BINTI KUTEGEMEA UPEPO WA KISULISULI UKULETEE MUME NI NDOTO ZA ALINACHA | BongoLife

BINTI KUTEGEMEA UPEPO WA KISULISULI UKULETEE MUME NI NDOTO ZA ALINACHA

NA : PADRI KAWONGA

       Katika nchi yetu Tanzania kunauhuru wa kuabudu, lkn kwa namna moja au nyingine uhuru huu unatumiwa vibaya na baadhi wa watumishi wa Mungu. Baadhi ya watumishi nyakati za hivi karibuni wanatumia matatizo ya watu kama msingi wa kuanzisha au kuimarisha makanisa yao. Ukienda ktk makanisa hayo waabuduo wengi wao ni wajane, wagonjwa, wagani, waathirika wa HIV/AIDS, wapweke, walioachwa, waliotendwa, waliofanyiwa ukatili, watu wenye matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawazo..n.k sasa ukitazama makundi haya ni ya watu wanaohitaji msaada wa haraka, lkn baadhi ya watumishi wa Mungu makundi haya ndio limekuwa shamba lao la kujivunia pesa.
          Hivi karibuni wamesikika wachungaji fulani wakikusanya kundi la mabinti wasioolewa, walozalishwa na kuachwa, walotendwa, wanaotafuta waume wa kuwaoa na kuwaamisha kuwa wataletewa waume kwa upepo wa kisulisuli. Huku ni kutiana ujinga katika hali ya matatizo. Hapa kilichohitajika ni hawa wachungaji kuwafanyia ushauri wa kiroho na kujua wanakosea wapi hadi wasiolewe. Pia sasa hivi katika nchi yetu tatizo hili ni kubwa, suluhu ya kudumu ni kuangalia malezi ya vijana na watoto katika familia. Sio  siri ukiona mabinti hawaolewi ujue kunatatizo la mfumo wa malezi katika familia, jamii na ngazi za majifunzo. Nyanja hizo ndio watumishi wa Mungu jikiteni huko na sio kuwapumbaza mabinti zetu kuwa watapata waume kwa upepo wa kisulisuli. Sasa hivi mtawaaminisha na kuwaozesha mabinti hao kwa watu ambao sio sahihi na madhara yake yatakuwa makubwa kama vile magonjwa kuongezeka, kupata walemavu wengi kwani wengi wa mabinti hao wanaenda kuozwa kwa wazee au watu ambao akili hazipo sawasawa.
           Binti usiaminishwe habari ya upepo wa kisulisuli kuwa utakuletea mume bali fanya yafuatayo utapata mume, angalia tabia zako, uvaaji wako, mawasiliano, status yako ya mahusiano, uchumi wako na utegemezi, usafi wako, kubwa zaidi Ucha-Mungu wako. Inawezekana mabinti wanakosea kwa kuhitaji mume mwenye sifa fulani aliyeandaliwa, lkn kumbuka sifa zingine unaweza kuzitengeneza wewe mfano mume mwenye pesa unaweza kumtengeneza wewe, mume mtanashaji, mnene au mwembamba, msomi, mtafutaji..n.k
            Wachungaji tuwasikilize kwanza matatizo yao kwanini hawaolewi, tukianzia hapo tutakuwa msaada mkubwa sana kwao, lkn kinyume na hapo ni ukandamizwaji na unyanyasaji na unyonyaji, tusiwageuze shamba la bibi kutokana na matatizo yao.
          Nilipenda sana tamko la Mkuu wa nchi fulani Afrika Mashariki kwamba Watumishi wa Mungu wote lazima wawe na Elimu ya dini kuanzia ngazi ya Diploma, na alifunga makanisa na misikiti yote ya watumishi wa Mungu wasio na Diploma. Hilo ni jambo litakaloondoa udanganyifu na unyanyasaji kwa miamvuli ya dini. Ukifanya tathmini katika nchi yetu, wengi wa Watumishi wa Mungu si msaada kwa matatizo ya watu wa sasa bali tunawatia ujinga na kuwaaminisha miujiza. Hatuwahimizi waende hospitali wakapate tiba sahihi na yenye miujiza ya kweli  kupitia Hospitali na Madaktari wenye hofu ya Mungu, hatuwahimizi kujitegemea bali tunawaombea miujiza ya kupata hela wakati sisi wenyewe tukitaka hela tunawaambia watuchangie. Tunalo la kutafakari juu ya elimu ya watumishi wa Mungu katika nchi yetu.
       Baadhi ya watu wanatumia vibaya vipaji walivyopewa na Mungu kama vile Sauti, Umbo, Sura, Ushawishi kujipachika miavuli ya watumishi wa Mungu kwa lengo la kujipatia fedha na hayo ndiyo matokeo ya kutiana ujinga kama vile upepo wa kisulisuli unaowachanganya mabinti zetu sasa. Mwisho mwishoni Afrika tujikaze, Tanzania tujikaze katika kuabudu na kumwamini Mungu wa kweli.
By Fr. Kawonga
Holy Family Parish-Mkongo

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : BINTI KUTEGEMEA UPEPO WA KISULISULI UKULETEE MUME NI NDOTO ZA ALINACHA
BINTI KUTEGEMEA UPEPO WA KISULISULI UKULETEE MUME NI NDOTO ZA ALINACHA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/binti-kutegemea-upepo-wa-kisulisuli.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/binti-kutegemea-upepo-wa-kisulisuli.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content