UKURASA WA 56 SEHEMU YA 10 | BongoLife

$hide=mobile

UKURASA WA 56 SEHEMU YA 10

UKURASA WA HAMSINI NA SITA 
SEHEMU YA 10

Baada ya dakika kumi, Cheing alitoka akiwa kavalia suti nyeusi ambayo ilimkaa vema sana. Alijiweka safi kana kwamba hakuwa na matatizo. 

"Hizi ni nguo ambazo mke wangu alininunulia. Nazipenda kuliko nguo zote."Akawaambia wale polisi. "Tunaweza kwenda Kim." Akamwambia yule mwanadada na kisha yeye akatangulia akiwaacha wale wawili wakijadili. 

Dakika tano mbele, Kim na Cheing walikuwa ndani ya gari huku mwanadada akiwa nyuma ya usukani wa gari na mawazo kadhaa yakipita kichwani mwake. Je? Apambane na Masai au aachane naye na kufutilia ushahidi atakaopewa na kijana yule wa Kiafrika. 

Nusu saa ilitosha kwa wawili wale kufika eneo walilokubaliana na Masai. Walimkuta Masai amefika na kasimama katikati ya barabara huku mikono yake kaificha kwa nyuma na tabasamu la uhakika likiwa limepamba uso wake. Gari lingine kabisa, yaani tofauti na lile analolitumia, lilikuwa pembeni yake likiwa na familia nzima ya Cheing. Mwanadada akasimamisha gari umbali wa mita hamsini na kumuangalia Masai ambaye alitoa simu na cha kushangaza, akaipiga kwa Sheiming Kim, mwanadada anayefanya kazi makao makuu ya polisi pale Korea Kaskazini. 

"Shuka ndani ya gari. Mpe usukani Cheing. Usithubutu kufanya ujinga wowote. Naona mpaka ndani na naziona silaha zote ulizona na alizonazo huyo fisadi muuaji. Mwambie aitoe hiyo bastola kwenye soksi na akupe wewe, pia ndani ya gari nitakaloileta familia yako, kuna bomu ambalo baada ya kubadilishana, nitakwambia jinsi ya kulitegua. Msijifanye wajanja, mtapoteza watu wasiyokuwa na hatia kama mlivyofanya jana." Masai aliongea bila kuogopa. 
Sheiming Kim, akafanya alichoambiwa na kumuonya Cheing. Mzee yule alimwambia mambo machache mwanadada yule ukiwemo wosia juu ya familia yake. Kisha baada ya maneno hayo machache, Cheing aliwasha gari na wakati huo Masai akamruhusu Mke wa Cheing naye awashe gari na kuja hadi pale barabarani. Mwanamama akafanya hivyo na Cheing alipofika katikati ya barabara, Masai akamruhusu yule mama naye aanze kwenda. 

"Cheing, ukijidai mjuaji tu. Nalipua gari la familia yako." Masai aliongea kwenye kipaza sauti kama kumuonya na Cheing hakuwa na jinsi, akapishana na familia yake huku mwanamama akimuangalia na machozi yakimtoka. Cheing hakuwa na la kufanya zaidi ya kupepesa midomo yake akimwambia mke wake kuwa anampenda. 

Gari la Cheing lilifika kwa Masai na kijana yule alimtaka Cheing atoke kwenye usukani. Cheing akafanya hivyo na Masai alimfunga pingu na kumuweka upande wa abiria. Akatoa kitambaa cheusi na kumvisha usoni, kisha akatwaa simu yake na kumpigia mwandada Sheiming Kim. 

"Kata waya wa buluu. Kisha fungua mkoba akaokupa huyo mama. Fanya vema." Masai alimwambia Kim. "Na kuwa makini, Six hayupo mbali na wewe."Akamaliza na kukukata simu. 
Maneno hayo ya mwisho ndio yakaharibu kabisa mipango ya mwanadada Kim kumfuatilia Masai. Kwa sababu kama Six alikuwepo maeneo yale, basi ni wazi alikuwa anamendea ule ushahidi ambao Masai alisema kuwa atampa Kim.
****
Kim aliingia ndani ya gari alilokuwepo Mke wa Cheing na kisha akamtaka ampe mkoba ambao Masai alisema kuwa unabomu. Mwanamama akafanya hivyo huku akiwa anatetemeka maana aliambiwa na Masai kuwa endapo mkoba ule utatikisika, basi mabomu yale yatajigonga na kulipuka.
Mkoba ulikuwa umezungushiwa nyaya nyingi lakini zikiwa ni za rangi nne pekee, yaani nyeupe, njano, buluu na nyekundu. Kim akatoa kikatio kidogo cha nyanya na kisha akakata waya wa buluu ambao aliambiwa aukate. Alipofanya hivyo, nyaya zingine zote zilijiachia na kisha mkoba ule ukafunguka. 
Hapo macho yakatua kwenye karatasi nyingi sana lakini juu ya karatasi hizo, kulikuwa na mfuko mdogo wa nailoni unaonesha hadi kilichopo ndani. Kulikuwa na kitunza kumbukumbu (memory card) na nje ya nailoni ile, kuliandikwa kwa Kikorea Kaskazini kwa maana ya "MUHIMU". Kim akachukua kile kifuko na kukiweka mfukoni na kisha akatizama huku na huko. Tayari Masai alikwishapotea eneo lile na sasa alibaki yeye na familia ya Cheing ambapo watoto wake walikuwa wamepitiwa na usingizi.

Sheiming aliingia ndani ya gari alilokuja nalo mke wa Cheing na kisha alimpa taarifa kuwa mkoba ulikuwa hauna bomu bali nyaraka muhimu ambazo alipaswa kuzifikisha mahali husika. 

Gari lao liliwashwa na Kim alianza safari ya kurudi alipotoka. Akiwa njiani anarudi ndipo akakuta gari la Six likiwa limekaa katikati ya barabara huku yeye akiwa kakalia boneti na sigara yake akiivuta na kupuliza moshi angani. Kim akasimama na kumtazama Six na kushindwa kujua afanye nini. 

Six akatoa simu yake na kumpigia mwanadada. "Naomba ulichopewa na huyo mjinga." Six aliongea kwenye simu. "Kabla sijawamaliza nyie wote." Akaongeza. Kim akawa katika wakati mgumu ambao hakuwahi kuukabili. 

"Inspekta, lakini ulisema nipate ushahidi kisha uhukumiwe, kwa nini unafanya hivi lakini?" Mwanadada akabwata kwenye simu. 

"Acha upumbavu wewe. Unadhani mambo yanaenda kizembe namna hiyo? Unadhani nipo tayari kuaibika wakati naweza kukimbia hiyo aibu? Leta ulichopewa kabla sijatumia nguvu."Akaongea Six na Kim alijua wazi kazi ya Six akiamua kuifanya. Six alikuwa ni mkali wa shabaha, akilenga tairi alikuwa hakosi, akilenga jicho ujue tayari umeshakuwa kipofu. Hamna ambaye hakumjua Six kwenye shabaha.
"Okay.. Sijapata mzigo mkubwa, ni mkoba tu?" Akaongea Kim. 

"Hamna shida. Mimi sitaki mkoba, nataka gari zima. Wewe toa watu wako nje na kuingia kwenye gari hili, usitoke na kitu chochote, zaidi ya watu." Six akaongea na bila kusita, Mke wa Cheing alitoka na mtoto mmoja na Kim alitoka na mtoto mwingine bila hata mabegi ya nguo. "Safi kabisa. Mnaweza kwenda mlipopanga kwenda."Six aliwapa ruhusa baada ya kuhakikisha hamna mzigo mwingine ambao walitoka nao. 

Mwanadada Sheiming akapanda gari la Six na kuondoka akiliacha lile gari la Masai akiwa nalo Six ambaye aliingia ndani yake na kuanza kulipekuwa. Aliuona ule mkoba na aliufungua. Alikuta makaratasi mengi lakini kubwa zaidi aliloliona, ni picha ambazo alikuwa anafanya mambo yake. Alimeza mate na kupitia picha moja baada ya nyingine. Zilikuwa ni picha ambazo Six hakudhani kuwa zinaweza kupatikana katika dunia ya leo. Akazama kwenye mawazo na kufikiria mengi sana.
Uzuri hata simu ya huyu mwanamke ninayo. Kama alipiga picha, hamna ambacho atafaidika." Akawaza huku anafungua faili moja na kukuta mambo mengi kuhusu yeye. "Huyu mpumbavu sijui katoa wapi haya mambo. Mh! Yawezekana anasiri hata za Rais huyu." Akazidi kuongea peke yake. Na mwisho wake wa upekuzi, uliishia kwenye nguo za watoto pamoja na za mama yao. Lakini hakukuta kitu. Akawasha gari na kuondoka eneo lile bila kujua gari lile si lake. 
****
MIAKA KUMI NYUMA

Katika Kijiji cha Pohang kilichopo Kusini mwa Korea, kulitokea janga kubwa la njaa hiyo ni baada ya Urusi kujitoa kwenye kuwapa msaada Wakorea. Watu pekee ambao walikuwa wanategemewa na Korea Kaskazini ni Japan ambao waliweza kuwasaidia Korea Kaskazini kwenye vita yao dhidi ya Korea Kusini ambao wao walisaidiwa na Marekani ambaye aliingia kama Mwanajeshi Umoja wa Umoja wa Mataifa (UN). Baada ya vita hivyo kuisha, ndipo Umoja wa Sovieti ambao uliongozwa na Urusi, ukawa upo bega kwa bega na Korea Kaskazini ambaye alikuwa katika hali mbaya kwenye uchumi. Lakini baadae Sera za Sovieti ambao walitumia sana ujamaa, zilifunikwa na sera za Ubepali (Capitalism) ambapo Marekani na Uingereza ndio walikuwa vinara wa kusambaza sera hizi duniani huku wakitumia mbinu za mapinduzi ya viwanda kulaghai baadhi ya nchi kuingia katika Ubepali. 

Ndipo katika Kijiji cha Pohang, njaa kubwa ikiwa imeikamata nchi, yenyewe ikapata nafasi ya kupata chakula kutoka Japan ambapo wapo karibu kabisa na kijiji kile. Baada ya msaada huo, serikali kupitia Waziri wake wa Afya wakaamua kwenda kugawa chakula hicho huku wakitaka kitakachobaki kiende mjini. 

Chakula kilikuwa ni kichache na haikuwezekana kwenda mjini na kwa sababu mjini hapakuwa na njaa kama vijijini, wakataka chakula hicho badala ya kugawana na wa mjini, basi wagawane na kijiji cha jirani. 

Taarifa zilipofika kwa Waziri teule wa kitengo hicho cha Afya mambo ya vyakula, alikataa katakata akisisitiza anataka kuona chakula hicho kikija na mjini. Kauli hiyo ikazua mtafaruku na ndipo Waziri yule alichukua jukumu la kumuhabarisha Waziri wa Ulinzi wa kipindi hicho ambaye ni Cheing. Naye bila kusita, akatuma wanajeshi ili waende kusimamia hali hiyo ambayo ilikuwa inaleta vurugu katika kijiji kile. 

Wanajeshi walipofika hali ikazidi kuwa mbaya baada ya wananchi kuja juu wakidai Serikali yao imewaletea wanajeshi angali chakula wamebarikiwa kupewa wao. Vurugu ikazidi kuwa vurugu na kikubwa wanajeshi wale waliweza kudhibiti chakula kile ili kisiharibe au kufanywa chochote kibaya. Hasira zikazidi kuwapanda wananchi wale wenye njaa. Wakaanzisha vita dhidi ya wanajeshi, vita ambayo ilitumia silaha za jadi pamoja na vitu vingine kama mawe na vyuma walivyokuwa wanavifua. 

Waziri wa Ulinzi ambaye alipewa jukumu na Rais kutuliza ghasia hizo kwa njia yoyote, ikabidi aongeze wanajeshi pamoja na silaha nzito. Kabla hajafanya lolote, alitoa wosia juu ya wananchi wale kuwa wafikirie watoto wao kabla hawajafanya upuuzi wanaotaka kuufanya. Wananchi hawakusikia na zaidi, walikusanya watoto wao na kuwaficha kisha wao wakaingia vitani kupambana na jeshi la nchi yao. 

Usiku wa manane, waliwavamia wanajeshi kwa silaha zao pamoja na chupa zenye petroli. Wakachoma mahema wanayolala Wanajeshi na lile ghala la chakula, nalo wakalipiga kiberiti. Wanajeshi wakawa hawana mbinu kwa kuwa tayari walikuwa wamedhitiwa ma wanakijiji.

Asubuhi yake, taarifa zikazagaa Korea ya Kaskazini kuwa wanakijiji wamechoma chakula na kuwadhibiti wanajeshi wa Jeshi la Korea. Na hilo likampa hasira Rais ambaye alitaka kumfuta kazi Waziri wa Ulinzi ambaye ni Cheing. Na ndipo kwa uoga mkubwa, Cheing akatuma jeshi la ukombozi kwa ajili ya kuwakomboa wanajeshi waliowekwa chini ya ulinzi na wanakijiji. 

Wanajeshi walipofika kwenye kijiji cha Pohang, walianzisha vita ya silaha za moto na wanakijiji na walijibu kwa sababu walikuwa na silaha hizo walizozikamata. Vita ilikuwa ni vita na ilidumu kwa saa moja. Jeshi la ukombozi lilikuwa limewaokoa wanajeshi wake na kuwakamata wanakijiji waliokuwa wameanzisha vita ile. Walipigishwa magoti na kufungwa kamba kwa nyuma pamoja shingoni kama vile watumwa. 

Simu ikapigwa kwa Waziri, naye alikuja kijijini na kuongea na wale wananchi kuwa hakupendezwa na tukio lile. Baada ya maneno mengi, aliamuru wananchi wale waachiwe huru huku wanajeshi wakitakiwa nao kuondoka na kuwaacha wananchi wale waendelee na majukumu mengine. Waziri alishangiliwa na kuonekana kuwa ni mkombozi toka kwenye ule utumwa. 

Baada ya wanajeshi kuondoka, wananchi wale walichukua miili ya wenzao na kuifanyia maziko huku bado wakiwa hawajawarudisha watoto wao waliowaficha kijiji cha jirani. Usiku huohuo, Waziri Cheing alipiga simu kwa mkuu wa jeshi la anga akiagiza kuwa atume ndege itakayoenda kuhangamiza kijiji kile. Mkuu yule wa jeshi alikataa kwa mara ya kwanza lakini alitishiwa sana, alikubali na kutuma ndege mbili ambazo zilienda kushusha mabomu kadhaa kwenye kijiji cha Pohang.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UKURASA WA 56 SEHEMU YA 10
UKURASA WA 56 SEHEMU YA 10
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/12/ukurasa-wa-56-sehemu-ya-10.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/12/ukurasa-wa-56-sehemu-ya-10.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content