UKURASA WA 56 SEHEMU YA 05 | BongoLife

UKURASA WA 56 SEHEMU YA 05

UKURASA WA HAMSINI NA SITA 
SEHEMU YA 5
Gari alilokuwa anaendesha Masai, lilifika kwenye barabara moja iliyokuwa juu sana. Masai akapaki gari lake pembeni, na kisha akachukua darubini na kuanza kutazama kwenye fukwe fulani zilizopo kwenye nchi ile. Ilikuwa tayari imetimu saa kumi na mbili ya jioni. 

Akiwa anatizama kwa darubini yake, aliweza kuona jumba kubwa la kifahari likiwa na walinzi kadhaa wakiambaa huku na huko katika kuboresha ulinzi wao.

"Naona kaongeza ulinzi." Man'Sai akaongea peke yake huku akifungua mlango na kutupia darubini yake kwenye nafasi ya abiria kwenye gari. "Ngoja usiku uingie." Akaingia ndani ya gari na kuanza kwenda juu zaidi ya barabara ile ndefu. 

Mwendo ule wa gari lake uligota kwenye hoteli moja kubwa iliyokuwepo chini ya mlima mmoja ambao ulizungukwa na vivutio vingi vilivyowafanya watu wengi watembelee mahali hapo. Masai alishuka toka kwenye gari lake la gharama na funguo akampa mpokea wageni wa hoteli ile. Naye akaingia ndani ya gari na kuliwasha lakini halikuwaka. Masai aligundua hilo na akarudi kisha akaamuru gari lile liwake bila hata ya kutumia funguo. 

Mhudumu alilipeleka gari lile kwenye kituo cha mafuta kimilikiwacho na hoteli ile. Na mhudumu aliweka mafuta lita kadhaa ikiwa kama huduma ambayo inapatikana katika hoteli ile kama ukipanga. Baada ya kujaza mafuta kwenye gari la Kijana wa Kitanzania, mhudumu alilipeleka gari lile kwenye sehemu maalum ya kuweka magari. Akachukua kibao fulani na kukiweka nyuma ya gari lile. Kibao kiliandikwa namba hamsini na sita. 

Alipomaliza zoezi hilo, akaenda moja kwa moja mapokezi na kumkuta Masai akiongea na mwanadada wa Kikorea. Akamkabidhi funguo ya gari lake na baada ya hapo, akamwambia mhudumu namba ambayo gari la Masai lilikuwepo. 

"Namba hamsini na sita ndipo gari lako lilipo."Mwanadada wa Kikorea aliongea kwa Kikorea na Masai akatabasamu kidogo kisha akachukua kibao cha kisasa kilichoandikwa namba ya sehemu ya gari lake lilipo. Tayari alikuwa na funguo ya gari, funguo ya chumba alichochukua na kibao cha 'parking'

"Ahsante mrembo."Masai akatoka pale na kwenda mlango wa pembeni ambao ulikuwa ni wa lifti. Akabonyeza kibonyezeo cha lifti kisha akasubiri lifti ile ishuke. 

"Parking namba hamsini na sita na ukurasa wa hamsini na sita. Vinazama kwenye ubongo wangu na kuleta picha ya kutisha." Masai alijiwazia peke yake na wakati huo lifti ilifunguka na yeye akaingia. Kisha akabonyeza kitufe cha kupandisha lifti, nayo lifti ikakubali kupanda hadi ghorofa ya tatu. 
****
Aliingia chumbani na moja kwa moja alikwenda hadi kwenye kabati na kulifungua. Alikuta suti kadhaa za maana ambazo huandaliwa na hoteli ile kama mteja atahitaji. Akatabasamu na kisha akaenda bafuni ambapo alifungulia maji yaliyoanza kujaza beseni kubwa la marumaru lililopo mule bafuni. Kelele za maji zikampa nafasi ya yeye kwenda hadi chumbani na kisha akavuta mkoba uliokuwa kwenye kabati lile la nguo. 

Mkoba (brief case) ule ulikwishaandaliwa na watu waliomtuma na chumba tayari kiliandaliwa. Hivyo hakuwa na shaka kuhusu huo mkoba na hata usalama kwa sababu hata kamera za chumbani kwake, zilikuwa zimezimwa. 

Masai akafungua na alikutana na bastola mbili aina ya D-Eagle mpya za rangi ya siliva. Akazikoki nazo zikatoa sauti iliyomezwa na maji yaliyoendelea kumiminika kwenye beseni la marumaru huko bafuni. 

Baada ya kuridhika, akafunga mkoba huku bastola zake akizisukumia chini ya mto. Akarudisha ule mkoba na kisha akaenda bafuni kujiswafi. 
****
Saa mbili aliamka toka kwenye usingizi mfupi uliyomchukua baada ya kutoka kuoga. Akaitazama saa yake iliyokuwa inatoa mlio na kisha akaizima. Akaenda kwenye kabati na kuchukua suti moja nyeusi kati ya nne zilizopo. Akajipara vema kabla ya kuvaa ile suti. Na baada ya kuvaa, akachukua bastola zake na kuzipachika kwa nyuma. 

Akatoka ndani ya chumba kile akiwa na funguo ambayo ni kadi ya kierektronia, pamoja na kibao cha sehemu ya kuweka magari na funguo ya gari. 

Akashuka hadi mapokezi na kuacha funguo, kisha akaenda hadi kwenye sehemu ya kuhifadhi magari. Yalikuwa mengi sana, na kwa kurahisisha kazi, alibonyeza kibao kile alichopewa, na kile kibao kilichowekwa nyuma ya gari lake, kikatoa mwanga mkali ambao unaweza kudumu kwa dakika mbili. Masai akaenda hadi pale kwenye kibao na kukisogeza pembeni. Akazama ndani ya gari lake na kuliwasha, na kisha akaelekea ambapo alipaswa kwenda. 
****
Kijana wa Kitanzania, alifika karibu na kwenye jumba kubwa la kifahari ambalo alielekezwa ndipo anaishi Waziri wa Ulinzi Mstaafu. Lakini usiku huo hakuwepo ila familia yake ilikuwepo. 

Masai akashuka toka kwenye gari lake na kuchukua darubini na kuanza kuangaza taratibu kwa kutumia darubini hiyo yenye uwezo mkubwa wa kuona hata gizani. Kila akichokiona, alikinakiri kwenye kitabu kidogo cha kumbukumbu na zaidi alikuwa anawahesabu walinzi ambao walikuwa wanafanya doria. 

Kuna vitu hakuwa na uhakika navyo, ikamlazimu kusogea toka pale alipo ili apate uhakika. Alifanikiwa kung'amua mambo mengi na hiyo ikamsaidia kurahisisha kazi aliyoagizwa. 

Baada ya kuridhika na alichokuwa anakitafuta, alirudi haraka alipoliacha gari lake ambapo ni kama kilimota moja toka pale kwenye nyumba ya Waziri Mstaafu. Akafungua boneti ya gari lile na kutoa begi moja kubwa na kulifungua zipu yake.

Kulikuwa kuna silaha kadhaa na yeye alichukua baadhi ya silaha hizo na kuanza kurudi kule ilipokuwa nyumba ya mtuhumiwa anaye mtafuta. Akiwa umbali wa mita mia moja kabla hajafika kwenye nyumba ile, alichomoa upinde wa kisasa wenye kamba za nyaya nne na podo yenye mishale mingi. Akachukua mawani ya kisasa ambayo iliweza kuona watu wa gizani na kuivaa, na baada ya hapo, akachukua mshale mmoja toka kwenye podo, na kuupachika kwenye upinde wake. 

Akavuta na kumlenga mlinzi mmoja ambaye alikuwa kasimama juu ya nyumba ile. Alipoachia, mshale ule ulienda kutua kwenye paji la uso na yule mlinzi alidondoka bila kelele na kubaki hukohuko juu kwa sababu paa la nyumba ile, ilitengenezwa kwa mfano wa paa la ghorofa.

Baada ya kumdondosha mlinzi yule kwa shabaha mwanana toka kwenye mshale wake. Akaangaza upande mwingine wa nyumba ile, napo kulikuwa na mlinzi ambaye alikuwa anaenda huku na huko katika kuhakikisha usalama upo eneo lile.

“Wa pili huyu. Katika idadi yangu ya waliopo juu. Hivyo bado wawili huku juu. Ila ngoja kwanza nimpe yule pale.” Masai aliongea huku akivuta kamba ya upinde wake na kumlenga mlinzi mwingine ambaye yeye alikuwa kwenye kibanda kidogo kilichokuwa karibu na geti. Mlinzi yule alipokea mshale wa kifua ambao ulimrusha vibaya na kwenda kugota naye ukutani.

Alipotazama juu, tayari mlinzi ambaye alikuwa kaenda mbali na upeo wa macho yake, alikuwa karudi karibu ambapo mwanga ulikuwa unammulika vema. Akavuta tena upinde uleule na kuuachia na hapo haikusikika sauti yoyote zaidi ya kishindo kidogo kilichotokana na mshale ule kuingia kwenye mdomo wa mlinzi yule.

Na hata baada ya kuangaza kwa mlinzi wa mwisho, napo alikutana na jambo lilelile ambalo alilihitaji. Mlinzi yule naye alipokea kile alichostahili.

“Hawa nadhani nimemalizana nao. Sasa bado hao wa chini.” Masai aliongea huku anashusha upinde wake na kuanza kufungua begi lake tayari kwa kuurudisha. Aliuweka vema bila kuufungua, na kisha akatoa visu viwili vikubwa na vingine vingi vidogo vilivyokuwa vimechomekwa kwenye mkanda maalumu kwa ajili yake.
Masai akatizama huku na huko kabla hajachukua maamuzi magumu ya kuingia ndani ya jengo lile kubwa. Akiwa tayari kwa ajili ya kuingia ndani, ndipo alikutana na kitu ambacho hakuwaza kama kitakuwepo eneo lile. 

