisogelea karibu akanifikia nikawa nimekaribiana nae umbali wa mita mbili akaniuliza kwa lugha ya kizaramo akisema " Binti unaitwa nani?" Nikamjibu naitwa Athumta akakubali kwa kutikisa kichwa chake,baadae kama sekunde moja hivi akaniuliza tena "Una sali kanisa gani?" Swali hilo likawa limenichanganya sana nikajiuliza huyu si ni shehe kwa nini ananiuliza swali linalohusiana na makanisa na si misikiti,kiukweli nikawa simuelewi kabisa ila nikamjibu tu kuwa mimi ni mkristo na nina sali katika kanisa la KKKT Tabata akaguna na kisha kuvua mkufu wake wa dhahabu aliokuwa ameuvaa shingoni akanitazama sana usoni akaniambia "Binti,hakuna haja ya kuendelea kutaabika hapa duniani,maisha ni haya haya hakuna maisha mengine baada ya kufa.Mimi nakushauri hama haraka ndani ya hilo kanisa na usiende tena maana siku zako zipo ukingoni waumini wa humo wanakuwazia mabaya.Ukizubaa tu umekwisha!! Kuna kanisa moja linaongozwa na mchungaji anayejulikana kwa jina la Pasto Samba,ni mchungaji mmoja mzuri sana na ana upako wa kimungu na anatenda miujiza mikubwa na mambo mengi mazuri ikiwemo kuwatajirisha waumini wake,hamia huko kuanzia leo".Yule Mzee baada ya kumaliza kuyazungumza hayo alinisihi na kunibembeleza sana niupokee ule mkufu wa dhahabu kama zawadi yake kwangu.Nilikataa kataa baadae nikakubali ule mkufu nikawa nimeupokea na kisha kuuweka ndani ya begi langu la shule nikawa nimeagana nae.Nilitembea nikaziacha hatua chache tu nyuma nikasema nigeuke nimtazame yule Mzee,,,cha ajabu baada ya kugeuka kumtazama sikumuona zaidi ya kuona mkia wa kiumbe kisichojulikana ukiishia ishia kwenye moja ya vichaka eneo hilo,,mwili wangu wote ukasisimka na kuanzia hapo nguvu zikawa zinaniishia,hazikupita hata sekunde tano nikaanguka pale na kisha kupoteza fahamu.Kuja kuzinduka nilijikuta nikiwa hospitalini nimelazwa,jioni yake tu nikawa nimepona kabisa na kurudi katika hali yangu ya kawaida .Baada ya siku tatu,moyoni nilianza kuhisi kuwa na nguvu ya ajabu mno ,nikakataa kila kitu ikiwemo shule nikamwambia mama yangu waziwazi kwamba mimi sitaki shule tena,nataka kumtumikia Mungu katika kanisa la mchungaji Samba.Mama alinishauli sana nisimuelewe mwisho akaniacha niendelee na maamuzi yangu.
Kuanzia hapo nikawa mtu wa ajabu ajabu tu,nikilala kidogo tu tayari sina ufahamu tena,ndoto za kutisha nazo zikawa zinaniandama.Mara niote nimesimama katikati ya Bahari nikiwa nimezungukwa na majoka mara niote nimemezwa na joka halafu linakuja kunitapika yaani ilikuwa ni tabu sana ndugu zangu.Kila nikijaribu kuwaza kumshirikisha mama kuhusiana na hilo,kinywani mwangu kuna kitu kama zipu kisichoonekana kilikuwa kikinizuia na kunifanya nibaki na siri hiyo hiyo miaka yote hiyo . Kiukweli baada ya kuwa muumini mkomavu wa kanisa la Mchungaji Samba,ndani ya miaka mitatu tu tayari nilikuwa nimeshamiliki majumba makubwa pamoja na magari makubwa na madogo.Baadae yule mchungaji akaja kuniambia ili nizidi kuwa na mali nyingi zaidi inanipasa kila baada ya mwezi mmoja nitoe sadaka.Siyo sadaka za pesa au vyakula bali ni sadaka za damu yaani kafara za kuuwa watu hususani ndugu zangu wa karibu .Sasa kwa vile akili yangu ilikuwa imetekwa hilo wala halikunipa shida nililikubali nikawa nauwa watu kwa majira tofauti tofauti wakubwa kwa wadogo ,na hilo nilikuwa nikilifanya nikiwa na muonekano wa nyoka japo sikuwa nikijielewa pindi nigeuzwapo kuwa nyoka.Niliendelea kufanya hiyo kazi kwa muda mrefu sana na nikawa nimeizoea.......Na ule mpango wangu wa kuoana na Luka sikutaka nioane nae hivi hivi tu bali nilikuwa na lengo nae tena kubwa na ndio maana ile siku ya kwanza kabisa nakutana nae nilijifanya kuwa kama binti mcha Mungu,mshamba,mkalimu nisiyejua chochote.Luka kwa kipindi hicho nilikuwa nimeshampima na kugundua alikuwa na damu kali yenye kila aina ya nyota nikawa napanga kumpoteza kwa njia yoyote ile,Daah! Mungu anisamehe sana,na ashukuriwe yeye maana ameniokoa tena ameniokoa kupitia huyu huyu Luka niliyekuwa nikipanga kumwangamiza na siku zote maisha mwangu nitamtukuza yeye na nitamwabudu yeye maana amenifungua kutoka katika dimbwi la matope niliyokuwa nimezamishwa,Mungu anitie tu nguvu".
Alimaliza Athumta kisha , Mchungaji akampigisha magoti akaanza kumuombea kwa mara nyingine tena,akawa amemaliza.Mambo yote yalipokamilika ,Tulisimama tukaanza kuomba kwa pamoja baadae tukaagana kila mmoja akaondoka kuelekea kwake.Mimi na Nancy tukaingia ndani kuendelea na maisha tukiwa tunaisubiria ile miezi mitatu ipite twende Mwanza .Basi siku hiyo ikawa imepita......Baada ya siku tatu,tulisikia taarifa za kifo cha mchungaji Samba kwamba mchungaji huyo alikutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni yaani baa akiwa uchi wa mnyama.Hilo likawa limeenea kihivyo na likapita vile vile kwani jamaa huyo alizikwa na habari zake zote zikawa zimeishia hapo.
BAADA YA WIKI MOJA.
Yapata majira ya saa mbili za asubuhi ndani ya kanisa la T.A.G.T Tabata,siku ya juma pili,Athumta,Lilian pamoja na Gerard wote waliokoka wakawa wamefanyika kuwa wana wa Mungu wakawa wapya si majoka tena .Nakumbuka siku hiyo hata baadhi ya ndugu zangu nao walikuwepo ndani ya hilo kanisa wakiushuhudia ukuu wa Mungu na miujiza yake ambayo aliitenda .Baada ya Ibaada kumalizika,Athumta alitualika mimi,mchungaji ,Gerard ,Hakimu ambaye nae tayari alikuwa ameshaokoka,Nancy mke wangu pamoja na Lilian twende nyumbani kwao kuna karamu ya maana ametuandalia.Huko tulifika mishale ya jioni jioni kwenye saa kumi na moja hivi.
"Acha basi.....Usinichekeshe mtumishi".Ni maneno ambayo aliyatamka Athumta baada ya kutaniana mawili matatu na pasto ."Kawaida tu Athumta,haya ni mambo madogo madogo sana". Mchungaji nae aliongea wakati huo mimi nikiwa nimekaa kimya nikitafakari .Basi tuliendelea kufurahi pale mpaka giza likaingia....Baadae tukaagana tukawa tumesambaa na kila mmoja akaelekea nyumbani kwake..
Basi maisha yakawa yanaendelea vizuri tu....Baada ya mwezi mmoja mbele,mke wangu alipata ujauzito yaani huo ujauzito aliupata ikiwa imesalia miezi miwili tu tusafiri kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya masomo ya Biblia pamoja na kumtumikia Mungu kwa ujumla maana huo ndo ulikuwa wito nilioitiwa.
BAADA YA MIEZI MIWILI.
"Wapendwa,kama ni safari nimeshaimaliza,vita nimejitahidi kuvipigana na kwa uweza wa Mungu nimeshinda.Kiukweli siku zote Mungu huwa hamtupi mja wake akiamua kumsaidia au kumtetea hakika hakuna hata mmoja awezaye kupinga .Kwa hapa nilipofika acha tu nimshukuru yeye aliye juu kwani kama siyo yeye sidhani kama ningekuwa hapa,bila shaka ningeshakufa zamani .Daah!! Sijui hata nisemeje ila ngoja tu niwaage.... Asubuhi hii kama mnavyo niona nitasafiri kuianza safari yangu ya kwenda jijini Mwanza kusoma kwenye moja ya vyuo vya Biblia mkoani humo.Nipende tu kusema,tusimuache Mungu katika maisha yetu,zaidi tuendelee kumtumikia yeye kwani atatufikisha salama safarini,,,,naondoka kimwili hapa Dar es salaam lakini siku zote nitakuwa nanyi rohoni".Maneno hayo niliyaongea siku ile nasafiri kuelekea Mwanza mbele ya kina Athumta na wenzake.Baadae tukashikana mikono tukamalizia na dua,tukaagana nao kwa kupeana mkono wa kwa kheri.Mimi na Nancy tukaliendea Basi letu tupande tuondoke.Hakika hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana."Kwa kheri Luka,kwa kheri Nancy tutaja onana baadae".Ni maneno ya Athumta yaliyokuwa yanajipenyeza mara kwa mara masikioni mwangu wakati Basi likizidi kutembea kusonga mbele.Maneno hayo alikuwa ameyatamka kabla mimi na mke wangu hatuja panda Gari kuondoka.
Hadi leo hii,Athumta amekuwa kama dada yangu,nampenda sana na namuomba Mungu azidi kumuinua katika huduma yake ya uhubiri na Uinjilisti kwani kwa sasa hakamatiki kwenye suala la neno la Mungu na ni mwana maombi mzuri sana .Hadi muda huu mimi ni mchungaji kwani baada ya kufika Mwanza na kuanza masomo yangu ya Theolojia nilitumia muda wa miaka minne nikawa nimemaliza ambapo baadae nilikuja kusimikwa rasmi kuwa mchungaji .Nimeokoka na nina mpenda Yesu.Nina watoto wanne na bado naendelea kuishi kwa amani ,pamoja na kwamba sina magari kama zamani.Duuh!! Ila nimemis sana rafiki yangu Hakimu na wenzake,,,likizo hii itabidi niende Dar kuwasalimia.
MWISHO.

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : NILIOA NYOKA
NILIOA NYOKA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2020/01/nilioa-nyoka.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2020/01/nilioa-nyoka.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content