Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 16 | BongoLife

Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 16

simulizi: BABA KIUMBE CHA AJABU
EPIDODE 16
INAENDELEA
Pamoja na kujua ubaya wao kwangu, bado sikutakiwa kuua nikijua kabisa chanzo cha kifo kinatokana na nini. Tulilala kila mtu na kitanda chake kwa kuzima taa. Katikati ya usiku niliota ndoto moja baba amegeuka kiumbe cha ajabu chenye manyoya na meno marefu. Nilimuona mama na ndugu zangu wakilia. Kilichonishangaza zaidi alionekana kama kiumbe kisicho na uhai.
Nilishtuka usingizini na kukaa kitako huku nikijiuliza ndoto ile ina maana gani, Nilijikuta nikishindwa kuelewa ndoto ile ina maana gani na kwa nini baba ageuke kiumbe cha ajabu chenye kutisha? Sauti za kilio nilizozisikia ilionesha wazi msiba ule ni wa baba. Niliamini ndoto ile iliashilia kifo cha baba lakini kubadilika kwa umbile la ajabu lilikuwa likiashiria nini?
Lakini sikutaka kuamini moja kwa moja kutokana na kauli ya mganga kuwa baba yangu atakufa kama nikikutana kimwili na mpenzi wangu na sharti lile nililitekeleza. Niliamini huenda ile ni ndoto ya kawaida tu wala haihusiani na ukweli wowote, kutokana na kutoelezwa chochote na mganga juu ya kupata ndoto yenye kiashirio.
“Vipi Masalu?” Sauti ya mpenzi wangu ilinishtua nikiwa katikati ya dimbwi la mawazo.
“Aah… safi tu,” nilijibu huku nikijitahidi kuficha kilicho moyoni mwangu.
“Safi, mbona umeamka na kukuona ukitupa mikono kama unazungumza na mtu kuna kitu gani kimekusibu?”
“Mmh! Kweli nimeona ndoto moja imenitisha sana.”
“Ndoto gani?”
“Nimeota nyumbani ndugu zangu wanalia baba akiwa amelala kitandani, lakini kitu cha ajabu amegeuka kiumbe cha ajabu chenye kutisha.”
“Sasa wasiwasi wako nini? hiyo si ndoto tu?”
“Huenda baba amekufa.”
“Masalu si ulielezwa atakufa kama tukikutana kimwili?”
“Ndiyo, hata mimi nashangaa.”
“Kwani mganga alikueleza nini juu ya njozi utakayoota?”
“Hakunieleza chochote.”
“Sasa wasiwasi wako nini?”
“Kwa vile baba hali yake ilikuwa mbaya, ndoto hii imenitisha sana.”
“Masalu acha kujitia presha bure, maisha ya baba yako yako mikononi mwako.”
“Mmh! Sawa, lakini niliingiwa na wasiwasi mkubwa.”
“Lala mpenzi.”
“Nashukuru kwa kunipa moyo.”
“Nipo hapa kwa ajili hiyo.”
“Asante mpenzi wangu kwa kunijali sina cha kukulipa.”
“Cha kunilipa baada ya kupona ni ndoa tu.”
“Omba jingine hilo umepata. ”
Niliagana na mpenzi wangu kila mmoja alilala, usingizi haukuchelewa kunichukua, haikuchukua muda mrefu njozi ilijirudia, tena safari hii niliwasikia wakilia huku wakitupia shutuma zao kwangu kuwa mimi ndiye chanzo cha kifo cha baba.
Nilishtuka tena kitandani na kuwasha taa, mpenzi wangu naye alishtuka na kuhoji kwa nini nimeamka tena.
“Masalu, vipi mpenzi wangu?”
“Mmh!” niliguna tu.
“Mbona sikuelewi?”
“Mmh! Ndoto bado inaning’ang’ania.”
“Umeota nini tena?”
“Bado kifo cha baba kinaendelea na safari hii nimewasikia mama na ndugu zangu wakinishutumu ndiye niliyesababisha.”
“Lakini bado itakuwa ni njozi tu kwa vile mawazo yako yote umeyahamishia huko.”
“Kwa hiyo nifanyeje?”
“Hebu iache njozi iishe wala usiamke.”
“Mmh! Ngoja nijaribu.”
Nilirudi kulala tena, ajabu nililala mpaka asubuhi bila kuota tena, mpenzi wangu ndiye aliyeniamsha.
“Masalu.”
“Naam.”
“Vipi upo sawa?”
“Nipo sawa, vipi?”
“Naona leo umelala sana.”
“Kwa muda huu ni saa ngapi?”
“Mmh! Ni saa tatu na nusu.”
“Ooh! Leo nimelala sana.”
“Inawezekana ni kutokana na kuamkaamka usiku kutokana na njozi ulizoota.”
“Na kweli.”
“Vipi uliota tena?”
“Sikuota, nimelala vizuri.”
“Unaona wasiwasi wako tu, njozi zingine hutokana na mawazo ya mtu.”
“Ni kweli, lakini ziliniweka kwenye hali mbaya kwa vile kama kweli baba atakufa ndugu zangu hawatanielewa.”
“Wasikuelewe vipi?”
“Si nitaonekana mimi ndiye niliyemuua.”
“Masalu acha kujitoa akili, ulikwenda sehemu gani kumroga baba yako?”
“Sijaenda popote.”
“Sasa?”
“Si inaonesha kuwa uchawi umewarudia.”
“Hukuwaroga?”
“Ndiyo.”
“Sasa wewe unaogopa nini?”
“Mmh! Suala la kuua si la kawaida.”
“Wangekuua wewe lingekuwa la kawaida au umefurahia kuuawa kwa dada yako Monika?”
“Swali gani hilo, hujui nilivyoumizwa na kifo cha dada yangu?”
“Sasa inakuwaje unaogopa vifo vya watu mnajua kabisa hawana nia nzuri na wewe?”
“Basi tuachane na hayo, tuoge tukapate chai.”
Niliamka kitandani na kwenda kuoga, baada ya kuoga tulikwenda kupata kifungua kinywa kilichokuwa mlemle kwenye hoteli tuliyokuwa tumepanga.
Wiki ilikatika tukiwa tumejificha na mpenzi wangu, hata simu niliamua kuizima ili kuondoa usumbufu wa ndugu zangu. Siku moja asubuhi tukiwa mgahawani tukipata kifungua kinywa niliamua kuwasha simu. Utafikiri kuna mtu alikuwa akisubiri kwa hamu nilipowasha tu simu iliingia. Kuangalia ilionesha namba ya kaka yangu, niliiangalia kwa muda bila kupokea mpaka ikakatika. Haikupita muda simu iliita tena alikuwa dada nayo niliiangalia bila kuipokea.
“Masalu mbona hupokei simu?”
“Achana nao.”
“Kina nani?”
“Si hawa wapuuzi.”
“Ndugu zako?”
“Ndiyo.”
“Hebu pokea uwasikilize kwa vile hujui wanataka nini?”
“Achana nao najua wanataka kunijua nilivyo.”
“Masalu si umeambiwa kuwa sasa hivi mtu hakusogelei, wasiwasi wako nini?”
“Sina wasiwasi ila sipendi kuwasikiliza kwa vile hakuna jipya la kuniambia.”
“Wasikilize.”
“Sitaki, wale sio watu siwezi kuwasikiliza watu wabaya kama wale.”
Mara simu ya mpenzi wangu iliita aliipokea na kuzungumza.
“Eeeh...Ndiyo...Shikamoo mama...Ndiyo...
Hapana...Lini?..... Leo...Sawa nitamwambia....
nitakujulisha....Hapana tupo Mwanza...Sawa mama nitamwambia....Haya mama.”
Baada ya kukata simu alinigeukia na kunitazama kwa muda.
“Vipi kuna usalama?”
“Kiasi.”
“Kuna tatizo nyumbani kwenu?”
“Hapana, kwenu.”
“Kwetu kuna tatizo gani?” nilishtuka.
Je nini kitaendelea?

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 16
Baba Kiumbe Wa Ajabu sehemu ya 16
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/10/baba-kiumbe-wa-ajabu-sehemu-ya-16.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/10/baba-kiumbe-wa-ajabu-sehemu-ya-16.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content