BLACK AMERICA SEHEMU YA 29 | BongoLife

BLACK AMERICA SEHEMU YA 29

BLACK AMERICA
(Mmarekani mweusi)
Mtunzi:Nelson Kimoyi
Sehemu ya 29
#Endelea___nayoo>>Alfajiri paalivyotimu bwana Jamali aliweza kijiandaa kwa ajili ya safari yake ya kwenda Singida kama ambavyo wameelewana yeye na General Brown........
Aliondoka mapema ili aweze kufika mapema aliondoka akiwa yeye na dereva wake
"kanyaga mafuta tuwahi"
Alimsihi dereva wake ambaye alikuwa ni kama anaendesha gari tartibu...........
Naye dereva alitii akafanya kama anavyotaka boss wake
******Igunga sasa pamekucha******
Asubuhi na mapema Laizer akiwa yupo katika chumba cha mahojiano huku O.C.D Bihamunuro akiwa ni mtazamaji tu 
"Edwine ulikubaliwa kazi ili uitumikie nchi yko na umeshindwa sasa basi hii ni nafasi ya mwisho kujitetea ili ufukuzwe kazi kuliko kupelekwa magereza nambie ukweli kabla sijaanza kutumia hizi zana za kutesea nani amekupa kazi??"
Laizer alimuuliza Sergeant Edwine kwa upole kabisaa huku akiwa hana hata lepe la hasira......
Naye Sergeant Edwine aliamua kuumwagika ukweli mtupu pasipo kuficha hata kidogo.....
Ilikuwa furaha kwa Laizer 
"vipi unaweza tupeleka nyumbani kwake??"
"bila shaka"
Alijibu Edwine wakamfungua pingu na moja kwa moja wakaelekea mtaa wa Uarabuni ambako ndiko nyumba ya bwana Jamali ilipo..........
Walifika wakagonga geti mlinzi akafungua ila alishtuka sana alivyomuona O.C.D Bihamunro akiwa kavalia mavazi ya kiasikari huku mabegani mwake akiwa na nyota 
"bila kupoteza muda nadhani umeshajua sisi ni akina nani vipi tumemkuta boss wako???"
Aliuliza Laizer mlinzi akakumbuka kuwa kabla ya bwna Jamali hajaondoka alimuonya na kumwambia kwamba mtu yeyote akija mwambie kuwa nimesafiri hujui mahali nilipoenda
"hayupo kasafiri hata sijui alipoenda"
Alijibu mlinzi huku akiwa na wasiwasi uliokisiri katika macho yake Laizer alicheka kwa kumkejeli
"napenda mtu mkweli siku zote usijiingize katka mkumbo usiokuhusu hii ni mara ya mwisho nakuhoji kirafiki mimi kama Laizer Zuber nambie ukweli boss wako kaenda wapi"
Hakika mlinzi yule alishtuka zaidi aliposikia jina la Laizer Kwani alikuwa akimsikiaga kwenye maredio tu kuwa ni mpelelezi namba moja nchini Tanzania sasa leo yuko mbele ya macho yake 
"boss kaenda singida kibiashara huo ndo ukweli mkuu" 
Laizer alitabasamu baada ya kuona mlinzi kalainika bila shuruti......
"okay tukihitaji msaada wako tutakutafta tena"
Kisha wakaondoka eneo hilo kurudi kituoni walifika wakiwa pamoja na mtuhumiwa wao Sergeant Edwine wakaingia mpaka ndani kisha O.C.D Bihamunuro akaanzisha maongezi
"Edwine umeniudhi sana kushirkiana na waharifu kwahiyo sitkufunga kutokana na Laizer alivyoniomba lakini.nakutimua kazi kwanzia sasa wewe sio askari ni raia wa kawaida tu na ukikamatwa na kosa lolote la kiuharifu wewe njia yako moja kwa moja ni jel"
Alisema O.C.D Bihamunuro huku akimpatia barua ya kumuachisha kazi Edwine aliitisha kikao kifupi ili maasikari wengine wajue kuwa bwna Edwine si askari tena kila
"hii iwe fundisho kwa maasikari wengine wenye tabia kama ya bwana Edwine na tukitoka hapa kikaoni askari mmoja ataelekea nyumbani kwa bwana Edwine akachukue kila kitu ambacho ni mali ya serikali"
Alisema O.C.D Bihamunuro na kisha akafunga kikao hicho
******Breking News******
"Taharuki singida tajiri mkubwa wa migodi ya dhahabu nchini Tanzania bwana Jamali Swalehe mwili wake umekutwa ukiwa hauna uhai katika moja ya hotel maarufu kwa jina la Singidian Hotel iliyopo mkoani singida yasemekena kuwa mpaka sasa chanzo cha kifo cha bwana Jamali Swalehe bado hakijafahamika mpaka sasa maaskari wamedai kuwa uchunguzi unafanyika na hii ndo habari kwa ufupi" 
Ni taarifa ambayo ilipata kusikika katika televisheni iliyokuwa katika kituo cha polisi Igunga taarifa ambayo ilimchanganya Laizer aliyekuwa amekaa na O.C.D Bihamunuro  
"niniiiiiii??"
O.C.D Bihamunuro alitamka kwa nguvu kiasi kwamba Laizer alishtuka........
"daaaah jamaa yupo makini sana kapoteza ushahidi namba moja ila ushahidi namba mbili tunao usijali mkuu"
Aliongea Laizer kwa kujiamini 
******Jinsi ilivyokuwa Singida******
Generql Brown alifika saa tisa usiku Singida kitokana na mwendo kasi aliokuwa akikimbiza gari lake......
Alifikia hoteli maarufu ya kitalii katika mkoa wa singida hotel ya Singidian Hotel and guest.....
Alichukua chumba kisha akalipia akaingia chumbani humo mida ya saa kumi akipanga mipango yake jinsi ya kumuua bwana Jamali kwani alishahisi kuwa kuna mtu anafuatilia nyendo zake.......
"sasa nitakachokifanya nitamuulia chumba kingine tofauti na hichi inatakiwa nidukue hii milango inayotumia card'
Alijisemea Brown huku akijikuna kichwa hakupumzika usiku huohuo akaanza kudukua/kuhack ile milango ya kikomputer ambayo funguo yake ni card ya kusugua tu mlangoni halafu unafunguka wenyewe na kweli aliweza kufanikiwa kwa hilo........
Kweli mzungu sio mtu wa mchezo mchezo kisha akachukua simu na kumpigia bwana Jamali muda ambao Jamali anapigiwa ndio muda alioanza safari 
"haloo mr brown ndo nimeanza safari sahivi alfajiri hii"
Alisema Jamali hakujua kama kuna mabaya yanakwenda kumtokea.....
Naye General Brown alifurahi sana kuona kuwa Jamali kaanza safari...
"okay bwana Jamali mimi mwenyewe nipo njiani naja nipo Kateshi jirani kabisa na Singida kwahiyo kama utafika kabla yangu kodisha chumba kwenye ile hoteli maarufu inayoitwa Singidian hotel kisha uniambie namba ya chumba nije nikupatie milioni miq tatu na hamsini ili zikusaidie kuongeza nguvu"
Alisema General Brown kimakusudi kabisa ili kuzida kumpa munkari bwana Jamali.........
Gari lq bwana bwana Jamali liliunguza mafuta kwa masaa mawili hatimaye likawa limeweza kufika Singida.....
Bwana Jamali alienda moja kwa moja mpaka katka hoteli aliyoelekezwa na General Brown qkakodisha chumba na kuingia humo kisha akatoa simu yake na kumpigia Brown
"ndiyo mr Brown nime fika ndugu yangu na nimechukua chumba namba 99 kwahiyo ukifika mapokezi sema chumba namba 99"

"worry out nimebakisha kilomita moja"
Kisha simu ikakatika Brown alikuwa na furaha isiyokuwa na kipimo baada ya bwana Jamali kujiingiza mkengeni yeye mwenyewe akakaa kama dakika kumi akiwa anajiandaa
"bastola haina kiwambo acha nimchome tu sindano ya sumu"
ITAENDELEA..........
Eeeeeeh marafiki zangu simulizi yetu inaelekea ukingoni.

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : BLACK AMERICA SEHEMU YA 29
BLACK AMERICA SEHEMU YA 29
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/black-america-sehemu-ya-30.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/black-america-sehemu-ya-30.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content