UNAFAHAMU KUHUSU KIHARUSI / STROKE , NI UGONJWA WA AINA GANI? | BongoLife

UNAFAHAMU KUHUSU KIHARUSI / STROKE , NI UGONJWA WA AINA GANI?


UNAFAHAMU KUHUSU KIHARUSI / STROKE, NI UGONJWA WA AINA GANI?

Stroke Ni Nini?

 Stroke au kiharusi ni tatizo linalotokea ghafla kwenye ubongo ambapo mtiririko wa damu kwenye eneo fulani la ubongo husitishwa ghafla au kupungua sana hivyo kusababisha eneo hilo la ubongo kukosa damu na virutubisho muhimu na seli za eneo hilo kuanza kufa.

 Hili linaweza kutokea pale mishipa ya damu ya kuelekea kwenye eneo hilo ikiziba au mishipa ndani ya ubongo katika eneo hilo kupasuka. 

Seli za ubongo za eneo hilo zikianza kufa kwa kukosa damu, shughuli zote zinazoendeshwa na eneo hilo la ubongo husimama kwa mfano kumbukumbu au misuli. Kiharusi ni ugonjwa wa dharura hivyo tiba inatakiwa ipatikane mapema iwezekanavyo. Kimsingi kiharusi huweza kumpata mtu ye yote wakati wo wote.Kuna aina tatu za stroke; ischemic, hemorrhagic na TIA. 

Kundi la watu lililo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu ni lile la watu wenye miili mikubwa, umri zaidi ya miaka 55, wenye historia ya ugonjwa huu kwenye familia zao, ambao hawafanyi mazoezi , wanaokunywa sana pombe au kutumia madawa haramu.

Kiharusi Husababishwa Na Nini?  

Kila moja ya aina za stroke hapo juu inasababishwa na vitu tofauti.Ischemic strokes, ndiyo aina ya stroke inayowaathiri watu wengi zaidi, asilimia 85 ya wagonjwa wa stroke hupatwa na aina hii ya stroke.

Aina hii ya stroke husababishwa na kuziba kwa arteri (mishipa ya kusafirisha damu safi) zinazoelekea kwenye ubongo au kusinyaa kwa mishipa hiyo hivyo kusababisha hali inayoitwa ischemia (upungufu mkubwa wa mtiririko wa damu).Kuziba kwa mishipa ya damu hutokea baada ya damu kuganda ndani ya arteri zinazoeleka kwenye ubongo au katika maeneo ya mbali zaidi na kusukumwa kwenye mishipa yenye kipenyo kidogo ndani ya ubongo.

 Mishipa hii inaweza kuzibwa pia na mafuta yaliyoganda ndani ya arteri (plaque).Hemorrhagic strokes, husababishwa na arteri ndani ya ubongo kuvuja damu au kupasuka. Damu hii iliyovuja huleta mgandamizo kwenye seli za ubongo na kuziharibu.

 Kupasuka kwa mishipa ya damu husababishwa na hypertension, trauma au dawa zinazofanya mishipa hii ya damu kupungua unene wake.Transient ischemic attack (TIA), hii ni tofauti na aina hizo mbili za stroke hapo juu kwani hapa mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo huvurugwa kwa muda mfupi kwa sababu zile zile tulizozitaja hapo juu tulipozungumzia ischemic strokes.

 Stroke ya aina hii ni ishara ya kutokea strokes nyingine baadaye kama hatua zinazostahili hazitachukuliwa.

Dalili Za Kiharusi (Stroke) - Ugonjwa wa stroke humpata mtu ghafla na dalili hutokea kwa muda mfupi sana.

 Dalili kuu za ugonjwa huu ni: Kuchanganyikiwa, mtu akipata shida ya kuongea na kuelewa anacho ambiwa , Maumivu ya kichwa yanakwenda pamoja na kupoteza fahamu kwa vipindi na kutapika , Ganzi katika viungo vya uso, mkono na mguu na hasa vikiwa vya upande mmoja wa mwili Kupana shida ya kuona kwa jicho moja au yote , Kupata shida ya kutembea vikichanganyika na kizunguzungu na kukosa mpangilio wa matendo ya mwili .

Athari za kiharusi zinaweza kuwa ni za muda mrefu. Kulingana na muda uliopita kabla ya kuugundua na kuutibu ugonjwa huu, mtu anaweza kupata ulemavu wa muda mfupi au wa kudumu.

