SABABU 16 ZA MIMBA KUHARIBIKA AU KUTOKA


sababu za mimba kuharibika
1. Asilimia 50-70% ya mimba zote zinazoharibika zenyewe wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito hutokana na matatizo ya kiasili au vina saba (genetics or chromosome abnormalities) kama;

*Autosomal *trisomy (22.3%)
*Monosomy (8.6%)
*Triploidy (7.7%)
*Tetraploidy (2.6%)

2.Magonjwa yanayotokana na kinga ya mwili (Collagen Vascular Disease)-Magonjwa haya hutokana na mwili wa binadamu kutengeneza chembechembe za antigen ambazo hushambulia viungo vyake venyewe . Magonjwa haya ni Systemic Lupus Erythematosus (SLE) na Antiphospholipid Antibody Syndrome.

Magonjwa haya husababisha mimba kuharibika mara kwa mara chini ya umri wa miezi mitatu ya mwanzo.Hivyo ni muhimu mgonjwa anayepata tatizo la kuharibika mimba mara kwa mara kufanyiwa kipimo cha damu mapema ili kugundua uwepo wa magonjwa haya na kupewa tiba stahiki.

3. Kukosekana kwa uwiano wa vichocheo (Hormonal imbalance) kama cushing syndrome, ugonjwa wa tezi koo ( thyroid diseases,) Polycystic ovary syndrome na Luteal Phase Defect.
Luteal Phase Defect - Ni upungufu wa kichocheo aina ya progesterone ambacho ni muhimu sana katika ukuaji wa mimba.

Ugonjwa huu pia huweza kugundulika kwa kipimo cha damu au kipimo cha kuchukua chembechembe za kuta za kizazi na baadae kuzipeleka maabara kwa ajili ya kuzipima. Mgonjwa hutibiwa kwa kupewa vidonge (supplement) vya kuongeza kichocheo hiki pungufu aina ya progesterone.

4.Matatizo katika maumbile ya mfuko wa uzazi (Uterine malformations) kama;

Septate uterus
Unicornuate uterus
Bicornuate uterus
Intrauterine adhesions

5. Uvimbe katika mfuko wa kizazi (Fibroids)

6. Kulegea kwa shingo ya kizazi (Cervical incompetence)

8.Mama mwenye kinga ya mwili dhaifu (Immunity problems) inayoshindwa kulinda kiumbe kilichomo kwenye mfuko wa kizazi dhidi ya uvamizi unaoweza kuambatana na vimelea vya asili vya baba mtoto

9.Trauma - Madhara ya kimwili ambayo yanaweza kusababisha kuharibika kwa mimba mapema ni pamoja na kufanya kazi kwa muda mrefu kupitiliza, kufanya kazi ngumu, kupigwa kwa mjamzito kwenye tumbo. Kukosekana kwa utulivu wa kiakili pia ni mojawapo wa chanzo cha kuharibika kwa mimba kwa mfano, kupatwa na hofu, uoga, huzuni, msongo wa mawazo nk.

10.Sababu za kimazingira kama madhara yatokanayo na sumu ya arsenic, madini ya risasi, dawa za kuua wadudu mashambani (pesticides), formaldehyde nk.

11.Uvutaji sigara na unywaji pombe - Wajawazito wanaovuta sigara au kunywa pombe wapo kwenye hatari mara mbili ya kuharibikiwa kwa mimba wakilinganishwa na wajawazito wasiokunywa pombe au kuvuta sigara

12. Matumizi ya dawa kiholela kipindi cha ujauzito pasipo maelekezo ya daktari - Dawa za maumivu za jamii ya Non-steroidal anti-inflamatory drugs (NSAIDS), dawa aina ya retinol ambazo hutumiwa kutibu magonjwa ya ngozi kama chunusi na eczema na dawa zinazotumiwa kutibu ugonjwa wa baridi yabisi (rheumatoid arthritis).

Dawa hizi jamii ya NSAIDS husababisha kuharibika kwa mimba kwa kuyumbisha viwango vya vichocheo (hormones) mwilini. Mamlaka ya chakula na dawa ya Marekani (FDA) katika ripoti yake ya mwaka 2011 imesema matumizi ya dawa aina ya ibuprofen kipindi cha umri wa miezi mitatu ya ujauzito yanahusishwa na kuzaa mtoto mwenye matatizo ya moyo, kupungua kwa maji ya uzazi (oligohydromnios) na kusababisha mama mjamzito kupata uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu sana (prolonged labour) .

13. Uzito uliopitiliza (obesity) - Ni mojawapo wa chanzo cha kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito.

14. Utapia mlo (Malnutrition) - Utapia mlo kwa mama mjamzito uhusishwa moja kwa moja na kuharibika kwa mimba kwa sababu ya ukosefu wa virutubisho muhimu kwa kiumbe kilichomo ndani ya mfuko wa kizazi.

15. Unywaji wa kinywaji chenye caffeine zaidi ya 200mg kwa siku huchangia kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki cha ujauzito. Kikombe kimoja cha chai (mug of tea) kina ujazo wa 75mg ya caffeine.Vilevile kikombe kimoja cha chai (mug of tea) iwapo mnywaji anatumia instant coffee, kina ujazo wa 100mg ya caffeine. Caffeine pia hupatikana kwenye vinywaji baridi kama coca cola, pepsi, kwenye vinywaji vya kuongezeka nishati mwilini (energy drinks) na kwenye chokoleti.

16.Umri mkubwa-Wanawake wanaoshika mimba kwa mara ya kwanza wakiwa na umri mkubwa wapo kwenye hatari ya kupata tatizo hili la kuharibika kwa mimba.

Kwa wanawake walio na umri chini ya miaka 30- Mimba 1 kati ya 10 huharibika
Kwa wanawake walio na umri kati ya miaka 35 hadi 39- Mimba 2 kati ya 10 huharibika
Nusu ya mimba zote za wanawake mwenye umri wa miaka 45 na kuendelea huishia kuharibika.
Wanawake wanaoshika mimba mara ya kwanza wakiwa na umri mkubwa wa miaka 30 na kuendelea wapo kwenye hatari kubwa ya kupata mtoto mwenye matatizo ya kuzaliwa (congenital malformations) na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa mimba hiyo kuharibika.

 *Share kwa wengine pia ili wengine wajue ili waweze kujikinga na jambo hili*

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SABABU 16 ZA MIMBA KUHARIBIKA AU KUTOKA
SABABU 16 ZA MIMBA KUHARIBIKA AU KUTOKA
https://lh3.googleusercontent.com/-Fa32DaPsru8/XZbMF-Yx6XI/AAAAAAAAC0o/mYJ4_grt1BEUPmlsnoLpQwhwgkisW_yQwCLcBGAsYHQ/s1600/mimba%2Bkuharibika.jpeg
https://lh3.googleusercontent.com/-Fa32DaPsru8/XZbMF-Yx6XI/AAAAAAAAC0o/mYJ4_grt1BEUPmlsnoLpQwhwgkisW_yQwCLcBGAsYHQ/s72-c/mimba%2Bkuharibika.jpeg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/sababu-16-za-mimba-kuharibika-au-kutoka.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/sababu-16-za-mimba-kuharibika-au-kutoka.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content