STORI YANGU; HATA AKILA MKE WANGU ATAKULA NA WANANGU!

STORI YANGU; HATA AKILA MKE WANGU ATAKULA NA WANANGU!

Wakati naoa nilikua sina kitu kabisa, ndiyo nilikua nimemaliza chuo na nina ajira lakini mshahaara ulikua mdogo sana, nilioa kwakua umri umeenda na niliona nitachelewa. Mke wangu alikua na vibiahsara vidogo vidogo lakini tulisaidiana, ni kama ndoa iliniletea baraka kwani baada ya miezi mwaka mmoja tu niliitwa kazini kwenye usahili ambao niliufanya miezi sita kabla, nilishakata tamaa ya kupata kazi.

Ni taasisi ya kimataifa, mshahara wa kuanzia ulikua milioni tano, nilikua kama kichaa, yaani kutoka mshahara wa laki mbili mpaka milioni tano sikuamini. Nilianza kujenga nyumba yangu, nikawajengea na wazazi wangu na miaka mitatu baadaye nilikua mtu mwingine kabisa, lakini sikua na amani katika ndoa yangu, ndugu zangu walikua hawapatani na mke wangu, rafiki zangu walimuona mke wangu mbaya.

Yaani kila siku ilikua kugombana, kwa maneno niliyokua nikisikia hata mimi nilijikuta namchukia mke wangu nilimuona kama sheteni na niliendelea kubaki naye kwasababu ya watoto tu. Nilikua karibu na ndugu zangu nikiwasaidia kwa kila kitu, mke nilimtenga hata pesa ya matumizi nikawa namuambia amuombe Mama yangu ambaye nilikua nikiishi naye, ndugu zangu wengine walikua wakimtukana na kuniambia nimuache kila siku lakini sikutaka wanangu wawili kulelewa na Mama wa kambo.

Siku moja nilikua nipo tu nyumbani, nikawa naingia kwenye mitandao, and nilikua napitiapitia kuna rafiki yangu mmoja ambaye mara nyingi namuambia matatizo yangu alinitag katika moja ya post yako. Ilikua ni Post ya jama aambaye alikutana na watoto wa marehemu rafiki yake, alipokuja kufuatilia alijua kuwa kumbe ndugu wa rafiki yake walimnyang’anya kila kitu mke wake, wakawatelekeza na watoto mpaka sasa wamekua ombaomba wanauza vitu barabarani.

Ilinichoma sana lakini kwa namna nilivyokua naishi na ndugu zangu niliamini kuwa hawawezi kunifanyia chochote. Pamoja an kupuuzia lakini sikua na amani kabisa, nilikumbuka kipindi nipo kwenye misha magumu msharaha mdogo hakuna mtu hata mmoja ambaye alimsema mke wangu, wote walimuona mwema na hakuna aliyejali kuhudu ndoa. Sijui nilipata wapi wazo lakini nilienda ofisini na kuomba likizo kazini.

Kwa bahati nzuri nilipata, sikumuambia mtu yeyote, lakini niliporudi nyumbani nilimuambia mke wangu kuwa kuna matatizo kazini na nimesimamishwa kazi. Niliwaambia ndugu zangu na kuwajulisha kuwa tunatakiwa kuondoka katika ile nyumba ya shirika. Siku iliyofata niliita gari na kuondoa vitu vidogo vidogo kwani fenicha na kila kitu vilikua vya ofisi. Ndugu zangu walishangaa lakini walinipa moyo, niliondoka mpaka kwa mdogo wangu wakiume ili kukaa kwa muda wakati nikijipanga.

Ulikua mwezi mmoja tu ambao sikua na pesa lakini ulikua ni mwezi amabo nilijua kuwa ndugu wengi na marafiki ni wakati unachotu na si kipindi huna. Kwanza maneno yalianza kuzunguka kuwa nimefilisika naishi kwa ndugu yake, pili shemeji yangu mke wa mdogo wangu alikua akinidharau, yaani mtu aliyekua akiniheshimu na kuninyanyekea kama mfalume ghalfa aliniona ndezi. Nikimuambia mdogo wangu niliona kabisa ananijibu kishingo upande kama ananiambia acha kuingilia ndoa yangu.

Baada ya kama mwezi hivi mdogo wangu aliniambia siwezi kuendelea kuishi kwake na familia yangu kwani mke wake hapendi wanagombana na mke wangu. Mimi nilinyamaza, nilitaka kwenda kwa Dada yangu ambaye naye alikua ni kinara wa kuniambia niachane na mke wangu lakini alisingizia kuwa nyumba ndogo, mara mke wake hataki. Mwisho walikaa kikao na kuamua kunipa kodi ya nyumba ili nikajitegemee, hakuna aliyetaka kuishi na mimi.

Niliongea nao kuhusu ada za wanangu (nilizaa kabla ya ndoa) wakaniambia hawana pesa niwahamishe kwenye shule za kawaida. wakati huo wote mke wangu aliendelea kuniheshimu kama mume wake, pamoja na kuwa hakua na Biashara ya maana lakini kila siku alikua akinipa Shilingi elfu tano, hata kama alikua hana kabisa ndiyo pesa ya nauli kwenda kwenye Biashara zake, alikua ananipa baadaye ananiomba buku.

Nilimuuliza kwanini anafanya hivyo akaniambia kuwa “Wewe ni mwanaume ulishazoea kutoa, ukiwa wakupewa hivi kila siku utachanganyikiwa, ni lazima angalau uwe na mtu ambaye anaweza kukuomba pesa.” Bila kuniambia mke wangu alienda na kukopa pesa milioni moja kwa Baba yake, alinipa na kuniambia tuongezee mtaji kwenye Biashara yake ili tufanye wote, alikopa laki tano kwa Kaka yake na kuja kunipa nikatafute nyumba tuhame kwani aliona kama nanyanyasika sana.

Wakati huo nilishamaliza likizo yangu, nilikusanya vitu vyangu na kurudi nyumbani kwangu. Mke wangu alishangaa, sikumuambia nilichokua nimekifanya bali nilimuambia kuwa kazini wamefanya uchunguzi na mimi sihusiki na chochote. Ndugu zangu walionekana kufurahia, walijifanya sasa kujali, walijifanya kunisifia na kusema kuwa walijua tu kuwa nitarudi, marafiki walionitenga walianza kunipigia simu tena.

Sikumuambia mtu chochote lakini nilijua kuwa, kama nikiwa hai wanaweza kunigeuka namna hii tena ndani ya mwezi mmoja vipi nikifa na kuacha wanangu. Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kuamua kuandika kisa changu, najua kuna baadhi ya ndugu watasoma na kunijua, ila wajue ni kwanini sasa hivi nimebadilika nawekeza na mke wangu. Ndiyo huwezi kumuamini kila mtu, wanasema usimuamini mwanamke lakini angalau hata mke wangu akinidhulumu atakula na wanangu kwani ndugu zangu nao watakula na watoto wao.

TUJIFUNZE KUPITIA HUU UJUMBE.
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Maoni

Chapisha Maoni