HOT BBQ CHICKEN WINGS ZA UKWAJU


HOT BBQ CHICKEN WINGS ZA UKWAJU

By Mapishi Yetu

MAHITAJI YA KUPIKA HOT BBQ CHICKEN WINGS ZA UKWAJU

Rojo la ukwaju zito 5 tblsp (tablespoon) waweza ongeza ukipenda.
Tomato ketchup 4 tblsp 
Dark brown sugar 3 tsp (teaspoon)
Soy sauce 3 tblsp 
Kitunguu saum 1 tsp 
Tangawizi mbichi 1 tsp
Pilipili kavu au ya unga 1tsp
Chumvi kiasi
Unga wa ngano nusu kikombe
Chiken wings 1 kg
Mafuta ya kukaangia 

MATAYARISHO YA KUPIKA HOT BBQ CHICKEN WINGS ZA UKWAJU

Changanya chicken wings na unga wa ngano mpaka zichanganyike vizuri. Weka mafuta juu ya jiko zikaange kwa moto wa katikati mpaka ziive na ziwe golden colour. Ziweke pembeni zijichuje mafuta.
.
Kwenye dish changanya ingredients zote zilobakia halafu weka kwenye jiko pika kwa dakika kama tatu au mpaka ichemke kidogo halafu weka chicken wings zako changanya vizuri mpaka kila moja imeingia bbq sauce. Tayari kwa kuliwa. Yaani ni tamu ajab unaweza kula kwa chips, mikate, wali au peke yake. Wafanyie wageni wako na utakuja kunipa ahsante baadae.
By @Salma Haroub
.
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni