UMUHIMU WA KUFUATA MAELEKEZO UNAPOTUMIA ENERGY DRINKS

ENERGY DRINKS

 ENERGY DRINKS


Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi, kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.

  vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari

Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha maoigo ya moyo kudunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu, na kusababisha kifo cha ghafla.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

Maelekezo yaliandikwa kwenye cupa za vinywaji hivi yana umuhimu mkubwa sana japo walio wengi hatuna tabia ya kusoma maelekezo kabla ya kutumia

JINSI GANI ENERGY DRINKS ZINAVYOFANYA KAZI KATIKA MWILI WA BINADAMU NDANI YA MASAA 24


Kwa ufupi ni kwamba kiungo kikubwa kwenye energy drinks ni caffeine,Caffeine inafanya kazi ya kuzuia uzalishwaji wa kichocheo cha mwili kinachohusika na kulala na kuhisi uchovu.Caffeine inapozuia uzalishaji wa kichocheo hiki mfumo wa fahamu huhisi kwamba mwili umepata matatizo hivyo kufanya kazi kwa kasi sana kuliko kawaida.Katika hali ya kuhisi mwili upo katika hatari ubongo kupitia tezi ya pituitary unazalisha kichocheo kinachojulikana kama ADRENALINE,hiki kinahusika kuufanya mwili kuwa tayari kwa kupigana au kukimbia wakati wa hatari(Fight or flight response).Kichocheo hiki sasa baada ya kuzalishwa kwa wingi kinafanya mapigo ya moyo kwenda kasi,shinikizo la damu kuongezeka na mboni za macho kutanuka( pupil dilatation).Hapa sasa mtu hujihisi mwili umechangamka.

DAKIKA KUMI ZA KWANZA BAADA YA KUNYWA

Unapokunywa energy drink yoyote inachukua muda wa Dakika kumi (10) Caffeine kuingia kwenye mzunguko wako wa damu matokeo yake mapigo ya moyo na shinikizo la damu linaongezeka na kufanya mtu ujisikia mchangamfu hata kama ulikua mchovu uchovu utasikia kama umeisha.


DAKIKA 15-45

Hapa kiwango cha Caffeine kwenye damu inafikia kiwango cha juu kabisa(Peak level) hapa mtu ndo anajihisi uchangamfu wa mwili zaidi.

DAKIKA 45-50

ndani ya kipindi hiki Kiwango chote cha Caffeine uliyokunywa kinakuwa tayari kimeingia kwenye mzunguko wa damu,Hapa ini linakabiliana na Caffeine kwa kufanya mwili kufyonza sukari zaidi hata ile iliyokuwa imetunzwa sehemu mbali mbali za mwili kuirudisha kwenye mzunguko wa damu.

SAA 1

Baada ya saa moja tokea unapokunywa vinywaji hivi,Kiwango kikubwa cha sukari kilichoingia kwenye mzunguko wa damu kwa ghafla na Kiwango chha caffeine kinaanza kushuka hali inayopelekea mwili kuanza kuishiwa nguvu ,hapa mtu anaweza kuanza kujihisi mchovu.

MASAA 5 HADI 6

Caffeine inachukua muda wa saa 6 hadi 5 kuwa imetolewa mwilini kwa asilimia 50%,(half life) kwa hiyo ndani ya muda huu kiwango cha caffeine kinakua kimepungua ndani ya mwili kwa asilimia 50%

MASAA 12

Hapa kiwango chote cha caffeine kinakuwa kimeisha kabisa mwilini

MASAA 12-24

Kutokana na Caffeine kuisha,mwili unaanza kuzoea hali mpya ya bila caffeine,Hivyo mtu anaanza kupata kitu kinachoitwa Caffeine withdrawl sydrome,Mtu anapata matatizo yafatayo Kichwa kuuma,kushtukashtuka,kusahau,kukosa choo au kapata choo kigumu,misuli kuuma

MADHARA YA KIAFYA YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MATUMIZI YA VINYWAJI HIVI


1.SHAMBULIO LA MOYO(CARDIAC ARREST)

Matumizi ya caffeine kwa kiasi kikubwa inapelekea kufanya misuli ya moyo kusinya na kutanuka kwa kasi sana ili kuongeza mapigo ya moyo hali inayoathiri utendaji kazi wa moyo na kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi.
Soma hapa report ya utafiti uliofanyika nchini Canada na kuonesha kuwa kweli energy drinks zinasababisha shambulio la moyo:

 *CANADIAN JOURNAL OF CARDIOLOGY RESEARCH ON ENERGY DRINKS
NDIO MAANA KATIKA CHUPA ZAKE UNASHAULIWA USINYWE WAKATI UNAENDA KULALA ILI UTAPOPATA SHIDA HII UWEZE KUOMBA MSAADA.

2.KIPANDA USO

Kama tulivyoona awali kiwango cha caffeine kinapoisha mwilini mtu anapata caffeine withdrawl sydrome inayoambatana na maumivu ya kichwa.Mtu anavopata caffeine withdrawl syndrome mara kwa mara inapelekea tatizo la kipanda uso

2.SHINIKIZO LA DAMU KUWA JUU( PRESHA YA KUPANDA)

Utumiaji wa vinywaji hivi inaweza kupelekea mtu kupata tatizo la shinikizo la damu kuwa juu(High blood pressure) Kwa inaathiri utendaji kazi wa misuli ya moyo

3.ADDICTION

Watu wengine wanaweza kupata caffeine addiction kwamba anakuwa hawezi kufanya kazi kwa ufanisi mpaka atumie energy drinks.

4.KISUKARI

kama nilivyoelezea awali jinsi gani energy drinks zinaathiri sukari mwilini,hii inapelekea kuvuruga utendaji kazi wa kongosho hasa sehemu inayozalisha Insulin na kupelekea mtu kupata tatizo la kisukari.

5.KUHARIBU MIMBA

Ndio maana kinywaji hiki hakiruhusiwi kutumiwa kwa mama mjamzito kwani kinaweza kupelekea kuharibu maumbile ya mtoto (kuzaa mtoto mwenye ulemavu) au kuharibu kabisa mimba

Kama ilivyo unapotumia kitu chochote kwa kiwango zaidi na ulichoelekezwa ni hatari kwa afya yako.Tutumie energy drinks kama ilivyoelekezwa kwamba ndani ya masaa 24 usizidishe chupa zaidi ya mbili.

Watu wengine wamekuwa wakihoji mamlaka za vyakula na dawa(TFDA),TBS kwa nini waruhusu vinywaji hivi kuuzwa kwa watu.tunachosahahu ni kwamba mamlaka hizi zinaifanya kazi yao vizuri kwa kudhibiti kiwango cha caffeine na viambata vingine vilivyo katika bidhaa hizi ndani ya chupa moja haviko katika wingi unaoweza kudhuru mwili. tatizo ni kwa watumiaji pale unapoelekezwa usizidi kiwango fulani ukazidisha.
 *AFYA YAKO NI* *JUKUMU LAKO.*

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UMUHIMU WA KUFUATA MAELEKEZO UNAPOTUMIA ENERGY DRINKS
UMUHIMU WA KUFUATA MAELEKEZO UNAPOTUMIA ENERGY DRINKS
https://1.bp.blogspot.com/-vR_tZOKljxk/XXquDERNmiI/AAAAAAAACzU/ntyrf7F_Hskw20-J19mxoLxzVoFs2P_UQCLcBGAsYHQ/s320/energy%2Bdrink.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-vR_tZOKljxk/XXquDERNmiI/AAAAAAAACzU/ntyrf7F_Hskw20-J19mxoLxzVoFs2P_UQCLcBGAsYHQ/s72-c/energy%2Bdrink.jpeg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/umuhimu-wa-kufuata-maelekezo-unapotumia.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/umuhimu-wa-kufuata-maelekezo-unapotumia.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content