SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI

🌷🌷🌷 KISA CHA KUTUNGWA, CHA MAPENZI 🌷🌷🌷 
           "SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI "

🌷🌷 "Una matatzo gani wewe? Sikukwambia mimi ufue shati langu la blue? Yaani kila siku wewe ni kusahau tu" akamkoromea mkewe.
Mke akatazama pembeni. "Samahani, nilisahau kabisa kama kuna shati la kufua". Mke akaongea huku akimpa mumewe tai nyekundu.
Mume akapokea kwa kuikwapua huku akionekana dhahiri kukasirika.
"Sipendi namna unavyoongea na mimi" mke akamwambia mumewe.
"Unamaamisha nini? Zungumza ueleweke wewe mwanamke. Sina muda hapa, nachelewa ofisini kwangu". Mume akafoka.

🌷🌷 Mke akakaa kitandani na kusema, "nenda tu kazini mume wangu".
Mume akashusha pumzi na kukaa kitandani karibu na mkewe.
"Nini kinakusumbua mke wangu?" Mume akamuuliza kwa upole kidogo.
"Hivi mim ni mke wako kweli?" Mke akauliza.
"Unawezaje kuniuliza hivyo? Umeanza lini upumbavu?" Mume akafoka tena.
Mke akamtazama tu mumewe huku akiwa kimya.
"Hiyo ndio sababu. Hebu angalia namna unavyoongea na mimi" mke akaongea zaidi.
"Kimsingi hauongei na mimi bali unaniamrisha. Unanikaripia, unanipa oda utafikiri meja wa jeshi kwa kuruta. Tokea lini wewe umekua bosi wangu? Wewe ni mume wangu na wala sio mkuu wangu...

🌷🌷 ...Nakusikia ukiyatumia maneno kama vile 'samahani', 'tafadhali' na 'pole' kwa wafanyakazi wenzako; lakini kwangu sikumbuki ni lini uliyatamka hayo maneno. Je kuwa mke wako ndio inamaanisha mimi ni mtumwa na nastahili kuhudumiwa hovyo hovyo na mume wangu?" Mke akatazama chini na kuendelea..
"Unaniabisha mbele za watoto na majirani, unaninyanyasa na kunipa amri utafikiri mtoto wa sekondari. Mimi ni mwanamke wako, mke wako, nijali basi kama msaidizi wako. Ona hua huniangalii hata machoni unapoongea na mimi. Je natia kinyaa hata sistahili kuangaliwa usoni?

🌷🌷 ...Unao muda na marafiki zako kila siku lakini kwangu huna muda, muda ulio nao kwangu ni pale unapotaka tendo la ndoa tu..na hapo ukimaliza hujali kama mimi nimeridhika ama laa unageuka upande wa pili..hakuna maongezi, hakuna mapenzi..najichukia kwa kweli! Mke akamtazama vizuri mumewe...Na kuendelea..
"Unapotaka kunipa kitu hunipi mkononi, unanitupia kama mbwa. Ukiangusha kitu mimi ndio wa kukiokota huku wewe ukiwa umekaa umeweka miguu juu ya meza...
...Tukiwa tunaenda mahala hautaki kutembea karibu na mimi, natembea nyuma yako, 

🌷🌷 je sina thamani ya kutembea na wewe? Umejaza rekodi na kumbukumbu ya mapungufu yangu na kila siku unayakumbushia, kwaio mimi sina zuri hata moja?
...Yuko wapi mwanaume aliekua ananijali, ananisikiliza na kunipenda? Je amefariki baada tu ya kuingia kwenye ndoa? Bado nahitaji huduma yako nzuri mume wangu, haswa wakati huu tukiwa na watoto. Onesha kunihitaji nami nitakupa mambo matamu tutakayoyafurahia sote kwa pamoja hata kwenye tendo la ndoa.
...Niite majina matamu kama zamani, usiniite 'mwanamke' sijali sana kuhusu kukuhudumia ila nahitaji heshima. Nahitaji unifanye nijisikie ni mpenzi wako.

🌷🌷 Nikubali, kuwa mpole kwangu, ukali wako unaniogopesha kuliko hata nilivyokua namuogopa baba yangu. Mimi sio housegirl. Ni mke wako ndani ya nyumba hii.
Mke akashusha pumzi na akamtazama mumewe baada ya kuongea yote ya moyoni mwake...mume hakuongea kitu. Mume akachukua simu yake na kupiga baadhi ya namba. Pamoja na kumueleza yote hayo lakini bado amempotezea na kuchukua simu yake..Mke akajisikia vibaya sana. Mke akasimama ili aondoke huku machozi yakimtoka, lakini mume akamshika mkono na kumrudisha kitandani huku akisikiliza simu aliyopiga.

🌷🌷 Mume akaanza kuongea, "Hallo, tafadhali ahirisha kikao tufanye kesho, nimepata dharuka kidogo. Kuna jambo la kifamilia nashughurika nalo". Akakata simu.
Mume akamuona mkewe akitabasamu. Akamkumbatia mkewe na kumbusu mdomoni.
"Nisamehe mpenzi wangu, sikua nafahamu kama nakuumiza. Je nikupe offer ya kukutoa lunch leo? Kuanzia leo na kuendelea, nitakuhudumia vizuri kama vile unavyotamani. Mumeo nimerudi sasa !!!

NOTE: 
πŸ•‹πŸ•‹ Mwanamke jifunze kuongea kwa upole endapo kuna jambo haulifurahii na linakuumiza juu ya mwenzako, ni nadra sana kwa mwanaume kuwa mgumu kwa mwanamke anaenyenyekea

πŸ•‹πŸ•‹ Dada na mama zetu majumbani munajisahau san kuna wakat ni kweli mnakumbwa na changamoto za mfumo dume au ukali uliopitiliza kutoka kwa waume zenu hadi ndoa zinakuwa chungu cha msingi tambua kila mwanadam na kasoro zake.

πŸ•‹πŸ•‹ Zibadili kasoro hizo kwa uwezo wako au ukishindwa ishi kulingana na kasoro hizo ingawa itakuwa ni udhaifu, pambana na kasoro hizo usikubari zikushinde, zibadili ili ndoa irejee ktk amani.

πŸ•‹πŸ•‹ Mimi ostadhi pongwer nakushauri kuna wakat, pindi unataka kutoa yako ya moyoni kumbuka kutafuta na kuchagua njia sahihi ili kero yako ifike pahala usika na iweze kufanyiwa kazi.

πŸ•‹πŸ•‹ Tumia upole wako kama mwanamke na lugha mzuri usiwe kama moto...lugha mzur na laini humshusha mwanaume yeyote aliyeko juu. Na ili maneno yaingie moyon namna sahih ni kupangilia mawazo na hisia zako za uongeaji.

πŸ•‹πŸ•‹ katu usitake kumbadilisha mmeo kwa msindo wa kitchen partyπŸ˜† usimsute mmeo utaharibuπŸ‘Œ jishushe ongea kwa upole ikiwezekana hata kutoa chozi πŸ˜† weka hata pilipili machoni ilimrad machozi yatoke ujumbe ufike sawasawa inshaallah dada na mama zangu mukifanyie kazi kisa hiki na jumbe hii ili tuijenge familia bora...tuseme amiiin.... 

  "SIRAHA KUBWA YENYE KULETA HURUMA YA MWANAUME 
          KWA MKEWE NI UPOLE NA UNYENYEKEVU WAKE" 

                               πŸŒ·πŸŒ·WABILLAH TAWFIQ🌷🌷

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI
SIPENDI NAMNA UNAVYOONGEA NA MIMI
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/sipendi-namna-unavyoongea-na-mimi.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/sipendi-namna-unavyoongea-na-mimi.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content