Featured Post

USHAURI | MUME HATAKI DADA AINGIE CHUMBANI

Kaka naomba ushauri wako, mimi ni mama wa miaka 42, nimeolewa na ndoa yangu ina miaka 18 sasa, muime wangu ni mtu mzima kidogo ana miaka 49, kusema kweli kwenye mambo mengine yupo vizuri, katika miaka 18 ya ndoa, hajawahi kunipiga, hajawahi kunitukana, ni mtu muelewa na si mtu wa wanawake ila mume wangu ana tatrizo moja.

Anapenda umwinyi sana, mimi nafanya kazi nayeye anafanya kazi, nyumbani tuna binti wa kazi, tukirudi wote tunakua tumechoka, lakini anataka bado mimi nifanye kazi za ndani. Kwenye chakula anakula chakula cha binti wa kazi, ishu inakuja kwenye kufua na usafi wa chumbani, mimi sio kama ni mvivu lakini kama mtu una binti wa kazi kwanini asifanye kazi za ndani wakati namlipa.

Sasa tatizo nikuwa, mume wangu hataki binti wa kazi kuingia chumbani kwetu, madai yake nikuwa yeye ni mtu mizima na binti wa kazi ni kama mtoto wake hivyo mazoea ya kuingia chumbani hataki. Kusema kweli tunagombana kwa vitu vidogo vidogo, mfano kazi zake nyingi anafanyia chumbani, kama binti wa kazi labda asubuhi wakati anatandika kitanda na kufanya usafi akiweka vitu vibaya basi mume wangua kirudi akaulizia kitu chake anataka ni mjibu mimi.

Kama ni kimuita binti wa kazi na kumuuliza labda kitu flani umeweka wapi basi mume wangu ataongea mpaka basi. Atalalamika na kusema kuwa nafanya makusudi kwakua namdharau lakini si kweli. Kaka mimi nafanya kazi, siwezi kufanya kazi za ndani pia, kufua mume wangu anafua mwenyewe kwani mimi nafuliwa na binti wa kazi ila yeye hataki na mimi namuachia anafua mwenyewe.

Sababu ya kuja kwako nikutaka kujua kama mimi nakosea au la? Hivi Kaka kama mwanamke anafanya kazi ni lazima kufanya na kazi za ndani wakati kuna binti wa kazi. Natana nijue kuna tofauti gani ya kitanda kutandikwa na binti wa kazi na mimi kutandika. Huoni kama ni mfumo dume kama wote tunafanya kazi kwanini mimi nifanye kila kitu, yeye hana shida na kwingine ugomvi wake mkubwa ni kwanini binti wa kazi anaingia chumbani kwetu?

Anataka afanye usafi kwingine lakini si chumbani na wala hataki nguo zake zifuliwe na binti wa kazi kwani anasema ni mtoto mdogo, naomba nisaidie hapo Kaka?
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni 1

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment
  1. Mm sio kaka ni mama ila ninakushauri : kuwa na mfanya kazi sio suluhisho la kusema ww usijishughulishe na chochote ndani ya nyumba yako mfanya kazi ni msaidzi tu wa kazi ndogo ndogo kwa pale unapobanwa kwa namna fulani natena usiwe unamruhusu kukufulia nguo za husband wako huo ni usungo👌 na usimruhusu kuingia chumbani kwako hata kwa bahati mbaya ni bora ukamtuma mtoto wako kama unae hata kama wakiume niheri ingawa sio vizuri mtoto wa kiume kuingia chumba cha wazazi wake hasa akisha balegh ila nibora kuliko dada wa kazi, mm nampongeza👏 huyo mume kwa msimamo wake💯 kumbuka jukumu la nyumba ni la mke nasio dada wa kazi, wengi tunakosea kwani hatujui nn thamani ya dada wa kazi ndio mana majukum yote tunawaachia wao nahii ni moja kati ya chanzo cha kuvunjika kwa ndoa, mke hujishughulishi kila kitu unamuachia dada wa kazi mwisho mume huondoa mapenzi kwako na kuyahamisha kwa dada wa kazi kwa uzembe wetu🤷‍♀ hivyo fuata matakwa ya mumeo mpikie umfulie wakati ameonyesha kukujali na uaminifu kwako mshukuru Allah kukupa mume bora nina mengi ya kukufunza ila kwa haya machache niishie hapa.✍

    JibuFuta