 Pamoja na madhara ya stroke kama yalivyoorodheshwa hapo juu, mgonjwa wa stroke anaweza pia kupata yafuatayo: Msongo wa mawazo , Maumivu kwenye mikono na miguu yanayoongozeka baada ya viungo hivyo kufanya kazi au kutokea mabadiliko ya hali ya hewa.

.Kupooza au udhaifu wa upande mmoja wa mwiliKupata shida katika kufanya matendo ya kuonyesha hisia za mwili Kushindwa kumudu matumizi ya kibofu cha mkojo au viungo vya njia ya haja kubwa.

 Tiba Za Stroke Na Namna Ya Kuzuia Stroke : Kwa vile aina kuu mbili za stroke, ischemic na hemorrhagic, kila moja ina chanzo kilicho tofauti, kila moja inahitaji tiba iliyo tafauti na ya aina nyingine. Ni shurti kujua kwa uhakika ni aina gani ya stroke iliyotambuliwa kwani tiba ya stroke ya aina moja inaweza kuwa na madhara kwa stroke ya aina nyingine.

 Tiba kwa Ischemic Stroke: Ischemic strokes hutokea pale mishipa ya damu inapoziba au kupungua kipenyo hivyo tiba ya tatizo hili ni kuhakikisha damu ya kutosha inaufikia ubongo. Tiba huanza kwa kotoa dawa za kuyeyusha damu au mafuta yaliyoganda na kuzuia hali hiyo isitokee tena.

 Aspirin yaweza kutumika au sindano ya tissue plasminogen activator (TPA).Tiba kwa Hemorrhagic stroke: Stroke ya aina hii hutokea pale damu inapovuja ndani ya ubongo hivyo tiba yake italenga katika kuzuia damu isiendelee kuvuja na kupunguza mgandamizo wa damu iliyovuja juu ya ubongo.

 Tiba huanza kwa kutoa dawa za kupunguza mgandamizo kwenye ubongo, kupunguza msukumo wa damu kwa ujumla na kuzuia kusinyaa kwa ghafla kwa mishipa ya damu. Upasuaji unaweza kutumika kurekebisha mishipa ya damu iliyopasuka .

Ili kujilinda na stroke au kuzuia stroke yafuatayo yanaweza kufanywa:

1- Kutotumia madawa haramuKula chakula chenye mboga na matunda kwa wingi na chenye cholesterol kidogo .

2 - Kufanya mazoezi kila wakati.

3 - Kuhakikisha unadhibiti blood pressure Kuhakikisha unadhibiti kiwango cha sukari mwilini .

4 - Kuwa una uzito unaofaa.

5 - Kunywa pombe kwa kadri au kuacha kabisa.

6 - Kuacha kuvuta sigara .

Katika mada nyingine tutazungumzia ugonjwa wa joints-

Arthritis na kuona aina mbalimbali za ugonjwa huo. Ugonjwa wa Gout ambayo ni namna moja ya Arthritis, tutauzungumzia kwenye ukurasa tofauti kutokana na kuwa watu wengi sana wanashambuliwa na ugonjwa huu, hivyo tukaona ni vyema kuupa uzito wa kipekee.

Tunaomba maoni yako kuhusu mada hii yetu ya leo, na usisite kuuliza maswali pale ambapo unaona hujaelewa..


COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UNAFAHAMU KUHUSU KIHARUSI / STROKE , NI UGONJWA WA AINA GANI?
UNAFAHAMU KUHUSU KIHARUSI / STROKE , NI UGONJWA WA AINA GANI?
https://lh3.googleusercontent.com/-6Pjb-rAZKyM/Xb_dXnsNNWI/AAAAAAAAC2k/w1wEehQYcI8DrK29WNqnJYwzJJhmakNZACLcBGAsYHQ/s1600/IMG-20191103-WA0004.jpg
https://lh3.googleusercontent.com/-6Pjb-rAZKyM/Xb_dXnsNNWI/AAAAAAAAC2k/w1wEehQYcI8DrK29WNqnJYwzJJhmakNZACLcBGAsYHQ/s72-c/IMG-20191103-WA0004.jpg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/11/unafahamu-kuhusu-kiharusi-stroke-ni.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/11/unafahamu-kuhusu-kiharusi-stroke-ni.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content