UGONJWA WA KISONONO - GONORRHEA

Ugonjwa wa Kisonono (Gonorrhoea) ni ugonjwa unaoshambulia watu wengi, wanaume kwa wanawake. Ni ugonjwa unaotibika ingawa kwa miaka ya karibuni, wadudu wa ugonjwa huu wameonyesha kuanza kutosikia tiba zinazotolewa. Kisonono
kisipotibiwa kikamilifu, huweza kuleta madhara ya kudumu kwenye mwili wa mgonjwa na kumfanya aweze kuambukizwa au kuambukiza UKIMWI kwa urahisi. Katika ukurasa huu tutaona chanzo cha ugonjwa huu, dalili zake na mwisho kinga na tiba inayoweza kutolewa kwa ugonjwa huu. 

Chanzo Cha Kisonono (Gonorrhoea).

Kisonono ni ugonjwa unaoambukiza kwa ngono – sexually transmitted infection (STI) – na unasababishwa na bakteria
aitwaye Neisseria gonorrhoeae au gonococcus. Bakteria huyu hupenda kuzaliana kwenye maeneo ya joto, yenye unyevunyevu yakiwemo maeneo ya shingo ya uzazi (cervix), nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na mrija wa kutolea mkojo nje (urethra). Bakteria hawa pia huweza kuzaliana kwenye mdomo, mkundu na mara chache kwenye koo na macho.
Kimsingi bakteria hawa hupatikana kwa wingi katika shahawa na usaha unaotoka katika uume wa mwanamme mgonjwa na katika majimaji ya ukeni. Bakteria hawa huambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa njia zifuatazo:
. Ngono zembe kupitia uke, mdomo au mkundu. Mwanamme anaweza kumwambukiza gono mwanamke hata kama hakutoa shahawa (manii) wakati wa kufanya tendo la ndoa
. Kuchangia vifaa vya kujistarehesha ambavyo havikuoshwa au kufunikwa na kondomu, kama vibrators na vimwanasesere
vya aina nyingine.
Mama mjamzito mwenye maambukizi anaweza kumwambukiza mtoto anayezaliwa na endapo mtoto huyo hatapewa tiba, anaweza
kupata upofu wa kudumu. Hivyo, mama mjamzito mwenye maambukizi anatakiwa apewe tiba kabla ya kujifungua.
Bakteria wa kisonono hawaambukizi kwa kubusiana, kushikana mikono, kuchangia bafu au taulo, mabwawa ya kuogelea, vyoo, kuchangia vikombe na vyombo ya kulia kwa sababu wadudu hawa wa kisonono hawana uwezo wa kuishi kwa muda mrefu nje ya mwili wa binadamu.

Dali Za Kisonono

Sio watu wote wenye kisonono wataona dalili za ugonjwa huu. Pale ambapo mgonjwa ataona dalili, zitaonekana katika siku kama 10 baada ya kupata maambukizi ingawa inaweza ikachukua hadi siku 30. Dalili atakazoziona mwanamme zinaweza kuwa tofauti kidogo na zile atakazoziona mwanamke.

Dalili Za Kisonono Kwa Mwanamme

. Kutokwa na uchafu uumeni wenye rangi nyeupe, njano au kijani unaofanana na usaha
. Maumivu kwenye mapumbu
. Maumivu wakati wa haja ndogo
. Kutokwa na uchafu kwenye mkundu, kuwashwa, kutokwa damu wakati wa haja kubwa
. Koo kukauka, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe shingoni
. Maumivu kwenye macho, macho kutopenda mwanga mwingi na kutokwa uchafu machoni unafanana na usaha
. Maumivu na kuvimba kwenye sehemu za maungio ya mifupa

Dalili Za Kisonono Kwa Mwanamke

. Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
. Homa
. Kutokwa uchafu ukeni wenye rangi ya njano au kijani
. Kuvimba eneo la uke
. Kutokwa damu katikati ya siku za mwezi
. Kutokwa damu baada ya kufanya tendo la ndoa
. Kutapika, maumivu ya tumbo na maumivu ya nyonga
. Maumivu wakati wa haja ndogo na kupata haja ndogo mara nyingi
. Kutoa uchafu kwenye mkundu, kuwashwa, maumivu au kutoa damu wakati wa haja kubwa
. Kukauka koo, kuwashwa, kumeza kwa shida au uvimbe kooni
. Maumivu kwenye macho, kutopenda mwanga mkali na/au kutoa uchafu kwenye macho unaofanana na usaha
. Kuvimba na joto kwenye maungio ya mifupa

Madhara Ya Kisonono

Kisonono ambayo haikutibiwa inaweza kuleta madhara makubwa na ya kudumu kwa jinsia zote.
Kwa wanawake, kisonono ambayo haikutibiwa inaweza kusababisha – pelvic inflammatory disease (PID) – ambayo inaweza kuharibu mirija ya uzazi na mara nyingine kusababisha ugumba. Kisonono ambayo haikutibiwa inaweza pia kusababisha mimba kutungwa nje ya nyumba ya uzazi (ectopic pregnancy), hali ambayo inaweza kumhatarishia mwanamke maisha yake.

Kisonono kinaweza kumsababishia mwanamke kuzaa njiti (mtoto kuzaliwa kabla ya siku) au mimba kuharibika. Mwanamke mwenye kisonono anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa uzazi na kukisababishia kichanga upofu wa kudumu, maambukizi kwenye maungio ya mifupa au maambukizi kwenye damu.
Mwanamme ambaye ana kisonono isiyotibiwa anaweza kupata maumivu makali kwenye mapumbu kutokana na ugonjwa uitwao
epididymo- orchitis na kumsababishia ugumba. Kisonono ambayo haikupewa tiba ya kutosha inaweza kumletea madhara kwenye tezi dume (prostate) na anaweza kupata makovu ndani ya mrija wa kutolea mkojo nje (urethra) na kufanya mkojo utoke kwa shida.
Kisonono huweza kusambaa hadi kwenye mifupa na damu hali ambayo ni hatari kwa maisha. Mtu mwenye gono anaweza
kuambukizwa UKIMWI kwa urahisi zaidi.

Tiba Ya Kisonono

Endapo vipimo vimeonyesha kuwa una kisonono, wewe na mwenzi wako wote mnatakiwa kutibiwa kwa kutumia antibiotics na kuacha kujihusisha na masula ya mapenzi hadi hapo tiba itakapokwisha. Baada ya kumaiza tiba, inashauriwa kujipa mapumziko ya angalau miezi 3 kuhakikisha kuwa maabukizi yote yamekwisha.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UGONJWA WA KISONONO - GONORRHEA
UGONJWA WA KISONONO - GONORRHEA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/ugonjwa-wa-kisonono-gonorrhea.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/ugonjwa-wa-kisonono-gonorrhea.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content