Featured Post

JINSI YA KUPIKA WALI WA MAUA

JINSI YA KUPIKA WALI MZURI WA NAZI NA MAUA WENYE KUNUKIA


WALI MZURI WA NAZI NA MAUA

MAHITAJI YA KUPIKA WALI WA MAUA

 • -Mchele
 • -Karoti
 • -Hoho
 • -Iliki
 • -Njegere
 • -Kitunguu saumu
 • -Tangawizi
 • -Nazi ya kukuna ni nzuri zaidi
 • -Chumvi

MAELEZO YA JINSI YA KUPIKA WALI WA MAUA

 1. -Kuna nazi yako vizuri uikamue na uichuje kidog kidogo kiasi cha maji yatakayotosha mchele wako kisha bandika tui jikoni lichemke
 2. -Osha njegere zitoe kwenye maji
 3. -Chambua iliki kisha zisage ziwe unga/robo kijiko cha chai
 4. -Chambua mchele na uoshe
 5. -Chambua kitunguu saum menya na tangawizi kisha visage kwa pamoja na mafuta ya kula kisha chota kijiko 1 kikuwa cha chakula cha mchanganyiko huo
 6. -Katakata karoti na hoho muundo wa vibox vidogodogo
 7. Jinsi ya kupika
 8. -Bandika sufuria yako jikoni,weka mafuta kidoogo saaana
 9. -Kisha kabla hayajapata moto weka njegere hii inazuia njegere kutorukaruka,koroga hadi njegere zibadilike rangi
 10. -Kisha weka Karoti endelea kukuroga
 11. -Weka mchanganyiko watangawiz na kitunguu saum koroga hapa usichelewe sana maana vitunguu huwa vinawahi kushika chini
 12. -Weka unga wa iliki kisha mchele
 13. -Koroga hadi vichanganyike haswaaa
 14. - Weka tui lako la Nazi lote ulilochuja kisha weka chumvi koroga na ufunike
 15. Baada ya muda angalia wali wako kama umekauka ile nazi uliyoweka kisha palilia(weka moyo juu na chini kidogo)
 16. Subiri kama dk 20 angalia kama umeiva weka hoho ulizokwisha zikata hapo awali kisha geuza kidoogo na funika tena kwa dk 5.
 17. Baada ya hapo waweza pakua wali wako ukiwa na harufu nzuuri na mauwa yake ambayo ni karoti ,njegere na hoho
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni