💞MANENO YA MKE NA MUME YANAVYOTAKIWA KUWA

*💞MANENO YA MKE NA MUME YALIKUA HIVI:-💞*

              🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹🌹

MUME: Mke wangu haujambo?

MKE: Sijambo mume wangu

MUME: mke wangu nimekumiss sana, upo hapo nyumbani muda huu?

MKE: mmmmh ndio nipo nyumbani, vipi mbona leo kuulizana hivyo?

MUME: mke wangu nimekukumbuka sana leo natamani nikwambie kitu

MKE: Leo na malaika watapiga makofi, maana sio kawaida yako kabisa haya nakusikiliza mume wangu

MUME: Mke wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.

MKE: Mmmmh unasema kweli?

MUME: Mke wangu kwa mara ya kwanza nilipokuona niliogopa kukuambia, hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa katika maisha yangu.

MKE: mbona haujawahi kusema jamani mume wangu?

MUME: Nakupenda mke wangu nafasi uliyotawala moyoni mwangu ni kubwa, hakuna ambaye anaweza kufikia uhodari wako, wewe ni mtu muhimu sana maishani mwangu.

MKE: Jamani mume wangu uko wapi sahizi? Navutiwa na maneno yako jamani

MUME: Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata tukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.

MKE: Nakupenda sana mume wangu tafadhali usiniache kweli, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu, njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.

MUME: Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi, ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda mpaka mwisho wa uhai wangu.

MKE: Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi inapopatikana si busara kuichezea tudumishe penzi letu laazizi wangu.

MUME: Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na maumivu yake ndani yangu.

MKE: Mume wangu ishia hapo hapo utaniua, uje umalizie ukishafika nyumbani nakuombaa.

MUME: Viungo vyote vya mwili wangu vinakuhitaji, inawezekana kwasababu nimeumbwa kwa ajili yako.

MKE: Jamani leo mume wangu umeniamulia, kumbe unanipenda hivyo!!

MUME: Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee, lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.

MKE: Utakuwa wangu wa maisha daima na penzi letu litakuwa kama mfuko wa hazina, tutalitunza kama zaidi ya mboni ya jicho.

MUME: Mke wangu najua u-mbali nami, majaribu ni mengi wapaswa kujihami, nitunziye zangu zabibu wangu tabibu, jitahidi kuwa mvumilivu nitakuja niwe nawe, Miss u Ma LOVE.

MKE: Nimeamini wewe ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunitibu, Love U.

MUME: Mapenzi mazuri yanasifa zifuatazo, kuridhishana, kupeana bila kubaniana, kubusiana, kusaheshimiana, kujaliana, kusubiriana, kusikilizana.Je, utaweza kujifanyia yote hayo? Nijibu mpenzi...

MKE: Mume wangu usiende mbali nami, njoo ufaidi utamu usioisha hamu, nitakupa mwili wangu ucheze nao hadi asubuhi, nitakulisha unachokitaka, sitakubania kwani naogopa wengine wanaweza kukupa... njoo leo uniambie unataka nini?

MUME: Nipe niridhike, nionjeshe usinilambishe nikigonga unikaribishe na Penzi letu tuliharakishe MKE WANGU.

MKE: Upweke waniuwa mpenzi. Nakupenda sana mpenzi wangu, wewe ndiyo Baba watoto wangu.

MUME: Sina pesa nyingi lakini moyoni mwangu najua wewe ndiye langu la moyoni.

MKE: Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?

MUME: Namini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!

MKE: Mapenzi yako ni ya dhati kwangu naahidi kukupenda zaidi na zaidi.

MUME: Usiyumbe mimi ni wako wa Maisha.

MKE: Asante sana mume wangu, leo umenipa kitu kipya najiona ni mpya kwako, nakusuburi kwa hamu, najikuta kutamani nikufuate uliko, nilitamani kila siku unifanyie hivi ila hatimaye leo umefanya, hakika unathamani kuliko kipato chetu, nimekupenda hadi nukta ya unywele.
nakupenda mume wangu.

*🌹🌹🌹HUO NI MFANO WA JINSI MWANAMKE ANAVYOPENDA KUAMBIWA MANENO MATAMU.🌹🌹🌹*
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni