PENZI LA MME WA MAMA SEHEMU YA 01 | BongoLife

PENZI LA MME WA MAMA SEHEMU YA 01

PENZI LA MME WA MAMA
( Sehemu ya 1)

Mme wangu leo nataka kukiri jambo moja kwako, naamini litakukera sana lakini naanza kuomba radhi nikiwa chini ya miguu yako, ”alisema Zainabu akimwambia mume wake ,
Masalanda. ..

“Ipi hiyo? Mbona unanitisha mke wangu, mwaka wa tatu sasa tangu tumeoana hujawahi kuniambia hivyo .” “Oooh ! Siku zote nilikuwa nafikiria namna ya
kukwambia mume wangu .“Sasa niambie basi .”

Zainabu alianza kuporomosha machozi na kumfanya mume wake huyo kushangaa na kukifikiria zaidi hicho kitu ambacho kimemfanya mkewe aamue kukisema...

“Labda ameamua kuachana na mimi sasa anashindwa kuniambia ?” aliwaza Masalanda “Utanisamehe kweli mume wangu ?“Nitakusamehe mke wangu, we niambie tu.”

“Unajua ... unajua wakati unanioa nilipokwambia nilizaa mtoto akafa na nikawa sipati mimba nilikudanganya mume wangu ... ”

“Ooo! Kumbe hukuwahi kuzaa kabisa?”
“Hapana, ila.....“Ila nini mke wangu hebu kuwa muwazi jamani!“Nina mtoto... ”
“Hee! Una nini ?”
“Nina mtoto mume wangu, nisamehe sana sikukwambia nilikuficha kwa sababu nilijua utaniacha wakati nakupenda sana mume wangu,” alisema Zainabu huku akiendelea kulia.Kwa mbali ,

Masalanda alianza kumuonea
huruma mkewe . Ni kweli walioana ukubwani sana kwani Masalanda alikuwa na mke akafariki dunia na mpaka kifo cha mwanamke huyo hakuwahi
kumzalia mtoto.Wakati anakutana na Zainabu, aliamini atadumu
naye kwa sababu wote ni watu wazima tayari.

Aliamini kwamba kwa sababu alishazaa mtoto akafa , basi watamtafuta mtoto wao kwa kudura za Mungu mwenyewe.
“Zainabu, ” aliita Masalanda akitumia sauti ya unyonge.“Abee .”
“Hebu nijibu maswali yangu kadhaa
nitakayokuuliza.“Sawa .”

“Huyo mtoto ana umri gani ?”
“Miaka ishirini na moja .”
“Anaishi wapi ?”
“Yupo kwa shangazi yake, Tanga.”
“Anaitwa nani?”
“Mwaija .”
“Baba yake yuko wapi?”
“Alishafariki dunia , si nilikwambia. ”

“Hebu fanya mpango aje hapa, tumlee sisi . Mimi nitakuwa baba yake.”
Zainabu alishtuka kusikia agizo hilo la mumewe kwani siku zote , shangazi wa mtoto huyo amekuwa akimwambia afanye juu chini amchukue binti yake kwani ameanza umachepele, anahofia asije akapata ujauzito akiwa nyumbani kwake ikaonekana amemtuma .

“Kweli mume wangu?”
“Kweli , imetoka moyoni mwangu , sina kinyongo na wewe. ”Zainabu aliachia tabasamu kavu huku akijifuta
machozi kwa kanga. Mumewe alimkumbatia,akampiga busu wakakaa sawasawa .
*

Ilikuwa siku ya tatu, Mwaija alikuwa ndani ya basi la Raha Leo lenye maandishi nyuma yanayosomeka; Tanga wadeka. Kila mara alimtumia meseji mama yake akimjulisha
alipofikia. ..

“Mama sasa tunapita Segera .”
Mama yake alimjibu sawa , akamtakia safari njema.

Moyoni Mwaija alikuwa na furaha iliyopitiliza ,alitaka sana kuishi na mama yake, hasa akizingatia kuwa anaishi katika Jiji la Dar es Salaam ambalo aliambiwa lina kila aina ya raha
na karaha !

Alipofika Chalinze , mama yake alianza safari ya kutoka Kigogo kwenda Ubungo kumpokea binti yake huyo ambaye ilikuwa inamuuma sana kuwa naye mbali

Basi lilifika ubungo, Mwaija akashuka, mama akashtuka moyoni maana mara ya mwisho alimuacha akiwa
na miaka kumu . Alimshangaa kumuona
amenenepa, amenawiri , ametakata ile mbaya, Kikubwa zaidi alimshangaza nguo alizovaa Mwaija alivaa suruali ya kubana, wenyewe wanaita skintaiti na t- shirt juu.

Kwa umbo alilokuwa nalo Mwaija , kila mwanaume alimuangalia kwa uchu wa mapenzi. ..“Ha mama jamani ,” alichangamka Mwaija na kumkumbatia mama yake kwa furaha. ..

“Shikamoo mama.”
“Marahaba mwanangu, lakini Mwaija hizo nguo kweli ni za kuvaa mbele ya watu , si za kulalia hizo?”
“Hamna mama, ndiyo fasheni yenyewe ya siku hizi. Mama upo Dar es Salaam lakini hujui mitindo?”

“Mimi sidhani kama nitapenda mwanangu , hata baba yako niliye naye siamini kama atakukubali kwa mavazi haya . Hapa natamani nikupeleke
wapi sijui ukabadili nguo ndiyo twende
nyumbani.”

“Jamani mama , basi nimekuelewa , twende tu nyumbani nitavaa kanga nikifika. ”Walianza safari ya kwenda nyumbani Kigogo Moyoni mama Mwaija alikuwa anaomba mumewe achelewe kurudi nyumbani ili wao
watangulie kufika na Mwaija abadili nguo haraka sana.. .

“Hivi na huyo shangazi yako ina maana alikuwa hakuoni unavyovaa ?”
“Alikuwa ananiona . ”
“Saw,Akawa anakuacha tu unaharibika
hivihivi?”Mwaija hakujibu swali hilo alihisi halimuhusu yeye zaidi ya shangazi yake .

Kufika nyumbani, mlango ulikuwa wazi ...
“Mswalie mtume, keshafika huyu , sijui itakuaje?”alisema moyoni mama Mwaija,
wakaingia ndani Sebuleni alikaa Masalanda , alipomuona Mwaija
akashtuka.. .

“Karibuni. ..karibuni sana. ”
“Asante , shikamoo, ” alisalimia Mwaija huku akikaa kwenye kochi kwa adabu .
“Marahaba, za safari?”
“Nzuri .”
“Karibu sana, karibu mwanangu, ” alisema Masalanda huku akimkazia macho Mwaija na kumshangaza mkewe kwani alikuwa amemkaribisha kwa uchangamfu uliokuwa mkubwa tofauti na alivyofikiria.

ITAENDELEAA (Yajayo yanafurahisha usikose)

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PENZI LA MME WA MAMA SEHEMU YA 01
PENZI LA MME WA MAMA SEHEMU YA 01
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/penzi-la-mme-wa-mama-sehemu-ya-kwanza.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/penzi-la-mme-wa-mama-sehemu-ya-kwanza.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content