Featured Post

KWIKWI HUSABABISHWA NA NINI? |FAHAMU JINSI YA KUZUIA KWIKWI

Baada ya kusoma makala inayohusu kijana mmoja aliyesumbuliwa na kwikwi kwa zaidi ya miaka miwili na nusu, na baadaye kutibiwa tatizo hilo kwa kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kutolewa tezi, nimeamua leo nizungumzie kwikwi.
Kwiki ni kitendo kisichozuilika ambacho hutokana na kusinyaa kwa kuta za kiwambo cha moyo au diaphragm. Kwa kawaida kwikwi ni kitendo kinachojirudia rudia mara nyingi. Sauti ya 'hic' inayotokea wakati unapokuwa na kwikwi husababishwa na kidaka tonge (epiglottis) 
ambacho hufunga haraka wakati hewa inapoingia kwenye koo. Kupiga kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara nyingine husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu. Kwikwi ya kawaida huweza kutulizwa kwa kunywa maji, lakini wakati mwingine kufanya hivyo hakusaidii.

 *Zifutazo ni sababu zinazoweza kukuletea kwikwi* 
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa, vitu ambavyo vinakiletea karaha kiwambo cha moyo au diaphragm husababisha kwikwi. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha jambo hilo na hizo tulizotaja hapo juu ni miongoni mwazo,ambapo matokeo yake ni humfanya mtu 

apige kwikwi. Kwikwi kwa kawaida huisha baada ya dakika chache au hata sekunde. Lakini iwapo kwikwi itaendelea kwa masaa au kwa siku, huweza kuwa ni tatizo muhimu la kitiba na pengine hali kama hiyo inaweza ikawa inasababiswa na ugonjwa.
Kuna baadhi ya watu hupata kwikwi sana wakati wa ujauzito, baada ya kufanyiwa operesheni na hata watoto wachanga pia hupatwa na kwikwi mara kwa mara. Wajawazito hupata kwikwi sana mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na mwanzoni mwa miezi mitatu ya pili. Kwikwi hutokea wakati wa ujauzito ni kwa sababu wakati huo uwezo wa 

kuvuta hewa ndani ya mapafu na kutoa nje huongezeka kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na hali ya kawaida. Hakuna sababu inayojulikana inayosababisha kwikwi kwa watoto wachanga, na wazazi wanashauriwa wasitiwe hofu na suala hilo. Hii ni katika hali ambayo kwikwi baada ya upasuaji husababishwa na nusu kaputi au anesthesia.

 *JINSI YA KUZUIA KWIKWI
Mara nyingi kwekwi huisha yenyewe ndani ya dakika sita,kwa kwikwi ya muda mrefu kutibu tatizo linalopelekea hiyo kwikwi ndio matibabu yanayoweza kuiondoa kwikwi, pia dawa zifuatazo hutumika kuondoa kwikwi ya muda mrefu...


Chlorpromazine
Metoclopramide
Baclofen
Njia nyingine za kumaliza kwikwi nyumbani ni kama zifuatazo
Kupumilia ndani ya mfuko wa plastic(funika mdomo na pua kwenye mfuko wa plastic huku ukipumua kwa dakika 1)
 kusukutua na maji ya baridi sana(ice water)
 Kuzuia kupumua(hold your breath) kwa muda wa sekunde 3 kama inavoonekana kwenye picha hapo chini
Na kunywa maji ya baridi kidogo kidogo
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni