Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 9 | BongoLife

Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 9

Simulizi : BABA KIUMBE WA AJABU
EPISODE 9
ILIPOISHIA
“Kwani anaumwa sana?”
“Toka asubuhi analia tu.”
“Kafanya nini?”
“Mmh, nenda ndani ukamuone.”
“Masalu,” baba aliniita.
“Naam baba.”
“Eti kuna nini?”
SASA MWEMWELEKA NAYO...
“Kuna vitu ambavyo sielewi.”
“Vitu gani?” Baba alisema huku akiingia ndani.
Alipoingia ndani alinikuta nimeshikilia mguu.
“Kuna nini?”
“Baba sehemu hii inaniwasha sana kufikia hatua ya kunikosesha raha.”
“Hebu nione,” nilimuonesha baba, baada ya kuona alisema:
“Kumbe hiki?”
“Ndiyo baba.”
“Sasa tatizo nini?”
“Kinaniwasha.”
“Usikikune kitapoa chenyewe.”
“Hapana baba bora niende hospitali.”
“Masalu usiende hospitali, ugonjwa juu si wa kawaida.”
“Wa nini?”
“Utajua tu baadaye, lakini chonde usiende hospitali.”
“Au ndiyo kama wa dada Monika?”
“Eti?” Kauli yangu ilimshtua baba na kunitazama mara mbili kama ndiyo siku yangu ya kwanza kuniona.
“Eti umesemaje?”
“Baba mbona umeshtuka hivyo?”
“Sijakuelewa, hebu rudia swali lako.”
“Nauliza, kisiwe kidonda kama cha dada Monika.”
“Mama yako ndiyo kwakwambia? Leo atanitambua,” baba alikuja juu.
“Baba badala ya kunijibu swali langu unakimbilia kutaka kumpiga mama au ndiyo umemuona gunia lako la mazoezi,” nilizidi kumchanganya baba na maneno yangu ambayo hakufikiria hata siku moja nitayatamka.
“Masalu mbona unanikosea heshima?”
“Sijakukosea heshima ila nataka kujua ukweli wa muwasho huu kwa vile nilibashiliwa kipindi kirefu.”
“Na nani?”
“Na dada Monika”
“Alikubashiria nini?”
“Alinieleza kuwa kifo chake kimetokana na kukikataa kidonda hiki, na ulichomuahidi ndicho kilichotokea.”
“Muongo, unamsingizia Monika wakati uongo wote kakupa mama yako.”
“Baba utamuonea mama bure, mama hajanieleza chochote zaidi ya kunifanya mtoto mdogo mambo ninayoyajua.”
“Mambo gani?”
“Kuhusu chanzo cha utajiri kidonda cha dada Monika mpaka kifo chake kilisababishwa nini na utabiri wake kidonda kikitoka kwake kinakuja kwangu.”
“Mmh,” baba aliguna, kisha alinitazama kwa muda na kuangalia juu kabla ya kushusha tena pumzi.
“Masalu.”
“Naam.”
“Niambie ukweli mama yako kakuambia nini juu ya huu muwasho?”
“Kaniambia ni muwasho wa kawaida, utapoa wenyewe.”
“Hakukuambia kitu kingine?”
“Hajaniambia, ndiyo maana nilijua ananidanganya, dada Monika alinipa siri nyingi, zingine hata mama hajui na bahati mbaya wakati anakufa nilikuwa mbali lakini kuna mengi mazito alitaka kunipa juu ya familia yetu.”
“Monika alikuambia nini?”
“Alinieleza jinsi kidonda chake kilivyoanza kama muwasho na mwisho kilikuwa kidonda kisichouma zaidi ya kutoka maji na kukatazwa asiyafute.”
“Mmh, pamoja na uongo wake nakuomba usimuamini ni mfitini yule.”
“Baba unataka kunihakikishia kidonda hiki sio kama cha dada Monika?”
“Nimekueleza usimfuate Monika ni muongo.”
“Kama muongo naomba na mimi uniondolee masharti ya kuwa na mke.”
“Masalu, umri wako bado.”
“Baba mimi si mdogo, ukweli ni kwamba huu muwasho mwisho wake ni kidonda ambacho kitaingiza pesa kwa njia ya kumwagika maji. Baada ya dada Monika kuyashindwa masharti yako uliamua kumuua na mimi nahofia utaniua.”
“Narudia tena kukueleza Monika ni muongo.”
“Baba nasema kama ndicho kidonda hiki basi nami nitakufa kama dada Monika.”
“Masalu kuna sababu ya kuzungumza kwa kituo.”
“Sawa baba lakini kaa ukijua kama muwasho huu mwisho wake ni kidonda cha utajiri sikitaki nakuomba unirudishe shuleni.”
“Nikurudishe shuleni fedha za shule utazipata wapi?”
“Kwani lazima nipate kidonda ili nisome?”
“Utasoma, lakini kumbuka fedha zinatafutwa na njia zake pesa zipo nyingi.”
“Moja wapo ni kidonda changu?”
“Masalu tutazungumza, hebu vaa kuna mali mpya nimeituma dukani mwako twende ukaiangalie.”
“Sawa baba,” nilikubali shingo upande na kukubali kuondoka na baba kwenda dukani kwangu. Nilipanga kutokwenda dukani baada ya kupata uhakika wa muwasho wangu.
Niliondoka na baba hadi dukani ambako alinionesha baadhi ya bidhaa alizoniagizia toka China, vilikuwa vitu vingi sana ambavyo vilifanya duka langu liongezeke. Kwa muda mfupi hata ndugu zangu walianza kunionea wivu. Wazo la haraka lilikuwa huenda aliyoyafanya dada Monika ya kutaka naye awe na maisha yake ndiyo yaliyosababisha hali ile.
Hali ya muwasho iliendelea kupungua na kuweka kitu kama gamba kwenye weusi ule. Siku moja asubuhi ilipoamka nilikuta lile gamba limetoka kutokana na kujigeuza na kuweka kidonda. Moyo wangu ulilipuka na kujua kazi imeanza, kutokana na maelezo ya awali kidonda kile hakikutakiwa kutibiwa.
Nilijikuta nikikosa raha pamoja na mali zote alizonipa baba sikuwa na furaha yoyote moyoni mwangu kuishi na kidonda kisichowekewa dawa mpaka mwisho wa maisha yangu. Nilipoamka na kukuta hali ile nilimweleza mama, naye alinipa jibu jepesi.
“Aliyokueleza dada yako yametimia.”
“Mama nitafanya nini, nitaishi hivi mpaka lini?”
“Masalu, ondoa wasiwasi kama nilivyokueleza toka mwanzo usishtuke sana kwa vile hali hii nilishakueleza mapema uishi vipi baada ya kutokea kwa hali hii.”
“Mama kusema ni rahisi, lakini haivumiliki, nitaishi vipi na watu wakijua nina kidonda kama cha dada Monika nitauweka wapi uso wangu?”
“Nani atajua, labda utawaonesha wewe.”
“Duniani hakuna siri.”
“Ukitaka iwe siri itakuwa siri.”
“Lakini kwa nini umenifanya hivi si mngeniuliza kuliko kunipa kidonda bila idhini yangu?”
“Mimi utanilaumu bure wa kumlalamikia ni baba yako.”
“Mama nami nitakufa kama dada siwezi kuishi maisha ya mipaka.”
Nilimuhakikishia mama sitakubali kuishia maisha yale bali nitakayoamua mwenyewe.
Siku ile mama aliniomba nisivae viatu na soksi bali nivae sandoz ili nisikibughudhi kidonda ambacho kilikuwa kimeanza kutoa maji. Ugumu wa kuishi maisha ya kidonda nilianza kuuona kwa kuamini mabadiliko yangu ya mavazi lazima watu watataka kujua kumetokea kitu gani kilichosababisha hali ile.
Siku ile nilishinda ndani nikilia japo mama alijitahidi kunibembeleza, sikuweza kumkubalia niliamini ule ulikuwa uonevu wa kupewa kitu nisichokipenda tena chenye masharti ya kumdhalilisha mtu.
*****
Taarifa zilimfikia baba aliyekuja kunipoza, alipofika alinikuta nimejifungua ndani kwani sikuwa na hamu ya kuonana na mtu. Alinigongea mlango kwanza nilikaa kimya bila kujibu lolote.
“Masalu hebu fungua tuzungumze.”
Sikumjibu nilikaa kimya, lakini aliendelea kunibembeleza mpaka nilipofungua mlango. Nilipomuona tu niliangua kilio.
“Baba mmenifanya nini?”
“Masalu mwanangu hebu tulia nikueleze jambo.”
“Kitu gani baba utachonieleza nikuelewe?”
“Najua umeshtuka kuona kidonda hicho, nataka kukueleza kila kitu ulichoelezwa na Monika kina ukweli. Lakini nakuomba utusamehe kwa uamuzi wa kidonda hiki kuhamia kwako.”
“Lakini kwa nini hamkunishirikisha mwenyewe?”
“Hatukuwa na jinsi, pia hakuna mtu mwingine katika familia yetu ambaye angeweza kukaa na kidonda hiki baada ya Monika kufa.”
“Baba mimi nitaweza wapi maisha ya mipaka?”
“Unaruhusiwa kufanya lolote kasoro kulala na mwanamke tu.”
“Baba huoni kunikataza kulala na mwanamke ni sawa na kuiondoa furaha yangu moyoni?”
“Kwani usipolala na mwanamke unapungukiwa nini?”
“Vingi baba, vingi sana hakuna raha ya mwanadamu kamili bila kuwa na mwenza.”
“Ni mawazo yako, ukiizoea wala haitakusumbua.”
“Na nikitembea na mwanamke?”
“Utamfuata dada yako Monika.”
“Bora nimfuate,” nilimjibu kwa hasira.
“Hapana usifanye hivyo kuna vitu vingi nilivyopanga kukufanyia kuliko watoto wangu wote, huoni hata sasa hivi wanakuonea wivu? Nakuhakikishia kukufanyia mambo mazuri. Nakuomba usiwe kama dada yako Monika.”
“Sawa baba,” nilikubali kwa shingo upande.
Kukubali kwangu baba alikufurahia sana na kunikumbatia, hakujua jinsi gani mwenzake nilivyoumia. Tuliondoka pamoja kwa maelekezo yaleyale ya mama ya kutovaa viatu na soksi ili kukiacha kidonda kipumue. Nilikubaliana na baba ambaye hakutaka niwe kwenye mawazo sana muda wa siku ile kuwa nami karibu muda wote.
Nilijilazimisha kuikubali hali ile kwa vile sikuwa na jinsi, hata ningefanya nini isingebadilika. Siku zilikatika huku nikipata maswali mengi kutokana na kubadilika na kuonekana mtu mwenye mawazo mengi. Watu wangu wengi wa karibu walitaka kujua sababu ya mimi kuwa katika hali ile.
Niliwaeleza nipo sawa, lakini hawakukubali na kunikubalia kwa shingo upande, siku zilikatika huku nikiendelea kuficha siri zangu. Tatizo lililonisumbua lilikuwa kwa mpenzi wangu ambaye siku za nyuma nilikuwa nikifanya naye mapenzi hadi kufikia hatua ya kumuahidi kumuoa.
Mwanzo nilijitahidi kumkwepa ili asijue sababu ya mimi kufanya vile, lakini kila siku nilipozua uongo alinikubali mwisho uongo uliisha.
“Masalu mbona siku hizi sikuelewi?”
“Kivipi?”
“Kila siku umekuwa mtu wa visingizio.”
“Lakini si nimekueleza sababu?”
“Sababu gani hizo?”
“Kwa hiyo unatakaje?”
“Nina hamu na wewe mpenzi wangu.”
“Si nimekueleza subiri mpaka tutakapooana.”
“Masalu usinitanie, si ni wewe uliyenilazimisha tufanye mapenzi kabla ya ndoa?”
“Ni kweli, lakini nimegundua tulifanya kosa.”
“Masalu niambie moja unanipenda hunipendi?”
“Nakupenda.”
“Basi nataka leo tulale pamoja.”
Kwa kweli kwangu ulikuwa mtihani mgumu wa kumkwepa mpenzi wangu nisifanye naye mapenzi. Jioni nilipotoka kazini alinipitia na kwenda La Kailo Hoteli, nilishindwa kumkatalia. Kumbe alikuwa amekwishachukua chumba kabisa, tulipofika tuliingia moja kwa moja ndani.
Je nini kitaendelea. ??

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 9
Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 9
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/baba-kiumbe-wa-ajabu-sehemu-ya-9.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/baba-kiumbe-wa-ajabu-sehemu-ya-9.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content