UCHAWI WA MAMA

SIMULIZI UCHAWI WA MAMA.

AUTHOR WHATSAPP 0655585220
UCHAWI WA MAMA

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 1

"Dada amka tusali amka dada"
"Nina using zipo mdogo wangu"
"lakin dada sio vizuri kulala bila kusali"
"mdogo wangu nimechoka kwani kutokusali siku moja tutahathirika na nini,we tulale bwana"
"sawa dada ila sio vizuri"
"we lala bwana"
"Caro kwani mama na baba wamesha lala?"
"Ndio dada"
"sawa tulale"
"sawa"
........**...............**...............
usiniuwe,usiniuwe mama usiniuwe.......
........lazima nikuuwe mwanangu napenda sana damu,hahahahahahahahah.
Nilishtuka kutoka kwenye ndoto hiyo ya maajabu huku jasho likiwa limenitanda mwili mzima,kutokana na uoga niliyo kuwa nayo juu ya ndoto ile na kuhaidi kuwa nitamueleza mama juu ya ndoto ile iliyo kuwa ikimuhusu yeye,nilitazama pembeni yangu tayari mdogo wangu Caro aliye kuwa akinisihi tusali kabla ya kulala tayari alikuwa katika usingizi mzito huku akiendelea kutoa sauti mithili ya mtu anaye chunga mifugo yake.
"Caro,caro,caro.."
"Abee dada"
"Amka mdogo wangu"
"kuna nini dada????"
"we amka"
mdogo wangu alimka kisha akaanza kupekecha macho yake ili apate kuona vizuri,kisha akanitupia swali?
"Dada kuna nini alafu ujui mda umeenda tunatakiwa kulala"
"Caro mdogo wangu nimeota ndoto mbaya kuhusu mama tena anataka kuniuwa"
"kukuuwa?"
"Ndio"
"mama yetu huyu??"
"si ndio mdogo wangu mbona una maswali mengi"
"dada nadya heli ungekuwa umeota ndoto kuhusu hata baba au hata mpenzi wako ningekusikiliza lakini kuhusu mama hiyo sio ndoto tena maana vyote ulivyo viota ni vya uongo"
"Caro mdogo wangu niamini"
Mdogo wangu caro alivuta shuka bila ya kuniongelesha kitu chochote,nikiwa bado ni mwenye hofu kubwa na kushindwa kupata usingizi kabisa.
Nikiwa nimeuwegemea mto wangu vyema huku kidore changu cha mwisho katika mkono wa kulia kikiwa mdomoni pia macho yangu yakiendelea kutazama juu ya paa la nyumba yetu kwa lengo la kufikiria ndoto ile,hivi itawezekanaje mimi kumuotea mama yangu mzazi tena kwa mabaya haiwezekana lazima nifanye uchunguzi yes.
Baada ya kuwa nimesha pata jibu nini cha kufanya nilivuta shuka kama kawaida ili niweze kupata usingizi.
..........***...........****
Mwanangu nadya namuuwa baba yako,atakaye fuata ni mdogo wako caro pia wewe utakuwa wa mwisho,hahahahahaha.
Nilishtuka kutoka katika ndoto ile iliyo kuwa ya pili kwa siku moja,tena ndoto mbaya heli ya kwanza haiwezekana hata kusahaulika katika siku zote.
Nilivuta shuka la mdogo wangu caro kwa lengo kumuamsha,
"dada mbona unapenda kunionea hivyo????"
"sio nakuonea mdogo wangu amka kumekucha"
"amna bhana niache nilale nadya"
"powa"
Nilishuka kutoka kitandani kwangu huku nikimuacha mdogo wangu caro akiendelea kuuchapa usingizi,kichwani kwangu nilitawaliwa na wazo kuu moja tena kuhusu ndoto mbaya nilizo ziota juu ya mama yangu.
"Au itakuwa mama ni mchawi nini,ila sio kweli kwa sababu yeye ni mtakatifu siku zote sikuwai kumuona anajihusisha na uchawi itakueje nimuote vibaya,izo ni ndoto tu hazina madhara"
Nilipiga hatua zangu za kuelea mpaka mahali mlango ulipo,kisha nikaufungua,nilikaribishwa na mwanga hafifu wa jua,nilielekea mpaka kwenye chumba cha mama kisha nikagonga,
"Nani?"
"mama ni mimi mwanao nadya,shikamoo?"
"marahaba,asubuh yote hii kuna nini,au unataka ukorofishane na baba yako??"
"alafu mama umenikumbusha hivi,baba amelala???"
"Ndio mwanangu"
"shikamoo baba??"
"mbona haongei???"
"hata mimi nashangaa namuona kajikunyata hata haongei"
"ebu mama fungua mlango"
Baada ya mda mchache mama alifungua kisha akapiga hatua za kuelekea kitandani kwake,pia na mimi nilifanya hivyo hivyo kama mama,nikiwa tayari niko ndani ya chumba cha mama ghafla nilimkuta baba kwenye kona ya chumba hicho,huku akiwa anatokwa na udenda mithili ya dondocha,jambo liliyo nifanya nipige kelele,
"caro,baba anakufa caro......"
"mama kamgeuza dodocha"
nilivyo maliza kuongea hivyo baba alipotea katika eneo lile huku mama akiendelea kunikazia macho wakati akiwa pale pale kitandani,
"mwanangu nadya baba yako kaisha fariki,mimi ndo nimemuuwa mwili wake uko hapa kitandani ule uliyo kuwa unauona ulikua mzimu wake tu"

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA...........
nilivyo maliza kuongea hivyo baba alipotea katika eneo lile huku mama akiendelea kunikazia macho wakati akiwa pale pale kitandani,
"mwanangu nadya baba yako kaisha fariki,mimi ndo nimemuuwa mwili wake uko hapa kitandani ule uliyo kuwa unauona ulikua mzimu wake tu"
je nini kitaendelea........
ENDELEA NAYO..........
"Mama kwani nini unamuuwa baba?amekukosea nini eeh si nakuuliza si nakuuliza"
niliongea kwa uchungu na hasira huku nikiendelea kumtazama mama aliyo onekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo.
"mwanangu nadya hicho kiherehere chako ntakuondoa duniani mimi we nichefua,nakupa onyo la mwisho kaa kimya"
"sikai mama siwezi kaka kimya kwa kifo cha baba yangu hata siwezi,niuwe na mimi niuwe mama"
mama tayari alikua kaisha pandwa na hasira bila kuniongeresha kitu chochote kile,aliinua godoro kisha akachuku kikopo kidogo cha mafuta kisha akafungua kulikuemo na ungaunga mweusi kabla ajaendelea akasema,
"mwanangu itabidi uwe mlinzi wa chumba changu,hata panya wadogo wadogo ufanye juhudi nisiwaone kabisa"
nilimuuliza mama kwa mshangao huku nikifuta machozi,
"mama unamaanisha nini??"
"mwanangu nadya nakufanya dondocha maana umenishida. siku nikihitaji kukurudisha katika ubinadamu wa kawaida nitakurudisha, kwa sasa utakuwa unakaa humu amna ambaye ataweza kukuona tofauti na mimi pia hautaweza kuongea kitu chochote, mimi tu ndo nina uwezo wa kuongea na wewe"
Baada ya kuwa mama amemaliza kuniambia hivyo,alitoa ungaunga kwenye kijikopo kile,kisha akanipulizia husoni,
"mama nakufa nakufa,caro nakufa....caro nakufa...baba nakufa...nakufa...."
Nilitamka maneno hayo mpaka nikajikuta nabadilika sijitambui,nilishindwa hata kusimama wala kuongea nilichokuwa nakijua ni kuwa mama ni mchawi,cha ajabu panya alikatisha katika mguu wa mama,nilinyoosha mkono wangu kwa hasira kisha nikamkamata na kuanza kumtafuna.
Jambo liliyomfanya mama aachie kicheko cha dharau
"hahahahahaha,itakubidi mwanangu uzoee hayo maisha,sasa mi natoka kwaheri"
mama alikuwa anapenda kuongea kwa vitendo hivyo baada ya kumaliza kuongea hivyo alifanya kama alivyo sema.
********
"Hivi huyu mama nadya anafanya ujinga gani huu,anacho takiwa kutambua ni kuwa mimi sijamuozesha na mwanangu aende kumuuwa,hamnaga ndoa ya hivyo ataniulieje mwanangu amemkosea nini???,lazima nilipize kisasi mizimu ya baba na mababu ahsanteni kwa kunipa taarifa hizo mizimu nawashukuru sana mizimu"
*********
"boss mbona leo nadya ajaja kazini??"
"sijui labda atakuwa anaumwa,mnataarifa yoyote kuhusi yeye??"
"boss nadya ndo secretary na uchapakazi wake unaujua anawakalibisha wageni kutoka nje ya nchi kuja katika kampuni yetu kwa heshimu ya hali juu itakueje hauna taarifa za mtu kama huyo??"
"jack mpigie nadya ili upate kujua kwa nini hajaja kazini??"
"sawa"
baada ya mda mchache jack ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya VT ya uchapishaji wa vitabu aliamua kumpigia nadya kisha simu ikaanza kuita,
"Hallow nandya vipi?"
"nadya hayupo amatoka nje me mdogo wake naitwa caro"
"mpe basi simu"
"haya"
Caro aliamka na kumpelekea simu nadya bila kujua yaliyo mkuta nadya,wakati akiwa amesha toka nje alikutana na mama yake,
"shikamoo mama?"
"marahaba"
"nadya yuko wapi kuna simu yake inayo toka ofisini"
"lete niongee naye"
"lakini mama nadya yuko wapi ni simu ya muhimu wala haikuhusu wewe kama kuongea nao mi nisha ongea nao.
*******
Nikiwa chumbani kwa mama niliendelea kusikia majibizano baina ya caro na mama hapo hapo ndipo nilipo kumbuka caro alivyo kuwa akinisihi tusali na mimi nikakumbuka kumbe kuna uwezekano mkubwa wa kuomba na kumludia mungu,nilifumba macho huku nikipiga magoti kwa majozi makuu na ya hali ya juu hili mungu hawezi kuniokoa katika kifungu kile cha kichawi,
"mungu najua nilikukosea,mungu najua mi nimkosefu mda wote ila wanasema mungu hamtupi mja wake nadhani hata mimi hivyo hivyo huwezi nitupa,naweka imani yangu yote kwako naomba uniokoe katika adhabu hii katika kifungu hichi cha dhabi,ushetani,uchawi na nguvu za giza,mungu nakutegemea wewe maana wewe ndo msaada wangu katika maisha yangu AMEN"
Nikiwa nimemaliza maombi ghafla.

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 3

ILIPOISHIA...............
"mungu najua nilikukosea,mungu najua mi nimkosefu mda wote ila wanasema mungu hamtupi mja wake nadhani hata mimi hivyo hivyo huwezi nitupa,naweka imani yangu yote kwako naomba uniokoe katika adhabu hii katika kifungu hichi cha dhabi,ushetani,uchawi na nguvu za giza,mungu nakutegemea wewe maana wewe ndo msaada wangu katika maisha yangu AMEN"
Nikiwa nimemaliza maombi ghafla.........
.............
JE NINI KITAENDELEA .......................
ENDELEA NAYO......................

Nilianza kujisikia mwepesi kisha nikasimama kama kawaida,nakuelekea nje,nikiwa tayari niko nje ya chumba cha mama,nilimkuta mama akiwa anaanika nguo huku mdogo wangu caro akiwa ameshika kiuno chake huku akiendelea kuangaza wapi nilipo aniletee simu,
"we caro nakuambia unipe hiyo simu hutaki ganda nayo sasa tuone kama utampata huyo nadya wako"
mama alimwambia caro,huku akiendelea kuanika nguo,kabla mama hajaniona caro aliniita kwa furaha huku moyoni mwangu nikiwa tayari nimesha jenga chuki juu ya mama yangu mzazi,jambo liliyo fanya nikae kimya mda wote huku nikiendelea kufikiria nifanye nini cha kumuuwa apotee duniani.
"dada nadya,ulikuwa wapi simu yako kutoka ofisini ilikuwa inaita"
caro aliniongeresha huku akininyooshea mkono kwa ajiri ya kunikabidhi simu,wakati akiwa anaendelea na zoezi lile
ghafla mama alianza kutetemeka huku akigeuka kwa kunishangaa na kushindwa kuhamini kuwa ni mimi au mzimu wangu.
Mama alitupa ndoo iliyo kuwa na baadhi ya nguo zilizo kuwa tayari kwa ajiri ya kuanikwa kisha akaingia ndani bila ya kumuongelesha mtu yoyote,kitendo hicho kili mshangaza caro kisha akaniuliza,
"dada kuna nini kati yako na mama alafu jana niliota ndoto mama amekufanya dondocha,baada ya hapo mungu akakusaidia ukatoka kwenye huo udondocha,kisha mama akafanya mpango akakuuwa,ndoto mbaya dada nilitaka nikuambia asubuh nikawa na usingizi,nadhani hii ilitokana na kutokusali kwetu"
"caro unasemaje mimi nikafa mimi,mimi amna sio kweli"
nilianza kuongea maneno mithili ya mtu aliye anza kuchanganyikiwa kitendo kile kilimfanya caro aanze kutoa machozi kisha akaanza kuita,
"baba,baba amka dada nadya amechanganyikiw
a,mama njoo mama njoo njooo mama nadya dada yangu dada yangu"
caro aliendelea kupiga kelele pale alivyo ona nadya anaanza kutoa mapovu mdomoni baada ya mama yake kuingia ndani na kuanza kumchezea kwa nia ya kummaliza,baaada ya kuwa caro ameona hali ile imezidi aliingia chumbani mwa mama yake kwa fujo na kumkuta mama yake akiwa uchi wa mnyama huku akiwa amewasha mshumaa huku akiendelea kuuzunguka, caro akiwa amesimama na kushangaa alianza kusikia maneno aliyo kuwa anazungumza mama yake kipindi alicho kuwa anazunguka mchumaa,
"nadya kufa nadya kufa,kufa nataka nyama yako njoo njooo kuzima"
kitendo kile kilimfanya caro amuulize mama yake huku akihema kwa shida na kushindwa kuhamini kama mama yake ni mchawi tena asiye kuwa na huruma,
"ma..........ma..........kumbe...wewe ni mchawi eti mama unataka kumuuwa nadya kakukosea nini we mama si unijibu ntakuuwa na mimi,baba njoo tumuuwe mama anataka kumuuwa nandya njoooo"
caro alianza kuongea kwa ujasiri mkubwa bila ya kujua kuwa baba yake kaisha fariki,mama yake aliendelea kuwanga kama kawaida kana kwamba hakusikia mwanae caro akiongea jambo hilo,lilimfanya caro kupiga magoti huku akilia kwa uchungu,na kumuomba mungu amuepushe na dhabi atakayo itenda mda sio mrefu,caro aliomba kimya kimya bila mtu kusikia,
"mungu naomba unisamee kwa nacho enda kukifanya"
Baada ya kuwa caro ameomba kwa mda mfupi alitoka nje na kuelekea jikoni kufata kisu,alipita nje na kumkuta dada yake nadya bado akiendelea kushika tumbo huku akilia,
"Caro,mama ni mchawi amemuuwa baba,na wewe atakuuwa"
taarifa ile iliyo toka kwa nadya ilimfikia caro na kumfanya asimame kwa mshangao kisha akadondoka chini na kupoteza fahamu.
*******
"mkuu naomba ruhusa niende duniani kuwaokoa wanangu angalia mama yao alivyo mkatili kitendo cha kuambiwa kuwa endapo akimaliza familia yake yote atapandishwa cheo hapo ndipo walipo kosea maana amekuwa mkatili sana ameniuwa mimi,na usipo nipa ruhusa pia hivyo hivyo atawauwa wanangu naomba ruhusu mkuu sitaki watoto wangu waje hapa nilipo najua mateso ya kuzimu ni makali ni makali sana ni vipi wanangu watoke kula nyama za ng'ombe huko duniani waje huku waanze kula nyama za binadamu na damu ya binadamu na wakati njia ya kuwahepusha kuja huku ipo,nakuomba mkuu nadya wangu atakufa,caro wangu atakufa nakuomba"
"sawa nimekupa ruhusa ila unatakiwa uchague kati ya familia yako nani aje huku kuziba nafasi yako"
"unamaana gani mkuu????"
"we si unaenda dunia unatakiwa uchague mtu kwenye familia yako ambaye atakuja huku ili huweze kuwasaidia wanao,na ukisema aje mke wako haiwezekani mke wangu ananguvu sana na yeye ndiye anaye.waleta huku sa uchague kati ya nadya na caro nani aje huku ili wewe huweze kupata nafasi ya kwenda huko duniani kupambana na mama yao kisha ukirudi kuzimu na utakaye kuwa umemchagua na yeye atarudi duniani"

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 4

ILIPOISHIA...............
"we si unaenda dunia unatakiwa uchague mtu kwenye familia yako ambaye atakuja huku ili huweze kuwasaidia wanao,na ukisema aje mke wako haiwezekani mke wangu ananguvu sana na yeye ndiye anaye.waleta huku sa uchague kati ya nadya na caro nani aje huku ili wewe huweze kupata nafasi ya kwenda huko duniani kupambana na mama yao kisha ukirudi kuzimu na utakaye kuwa umemchagua na yeye atarudi duniani"
je nini kitaendelea...........
ENDELEA NAYO.........
*********
"Mungu nisaidia mimi nadya,ona navyo teseka mungu niangalie kwa jicho la tatu mungu,nipo chini yako mungu naomba mama yangu ashindwe kwa chochote anachokifanya juu yangu,mungu mchome moto utakao enda kuangamiza nguvu zake za giza,nguvu za kichawi,na nguvu zote za kishetani AMINA"
Nilifanya ibada ya mda mfupi huku bado nikiwa pale chini,ghafla sikuhamini baada ya kujisikia naanza kupata nguvu mpya na kunifanya niweze kusimama upya,niligeuka upande wa pili kwa masikitiko makubwa,nilitahamaki na kushangaa baada ya kumkuta mdogo wangu caro bado akiwa pale pale chini huku akiwa amepoteza fahamu.
Nilipiga hatua chache za haraka haraka huku nwilini mwangu nikijisikia ni mwenye nguvu za kufanya chochote kile,nilifanikiwa kufika mpaka mahali ambapo mdogo amepoteza fahamu kisha nikaanza kumuamsha kwa lengo la kurudisha fahamu zake,
"caro,caro,caro,caro mdogo amka amka caro,mimi ni mzima angalia caro mimi dada yako nimesimama amka basi"
cha ajabu baada ya kuwa nimejitambulisha kama dada yake caro,caro aliweza kunisikia vyema na kuitikia wito wangu kisha akaanza kuamka kana kwamba alikua kwenye usingizi mzito na wa maajabu pia,
"dada nadya nipo wapi na hapa nafanya nini?"
"mdogo wangu caro,ulikuwa umepoteza fahamu baada ya kuwa nimekupa taarifa za msiba wa baba......."
"Dada nadya mama yuko wapi??"
Caro alinitupia swali lile liliyo nifanya nikimbie haraka kuelekea chumbani kwa mama huku nikimuacha caro akiwa bado ni mtu aliye shindwa kurudisha kumbu kumbu za tukio liliyo pita kabla ajapoteza fahamu.
Nikiwa tayari nimefanikiwa kufika chumbani kwa mama ghafla mwili ulianza kutetemeka huku kijasho chembamba kikiendelea kunitoka kwa nilicho kiona.
********
"mkuu sitakubali mwanangu yoyote aje huku kuzimu apate mateso kama nayo yapata hivi sasa na sidhani kama kuna mwanangu yoyote anaweza kuishi maisha ya huku hata kidogo,tafadhali mkuu naomba sharti jingine tafadhali tofauti na hilo la kuchagua mwanangu kuja huku"
"bwana thomas sina kingine cha kukusaidia kuhusu wanao akiwa ni caro na nadya.kama umeshindwa kufanya shart ilo basi,maana nadhani ukifanya hivyo itakuwa njia moja wapo ya kuwalaghai mizimu maana wana idadi ya kila anaye jiunga humu ila hawana idadi kila anaye jiondoa humu maana wanacho jua wao ni vigumu kutoroka kuzimu maana tayari we dunia ni mfu na ukienda unaishi kama nafsi,iyo ndo sababu kuu inayo wafanya wawe na idadi ya wanao jiunga na pia kinacho fanya ujiunge kuzimu ni dhabi zako mimi sikukuleta bwana thomas ulitenda dhabi mwenyewe duniani yamekukuta yaliyo kukutana na mke wako tunamsubili kwa hamu kama wewe tulivyo kuwa tunakusubili"
"najua mkuu yote ni makosa yangu ila huu sio mda husika wa kujilaumu ila nachotaka niwasaidie wanangu wasiweze kuja huku kama mimi, huku kuna shida wataweza kulaumu uzao wangu watamuhuzi mungu kwa kusema heli nisinge waleta dunia na hii itakuwa laana ya uzao wangu ujao utakao toka kwa wanangu walio bakia"
"basi sawa nimekuelewa bwana thomas ila shart ni moja nalo kupa huko duniani,uende ukawasaidie wanao ila kitu kimoja,mama yao ana nguvu sana na anao uwezo wa kukurudisha huku naomba ufanye kitu kimoja jitahidi asingundue kuwa umerudi duniani kama mzimu hakikisha hilo,safari njema".
"ahsante sana mkuu naenda kuwasaidia wanangu mkuu kisha nitarejea"
"sawa safari njema.
********
Baba yake thomas abaye ni babu yake nadya aliaanza kujiaandaa kwa safari ya kuelekea mjini kwa ajiri ya kumuuwa mama nadya kwa sababu ya kumuuwa mwanae bila kosa,kabla ajaanza safari alianza kuongea nwenyewe Mithili ya kichaa,
"nafunga safari ngoja nieleke mjini kupambana na uyo mama nadya lazima nimuuwe haiwezekani anamuuwa mwanangu thomas,amemkosea nini,amemfanyia nini yani amevunja mila za kwetu kabisa anashindwa kuishi na mwanangu kwa miaka tuliyo kubaliana kuwa atadumu kwenye ndoa,sasa basi safari yangu inafikia kwenye nyumba ya mwanangu sa ngoja tuone kama ataweza uganga wangu"
"mama thomas njoo mke wangu unisindikize naelekea mjini kwa mwanangu kumuenzi maana hata msibani hatujaalikwa,mwili wa mwanetu hatujauona"
"unasemaje baba thomas,thomas wangu amekufa???"
"Ndio"
"we umejuaje???!"
"mizimu imeniambia we unajua hapa kijijini asilimia kubwa taarifa nyingi tunapokea kutoka kwenye mizimu vita ya kikabila kila kitu,mda wa njaa,kiangazi mda gani kitakuepo,we si unajua kila kitu ni mizimu"
"mama weeee weeeeee mwanagu nwanangu thomas uwiiiiiiii mme wangu mbona hukuniambia toka zamani.........?"
""mke wangu naomba ukae kimya ndo nilikuwa sitaki kukupa taarifa hizi utakorofisha mizimu"
mama thomas alimtupia swali mumewe huku akiendelea kufuta machozi
"nani amemuuwa mme wangu???"
"mke wake"
"eti nani mme wangu leo nauwa mtu twende huko huko mjini kitaelewa lazima ale nyama ya mwanangu haiwezekani"

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 5

ILIPOISHIA..................
mama thomas alimtupia swali mumewe huku akiendelea kufuta machozi
"nani amemuuwa mme wangu???"
"mke wake"
"eti nani mme wangu leo nauwa mtu twende huko huko mjini kitaelewa lazima ale nyama ya mwanangu haiwezekani"
ENDELEA NAYO................
**
Niliendelea kumshangaa mama na kutokuamini kama ni yeye au ni mauza uza yanayo nitokea,baada ya kumshuhudia mama yangu mzazi akiwa ame badilika na kuwa paka mkubwa mweusi huku akiwa anaunguruma mithili ya nguruwe anaye taka kuchinjwa.
Nikiwa bado nipo katika chumba kile, paka yule mkubwa niliye dhania kuwa ni mama alianza kunena,
"mwanangu nadya umejifanya mjanja unapiga ibada za kutaka kunimaliza mimi sasa nakuambia naanza kuwa mkatili inaonekana nilikuwa nawaogopesha ila sasa hivi nataka niwape shida mpaka muone ulimwengu umekuwa mchungu"
"hivi mama unaweza kupambana na mungu wewe???,alafu kubadilika kwako hakunitishi hata kidogo, mama nina kuchukia milele"
kutokana na kauli zile za kijasiri nilizo zitoa huku nikiwa nimesimama mbele ya paka yule mkubwa ambaye ni mama,kitendo kile kilimfanya paka yule kubadilika na kuwa simba kisha akaanza kupiga hatua za kuja maeneo nilipo kwa lengo la kunishambulia,nilikuwa sina jinsi nilicho kifanya ni kusimama na kusubili kifo,ghafla nikiwa kwenye mlango wa chumba cha mama huku nikiwa nimekinga mikono yangu usoni kwa njia ya kuzuhia simba yule ambaye ni mama asiweze kunikwangua usoni na kunizulu,alikuja caro huku akiwa ameshikilia kisu na kumchoma simba yule kisha akadondoka chini,
"caro umefanya nini???"
"Dada nilikuwa hapo nje na nilikuwa nasikia kila kitu anacho kiongea mama,wakati anataka kukumaliza nikaona sio vyema kukuacha upoteze maisha wakati mimi nipo nikaona bora nikusaidie"
"du,utakuwa umemuuwa mama,????"
"Dada acha afe, mpaka sasa umeniambia baba ameshakufa ila sijui mwili wake huko wapi,naskia tu amekufa pili mama sikuizi amekuwa mkatili sijui ni kwa nini??"
Wakati nikiwa naendelea na mazungumzo baina yangu na caro simba yule alibadilika na kuwa binadamu wa kawaida na alikuwa si mwingine bali mama, kisha akasimama na kujinyoosha,wak
ati mama akiwa tayari kaisha amka katika eneo lile alilokuwa ameanguka alipita katikati yangu na caro bila kutuongelesha kitu chochote kisha akaachia kicheko cha dharau na maneno ya kejeri,
"hahahahahahah,lazima mfe kama mme wangu alivyo kufa hahaha,ngoja nikitoka zambia mtanikoma"
mdogo wangu caro alivyo jaribu kutaka kumuongelesha mama nilimzuia maana nilijua angeamsha fujo nyingine ambayo haijawai kutokea.
tuliendelea na shughuli zetu kama kawaida bila ya kuongea na mama jambo lolote huku na mama akiendelea na shughuli zake kama kawaida.
Lakini cha ajabu mama aliendelea kutufanyia wema wa mda mfupi ambao tuliushangaa,al
ishawai kusema hawezi kupika ingari anao vijana wakubwa kama sisi hivyo ,kutokana na kauli ile tulikuwa tunapika hata kufua nguo vyote tulivifanya lakini cha ajabu,kila kitu alikifanya mama na kutushangaza hata sisi.
wakati ukiwa umesha fika mda ambao tulihisi kwetu sisi ndio mda muafaka wa kuweza kula chakula cha usiku tuliweza kufanya hivyo.
***
wakati nadya na caro wakiendelea kupata chakula cha usiku kilicho pikwa na mama yao ambaye,alishindwa kuongea nao kuanzia asubuhi kutokana na tukio la kutisha la mda mfupi lililokuwa limetokea,mama yuke aliweza kupiga hatua zake kwa ajiri ya kuelekea katika chumba cha wanae na kuweka dawa chini ya godoro wanalo lalia wanae,baada ya kuwa amemaliza kuweka dawa katika godoro la wanawe aliondoka kwa kusema maneno,huku akiwa na furaha,
"safi sana lazima mfe wanangu sijui nani atawasaidia sijui kabisa,hahahahaah."
kipindi caro na nadya wakiwa wamemaliza kupata chakula cha usiku waliweza kupiga hatua za kuelekea katika chumba wanacho lala wao kwa ajiri ya kujipumzisha,walipiga hatua kadhaa kisha wakafika katika chumba chao,
"Dada nadya subili kwanza kumbuka kusali kabla ya kulala"
"ilo ni kweli caro mdogo wangu ila tusali nini sasa hapo we unaona mama yetu amekuwa mwema unasema mambo ya kusali,we tusali tunasali tujikinge na nani sasa????eehh lala bhana"
"we umeanza kuniuzi dada nadya we unajua madhara ya kutokusali,"
"basi caro umezidi kujifanya mlokore basi mimi silali kitandani na lala chini ,maana umesha nikela, sasa sitaki hata kulala na wewe"
"basi dada nadya kama hutaki kulala na mimi na mimi sitaki kulala na wewe naenda kulala sebleni"
"Nenda na mimi nalala chini maana umenikela"
Kitendo kile kiliwafanya kuepuka dawa iliyo kuwa imetegwa kitandani kwao kwa ajiri ya kuwamaliza.
****
asubuh na mapema nikiwa nimelala chini ya sakafu nilishtushwa na kofi kali kutoka kwa mama,
"we nadya tabia gani umeianza???"
"tabia gani mama???"
"nakuuliza swali na wewe unaniuliza tunashindana??ni kwa nini hukuweza kulala kwenye kitanda na kumfukuza mdogo wako caro alale sebleni??!"
"hama kweli we mama ndo mchawi sugu unanilazimisha mimi kulala kwenye kitanda kama sijapenda au umetega dawa nini??mbona umekaa kimya,sasa basi nitalala endapo nikisha fanya usafi"
"unasemaje??"
"hivyo ulivyo sikia mama ndiyo nimesema"
mama aliondoka kimya bila ya kuniongeresha jambo lolote lile,
"kumbe usingizi wa sakafuni ni mtamu hivi ngoja niende kazini mambo mengine baadaye"
Nikiwa pale sakafuni nilishtuka kwa kupa baada ya kusikia yowe iliyokuwa ikitoka kwa mdogo wangu caro,
"Dada nadya nakufa mama amenimwagia maji ya moto nakufa nakufa dada njoo nakufa,mama acha kuniongezea maji mengine utaniuwa dada wai nakufa"
****
wakati wazazi wa thomas amabaye ni babu yake nadya wakiwa wapo gest ya kituo cha basi kwa ajiri ya kusubili kukuche na kuanza safari rasmi ya kuelekea mahali alipokuepo nwanao mpendwa baba nadya ambaye alikuwa ni marehemu kutokana na kuuliwa na mke wake.
yalikuwa ni majira ya saa sita usiku huku babu nadya akiwa ameshindwa kupata usingizi huku akihisi kuwa hata kukucha kunachelewa kutokana na kuwa alikuwa na hamu ya kutaka kuanza vita na mke wa mtoto wake ambaye ni mama nadya,babu nadya akiwa ni mwenye mawazo tele huku akiwa amelala katika kituo cha kusafiria huku mke wake akiwa ameuchapa usingizi,ghafla ulitokea mzimu wa mwanae,
"Baba najua utaumia sana kutokana na kifo changu kilicho tokana na mwanamke yule katili uliye nilazimisha nimuoe,baba nalia kwa uchungu na masikitiko makubwa,wanangu wanapata shida watakufa baba,nenda pale kwa njia nzuri ili uwasaidie wanangu ukienda kwa vita na shali hutaweza kufanikiwa hata kidogo"
baada ya kuwa mzimu wa baba yake nadya umemtokea babu yake nadya nakumsihi kwa kumpa onyo kali juu ya anacho taka kukifanya,babu nadya alitoa chozi kisha akahaidi kutekeleza wakati babu yake nadya anataka kulala ili aweze kuliona jua la kesho kwa haraka alitokewa na kundi la wachawi watano katika chumba chake,kitendo kilicho fanya aogope sana kisha mkuu wa kile kikosi cha wachawi alianza kuongea,
"kama unataka kupona achana na mama nadya rudi kijijini la sivyo tutakuuwa"

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 6

ILIPOISHIA............
baada ya kuwa mzimu wa baba yake nadya umemtokea babu yake nadya nakumsihi kwa kumpa onyo kali juu ya anacho taka kukifanya,babu nadya alitoa chozi kisha akahaidi kutekeleza matakwa ya mwanae ambaye alikuwa ni marehemu,cha ajabu wakati babu yake nadya anataka kulala ili aweze kuliona jua la kesho kwa haraka alitokewa na kundi la wachawi watano katika chumba chake,kitendo kilicho fanya aogope sana kisha mkuu wa kile kikosi cha wachawi alianza kuongea,
"kama unataka kupona achana na mama nadya rudi kijijini la sivyo tutakuuwa"
je nini kitaendelea.................
ENDELEA NAYO...........
****
Baada ya kuwa nimesikia kelele kutoka kwa mdogo wangu caro niliweza kukimbia kutoka chumbani kwangu na kwenda sebleni kwenda kushuhudia kinacho endelea na kilicho fanya mdogo wangu kupiga kelele kama ile.
wakati nikiwa nakimbia kwa haraka na kwa fujo zaidi huku nikiwa na hasira juu ya mama,ghafla nilikutana na mama akiwa katika mlango wa sebleni huku akiwa amesimama na kunikazia macho,sikuweza kumuongelesha kitu chochote nilichokifanya ni kutafta upenyo katika mlango ule ambao ungenifanya mimi kupita sebleni na kumtazama mdogo wangu caro nini kilicho mkuta,lakini kilicho nichanganya zaidi na kunifanya nianze kuwa na wasiwasi juu ya mama ni kutokana na kuwa kipindi nilipo jaribu kupita alinizuhia na sikujua ni kwa nini alifanya hivyo,
"dada nadya nakufa dada yangu njoo unipelekee hospitalini"
ilisikika sauti kutoka sebleni ilikuwa inatoka kwa caro huku ikiashilikuwa kuwa alikuwa amekubwa na matatizo makubwa ambayo yange hitaji msaada wa haraka,
kitendo kile cha mama kuendelea kunizibia kila nilipokuwa najaribu kutafta upenyo wa kuweza kumuokoa mdogo wangu ambaye kufikia mda huo bado nilikuwa sijui amekubwa na nini!!!
kwa mara ya kwanza kabisa niliweza kumzaba kofi mama na kumfanya adondonke chini,hata mimi nilishangaa maana katika nafsi yangu sikuwa na uwezo hata kidogo ila nilijistukia nimempiga kofi mama tena kofi la kichawi liliyo fanya yeye kupoteza fahamu.
"mungu wangu,mdogo wangu caro umekumbwa na nini mbona mguu wako unaanza kutoa maji maji"
"Dada nalia kwa uchungu na masikitiko makubwa,mama alikuja subuh hapa na kuanza kunigombeza ni kwa nini ninaangalia Tv mpaka napitiliza nalala hapa je mgeni akija,nikamjibu kuwa nikuwa naangalia TV ila niliamua kulala hapa ,akaanza kusema tumeanza kumdharau ngoja atukomeshe ndio akaja na maji ya moto kisha akanimwagia mguuni"
"pole sana mdogo caro,leo wiki ya kwanza inakatika ni mauzauza humu ndani pili kazini sijaenda wiki nzima jambo liliyo fanya hali yangu ya kifedha kupungua sa cha msingi tutaishi na huyu mama yetu kibabe twende hospitalini mdogo wangu"
niliweza kumpeleka mdogo wangu mpaka hospitalini kisha akaanza matibabu rasmi.
nikiwa nasubili majibu kutoka kwa dokta, ness mmoja mnene aliweza kuniita
"samahan dada unaitwa na dokta"
niliweza kumfuata kwa nyuma mpaka kwenye chumba cha dokta
"karibu sana, we ndo ndugu wa mgonjwa huyu alioungua na maji??"
"ndio mimi!!!"
"ukoje naye au naweza kusema undugu wenu ukoje??"
"mtu na dada yake,mimi ndo dada yake"
"aha sawa je mnaishi na mama na baba yenu"
Daktari aliniuliza swali lile liliyo nifanya kukaa kimya kwa mda kadhaa
"mbona haunijibu??"
daktari aliongeresha kwa sauti ya juu iliyo nifanya nitoke kwenye mawazo
"dokta hatuna baba wala mama"
"aha sawa sasa, kutokana na maelezo ya vipimo baada ya kuwa nimefanya vipimo kwa mdogo wako,inatakiwa usaini ili, akatwe ule mguu kutokana na kuwa alimwagiwa maji yenye chumvi nyingi, hivyo yalifanya mguu wake upate majeraha makubwa kwa mda mfupi na kuaanza kuozesha baadhi ya sehemu katika maeneo ya mguu ule hasa kwenye ile joint yake"
"amna daktari haiwezekani mdogo wangu kukatwa mguu'haiwezekani daktari"
"kama unataka kuokoa maisha yake utasaini kwenye iyo karatasi,tuta kuruhusu ndani ya nusu saa ulifikilie hilo,baada ya nusu saa kama utakuwa ujatia saini hatutakuruhusu kutia saini maana utakuwa umesha chelewa"
****
wachawi wale waliendelea kubishana na babu yake na nadya huku wakiendelea kumpa vitisho vikali,kwamba asijaribu hata kidogo tena aondoe katika fikra zake,kuhusu swala zima la kutaka kumuangamiza mshirika mwenzao ambaye ni mama nadya,
"amna haitawezekana hata kidogo mimi kurudi kijijini haitawezekana kama mnaniuwa mniuwe"
"we mzee acha kuwa na kiburi cha kutaka kuwasaidia watoto eti kisa wewe ni babu yao na pia una nguvu za kiganga hapa utaumia utakufa tu na huweza kufanikiwa hata kidogo na kama unataka kifo nenda kwa hao watoto utakipata utakacho kipata"
kutokana kauli zile kutoka kwa wachawi wale,zilimfanya mzee yule kuonyesha kuwa anazo nguvu ambazo anao uwezo wa kupambana na mtu yoyote yule bila kujari ni mtu gani na anao uwezo gani.
mkuu wa wachawi alianza kutoa amri kwa wachawi wenzake kwa lungha isiyo fahamika,kisha wachawi bila kupoteza mda walimchukua bibi yake nadya bila babu yake nadya kugundua na kupotea naye kisha wakamuacha mkuu wao akiendelea kuongea na babu yake nadya ili asiweze kugundua kwa haraka,bila ya babu yake nadya kugundua kuwa mke wake ameshakuchukuliwa aliendelea kujitapa kwa mchawi yule,
"nasemaje sirudi kijijini mi sio mtoto wa kunitisha tisha"
"basi sawa we sio mtoto ila ukirudi kijijini ndio utampata mke wako huko maana tumesha anza kuwarudisha pole pole"
kutokana na kauli ile ya mkuu wa wachawi ilimfanya babu nadya kugeuka nyuma kwa lengo la kumuangalia mke wake kama yupo,alianza kupatwa na hasira pindi tu alipongudua mke wake hayupo ,wale wachawi wengine wamesha mchukuwa,kutokana na kitendo kile babu nadya alikasirika na kuingiza mkono wake mfukoni kisha akabadilika na kuwa fisi
"jambo lile lilimshangaza mkuu wa wachawi na kuanza vita mpya kabisa na babu nadya mzee mwenye nguvu za mizimu........
je nini kitaendelea.

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 7

ILIPOISHIA.........
"basi sawa we sio mtoto ila ukirudi kijijini ndio utampata mke wako huko maana tumesha anza kuwarudisha pole pole"
kutokana na kauli ile ya mkuu wa wachawi ilimfanya babu nadya kugeuka nyuma kwa lengo la kumuangalia mke wake kama yupo,alianza kupatwa na hasira pindi tu alipongudua mke wake hayupo ,wale wachawi wengine wamesha mchukuwa,kutokana na kitendo kile babu nadya alikasirika na kuingiza mkono wake mfukoni kisha akabadilika na kuwa fisi
"jambo lile lilimshangaza mkuu wa wachawi na kuanza vita mpya kabisa na babu nadya mzee mwenye nguvu za mizimu........
je nini kitaendelea...................
ENDELEA NAYO..............
*****
Niliweza kufanya maamuzi kutoka kwenye akili yangu,baada ya kuona mda unazidi kukatika bila ya kufikiria kitu choochote,machozi ya uchungu yaliendelea kunitoka na kunifanya wakati nikitaka kusaini najikuta natetemeka sana,jambo hili lilipelekea mda uzidi kwenda na kunifanya mimi nichukue maamuzi magumu ya ujasiri ili niokoe thamani ya mdogo wangu. bora aendelee kuishi huku akiwa mlemavu kuliko kupoteza vyote nakuweza kukumbwa na umauti,nilifanya maamuzi ya dakika moja kisha nikachukua karatasi kwa lengo la kusaini huku nikiwa mwenyewe katika kile chumba cha daktari,sikuwa na hofu kuhusu ni namna gani taarifa itamfikia daktari maana tayari alikwisha niambia baada ya nusu saa atakuja kuchukua majibu.
Niliivuta katarasi na kushikilia biki kwa ujasiri huku machozi yakiendelea kunitoka na kuidondokea ile karatasi,jambo hilo lilinifanya niumie lakini nilikuwa sina jinsi kwa wakati huo,nilianza kushika biki kwa nguvu zangu zote kisha nikatazama mahali palipo andikwa "SIGN...................."nika
jikaza kisha nikaanza kusaini katika ile deshi iliyo mbele ya neno SIGN,cha ajabu kila nilivyo jaribu kusaini nilikuwa nahisi mwili unakuwa mzito,ghafla alikuja nyuki niliyo shindwa kujua ametokea wapi!!!!! kisha akaning'ata kwenye kidore kilicho kuwa kimeshikilia biki,ghafla mkono wangu ulianza kuuma kitendo kilicho nifanya nipige yowe kali za maumivu zilizo changanyana na mkwaruzano wa sauti,kitendo kile kilinifanya niwe katika hali ya uchizi na kushangaa wapi nyuki anaweza kumuuma binadamu bila sababu ya msingi,nikiendelea kukumbuka hivyo basi nazidi kupiga yowe kali maana niligundua huo utakuwa uchawi wa mama na sio kitu kingine.
nilipelekwa kwenye chumba kilicho andikwa ACU chumba cha wagonjwa mahututi kisha nikaanza kufanyiwa uparesheni ya mkono wa lengo la kutoa kile kilicho ndani ya kidore changu kinachonifanya niumie,cha ajabu kabla hata madaktari hawajaanza kunifanyia uparesheni tayari nilikuwa nimesharudi katika hali yangu,kitendo hicho kiliwashangaza hata madaktari walio kuwa wamepangwa kunifanya oparesheni maana nilisikia wanasema tangia wazaliwe hawajai kuona kitu kama hicho,baada ya kuwa nimesha ruhusiwa niliweza kukaa katika bechi za kusubili wagonjwa niliangalia mdaa katika saa yangu ya mkononi,tayari ilikuwa imetimia saa 10:30 jion ,maana hata tayari mda wa kusaini umeisha,kitendo kilicho fanya nianze kushikwa na mawazo juu ya mdogo wangu kwa kushindwa kusaini kwani nimehatarisha maisha yake.
kama kawaida yake yule ness mnene akaja kuniita kwa ishara kwani hata yeye tayari alikuwa amesha anza kuniongopa kutokana na tukio la ghafla liliyokuwa limenitokea,niliweza kumfuata kwa nyuma nyuma mpaka pale alipo nionyesha kwa ishara mahali napo takiwa kuingia,nilifanya kama alivyo nielekeza.
nilishindwa kuamini macho yangu baada ya kumkuta mdogo wangu akiwa mzima tena wa afya,kisha akaniita huku akidondosha machozi
"Dada nadya Dada nadya"
niliweza kupiga hatua chache mpaka pale alipo kisha tukakumbatiana,
"mdogo wangu caro unaendeleaje???"
"Dada mimi ni mzima hata nashangaa mguu umepona ghafla tu hapa nasubili ruhusa kutoka kwa madaktari"
"pole sana mdogo wangu"
"ahsante dada nadya"
Tukiwa tunaendelea na mazungumzo yetu tulisikia sauti ya mtu ikizungumza huku ikwa inajirudia rudia (mwangwi) iliyo tufanya tukumbatiane kutokana na uoga tuliyo kuwa nao,
"wanangu wanangu mimi baba yenu baba yenu,nipo karibu yenu chochote mnacho ona kinaendelea ni msaada kutoka kwangu,wanangu mnapo enda nyumbani kueni na muwe na tahadhari kwa mama yenu kwani ni mtu mbaya sana,aliweza kuniuwa kisha akala nyama yangu akiwa na wachawi wenzake,mwanangu nadya mimi ndiye niliwafanya mbishane na mdogo wako ili msilale kitandani kwani mama yako alikuwa amewategea dawa kwa ajiri ya kuwauwa,pili wewe caro ulikuwa aumwi yalikuwa ni mauzauza ambayo yangefanya ukatwe mguu hivyo nikaamua kutuma nyuki ili aweze kumng'ata nadya ili ashindwe kusaini,sasa basi nawaombeni kueni makini mimi nipo jirani nyuma yenu popote mlipo,ila mfanye juu na chini mama yenu asingundue kama nawasaidia maana anao uwezo wa kunirudisha nilipo toka safari njema"
*****
mama nadya aliweza kusimama na kupata nafuu baada ya mfupi toka apoteze fahamu,kutokana na kitendo kile cha kupigwa kofi la kichawi na nadya kilimkera na akagundua hapa itakuwa anapambana na nguvu ya ziada inayo wasia nadya na caro hivyo akaamua kuwaita wachawi wenzake kwa ajiri ya kulizungumzia jambo hilo,mama nadya bila kupoteza mda aliingia chumbani mwake kisha akainama chini ya kitanda na kuchukua kibuyu kisha akaenda nacho sebleni.
mama nadya alianza kupuliza kibuyu kile huku akiendelea kutamka maneno aliyo yajua yeye mwenyewe,baada ya mda mchache walitua pale kundi kubwa la wachawi kisha wakaanza kucheza ngoma za asili kabla hata ya kuanza kuzungumza,wakiwa tayari wamesha maliza kila kilicho takiwa kufanywa kabla hawajaanza mazungumzo,mama nadya alianza kwa kusema,
"nimewaiteni hapa kwa msaada mmoja nyie mnajua mimi sishindwi na kitu"
"Ndio,ndio mkuu"
"kwa sasa nahisi kuna mtu anatumia nguvu za ziada kuwasaidia wakina nadya na caro sina huakika kama ni mungu au laah ila najua ni mzimu ila mpaka sasa sijui ni mzimu upi ila nahitaji msaaada wenu"
mchawi mmoja alisimama kwa niaba ya wengine huku wote wakiwa wako uchi wa mnyama,
"nacho kushauli mkuu mi nina dawa nimeitoa zimbabwe huko ndo inapatikana tu kazi yake ni kuzuhia mizimu sa cha msingi we ichukue iweke kwenye maji kisha uanze kumwaga hayo maji yake kwa kila mlango wa humu ndani.kazi hii ifanye kabla hata wanao hawajarudi,baada ya hapo kama walikuwa na mzimu utashindwa kuingia ndani utakuwa unaishia nje hivyo utakifanya kila unacho kitaka"
"ahsante sana mshilika ndo maana nawategemea,si mnajua mi sina mda maalumu wa kazi ngoja nianze kuiweka hi dawa ili ianze kufanya kazi kabla hawajaja
je nini kitaendelea...

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 8

ILIPOISHIA.............
nacho kushauli mkuu mi nina dawa nimeitoa zimbabwe huko ndo inapatikana tu kazi yake ni kuzuhia mizimu sa cha msingi we ichukue iweke kwenye maji kisha uanze kumwaga hayo maji yake kwa kila mlango wa humu ndani.kazi hii ifanye kabla hata wanao hawajarudi,baada ya hapo kama walikuwa na mzimu utashindwa kuingia ndani utakuwa unaishia nje hivyo utakifanya kila unacho kitaka"
"ahsante sana mshilika ndo maana nawategemea,si mnajua mi sina mda maalumu wa kazi ngoja nianze kuiweka hi dawa ili ianze kufanya kazi kabla hawajaja
je nini kitaendelea................
ENDELEA NAYO....................
*****
mapambano zidi ya babu yake nadya na wachawi wa mama yake nadya yalianza baada ya babu yake nadya kukasirishwa na tukio zima la wachawi wa mama yake nadya kumchukua mke wake, mkuu yule wa wachawi alijibadilisha na kuwa nyoka baada ya kuona babu yake nadya amejibadilisha na kuwa fisi,walianza kushambuliana kama wanyama poli,nyoka ambaye ni yule mkuu wa wachawi alianza kwa kumrushia sumu machoni ili fisi ambaye ni babu yake nadya asipate kuona vizuri ila kutokana na nguvu alizokuwa nazo babu yake nadya hivyo sumu hiyo haikumdhulu hata kidogo,fisi yule alimfuata nyoka kisha akamng'ata shingoni na kuanza kumgalagaza mithili ya mtu aliye fungwa na kamba huku akiendelea kuvutwa na gari,kutokana na ujuzi hule ulimfanya nyoka yule kuishiwa nguvu kisha akabadilika na kuwa mkuu yule wa wachawi kisha akaamua kumuomba msamaha babu yake nadya na kuhaidi atampa mke wake,babu yake nadya alibadilika na kuwa binadamu wa kawaida kisha akaomba mke wake aje mda huo la sivyo atamuuwa na hana huwezo wa kumtoroka.
Mchawi yule bila kubisha aliongea kwa sauti iliyo juu kwa maneno ya kichawi ,ghafla walikuja wachawi huku wakiwa wamemshikilia mke wa babu yake nadya ambaye ni bibi yake nadya.
Mchawi yule mkuu ambaye tayari alikuwa na majeraha yaliyokuwa yakionekana vyema katika sehemu mbali mbali.za mwili wake kutokana na kuwa alikuwa uchi wa mnayama, na pia mda sio mrefu alikuwa na pambano baina yale na babu yake nadya.wachawi wale waliweza kutii amri kisha wakamrudisha bibi yake nadya bila ya kumzulu na kitu chochote kisha wakaondoka.
baada ya kuwa wameondoka babu yake nadya aligeuka na kuanza kumkagua mke wake ambaye alionekana bado kuwa katika hali ya usingizi,kutokana na kuwa tayari palikuwa pamesha anza kukucha hivyo alihitaji kumuamsha cha ajabu alijaribu kila anavyo weza lakini mke wake hakuitika"
babu nadya aliweza kuchukua begi lake kisha akaingiza mkono na kuchomoa kopo kubwa liliyokuwa na dawa iliyokuwa na rangi nyeupe kisha akamimina ule unganga kwenye kiganja na kuupaka machoni ,akuamini macho yake baada kukuta kumbe wachawi walikuwa wamemletea gogo na sio mke wake.
*****
nikiwa naendelea kushangaa sana maneno yale yaliyo toka kwa baba na kuniacha mdomo wazi mimi pamoja na mdogo wangu itakueje mzimu wa baba ututokee ama kweli tunashinda tunashida hasa ya kupambana na mama yetu mwenye roho ya paka ndani yake,hayo yote yalikuwa ni mawazo yangu baada ya kuwa mda si mrefu baba ametoka kuzungumza na sisi.
"caro mbona unawaza sana???"
"Dada kutokana na maneno ya baba nahisi kuchanganyikiwa naogopa hata kwenda nyumbani!!!!"
"kwa nini mdogo unaogopa???"
"Dada nadya kama mama aliweza kula nyama ya baba mume wake wa ndoa,je kwa upande wetu ambao alituzaa wenyewe si huko kutukaanga kabisa,hicho ndiyo kinafanya niogope hata kwenda nyumbani"
"cha msingi basi kama huitaji kwenda nyumbani tutatafta pa kukaa,nimefanya hivyo kwakuwa nimesikiwa maneno ya baba anatumia njia nyingi kutusaidia huwezi jua tukio lililopo kule nyumbani labda ametumia njia hiyo kutusaidia!!!!!"
"Ndio dada nadya huwezi jua"
"Basi sawa ngoja niongee na daktari atupe ruhusa ya kuondoka hapa"
"sawa mi nipo nakusubili"
niliweza kuondoka na kumuacha mdogo wangu caro kisha nikaelekea kwa daktari,nilipokea maelekezo ya daktari pia akatupa dawa za maumivu endapo mdogo wangu akisikia maumivu yoyote basi dawa zile zinakuwa msaada mkuu kwake.
Tuliondoka tukiwa na caro moja kwa moja nikaelekea kwa rafiki yangu kipenzi judithi tuliye kuwa tunafanya naye kazi pale ofisini,kwake hakukuwa mbali na hospitalini hapo hivyo tuliweza kuchukua dakika kadhaa kisha tukawa tumefika
"hodi,hodi,"
"nani??"
"judithi ni mimi nadya"
"Nadya??"
judithi aliongea kwa mshituko uliofanya akaja kufungua mlango kwa pupa,
"ooh my friend ulikuwa umepotelea wapi hata kazini hauji???"
"mmmh judithi rafiki yangu siku ngapi ngapi hebu nipokee kwanza mwenzako nina shinda unioni hata nina mdogi wangu nina shida nipokee kwanza"
"haya ingieni ndani basi"
wakati tukiwa tumefika ndani kwa judithi ghafla mzimu wa baba ulitutokea kisha ukaanza kutusihi kwa ishara tusiweze kuingia ndani mwa judithi...........
je nini kitaendelea....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 9

ILIPOISHIA.............
mmmh judithi rafiki yangu siku ngapi ngapi hebu nipokee kwanza mwenzako nina shinda unioni hata nina mdogi wangu nina shida nipokee kwanza"
"haya ingieni ndani basi"
wakati tukiwa tumefika ndani kwa judithi ghafla mzimu wa baba ulitutokea kisha ukaanza kutusihi kwa ishara tusiweze kuingia ndani mwa judithi...........
je nini kitaendelea....................
ENDELEA NAYO.................
*****
mama nadya alianza kumwanga maji ya dawa kwa kila mlango wa mle ndani kama alivyo elekezwa na wachawi wenzake,alifanya hivyo huku akiendelea kuimba nyimbo za kikabila chao kwa njia ya kujirizisha kwa kile afanyacho,alifa
nya hivyo huku kichwani kwake akiingiwa na mashaka juu ya wanawe walio chelewa kuja nyumbani tangia waondoke awajaweza kurudi na kumpa hofu mama yule mpaka yeye kusahau kuweka dawa katika mlango mkuu wa kuingilia ndani na kudhania kuwa tayari kaisha uwekea dawa. aliweza kupeleka ndoo iliyokuwa imebakiwa na dawa katika chumba chake,alivyo fanikiwa kufanya hivyo alikwenda katika chumba cha wanae ambaye ni nadya na caro akafanikiwa kupachika mjusi ulio kauka chini ya godoro wanalo lalia wakina caro na nadya kwa kuhisi amna njia yoyote yakuwafanya watoloke dawa ile ya kichawi inayokufanya ufe na kuoza hapo hapo,
akiwa amesha maliza kila kitu alielekea jikoni kwa ajiri ya kuandaa chakula .mama yule,aliamua kuandaa chakula ambacho anakipenda nadya na caro kisha akatia dawa itakayo wafanya nadya na caro washindwe kukumbuka mabaya yote yaliyo fanywa na mama yao. hivyo waweze kuwa hata wanalala bila ya kumuomba mungu,kisha akatenga chakula mezani na kuelekea moja kwa moja sebleni kwa ajiri ya kuwasubili wanawe ambao wapo kwa judithi,mama yule alikaa kwa mda mrefu bila kutokumuona mtu yoyote,alicho kifanya nikuendelea kuweka dawa kila kona ili wakisha ingia katika nyumba hiyo, waweze kupoteza maisha hapo hapo,mama yule aliweze kupachika mjusi mwingine kwenye begi la nadya ili pindi tu anapojaribu kubadilisha nguo,aguse dawa ile na kuanza kuoza mikono.
"mmmh mbona hawa awaji au itakuwa huo mzimu umewazuhia kuingia humu ndani nini sielewi mbona mipango yangu inaharibika.
wakati mama nadya akiendelea kufoka kuhusu swala la kuchelewa kwa kina nadya na caro tangu tu walipo kwenda hospitalin kwani kinacho muhuzi mama yule alipigwa kofi la kichawi kutoka kwa nadya hivyo alijua kuna nguvu ya ziada inayo msaidie nadya,na alijua nadya na caro ni watu wasiokuwa na hakili za kufikili hivyo wangerudi tu,hayo ndiyo yalikuwa mawazo naffkra za mama yake na nadya,ghafla mlango ulianza kubishwa kwa nguvu,kitendo hicho kilifanya mama nadya kuachia tabasamu kali sana kisha akaitikia kwa sauti ya madeko utadhani yuko na mumewe.
"Nakuja"
mama yule alipiga hatua za furaha za kwenda kufungua mlango,wakati akiwa tayari amesha fika katila eneo la mlango ule, alianza kuvuta chapya kwa ajiri ya kumfungulia aliye kuwa nje,maana fikra zake zilikuwa zinamuonyesha itakuwa nadya na caro wamerudi,baada ya kuwa amesha fungua mlango,moyo wake ulipiga paaa baada kutazama na mtu tofauti kabisa na aliyekuwa akidhania kuwa ni nadya au caro.
*****
mzimu wa baba uliendelea kunisihi kuwa nisiweze kukaa kwa judithi,lakini niliona kitu nacho shauliwa na mzimu wa baba ni upuuzi sasa kama hataki nikae na judithi rafiki yangu mtu niliye mzoea tena ninafanya nae kazi namjua kwanzia nwanzo hadi nwisho leo hii niondoke na kwenda kufa kwa mama,
"Dada nadya tuondoke"
"caro mdogo wangu sio kila kitu tutamsikiliza mtu cha msingi tupotezee"
tuliongea maongezi ya kumfanya judithi asiweze kuelewa kilichokuwa kinaendelea baina yangu na caro,jambo lile lilifanya judithi kutukazia macho kisha akaanza kufikilia kwa umakini kitu gani tulicho kuwa tumaanisha alivyo jaribu kutumia akili ya kuzaliwa akaona hata elewa akaamua kunitupia swali,
"nadya mnaongea kuhusu nini?mbona hunishilikishi rafiki yangu???"
"we acha tu rafiki yangu kama nilivyo kwambia tuna matatizo tutawekana sawa"
jambo lile lilimkera judithi akatamani kujua tulikuwa tunaongelea nini kisha akaondoka katika eneo lile akiwa amekasirika,tukiwa tuko na caro tuliweza kushangaa kitendo hicho,tulichokifanya kwa wakati huo tuligeuka maeneo baba alipokuwa ili aweze kutueleza kiundani zaidi lakini tayari mzimu wa baba ulikuwa umesha tokomea katika eneo lile.
judithi aliweza kurudi kisha akatuelekeza chumba kwa ajiri ya kupumzika tuliweza kuelekea mahali alipotuelekeza kuwa ndo mahali tunapotakiwa kulala kisha tukaelekea katika chumba alicho tuelekeza,tukiwa tumesha elekezwa na judithi tuliweza kuelekea moja kwa moja huku tukimtazama judithi kwa jicho la pili,maana mzimu wa baba ulikuwa umetupa tahadhali kuwa pale hapatufai hata kidogo,na pia judithi alibadilika ghafla baada ya kuwa tumemficha siri ile ya kuwa tulikuwa tukizungumza na mzimu wa baba,tukiwa tayari tuko katika chumba alichokuwa atuelekeza judithi kuwa ndio mahali tunapo takiwa kupumzika kwa ajiri ya kesho tulianzisha mazungumzo mimi na caro,
"caro leo tusali tena tusali mdogo"
"ahahahah Dada nadya hatimaye sasa hivi unapenda kusali mambo yamebadilika"
wakati tukiwa tunataka kuanza kusali tulisikia.sauti iliyojawa na hasira kutoka mlangoni,ilikuwa sauti ya judithi.
"humu ndani hamna sheria ya kusali mkisali tu nawafukuza usiku huu mnaenda kubakwa huko nje"
"rafiki judithi usijifunze kuishi na roho ya wanyama na akati wewe ni binadamu"
"unasemaje wewe??sasa nadya unanipanda kichwani katika nyumba yangu???"
"amna judithi"
"amna nini kwanza tokeni muende kwenu toka "
"rafiki yangu judithi hii saa 8:00 mda umeenda sana tutaenda wapi tuone huruma wenzio"
"onyo langu la mwisho hakuna kusali hukifanya hivyo hakuna cha urafiki hapa wala cha undugu nakufukuza"
"sawa"
baada ya mda mchache tulisikia paka akianza kulia nje ha mlango wetu alipiga kelele sana tena sana na kutufanya sisi tuanze kupiga kelele za uoga"
mzimu wa baba ulitutokea na kutufanya tunyamaze,
"wanangu huyu judithi ni mchawi tena hatari na anashindana na mama yako katika kupandishwa cheo hivyo moja kwa moja anajua ujio wenu mmetumwa na mama yenu na anachokifanya yeye kwa wakati huu ni kutaka kuwamaliza amewategea dawa chini ya godoro mwiitoe maana ni dawa inayo pendwa na wachawi pili inauwa haraka maana unaanza kuoza kiungo kimoja baada ya kingine,ndo maana tangia mwanzo niliwasihi msiweze kulala humu lakini hamkunielewa,
Tulianza kulia kwa uchungu huku tukiendelea kumuomba baba msaada ambaye kwa sasa alikuwa anatutokea na sio kutumia sauti yake kama mwanzo,
"baba tusaidie,baba tusaidie"
je nini.......kitaendelea.....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 10

ILIPOISHIA...................
mzimu wa baba ulitutokea na kutufanya tunyamaze,
"wanangu huyu judithi ni mchawi tena hatari na anashindana na mama yako katika kupandishwa cheo hivyo moja kwa moja anajua ujio wenu mmetumwa na mama yenu na anachokifanya yeye kwa wakati huu ni kutaka kuwamaliza amewategea dawa chini ya godoro mwiitoe maana ni dawa inayo pendwa na wachawi pili inauwa haraka maana unaanza kuoza kiungo kimoja baada ya kingine,ndo maana tangia mwanzo niliwasihi msiweze kulala humu lakini hamkunielewa,
Tulianza kulia kwa uchungu huku tukiendelea kumuomba baba msaada ambaye kwa sasa alikuwa anatutokea na sio kutumia sauti yake kama mwanzo,
"baba tusaidie,baba tusaidie"
je nini.......kitaendelea........
ENDELEA NAYO................
****
babu yake nadya akiwa amekaa huku msongo wa mawazo juu ya mke wake ukiendelea kumkuba,alamu ya bus ililia na kumfanya babu yake nadya kuachia maneno ya kejeri,
"hawa wajinga wakijua unashida tu ni kosa la jinai maana kila kitu kinaenda haraka,ila sio mbaya mke wangu nitampata tu ila kinacho nipa mawazo je ntampaka katika hali gani du,haya maisha hivi yamekueje mbona yanaishi kwa kuniandama ila lazima nipambane nayo siwezi kukubali hata kidogo maana cha msingi ni kuwamaliza maadui wangu na sio vinginevyo ,msaada ulio baki ni wadawa zangu tu,na katika mipango yangu iliyo baki inatakiwa niende kwa mama yake na nadya yule ndo nitamtumia ili aweze kunionyesha mke wangu alipo nikisha pata mke wangu namuuwa maana hapa duniani amna rafiki hata kidogo"
babu nandya aliendelea kuongea huku akipiga hatua za kuelekea mahali bus lilipo,akiwa tayari amesha panda basi kwa ajiri ya safari ya kuelekea dar es salaam,kuna sauti ya mtetemo kutokana katika mizimu ya kwao ilianza kumpa taarifa kwa njia ya sauti,
"mke wako yupo humo ndani ya bus yupo na wale wachawi ila kwa sasa huwezi muona hata utumie dawa gani ila dawa kuu iliyo bakia chukua kisu ukate.damu yako kisha ikimwagika chini ujue tayari mambo yamejipa hivyo utafanikiwa kumuona humo ndani ya basi na kuweza kumuokoa kwani wanampango wa kumkata ulimi.ili asiweze kuzungumza jambo lolote lile"
ujumbe ule ulio toka kwa mizimu ya kwao na babu yake nadya ,na kumsisitiza aweze kufanya kama alivyo ambiwa kama anamtaka mke wake kabla hata ajakatwa ulimi ili asiweze kuumia.
"babu yake nadya aliweza kufanya kama alivyo elekezwa alichukua kisu katika begi lake kisha akajikata,cha ajabu alivyo zidi kujikata ndivyo damu zilivyo zidi kutoka na kumfanya aweze kumtazama mke wake vyema akiwa ameshikiliwa na mkuu yule wa wachawi,kilicho fuata babu yake nadya alijifanya kama ajawaona wachawi wale kisha akachukua dawa kwenye begi iliyokuwa na muonekano mithili ya mkaa kisha. akatafuna na kumfanya.apotee katika eneo lile,jambo liliyo mchanganya mkuu yule wa wachawi kisha akauliza,
"nyie yule mzee ameenda wapi,mkuu we achana naye.hata hivyo hana huwezo.wa kutuona hana kwa nini tumuogope"
"ila ni.kweli"
babu nadya aliwatokezea kwa nyuma yao bila wao kutarajia kisha akaanza kuwashambulia kwa kuwapiga makofi ya kichawi yaliyo wafanya wapoteee katika eneo lile, kisha babu nadya akaanza kumtemea mate mke wake kinywani na kumfanya aanze kurudisha fahamu zake kwa kuaanza kwa kukohoa,
"ko ko ko ko ko ko"
"mme wangu tuko wapi??"
"mke wangu tupo ndani ya basi ila mpaka sasa amna mwenye huwezo wa kutuona nimeona tutumie.hii njia ili wasituombe ticketi"
"sawa mme wangu"
"ila mke wangu kuna matatizo makubwa yametukuta ila nitakueleza tukisha fika"
"aya mme wangu"
safari ya babu nadya na bibi nadya iliyo kuwa na mauzaza mengi iliendele,ilifika kipindi kondakta akaanza kuomba ticket kwa kila aliemo mle ndani,ila cha ajabu alivyo fika kwa babu yake na nadya aligeuza na kuendelea kwa kuwaomba watu wa mbele,kitendo hicho kilimchekesha babu yake nadya kisha akasema,
"MAMA NADYA ATANIKOMA"
***
mama nadya alishangaa baada ya kutembelewa na mdogo wake aliyekuwa chuo,
"dada mbona hauna furaha pindi tu ulivyo niona"
"amna mwanangu mbona furaha ninayo"
"sawa dada kama unafuraha ni sawa,ila mimi nimechoka pia nitakaa hapa wiki kutokana na dharula iliyopo chuoni"
"unasema utakaa wiki???"
"ndio"
"makubwa"
"Dada basi fanya kitu kimoja sehemu ya kulala na kitu kingine ambacho ningependa kukuuliza nadya na caro wako wapi????"
kutokana na maswali ya mdogo wake na mama yake nadya yalimpa wakati mgumu mama nadya maana ujio wa ghafla wa mdogo wake utamfanya mipango yake kuharibika,cha msingi "nimuuwe tu kwani nitapata hasara gani!!!!"
kabla mama nadya ajafanya maamuzi juu ya kutaka kumuuwa mdogo wake kwa kisingizio kuwa atamuaharibia mipango yake,aliyo ipanga pia kila sehemu ametega dawa kwakuwa mdogo wake atakaa pale wiki itabidi aondoe kila dawa ili zisiweze kumzuru mdogo wake'jambo hilo lilimfanya akae kimya huku akiendelea kufikilia nini cha kufanya au amuue tu mdogo wake,kabla ajatoa maamuzi juu ya mdogo wake,mdogo wake alivunja ukimya na kumfanya mama nadya kushindwa cha kufanya
"Dada tayari nyumbani wanataarifa kuwa nipo hapa sasa unavyo kaa kimya inaamanisha ujapenda ujio wangu kuja hapa"
"hapana frank nina mawazo yangu binafsi alafu nakuomba uondoke tu utakuja kesho ngoja nikuletee hela ya gest kesho ndo utakuja kuna mambo yameingiliana ndo maana umekuta hata caro na nadya awapo"
"iyo sio mbaya sana Dada nitafanya hivyo ili kurudisha furaha yako ila kabla sijaondoka nataka niongee kwanza na shemeji kisha mi nitaondoka na kurudi kesho kama ulivyo sema"
kutokana na maswali ya frank yalimpa wakati mgumu mama nadya mpaka akashindwa kumijibu,
"frank tafadhali ondoka mdogo wangu kesho njoo utamkuta sasa hivi amelala unampigia kelele"
"wiki mbili zilizo pita shemeji alinipigia simu na kunisihi likizo ya chuoni nije kumuona hata kama ni usiku wa maneno ataamka, samahan dada muamshe niongee nae na kama hutaki nitamuamsha mimi mwenyewe"
je nini kitaendelea...

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA...........
wiki mbili zilizo pita shemeji alinipigia simu na kunisihi likizo ya chuoni nije kumuona hata kama ni usiku wa maneno ataamka, samahan dada muamshe niongee nae na kama hutaki nitamuamsha mimi mwenyewe"
je nini kitaendelea..................
ENDELEA NAYO.......
****
Tuliendelea kuuomba mzimu wa baba uweze kutusaidia tuweze kuepuka kasheshe ile,tulilia kwa uchungu jambo liliyo fanya mzimu wa baba kukasirika kisha ukaanza kutuambia maneno yaliyo tupa moyo na nguvu nyingi,ila baadhi ya maneno aliyo tuambia yalituvunja moyo na kutufanya tushindwe kufanya baadhi ya vitu,
"wanangu najua mnashida,niliwaambia msiweze kuingia humu ndani nilijua nguvu za huyu rafiki yenu judithi hivyo nikaamua kukupa tahadhari mapema ili huweze kujikinga naye,kwa sasa mimi ndiyo nimemfanya mpaka sasa hivi ashindwe kuingia humu ndani na kuweza kuwamaliza ndo maaana yuko hapo nje anapika kelele,na kushindwa kuelewa nini kilicho mfanya mpaka ashindwe kuingia humu ndani na kuwamaliza,ila kiufupi mpaka sasa hivi mimi ndiyo nimemfanya ashindwe kuingia humu ndani,watoto wangu nadya na caro nawapenda sana ila kwa matatizo yanayo wakuta ningekuwa na uwezo ningewatoa dunia kwa mda kisha matatizo yaki isha niwarudishe ila huko napo ishi afadhali ya huku.kwa sasa msaada wangu kwenu ni kuwasihi mumuombe mungu maana kama nilivyo waambia tangia mwanzo rafiki yenu anazo nguvu za ajabu kunizidi kwaherini.
Wakati baba akiwa ameongea maneno mengi tena kwa msiistizo huku akiwa anadondosha machozi ya damu,aliweza kutokomea katika eneo lile.jambo liliyo pelekea sisi kuingiwa na hofu zaidi moyoni mwetu,judithi akiwa upande wa nje huku akiwa amebadilika na kuwa paka aliendelea kupiga kelele na kuanza kuongea sauti ya mtoto huku akitusihi tufungue mlango kwani "ana hamu na damu zetu tunavyo zidi kuchelewa ndivyo hamu inazidi"
kutokana na maneno yale ya judithi yalinifanya nianze kutokumuamini mtu yoyote tofauti na mungu kwani ndiye mtu wa kumtegemea,cha muhimu nilicho kifanya ni kumsihi mdogo wangu caro,
"mdogo wangu caro,kama unavyo ona tuko matatani na tuliye kuwa tunamtegemea ni mzimu wa baba na mpaka sasa,umesha tokomea machoni mwetu,nacho kuomba tufunge maombi nadhani, kama mungu atakuwa ajapenda tufanyiwe hiki kitu nadhani atatusaidia,lakini kama atakuwa anapenda kifo chetu kiweze kutokea leo hii sisi tuweze kutokomea duniani nadhani huu ndo utakuwa mwisho wetu"
Niliongea kwa uchungu huku nikiendelea kudondosha chozi,maana tulijua mwisho wetu umekaribia,mdogo wangu alishindwa hata kuongea mda wote alikuwa analia kwa kwikwi jambo liliyo nifanya hata mimi niendelee kulia kwa uchungu mkubwa kutokana na kuwa mdogo wangu alikuwa analia.ghafla tukiwa tunaendelea kulia kwa zamu mimi pamoja na mdogo wangu judithi tayari alifanikiwa kuingia ndani na alikuwa mbele ya macho yetu.akiwa na miguu ya ng'ombe,macho ya paka na nywele ndefu zenye rangi ya brown mithili ya simba zilizo mfunika usoni huku nywele hizo zikiwa zimechakaa kuliko kawaida pia akiwa na kucha ndefu,kisha akazungumza,
"LEO LAZIMA MFE.
*****
frank aligoma kuondoka katika ile nyumba ya mama nadya mpaka pale atapofanikiwa kumuona baba nadya ambaye alikuwa ni marehemu pia alikuwa shemeji yake frank,kitendo kilicho fanya mama nadya awe mkali juu ya mdogo wake frank maana aliona ujio wa frank katika ile nyumba unaweza kuharibu kila kitu,hivyo hakutaka hata kimoja kiende kinyume na matakwa yake.
"Dada hivi unanijua unanisikia siondoki hapa mpaka nimuone shemeji kwa nini unanigombeza kwanini unielewi dada,si nakuuliza sasa mimi nipo jikoni siondoki mpaka nimuone shemeji nimemaliza"
Frank alipiga hatua za kwenda jikoni kwa ajiri ya kupata chakula cha usiku,huku akimuacha mama nadya akiwa katika msongo wa mawazo huku akifikilia jambo gani atamfanyia mdogo wake aelewe na aondoke pale nyumbani bila kuharibu mipango yake.kwani tayari alikwisha weka dawa katika kila eneo la mle ndani na alihofia labda zinaweza kumuathili
Mama frank aliamua kumuacha frank adhuhilike na zile dawa ili apunguze kihele hele kwani alimsisitiza vya kutosha,baada ya kuwa frank amesha fika jikoni aliweza kupakuwa chakula ambacho mama nadya alikuwa amewaandalia wanawe kisha akawa ameweka dawa itakayo wafanya wanawe wapoteze kumbukumbu.lakini cha ajabu chakula kile alienda kula frank,kitendo kilicho fanya mama nadya afraha maana hapo hapo ndipo alipo pata wazo maana alitegemea baada ya kuwa frank amekula chakula kile atasahau kila kitu na ataacha kumuulizia hata baba nadya kwani dawa ile itamfanya apotezee kumbukumbu.
Frank aliweza kupakua chakula kama kawaida huku akiwa amemuacha mama nadya sebleni,frank aliweza kuelekea na chakula mpaka sebleni kisha akamkuta mama nadya akiwa kwenye kochi huku akionekana ni mwenye furaha kuliko mwanzoni kitendo kilicho mshangaza frank.
'Dada mbona umeanza kuwa na furaha sana"
"amna mdogo wangu we kula"
mama nadya alichokuwa anamuomba mungu ni frank aweze kula chakula kile chenye dawa ya kumfanya mtu kushahau na kupoteza kumbukumbu,kabla frank ajaanza kula alianza kutamka maneno ya kichawi yaliyo mshangaza mama nadya.
je nini kitaendelea....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 12.

ILIPOISHIA..................
mama nadya alichokuwa anamuomba mungu ni frank aweze kula chakula kile chenye dawa ya kumfanya mtu kushahau na kupoteza kumbukumbu,kabla frank ajaanza kula alianza kutamka maneno ya kichawi yaliyo mshangaza mama nadya.
je nini kitaendelea..........
ENDELEA NAYO..............
******
Safari ya Babu nadya iliendelea kama kawaida,kipindi Babu nadya akiendelea kujivunia kwa kuwa na nguvu za mizimu zilizo msaidia kwa kila jambo mpaka kufikia tamati ya kujivunia kuwa mzee kwani angekuwa kijana asingeweza kuendekeza nguvu za mizimu hata kidogo.
wakati safari ya Bus hilo liitwao MORNING EXPRESS ikiendelea,mauzauza yalianza kutokea na kumfanya Babu nadya kushangaa jambo lile kisha akasimama baada ya kuona Bus limeanza kuyumba huku asilimia kubwa ya abiria wakianza kumuomba mungu huku wengine wakiendelea kujilaumu kwa kupanda Bus la MORNING EXPRESS kwani tatizo lile lilianza ghafla tu,kitendo kilicho fanya wahisi kuwa labda Bus litakuwa ni bovu.
"hivi hawa wachawi wananitaka nini mimi jamani,sasa kinachofuata ni kumaliza mmoja baada ya mwingine"
Babu nadya aliongea huku akiwa bado amesimama ili aweze kujifikiria aanze wapi aishie wapi!!!! huku mke wake ambaye ni Bibi nadya akiwa katika wimbi zito la usingizi na kushindwa kuelewa nini kilicho kuwa kikiendelea ndani ya Bus.
wakati Babu nadya akiendelea kusimama alipata wazo liliyo mfanya aachie tabasamu la mda mfupi kisha akarudi katika hali ya umakini na kutazama upande wa nje wa Bus kwa kutumia dirisha la Bus hilo,kwa lengo la kutambua nini kinacho fanya Bus liyumbe kwa kasi mithili ya mlevi aliye kunywa kreti zima la bia zilizo mfanya atembee huku akiyumba yumba. pia hata Bus lilikuwa likiyumba yumba hivyo hivyo.
kipindi ambacho Babu nadya alikuwa akiendelea kutazama upande wa nje wa Bus hilo kwa kutumia dirisha dogo lililo kuwemo ndani humo, aliangalia upande ambao mlango wa dereva ulikuwepo na kushuhudia mkuu yule wa wachawi akiwa na fisi wake huku akiendelea kung'ang'ana kwa kufungua mlango wa dereva ili aweze kucheza na akili za dereva kwa kutumia nguvu za kichawi,ili ziweze kumfanya aendeshe pasipo umakini na kufanya Bus kupata ajari,lakini kitu kilicho mchanganya zaid Babu nadya ni kuwa kundi kubwa la wachawi walikuwa wamezingira Bus lote huku wakiwa na fisi zao,kutokana na kuwa Bus hilo, lilikuwa lipo katika MWENDOKASI wake,iliwawia vigumu wachawi wale kufanya walicho kitaka na kujikuta wakati mwingine Bus linaongeza kasi na kuwafanya wabaki nyuma,kutokana na kasi ile ya Bus ilifanya Bus kuwa katika hali ya utulivu na kuacha kuyumba,kitendo hicho kiliwafanya abiria waanze kupunguza presha zao juu ya kupata ajari na kuacha kupiga kelele zilizokuwa zikimchanganya hata dereva na kwani walikuwa wakihisi kuwa mda wowote Bus linaweza kupinduka.kumbe!!!!! ilikuwa kazi ya wachawi.
kutokana na mauzauza hayo ya kichawi yaliyokuwa yakiendelea na kushindwa kumtisha Babu nadya na kumfanya arudi kwenye siti yake huku akiagua kicheko,kutokana na kuwa "WACHAWI WANATUMIA NJIA HATARISHI ILI WAWEZE KUKUMALIZA,LAKINI WANAJIKUTA WANASHINDWA KUKUMALIZA",jambo ilo lilimfanya Babu nadya abaki anatingisha kichwa Mithili ya mtu anaye kataa jambo.
kutokana na utulivu ule ulimfanya kila mmoja wa abiria kutoa shukrani kwa mungu,huku wengine wakitamka maneno waliyo hisi yanafaa kutamkwa kwa mda huo,kutokana na vitendo hivyo vibaya vilivyo fanywa na abiria wachache wao waliokuwa wakimlaumu dereva kuwa uzembe wake ndiyo ulikuwa umesababisha yote hayo.Babu nadya alijisemea kinafsi kuwa angelikuwa amelipia katika Bus hilo,angeweza kujitokeza na kuwasimulia nini kilicho kuwa kinaendelea maana lawama nyingi zilienda kwa dereva.
"Dereva hayupo makini,kwa nini anaendesha kama haoni je tungekufa???sasa hivi sisafiri tena maana naona siku zangu za kufa zimekaribia"
"Usiseme hivyo kaka yangu mungu ndiyo anaye weza kutenda kila jambo"
"we mama boya nini?unasema mambo ya mungu na unaona ligari libovu hili,au unanjama za kunifanya niweze kupanda hili liBus libovu libovu"
"jaman hee mnaona kabisa huu ni uzembe kwa Dereva alafu mnasema ni mipango ya mungu ya nyie amjui kifo nyie"
wengi waliendelea kutoa lawama kwa dereva,kitendo kilicho mkera hata Babu nadya na kutamani hata kujibadilisha ili aweze kuwaambia nini kikicho kuwa kinaendelea,lakini kwa upande wa watu wengine walionekana kutokusikiliza maneno ya watu,huku wakiendelea kutoa shukrani,
"Ahsante yesu"
"alhamdulilah"
kila mtu aliongea kitu alicho hisi ni pongezi kubwa litakalo mfanya mungu ajue kuwa amewapa msaada wa kutosha,ila kwa upande wa dereva alikuwa kimya mda wote jambo liliyo fanya watu waanze kushangaa,kutokana na kuwa walmsema dereva kwa mda mrefu lakini dereva akuweza kuongea chochote wala kutikisika kitendo kilicho fanya watu wote kukaa kimya huku wakiendelea kupata hofu kutokana na ukimya wa dereva,mama mmoja aliyo onekana kuwa na muonekano wa mtu mwenye imani zake alipiga hatua huku Bus likiendelea kwenda kama kawaida huku yeye akiwa na lengo la kumuangalia dereva nini kilicho mkumba,wakati akiwa tayari amesha mfikia dereva huku wengine wakibaki kumtazama,alianza kugusa bega la Dereva kwa nia ya kumsihi ageuke nyuma.ghafla. watu walianza kuziba kutokana na harufu kali iliyo toka kwa dereva.
Dereva alikuwa amesha anza kuoza kwa kutoa funza puani kutokana na kuwa tayari alikuwa amesha kufa zamani,huku akiwa na alama shingoni zilizo za tobo mbili mithili ya mtu aliyong'atwa na nyoka, zilizo endelea kutoa harufu kali pamoja na damu nyeusi mithili kinyesi cha bata anaye toka kulalia mayai yake.
Kutokana na tukio lile la ajabu liliwafanya watu waanze kupiga kelele,hata walio kuwa na imani zao,walipiga kelele tena wao ndo walipiga kelele kuliko wengine,kwa upande wa yule dada aliye enda kumgusa dereva kwa lengo la kumsihi aweze kugeuka ili apate kufahamu kilichokuwa kikiendelea alikuwa tayari amesha poteza fahamu.
je nini kitaendelea uskose sehemu ijayo upate kufahamu nini kilicho endelea ndano ya Bus ilo....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 13

ILIPOISHIA...............................
Kutokana na tukio lile la ajabu liliwafanya watu waanze kupiga kelele,hata walio kuwa na imani zao,walipiga kelele tena wao ndo walipiga kelele kuliko wengine,kwa upande wa yule dada aliye enda kumgusa dereva kwa lengo la kumsihi aweze kugeuka ili apate kufahamu kilichokuwa kikiendelea alikuwa tayari amesha poteza fahamu.
je nini kitaendelea uskose sehemu ijayo upate kufahamu nini kilicho endelea ndano ya Bus ilo..................
ENDELEA NAYO.....................
******
"judithi tusamee judithi mbona sisi hatuna kosa"
niliongea huku machozi yakiendelea kunitoka,kitendo kilicho fanya nizidi kumchukia mama yangu kwani bila yeye matatizo yote hayo yasingeweza kutokea na kunikumba mimi pamoja na mdogo wangu caro.
Judithi aliendelea kubadilika na kuwa kiumbe anaye tisha kwani alianza kuota magamba katika tumbo lake yaliyo mfanya apige kelele zilizo tupa uoga,lakini kwa mdogo wangu caro ilikuwa tofauti kwani yeye mda wote alikuwa kimya huku akiwa amefunga macho yake pia akiwa ameunganisha mikono yake na kuisongeza katika kinywa chake.
Sikuelewa alikuwa anafanya nini??,ila nilicho kuwa na kishuhudia kutoka kwake ni kucheza kwa mdomo wake mithili ya mtu anaye ongea lakini hatoi sauti.
Judithi alianza kupiga hatua za kuja upande tuliyo kuepo huku akiwa amebadilika na kuanza kutoka damu mdomoni mwake,zilizo nifanya ningundue kuwa kifo kipo karibu yangu,kutokana na kuwa tayari judithi alikuwa amebadilika sana, ungekuwa huna mfahamu judithi usinge tambua kuwa ndiye.
Mdogo wangu caro aliendelea na vitendo vyake vilivyo nishtua na kunifanya nijiulize kwa nini Caro yuko kimya katika hali ya hatari kama hii kwani anafanya nini cha muhimu kilicho mfanya ashindwe kujua kama tupo kwenye hatari pia nikiwa bado nashangaa nisijue nini cha kufanya ghafla nilianza kumuona judithi anarudi katika hali yake huku akiendelea kupiga kelele za kuomba msaada.
"Nadya nakufa,nakufa nadya moto unanichoma moto nadya nakufaa"
judithi alipiga kelele huku akiendelea kugalagala upande wa chini mithili ya nyoka anaye taka kukata roho.
Nilianza kumtingisha caro ili apate kuona kinacho endelea mahali pale,lakini caro hakuweza kugeuka wala kutikisika kitendo kilicho nifanya nianze kupata hofu juu ya mdogo wangu caro na kugundua kuwa labda itakuwa amechezewa na wachawi, kutokana na kuwa alikuwa mkimya mtu wote pia hata katika hali ile ya hatari,ndiyo moja kati ya vitu vilivyozidi kunipa hofu juu ya mdogo wangu.
judithi aliendelea kupiga kelele na kunizidi kunichanganya,hii ni kwa sababu nilidhani judithi anajiandaa kutumaliza kutokana na kuwa alivyo zidi kupiga kelele ndivyo alivyozidi kurudi katika hali yake pia aliendelea kutisha hata kumtazama.
Nikiwa katika kile chumba huku nikiendelea kushangaa maajabu ambayo sikubahatika kuyaona katika maisha yangu,mdogo wangu caro alianza kufungua macho polepole kisha akasema kwa sauti iliyo penya maskioni mwangu vyema na kwa msikio wa hali ya juu"AMEN"
Baada ya kuwa mdogo wangu ametamka neno hilo,nilimtupia swali huku hofu ikiendelea kunitanda juu ya usalama wa maisha yetu,
"Caro ulikuwa unafanya nini mdogo wangu tutakufa ona judithi,ona caro anavyo badilika tumuombe mungu hatuokoe"
"Dada nadya nilikuwa kwenye ibada fupi ya kumuomba mungu haweze kutuepusha na janga hili,ndo maana unamuona judithi rafiki yako anazidi kubadilika na kurudi katika hali yake"
Nilishangaa kusikia maneno yenye ujumbe mzito kutoka kwa mdogo wangu kwani sikutegemea kama angepata ujasiri wa kuweza kufanya ibada ingali tupo kwenye hatari.
"ahsante sana mdogo wangu,mungu akubariki"
Tukiwa tunaendelea na mazungumzo mimi pamoja na mdogo wangu,judithi alisamama huku akionekana kuwa mchovu mithili ya mtu anaye toka usingizini.
"Rafiki yangu nadya,naomba mnisamee kwa nilicho wafanyia niko chini ya miguu yenu kwanzia leo sitaweza kujishughulisha na uchawi naomba mnisamee,adhabu niliyo ipata kutoka kwa mwenyezi mungu imekuwa funzo kwa upande wangu kwani nimepata mateso ya kuchomwa na moto wa mda mchache lakini naskia maumivu mwili mzima,naomba mnisamee"
*******
kipindi frank akiwa amesha maliza kutamka maneno yale ya kichawi,ghafla chakula kilibadilika na kuwa na uchafu mwingi ulio mfanya frank kushtuka huku mama nadya akionekana kama haoni kinacho endelea.
"Dada we ni mchawi si ndiyo"
Frank alimuuliza dada yake ambaye ni mama nadya huku akiwa anamnyooshea kidore,kutokana na swali lile lenye ukweli ndani yake lilimfanya mama nadya kuanza kuona aibu kisha akainamisha kichwa chini.
"Dada si nakuuliza wewe ni mchawi?????"
Mama nadya alimjibu mdogo wake kwa hofu huku akionekana kumuogopa mdogo wake kwani hayo maneno ili ufanikiwa kuyajua ni lazima uwe na cheo uchawini.
"Hapana mdogo wangu mi sio mchawi"
"Dada hivi wewe unadhani unapata faida gani kuwa mchawi,sasa kama unataka kuniuwa mimi mdogo wako nimekukosea nini dada"
frank aliongea kwa majonzi na msikitiko makubwa huku akiendelea kuchunguza chakula kile kilicho endelea kujaa funza kwa ghafla, kisha frank akatupa sahani ile chini.
"Dada yani wewe heli hata shuleni kwetu,ila wewe umezidi uchawi.shuleni kwetu uchawi umetawala mpaka baadhi ya wanafunzi ikiwemo na mimi tulikaa kikao kisha tukalijadili hili,njia gani tutazitumia kupambana na uchawi wa pale chuoni,kutokana na kuwa ulikuwa kero sana kwani baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakishika nafasi ya kwanza walishika nafasi ya mwisho,pia waliokuwa wanashika nafasi ya mwisho waliweza kushika nafasi ya kwanza.ikiwemo mimi nilikuwa nashika nafasi ya pili lakini ilifika hatua nikawa nashika nafasi ya pili kutoka mwisho.hivyo basi tuliweza kukubaliana kukutafta mnganga tulikuwa watu wachache,baada ya kuwa tumefika kwa mganga,mganga aliweza kutukinga kwa zindiko kubwa la kichawi,hivyo dada yangu hata ufanye nini huwezi kunipata hata kidogo najua umesha muuwa shemeji ila nitakaa hapa hapa mpaka nijue ni lini hutaacha uchawi la sivyo tutauwana humu ndani"
Frank aliongea maneno mengi yaliyo mfanya mama nadya kukasirika kisha akaanza kupanga shambulio la kummaliza frank....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA.................
Frank aliongea maneno mengi yaliyo mfanya mama nadya kukasirika kisha akaanza kupanga shambulio la kummaliza frank....
JE NINI KITAENDELEA................
ENDELEA NAYO...............
****
Babu nadya alikuwa katika hali ya mshangao,maana hakuamini kuwa Dereva ataweza kufanyiwa vile kama alivyo fanywa.
"Nimeshajua hawa wajinga wanafanya haya yote kwa ajiri yangu sasa ngoja niwachezee mchezo usio kuwa na mashabiki"
Babu nadya mda wote alikuwa anaongea kwa vitendo,hapo ndipo alipo muamsha mke wake,huku uso wake ukiwa umebadilika na kutoka kwenye mzaa,abiri karibia wote walikuwa tayari walisha poteza fahamu na ukimya ulikuwa tayari umesha chukua nafasi.
"Mke wangu amka???"
"Mme wangu twende wapi si unaona safari bado inaendelea"
"Mke wangu ebu paka hii dawa machoni mwako"
Babu nadya alimpa mke wake unga unga mweupe aliyo uchomoa katika karatisi liliyo fungwa na kuleta muonekano wa fundo.
Bibi nadya aliweza kupaka paka ule unga machoni mwake,baada ya kuwa amepaka machoni mwake,mapigo yake ya moyo yalianza kudunda,na kumfanya amrukie mme wangu na kukumbatia kutokana na hofu iliyo kuwa imemtanda, baada ya kuwa ameona maajabu ndani ya ilo Bus,kisha akamuuliza mme wake.
"Mme wangu tutakufa humu,ona wachawi wanavyo mtesa yule dereva,lakini kabla sijapaka dawa nilikuwa naona dereva yuko sawa,na hawa abiri nilijua wamelala,mme wangu kumbe wachawi ndo wanafanya haya yote,nme wangu nakuomba tumsaidie yule dereva ona wanavyo msubua makusudi ili mradi afanye gari lipate ajari mme wangu"
Bibi nadya aliongea huku akionekana kuchanganyikiwa sana hii ni kutokana na kuwa alivyo kuwa akimuongelesha mme wake,mme wake hakuweza kumjibu kitu chochote kana kwamba hamsikii.
hapo ndipo bibi nadya alizidi kumuongelesha mme wake huku akiwa anamtingisha na kumvuta ili apate kumsikia kwa umakini.
"Mke wangu usinione nimekaa kimya,nacho fikiria niwauwe hawa wachawi au laah,maana wamezidi sasa hata kama nikuzidi wamezidi.wameanza kuvuka mipaka yangu sasa,ebu fikiria mke wangu nisinge kupaka hii dawa machoni mwako ??? si ingeniwia vigumu kukuelewesha kinacho endelea,kwa macho ya kawaida unaweza dhani ya kuwa dereva amekufa,ingali bado gari linaendelea kwenda,lakini ukiwa na dawa machoni mwako ndiyo kama unavyoona pale mbele mke wangu,wanamtesa sana dereva na kumsumbua,hivi mke wangu unajua dereva hata yeye hawaoni anacho jua labda kuna wadudu wanamuwasha si unaona anavyo jikuna lakini bado anaendelea kuendesha gari hili.
"Ndio mme wangu naomba huwaokoe watu wa humu,kifo mme wangu sio kizuri hata kidogo nakuomba."
"sawa mke wangu ntafanya hivyo,ila ingekuwa sijatoa sadaka kwa mizimu yetu ,wale wachawi wangeweza kutuona hata sisi na kuanza kutushambulia,mpaka sasa hivi wanahisia tu kama niko humu ila hawana huakika.
"kwani sadaka gani umetoa mme wangu???"
"angalia huu mkono hauoni nimejikata"
"pole sana mme wangu"
"usijari"
Yalikuwa mazungumzo baina ya Bibi nadya na Babu nadya huku wote wakionekana kuwa ni watu wakarimu na wanao penda amani,Babu nadya aliweza kuchukua begi lake liliyokuwa na muonekano wa uchakavu,aliweza kuingiza mkono wake kisha akachomoa mti mdogo ulio kauka pia ukiwa katika muonekano wa bunduki.Bibi nadya alimuuliza mme wake huku akiwa amejikinga nyuma ya mgongo wa mme wake ili asipate kuona kinacho endelea kwa dereva pia wote wawili wakiwa bado wamesimama.
"mme wangu nini hicho???"
"mke wangu hii ni siraha kubwa sana na naipenda sana"
Babu nadya alimjibu mke wake huku akionekana kuwanyooshea wale wachawi huku akiwa amefumba jicho moja.
"kazi yake nini mme wangu???"
"hutumika kuuwa wachawi tu,na wewe kama sio mchawi haiwezi kukuuwa hata kidogo,pia kuna maneno unatakiwa utamke badala ya kuwa umewalenga"
"mbona mme wangu hukuwai kuniambia haya yote,unakuja kuniambia leo mme wangu we unadhani mi napenda unavyo nificha kila kitu??"
"Nia na madhumuni ya kutokukuambia kule kijijini ni kuwa ungeweza kuathiri kila mchawi unaye mfahamu na ungesababisha vifo vingi sana vya wachawi,mke wangu tangia hii safari yetu imeanza sijahitaji kuuwa mchawi hata mmoja kwani hata wao kwenye familia zao wanategemewa sana kuliko unavyo fikiri,pia sio kila mchawi anapenda kuwa mchawi wengine wanalithishwa na dungu zao,ndo maana sikutaka kukuambia maana najua nilazima ungesababisha vifo tu,kingine mke wangu nakwambia sasa hivi kwakua tupo kwenye hatari mda wowote naweza nikauwawa na hawa wachawi wewe ukanifikiwa kufika kwa mkwe wetu mama nadya na ukammaliza kwa kosa aliyo lifanya"
"sawa mme wangu nimekuelewa."
"Bado dakika 20 tufike stendi ila nahisi hawa wachawi hawataruhusu tuweze kufika salama cha msingi ngoja nianze kuwamaliza kuanzia sasa"
Babu nadya alianza kuwaonyesha wachawi ka mti kale huku akitamka maneno aliyo yafahamu yeye mwenyewe"
Baada ya kuwa ametamka maneno yale kelele za wachawi zilianza kusikika huku zikiomba msaada.
"Mungu tunakufa,tunakufa tusaidie"
Babu nadya alichia tabasamu na kicheko kikali kwani hakutarajia kama hata mchawi anaweza kumuomba mungu,kutokana ns kuwa alikuwa tayari amesha wafyatua wale wachawi kwa nguvu zilizomo ndani ya mti hule na kuwafanya watoweke katika eneo lile,Bibi nadya pia na yeye aliweza kuachia tabasamu na kicheko kikali kilicho mfanya mme wake amkumbatie.
"Mme wangu kumbe hata wachawi wanamjua mungu"
"Mke wangu kuna mtu asiye mjua mungu,hata jambazi anapoenda kuvamia sehemu lazima amuombe mungu ili afanikiwe kumuuwa mwanadamu mwenzake, mara nyingi mungu anamsaidia kila amuombae ndo maana majambazi wengi wanafanikiwa kuvamia na kuondoka bila kudhuhulika na kitu chochote"
"Ni kweli mme wangu usemacho umenifrahisha sana mme wangu,tangia umenioa leo ndo umenifrahisha zaidi ya siku zote na najivunia kuwa na mme kama wewe jemadari langu"
Bibi nadya aliongea kwa furaha ya hali ya juu huku akionekana tayari alikiwisha sahau kifo cha mtoto wake thomas ambaye ni baba yake na nadya.
Hatimaye Dereva alicha kujikuna kisha akatamka neno la hasira na kukejeri bila kujua nani alikuwa anafanya hivyo.
"Duu!! mbona kila siku naoga kwani najiwasha kama haga siogi aaah miili ya kijinga jinga hii najutia kuwa na limwili hili je ningesabisha ajari sijui ingekuwaje haaaa!!!!"
Dereva aliongea huku akipiga honi ya kuashiria kila mtu akaye tayari kwani tayari Bus ilikuwa imesha fika stendi.
abiria wote walio kuwa ndani ya gari lile,walisimama kana kwamba wanatoka kwenye usingizi na huku kila mtu akiwa amesahau matukio yote yaliyokuwa yametokea na hii yote ilikuwa kazi ya Babu nadya,baada ya kuwa amewashambulia wale wachawi,aliweza kutamka maneno yaliyo fanya kila mtu ndani ya Bus hilo,kusahau kila kilicho tokea isipokuwa yeye na mke wake.
je nini kitaendelea.....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA.................
wanatoka kwenye usingizi na huku kila mtu akiwa amesahau matukio yote yaliyokuwa yametokea na hii yote ilikuwa kazi ya Babu nadya,baada ya kuwa amewashambulia wale wachawi,aliweza kutamka maneno yaliyo fanya kila mtu ndani ya Bus hilo,kusahau kila kilicho tokea isipokuwa yeye na mke wake.
je nini kitaendelea.......................
ENDELEA NAYO...........
*****
Nilisimama na mdogo wangu caro kisha tukapiga hatua mpaka pale alipo judithi,kisha nikamuinua kwa kumshika mkono maana alikuwa amenipigia magoti.
"judithi Rafiki yangu kuokoka sio lazima uende kanisani,jaribu hakika utaweza kuna baadhi ya mambo hayana faida hebu fikiria bila sisi kuja hapa si ungeendelea na uchawi??"
"Ndio rafiki yangu nadya"
"Unaishi kwa kumuomba mungu kumbe mabaya yamekuzunguka ona sasa,we si ndiyo uliyekuwa unanipigia simu kila siku unanisihi ya kuwa twende kanisani,ona leo hii siamini kama wewe ulikuwa mchawi na bado ulikuwa unaendelea kuficha makucha yako kwa kutumia dini ili usiweze kufahamika mapema"
Niliendelea kuzungumza huku hasira zikiendelea kunikabili,pia na machozi yakianza kuchukua nafasi yake.
"we judithi we si ndiye uliyekuwa unanisihi niweze kumuomba mungu anisaidie kwa kila ninalo ona ninanikabili,hasa kazini uliweza kunishauri niweke juhudi jatika kuchapa vitabu pia nisiweze kufanya kazi bila ya kumtanguliza mungu si ni wewe,judithi usije ukawaza yakuwa una rafiki kama mimi shenzi"
Niliongea kwa majonzi makubwa huku nikishika mkono wa mdogo wangu kwa jaziba ili tupate kuondoka,lakini mdogo wangu hakuweza kukubaliana na tukio lile.
"Dada nadya jifunze kusamehe ona sasa usipo msamee wewe nani? atamsamee nani,niko chini ya miguu yako dada naomba umsamee rafiki yako wanasema sameh saba mara sababini ujawai msamee na pia hajawai kukukosea tofauti na sasa lakini unahesabu umesha msamehe zaidi ya mara sabini kweli???"amna dada nakuomba nisikilize"
""Caro niache,naomba uniache utaanzeje kumsamehe shetani"
Baada ya kuwa nimemtamkia judithi ya kuwa ni shetani alianza kulia huku akiniomba nimsamehe kwani hakujua nini kilichokuwa kinamfanya yeye kuwa mchawi ni kama alikuwa amerogwa.
"Nadya kumbuka tumetoka mbali,kumbuka ni mangapi tumefanya nakuomba nadya nisamee nakuomba niko chini ya miguu yako"
kutokana na kuwa judithi alilia kwa uchungu mkubwa ulio nifanya hata mimi kumuonea huruma kisha nikazungumza nae huku nikimfanya mdogo wangu caro kuachia tabasamu la furaha.
"nimekusamehe rafiki yangu kwani kutenda kosa sio kosa bali kurudia kosa ila kabla ujafanya kila kitu unacho takiwa kufanya nakusihi tubu ili mungu apate kukusamehe kama mimi nilivyo kusamehe"
"sawa nadya nitafanya hivyo cha msingi nilihitaji msamaha kutoka kwako kwani nimekukosea sana Nadya,pia ahsante caro kwa kumshauli dada yako nadya yaliyo mema mpaka kufikia tamati ya kunisamehe ahsante sana"
judithi alimpa pongezi sana caro,huku pia na caro akionekana kufrahi sana kwa kuona nimemsamehe judith kwani alimuonea huruma sana.
Furaha ile ilizidi kuchukua nafasi huku judithi akionekana mwenye furaha lakini alikuwa mda wote akiona aibu hii ni kutokana na kuwa alirihisi labda bado tunakumbuka tukio lake la mda mfupi liliyo pita.
"Nadya na caro nawaombeni mlale tutaongea kesho kwani mda umesha enda"
nilimjibu kwa dharau huku nikionekana dhahiri kuwa nilicho kifanya hakikutoka moyoni mwangu bali nilifanya kwa ajiri ya kumfrahisha caro tu,wakati nikiwa nimekaa kimya kwa mda mrefu,judithi aligundua kuwa na mfikilia yeye,ni ulikweli alikuwa sahihi kwa alicho kiwaza kwani nilkuwa namfikilia yeye huku nikiendelea kuwaza nimfanye nini judithi kwani nimesha anza kuwachukia wachawi maishani mwangu,nikiwa bado naendelea kuwaza na kuwazua judithi aliondoka na kwenda kulala bila ya kuongea kitu chochote kile,kisha caro hakuweza kufanya kama nilivyo fanya,aliweza kumpungia mkono judithi kisha akazungumza.
"kwaheri judithi,usiku mwema"
judithi hakuweza kumjibu caro kitu chochote tofauti na kuongeza hatua za kuelekea nje ya chumba kile,jambo lile lilifanya caro kushtuka kisha akaniuliza.
"Dada nadya umemfanya nini judithi mbona amekasirika????"
"sijamfanya kitu ni matatizo yake mwenyewe"
"lakini dada umemsamehe kutoka moyoni???"
"sijamsamehe angetaka nimsamehe angeweza kuleta kila tunguri lake hapa na tuvichome ndo ningemsamehe kwani akibaki navyo itafika siku atatamani kurudi kwenye uchawi pia ataweza kurudi na hapa nimemwambia nimemsamehe ili nafsi yake ilidhike"
wakati tukiwa tuanaendelea kuzungumza,mzimu wa baba ulitutokea
"wanangu mme fanya makosa kumruhusu judithi aondoke, mtakufa mtakufa mtakufa"
baba aliongea kwa sauti ya mwangwi iliyo kuwa ikijirudia rudia kisha akatoweka
****
Mama nadya alizidi kufikiria ni kitu gani atamfanya frank,kisha akapata wazo na kumuita frank kwa sauti ya madeko mithili ya mke anavyo muita mme wake pindi anapo hitaji wafanye tendo.
"Frank njoo mdogo wangu"
Frank akiwa anapiga hatua za kuelekea chooni,aliweza kuitikia wito ule kisha akasitisha hatua zile za kuelekea chooni na kurudi kwa dada yale ambaye ni mama nadya.
"unasemaje dada au unataka uniteke et??? maana wachawi hawatabiliki"
"amna mdogo wangu usinifikirie hivyo nilihitaji nikuonyeshe sehemu unayo takiwa kulala"
"sawa nionyeshe"
"Nifuate"
Frank alianza kumfuata mama nadya kwa lengo la kuonyeshwa mahali anapo takiwa kupumzika kwa usiku ule,walichukua mda kadhaa kufika katika chumba husika,kisha mama nadya akafungua mlango na kutangulia kwa kuingia ndani kisha frank akafuata.
"mdogo wangu hichi ni chumba cha ndugu zako caro na nadya,kwa sasa hivi wametoka wapo safari,kabla hawajarudi utakuwa unajipumzisha hapa,baada ya kuwa wamerudi tutaangalia sehemu mbadala unayo takiwa kupumzika kwa mda mfupi utakayo kuwa hapa."
Baada ya kuwa mama nadya amemaliza kuzungumza alipiga hatua za kuondoka kwenye kile chumba huku akimuacha mdogo wake ambaye aliendelea kukichunguza chumna hicho.
"Du mbona hiki chumba nahisi akinifai,alafu sio lazima nilale humu"
Frank aliongea huku akipiga hatua za kurudi sebleni na kutoka ndani ya chumba hicho.
"Dada,dada???"
"abee mdogo wangu??"
"huko wapi dada??"
"mbona mimi nipo sebleni"
Frank aliongeza hatua kadhaa kisha akawa amefika sebleni na kumkuta dada yake akiwa amewasha Tv huku akiendelea kutazama baadhi ya channel zilizoendelea kurusha miziki nyakati za usiku,baada ya kuwa mama nadya amecha kutazama Tv aligeuka na kumtazama mdogo wake kisha akamtupia swali.
"wewe mbona hajalala saa nane hii usiku unataka kesho huamke saa nne asubuh"
"Dada kama chuoni mtu analala saa kumi anaamka saa kumi na moja,pia hata mimi nilisha fanya hivyo zaidi ya mara miamoja,sembuse saa nane,kingine dada tumia uchawi mwingine huo unao utumia umexpaya kwani kwenye kile chumba ulicho nipeleka kuna dawa umeweke na usijiulize nimejueje"
kutokana na maneno ya frank yalionekana dhahiri ni mtu mwenye kinga ya hali ya juu.
je nini kitaendelea......

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 16

ILIPOISHIA.............
"Dada kama chuoni mtu analala saa kumi anaamka saa kumi na moja,pia hata mimi nilisha fanya hivyo zaidi ya mara miamoja,sembuse saa nane,kingine dada tumia uchawi mwingine huo unao utumia umexpaya kwani kwenye kile chumba ulicho nipeleka kuna dawa umeweke na usijiulize nimejueje"
kutokana na maneno ya frank yalionekana dhahiri ni mtu mwenye kinga ya hali ya juu.
je nini kitaendelea...................
ENDELEA NAYO.......................
*****
Tayari "BUS LA EXPRESS" ilikuwa imeshafika stend,abiri wote walianza kushuka akiwemo Babu nadya pamoja na Bibi nadya,huku wakiendelea kuachia tabasamu la furaha kutokana na kuwa mungu amewasaidia wameweza kupita vikwazo vyote vilivyokuwa vimetokea huku wakihisi ya kuwa wamepitia vikwanzo vingi lakini hatimaye wamefika stend salama, condakta alianza kuwaruhusu abiria wote waweze kushuka katika Bus lile kwani tayari Bus lilikuwa limeshafika mahali husika.
Babu nadya pamoja na mke wake walikuwa wa mwisho kushuka katika Bus ile.
kutokana na kuwa tayari yalikuwa yamesha timia majira ya saa nane usiku hivyo babu nadya hakuweza kwenda moja kwa moja mahali ilipo nyumba ya kina nadya.
Abiria wote walihitaji walale kwenye hicho kwani mda ulikuwa umesha enda,kwakua Babu nadya hakuweza kulipia ada yoyote ya usafiri,pia alikuwa haonekani na mtu yoyote tofauti na mke wake,alihitaji kulala ndani ya Bus hilo hilo waliyo kuja nayo na hii ni kutokana na kuwa katika kituo kile cha Bus nafasi zote za wageni wa emengercy zilikuwa zimejaa hivyo aliona hicho ndio kitu cha muhimu kwa wakati huo.
"Mme wangu kwa nini tusijiondoe hizi dawa kisha waweze kutuona labda kuna nafasi iliyo bakiya wanaweza kutupatia kwa kudhania ya kuwa na sisi ni abiria kama wengine???"
"Mke wangu,hapa jijini Dar es salaam watu wengi hawana makazi ya kuweza kupumzika nafasi za usiku hivyo wanatumia nafasi hii ili wapate sehemu za kulala,kwaiyo mke wangu kwenda pale mpaka uoneshe ticket yako hata kama umeipoteza hawatakusikiliza hata kidogo"
"Makubwa mme wangu"
"Ndo hivyo mke wangu"
wakati abiria wengine wakielekea kwenye kituo cha bus kwa ajiri ya kupewa sehemu zitakazo fanya wapumzike kwa ajiri ya kesho maana mda ulikuwa umeshaa enda,lakini wa upande Babu nadya yeye pamoja na mke wake,waliweza kurudi ndani ya Bus kwa ajiri ya kujipumzisha ili wapate kuiona kesho.
wakiwa wamefanikiwa kuingia ndani ya Bus lile,walielekea na kwenda kukaa kwenye siti za nyuma kabisa zilizo tawaliwa na giza totoro,baada ya kuwa wamekaa kwenye siti za nyuma huku wakiwa wametulia tulii,walianza kusikia mazungumzo kutoka upande wa nje.katika mazungumzo yale walihisi ya kuwa kuna sauti wanaifahamu.
"We dereva funga mlango wa iyo Bus hauoni uko wazi???"
"Sawa boss,ila mbona nilikuwa nimeufunga"
"ebu kagua umo ndani labda machokoraa watakuwa wameingia"
"Sawa boss"
Babu nadya alisikia mazungumzo hayo kutoka upande wa nje lakini hayakuweza kumpa hofu hata kidogo kwa alijua katika mwili wale kuna dawa insyo mfanya hasionekane.
Hatua za mtu aliyo ruhusiwa kukagua ndani ya Bus aliye kuwemo Babu nadya pamoja na mke wake, zilizidi kuongezeka na kuja ndani ya Bus lile,Baada ya kuwa mtu yule amefanikiwa kuingia ndani ya Bus,aliweza kuwasha tochi yake iliyo kuwa na mwanga mkali sana,pia ulikuwa ukimuumiza macho Babu nadya pamoja na mke wake na kuwafanya washindwe kuona vizuri,pia dereva yule mkononi alikuwa na panga yake iliyoonekana kuwa bado ni mpya,kutokana na kuwa Babu nadya pamoja na mke wake walikuwa na dawa mwilini mwao iliyo wafanya wasiweze kuonwa na mtu yoyote yule, lakini kwa upande wa dereva ilikuwa tofauti kwani yeye akuweze kuona mtu katika siti zile za nyuma ila alihisia ya kuwa maeneo waliopo wakina Babu nadya kutakuwa na mtu, Dereva yule hakukata tamaa aliweza kupiga hatua mpaka alipo Babu yake nadya pamoja na Bibi yake kisha akamulika eneo lile kwa kutumia mwanga wa tochi yake uliyokuwa na mkali sana kisha akazungumza
"mbona hamna mtu ila fikra zangu zinaniambia kuna mtu,amna aga nina tabia ya kueshimu sana fikra zangu"
Kutokana sauti ya dereva iliyokuwa ikikwaruza mda wote ilimfanya Babu nadya kumgundua dereva yule,kwani mara ya mwisho kusikia sauti kama ile ya dereva ni pale alipokuwa akilalamika ya kuwa anawashwa kumbe alikuwa akichezewa na wachawi kwa lengo la kumfanya asababishe ajari.
Dereva yule aliweza kuchomoa panga yake kisha akakata mahali pale alipo hisi ya kuwa kuna mtu. kutokana na kuwa alikuwa amemlika Babu nadya pamoja na Bibi nadya kwa kutumia mwanga wa tochi yake,hivyo iliwawia vigumu Babu nadya pamoja na Bibi nadya nadya kuelewa kinacho endelea.
Dereva yule aliyekuwa na msimamo wa kipekee,baada ya kuwa ameshunguza katika siti zile za nyuma na kugundua ya kuwa amna mtu, aliweze kukata mahali pale kwa kuhisi ya kuwa kuna mtu lakini sma itakuwa amejificha,baada ya kuwa amekata mahali pale Bibi nadya alianza kupiga kelele zilizo mfanya Babu nadya kuanza kushtuka.
"mke wangu umekueje???"
"mme wangu nakufa mme wangu,nimekatwa na panga angalia mme wangu kichwa changu kinavuja damu angalia mme nakufa nakuacha mme wangu mwenyewe mme wangu mimi nakufaa"
Bibi nadya aliongea huku akimaanisha,kwani tayari alikwisha anza kutoa kelele na yowe kali za maumivu,pia akimuomba mme wake ambaye ni Babu nadya aweze kumsaidia.
Baada ya kuwa Dereva yule amelidhika kwa tukio lile aliyo lifanya maana yeye kwa upande wake aliona kama amekata hewa tu lakini amna kilicho endelea hata kelele za.Bibi nadya hakuweza kuzisikiliza hata kidogo,pia hata damu kwenye panga lile hakuweza kuziona hii inatokana na dawa walizopaka wazee wale.
Babu nadya alianza kutoa ukelele wa maumivu kwani hakutegemea tukio lile la kizembe kama lingetokea na aligundua kilicho sababisha hayo yoye ni ule mwanga wa tochi ya yule dereva iliyo kuwa na mwanga mkali ulio mfanya Babu nadya mda wote aangalie pembeni.
"Mme wangu nakufa na bado nakupenda"
"amna mke wangu huwezi kufa mke wangu na kama unajiskia unezidia sana nikupake dawa hii itakayo kufanya upone mdaa huu ila baada ya siku ni lazima ufe"
Babu nadya alizungumza na mke wake kwa uchungu mkubwa huku akiendelea kumshuhudia Dereva yule aliyezidi kupiga hatua za furaha maana baada ya kufanya tukio lile ,alijiskia ni mwenye amani mda wote ni tofauti na mwanzo kabla ajafanya tukio lile, Dereva yule alifanya tukio dogo kwa muonekano maana yeye alikuwa hajui nini kilichokuwa kuwa kinaendelea lakini tukio lile l lilikuwa hatarishi kwa Babu yake nadya pamoja na Bibi yake.
Babu nadya alianza kupandwa na hasira hivyo akaweza kumlaani dereva kwa maneno ya kichawi ili aweze kuchanganyikiwa mpaka afe,baada ya kuwa amemlaani dereva yule,dereva aliongeza kasi ya kutoka ndani ya bus lile kisha akaanza kupiga kelele zilizo wafanya walinzi wa pale stend waanze kusogelea Bus lile kwa lengo la kumuomba aliye fanya tukio hilo ajisalimishe kabla awajaingia kumshambulia,bila ya kujua kuwa dereva alipewa laani zilizo mfanya achanganyikiwe.
Babu nadya aliendelea kumpa matibabu mke wake bila ya kujari yanayo endelea huko nje,lakini mke wake hali ilizidi kuwa mbaya,kisha Babu nadya akamuuliza mke wake.
"Mke wangu naona hali yako inazidi kuwa mbaya kwa kunusuru maisha yako naomba nikupake hii dawa itakayo kufanya upone ilo jeraha kwa mda huu pia baada ya siku tatu ni lazima ufe,ila ahadi hii inaweza ikatimia au isitimiye kwani ikiwa sasa hivi ulitakiwa ufe basi baada ya siku tatu utakufa,lakini ikiwa sasa ilitakiwa upone na sio ufe basi utaendelea kuishi kama kawaida, vipi mke nikupake???"
Babu nadya alimuuliz swali mke wake huku mkono wake ukiwa umeshikilia unga unga mweusi ulio kwenye karatasi jeupe,aliokuwa ameuotoa kwenye begi lake.
je nini kitaendelea....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 17

ILIPOISHIA...............................
"Mke wangu naona hali yako inazidi kuwa mbaya kwa kunusuru maisha yako naomba nikupake hii dawa itakayo kufanya upone ilo jeraha kwa mda huu pia baada ya siku tatu ni lazima ufe,ila ahadi hii inaweza ikatimia au isitimiye kwani ikiwa sasa hivi ulitakiwa ufe basi baada ya siku tatu utakufa,lakini ikiwa sasa ilitakiwa upone na sio ufe basi utaendelea kuishi kama kawaida, vipi mke nikupake???"
Babu nadya alimuuliz swali mke wake huku mkono wake ukiwa umeshikilia unga unga mweusi ulio kwenye karatasi jeupe,aliokuwa ameuotoa kwenye begi lake.
je nini kitaendelea......................
ENDELEA NAYO...................
***
Mama nadya hapo ndipo alipoona mambo yanazidi kuwa magumu,kwani alicho kifanya kwa wakati huo ni kuwa mpole kwa frank kwani aliona frank anakinga ya kimataifa iliyo mfanya yeye kuanza kuona mambo yamebadilika.
"Dada mbona unawaza unafikiri njia ngani utakayo tumia kuniangamiza,hahahahaha alafu kingine nacho taka kukuambia dada mpenzi wangu sharifa,mchumba wangu huyo nilipatana naye pale pale chuoni,baada ya kuwa nimepatana naye tulianza mahusiano bila kujuana vizuri. cha ajabu yalikuwa nimajira ya usiku huku nikiwa kitandani kwangu sharifa alinitokea na kuniambia ya kuwa yeye ni jini kwakua nilikuwa nampenda hivyo sikuweza kuachana naye,matatizo yaliyo zidi pale chuoni kwa yeye binafsi aliweza kunipunguzia nguvu alizokuwa nazon ili niweze kuishi kwa amani maana mganga yeye alitukinga tu lakini sharifa aliweza kunipunguzia nguvu zake hivyo usijaribu hata kidogo kunifanyia huuni wa uchawi wa kizamani zamani maana nina uwezo wa kufikiria kitu ambacho mtu anakiwaza cha msingi kuwa makini."
Frank alimwambia maneno mengi dada yake yaliyo mfanya aanze kumuogopa frank,mama nadya hakuweza kumjibu kitu chochote frank hivyo mda wote alikuwa kimya na kushindwa nini cha kufanya,wakati mama nadya akiendelea kuwaza frank alivuja ukimy uliyokuwa umemtawala ghafla.
"Dada sasa hivi utaishi kwa amri yangu naomba uende kulala"
Bila ya mama nadya kumjibu kitu chochote frank,aliweza kupiga hatua za kuondoka mahali pale kwa lengo la kwenda kulala kama alivyo sema mdogo wake,baada ya kuwa mama nadya ameondoka eneo lile frank aliachia kicheko cha dharau.
"hahahahahhahhahha,yani kwenye huko wetu we tu ndo mchawi du yani kufikia kesho inatakiwa uwe umesha acha uchawi wako huo maana nachukia wachawi waliweza kuniharibia matokea yangu ya mwaka wa kwanza pale chuoni,mpaka kufikia tamati ya kuwafanya wazazi wangu wakate tamaa ya kunilipia pale chuoni kutokana na ubovu wa matokea yangu.nachukia sana wachawi."
Frank aliongea maneno hayo huku akionekana kulengwa na machozi yaliyo mfanya achomoe kitambaa chake kisha akaanza kupekecha macho yake kwa lengo la kufuta machozi yale yaliyokuwa yameanza kumlenga.
wakati frank akiwa kwenye sofa lile la pale seblen,aliweza kuvua soksi yake akabakiwa na kaushi,lango kuu la yeye kufanya hivyo ni kujiandaa kwa ajiri ya kulala kwenye sofa zile.
Hatimaye alifanikiwa kujiweka sawa kisha akapanda kwenye kochi na kuanza kuhuruhusu usingizi kuchukua nafasi huku pia mama nadya alishindwa kulala kutokana na msongo wa mawazo na kuhisi kuwa kama mda wa kuacha uchawi au lazima afe utakuwa umetimia
******
Baada ya kuwa mzimu wa baba umetupa taarifa ile mimi pamoja na mdogo wangu caro,tuliweza kupiga magoti nakuanzisha maombi huku wote tukiomba kwa pamoja,jambo liliyo pelekea judithi arudi eneo lile tulio kuwepo na kutoka chumbani mwake,judithi alianza kulia kwa uchungu mkubwa huku akiomba tumuache ataleta kila kitu chake ili tuweze kukichoma eneo lile.lakini ilikuwa kama anajiongelesha mwenyewe maana amna ambaye kati yetu alifikilia kuacha maombi na kumsikiliza judithi alichokuwa anasema.
Caro alikuwa anamuomba mungu huku machozi yakimlenga ila kwa upande wangu nilimuomba mungu huku nikiwa nimetulia na kwa imani thabiti iliyo fanya judithi azidi kulalamika yakuwa kuna moto unamchoma hivyo tusiweze kuendelea na maombi.
tuliendelea kuomba mpaka tukasikia judithi anaanza kulia kama mtoto,lakini kwa wakati huo hatukuwa na huruma hata kidogo juu ya judithi,tulicho kifanya ni kuendelea na maombi.
wakati tukiwa tunaendelea na maombi mimi pamoja na mdogo wangu tulimsikia judithi anatoka katika kile chumba tulichopo kwa kasi kisha baada ya mda kadhaa alirudi na baadhi ya vitu tulivyoweza kuvifahamu baada ya kuwa ameviweka chini,hatukutaka kuangalia ameweka nini upande wa chini,tuliweka msimamo juu zaidi ya maombi yetu na sio vinginevyo,maana tungesitisha maombi judithi angeweza kutushambulia kwa kasi maana angejua tayari tumeshajua kinachommaliza.
Tuliomba zaidi ya nusu saa kisha mdogo wangu Caro akatanguliza neno "AMEN"nami nikamfuata.
hatukuamini macho yetu baada ya kumkuta judithi ameshikilia kiberiti huku upande wa chini akiwa ameweka vitu mbalimbali vya kutisha vingine hatukuweka kuvifahamu lakini vingine tulivifahamu,tulifanikiwa kuona mkono wa mtoto mchanga,ilizi,shanga,na vingine vingi tulivyo shindwa hata kuvielewa ni vi nini,tukiwa tayari tumesha anza kuogopa huku tukitumia makalio yetu kurudi upande wa nyuma maana tuliona tukikimbia tunaweza kumalizwa na judthi maana alikuwa ameungua na moto mwili mzima uliyo fanya ngozi yake kuweka mabaka baka ya damu.
Judithi hakuweza kutuongelesha kitu chochote,aliweza kuwasha kiberiti chake kisha akachoma vitu vyote vilivyopo eneo lile,baada ya amevichoma alizungumza kwa nguvu tena kwa hisia kali sana.
"kwanzia leo naacha uchawiii sitaki tena uchawi sitakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii"
judithi aliongea hivyo kisha akatukimbili mimi pamoja na mdogo wangu.
"Naomba unisamee kwa mara pili nadya naomba"
judithi akiwa anatuomba msamaa huku akiwa analia,tulisikia jogoo anawika mara kadhaa jambo liliyo tushangaza.
"Caro mdogo wangu angalia kwenye simu yangu saa ngapi sasa hivi???"
kutokana na swali lile lilimfanya judithi kunyamaza na kuacha kuendelea kulia,baada ya kuwa caro amesha angalia ni saa ngapi alimjibu nadya kwa hofu kubwa.
"saa kumi na moja na nusu"
"sawa caro,judithi tumekusamehe na kwaheri...."
niliongea hivyo huku nikimaanisha,mimi pamoja na mdogo wangu tuliondoka na kumuacha judithi nyumbani kwake.
tulianza safari ya kurudi nyumbani huku tukihisi ya kuwa hata mama tunaweza kupambana nae kwa kutumia neema ya mungu.
je nini kitaendelea....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA..............
niliongea hivyo huku nikimaanisha,mimi pamoja na mdogo wangu tuliondoka na kumuacha judithi nyumbani kwake.
tulianza safari ya kurudi nyumbani huku tukihisi ya kuwa hata mama tunaweza kupambana nae kwa kutumia neema ya mungu.
je nini kitaendelea..........................
ENDELEA NAYO...............
*****
walinzi wa pale stend walizidi kuzunguka gari lile huku wakiendelea kutoa kelele na sauti kali sana kana kwamba wanahuakika Dereva yule aliyetoka mle ndani kwa kasi ya ajabu itakuwa kuna jambazi ameweza kumdhulu kwa siraha kali iliyo mfanya dereva achomoke mbio ndani ya Bus lile huku akiwa anapiga kelele na kukimbilia mahali pasipo julikana.hawakujua ya kuwa kazi yote ilifanywa na Babu nadya.kwa upande wa ndani wa Bus hilo, Babu nadya alikaa huku akiwa na majonzi makubwa ya kuhusu shabulio la ghafla aliyo lipata mke wake.kutokana na kuwa Babu nadya pamoja na mke wake uzee ulikuwa unawanyemelea hivyo waliona ya kuwa mwisho wao umeanza kufika. hofu kuu ya Babu nadya ilikuwa sio walinzi waliokuwa wamesimaa nje huku wakiendelea kutoa fujo za huku na kule,hofu yake kubwa ilikuwa je mke wake akifa je yeye hataishije ikiwa amemzoea mke wake pia anatamani kila mda aweza kuona tabasamu la mke wake.kwa uzuri wa mke wake japokuwa uzee nao haukuwa mbali naye lakini alikuwa na sifa za kila aina hivyo kufikia hatua ya mme wake ambaye ni Babu nadya kumuundia msemo wa kipekee"NISINGE KUPATA WEWE NINGEKUWA NIMESHA KUFA"
Babu nadya akiwa anaendelea kumkumbatia mke wake,huku damu za mke wake zikiendelea kutapakaa katika mavazi yake yaliyo kuwa chakavu.
mke wake alianza kujisikia mwepesi anghalau wa kusema neno.
"mme wangu navyo jisikia nahisi nitakuacha na upweke ila sitakufa mpaka nijue tamati ya mwanangu inaishia wapi???lazima nihakikishe nakufa huku nikiwa tayari nimesha lipiza kisasi cha mwanangu,"
kabla Bibi nadya ajaendelea kuongea macho yake yalibadilika na kuwa mekundu kisha yakaanza kutoa damu,jambo liliyo fanya Babu nadya kupiga kelele huku akitamka neno liliyo mfanya azidi kuongeza sauti ya kulia na ya uchungu zaidi.
"mke wangu kwa nini hukusema nikupakee hii dawa mke wangu na unajua hii dawa huwezi kumpaka mtu bila hiali yake mke wangu ona sasa unakufa unaniachaaaaaaaa"
Babu nadya alianza kulia kama mtoto kitendo kilicho fanya machozi yaanze kumtoka mfululizo,kwa sababu babu nadya alikuwa na dawa tena tishio inayoweza kummaliza mtu bila ya mtu huyo kusikia maumivu yoyote,Babu nadya aliweza kumeza dawa zile kwa lengo la kujiuwa ili amfuate mke wake huko huko alipoenda.
Baada ya kuwa Babu nadya amemeza dawa ile ya kienyeji iliyoonekana kama tawi la mti flani. hapo hapo alidondoka chini na kupoteza maisha,na kumlalia mke wake ambaye na yeye tayari alikuwa amesha kufa,kwakuwa mashart ya ile dawa walio kuwa wamepaka walikuwa tayari wameyavunja kwakuwa hutakiwi kumwaga damu hata kidogo hivyo Babu nadya na Bibi nadya waliweza kumwaga damu kitendo kilicho fanya miili yao kuonekan na watu wote,kwa upande wa nje wa Bus hilo walinzi walijipanga kisha wakaingia ndani ya Bus hilo,huku wote wakiwasha tochi zao,kutokana na mwanga mkali wa tochi zao iliwafanya waweze kuona miili ile ya Babu nadya pamoja mke wake huku wakiwa wamepoteza maisha,kilicho wafanya walinzi wale wagundue ya kuwa Babu nadya pamoja na mke wake ni watu walio poteza maisha,hii ni kutokana na kuwa miili yao ilikuwa imetakapaa damu.tukio lile lilikuwa la kimaajabu kwani hawakujua nani amewauwa watu wale,ila kwa akili ya haraka haraka kutokana na mavazi ya Babu nadya pamoja na Bibi nadya yaliyo kuwa chakavu,hivyo walinzi wale waliwachukulia kama machokolaa walio kuwa wanatafta sehemu ya kulala pia kwa fikra za walinzi hao waliweza kugundua ya kuwa baada ya kuwa dereva amewauwa hakuweza kuamini hivyo ndo maana akaanza kukimbia ili tusiweze kumkamata.
Kifo cha Babu nadya pamoja na Bibi nadya kiliumiza mzimu wa Baba nadya kwani aligundua ya kuwa Baba yake amesha kufa hivyo anakuja sehemu ya mateso kama ile,alimuomba mungu haweze kuwaepusha wazazi wake wasiweze kuja mahali alipo maana alijua shida ya sehemu alipo maisha ya kushindia nyama za binadamu pamoja na damu.
walinzi wale walichukua miili ya wazee wale,kisha wakaipeleka police kwa lengo la kutoa taarifa,kutokana na maelezo ya walinzi wale iliwafanya askari washughulikie suala la kuzika ile miili wenyewe pia wakafungua kesi kwa yule dereva ya kuwa ameuwa bila ya kukusudia.
police waliweza kumtafta kila mtaa na kufanikiwa kumpata yule Dereva akiwa katika jalala kuu huku akiwa amechanganyikiwa na kuchafuka mwili mzima,askari hawakujari ilo,waliweza kumchukia dereva yule kisha wakampeleka mahakamani kwa ajiri ya hukumu,kutokana na kuwa dereva yule alikuwa amechanganyikiwa hivyo aliweza kusema yeye ndo ameuwa,jaji alitoa hukumu ya kuwa dereva yule afungwe kifungu cha miaka 30 jela,dereva akushangaa kusikia kitu kama hicho kitu alicho sema ni kimoja.
"ahsante sana jaji nilikuwa sina sehemu ya kulala hahahahahahaa mungu akubariki"
je nini kitaendele....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 19

ILIPOISHIA........
police waliweza kumtafta kila mtaa na kufanikiwa kumpata yule Dereva akiwa katika jalala kuu huku akiwa amechanganyikiwa na kuchafuka mwili mzima,askari hawakujari ilo,waliweza kumchukia dereva yule kisha wakampeleka mahakamani kwa ajiri ya hukumu,kutokana na kuwa dereva yule alikuwa amechanganyikiwa hivyo aliweza kusema yeye ndo ameuwa,jaji alitoa hukumu ya kuwa dereva yule afungwe kifungu cha miaka 30 jela,dereva akushangaa kusikia kitu kama hicho kitu alicho sema ni kimoja.
"ahsante sana jaji nilikuwa sina sehemu ya kulala hahahahahahaa mungu akubariki"
je nini kitaendele..............
ENDELEA NAYO..........
yalikuwa ni majira ya saa mbili asubuh mama nadya aliamka huku akionekana kuchoka sana na hii ni kutokana na kuwa alikuwa na msogo wa mawazo juu ya mdogo wake frank aliyekuwa anamuumiza kichwa sana na kumfanya ashindwe cha kufanya abaki tu kuwaza na kumuomba mungu aweze kumsaidia ili aweze kumuuwa mdogo wake frank,mama nadya hakukosa wazo kila mda alipofikiria alikuwa akipata wazo jipya,hapo ndipo alipo ona kuna maana kubwa ya kuwaita wachawi wenzake,aliweza kushika kibuyu chake kisha akakipuliza na kutamka maneno ya kichawi yaliyo fanya kundi kubwa la wachawi kujaa ndani ya kile chumba huku wakiwa pungufu huku wenginne wakiwa na majeraha kadhaa wa kadhaa, kitendo kilichokuwa kinamshangaza mama nadya baada ya kuona mabadiliko makubwa katika kundi lile la wachawi ni baadhi ya wachawi kuja tofauti na muonekano wa kichawi na kuja kawaida kama binadamu wa kawaida.mama nadya akiwa bado anaendelea kufikiria yale mabadiliko ya ghafla, mkuu yule wa wachawi aliyenusulika kuuwawa na Babu nadya huku akiwa kipindi akiwa chini ya mama nadya alisimama kisha akaanza kuzungumza.
"mkuu utatuwia ladhi pia umetuita kwa ghafla kuja hapa,ila sio vibaya cha muhimu unavyo tuona hapa kuna baadhi ya washilika mwenzetu wamesha poteza maisha na hii ni baada ya kuwa umetutuma tumuuwe mkwe wako,sasa basi kuna baadhi ya wachawi hapa kama unavyo waona hawajaja hapa kwa muonekano wa kichawi kuna yule pale na huyu hapa na pia na huyo wa pembeni yako wamekuja kujihudhuru na uchawi pia hata mimi mkuu nimekuja kujihudhuru na uchawi maana nahisi nimetenda dhambi kwa kosa la kumuingilia dereva wa lile Bus la EXPRESS kwa nia ya kukwepa lisasi ya kichawi iliyokuwa imepigwa na Babu nadya lakini kutokana na tukio hilo lilinifanya nikae kwenye mwili wa dereva huyo mpaka majira ya usiku,ilipofika majira ya usiku niliweza kumsukuma dereva yule kwa kutumia nguvu za kichawi huku nikiwa bado nipo ndani ya mwili wa huyo dereva, mpaka akaenda kumkata Bibi nadya kitendo kilicho fanya apoteze maisha kisha nikatoka ndani ya mwili wa dereva huyo,baada ya kuwa nimetoka nilishuhudia dereva akifanywa na Babu nadya kuwa kichaa,pia hata Babu nadya alijiuwa palepale kwaiyo nahisi nimetenda dhabi nahitaji kumrudia mungu ili apate kunisamee dhambi zangu"
Baada ya kuwa mchawi yule amemaliza kuongea mchawi mwingine alidakia,
"Mkuu kwa mimi kama mimi siwezi tena kuwa mchawi kwani nimeona hauna faida mkuu,mda tunao tumia kuwalonga wenzetu wenyewe wanazidi kupiga hatua na kufanya maendeleo makubwa kwenye nchi hivyo nimeona pia hata mimi nadhani nchi inanitegeme,mkuu kipindi nilikuwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuwa mwalimu wa Sekondary na sikuwa na ndoto ya kuwa mchawi hivyo nahitaji nitimize ndoto yangu"
Baada ya kuwa wachawi wale wameongea mambo mengi yaliyo mfanya mama nadya kuinamisha kichwa chini.ghafla Frank aligonga mlango wa Dada yake huku akimuomba afungue na wala hasiwaruhusu wachawi kuondoka,kutoka
na na kuwa mlango wa mama nadya ulikuwa ujafungwa vizuri na hii ni kutokana na kuwa usiku mama nadya alikuwa na mawazo hivyo hakuweza hata kufunga mlango kutokana na mawazo yaliyo kuwa yamemtanda kila sehemu ya mwili hivyo ilimpa nafasi Frank ya kuingia ndani bila ya kukalibishwa na mtu.
*****
Kwakua tulikuwa tuna njaa sana mimi pamoja na mdogo wangu hivyo tuliweza kwenda M-PESA kisha nikatoa hela ili tuweze kupata chakula cha usubuh katika mgahawa uliokuwa karibu na sisi,nilifanikiwa kutoa kiasi kadhaa kwa ajiri ya kupata chakula cha asubuh,tuliweza kutoka pale M-PESA huku tukiwa tunafuraha kwani hata sisi hatukujua furaha hiyo imetoka wapi,ila kwa upande wetu tulingua kilicho tufanya sisi ni kuwa na furaha ni baada ya kuwa tumefanikiwa kupambana na mchawi kwa kutumia nguvu ya mungu.
Tulipiga sentimita kadhaa kisha tukafanikiwa kuuona mgahawa ulio kuwa umeandikwa bango kubwa liliyo onekana vyema.tukiwa tunazidi kupiga hatua ili tuweze kuufikia mgahawa hule,caro aliaanza kusoma maandishi yale kama mtu anaye jifunza kusoma"MAMA JAMES MGAHAWA"
Hatukuchukua mda tulikuwa tayari tumefika katika mgahawa hule,huku moyoni tukijua ya kuwa sisi ndiyo tutakuwa wateja wa kwanza katika mgahawa hule,baada ya kuwa tumeingia tulikaribisha na mama aliyoonekana kuwa mtu anaye penda ugomvi na hii ni kutokana na kuwa alikuwa na makovu mengi mwilini mwake,aliweza kutuangalia kwa jicho la wizi wizi kisha akatukaribisha kwa sauti iliyo jaa besi ndani yake.
"Karibuni"
tuliitikia kwa pamoja kisha nikaamuuliza caro.
"caro utakula nini???"
"chochote kile utakacho nichagulia dada yangu"
"sawa"
Nilimuuliza mama yule aliyo onekana kuendelea na shughuli zake za upishi huku akionekana kuwa yuko mwenyewe katika mgahawa ule.
"Mama samahan.kuna nini na nini???"
"kwa sasa mdogo wangu vilivyopo ni chapati,mahalagwe,chai ya maziwa na ya rangi,maana si unajua bado asubuh kwaiyo bado sijapika vyakula vingine"
"hebu samahan mama nitajie na bei kabisa si unajua sasa hivi tunakula kwa bei"
"Dada kuhusu bei ondoa shaka,chagua unavyo vihitaji ntakuambia na bei,pia naomba mkanawe pale kisha mje kukaa"
je nini kitaendelea....

UCHAWI WA MAMA SEHEMU YA 20

(MWISHO)
ILIPOISHIA................
Nilimuuliza mama yule aliyo onekana kuendelea na shughuli zake za upishi huku akionekana kuwa yuko mwenyewe katika mgahawa ule.
"Mama samahan.kuna nini na nini???"
"kwa sasa mdogo wangu vilivyopo ni chapati,mahalagwe,chai ya maziwa na ya rangi,maana si unajua bado asubuh kwaiyo bado sijapika vyakula vingine"
"hebu samahan mama nitajie na bei kabisa si unajua sasa hivi tunakula kwa bei"
"Dada kuhusu bei ondoa shaka,chagua unavyo vihitaji ntakuambia na bei,pia naomba mkanawe pale kisha mje kukaa"
je nini kitaendelea.................
ENDELEA NAYO.............
Tuliweza kutoka nje na mdogo wangu kisha tukanawa na kurudi mgahawani.
"Dada tuletee chai ya maziwa vikombe viwili,chapati nne na mahalagwe vibakuli viwili,jumla.itakuwa shingapi???"
"elfu tatu"
"sawa tuletee"
mama yule alikuwa shapu japokuwa aliluwa mwenyewe aliweza kuleta kama tulivyo mwangiza kisha nikamchomolea noti ya shilingi elfu kumi.
"heee yote hii asubuh yote hii"
" mmmh mama yangu ndo hiyo tunayo!!!!"
"sawa nipe dakila moja"
mama yule aliweza kuondoka katila eneo lile huku akiwa anakimbia mithili ya mwanaume japokuwa yeye alikuwa ni mwanamke,jambo lile lilimfanya caro aachie kicheko kisha akaanza kula,na.pia niliweza kufanya hivyo kama alivyo fanya.
Tulikula kwa haraka ili tuweze kuondoka na kufika nyumbani mapema,wakati tukiwa tunaendelea kula alingia kijana mmoja katika mgahawa huo huku akiwa ameshikilia panga katika mkono wa kulia huku mkono wa kushoto alikuwa ameshikilia gazeti,bila kutuongelesha kitu chochote aliweza kuweka gazeti lile mezani kisha akaenda mahali wanaponawia wateja.
tukiwa tunaendelea kula niliweza kulitazama gazeti lile na kushindwa kuamini kwa nilicho kiona,maana niliona watu niliyoweza kuwafahamu kama Babu yangu pamoja na Bibi yangu wakiwa wamekufa huku kichwa cha habari kikiwa kimeandikwa"DEREVA AWAUWA ABIRIA WAKE"
kutokana na jambo lile lilinifanya hamu ya kula ikapotea kisha nikamshika mdogo wangu huku nikimsihi tuondoke.
"Dada mbona umebadilika hivyo si tusubiri chenchi"
"amna mdogo wangu we twende"
caro alishindwa kuelewa ni kitu gani kilicho ni kumba ghafla na kunifanya nibadilike kwa mdaa mfupi,lakini sikutaka kumwambia ukweli kwani hata mimi sikuwa na ukweli,wakati tukiwa tunazuzana huku jamaa yule aliye kuja na gazeti akiendelea kutushangaa niliita bajaji italkayo tupeleka nyumbani.
****
frank alifanikiwa kuingia hadi ndani kitendo kilicho fanya wachawi wamkodolee macho,Frank nae hakutaka kuona aibu hata kidogo nae aliweza kuwakodolea macho wachawi wale kisha akazungumza.
"nyie wachawi poteeni hapa fasta"
"we kijana sisi tumeacha uchawi ingekuwa hatujaacha tungekuuwa maana unaongea bila adabu"
mkuu yule wa wachawi aliongea huku akinyooshea kidore frank jambo liliyo fanya frank akasilike kisha akamnyooshea kidore mchawi yule huku akisema nakupa onyo,ghafla mchawi yule aliaanza kujinyoonga mwenyewe kitendo kilicho fanya wachawi wote kupotea eneo lile kasoro mama nadya yeye alionekana.kujikinga na mto mda wote.
mchawi yule alijinyonga mpaka ikafikia hatua akaanza kulia.
"nisamee nisamee"
Frank aliacha kumnyonga kisha mchawi yule akapotea eneo lile jambo liliyo fanya mama nadya aanze kulia kama.mtoto pia asiamini yaliyo kuwa yanaendelea.
wakati mama nadya anataka kuzungumza mlango wake ulibishwa kisha nadya na caro wakaingia huku wakionekana kuchakaa mithili ya mtu anaye mwenye mashetani,nadya na caro waliweza kupiga hatua kisha wakakaa chini huku wakimshuhudia ndugu yao frank.akiachia tabasamu la furaha kwa kuwaona.
nadya aliweza kumsalimia frank kwani alishawai kuonyesha na na Baba yao picha ya frank hivyo aliweza kumfahamu kama mjomba wake ila kwa upande wa caro alikuwa hamfahamu kabisa.
"shikamoo mjomba"
"marahana nadya"
"shikamoo mjomba"
"marahaba caro"
Baada ya kuwa nadya na caro wametoa salamu zile waliweza kumuangalia mama yao kwa jicho la hasira ma chuki,kisha frank akazungumza.
"Nadya na caro mama yenu ambaye ni dada yangu ni mchawi na nataka.atubu mbele zenu kisha achome kila tunguri lake kisha hawarudishie baba yenu"
"Baba yetu???baba yetu atarudije wakati amesha kufa"
"amna nadya we uliwai kuona mazishi ya baba yako au mwili wake???"
"hapana"
"basi kuwa mpole"
Mama nadya bila kuongea kitu chochote aliweza kuchukua tunguri analo tumiaga kuwaita wachawi wenzake kisha akatamka maneno anayo yajua yeye mwenyewe baada ya dakika kadhaa Baba nadya alitua eneo lile,kisha mama nadya akazidi kutamka maneno yale ghafla ten Bibi nadya akatua pale pamoja na Babu nadya,kisha akazungumza huku wakiwa na mawazi yenye udongo pia afya zao zikiwa zimedhohofika.b
aada ya kuwa mama nadya amemaliza kufanya tukio ilo la ajabu alianza kuzungumza huku akiwa amempigia magoti mme wake,wakwe zake,mdogo wake pamoja na mdogo wake.
"Frank mdogo wangu,baba mkwe wangu,mama mkwe wangu pamoja na watoto wangu naomba mnisamee,maana niliweza kuwatunza uzimuni kwetu ili.mwezi ujao tuweze kula nyama zenu lakini nimegundua ya kuwa mugu ndio kila kitu naombeni mnisamee"
kwakuwa mama nadya aliongea kwa majozi makubwa huku akiwa analia wote waliweza kumsamehe ila kwa mashart ya kuwa anatakiwa achome kila tunguri lake pia atoe ushuhuda katika makanisa mbalimbali.
baba nadya aliweza kuwashukuru watoto wake pamoja na Frank maana bila wao wasingeweza kurudi duniani,pia Babu nadya pamoja na.Bibi nadya waliweza kurudi kijijini na maisha yakaendelea kama kawaida.
MWISHO..........
ASANTENI SANA KWA KUWA WAFATILIAJI WANGU WAZURI,
NAWASHUKURU VYOTE


COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UCHAWI WA MAMA
UCHAWI WA MAMA
https://1.bp.blogspot.com/-tgN2AIjo28w/XXdwf6a321I/AAAAAAAACzI/6f-aYqGA-dge766tFR2kX-byCzpheNgBACLcBGAs/s320/UCHAWI%2BWA%2BMAMA.%2B1.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-tgN2AIjo28w/XXdwf6a321I/AAAAAAAACzI/6f-aYqGA-dge766tFR2kX-byCzpheNgBACLcBGAs/s72-c/UCHAWI%2BWA%2BMAMA.%2B1.jpg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/uchawi-wa-mama.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/uchawi-wa-mama.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content