KWA NINI BAADHI YA WANAWAKE HULIA WAKATI WA TENDO LA NDOA?

Inaelezwa kuwa hatua ya baadhi ya wanawake wakati wa tendo la ndoa ni kama kutua mzigo wa moyo na kisaikolojia. Kupitia kilio hicho, mwanamke huonesha furaha yake ya kuwa karibu na mumewe na kuonesha kuwa hana tatizo la kuelezea kuridhia kwake na kufika kileleni. Baadhi ya nyakati mwanamke huyaelezea yote hayo kupitia kilio.

Lakini kwa upande mwingine, mwanamke anaweza akalia kwa sababu ya kutofurahia tendo la ndoa, jambo linaloonesha kuwa hakuna utamu kwenye tendo husika na kuonesha kuwa wanandoa husika hawana mrandano.

Hivyo, mchanganyiko wa hisia za furaha na kufika kileleni au kutofurahia tendo kama atakavyo, humfanya alie.

Hivyo unapokutana na hali hiyo ya mwanamke, usimkasirikie, usimkimbie na kumgeuzia mgongo kwa kuamini kwamba hajakufurahia au hakupendi. Bali unatakiwa kujua kwamba katika hali ya kwanza mwanamke anafurahia tendo la ndoa pamoja nawe na anakujali, lakini katika hali ya pili unatakiwa umsaidie aweze kufurahia tendo na kuboresha ukaribu wa kimwili na kisaikolojia kati yenu ili kufikishana kileleni kama inavyotakiwa.

Nakutakieni usiku mwema
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni