PENZI LANGU LINAVUJA DAMU SEHEMU YA 1 | BongoLife

$hide=mobile

PENZI LANGU LINAVUJA DAMU SEHEMU YA 1

RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO
 
SIMU: 0718 97 56 59

SEHEMU YA 1

   Katika kipindi cha makuzi yangu, nilibahatika kukutana na wasichana wengi warembo. Wapo walionivutia na kufanikiwa kuwa nao karibu japo kiurafiki wa kawaida. Na wapo ambao hata salamu yao tu sikufanikiwa kuipata. 

   Wapo ambao niliishia kuwasifia kwenye mitandao ya kijamii. Wapo ambao nilifanikiwa kukutana nao baada ya kujuana kupitia mitandao hiyo. 
Wapo ambao nilifanikiwa kuanzisha nao mahusiano ya kimapenzi na mpaka tunaachana hatukuwahi kuonana.

   Kiufupi nawapenda sana wasichana wazuri. Sio lazima niwe nao kimapenzi, hata nikiwa karibu nao tu hua nafurahi.
   
   Mimi pia ni mfuasi mzuri wa picha. Napenda sana kuweka kumbukumbu. Toka nilipokua mdogo, nilikua naweka miambilli miatatu kisha akipita mpiga picha basi nalipia huduma hiyo kwa pesa yangu. 
 
   Katika albamu yangu ya picha. Kulikua na picha nyingi sana za watu mbalimbali hususani watoto wenzangu. Ila kilichokuja kunishtua baada ya kutilia maanani utazamaji wa picha hizo za utotoni, nilibaini kitu ambacho kinanifanya nifurahi kila nipitashapo macho yangu kwenye albamu hiyo. Ni vile nilivyokua napenda kukaa karibu na watoto wa kike toka kipindi ambacho sina ufahamu sawasawa.
 
   Yaani mapozi yangu yote lazima nitamshika mtoto wa kike mkono,bega au kiuno. Hata nisipomshika basi nitakua nimegusana nae kivyovyote vile.
 
   Hua nacheka nikikumbuka matukio hayo ya utotoni. Maana yananipa tafsiri kua nimekua mkubwa na tabia yangu niliyokua nayo toka utotoni. Tabia ya kupenda wasichana. Sema kwa sasa kidogo nimeongeza kipengele. NAPENDA WASICHANA WAREMBO.

   Mnamo mwaka 2010 ndio mwaka nilioanza kujitegemea huku nikisubiri matokeo yangu ya kidato cha nne. Miezi mitatu kilikua ni kipindi kirefu sana cha kusubiri mpaka matokeo yatoke. Hivyo kwa sisi tuliotoka shuleni ni kazi sana kukaa nyumbani bure bila kuingiza kitu chochote. Maana hata kile kiasi cha pesa kidogo tulichokua tunapewa na wazazi wetu wakati tunaenda shuleni kilikua kimekomea hapo.

   Ili kupambana na ukame wa pesa, ilinibidi nitafute kazi kama si kibarua cha kunishikiza wakati nasubiri matokeo yangu ya kidato cha nne.

   Sikua na hofu kubwa ya kufeli kutokana na jinsi nilivyojaza majibu yangu kwa kadri niwezavyo. Pia sikua na ubavu wa kusema kua nitafaula kwa daraja la kwanza.

   Niliamini kua nitafaulu daraja la pili kwa asilimia kubwa sana.
na hata ikitokea nimeanguka sana basi itakua daraja la tatu. Nalo pia si daraja ambalo nilikua nafikiria kupata kwa vile mtihani uliyvokuja kwenye njia zangu nilizosoma wakati wa mwishoni. Kizungu tunaita ‘Final Touch’.
 
   Ila kwa upande mwengine wa shilingi kwakua mtihani ni mtihani...niliweka imani tu moyoni ili kukabiliana na matokeo yoyote yatakayotoka.

   Katika mahangaiko yangu yangu ya kutafuta kibarua, nikafanikiwa kuonana na kijana mwenzangu. Japo yeye alinitangulia umri kwa miaka kadhaa. Ila kwa jinsi alivyojiweka, sikuweza kumpa shikamoo zaidi ya salamu zetu za vijana.

   Nakumbuka jina lake anaitwa Sebastian. Jina la utani alikua anajiita Mwarabu wa Misri. Hivyo alijibatiza jina na kujiita Al-Hadaad.

   Huyo kijana alinipatia ajira ya kumuandika bango lake baada ya kufungua ofisi ya kukodisha mikanda ya filamu. 

   Kwakua nina fani nyingi na uchoraji ni moja ya fani iliyonipa umaarufu sana mtaani kwetu, nilimtajia bei zangu mbalimbai hasa kulingana na huduma anayotaka na baada ya maafikiano nikaenda kununua rangi na brashi kisha nikaifanya kazi yake.

   Alivutiwa na kazi niliyoifanya na kunipa ujira wangu kama tulivyokubaliana hapo awali.
   “hivi unamjua kijana yeyote mjanja mjanja ambaye anaweza kutumia computer vizuri, Akawarushia watu nyimbo kwenye simu na kuchoma CD?..... Nataka nimuache hapa ofisini maana mie nipo bize na mambo mengine”
Kauli hiyo kwangu ilikua ni kama nyota ya Jaa. Maana sikuremba mwandiko, niliweza kumwambia kua hata mie naweza hiyo kazi na kipindi hicho nilikua tu nyumbani baada ya kumaliza masomo yangu ya kidato cha nne. 

   Basi bila hiyana bosi wangu huyo akanipatia ajira nyingine. Ajira ngeni ambayo sijawahi kuifanya hata siku moja kwenye maisha yangu. 

   Hiyo computer yenyewe nilikua naishia kuiona tu ila kiukweli sikuwahi kutumia. Hata kibonyezeo cha kuwashia tu nilikua sijui kinakaa wapi.
 
   Hivyo niliongopa kua mie ni mtaalamu wa kifaa hicho ilimradi tu nipate kazi. 
Eeh, maana hata kinyozi hujifunzia kwenye vichwa vya watu. Cha msingi ni usiri wake na kujiamini tu ndio kunamfanya afanye kazi nzuri na mteja kumlipa na kumsifia kwa kumpendezesha bila kujua kua hata huyo kinyozi moyo ulikua unamdunda wakati anaifanya kazi hiyo.
   Kwakua hata Al Hadaad mwenyewe alikua hajui lolote kuhusiana na Computer, niliwasiliana na kaka yangu wa mtaani. Anaitwa Julius Semindu.

   Huyu ni mmoja kati ya watu walionipa somo la kuijua Computer kwa siku moja tu.
 Kwanza aliniambia computer ina mambo mengi sana. Yahitaji miaka dahri kujifunza na sidhani kama utaweza kujua kila kitu. Maana kila siku yanaongezeka mambo mapya. Ila ni rahisi sana kuitumia pindi pindi utakapojua wewe kama wewe unahitaji kujua kitu gani. 

  Maneno yake yalinikaa kichwani na nikaweza kugundua kua mimi sihitaji kujua vitu vingi kwenye matumizi ya kifaa hicho. Ila nahitaji kujua jinsi ya kuwasha, kuzima, kuchoma CD na kurusha nyimbo kwenye simu.

   Kwa kutumia computer yake, alinielekeza vitu hivyo. Na alipofika ofisini kwangu na kuiona computer mpya ambayo bosi wangu ameninunulia, ilikua haina programu za kuweza kufanya kazi nilizoorodhesha kuhitaji kufundishwa. Haikua na nyimbo pia.

   Aliniwekea hizo program na kunieleza jinsi ya kuziweka. Pia alichukua kifaa chake alichonijulisha kwa jina la External Disc na kunijazia nyimbo chache zilizokua humo. 

   Kwa mara ya kwanza nikaona kumbe kutumia Computer ni rahisi, nilikua niogopea bure tu hapo awali. 

   Nikaanza kuitumia kwa kasi. Nakumbuka mara kadhaa niliamua kukesha ofisini na sirudi nyumbani kwa kucheza magemu ambayo hapo awali nilikua nalipia kwenye vituo vya PlayStation.

   Baada ya mwezi mmoja tu kupita, nikawa fundi. Nilikua naweza mpaka kubadilisha window. Bado nikawa najua matatizo ya Computer na kuna baadhi ya watu waliniita fundi Molito wengine Mr. Computer Solution kwakua niliweza kuwarekebishia Computer zao.

   Uchangamfu wangu ulinifanya nitengeneze marafiki wengi na kujipatia wateja wengi pia. Niliweza kumshinda hadi mpinzani wangu ambaye ndiye alikua anatamba kwa kukodisha CD eneo hilo. 

   Wateja wengi waliokua wanakuja ofisini kwangu walikua wananisifia na kuniambia kua mimi ni mpole na sina Dharau kama alivyo mpinzani wangu kwakua alitangulia eneo hilo lililokua na uhaba wa maktaba hizo za mikanda.

   Sikua mvivu wa kufuatilia CD ninapozikodisha na kuna baadhi ya wateja ambao kwao pesa sio tatizo. Kila CD mpya ikitoka nilikua nawapelekea wao kwanza nyumbani.

   Siku moja nikiwa ofisini. Mishale ya saa tatu asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa nikawa napanga CD zangu. 

   Maana nilikua naipenda kazi yangu vilivyo. Kuna wakati nilikua napata pesa mara nne ya kiwango cha pesa alichoniwekea bosi wangu kwa wiki. Hivyo hata kimuonekano nikaanza kupendeza. Usafi wangu kimavazi ukawa kivutio hadi kwa wasichana. Na wengine hawakusita kunisifia bila kuficha. 
   “Molito jamani.... Umetoka waaaoooh!”
   
   Nilitabasamu na kushukuru kila nigunduapo kua nilikua nastahili kusifiwa kwakua nilikua naenda na wakati. Wakati huo tulikua tunaita kuripuka pamba.

   Nikiwa katika kupangapanga vitu vyangu vizuri na kufuta vumbi, nilisikia sauti nzuri ikinisalimia. Ni sauti niliyohisihi imetokea puani. Niliunyanyua uso wangu na kumtazama msichana huyo aliyesalimia.
 Hamadi! 
   Nilikutana na sura ngeni ya Malaika imesimama mbele yangu. Msichana mzuri hasa ambaye kwenye kumbukumbu zangu sidhani kama nilishawahi kumuona hapo kabla. 

   Niliganda sekunde kadhaa nikimtazama. Mawazo yote yalikusanyika na kuwa kwake. 
Kweli hua napagawa nikiona wasichana wazuri pindi wafikapo ofisini kwangu, ila huyu alinipa mfadhaiko kabisa na kujikuta napatwa na kigugumizi cha kujibu salamu yake.
 
   Siku zote hua na sauti kubwa na hutoka kwa kujiamini na kuitia mbwembwe ili kuwavutia wasichana hao wapya kwenye macho yangu, lakini siku hiyo nilitoa sauti ndogo ambayo hata mie mwenyewe sikujisika vizuri nilikua naongea vitu gani.

   Ila kiufupi nilijibu salamu yake na kumruhusu aseme shida yake iliyomlea pale ofisini kwangu.
   “kaka, nimesoma kwenye bango lako hapo kua unatengeneza Computer.” 

   Nilishtushwa tena na sauti hiyo ambayo ilinitoa kwenye mawazo nisiyoyajua kutokana na kuduwaa na kunirudisha tena kwenye uhalisia wake. Sauti hiyo nyembamba ilikua kama ina kamtekenyo fulani hivi iliyonifanya nitabasamu kama kichaa aliyevuta marijuana.
   “eeh.. Natengeneza ndio.”

   Jibu langu lilimfanya aweke mkoba wake juu ya kabati langu la vioo nililoandika maneno ya kuwazuia watu kutoegemea kabati hilo.

   Alifungua zipu ya mkoba wake na kutoa laptop ndogo na kunikabidhi. 
Nilipokea laptop hiyo kabla hata sijaulizia ugonjwa unaousumbua kwenye laptop hiyo nikajaribu kuiwasha.

   “haiwaki, toka jana imezima tu yenyewe. Hapa nilipo nimechanganyikiwa sana kaka yangu.” sauti ya msichana huyo aliyeniambia amechanganyikiwa ilikua inanichanganya hata mie kwa kiasi kikubwa. Nyie acheni tu. 
   “itakua window imeharibika... Mara nyingi window zikifa husababisha tatizo kama lako. Wala usijali dada yangu. Mimi ndiye Master computer Solution .. Karibu sana.” nilitoa majibu uchwara bila kujua uhalisia wa tatizo lenyewe. Nikapata na ujasiri wa kujisifia angalau kumtoa wasiwasi mtoto mzuri. Maana chuma kama hicho kilichopo mbele yangu kuhuzunika wakati mwamba nipo namuangalia, haikupendeza moyoni mwangu.
   “itapona eeh?” 
aliuliza msichana huyo baada ya kutoa majibu kwa mgonjwa kabla sijampima na kumletea faraja kidogo. Nilipata ujasiri wa kumtazama usoni kwa mara nyingine.
 
   Hakika nilipomtazama kwa makini, niliweza kugundua jinsi gani alivyokua anaipenda Laptop yake.
“kwakua umeshaileta kwa daktari bingwa wa matatizo yote ya computer... , we ondoa shaka. Kuwa na amani dada yangu” niliongea hivyo na kuachia tabasamu pana lililompa matumaini mrembo wa watu.
   “Nitashukuru wewe, maana naitegemea hiyo kwa ajili ya masomo yangu.” binti huyo aliongea na kunifanya nitikise kichwa kuashiria kua hilo lilikua tatizo dogo tu kwangu.

   Uteke wa mwili na kifua chake kidogo kiliweza kunipa makadirio ya umri wa binti huyo. Alionyesha wazi alikua ana umri chini ya miaka kumi na nane. 
   “unasoma kidato cha ngapi?” 
niliuliza hilo swali huku nikiweka dawa kwenye sponji na kuanza kuifuta vumbi Laptop hiyo kama niliambiwa nifanye hivyo na mmiliki.
   “ndio tumetoka kufanya mitihani ya kidato cha pili. Natarajia kuingia kidato cha tatu hapo mwakani tukijaaliwa.”

   Sauti yake iliweza kunivuntia na kutamani niwe namuongelesha kila dakika ili niweze kuisikia. Mara nyingi hua sichagui rangi pindi nimuonapo msichana mrimbwende,ila msichana akiwa mzuri na mweupe hunivutia zaidi. 

   Ila kwa huyo msichana alizidi kila kitu nilichokua napenda kumuona msichana mzuri anacho.

   Lafudhi yake ya kipwani ilinifanya nishindwe kujua asili yake hasa ni ipi. Ila nywele zake za kimanga ziliweza kunifanya nihisi kama si uzawa wa kutoka Tanga basi utakua udongo wa Mombasa.
   Maana lafudhi yake ilikua nzuri na ya kupendeza hasa kwenye ngoma za masikio yangu.
Mwili mwembamba na kifua kidogo kilichobeba matiti yanayochupukia ndiyo yaliyonifanya nishindwe kuendelea kuutalii mwili wa msichana huyo. 

   Mtindo wa nywele zake nyingi nao ulizidi kumfanya aonekane mzuri hasa kila nifunguapo kope zangu kumtazama.
   “Nitarudi baadae basi ili tujue tatizo ni nini kaka yangu.” 
 nilishtushwa na kauli hiyo ya kuashiria kuniaga. Sententensi hiyo ilinifanya niache kazi niliyokua naifanya hapo awali na kuchukua karatasi maalumu yenye gundi na kubandika kwenye Laptop hiyo.
   “unaitwa nani, nataka kuandika jina lako hapa juu.” niliongea maneno hayo huku nikiwa nimeshika kalamu ili anitajie jina lake niweze kuliandika.
   “Naitwa Haiba.” alijitambulisha na kunifanya nishtuke kidogo.
Jina lake lilinisisimua sana. Maana mpaka muda huo alikua amekamilisha upekee wake. 
Toka nazaliwa sikuwahi kulisikia jina hilo kwa mtu mwengine zaidi ya kulisikia kwenye masomo tu ya shule ya msingi. Haiba na Michezo.

   Nilibaki natabasamu na kuliandika jina hilo kwenye kile kikaratasi nilichokibandika kwenye Laptop yake.
   “kwa heri.”

   Sauti hiyo ilichomoka kwenye midomo ya Haiba na kuunganishwa na kitendo bila kusubiri ruhusa kutoka kwangu.
   “Molito tuliza mizuka......hawa wanafunzi wa shule wanikalie mbali kabisa.”  
Niliongea maneno hayo na moyo wangu. Lakini macho yaliendelea kumsindikiza mrembo huyo ambaye alikua anatembea taratibu kama twiga. Lakini huko nyuma anatingisha mkia kama samaki. 

   Basi nikatikisa kichwa changu kama ishara ya masikitiko ya amani na kuusifia uumbuji wa muumba na kuiweka chaji Laptop hiyo kwa matarajio kua itaamka angalau kidogo ili nipate pakuanzia kwenye ufundi wangu.

   Ilinichukua zaidi ya masaa mawili kutazama kama itaonyesha ishara ya chaji kuingia, ila laptop hiyo ilizidi kuniumbua. Maana ilikua inapitisha moto lakini haiwaki. Hivyo ufundi wangu wa kupiga window tu ulinigomea na kuniambia kua laptop hiyo inahitaji mtaalamu zaidi yangu.
“leo fundi uchwara kapatikana.”
Nilijisemea baada ya laptop hiyo kunitoa jasho vilivyo.
   “sasa akija mwenyewe na kutaka kujua ugonjwa wa laptop yake nitamjibu nini Molito mimi?” 
Swali hilo lilinifanya niwaze sana. Maana ni kweli sikutaka kuumbuka kwa mtoto mzuri.
 HAIBA!
   Akilli yangu ilichaji haraka na kumkumbuka kaka yangu Semindu. Ila nilikuja kugundua kua yeye hakua mtaalamu sana wa hizi kazi ama hakua anajishughlisha nazo. Ndipo nikamtafuta rafiki yangu mwengine. Anaitwa Elias Vitalis, sema mtaani tumeshazoea kumuita ‘Killer’

  Hili jina hata mimi mwenyewe sikujua ni nani alimpatia na kwa sababu gani, ila umaarufu wake unalishanda hata jina lake halisi la kuzaliwa.

   Nilifunga ofisi na kwenda ofisini kwa Killer. Niliweka laptop mezani na kutaka kujua tatizo ni kitu gani.
  
   Mtaalamu huyo alianza kuichunguza Laptop ya Haiba baada ya kumpa maelekezo kamili juu ya tatizo la Laptop hiyo. 

   Alijaribu kuchomeka waya na kuunganisha na kioo cha Computer yake ya mezani ili kuangalia tatizo hasa ni kitu gani.

   Ufundi huo ulikua mpya kwangu. Hakika Killer alitumia njia ambayo sikuwahi hata kawaza kama inatumika. Ila hillo tukio liliniongezea elimu zaidi kwenye ufundi wangu.
Niliishuhudia laptop hiyo ikiwaka na kila kilichokua kwenye Laptop ya yule binti kiliweza kuoneakana.
   "Kioo cha hii Laptop ndiyo kina shida. Na kubadilisha ni laki moja na ishirini. Hapo pesa yetu hatujachukua.” 
Maneno ya Killer yalinifanya nitabasamu. Maana alikua yupo vizuri sana kwenye fani hiyo na hakusomea darasani. Hivyo nimtazamapo, hunipa ari na moyo wa kuamini naweza kuwa fundi mkubwa kama yeye siku moja. 

   Maana ofisini kwake sijawahi kumkuta aakiwa amekaa tu hivi hivi bila kutengeneza kitu chochote. Na muda huo huo kuna watu waliingia na kuhitaji kupigiwa window mashine zao.  
 
   Nilimshuhudia akitengeneza elfu arobaini hapo hapo nilipo tena kwa dakika chache tu nilizokaa karibu naye.

   Basi nikaichukua laptop hiyo na kuiweka kwenye begi na kurudi ofisini kwangu.
   “Molito, kuna dada sijui mwarabu yule, amekuja kukuulizia. Amekaa kama dakika kumi hapa akikusubiria.”
Nilipata ujumbe kutoka kwa dada muuza chakula kutoka kwenye fremu ya pili.
   “Hajaacha maagizo yoyote?” ilinibidi niulize. Maana sikua na hofu tena na nilikua naweza kumuelekeza hata akihitaji niifanye njia aliyokua akiitumia Killer nilikua nimeshajua jinsi ya kufanya.
   “amesema atarudi tena baada ya swala ya magharibi.” 
Jibu hilo lilinifanya niangalie saa yangu. Ilikua mchana wa saa nane. Nikahisi huenda Haiba anatoka mbali ndio maana msaa yake ya kuja ofisini kwangu yanapishana parefu.
   “leo una chakula gani?”
 muda huo ulitosha kabisa kunifanya nitamani kupata maakuli. Maana toka nianze kupata visenti niliwazuia nyumbani kuniletea chakula kama ambavyo mdogo wangu alikua akifanya hapo awali wakati naanza kazi.
  “kuna wali maini, samaki maharage kama kawaida. Tena leo mboga za majani zipo mbili. Kisamvu na tembele. Uamuzi wako tu. Dagaa kwa wateja wa ugali.”
Dada huyo katika orodha yake, ugali aliuweka mwishoni kwakua alikua anafahamu mimi sio mpenzi wa ugali. Hua nakula mara mojamoja sana. 
  “wali maini itakua poa. Weka wa kushiba mama. Kile kipimo cha mbeba zege.” 

   Ni kawaida yangu kusema hivyo. Japo si mlaji sana na dada huyo kipimo changu alishakijua. Hivyo ilikua ni sehemu ya utani na kumfanya acheke.

   Alinipatia CD zangu ambazo wateja walizirejesha wakati ambao sikuwepo. Nilizipokea na kutiki majina yao. Maana katika vitu ambavyo mazoea nilikua naweka pembeni wakati wote, ni mtu kukaa sana na CD yangu.

  Sikuona ugumu kumuachia rafiki yangu ofisi pindi niondokapo, nilihakikisha kila mteja wangu napajua anapoishi. Hiyo ilinisaidia kupunguza kilio cha kuibiwa CD kama wenzangu walivyokua wakilalamika. Labda ziharibike tu kwakua kila mteja ana usataarabu wake wakati wa matumizi na utunzaji.
   
   Masaa yalisogea taratibu sana. Nikahisi huenda ni kiu niliyokua nayo ya kuonana na yule msichana mzuri kwa mara nyinngine. Msichana ambaye amenifanya nimkumbuke kwa sauti yake na muonekano wake kila baada ya nusu saa.

   Kufumba na kufumbua, saa yangu iliyokua kwenye kioo cha computer ilinisomea kua ni saa moja kamili jioni. Lakini msichana huyo hakutokea.

   Muda huo alifika mteja wa kuchoma CD ofisini kwangu. Nilimkaribisha na tukaanza kuchagua nyimbo alizotamani ziwepo kwenye CD yake.
   “mambo zenu.”

   Ilikua ni kama shoti niliyopigwa na kushtuka bila kificho baada ya kuisikia salamu hiyo iliyonijulisha kua Haiba amefika. Nilimtazama haraka na kumfanya agundue kua amenishtua kwa salamu hiyo. Aliachia tabasamu binti huyo maridhawa.
   “safi, karibu.”
Tuliitikia sambamba mimi na yule mteja aliyekuja ofisini kwangu kwa shughuli ya kuchoma CD. Ilibaki kidogo tu nimuuliza yule mteja kama na yeye ana hisa zake pale ofisini mpaka anapata kibali cha kukaribisha watu. 

   Ila nikamezea tu, asije kuniona nina nongwa bure. Nikamsonya ndani kwa ndani bila mtu yeyote yule kusikia kisha macho yangu yote yakanasa kwenye sura ya Haiba.
 
   Mtoto mzuri alishabadili nguo zake na kubadili mtindo wa ubanaji wa nywele pia. 
Safari hii hakuniruhusu nione macho yake moja kwa moja. akaongezea na miwani yenye rangi ya bluu kwa mbali japo vioo vya miwani hiyo viliweza kuonesha ndani. 
Dah! 
   Kweli Mungu alimuumba mtoto Hiba na mama yake alimzaa kwa kutanua vizuri miguu bila kumbana. 
Maana nilishindwa hata kuweka kasoro japo kuna usemi unasema kua hakuna kizuri kisichokua na kasoro ndani yake.
   “Pole jamani kwa kukushtua.. Sikujua kama hujaniona.” 
Sauti murua ilipenya masikioni mwangu. Mpaka nikawa namuonea wivu yule mteja kwa kuisikiliza. Nilitamani hata nimalize kazi yake haraka aondoke niendelee kuisikia sauti hiyo peke yangu. 
   “kweli nimeamini kua ugonjwa wa shambulio la moyo hauwezi kumpata mtu mwembamba kirahisi. Ningelikua bonge ningelianguka sasa hivi.” 
niliongea maneno hayo na Haiba akaanza kucheka hadi akajizuia mdomo wake na mkono kwa aibu aliyokua nayo. 

   Yule mteja naye akacheka. Alikua ananikera sema tu hajui. Nilitamani hata vichekesho vyangu asicheke. Maana nilifanya yote hayo kwa ajili ya Haiba. 

   Kwakua ofisi yangu ilikua kubwa sana, ili isipwaye, bosi wangu alinunua sofa lengine la watu watatu na kuliweka humo ndani. Hivyo ikawa rahisi kumkaribisha Haiba ndani ya ofisi na akakubali kuingia na kwenda kukaa kwenye sofa hilo ambalo lilikua linatazamana na sisi tulipokaa. Ambapo napo kulikua na sofa la watu wawili.
   “samahani ngoja nimalizane na huyu mteja dakika mbili tu kisha nitakupa matokeo ya kifaa chako.” niliongea maneno hayo huku nikimmiminia tabasamu lote msichana huyo. 
Naye alinilipa japo kiuchoyo. Alitabasamu kidogo tu.
  “usijali.”
Jibu lake likazua ukimya wa maongezi na sauti za miziki mbalimbali zikaanza kusikika kwa sauti isiyokera.

   Baada ya kukamilisha idadi ya nyimbo alizokua akizihitaji mteja huyo. Nilichoma CD na kumpatia kisha na yeye akanipatia pesa yangu.
Nilitoa tabasamu kinafki kwa mteja huyo na maneno murua ya kumkaribisha kwenye ofisi yangu kwa mara nyingine yakanitoka. 

   Na yeye bila hiyana alinirejeshea shukurani na kuondoka huku usoni mwake akiwa amejawa na tabasamu la kweli kuashiria kua ameridhika na huduma niliyompatia.

   Niliyageuza macho yangu na kumuangalia Haiba. Nilipokelewa kwa tabasamu murua lililoukosha moyo wangu. Nami kama ada yangu, wala sikutaka kupoteza maksi kizembe mtoto wa kiume. Nilimlipa tabasamu lenye afya zaidi yake. 
ITAENDELEA.......

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI LANGU LINAVUJA DAMU SEHEMU YA 1
PENZI LANGU LINAVUJA DAMU SEHEMU YA 1
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/penzi-langu-linavuja-damu-sehemu-ya-1.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/penzi-langu-linavuja-damu-sehemu-ya-1.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content