“Shit.” Akatukana tusi dogo na kisha akarudi nyuma kidogo palipokuwa na giza zaidi. Nje ya geti kulikuwa na mlinzi mmoja kakaa kwenye jiwe. Wakati Masai anajiandaa kwenda kuingia ndani, mlinzi yule aliwasha kiberiti na kuchoma sigara yake. Bahati ilikuwa kwake kwa sababu mlinzi yule hakumuona na bado alikuwa mbali. 

“Sigara ni hatari kwa afya yako na pia kwa uhai wako.” Aliongea maneno hayo huku akichomoa tena upinde na mshale wake toka kwenye begi na kumlenga yule bwana ambaye alikuwa anaendelea kuburudika na moshi wa sigara. Kifo kilimchukua kirahisi sana, yaani bila shida wala kelele. Mshale wa mdomoni, ulitosha kabisa kusimamisha uhai wake.

Baada ya tukio hilo, Masai akarudisha tena mshale na upinde wake, kisha kwa umakini zaidi, akaanza kuelekea kwenye geti kubwa la nyumba ile ambapo juu ya uzio wake kulikuwa na nyaya za umeme na juu ya pembe mbili za getini, kulikuwa na kamera mbili ambazo kabla ya Masai kufanya lolote alihakikisha zinazimwa na ndipo aanze kazi iliyompleka.

Alifika kwenye lile geti na kumtazama yule mlinzi aliyemtungua kwa mshale wa mdomoni, akamsogeza pembeni na kisha kuchukua simu yake ya upepo na kuifungua haraka. Na baada ya zoezi la kuifungua yote kukamilika, akachomoa kitu fulani kwenye mkoba wake aliokuja nao, na kitu hicho akakiunga vema kwenye nyaya za kidaka sauti. Na alipohakikisha kuwa zoezi hilo lipo vema, akaifunga simu ile ya upepo au ‘radio call’ kwa lugha ya Kiingereza, na kuiweka chini ya pembe moja ya geti lile.

Akaliangalia geti lile vema hasa nyaya za umeme ambazo zilikuwa zinatokwa na cheche kila baada ya sekunde mbili kuonesha kuwa kulikuwa na umeme unatumika kwa wakati ule. Macho yake yakaanza kufuatilia taratibu zile nyaya na mwishowe yaligota kwenye kiunganishi kimoja ambacho kilikuwa na rangi nyekundu na nyeupe.

Hapo tena, Masai akachomoa kitu kingine toka kwenye begi lake. Kilikuwa mfano wa bastola moja ya plastiki, na alifunga kitu mbele yake na kulenga pale kwenye kiunganishi cha zile nyaya. Alipoachia, kile kitu alichokifunga mbele ya bastola ile ya plastiki, kilienda na kunasa kwenye kiunganishi cha waya ule. Masai akatabasamu tabasamu la ushindi na kisha alivua mawani yake ambayo ilikuwa inamsaidia kwa asilimia kubwa kuona vitu alivyotaka hasa vile vya gizani kasoro yule mlinzi mvuta sigara.

Alipotoa mawani ile, akavaa mawani nyingine ambayo hii allipoibonyeza kwa pembeni, ilibadilika na kuwa ya kijani. Na alipoibonyeza tena upande mwingine, ilitoa muale mkali mwingine wa mwanga wa kijani lakini safari hii aliweza kuona kuwa nyaya zile hazina tena umeme baada ya kile kidude kwenda kuuzima kwenye kile kiunganishi. Alipotizama getini, hakuweza kuona na hapo aligundua kuwa mawani ile haina uwezo wa kupenya kwenye vitu vya chuma.

Akaweka tena begi lake chini na kupekua na alipoibuka alikuwa kakamata viatu ambavyo alivua vile alivyokuja navyo na kuvaa vile ambavyo vilikuwa ni vidogo na vyepesi hata kwa kuvitizama.
Alipomaliza kuvivaa, akachukua baadhi ya silaha nyingine na kuzivaa mwilini mwake. Taratibu alirudi nyuma umbali wa mita kumi na kisha kwa kasi akaanza kukimbilia getini, kabla hajafika getini, akabonyeza rimoti ndogo mkononi kwake na viatu vyake vikamrusha juu na wakati yupo juu, alirusha visu viwili vidogo ambavyo vilikata nyaya zile za umeme na bila wasiwasi zikakatika bila ya kuleta hata shoti. Mwili wake ukaingia ndani na kabla hajatua chini, macho yake yalishuhudia walinzi wawili ambao walikuwa wanafanya doria mule ndani. Kwa kasi, Masai akachomoa visu vingine vidogo na kuvirusha ambapo viliwakuta wale walinzi, na wao bila hiyana wakapoteza muelekeo wa maisha baada ya visu vile kutua shingoni.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,156,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,13,biashara mtandaoni,3,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,118,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,229,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UKURASA WA 56 SEHEMU YA 05
UKURASA WA 56 SEHEMU YA 05
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/12/ukurasa-wa-56-sehemu-ya-05.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/12/ukurasa-wa-56-sehemu-ya-05.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content