FAIDA YA KANGA KWA MUME

Kanga vazi la haiba, kanga ina nyingi huba 
Kanga chanzo cha mahaba, kwa yule mwenye huba 
Vip mwaiacha kanga, mapenzi kuyavuruga 
Jina zuri kwenye kanga, ni kinga ndani ya nyumba 

🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸

Kuna zile zenye shani,, katikati kuna jani 
Ukivaa maungoni ,bwana huwa taabani 
Likaapo kiunoni,, jina njoo mwandani 
Kama huna kitu ndani, kanga huleta faraja 
Kanga vazi la haiba, humtuliza hubby 

🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸

Kanga huwa zasemana ,mama humuita baba 
Kwa sauti ya mwanana, na macho kukonyezana
Bwana huwaza vyamana ,vyakula vilomwanana
Karibu wangu mahabuba uje unitibu kikubwa 
Hilo ni jina la kanga, zuri lenye haiba 

🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸

Tena kanga za chombeza,natena huwa zaliza 
-ukivaa huwa watizama, jina zuri la heshima 
Hususani kinamama, wavaa bila kutizama 
Kisimani wapitiza, natena unatembeza 
Nakutamani jirani, karibu kwangu chumban 
Sivizuri Mwapoteza kanga, jina tambueni 

🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸🌻🌸

KANGA VAZI LA HAIBA VAENI KWA MAHABA MKIWA NA WAUME ZENU SIYO MITAANI

🌸🌻
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni