Featured Post

MISEMO YA WATU WENYE WIVU (MANENO YA WAKOSAJI)

1. Siwezi kununua gari kwa mkopo.
2. Huyo bwana wake mkubwa kuliko yeye, alitafuta pesa tu.
3. iPhone kitu gani, simu simu tu Tecno inanitosha bora mawasiliano.
4. Siwezi kula chakula cha kwenye friji, kwanza hata microwave zinaleta kansa. 5. Amejifanya amesoma lakini hamna kitu hata haolewi.
6. Siwezi kuendesha Vits bora nitembee kwa miguu tu. 
7. Kuoa/kuolewa ni stress tu bora nikae single.
8. Anajiona mrembo wa maana, siku hizi kuna warembo basi wote makapi tu, washatumiwa vya kutosha, wamechokeana balaa.
9. Anaendesha V8 halafu anaishi uswazi.
10. Hiyo nguo anadai kanunua laki 3 Dubai wakati Kariakoo ni elfu thelathini tu.
11. Hilo gari na kazi amepata baada ya kulala na boss wake.
12. Hata kama ana degree, maisha yake sawa tu na yetu.
13. Kwani Mercedes ina miguu mitano, gari gari tu bora usafiri, spacio inanitosha tena inamudika, kikubwa muombe Mungu ufike salama mengine mbwembwe tu.
14. Siwezi nunua gari kabla sijajenga, unataka ninunue gari leo nipaki kwenye nyumba ya nani?.
15. Anakwenda gym kila siku ila ana umbo baya kinoma.
16. Anajifanya kuongea kizungu wakati kwao shamba tu.
17. Anaringaaa lakini ataachwa tu, subiri tuone macho yetu, kikubwa tuombe uzima.
18. Wanajiona wakishua wakati baba yake freemason na hela ya kujenga nyumba na kununua gari walimtoa kafara mtoto wa mwisho.
19. Ana umbo zuri lakini hajui kuvaa, kwanza huwa anaazima nguo na vipodozi.
20. Hakuna jipya kwenye ndoa.
21.Usione amenenepa hivyo anatumia ARV.
22. Eti ana simu kali wakati alichota mapesa ya kampuni, mwizi mkubwa yule si wa kuzoea.
23. Muziki ulikuwa zamani siku hizi hamna kitu.
24. Mpira ulikuwa zamani siku hizi kuuza sura tu.
25. Siasa ilikuwa zamani siku hizi michosho tu.
26. Elimu tulisoma sisi ila kizazi hiki hamna lolote ni kupoteza tu pesa.
ONGEZA NILIZOSAHAU TWENDE SAWA ILI TUJIKOMOE WENYE WIVU.😀
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni