SABABU ZA KIZUNGUZUNGU

Moja ya malalamiko ya kiafya yanayowaleta watu hospitalini ni kizunguzungu. Kizunguzungu ni hali ya kuhisi kama vile vitu vilivyoko karibu nawe vinazunguuka (vertigo) au kusikia kichwa chepesi au kukosa uwiano (balance) na kujikuta mtu anapepesuka. Kwa aliyelala atahisi kitanda kinayumba yumba au kuzunguuka.
Kwa kuwa na kizunguzungu kunaweza kukaathiri shughuli zako za kila siku. Lakini pia ni mara chache sana kizunguzungu kikawa ni dalili za tatizo linalo hatarisha maisha.

Watu wanaopata kizunguzungu wana namna mbalimbali za kuelezea dalili zake, mfano:
Kuhisi kama kichwa au mwili mzima unazunguuka
Hali ya kujisikia kama unataka kupoteza fahamu au kichwa kuwa chepesi
Kukosa balance
Kuhisi kama unaelea angani au kwenye maji

Dalili za kizunguzungu                                            

Dalili hizi zinaweza kuanza mara baada ya mtu aliyekuwa amekaa akaamka kiasi cha kumfanya atulie kwanza kabla ya kuanza kutembea, au aliyesimama anapotembea, au kugeuza kichwa.
Hali ya kizungunguzu mara nyingi huambatana na kichefuchefu. Kizunguzungu kinaweza kudumu kwa sekunde au hata wiki kadhaa na kinaweza kujirudia rudia baadae baada ya kutulia kwa muda fulani

Sababu za kwenda hospitali

Inashauriwa kumuona daktari utakapoona dalili zinajirudia rudia, au unapopata kizunguzungu ambacho ni cha ghafla na kikadumu kwa muda mrefu. Pia kikiambatana na dalili zifuatazo:

 • Maumivu makali ya kichwa
 • Maumivu ya kifua
 • Kupumua kwa shida
 • Ganzi ya ghafla au kupooza kwa miguu, mikono au usoni
 • Kupoteza fahamu
 • Kuona maruweruwe (double double)
 • Mapigo ya moyo kwenda mbio na au kupiga ovyo ovyo bila mpangilio
 • Kuchanganyikiwa au kuongea kwa shida
 • Kutapika kusikokoma
 • Kujikwaa kwaa bila sababu au kutembea kwa shida
 • Degedege
 • Kutosikia vyema kwa ghafla

Chanzo cha kusababishi kizunguzungu


 • Ziko sababu kadha wa kadha zinazoleta kizunguzungu kama matatizo ya masikio, athari za kusafiri, dawa, magonjwa kama Malaria, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, Kisukari, na ajali. Jinsi kizunguzungu kinavyokufanya ujisikie au mambo yanayofanya kianze au muda kinaokuwepo na dalili zingine zinazoambatana nazo, vyote hivyo hutoa mwanga kwa daktari kujua chanzo.
 • Matatizo ya viuongo vya ndani vya sikio.
 • Uwiano (balance) anaokuwa nao mtu aliye mzima na kumwezesha kutembea bila kupepesuka unatoka na kazi ya viungo mbalimbali vya hisia vya mwili wa binadamu. Viungo hivi ni:
 • Macho, kazi yake ni kukuwezesha kujua uko wapi na unatembeaje au kosogea.
 • Mishipa ya fahamu, kazi yake ni kupeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mwendo na mwili ulipo
 • Sehemu ya ndani ya sikio, Sikio lina sehemu kuu tatu, sehemu ya nje ambayo tunaiona kwa urahisi, sehemu ya kati ilipo ngoma ya sikio, na sehemu ya ndani kabisa ya sikio ambayo ni baada ya ngoma, hii huwa hatuioni kwa macho. Sehemu ya ndani kabisa ya sikio ina viuongo ambavyo vinatusaidia kupata uwiano (balance) wa mwili kwa kusaidiana na viungo vingine nilivyovitaja hapo juu. Husaidia kujua nguvu za uvutano (gravity) na kukufanya ujue kama unaenda mbele au unarudi nyuma.
 • Kizunguzungu cha kuhisi vitu vilivyoko karibu nawe vinazunguuka kitaalam Vertigo (inatamkwa Vetaigo). Hii husababishwa mara nyingi na matatizo ya masikio ambapo viungo vilivyo kwenye sehemu ya ndani ya sikio (Inner Ear) kupeleka taarifa zisizo sahihi kwenye ubongo na hizo taarifa zinakuwa haziwiani na zile ambazo macho na mishipa imepokea. Unapata aina hiyo ya kizunguzungu kwakuwa ubongo unakuwa busy kujaribu kupata ukweli halisi wa hizi taarifa. Aina hii ya kizunguzungu huletwa na magonjwa yafuatayo:
 • Kizunguzungu kisichofahamika chanzo (Benign Paroxysmal Positional Vertigo) – Kizunguzungu hiki hakina athari kubwa kwa maisha ya muhusika. Aina hii ya kizunguzungu hakifahamiki chanzo chake (idiopathic), kwa lugha nyepesi tungesema cha kuzaliwa nacho. Hutokea pale mtu anapobadili mkao ghafla; kuamka na kukaa kitandani ghafla au kusimama ghafla kwa mtu aliyekuwa ameketi. Pia kugeuza au kuinamisha au kuangalia juu haraka.
 • Uambukizo; Mishipa ya fahamu ya sehemu ya ndani ya sikio inapopata uambukizo wa aina fulani ya virusi na kusababisha kizunguzungu na wakati mwingine hata kutosikia sawa sawa.
 • Kujaa kwa majimaji sehemu ya ndani ya sikio (Meniere’s disease); hapa tunamaanisha maji yanayotengenezwa ndani ya sikio kwasababu fulani fulani huzidi kiwango kinachokubalika na kusababisha kizunguzungu ambacho hudumu kwa masaa kadhaa. Pia huleta kuziba na kuzibuka kwa masikio, sauti za kengele na kuhisi kama vile sikio limezibwa kwa pamba.
 • Kipanda uso (Migraine). Watu wanaopata matatizo ya kipanda uso hupata pia kizunguzungu hata kama kwa wakati huo kichwa hakiumi. Kizunguzungu wanachopata hawa huwa kina dumu kwa dakika hadi saa kadhaa na kupotea. Pia wanakuwa na hali ya kutotaka makelele, sauti ndogo wao huhisi ni kelele kubwa sana.
 • Matatizo ya mzunguuko wa damu unavyoweza kuleta Kizunguzungu
 • Kushuka kwa shinikizo la damu (Low Pressure). Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kunaleta kizunguzungu cha muda mfupi. Hali hii inaweza kutokea iwapo utasimama ghafla kama ulikuwa umeketi au kuamka na kuketi kitandani ghafla. Kubadilika kwa mkao wa mwili huku kunasababisha shinikizo la damu lishuke ghafla kwani mwili unakuwa haujapata muda wa kujiweka sawa.
 • Matatizo ya kutozunguuka vyema kwa damu; huku kunatokea kwa watu wenye magonjwa ya moyo kuwa mkubwa (Cardiomyopathy), shambulio la moyo (Heart attack), na mapigo ya moyo yaliyoparaganyika (Arrhythmia). Matatizo haya yote yanababisha moyo ambao ndiyo pump, kupungua uwezo wa kusukuma damu ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya mwili, ikiwemo ubongo na sehemu ya ndani ya sikio.

Sababu zingine zinazoleta kizunguzungu


 • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
 • Dawa zinazotumika kutibia matatizo mbalimbali yanaweza kuwa chanzo cha kizunguzungu. Mfano dawa za kuzuia degedege, dawa za sonona, na dawa za kutibu shinikizo la damu pia huwa ni sababu kwani kuna wakati hushusha shinikizo la damu kufikia chini ya kiwango.
 • Aina fulani ya magonjwa yanayomfanya mtu kuwa na wasiwasi kuliko kawaida huleta kizungunguzu.
 • Upungufu wa damu. Kupungua kwa wekundu wa chembechembe nyekundu za damu huleta kizungunguzu kwani kiwango cha hewa ya oxygen kinachozunguuka kinakuwa kidogo.
 • Kushuka kwa sukari. Hali hii huwapata watu wenye kisukari wanaotumia insulin ambayo inaweza kusababisha sukari kushuka sana. Pia hata wenye njaa kupita kiasi.
 • Joto kali na kupungukiwa maji. Joto kali husababisha kutokwa na jasho jingi hivyo maji mwilini kupungua na kuleta kizunguzungu.

Athari za kizunguzungu


 • Athari kubwa za kizunguzungu zinakuja pale ambapo kizunguzungu kinapoweza kusababisha muhusika kuanguka chini. Kitendo cha kuanguka kinaweza kuleta majeraha mbalimbali mwili kulingana na namna na mahala alipoangukia muhusika. Athari nyingine ni za kiuchumi na kijamii pale ambapo kizunguzungu kikiwa cha muda mrefu na kusababisha muhusika ashindwe kushiriki shughuli za kumuingizia kipato na za kijamii.
 • Utambuzi
 • Utambuzi wa matatizo yanayoleta kizunguzungu yatahusisha uchukuaji wa maelezo na kufanya vipimo ambavyo daktari ataona vinafaa.
 • Matibabu
 • Yatategemeana na chanzo kilichogundulika. Matibabu yanaweza kuhusisha dawa, upasuaji na mazoezi.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SABABU ZA KIZUNGUZUNGU
SABABU ZA KIZUNGUZUNGU
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/sababu-za-kizunguzungu.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/sababu-za-kizunguzungu.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content