LUTKAS (Kitabu CHA Uhai)

SIMULIZI: LUTKAS (Kitabu CHA Uhai)
MTUNZI: JAFARI MPOLE

LUTKAS (Kitabu CHA Uhai)

LUTKAS SEHEMU YA 01


Mvua kubwa ilipata kunyesha katika mji wa Newyork Marekani. Mvua iliyoambana na radi pamoja na ngurumo za kutisha hali iliyofanya baadhi ya watu waliokuwa ndani ya Hospitali ya Presbayterian kuingiwa na woga kwenye mioyo yao. Manesi na baadhi ya wazazi waliopo ndani humo walikuwa na kazi ya kufungwa madirisha vioo kusudi upepo mkali usipate kuingia ndani. Ni hospitali iliyokuwa ikihudumia watoto wenye magonjwa mbalimbali ndani ya mji huo hivyo kila mzazi aliyefika siku hiyo alihakikisha mwanaye anakuwa salama na kumtoa hofu juu ya radi na ngurumo zile zilizoambatana na mvua kali.
Katika wodi moja ya watoto, manesi wawili walikiwa na kazi ya kushirikiana na mwanamama mmoja ambaye binti yake alikuwa anapiga makelele kana kwamba amechamganyikiwa. Zoezi hili liliwafanya baadhi ya wagonjwa wengine waliokuwa kwenye vitanda vyao wakae kumuangalia mwenzao anavyozidi kuleta zogo mule ndani.
"Sasa tunamsaidia vipi binti huyu jamani maana hatuelewi alikuwa mzima gafla tu amebadilika na kuwa hivi?"aliuliza nesi mmoja akiwa amemshika mkono mtoto yule aliyekuwa anazidi kuleta tafarani.
"Punde atakuja msichana wangu wa kazi kuna kitu nimemuagiza alete haraka, nadhani itafanya mwanangu atulie."alisema mwanamama yule akiwa anamtazama mwanaye akiyeonesha kutetema mwili kwa hasira. Wale manesi waliposikia vile iliwabidi wasubiri hadi kujua hatma ya mtoto huyo inakuwaje. Mvua ilizidi kumwagika ardhini na kufanya hata hali ya hewa kuonekana giza angali ni Alasiri bado.
Dakina kadhaa mbele wakiwa wanaendelea kumtuliza binti huyo bila mafanikio aliwasili msichana wa mama huyo ambaye alimwona tu akanyanyuka na kumsogelea. Alikabidhiwa kitabu fulani na msichana yule, naye bila kuchelewa alikishika na kurudi hadi pale alipolazwa binti yake akiwa anazidi kufurukuta mikononi mwa wale manesi. Mama huyo alikinyanyua kitabu kile na kukilaza kwenye kifua cha binti hiyo. Gafla tu zogo lililokuwa likiendelea likatulia na binti yule akapata kuonekana amepoa kabisa na kukumbwa na usingizi mzito palepale. Mama mtu alishusha pumzi baada ya kuona mwanaye ametulia sasa. Aliwaacha manesi wale katika hali ya mshangao wasijue imekuwaje. Wakabaki wanakitazama kile kitabu kilichopo kifuani mwa binti yule aliyeonekana kuhema huku akiwa usingizini.
"Muacheni apate kupumzika kwanza, atakuwa sawa."alisema mama wa binti yule kisha akanyanyuka pale alipo na kutoka ndani ya chumba kile. Manesi wakawa wanamtazama yule msi hana aliyeleta kile kitabu akiwa anamuangalia binti wa bosi wake akiwa pale kitandani amelala. Ilibidi wafanye vile walivyoambiwa, walimuacha binti yule pale kitandani akiwa ameweka mkono wake kwenye kitabu kile.

Hakuwa na furaha mama muda wote mama wa binti yule, si mara ya kwanza wa mbili kwa binti yake kutokewa na hali ile. Alikumbuka siku moja mwanaye akiwa bado mdogo sana alimuweka mahala na kumuwekea vitabu vya kuchezea huku yeye akiendelea na kazi za jikoni. Siku hiyo alikuwa anaandaa chakula cha jioni kwaajili ya mumewe ambaye alikuwa safarini yapata miezi saba tangu kuondoka kwake na hakuweza kuonana na familia yake na siku hiyo ndio alikuwa akirejea. Muda wote huo akiwa zake anafanya mapishi hayo alikuwa akiwasiliana na mumewe kwa njia ya simu huku wakionana kwa kutumia mtandao, maongezi ya hapa na pale yaliendelea baina ya wanandoa hao.
"Umeshaliandaa jina zuri la kumpa mwanao? Maana hadi sasa zikuweza kumpatia jina lolote lile nakusubiri wewe baba yake, si unajua nafuata ahadi yetu."aliyasema hayo mama yule huku akiitazama simu yake kumuona mumewe akiwa kwenye ndege.
"Huwezi amini muda wote tangu naanza safari nawaza jina la zuri la utofauti nitakalompa mwanangu. Dakika tano tu nyuma nikapata kulichagua na naamini litafaa kwa mwanangu."alisikika baba wa familia hiyo akionekana mwenye furaha sana kwenye simu ya mkewe.
"Eh haya jina gani hilo umempa binti yako?"aliuliza mama yule akiwa anaweka chumvi kwenye mboga.
"Usijali nitakapofika nikakwambia."
"Hapana niambie sasa nianze kumwita mwanangu.alisema mama yule na kumfanya mumewe afurahi.
"Lutfia... ndilo jina nimelichagua kumwita mwanangu, ataitwa Lutfia.alisema baba yule na kumfanya mkewe afurahi kusikia vile. Alijikuta akiacha hata kupika pale na kwenda kumchukua mwanaye ambebe kwa furaha.
"Lutfia mwanangu baba yako amekupa jina zuri kama wewe... Mwaaaah!"ilikuwa nifuraha ya aina yake kwa mama huyo kumwita mwanaye kwa mara ya kwanza jina lake ambalo muda mfupi mumewe amepata kulitaja. Sauti ile ilimfanya hata mumewe kule alipo afurahi kusikia mkewe akilifurahia jina hilo. Punde tu mtandao ukakata wa mawasiliano katika simu. Kila aliyekuwa anawasiliana na ndugu zake waliona gafla mtandao unakatika katika na kusababisha kukosa kwa mawasiliano. Muda huo mvua kali ilikuwa ikinyesha huku ngurumo za radi zikiambatana kwa pamoja, hali hiyo ilileta tafarani hata kwa marubani waliokuwa wakiiongoza ndege hiyo kwani gafla mawasiliano baina yao juu na makao makuu kutoweza kuwasiliana kutokana na kutopatikana kwa mtandao. Kila wakijaribu jitihada zao lakini hali inakuwa mbaya maana hakuna hata mtambo unaoonesha muelekeo wa safari yako. Ndege ikawa ipo tu hewani inakwenda bila kujulikana inapoelekea. Haraka ika idi watoe taarifa kwa wahudumu wa ndege hiyo kuwaeleza hali halisi.

Abiria wote waliona tatizo lile huenda ni hali ya hewa tu hawakuyilia maanani sana na punde tu walipata kusikia Tangazo kutoka kwa wahudumu wa ndege hiyo kuwa kuna tatizo la mitambo upande wa marubani hivyo wanaomba watulie maana wanajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hilo. Kauli hiyo ndio ikawafanya sasa watu wachanganyikiwe na wengine wapate woga wa hali ya juu. Vilio vikaanza kusikika huku kila mmoja akimuomba Munvu kwa namna yake aweze kunusuru wapate kuwa salama wote. Baba Lutfia alipata hofu kuona ni mtihani unaompata kwake. Ni muda mchache tu amepata kuongea na mkewe na kushuhudia akiandaliwa chakula wapate kula pamoja. Alihisi huenda nafasi hiyo akaikosa maana tatizo hilo ni kubwa sana. Alikunja mikono yake na kumuomba Mungu asaidie kuweza kunusuru ndege ile.

Huku kwa Mama Lutfia alikuwa mwenye kupatwa kigugumizi haamini kile ambacho anakiona mbele yake. Muda wote alikuwa akimtafuta kwenye mawasiliano lakini mumewe hakuonekana kama yupo hewani. Alimtazama mtoto wake akiwa amemuweka pale chini huku ameshika kalamu, vitabu mbalimbali vikiwa mbele yake.
Jina la Lutfia liliandikwa kwenye kila kitabu kilichopo pale mbele ya mtoto. Hakuamini kama mtoto wake mdogo kabisa hata kusimama bado angeweza kuandika jina lake kwenye vitabu vyote, tena cha ajabu ni kwamba jina hilo limepatikana muda sio mrefu lakini ajabu mtoto huyo amelijua tena na kuliandika kabisa.

Kesho yake asubuhi mapema vyombo vya habari pamoja na media zengine mitandaoni zilianza kusambaza taarifa za ndege itokayo Nchini Kenya kuelekea Marekani imeanguka kwenye kijiji kimoja kilichopo msituni huko maeneno Madagasca na huzuni ni kwamba hakuna aliyepona kwenye ajali hiyo, hii ni kutokana na ndege kuweza kulipuka pindi ilipofika chini kwa kasi kama ilivyoelezwa na wenyeji wa visiwa hivyo. Watu wengi ambao ndugu zao walipatwa na ajali hiyo walihuzunika sana baada ya kupata taarifa hizo. Zoezi la kuokoteza mabaki ya vitu vilivyosalia kwenye mlipuko wa ndege huo liliendelea na maaskari wa upelelezi na usalama. Ilichukua siku mbili nzima kupekuwa na kujua kama watapata kuona lolote, lakini mwisho wa siku ilijulikana ni kukatika kwa mawasiliano ndiko kulifanya ndege hiyo kuweza kukosa muelekeo na kutokea janga hilo. Hakukuwa na jinsi serikali iliandaa mazishi hayo yawe ni ya Taifa na kila pahala iliweza kushushwa bendera ya Nchi ya Kenya kuwapa heshima ya mwisho marehemu wote. Hakika ulikuwa ni msiba kwa Taifa zima kuwapoteza ndugu na jamaa zao. Mama Lutfia alikuwa mwenye uchungu mkubwa sana siku hiyo, na hata baada ya zoezi hilo la mazishi ya pamoja kukamilika kila mtu aliweza kurejea kwake kuendelea na mambo mengine.

Yote hayo alikuwa akiyakumbuka Mama huyo akiwa zake amekaa kwenye benchi la hospitali sehemu ambayo watu hukaa kusubiria ndugu zao.
"Mume wangu!.. umeniachia zawadi na ukumbusho ulio bora katika maisha yangu siku zote. Mwanao amekuwa sasa na kila siku nimekuwa naona mabadiliko kwake. Hakika ni mtoto mwenye kipawa sana tangu siku ya kwanza wewe kulitamka jina atakaloitwa binti yetu. Asante mumewangu, Lutfia nitamlinda siku zote za maisha yangu."alisema Mama Lutfia akivuta taswira kana kwamba yupo na mumewe. Alinyanyuka taratibu na kurejea tena hadi kwenye chumba ambacho amepatwa kulazwa mwanaye na kumwona akiwa amelala tu pale kitandani huku akiwa amekumbatia kile kitabu. Alirudi tena kule nje kukaa kwenye kitu akisubiri maendeleo ya mwanaye.

Wakati hayo yanaendelea ndoto za ajabu zilikiwa zikimjia mtoto Lutfia akiwa pale kitandani amelala. Ndoto iliyomwonesha akiwa amekishika kitabu kimoja na kukifungua kuangaza kurasa fulani iliyopo kwenye kitabu kile alipata kuona maneno ambayo yalimfanya ashtuke. Gafla tu macho yake yakabadilika na kujikuta akifunga kile kitabu haraka na kuanza kukimbia kuelekea mahali. Hata alipofika mbele alipotea kimazingira ya ajabu hata asijulikane alipoelekea.
Alikurupuka kitandani na kuanza kuhema sana huku jasho likimtoka, alipiga kelele kumuita mama yake na muda huohuo akapata kuingia mama huyo akionesha kuwa na wasiwasi baada ya kumwona mwanaye amekaa pale kitandani hospitali akiwa anahema.
"Vipi mamayangu... umepatwa na nini?"aliuliza mama mtu akimtazama binti yake huku akimshika nywele zake kama kumfariji.
"Mama.. nimeota tena..!"alisema mtoto Lutfia akiwa amewekewa dripu pale alipo.
"Mh mwanangu umeota nini tena?"
"Nasoma kitabu,nimeota mama nasoma kitabu na mara nikabadilika macho yangu yakawa makali sana eti, halafu nikaanza kukimbia gafla nikapotea hata sijui nilipoelekea."alisema Lutfia huku akimtazama mama yake.
Maelezo yale yalimtia hofu mama mtu na kujikuta akinyanyuka na kukaa vizuri karibu na mwanaye.
"Lutfia mwanangu, hizo ni ndoto tu na kila siku nakwambia usiogope kuhusu ndoto muhimu kumuomba Mungu pindi hali hiyo ikitokea sawa mwanangu!"
"Lakini kila siku najiota mimi tu Mama kwanini nisiote hata watu wengine au hata wewe, na kila nikijiota lazima nijione natisha, kwanini?" hakuweza kupata jibu kamili binti huyo na hakutaka kuyaelewa maelezo ya mama yake. Hakika ilikuwa ni zaidi ya mara tatu ndoto kama hizo zinajirudia pindi akiwa usingizini.
Mama mtu alikosa jibu la kusema mbele ya binti yake, alitamani kumweleza jambo lakini nafsi yake inasita kusema. Lakini alipoona binti yake anakuwa na shauku ya kutaka kujua sababu ilimbidi amweleze ukweli.

LUTKAS SEHEMU YA 02


Mama mtu alikosa jibu la kusema mbele ya binti yake, alitamani kumweleza jambo lakini nafsi yake inasita kusema. Lakini alipoona binti yake anakuwa na shauku ya kutaka kujua sababu ilimbidi amweleze ukweli.

Alimshika mkono mwanaye uliokuwa na sindano inayopitisha maji yatokayo kwenye dripu. Taratibu akakifungua kile kitabu na kumuonesha mwanaye.
Muda huohuo waliwasili manesi wawili wakiwa na wameshika vifaa na dawa za mgonjwa.
"Samahani mama tunaomba utupishe kidogo tumhudumie mwanao."alisema nesi mmoja kwa sauti ya upole. Ilimbidi mama mtu amtazame mwanaye kwa tabasamu.
"Manesi wamekuja kukutibu mwanangu wacha upate dawa kwanza ukipona mambo yoye yatakaa sawa."alisema mama huyo na kumsogelea mwanaye kumbusu kwenye paji la uso kisha akanyanyuka kuelekea nje. Lutfia akawa anamtazama tu mama yake hadi alipotokomea. Aligeuka na kuangalia kile kitabu kilochoandikwa LUTKAS jina ambalo lilimfanya akipende sana kukisoma kitabu hicho. Huku manesi wakiendelea na zoezi la kutoa dripu na kuweka lengine binti huyo alikuwa mbali akifikiria siku ambayo aliulizwa na mama yake kwanini anapenda kusoma kitabu kile.
"Yaani mama nimeshajiwekea ratiba kila siku lazima nisome mara tatu hichi kitabu."alisema Lutfia akiwa kwenye sare za shule amekaa na mama yake.
"Umepewa na mwalimu shuleni usome au?"aliuliza mama mtu akiwa amekishika kitabu hicho alichokuja nacho Lutfia.
"Ndio, kuna mwalimu mgeni amekuja shuleni akanipa niwe nasoma. Alinambia nikisoma kitabu hiki nakuwa na akili nyingi daradani."alisema Lutfia akiwa anatabasamu tu. Maneno yale yalimshtua mama yake baada ya kuyasikia .
"Sasa mbona kina maneno magumu ambayo kwa darasa lako la awali hupaswi kusoma haya?"
"Mbona najua kusoma mama, nimekaa naye muda mrefu akanifundisha nikaweza. Saivi hata ukinambia nisome popote naweza nampenda sana yule mwalimu mgeni."alisema Lutcia akizidi kumpa mama yake sifa za mwalimu huyo mgeni. Hakuwa na amani Mama Lutfia baada ya kuona mambo hayo yanajitokeza tena, alishafahamu kipawa alichonacho mwanaye angali bado mdogo sana hivyo haya yanayozidi kutokea anaona kama mwanaye ataingia kwenye matatizo. Ilimbidi wapange hapo kesho pindi ampelekapo shule akapate kuonana na huyo mwalimu mgeni amfahamu na kujua lengo hasa la kumpa mtoto wa awali kitabu ambacho watu wa madarasa ya juu ndio hukisoma.

Alikuwa akiyakumbuka hayo yote na kuja kugeuka wale manesi ndio walikuwa wanaweka vifaa vyao wapate kuondoka baada ya kumchoma sindano ya dawa na kumuwekea dripu lengine bila yeye kuelewa kilichoendelea.
Muda mfupi tu mama yake akaingia tena baada ya wale manesi kutoka.
"Pole sana mwanangu, utapona tu lakini usijali."alisema mama mtu akimuonea huruma mwanaye baada ya kuoma ametundikiwa dripu lengine.
"Kawaida mama yangu, ehee tuendelee na yale tuliyokuwa tunajadili."alisema Lutfia akiwa makini kumsikiliza mama yake ambaye alishangaa kuona mwanaye huyo hasahau. Alitabasamu tu na mwishowe akavuta kiti kilichopo pembeni na kukiweka karibu na binti yake.
"Mwanangu, sio mambo mengi yenye maelezo ya kujaza kurasa ila nataka uyashike machache na yenye maana. Kama unakumbuka kipindi kile waanza shule ulipewa hichi kitabu na uliyesema ni mwalimu mpya shuleni, sasa siku ile tulipofika shuleni nikaenda kwa mkuu wa shule ili nimfahamu huyo mwalimu mgeni aliyekupa wewe hicho kitabu. Kiukweli hakukuwa na mwalimu yeyote mpya shuleni kwenu na hakukuwa na malengo ya kumuongeza mwalimu mpya. Hivyo ulivyonambia vile nikapatwa na mshangao na kuhisi huenda mtu huyo aliyekupa wewe kitabu ni mtu mbaya."
"Inamaana siku ile hukumwona mwalimu Alie? Mbona mimi naonana naye kila siku na hata darasani anaingia kufundisha na wenzangu wote tunafundishwa darasani!"
"Niskilize mwanangu, ninachokwambia ndio ukweli halisi na wala usipinge. Wewe ni muhimu sana tena sana, Lutfia sio wa kusoma shule ya awali kwasasa ila wapaswa usome elimu za juu. Mwanangu umejawa na kipawa bahati za akili za asili na ndio maana ulivyopewa kitabu ukawa unasoma tu bila kufundishwa. Na huyo Madam Alie unayesema wewe hakuwa mtu wa kawaida, hakuwahi kuwepo shuleni kwenu ndio maana wewe pekee ndiye uliyemuona. Hata ukirejea tena shule kuwauliza wenzako hawamfahamu japo ulishuhudia akisomesha ndani ya darasa."alisema Mama mtu na maelezo yako yalimwacha njia panda mwanaye.
"Inamaana Madam Alie hakuwa Mwalimu? Sasa imekuwaje?"
Sina uhakika kama alikuwa ni mwrma au mbaya kwako, ila ninachokua mimi kiwa ni yeye ndiye aliyekupa hichi kitabu. Huenda kinamaana kubwa sana ndio maana kila unapoumwa najaribu kukileta kiwe karibu na wewe na kweli huwa unajisikia nafuu hata ukiwa unaumwa na maradhi makubwa. Hivyo sasa uwe unatambua kuwa wewe unazawadi ya akili zaidi ya wenzio na sahau kuhusu huyo Madam Alie."alisema mama mtu akimuelewesha binti yake aliyeko kitandani muda huo.
"Sawa mama nimekuelewa, nitajitahidi nimsahau."alisema Lutfia baada ya kupewa maelezo ya kina jinsi hali ilivyokuwa. Mama alimsogelea na kimkumbatia mwanaye ambaye ndiye wa pekee.

Baada ya juma moja kupita hali ya Lutfia iliweza kuwa sawiya na hata daktari akatoa ruhusu ya mtoto huyo kuweza kurejea nyumbani pamoja na mama yake. Alipewa dawa na ushauri wa kiwa karibu sana na mwanaye kuweka usalama wa karibu kama kunaweza kutokea utofauti wa kiafya kwa binti yake. Mama mtu alimuweka mwanaye kwenye gari yake naye akapanda kuanza safari ya kurejea nyumbani akiwa mwenye furaha kumuona mwanaye amerudi katika afya yake ya awali.
Njiani Lutfia alikuwa mwenye kutazama tu nje kuona baadhi ua watu mbalimbali na majengo marefu ya kila rangi. Katika kitazama kwake alipata kumuona yule Madam Alie ambaye aliwahi kuwa shuleni kwao na ndio mwanamke aliyempatia kile kitabu kilichoandikwa LUTKAS. Alimtazama kwa makini akionekana kumpungia mkono Lutfia huku gari likiwa kwenye mwendo. Alipatwa na mshangao wa gafla maana aliambiwa mtu huyo hakuwahi kuonekana shuleni pale, imekuwaje anamwona tena mitaani?
Alibaki mwenye kujiuliza swala jilo bila kulipatia jawabu. Alitamani kumweleza mama yake lakini hakuona umuhimu wa kusema alochokiona maana hata mama yake haamini kiwepo kwa Madam huyo. Gari lao likazidi kusonga mbele wakirejea zao nyumbani. Lakini hali ile haikuwa ya mara moja kwa Madam yule kuweza kuonekana na binti Lutfia wakiwa wanarejea kwao hali iliyomfanya ashindwe kujizuia kuongea.
"Mama yule Mwalimu namuona ananipungia mkono yule pale.."alisema Lutfia na kumfanya mama yake aliyekuwa ameshikilia usukani atazame kwenye saitimila za gari lake.
"Yupo wapi?"aliuliza Mama mtu huku akiweka umakini pande zote mbili. Mwanaye alioneaha upande ambao mwalimu yule amepata kuonekana. Ilimlazimu mama mtu aliweke kwanza gari pembeni ya barabara na kushuka kutazama kila sehemu kuangalia lakini hakuweza kuona lolote, alimsogelea mwanaye.
"Wewe umemuona wapi?"
"Alisimama pale karibu na kibanda kile cha kupiga simu ajabu saivi simuoni tena baada ya kusimamisha gari!"alisema Lutfia akiwa naye anatazama huku na kule baada ya kutomwona tena mwalimu yule.
Ilimbidi mama mtu asogee kwa mwanaye kumpa tumaini.
"Sikia mwanangu nikwambie. Haya yote ni majaribu tu wala usiwe na hofu juu ya haya naamini ipo siku yatakwisha, wewe ona kama ni kawaida tu wala usiogope mwanangu sawaeeh."alisema mama Lutfia na mwanaye akamuelewa. Alirejea tena kwenye usukani na kuanza tena safari yao kuelekea nyumbani.

LUTKAS SEHEMU YA 03


ILIPOISHIA..
"Sikia mwanangu nikwambie. Haya yote ni majaribu tu wala usiwe na hofu juu ya haya naamini ipo siku yatakwisha, wewe ona kama ni kawaida tu wala usiogope mwanangu sawaeeh."alisema mama Lutfia na mwanaye akamuelewa. Alirejea tena kwenye usukani na kuanza tena safari yao kuelekea nyumbani.

TUENDELEE LEO
Huku nyuma yule Madam Alie aliyesadikika kuonwa na Lutfia alipata kulitazama gari la mama na binti yake likitokomea zaidi. Muda wote alikuwa akiwafuatilia kujua zaidi wanapoelekea, na baada ya kufahamu kitu aligeuka na kupotea zake gafla pale alipo.
Alikuja kutokea makaburini, makaburi ya karne na karne, miaka mingi imepita hadi baadhi yao yamepoteza kabisa muonekano. Yule mwanadada alisimama kwenye kaburi moja ambalo limepata kuonekana likiwa bado halikuchakaa sana. Alisogea hadi kwenye msalaba wa kaburi lile na kuushika ukiwa unasomeka jina la ALIE SANDRO (BORN) 17 Sept. 1973 (DIE) 17 Sept. 2001. Ni wazi kwamba ndilo jina lake halisi likiwa limeandikwa kwenye msalaba ule ukionesha mwaka aliozaliwa hadi mwaka ambao umauti umemkuta na haikujulikana imekuwaje hadi kuweza kuishi tena angali ni mfu. Taratibu alishuka chini na kujilaza pale kwenye kaburi lake lililopambwa na kujengewa kwa tofali. Alipohakikisha amelala chali mwili wake ukaanza taratibu kididimia kwenda chini hadi ulipotokomea kabisa ndani ya kaburi lile.

Hadi kufika jioni ya siku hiyo Mama Lutfia alikuwa ameshaanda chakula cha jioni kwaajili ya mwanaye kutokana na hali aliyokuwa nayo toka warudi kutoka hospitali. Ni mtoto pekee hivyo alihakikisha anamfanyia kile anachokitaka ikiwa ni moja ya malezi aliyopanga kumlea binti yake huyo.
Muda wote huo akiwa anaandaa chakula kukiweka mezani ili wapate kula na mwanaye na wala hakutaka msaada wa mfanyakazi wake wa ndani kupika siku hiyo, Lutfia alikuwa anasoma kile kitabu cha LUTKAS kwa umakini wa hali ya juu. Mama mtu alitoa vinywaji kwenye friji na kuviweka pale mezani. Akiwa anaendelea na zoezi hilo alisikia binti yake akishtuka pale alipokaa akiwa ameshika kile kitabu. Haraka akageuka kumtazama.
"Wewe una nini?"aliuliza mama mtu akiwa anamtazama mwanaye.
"Mama kwani leo tarehe ngapi?"aliuliza Lutfia na kumfanya mama yake ashindwe kumuelewa. Alipokumbuka kitu aliachia tabasamu kidogo na kumgeukia mwanaye.
"Kumbe unakumbukumbu kuhusu baba yako eh! Ni kweli leo ni siku yake aliyofariki. Na baadae tutasali kumuombea rehma huko alipo."alisema Mama Lutfia na kuendelea na kuandaa chakula.
"Hapana mama nina maana tofauti kabisa, nataka kujua leo ni tarehe ngapi?"alisema Lutfia.
"Ni tarehe 17, vipi kwani?"aliuliza mama huyo huku akimtazama mwanaye aliyeonekana kuwa siriasi kumtazama mama yake.
"Mungu wangu ni SEPTEMBER 17 kumbe? Oh my GOD inamaana hili laweza tokea kweli au!"alisema Lutfia huku akiangalia kitabu kile. Alimwacha mama yake kwenye mabano ashindwe kuelewa kinachoendelea. Ilimbidi aache kazi zake na kusogea karibu na mwanaye pale alipokaa na kupeleka macho yake kwenye kile kitabu ambacho Lutfia amepatwa na hofu baada ya kuangalia mambo mule ndani ya kitabu.
"Mama, leo kuna viumbe vinatakiwa kufufuka kutoka ardhini kuja duniani. Hawa sio wa heri, wanakuja duniani kutafuta kitu chao na hapa wanaonekana kuwa watamwaga damu sana za watu kusudi tu wapate wanachokitaka. Hakika nimepatwa na woga mama.. I swear. (Naapa)." Alishindwa kujizuia Lutfia akajikuta naye anadondosha chozi.
"Mbona sikuelewi mwanangu, kwani kumeandikwa nini humo hadi uyaseme hayo?"aliuliza mama mtu na ikabidi aelezwe yale yote aliyoyasoma na kuyaona ndani ya kitabu kile.
"Hawa viumbe wanatumia siku moja ambayo ni pekee kwao kuja duniani kutafuta kitu chao hivyo hawaoni tabu kuua. Na mauaji yao ni ya watu wengi sio ya mmoja mmoja."alizidi kumuelewesha mama yake juu ya swala zima linaloendelea.

Hali iliyomfanya mama yake baada ya kuambiwa hivyo alishtuka na kujikuta hata yeye akae kwenye kiti mwenyewe, akivuta kumbukumbu na matukio ya nyuma kukumbuka tarehe kama hiyo ndio siku aliyoweza kuongea na marehemu mume wake akiwa safarini na ndio siku ambayo ajali ile ya ndege ilipata kutokea na kuua watu wote akiwemo mumewe. Aligeuka kumtazama mwanaye wakajikuta wanaangaliana tu.
"Mwanangu... ni... ni kweli. Nimeamini kweli yaliyoandikwa humo huenda yakawa sahihi."
"Unamaana gani kusema hivyo?"aliuliza Lutfia akiwa haelewi.
"Baba yako alifariki tarehe kama ya leo na ilikuwa ni ajali ya ndege hivyo walipoteza maisha watu wengi. Huenda hao viumbe ndio waliosababisha hilo litokee. Oh Mungu wangu!"alichoka baada ya kuupata ukweli sasa. Taratibu binti alinyanyuka pale alipo na kumsongelea mama yake kumfariji, wakabaki wamekumbatiana usiku ule.

Siku hiyo ilikuwa ndio siku pekee ya kuapishwa rasmi kiongozi wa viumbe ambavyo si binadamu wa kawaida. Umati wa viumbe hivyo walifurika kwenye uwanja maalumu wa makutano yao ndani ya mji wao mkuu uliobatizwa jina la UWANJA WA DHAHABU. Hii ni kutokana na ufalme wao uliokuwa ukiongozwa na Mfalme aliyekuwa na umiliki mkubwa wa dhahabu. Hadi kuamua kutengenezewa kiti chake cha kifalme ambacho kilipambwa na dhahabu tu. Na siku hiyo ndiyo binti yake wa pekee Kasma anatawazwa kuwa kiongozi wa jamii hiyo mara tu baada ya kutangazwa kifo cha Mfalme huyo ambaye alikuwa akiugua kwa muda mrefu sana.
Walikuja wazee waliokuwa karibu na marehemu wakasogea hadi pale alipo Kasma akiwa amekaa kwenye kiti cha dhahabu huku umati wa watu wakishuhudia kinachoendelea. Walimpa heshima yake kama kiongozi wao na taratibu binti huyo akainuka na kusogea mbele. Alisogea mzee mmoja akiwa ameshika kofia ya kifalme uliyokuwa ikiwaka kwa dhahabu na taratibu akamvisha Kasma kichwani. Shangwe na kelele za furaha zilisikika ndani ya uwanja huo baada ya kushuhudia wameapata kiongozi mpya wa kuwaongoza.

Kelele na shangwe hizo za furaha zilimfanya Lutfia akurupuke kitandani. Alitazama huku na kule kwenye chumba chake kilichokuwa na giza totoro. Alitega sikio kusikiliza kelele zile zinapotokea lakini ajabu zinasikika tu masikioni mwake wala hajui muelekeo wa wapi kelele zile zinapotoka. Alijaribu kuziba masikio kusudi asipate kusikia lakini haikuwa rahisi. Hali hiyo ilivyoendelea hata yeye alijikuta akikasirika sasa na kuona ni kero usiku ule, alijikuta akipiga ukelele kwa sauti na kwa hasira.
"I N A T O S H A A A A A A A A!"
Sauti iliyowafanya wale viumbe wote waache kupiga makofi na kushangilia kwa muda mrefu baada ya kiongozi wao mpya Kasma kusema hivyo.
"Leo ni siku ya kipekee kwetu na ikumbukwe siku kama ya leo Mfalme wetu, baba yangu alituacha katika ulimwengu huu. Na lengo letu ni moja nadhani kila mmoja wenu anafahamu jukumu lake hivyo sitapenda niongee sana leo... KASMAAAA...."
"KIONGOZI MILELEE......!"waliitikia watu na shangwe zikaendelea za furaha.
Kule alipo Lutfia alibaki kushika masikio yake tu kujaribu kutosikia lolote lakini kila kilichozungumzwa alipata kusikia kule alipo kwao na kufahamu kuwa anasikia mambo ambao watu wanaongea hata wakiwa mbali.

Zoezi la kuapishwa na kutambulishwa rasmi binti Kasma kuwa ndiye kiongozi wa jamii yao lilipokwisha kila myu alikwenda kwenye mahala pale, na ndipo hata Lutfia akapata nafuu kidogo ya kutosikia tena kelele zile za shangwe. Alitulia kitandani kwake na kuanza kutafakari ni uwezo wa aina gani alionao hadi kuweza kusikia jambo ambalo haliongelewi mahala pale alipo. Hakuweza kupata jibu kamili ilimbidi asogeze kitabu chake na kujifunika shuka kuutafuta usingizi.

Usiku huo kwa Kasma ulikuwa wa aina yake, furaha ya kuwa rasmi kiongozi mwenye umri mdogo sana kiweza kuongoza watu wa jamnii yake na mali zao. Haikuwa kazi rahisi lakini kwa jinsi alivyokuwa akijiamini aliona ni jambo la kawaida kwake. Akiwa amejipumzisha kwake alisikia mlango ukigongwa na wakatomea wazee watatu hadi pale alipo na kumpa heshima yake.
"Vipi kuna jambo jipya kutoka kwenu mmelileta?aliuliza Kasma akiwa anawatazama wale viongozi.
"Bila shaka Malkia wetu, kuna swala hapa yatupasa tukutaarifu mapema na ni wewe ndiye mwenye kutoa ushauri au neno la mwisho."alisema Mzee huku akimtazama Kasma.
"Ni jambo gani hilo mnataka kunambia?"aliuliza Kasma akiwa makini kuwasikiliza.
"Malkia, baba yako aliacha jambo hapa ambalo ndio tulikuwa tunalifanyia kazi, lakini zoezi hili lapaswa kufanyika na viongozi ambao wanatutawala katika uongozi. Hadi baba yako kufariki juwa kwamba kuna mambo aliyafanya makubwa na baadhi kayaacha, hivyo mengi yakupasa kuyamaliza. Ikumbukwe enzi za Mfalme alikuwa anafanya majukumu yake japo baadhi alikuwa anakosea, hivyo alipaswa kupata adhabu na huenda Miungu ikaona adhabu yake ni kifo kama ilivyokuwa. Hivyo nawe kaa ukijua kwamba utakapokwenda kinyume na kile kinachohitajika basi mapema sana utahusika moja kwa moja. Kuna kitabu cha karne na karne tumekuwa tukikitafuta lakini tumekikosa. Tulijaribu kumshauri baba yako tuweze kwenda duniani tukapekue kila sehemu kujua kama tutaweza kupata ukweli lakini alikataa. Hivyo tunakuomba wewe kama ndiye mhusika na kiongozi wa hili uweze kutoa amri ili tutume vijana waweze kuingia kuifanya kazi hii."alisema yuke mzee kwa unyenyekevu japo ni mkubwa kiumri.
"Hicho kitabu kinamaana gani kubwa hasa hadi kifuatiliwe hivyo? Na kwanini baba akatae enzi za uhai wake muje kuniambia mimi sasa?"aliuliza Kasma akiwa anamtazama yule mzee. Alitazama chizi kwa muda kisha akanyanyua uso wake kuwatazama wenzake walio pembeni yake na kugeuka kumuangalia Kasma.
"Ni kitabu cha Uhai... Kina thamani kubwa sana kwetu endapo tutakipata. Unafahamu fika kwamba pamoja na uwezo tulionao lakini badi tuwachache hivyo endapo tukapata kitabu hio ambacho kinauwezo wa kufufua watu waliozikwa muda mrefi na itasaidia kuwafanya wafu hao kuwa kama sisi ili tuzidi kuongezeka maana kuna kazi kunwa ya kufanya siku za mbeleni. Mfalme enzi za uhai wake alikataa kwakuwa alikuwa na hofu ya wale wabaya wake aliowaua hapo nyuma endapo wakifufuka wanaweza kumgeuka na ndio sababu ya yeye kukataa kabisa kutafuta kitabu hicho."alisema yule mzee kwa umakini akijaribu kumuelewesha binti Kasma ambaye ndiye kiongozi wao kwasasa.
"Na kwanini umesema awali kwamba mimi ndio mhusika wa hili?"aliuliza Kasma.
"Jina la kitabu tunachokitafuta linatokana na jina lako, japo herufi za awali hatujapata kujua maana yake hasa. LUTKAS ndio jina la kitabu hicho hivyo baada ya kukipata kitabu hicho ndio tutajua ukweli hasa wa yaliyomo ndani na hata kujua herufi za awali zinamaanisha nini."alisema Mzee yule na kumfanya Kasma afahamu ukweli wa kitabu hicho. Kumbe hata chimbuko la jina lake limetokana na jina la kitabu kile. Alijikuta akipata shauku ya gafla ya kukipata kitabu hicho kujua kina nini hasa ndani yake.

Usiku huo kule makaburini kulipata kuonekana utofauti, ardhi inajiachia kuwa na mipasuko. Juu ya makaburi kukaanza kuonekana viungo hasa mikono ikianza kuchomoza. Makaburi mengi yalipata kuonekana hali hiyo na tayaribu viungo vengine vikajitokeza na mwishowe miili ya wafu wengi ikiamka kabisa ikiwa na sura za kutisha na mavazi yaliochakaa. Walisogea na kukusanyika pamoja na mwishowe akapata kutokea msichana aliyeonekana walau kutoharibika mwili sana tofauti na wenzake. Alisogea hadi pale walipo wenzake wakiwa wanamuangalia yeye.
Alinyanyua mikono yake miwili na kuwaonesha wenzake walio mbele yake, taratibu wakaanza kuonekana miili yao inarudi kuwa kama watu walio hao. Kila mtu akawa anajitazama jinsi alivyo na kubaki kufurahi kwa kujiona wakiwa na muonekano mpya.
Walimtazama msichana yule anbaye naye alibadilika na kuwa mtu wa kawaida kabisa. Ni Alie yule msichana aliyeonekana na Lutfia mara kwa mara hata kusadikika kuwa alikuja shuleni kwao na kujifanya ni mwalimu. Aligeuka na kuanza kuongoza njia kuondoka huku wenzake nao wakimfuata.
NAAM,WAFU WANARUDI TENA DUNIANI WAKIONGOZWA NA ALIE. HUKU NAPO KASMA ANA HAMU YA KUKIPATA KITABU CHA LUTKAS. NINI KITATOKEA HAPO MBELENI?

LUTKAS SEHEMU YA 04


ILIPOISHIA
Ni Alie, yule msichana aliyeonekana na Lutfia mara kwa mara hata kusadikika kuwa alikuja shuleni kwao na kujifanya ni mwalimu. Aligeuka na kuanza kuongoza njia kuondoka huku wenzake nao wakimfuata.

TUENDELEE.
Kesho yake asubuhi Lutfia alijiandaa na kuvaa sare zake za shule. Alipokamilisha zoezi hilo alichukua begi lake na kutoka chumbani kwake kuelekea sebuleni ambapo alimkuta dada wa kazi akiwa anafanya usafi. Alipomuona Lutfia akiwa kavalia sare za shule alishangaa ikabidi asimame kumtazama.
"Wewe mbona hivyo? umepona kwani?"aliuliza yule msichana akiwa ameshika kitambaa.
"Najisikia niko sawa ndio maana nimeona niende shule."alisema Lutfia.
"Mungu wangu...! Mamaa... Mamaa!!."aliita yule mfanyakazi na kusikia akiitikiwa. Muda mfupi alitokea mama Lutfia akionekana kutoka usingizini.
"Mbona tunaitana asubuhi asubuhi kuna..."alishangaa kumuona mwanaye akiwa kavalia sare zile za shule.
"Haya wewe vipi na hizo Uniform?"
"Nataka kwenda shule."aliongea Lutfia na kumfanya mama yake ashangae.
"Hebu usiniletee matatizo miye bado hujawa sawa na hata walimu wanafahamu kwamba unaumwa. Pumzika ukiwa sawa utaenda mwanangu sawa.!"alisema mama mtu lakini maneno yake hayakuweza kumshawishi mwanaye asitishe zoezi lake.
"Mimi niko sawa sasahivi siumwi mama na ndio maana nimeamka na hamu ya kwenda shuleni. Ningekuwa naumwa wala nisingetamani kwenda. Jiandae unipeleke."alisema Lutfia akionesha kuwa na msimamo. Walijaribu kumuelewesha lakini haikusaidia na mwishowe wakaamua kufanya kile anachokitaka. Ilibidi mama mtu ajiandae aweze kumpeleka mwanaye shuleni.

Upande wa pili Kasma alikubaliana na yale maelezo ya wazee wale na kuhitaji swala hilo lifanyike haraka la kukipata kitabu hicho ambacho kinasadikika hata baadhi ya herufi za jina lake zinatokana na jina la kitabu hicho. Bila kuchelewa waliwandaa baadhi ya wenzao na kuanza safari ya kuelekea duniani kupata kujua wapi kinapatikana kitabu hicho. Walimuacha kiongozi wao akiwa mwenye furaha akiamini zoezi hilo likifanikiwa basi atakuwa na amri ya kuwaamuru hata wafu kile ambacho anataka yeye.
Huku upande wa pili Mama Lutfia alikuwa akiendesha gari kumpeleka mwanaye shule. Alikuwa akimtazama kupitia kioo kidogo cha mbele na kumwona binti yake nyuma ya siti akiwa anafunua funua kurasa za kitabu. Taratibu ile hali na mabadiliko kwa mwanaye akaanza kuyazoea na kuona ni kama zawadi tu amepewa na Mungu maana hakuna mtoto wa makamo yale angeweza kusoma tu kitabu chenye maelezo mengi na hata maneno magumu. Alijikuta akikumbuka matukio mengi ya nyuma aliyofanya mwanaye Lutfia na kuona hakuna haja ya kuwa na hofu juu yake. Alitabasamu tu mwenyewe na kufungua redio akitafuta nyimbo nzuri yenye kumfurahisha.
Katika kutafuta stesheni ya redio akapata kusikia taarifa ya habari ikisomwa, ilibidi aache kuendelea apate kusikiliza vizuri. Ilikuwa ikiongelea vifo vya watu kumi na wa nne waliofariki ndani ya Hospitali ya watoto ya Presbayterian. Na chanzo cha vifo hivyo vya gafla haikujulikana mapema maana muda wote madokta wakishirikiana na manesi walikuwa makini kuwahudumia wagonjwa wao. Taarifa ile ilimshtua sana Mama Lutfia na kujikuta akigeuka kumtazama mwanaye ambaye naye baada ya kusikia hivyo alishangaa.
"Mama ni ile Hospitali niliyolazwa mimi ndio kumetokea tukio hilo?"aliuliza Lutfia kutaka kujua huku mama yake akiwa mwenye woga. Alimwitikia mwanaye kwa kichwa kuashiria ndiyo hiyohiyo Hospitali ambayo jana tu amepata ruhusa ya kutoka na mwanaye hospitalini hapo. Hivyo laiti kama wangebaki kwa siku kadhaa tu huenda hata mwanaye akawa miongoni mwa wahanga wa tukio hilo.
"Hatupaswi kwenda shule tena mama twende tukajue imekuwaje huko hospitali."alisema Lutfia.
"Hapana kwasasa nikupeleke tu shule sidhani kama tutaweza kupata nafasi ya kuingia hospitali maana askari watakuwa wamefika wengi kujua chanzo hasa cha tatizo hilo."alisema mama mtu akiwa anazidi kukanyaga mafuta.
"Siwezi kwenda shule mama nielewe, nimekaa Hospitali pale na wenzangu sijui kama wapo hai au ndio muongoni mwa hao waliofariki, nahitaji walau nikaione tu hiyo hospitali. Nakuomba nipeleke mama."alisema Lutfia kwa uchungu hali iliyomfanya mama yake amtazame tu kwenye kioo kidogo cha mbele. Alishusha pumzi kuona mwanaye amebadili maamuzi ya shule tena na kutaka waende hospitali. Ilimbidi abadili njia na kuanza kuelekea katika Hospitali hiyo akimsikiliza mwanaye maana anampenda sana na ndiye mtoto pekee.

Watu wengi walionekana nje ya Hospitali ya Presbayterian baada ya kusambaa kwa taarifa zile za vifo vya watoto 14 kwa pamoja. Wazazi wengi walipata kuwasili Hospitalini hapo kujua kama watoto wao wamenusurika au ni miongoni mwa hao waliofariki. Vilio na kelele za hapa na pale zilisikika kwa baadhi ya wazazi mara baada ya kujua kuwa watoto wao wamepoteza maisha. Askari walikuwa na kazi ya kuwazuia watu nje wasiweze kuingia ndani ya Hospitali kiholela. Daktari pamoja na askari wakubwa waliingia kwenye chumba cha miili ya watoto waliokumbwa na umauti na kuoneshwa jinsi ilivyokuwa. Hakika wengi wao waliharibika sana hasa tumboni kukionekana kama kutobolewa huku miili mengine ikinyofolewa baadhi ya viungo tumboni. Hakika ulikuwa ni ukatili wa hali ya juu hasa kwa watoto wadogo wale.

Huko nje ya Hospitali kulizidi kufurika umati mkubwa wa watu huku vyombo mbalimbali vya habari vikiwasili kutaka kuchukua taarifa mbalimbali zinazoendelea pale. Muda huo walifika mtu na mwanaye na kuweza kupaki gari pembeni huku wakitazama umati wa watu uliofurika nje ya Hospitali hiyo.
Mama Lutfia alianza kushuka kwanza akimsihi mwanaye asitoke ndani ya gari kwanza aangalie mazingira jinsi yalivyo. Lutfia alibaki ndani ya gari akitazama tu jinsi watu wakizuiwa na askari wengi waliozunguka Hospitali hiyo. Alipataka kuona baadhi ya wanamama wakilia kwa uchungu huenda wakawa na shauku ya kujua hatma ya watoto wao. Katika kuangaza macho huku na kule alipata kuwaona watu wawili wakitokomea kuelekea njia nyengine. Walikuwa ni wazito hata kutembea huku miili yao ikionekana kuchangaa hasa mavazi yao huku midomo yak ikitokwa na damu. Lutfia alishtuka kuona vile na kujikuta akiona kuna picha zinamjia kichwani mwake na kuhisi watu wale alipata kuwaona sehemu. Alipotafakari kwa umakini sana ndipo akakumbuka ni muda ule ambao alikuwa akisoma kitabu na kujikuta akishtuka hadi kuamua kumuuliza mama yake kuhusu tarehe ya siku ile ya jana ambayo ilikuwa ni Tarehe 17. Ni wazi kwamba lile tukio alilokuwa akilisoma kwenye kitabu kuwa kuna viumbe vinakuja duniani kutafuta kitu chao na damu nyingi za watu zitamwagika basi tukio lenyewe huenda likawa ndio hilo la kufariki kwa watoto hao. Alihamaki baada ya kuujua ukweli huku viumbe wale wakitokomea. Kwa ujasiri wa hali ya juu alijikuta akiufungua mlango wa gari na kushuka. Haraka akaanza kukimbia kuwafuata wale viumbe kule walipoelekea.

Upande wa pili shuleni kwa Lutfia alipokuwa akitaka kwenda kulionekana kupo tofauti. Kulikuwa kimya kwa muda huku kwa mbali sauti za ngurumo zikisikika. Dakika kadhaa tu wakapata kuonekana viumbe vya ajabu wakitoka ndani ya shule hiyo wakiwa wamelowa damu midomoni na mikononi. Walitoka haraka hadi huku wakionekana kunusa nusa harufu ya hali ya hewa kisha wakatazamana. Taratibu wakabadilika palepale na kuwa na miili mizuri kama watu wa kawaida. Mmoja wao akanyoosha kidole kuashiria ndipo wanapotakiwa kwenda na muda huohuo wakaanza safari ya kuelekea huko.

Safari ya watu wa Kasma iliwasili duniani, lengo hasa ni kutaka kujua wapi kilipo kitabu kile cha LUTKAS. Kwa uwezo walionao wakawa wananusa tu harufu kujua wanaanzia wapi. Lakini kila wanaposikiliza harufu wanajikuta wakinusa harufu ya damu tu hali iliyowafanya washangae hata wa na kubaki kutazamana. Ilibidi wafanye mpango wa kuelekea kwenye harufu hiyo kujua kumetokea nini.
Kule alipoelekea Lutfia aliangaza macho yake huku na kule bila kuona mtu yeyote. Awali aliona kwa macho yake viumbe ambavyo havikuwa vya kawaida na ndio sababu ya kushuka kwenye gari kuweza kuwatazama vizuri. Alitembea huku na kule kuwatafuta lakini hakuweza kuona lolote. Aliamua kugeuka tu na kuanza kuondoka zake kurudi kwenye gari lao. Akiwa anatembea alisikia nyuma yake kama kuna mtu anamfuata. Ilibidi asimame kwanza akiwa mwenye ujasiri wa hali ya juu na haraka akageuka kutazama nyuma. Ajabu alipata kumuona yule mwalimu Alie akiwa mwenye kutabasamu.
"Lutfia mbona upo huko pekeako?"aliuliza Alie akiwa kwenye sura yake ya usichana mwenye mvuto. Lutfia akabaki kumtazama dada huyo kwa makini sana kuanzia juu hadi chini lakini hakupata kuona utofauti wowote kama alivyoelezwa na mama kuhusu dada huyu aliyejifanya ni mwalimu wa shule yao lakini walipofuatilia hakuweza kujulikana shuleni hapo.
"Kuna watu niliwaona wakiwa wanavuja damu wakielekea huku hivyo nikashuka kuwaangalia maana walikuwa tofauti sana."alisema Lutfia akitazama njia ile aliyoona kiumbe yule akitokomea.
"Una uhakika uliwaona kwa macho yako?"aliuliza Alie kwa sauti ya kusisitiza zaidi hali iliyomfanya Lutfia kwa akili zake za haraka ahisi jambo. Alirudia tena kumtazama Alie machoni na hata muonekano wake, moyo wake ukaanza kukataa uhalisia wa dada huyo kimuonekano.
"Nahisi nilikuwa naota maana ninekurupuka kwenye gari nikatoka haraka kuja huku, sasa sijui ilikuwaje."alisema Lutfia akibadili maelezo yake baada ya kumhisi tofauti Alie.
"Okay basi hakuna shida, si vizuri kutembea pekeako ni vyema ukarudi kwenye gari."alisema Alie na kumfanya Lutfia ageuke na kuanza kupiga hatua kurudi kwenye gari.
"Mbona haniulizi nipo na nani mahala hapa? Na kama kweli ni mwalimu na mimi ni mwanafunzi si atakuwa anajua kuwa nilikuwa naumwa?sasa mbona haniulizi maendeleo yangu? Na kama hajui kwanini haulizi kuwa muda wa shule huu na nipo huku maeneo ya Hospitalini. Yeye kwani amefuata nini huku?" Ni maswali ambayo yalimzingira kichwani mwake bila kuyapata majibu. Kitu pekee ambacho hawezi kuvumilia Lutfia ni kukaa na kitu moyoni, alijikuta akigeuka tena kumtazama Alie akiwa amesimama.
"Kwani wewe si Mwalimu wangu! Mbona upo hapa muda huu wa shule?"aliuliza Lutfia na kumfanya Alie akumbuke kumbe aliwahi kubadilika na kuonekana kuwa ni mwalimu wa shule anayosoma Lutfia. Haraka akatafuta namna ya kumuaminisha binti huyo asiweze kumhisi vibaya.
"Nilipata taarifa kuwa kuna watoto wamepata tatizo hivyo kuna ndugu yangu mwanaye yupo humu hospitali hivyo nimekuja kushirikiana naye kujua hali ya mwanaye kama yupo hai au laa."alisema Alie na kumfanya Lutfia asilizike na majibu yake. Alikuwa na akili sana za kumfahamu mtu kwa maelezo tu.
"Ahaa sawa, basi mimi narudi kwenye gari nimsubiri mama yangu, kwaheri."alisema Lutfia na kuondoka zake akiwa amejiridhisha kuwa kweli yule si mwalimu kama alivyodhani awali.
Alie alikuwa akimtazama Lutfia kwa namna yake, muda wote huo alikuwa akimhisi binti huyo huenda akawa na nguvu fulani ambazo ni muhimu sana endapo wakimtumia. Ndio maana alikuwa akimfuata hata shuleni lengo ni kuhakikisha kile anachokihisi kama ni kweli lakini hadi leo hana uhakika wa kweli kama binti huyo ana nguvu anazozihisi zipo ndani yake na wala hajui kama ndiye binti ambaye ana kitabu ambacho kinatafutwa na pande zote mbili wao pamoja na watu wa binti kiongozi, Kasma.LUTKAS SEHEMU YA 05


ILIPOISHIA..
Ndio maana alikuwa akimfuata hata shuleni lengo ni kuhakikisha kile anachokihisi kama ni kweli lakini hadi leo hana uhakika wa kweli kama binti huyo ana nguvu anazozihisi zipo ndani yake na wala hajui kama ndiye binti ambaye ana kitabu ambacho kinatafutwa na pande zote mbili wao pamoja na watu wa binti kiongozi, Kasma.

TUENDELEE LEO..
Ilimbidi mama Lutfia asogee mbele kabisa walipo watu ili kupata kujua kinachoendelea pale. Alipata kishuhudia daktari akiwa amesimamiwa na Polisi wawili pembeni wakimpa ulinzi. Kazi yake ilikuwa ni kuita jina la mzazi wa mtoto aliyejiandikisha kumhudumia siku zote. Hali hiyo ikawafanya baadhi ya wazazi wengine kuwa na hofu maana ukiitwa ni wazi kwamba ndio mwanao amepatwa na umauti hivyo unakwenda kuhakikisha kama ndiye mtoto wako. Zoezi hilo liliwafanya watu wengine kuwa roho juu huku wengine wakiomba Mungu watoto zao wawe salama.
Hakika ilikuwa ni majonzi na huruma ya hali ya juu nje ya hospitali hiyo. Muda mfupi alipata kuonekana mwanamama akitoka nje akiwa analia sana huku akipepesuka kukosa nguvu hali iliyofanya askari wamsaidie kumshika kumuweka mahala salama kwanza. Watu walipodadisi wakapata kufahamu mama yule alipoteza wanae mapacha kati ya watoto 14 walisafikika kuuawa.
Mida mfupi ving'ola vya msafara wa ulipata kusikika kuwasili maeneo yale na kuwafanya Polisi waanze kuwasambaratisha watu. Aliwasili Waziri wa afya wa nchini humo akiongozana na walinzi wake wawili nyuma moja kwa moja wakaingia ndani ya Hospitali hiyo. Mama Lutfia kuona vile akafahamu swala hilo kweli limewagusa watu wengi hata serikali kwa ujumla. Hakutaka kupoteza muda tena wa kuangalia pale baada ya kumkumbuka mwanaye amemuacha kwenye gari. Haraka akageuka na kurejea kwenye gari lake akimkuta mwanaye anasoma kitabu kama ilivyo kawaida yake.
"Kwakweli watu ni wengi mno mwanangu ni bora hata ulivyobaki humu. Muda mfupi tu amewasiri Waziri kwenda kushuhudia hali halisi."alisema Mama Lutfia huku akifunga mlango wa gari na kuvaa mkanda vizuri.
"Hukubahatika kuona sura ya maiti yeyote?"aliuliza Lutfia kwa sauti ya chini.
"Hapana sikuweza kuona. Na sidhani kama kuna mtu ataona zaidi ya ndugu ambaye ndiye mhusika mkuu anayepaswa kumtambua mtoto wake. Cha kushukuru Mwanangu umeweza kuruhusiwa mapema na upo salama huenda ungekuwa bado upo sijui ningepatwa na mshtuko gani kisikia taarifa hizi."alisema mama Lutfia akiwa ameshikilia tu usukani bila kuwasha gari akiangalia tu umati wa watu pale.
Lutfia alibaki kumeza mate tu na kuona huenda angekumbwa na dhoruba hilo na ni bahati tu kwake kuweza kupewa ruhusa. Alishusha macho yake na kukitazama kile kitabu akiwa ameweka kidole chake kwenye mstari mmoja ulioonesha idadi ya watu wengi kupoteza maisha pindi viumbe hao watakapoingia duniani. Na muda huohuo gari la wagonjwa lilipata kuonekana kutoka Hospitalini pale haraka kwenda sehemu huku Mama Lutfia akilitazama tu likitokomea.
"Mh mwanangu siku ya leo imekaa vibaya hata najikuta moyo unakuwa mzito hata kukupeleka shule mwanangu. Turudi tu nyumbani kwanza mambo yakikaa sawa nitakupeleka sawa mwanangu."aliongea Mama mtu kwa kubembeleza akijua mwanaye ni mbishi.
"Mama.."aliita Lutfia na kumfanya Mama yake ageuke nyuma kumtazama.
"Hawa viumbe nahisi leo watazunguka mji mzima wakitafuta kitu chao. Japo ni ngumu kukipata ila yataka kuwa makini. Yule mwalimu Alie sio mwalimu leo ndio mimeamini."alisema Lutfia na maneno yake yalimshangaza mama yake. Ilibidi amueleze hali halisi ilivyokiwa pindi alipotoka kwenye gari hilo muda ule. Hakuwa na la kusema tena baada ya ukweli wa msichana yule kuweza kujulikana.
"Siku zote mimi namuomba Mungu mwanangu aweze kukulinda, wewe ndio nimekubakisha hapa duniani nategemea kukuona kila siku katika maisha yangu. Lutfia mwanangu amekupa zawadi ya akili sana na ndio maana umeweza kumtambua mapema. Safi sana mwanangu, ila yakupasa uwe makini tu."alisema mama mtu na binti yake huyo akamuitikia. Lutfia alitaka kuendelea kuongea mambo mengine baada ya kuona upendo wa mama yake juu yake lakini nafsi inamkatazama kabisa asiongee. Alisogea karibu na mama yake na kumbusu kwenye paji lake la uso kisha akarudi kwenye kiti alichokaa. Mama alitabasamu tu na kuwasha gari kurejea nyumbani na mwanaye.

Muda huohuo wale viumbe waliotumwa na Kasma waliweza kufika Hospitalini pale na kushuhudia umati ule wa watu huku askari wakiwa makini kuhakikisha utulivu unatawala eneo lile. Walitazama baada ya kushangaa wingi ule wa watu na kuamua kwenda ndani kuangalia imekuwaje. Gafla tu wakapotea pale walipo na sekunde kadhaa tu wakaweza kutokea ndani ya chumba kimoja kikionekana kina mavazi na vifaa vingi vya hospitali.
Waliamua kuchukua sare za madokta wakazivaa kusudi wasiweze kutambulika kwa wepesi lengo likiwa ni kuingia kila chumba kuangalia kile walichokinusa.

Huku nje ya Hospitali baba mmoja alikuwa pamoja na mwenzake alikuja kumuangalia mtoto wa rafiki yake aliyelazwa katika hospitali hiyo. Wakiwa kwenye kusubiri utaratibu unaoendelea alipata kupigiwa simu na mtu, alitazama namba iliyopiga na kupata kufahamu, akapokea.
"Ndio Mwalimu habari za asubuhi... Nipo hospitali kuna rafiki yangu amekuja kumuangalia mtoto wake... Sasa hivi?.. Kuna nini tena?!... NINI?... Okay Okay nakuja sasahivi.. nakuja.!"alisema baba yule kwa sauti ya hofu akakata simu.
"Vipi kuna nini?"aliuliza mwenzake aliyekuja naye kumuangalia mtoto wake.
"Aisee shuleni kwa mwanangu Tedy kuna matatizo mwalimu mkuu ndio amenipigia niende haraka, ngoja niwahi tutawasiliana."alisema yule mwanaume na haraka akatoka eneo lile na kupanda gari lake safari ikaanza kuelekea shuleni kwa mwanaye.

Huku ndani ya Hospitali wale viumbe walikuwa wakiendelea kupita kila wodi wakiwa kwenye mavazi ya udaktari hata wasiweze kutambulika na madokta wenyewe. Walipishana hata na askari waliokuwa wakiweka ulinzi kila sehemu bila kutambulika wakizidi kusonga mbele. Walifika kwenye wodi moja wakapata kuona Polisi wakiwa na madokta wakifunua makabati yaliyopangwa. Ni wazi kwamba ilikuwa mochwari, Polisi walifika kuchunguza mauaji hayo ya watoto wadogo yalitokea vipi. Walifunua maiti ya mtoto mmoja na kujionea jinsi ilivyoharobika upande wa tumboni na shingoni. Wale viumbe waliokuwa kwa nje walitazama kwa makini na macho makali sana wakapata kuona jinsi maiti ile ilivyoshambuliwa. Walistuka na kugeukiana kutazama baada ya kutambua kitu. Haraka wakatokomea na kutokea upande wa nje kabisa. Walitazama huku na kule kana kwamba wanatafuta kitu na kuamua kugawana kila mtu apite mahala pake watafute. Walishapata kujua kuwa aliyefanya mauaji yale si mtu wa kawaida hivyo kwa vyovyote hawatakuwa mbali na tukio hilo.
Na kweli kile walichokifikiria ndio kilikuwa hivyo. Alie alikuwa juu ya gorofa moja amekaa akiwatazama tu wakigawana njia za kwenda. Anawafahamu nia yao hasa ya kuja duniani. Alijikuta anashikwa na hasira hadi kubadilika sura yake na kuonekana mfu aliyeoza.

Lutfia na mama yake waliwasili nyumbani na moja kwa moja akajiyupa kwenye kochi akiwa na sare zake za shule. Alitokea yule dada wa kazi na kushangaa wamerejea.
"Mama, vipi mbona mmerudi mapema hivyo?"
"Ah we acha tu, hebu niandalie chakula sijala hapa huyu kanikurupusha asubuhi asubuhi."alisema mama Lutfia na kukaa kwenye sofa karibu na mwanaye. Yule mfanyakazi alielekea kuandaa chakula akiwaacha mtu na mwanaye pale sebuleni. Aliwasha televisheni mama Lutfia na kutafuta stesheni, alipata kuona chaneli moja ikionesha matukio yanayoendelea kule Hospitalini walipotokea. Alionekana mwanadada mmoja mwandishi wa habari akiongea hali halisi ambayo inaendelea pale Hospitali kuwa Polisi wamefika kujua kilichosababisha hadi kutokea kwa mauaji hayo. Aliongea mambo mengi sana huki Lutfia na mama yake wakitazama hadi baadhi ya watu na wazazi wa watoto waliokuwa ndani ya hospitali wakihojiwa pale na kuonyesha uchungu walionao moyoni. Huruma ilimjia Lutfia na kujikuta akisika kitabu chake akilitazama tu lile jina lililoandikwa kwenye kitabu kile, LUTKAS.
Wakati watu wakiendelea kuhojiwa na televisheni ile gari la kubeba wagonjwa mahututi( Ambulance) lilisikika kulia kin'gola chake likiwa linakuja kwa spidi hadi kufika nje ya Hospitali ile. Haraka ikaletwa machela kadhaa na kuwekwa wagonjwa waliotolewa kwenye gari lile. Watu wote waliokuwa nje ya Hospitali ile walishangaa kuona miili ya watoto wa shule watatu wakionekana kudhurika sana, damu zilitapakaa kwenye miili yao. Tukio hilo lilirushwa moja kwa moja kwenye Televisheni na kuweza kuonekana watoto wale wa shule wakikimbizwa kupata matibabu.
Alionekana baba mmoja akiwa anasaidiana na manesi kukimbiza machela iliyokuwa na mtoto. Ni yule baba aliyepigiwa simu muda ule na mwalimu akiombwa kuweza kufika haraka shuleni. Mwanaye alikumbwa na dhoruba hilo hivyo alikiwa akihakikisha mtoto wake anakuwa salama. Askari waliokuwa ndani wakichunguza miili ile ya watoto walishangaa kuona kuna watoto wengine wa shule nao wanaingizwa ndani ya hospitali ile. Walipoangalia majeraha yaliyopo kwenye miili yao ni sawa na yale ambayo yapo kwenye maiti za watoto waliouawa pale Hospitali.

Yote hayo Mama na mwanaye Lutfia walikuwa wakishuhudia kwenye runinga. Mama alimeza mate kwa tabu sana maana haamini kile anachokiona kwenye televisheni ile. Aligeuka kumtazama binti yake ambaye naye alishikwa na bumbuwazi baada ya kuwaona watoto wenzake ambao wanasoma shule moja wakishushwa kwenye gari ya wagonjwa na kuwekwa kwenye vitanda wakiwa wametapakaa famu kwenye miili yao wakiwahishwa kutibiwa. Ilimbidi mama mtu azime runinga kabisa huku akishusha pumzi kwa woga na hofu iliyoanza kumtawala.
Ilikuwa ni muda mfupi tu wametoka kule hospitali kuangalia tukio la mauaji. Hata alipotoka pale akataka ampeleke mwanaye shule kama alivyotaka mwanaye Lutfia lakini yeye hakutaka iwe hivyo na kumtaka mwanaye warudi tu nyumbani siku hiyo maana alikuwa na wasiwasi sana. Na kweli wasiwasi wake umemsaidia maana laiti mwanaye angempeleka shule siku hiyo basi tatizo hilo lingeweza kumpata hata mwanaye. Alibaki kinshukuru Mungu kwa kuweza kunusuru jambo hilo na kumuomba aweze kuleta baraka zake kwa watoto wale waliokumbwa na balaa hilo.

Ilibidi Polisi wamtafute mwalimu wa shule hiyo na kukaa naye awaeleze imekuwa hadi jambo hilo kutokea. Walimchukua na kumpeleka kituoni kuweza kumhoji kwanza huenda wakapata kitu.
"Kuna mtu uliyeweza kumuona akiyafanya haya kwa wanafunzi wako.?aliuliza Polisi akiwa na wenzake wawili wakimtazama yule mwalimu aliyeonekana kuwa na woga.
"Hapana.. sijui lolote lile. Mimi nilikuwa ofisini wanafunzi walikuwa darasani, sasa wakiwa wanaimba nyimbo za kuanza masomo na nilikuwa ofisini nawasikia. Gafla nikaona wameyulia kimya, awali nikahisi wameamua kunyamaza tu maana nilikuwa nakazi namalizia, lakini ukimya ule nilipata mashaka mara baada ya kusikia kama kuna ngurumo. Kama wanyama wanagombania kitu, ndipo nikatoka ofisini kwenda kuangalia darasa. Ah nilishangaa kuona watoto wote wakiwa wamelala kwenye madawati na baadhi yao ndio hao wametobolewa hivyo kwenye miili yao ikitokwa na damu sana. Sikuona mtu wala kiumbe yeyote pale hadi nikashikwa na mshtuko wa gafla nikapoteza fahamu. Nakuja kushtuka naamshwa na walimu wenzangu ambao nao waliweza kuona tmiili ya watoto wale na wengine ndio walikuwa wanaamka kana kwamba walilala wote kwa muda. Nikawaeleza hali halisi na ndio tukapiga kwanza huduma ya msaada wa gari kuweza kuwachukua watoto walidhurika kuwaleta Hospitali na kuanza kutoa taarifa kwa wazazi wa watoto waliodhurika."alijielezea kwa ufasaha yule mwalimu na Polisi wakamuelewa.
"Na hakuna mtu yeyote unayemuhisi labda aliyehusika na hili?"aliuliza Askari mmoja akimrazama yule mwalimu. Alitafakari na kumuangalia yule askari.
"Kuna mtu nahisi huenda anafahamu lolote."alijibu yule mwalimu.
"Ni nani huyo?"waliuliza kwa pamoja maaskari wakimtazama yule mwalimu.
"Lutfia.. mmoja wa wanafunzi wangu ambao leo hakufika shuleni."alisema yule mwalimu na kuwafanya wale askari watazamane baada ya kupata habari hiyo mpya.

LUTKAS SEHEMU YA 06


ILIPOISHIA
"Kuna mtu nahisi huenda anafahamu lolote."alijibu yule mwalimu.
"Ni nani huyo?"waliuliza kwa pamoja maaskari wakimtazama yule mwalimu.
"Lutfia.. mmoja wa wanafunzi wangu ambao leo hakufika shuleni."alisema yule mwalimu na kuwafanya wale askari watazamane baada ya kupata habari hiyo mpya.

SONGA NAYO...
"Unamaana gani kumtaja mwanafunzi wako ukimhisi anahusika angali ni mdogo?"aliuliza askari mmoja akiwa anamtazama mwalimu yule.
"Hadi nimemtaja yeye basi nimekuwa na wasiwasi naye. Si mara moja wala mara mbili nimekuwa nikimkuta darasani pekeake anaanza kujibadili na kuonekana tofauti. Anakuwa kama mfu aliyeoza sana na ndio maana kwa tukio hili lililotokea nimekuwa na mashaka naye. Ili muamini kama ndiye tazamaneni yeye hakuwepo kwenye darasa wakati haya yanatokea sasa alienda wapi kama sio ndio mhusika mkubwa." alisema yule mwalimu na kuwafanya askari wabaki njia panda.
"Mh hili swala ndio naanza kulisikia leo katika kazi yangu. Mtu abadilike kuwa mfu aliyeoza tena ni mtoto na kuanza kufanya tukio hili, hapana siamini."alisema askari mmoja na kumfanya mwalimu yule aingilie.
"Usichoamini wewe hapo ni nini? Ukweli halisi ndio huo na yule mtoto nimekuwa nikimuogopa sana tangu nimuone kwa macho yangu akiwa katika hali hiyo."
"Mwalimu, mambo kama haya ni nadra sana jeshi la Polisi kuweza kuthibithisha. Huu ni sawa na uchawi na serikali haiamini imani hizo kwakuwa ushahidi unakosekana. Mathalani nikasema sawa mtoto huyo ni mtuhumiwa lete ushahidi utatoa ushahidi gani?"aliuliza askari mmoja na kumfanya mwalimu yule akose la kusema.
"Lakini kama kweli amemuona kwa macho yake mimi nadhani huo ni ushahidi tosha. Atafutwe huyo binti aletwe hapa aulizwe. Swala dogo hilo hasa kwa mtoto mdogo anaweza akaongea ukweli."alisema askari mmoja na yule mwalimu akatetea maneno hayo. Walijadili kwa muda mrefu sana bika kupaja jibu kamili. Na baada ya muda walipofikia muafaka wakaamua akakamatwe binti Lutfia naye aje kuulizwa maswali ya kujibu lengo kutaka kujua ukweli wa mambo.
Muda huohuo Askari mkuu alitoa oda kwa vijana wake waende nyumbani anapoishi binti huyo. Yule mwalimu ndio aliwapa maelekezo wapi anapoishi mwanafunzi huyo hivyo ikawa rahisi kwa askari hao kuanza safari yako kuelekea sehemu husika. Wakaachwa askari kadhaa pale kituoni na mwalimu yule, muda mfupi aliaga kwenda maliwato mara moja. Alipofika tu alisogea kwenye kioo kikubwa kilichopo kwenye kuta na kuanza kujiangalia alivyo. Taratibu mwili wa mwalimu yule ukaenda chini kudondoka gafla na kuonekana kivuli kinatoka mwilini mwake na kusimama pembeni. Kilianza kubadilika hadi kuonekana mtu kabisa akiwa anamtazama yule mwalimu pale chini.
Hakutaka kuchelewa aliongoza njia kuelekea kule walipokwenda Maaskari.
Muda wote alikuwa akimtumia mwalimu kuongea maneno ambayo si mazuri kwa binti Lutfia akawa matatizoni, na lengo ni kutaka kumtambua binti huyo ajue tu undani wake maana hakutaka kuamini kama ni kweli binti huyo ni wa kawaida.

Muda huo mama na mwanaye walikuwa sebuleni kila mtu akiwa na mambo yake. Muda wote Lutfia alikuwa akisoma zake kitabu kile kitabu. Katika hali hiyo alipata kuona gafla karatasi zikifunguka zengewe kwa haraka hadi kufika kwenye kurasa moja ikasimama. Hali hiyo ya gafla ilimshtua Lutfia na kuona jambo hilo ni geni kwake. Lakini kwa akili zake akapata kujua huenda sehemu hiyo ikawa na maana kubwa kwake ndio maana imejifungua yenyewe.
Alianza kusoma maelezo yaliyopo kwenye kurasa hiyo, alistaajabu kuona kuna mazungumzo baina ya watu wawili wakiwa wanajibizana lengo ni kutafuta muafaka, ajabu jina lake analikuta ndani ya kitabu hicho na ndiye mtu aliyekuwa akijibizana na mwenzake. Ilibidi aweke umakini apate kusoma vizuri.
"Kwani nimefanya kosa gani hadi nipate hukumu hiyo, si nilishakueleza kuwa sijafanya jambo lolote."
"Sikia Lutfia nikwambie, hili swala usichukulie ni jepesi kama unavyodhani. Elewa aliyeuawa ni mtoto wa Mfalme na wewe ndiye mtu ambaye kutwa nzima jana ulikuwa naye. Kile kitendo cha yeye kurudi kwenye falme alianguka na kusaidiwa na walinzi kuweza kumpeleka ndani. Mfalme hatakuelewa hata kidogo maana kila mtu anajua kwamba ni wewe ndiye ulikuwa naye. Kasma tayari ameshapoteza maisha na inasadikika aliwekewa sumu kwenye chakula. Sasa nimekupa tu taarifa kwamba askari wa kifalme wanakutafuta na wamepewa amri wakukamate na lazima utauawa tu endapo ikafahamika umehusika. Kama una uwezo toroka sasahivi usisubiri lolote, Kimbia kabisa uende nje ya taifa hili."
"Hapana, hapana siwezi kufanya hivyo, naondokaje kwenye taifa hili angali sijafanya kosa lolote! Nitaondokaje nimwache mama yangu niliyekuwa naye siku zote!"
"Sahau kuhusu mama na ndio maana awali nimekwambia hili jambo usione ni la kawaida ukalidharau, unaweza poteza maisha yako elewa aliyekufa ni mtoto wa pekee wa Mfalme usishangae hata yeye akawa anakusaka.."
"Mimi nachanganyikiwa jamani hata sielewi nifanyaje ah!Sasa... ah! Sasa nafanyaje jamani, nitaenda wapi mimi.!"
"Mimi nitakushauri jambo moja kama utalikubali sawa. Kimbilia kwenye falme ya Maskoof. Hawa wana uadui mkubwa na ufalme wetu hivyo itakuwa ni ngumu wao kukufuata pindi uingiapo humo."alisema yule mtu kumuelewesha Lutfia. Alikosa hata nguvu ya kusimama na kujikuta akikaa kwenye gogo lililo pembeni yao. Alitafakari inakuwaje jambo ambalo hajafanya lakini limekuwa ni kesi iliyokubwa kwake. Ushauri aliyopewa wa kuweza kuondoka kwenye taifa hilo aliona mgumu sana kwake maana anajua atamwacha mama yake akiwa mpweke. Lakini upande wa pili aliona ni bora kwake kuondoka kuliko kubaki akapata adhabu hata kuuliwa akamuacha mama yake milele. Alimtazama yule mtu aliyekuwa akiongea naye muda huo na kuona bora afate kile alichoshauriwa.
"Sawa, nitafanya hivyo."alikubali kwa unyonge na hakuwa na jinsi bora aokoe maisha yake.
Yule mtu alimsogelea Lutfia na kunyoosha mkono wake wa kulia kuhitaji ashikwe na binti huyo. Muda huohuo jeshi la Mfalme lilipa kuwasili eneo hilo baada ya kuwafuatilia kwa muda mrefu na kujua kuwa mhusika wanayemtafuta yupo kwenye msitu huo. Mmoja wa maaskari hao alipata kuwaona Lutfia na yule mtu na haraka akawajulisha na wenzake wakawa wanawafuata kwa haraka sana.
Lutfia naye alinyanyua mkono wake na kuweza kushikwa na yule mtu na muda huohuo kukaanza kuonekana kimbunga kikubwa sehemu ile waliyosimama. Macho yao wote wawili yakabadilika hali iliyowafanya wale askari wastaajabu. Nao hawakutaka kuwapoteza baada ya kujua wanataka kukimbia wakatia upinde na mishale wakaanza kuwashambulia mfululizo na kwa bahati, mishale ile ilitua mwilini mwa mtu yule aliyeugulia kwa sauti maumivu aliyopata. Lutfia alishangaa kuona vile na kushuhudia yule mtu macho yake yanarudi kama awali kuonesha kweli amejeruhiwa vibaya.
"Usijali.. Lazima utaondoka tu hapa."alisema yule mtu huku akionesha kuzorota mwili. Alikosa hata nguvu ya kusimama imara lakini hakukubali kufeli wala kuvunja ahadi ya kumtorosha binti huyo kwenda kwenye falme nyengine. Lutfia alipata kuona wale askari wakizidi kuja karibu na pale wali. Alishangaa anakumbatiwa kwa nguvu zote na yule mtu huku akipiga kelele anachomoa kitu chenye ncha kali mwilini mwake. Yalikuwa ni maumivu ya mishale iliyopenya mgongoni mwake akimzuia Lutfia asiweze kudhurika.
"Mimi nipo nyuma yako hawawezi kukukamata abadani, kamata hiki kitabu. Nadhani kitakusaidia huko uendako."alisema yule mtu akiwa amemkumbatia binti Lutfia, alitoka kitabu hicho kwenye nguo yake kuukuu na kumpatia binti huyo.
"Lakini kwanini unajitolea sana kwaajili yangu bila kujali maisha yako?"aliuliza Lutfia akionesha kumuonea huruma.
"Wewe ni bora kwangu, usijali kuhusu mimi ipo siku tutaonana tena ila kwasasa nenda kwenye taifa la Maskoof japo yataka utumie akili za ziada na ushawishi mjubwa ili waweze kukuamini na kukupokea. Waeleze ukweli wa mambo wala usiwe muongo kwenye maelezo yako kwani Mfalme wao ana uadui mkubwa sana na mtu yeyote muongo, naomba nikuage na kamwe usikae mbali na kitabu hicho."alisema yule mtu na taratibu akaanza kuonekana kupuputika kama vumbi hali iliyomfanya hata Lutfia ashangae. Wale askari walibaki kustaajabu kuona tukio hilo na kusahau kabisa lengo lao hasa ni kumkamata binti hiyo. Mavumbi hayo yalipotea hewani na ndio ukawa mwisho wa myu yule aliyekuwa katibu sana na Lutfia.
Naye bila kuchelewa alikamata kile kitabu na kuyafumba macho yake huku wale askari wakianza kumsogelea haraka. Alipofumbua hakuweza kuwa Lutfia yule wa awali, macho ya kutisha yenye kiwaka kama miale ya mwanga mkali yalipata kuonekana. Alitamka maneno kadhaa na punde tu akapata kutokea eneo lile akiwaacha wale askati wakibaki kushangaa tu.

Yote hayo alikuwa akiyasoma Lutfia kwenye kile kitabu chake akiwa zake sebuleni na mama yake. Kwa matukio yale aliyoyaona alipatwa na mshangao yu kuona kumbe hata jina lake limepata kitumika ndani ya kitabu.
"Lakini huyu Kasma aliyesadikika ameuliwa na Lutfia kwa kuwekewa sumu ni nani? Na hili jina langu limekujaje humu?. Ah kumbe ni maneno tu ya kitabu maana nishahisi ni kweli nimeua maskini nikaogopa."alisema Lutfia na kujikuta akitabasamu baada ya kusoma kurasa kadhaa kwenye kitabu kile cha LUTKAS.
Muda mfupi baadae ulipata kusikika mlango kugongwa. Ilimbidi yule dada wa kazi akafungue mlango kujua ni nani anayebisha hodi. Hata alipofika mlangoni alishtaajabu kuwaona askari watatu wakiwa katika mavazi yao ya kazini.
"Bila shaka hapa ndio kwa Mr.Kassim. Na tumemkuta mkewe mama Lutfia.!"aliongea Askari mmoja akiwa anamtazama yule mfanyakazi. Aliwatazama kwa hofu na kuitikia kwa kutikisa kichwa kumaanisha ndio penyewe.
"Haya turuhusu tuingie tuna mazungumzo naye mara moja."alosema askati yule na kumsogeza dada pale mlango na wao wakaingia bila kuruhusiwa. Mama Lutfia alishangaa kuona askari wanaingia gafla tu ndani kwake. Lutfia alipowatazama wale askari alishtuka sana maana hakutegemea kabisa.
Walitoa salamu kwa mwenye nyumba hiyo na lengo lililowaleta hapo ni kumhoji binti yake.
"Mwanangu amefanya nini tena?"ni swali ambalo lilimfanya hata mwanaye abaki kuwatazama wale askari.
"Kuna mambo nahitaji kumuuliza. Hivyo nahitaji kuongea na yeye mhusika kwanza huenda akanipa mawili matatu."alisema askari na kumfanya mama mtu apate woga kwa ujio ule bila kujua kimetokea nini hadi mwanaye kuhitajika. Wale askari wengine walikuwa wakiitazama nyumba ile kwa ndani jinsi ilivyo wakionesha umakini wao. Alisogea askari yule hadi pale alipo Lutfia akiwa ameshika kitabu. Yule askari alikaa na kujenga tabasamu. Alikitazama kile kitabu kilichoonekana kwa nje herufi kuu za kusomeshea kwa yale madarasa ya awali. Alitazama pembeni na kuona vitabu vyengine vya masomo tofauti.
"Unaitwa nani wewe?"aliuliza yule askari huku akimtazama Lutfia.
"Lutfia."alijibu kwa kulitamka jina lake.
"Lutfia nani?"
"Mnamuhitaji nani kati ya sisi? mama, baba au mimi?"aliuliza Lutfia huku macho yake yakiwatazama wale askari wengine waliosimama mlangoni kwa ulinzi.
"Usijali, tumekuja kwa wema tu wala ondoa shaka. Lengo la kuuliza jina la baba yako ni kumfahamu tu."
"Mlipokuja bila shaka huko mlipotoka mlielekezwa nyumbani kwa Mr.Kassim ndio hapa na naamini hata dada aliwafungulia mlango na mkalitaja jina la baba ili mpate uhakika. Sasa yule pale ndiye mkewe na mimi ni binti yao, haya nikutajie tena jina la baba yangu au ushalijua?"aliuliza Lutfia na kwa maneno yale tu yakampa jibu yule askari kwamba binti huyo ana kipawa cha kuongea.
"Basi sawa tuachane na hayo. Kuna swala moja hapa tunahitaji kufahamu kutoka kwako. Una taarifa zozote kuhusu tukio lililotokea shuleni kwenu?"
"Kumetokea nini?"
"Kuna mauaji yametokea wanafunzi watatu wameuawa."
"Mh sijasikia hilo swala ndio napata taarifa yako."
"Basi sawa kama ndio umesikia muda huu hali halisi ndio hivyo. Miili imepelekwa hospitali na tulikuwa na mkuu wa shule akatuambia kuna wanafunzi ambao hawakugika shule hivyo tukaona yuje kuwapa taarifa hizo kila mmoja wenu na kuwatoa hofu upelelezi unaendelea tutawabaini waliofanya hayo."alisema yule askari na Lutfia akaitikia. Alisimama yule askari na kumpatia taarifa hizo pia mama mwenye nyumba hiyo japo taarifa hiyo waliifahamu kabla lakini kwakuwa wanahojiwa na Polisi na mwanaye ameonesha kutojua chochote naye akajifanya ni mgeni wa hilo. Muda mchache wale askari wakapata kuondoka kidogo mama mtu ashushe pumzi maana alikiwa anaogopa mwanaye kupata na shida.
"Vipi upo salama mwanangu, maana nyumba hii haikuwahi kuingia askari humu hawa ndio wa kwanza, nikajua watakukamata na wala sjajua wamefuata nini hasa cha maana wanatutisha tu."
"Wala usijali mama, wale sikuwa nawaogopa hata kidogo japo sina uhakika sana wa akili zangu ila nimefahamu tu huenda hawa ndio wanahusika."alisema Lutfia na kumshangaza mama yake.
"Wewe mtoto hebu nyamaza, hao Polisi wanahusikaje na tukio hilo wakati ndio wanachunguza kujua ukweli."
"Niamini mama mimi ni mwanao. Hawa sio watu wa kawaida, tangu walipoingia tu nilipowatazama, hawakuwa binadamu. Sura zao zilikiwa zinatisha kama majini na ndio maana nikawa nawatazama tu wale wawili waliosimama nipate kuwaona vizuri. Hawa ndio wanaanza kuiharibu dunia na kutaka kitu chao. Wamekuja duniani kutafuta kitabu."alisema Lutfia na kumfanya mama yake ashangae. Alinyanyuka kwenye kiti alichokalia na kunyanyua mto akatoa kile kitabu huku akimuonesha mama yake.
"Hiki ndio kitabu wanachokitafuta siku zote, na kamwe hawataweza kukipata. Na endapo wakikipata basi dunia inauwezekano mkubwa watu wakaja kubadilika na kuwa tofauti , watakuwa kama wao. Hawa ndio wameua kule Hospitali na hawa ndio wamenipoteza rafiki zangu shuleni."alisema Lutfia kwa maelezo mazuri, alimwacha mama yake kushika tu mdomo haamini kile ambao anakisema mwanaye. Alinyanyuka pale alipo Lutfia na kumsogelea mama yake na kumshika mashavu.
"Mama.. hivi unaweza kukaa kuvumilia siku ngapi usinione mwanao?"
"Luftia, mbona unaongea hivyo! Unafahamu fika wewe ndio kila kitu kwangu siwezi na sitapenda ukae mbali na mimi mama yako."alisema mama mtu na kuishika mikono ya mwanaye ikiwa mashavuni kwake.
"Basi sawa, ila nakuomba sana anza kujifunza kukaa mbali nami kwa muda tu mama yangu na nina maana kubwa sana."alisema Lutfia akizidi kumchanganya mama yake.
"Unamaana gani tena jamani mbona sikuelewi.?"
"Kuna safari nahisi nitaenda, japo sijanua nikienda nitarudi lini lakini naamini nitarudi mapema kwaajili yako."alisema Lutfia huku akimtazama mama yake aliyebaki njia panda.
"Safari gani hiyo mwanangu?"aliuliza mama mtu na muda huohuo mlango wa nje uligongwa. Tena safari hii uligongwa kwa mkupuo na haraka yule dada wa kazi akaenda kufungua mlango, alistaajabu anasogezwa pembeni na kupata kuingia askari watatu hadi ndani. Mama Lutfia alipowaona wale askari tena akanyanyuka.
"Nyie mmefuata nini tena hapa? Au kuna kitu mmesahamu?"alionhea kwa hasira mama mwenye nyumba baada ya kufahamu wale wamejigeuza askari wakati ni viumbe tofauti.
"Maamaa!"aliita Lutfia na kumfanya mama yake ageuke kumtazama.
"Waache hao ni askari."alisema Lutfia kwa sauti ya upole na kumfanya mama yake apoe baada ya kujua kumbe hawa ndio wenyewe haswa.LUTKAS SEHEMU YA 07


ILIPOISHIA
"Maamaa!"aliita Lutfia na kumfanya mama yake ageuke kumtazama.
"Waache hao ni askari."alisema Lutfia kwa sauti ya upole na kumfanya mama yake apoe baada ya kujua kumbe hawa ndio wenyewe haswa.

TUENDELEE
Alirudi nyuma na kusimama kwa heshima huku akiangalia chini.
"Bila shaka hatukukosea nyumba, hapa ndipo kwa marehemu Mr.Kassim."aliongea askari mmoja akionekana ndiye mkubwa wao kwa wenzake wawili aliokuja nao. Mama Lutfia aliitikia na kuwasikiliza.
"Sisi ni askari kutoka kituo cha upelelezi na tumekuja hapa kwa dhumuni moja tu, tunahitaji tuongozane na binti yako kituoni kuna maswali anapaswa kujibu, na kama akitupa majibu yenye kueleweka tutamrudisha."alisema yule askari na kumfanya mama Lutfia amtazame.
"Amefanya nini hadi mtake kuondoka naye?"
"Kuna upelelezi wa jambo fulani tunahitaji kupatia kweli."
"Yaani muondoke naye? Mumpeleke wapi mwanangu pekeake. Sitotaka binti yangu aondoke na watu tu angali mimi nipo. Naomba sana kama akienda nitakuwa pembeni yake sitotaka kumuacha mwanangu kwakweli. Nawaombeni sana."alisema mama huyo na yule askari akakubaliana naye. Askari huyo alisogea karibu na Lutfia akachuchumaa na kuwa sawa naye.
"Kuna mahala tunaenda kukuulia maswali kidogo ukimaliza utarudi na mamako sawaò."
"Niahidi kama mkimaliza kuniuliza nitarudi nyumbani."alisema Lutfia kwa kujiamini na askari yule akakubaliana naye hivyo. Hakuwa na pingamizi alishuka kwenye kiti na kushikwa mkono na askari yule wakaanza kutoka nje. Alikuja dada yule wa kazi na kuachiwa maagizo na mama Lutfia. Alichukua simu yake na kuanza kufuata nyuma kisha wale askari wengine wakafuata wakiwa nyuma yake. Hata walipofika nje walipanda kwenye gari na safari ikaanza kuelekea kituoni.

Upande wa pili wale viumbe waliotumwa na Kasma kuhakikisha wanapata kujua wapi kilipo kile kitabu cha LUTKAS, walikuwa wakitembea kila mji huku wakitumia hata nguvu zao za ajabu kuweza hata kutambua lakini ilikuwa ni kazi ngumu kwa upande wapo na hawakukata tamaa abadani. Wanajua amri imetoka kwa Malkia wao hivyo lazima wahakikishe wanapata kile kilichowaleta duniani japo si kazi rahisi kuweza kufanikiwa kwa wepesi.

Yule mwalimu aliweza kuonekana pale Polisi tena akiwa amekaa kwenye kiti akizidi kuhojiwa na askari. Hii ni baada ya kurejea kutoka maliwato kama alivyoomba. Walizidi kumuuliza maswali mengi ambayo yaliweza kuwaridhisha kwa kile ambacho amekuwa akiwajibu. Muda mfupi baadae waliwasili wale askari waliokuwa na binti Lutfia huku mama yake akiwa na mwanaye, moja kwa moja waliingia hadi kituoni na kuwafanya askari wote waliokuwa kituoni hapo wamshangae binti huyo mdogo. Walishapata taarifa zake kwa kile ambacho kimetokea hivyo kwa umbo lake tu liliwashangaza sana wote mule kituoni. Hata mama mtu alipata kushangaa kuona hali ile mwanaye akitazamwa na askari namna ile. Akajua huenda kuna jambo baya limetokea dhidi ya mwanaye maana sio kawaida.
Lutfia alibaki kuwatazama nao na kufahamu huenda kuna taarifa mbaya wameisikia kutoka kwake na ndio maana ameweza kushikiliwa na Polisi. Alipogeuka pembeni alipata kuona sura ya yule Mwalimu wake wa shule. Lakini ajabu akajikuta kupatwa na hofu kubwa sana iliyomfanya ahisi utofauti. Alimsogelea hadi pale alipokaa mwalimu na kumpa heshima yake wakabaki kutazamana. Askari alimshika mkono Lutfia na kumtaka waingie kwenye chumba cha mahojiano wakiwa wawili. Ilibidi Lutfia aongozane na Polisi yule akiwa na mwenzake huku akimuacha mama yake akiwa amekaa kumsubiri.
"Kaa kwenye kiti."alisema Polisi akimuamuru Lutfia akae baada ya kuingia kwenye chumba kimoja wakiwa watu watatu tu. Binti huyo akafuata kile alichoambia na kukaa.
"Haya, nahitaji kufahamu majina yako."aliongea askari yule akikaa na yeye huku akimtazama binti huyo.
"Naitwa Lutfia Kassim."alijibu.
"Unasoma.?"
"Bila shaka,nasoma."
"Unaweza kunikumbusha kati ya juzi au jana kitu gani mmejifunza shuleni kwenu?"
"Hapana sikujifunza kitu chochote siku hizo mbili kwakuwa sikufika shuleni."
"Kwanini hukufika shuleni?"
"Nililazwa hospitali nilikuwa na matatizo, na sio siku hizo mbili tu nahisi wiki nzima sikuweza kitokea shuleni."
"Unasumbuliwa na nini?"
"Mimi sijui, ila mama yangu ndio anafahamu ugonjwa wangu."alisema Lutfia na kuwafanya wale askari watazamane.
"Sasa mama yako aliwaambia shuleni kama unaumwa?"
"Bila shaka. Wanajua walimu wote kuanzia wa darasa langu hadi mwalimu mkuu walipata taarifa zangu. Na uzuri wake hata mwalimu mkuu amefika hapa nimemsalimia."
"Sawa, na lini ulitoka hospitali.?"
"Nimetoka hospitali jana."alisema Lutfia na kuwafanya askari wale watazamane kuona kumbe wamemchukua mtoto angali bado si mzima.
"Una uhakika wa hicho unachosema?"
"Nililazwa katika hospitali ya Presbyterian takribani wiki na nilipopata nafuu na kuonekana naweza hata kutembea nikaruhusiwa. Hata mkienda hospitalini kupata uhakika mnaweza kwenda."alisema Lutfia kwa kujiamini sana, hali iliyofanya wale askari waamue kumuita mama yake hadi mule ndani akapata kukaa.
"Mama tumekuita hapa utueleze ukweli wa mambo, tunaomba kufahamu mwanao alilazwa hospitali kwa tatizo ugongwa gani.?"aliuliza askari mmoja akimkazia macho mama Lutfia ambaye swali lile lilimfanya ageuke kumtazama mwanaye ambaye hakuonesha dalili za kujua lolote. Alimeza mate kidogo kisha akageuka kumtazama yule askari aliyemuuliza swali.
"Mwanangu anatatizo la kupoteza kumbukumbu, pia huwa anaweweseka sana, hali hii ilimpata tangu akiwa mdogo kabisa na nilijitahidi kuhakikisha anapata matibabu ili apate kupona kabisa lakini swala hili limekuwa gumu japo kwasasa kuna afadhari na ndio maana hata shule amekuwa akisuasua kuhudhuria. Ni jana tu ndio ametoka hospitali alikuwa kalazwa hivyo hapo bado hayupo sawa na ndio leo mmekuja kutuchukua tuje hapa kituoni."alisema mama Lutfia na maelezo yake yakiendana na yale aliyosema binti yake.
"Sasa mama sikia, kuna kesi hapa ya mauaji imepata kutokea shuleni kwa mwanao anaposoma. Watoto watatu wameuawa kikatili kabisa na katika kupeleleza tukapata kuambiwa na kiongozi wa pale shuleni akiwa anamhisi binti yako. Hii ni kwasababu ya kumuona binti yako si mara moja akibadilika na kuwa kiumbe wa ajabu, anakuwa kama mfu mwenye kutisha. Sasa kwa maelezo yake aliyotueleza na tukiangalia na yale mauaji jinsi watoto wale walivyofanyiwa hadi kupoteza maisha tunapata picha moja yenye ukweli. Sasa unavyotuambia kuwa alikuwa Hospitali binti yako tunashindwa kuamini haya mambo, tumuamini nani kati yanu."alisema askari yule akionesha yupo makini na kazi yake.
Mama mtu baada ya kusikia habari za mwanaye kuhusu kubadilika alishtuka maana anafahamu mwanaye kuna uwezo anao lakini hakuwahi kusikia mahala kama mwanaye amebadilika na kuweza kudhuru binadamu.
"Haha hapana kwakweli huyo aliyesema hayo anadanganya. Lutfia ni mwanangu wa kumzaa na hata siku moja sijawahi kumuona katika hali hiyo wala kusikia kwa watu hata shuleni kwao pia kama amekuwa hivyo mnavyosema. Hii ni taarifa mpya na ngeni kwangu kuisikia kwakweli."alisema mama akimtetea mwanaye.
"Huu ni upelelezi wa awali tulioufanya na katika hilo ndio tumepata mtu aliyetuambia habari hizo, hivyo jukumu letu ni kuhakikisha tunapata ukweli na kujua mhusika wa tukio hilo. Hivyo sitakataa kama sio mwanao wala sitakubali hayo maelezo yako kwa haraka. Hii ni kesi hivyo tutazidi kufuatili na tutapeleleza zaidi na kwengine ili tumpate mhusika maana hata hiyo hospitali inayosemekana mwanao alilazwa kumetokea mauaji ya watoto kumi na wanne. Hebu uwe ni wewe Polisi, halafu mwanangu hayupo shule amelazwa hospitali. Siku anapona anaondoka hospitali kunatokea mauaji ya watu zaidi ya kumi, siku hiyohiyo shuleni anaposoma mwanangu kunatokea mauaji ya watoto watatu. Utakosa kuwa na wasiwasi juu ya mwanangu ikiwa kunatokea taarifa kwamba anahisiwa kuhusika?"aliuliza askari yule akimtazama mama Lutfia ambaye alikosa hata neno la kusema.
"Askari, bila shaka una mtoto, anasoma shule gani?"aliuliza Lutfia kwa sauti upole na wote wakamgeukia kumtazama.
"Mwanangu alikuwa anasoma shule na Seminary ila nimemuhamisha kwasasa kuna mwalimu anakuja kumfundisha nyumbani tu."alijibu yule askari.
"Je, na leo hii ukirudi nyumbani kwako ukute kuna taarifa za watoto watatu wa Seminary hawaonekani wamepotea. Ila mwalimu wa shule hiyo akawa anamhisi mwanao kwakuwa watoto wale walikuwa wanampenda sana mwanao huenda kuhama shule kwa mwanao kumefanya tukio hilo litokee. Je mwanao atapata kesi ya kuwapoteza wenzake?"aliuliza Lutfia huku akimtazama askari yule aliyebaki kumuangalia tu mwenzake. Kimya kilitawala kwa sekunde chache mule ndani na binti huyo akaendelea.
"Kifo ni mipango ya Mungu, ila hutumia njia mbalimbali kukamilisha tukio husika. Nawezaje kuyafanya hayo yote angali bado naumwa? Na kama nadhaniwa si mtu wa kawaida madaktari ndio wangegundua katika vipimo vyao hospitalini kule nilipolazwa. Kwani mfu anakuwa bado anadamu? Maana nimetolewa damu yangu ikapimwa na madokta huku nikishuhudia. Mimi nashauri muende na hospitali huko huenda daktari akawa ameona kitu tofauti mwilini mwangu na mkapata uhakika zaidi kuhusu mimi."alisema Lutfia kwa upana zaidi. Maelezo yake tu yakamfanya Askari apate kutoa akilini ile kesi inayomhusu binti huyo. Lakini mwishowe akaamua kumuita kabisa yule mwalimu mule ndani na kumruhusu akae. Alimtazama akionekana kuwa na wasiwasi muda wote.
"Unamfahamu huyu binti?"aliuliza yule askari. Yule mwalimu aliitika kuwa anamfahamu.
"Wewe ndio mwalimu wa shule anayosoma si ndio!"
"Ndio ni mimi mwalimu wake."
"Ulikuwa na taarifa za kuumwa kwa binti huyu?"aliuliza askari yule.
"Kuumwa? Mh hapana."alisema yule mwalimu na kumfanya hata mama Lutfia amshangae.
"Hee wewe mwalimu! Si wewe ndiye tuliyeongozana hadi hospitali na ukamuona kabisa Lutfia amelazwa akiwa hajitambui. Au sio wewe mwalimu Alphonce.!"alisema mama Lutfia akimshangaa mwalimu yule aliyeonekana kutojua ugonjwa wa Lutfia.
"Mimi? Hapana kwakweli, unamtetea tu mwanao mama na huenda ukweli na wewe ukawa unaujua. Askari niamini kile nilichosema, huyu ni mwanafunzi wangu muda wote nipo naye hadi jioni ndio anarudi kwao hivyo namfahamu tabia yake kuliko hata mama yake. Amini kile nilichokisema, huyu sio mtoto wa kawaida."alisema Mwalimu Alphonce akionesha kushikiria msimamo wake.
"Askari...."aliita Lutfia na kuwafanya wale askari wamtazame.
"Huyu sio mwalimu wangu, amini ninacho waambia huyu sio mwalimu. Na kwa kuhakikisha kuwa huyu siye naomba utoe amri waletwe wanafunzi wenzangu walau watatu waje hapa na huyu anayejiita mwalimu atuongoze wimbo wa shule tuimbe sote maana ni yeye ndio aliyeutunga na kutufundisha wimbo huo. Hapo ndipo tutaamini nani mkweli maana hata mimi ninahisi huyu ndiye anahusika na mauaji ya wenzangu."alisema Lutfia na kuwafanya wale askari washangae. Walimgeukia yule mwalimu aliyeonekana kushtuka baada ya kuambiwa hivyo. Hata mama yake alimshangaa mwanaye baada kuyasema hayo.


LUTKAS SEHEMU YA 08


ILIPOISHIA
Walimgeukia yule mwalimu aliyeonekana kushtuka baada ya kuambiwa hivyo. Hata mama yake alimshangaa mwanaye baada kuyasema hayo.

TUENDELEE
"Unamaanisha nini kusema hivyo? Inamaana huyu siye mwalimu wako?"aliuliza askari wa pili huku akimtazama binti huyo.
"Moyo wangu unakataa kuwa huyu siye. Alichosema mama kuhusu mwalimu Alphonce ndio tabia yake. Mwalimu alikuwa rafiki kwangu na ndio maana alikuja Hospitali. Mwalimu wangu hawezi kunisahau, mwalimu wangu hawezi kuongea maneno kama haya huenda akawa sio yeye."alisema Lutfia akizidi kuwaaminisha askari wale.
Yule mwalimu alibaki kushangaa tu kuona hata askari wanamsikiliza binti yule. Kwa akili za haraka akataka kulikwepa zoezi hilo akijua lazima ataumbuka maana hana analojua lolote. Alibaki kumtazama Lutfia tu ambaye naye hakuweza kuyatoa macho yake kumtazama mwalimu huyo.
"Kwa mliyoyafanya kuua watoto wasio na hatia ni dhambi kubwa sana na lazima mtalipa kwa hilo mlilolifanya."yule mwalimu alishangaa kusikia maneno hayo masikioni mwake akabaki anashangaa tu kutafuta sauti hiyo ilipotokea.
"Sasa kazi kwako uchague kudhalilika mbele ya Polisi uondoke mwilini kwa huyo mwalimu sasa hivi. Una muda watoka nadhani ulichokuwa unakitaka sasa umekipata, mimi ndiye hasa uliyekuwa ukitaka kujua kama nipo vipi."
Hakika alishangaa yule mwalimu kuona mtu anayeyasema hayo muda wote alikuwa ni yuleyule mhusika aliyemsakizia kesi ya mauaji ya wenzake.Walikuwa wakisikilizana wawiki tu na hakuma mwenyine aliyeweza kusikia. Hata yeye alitabasamu tu baada ya kuujua ukweli leo kwamba ni kweli binti Lutfia si mtu wa kawaida.
Alikuwa ni Alie ndani ya mwili wa mwalimu yule akijaribu kumuweka matatizoni Lutfia akijua huenda akatumia nguvu zake kujitoa mikononi mwa Polisi. Na mwisho wa yote anajitambulisha mwenyewe binti huyo na kujionesha dhahiri kuwa yeye ni nani hasa. Alicheka sana pale na kuwafanya hata wale askari wamshangae mwalimu huyo, aliamua kunyanyuka pale na kuanzisha vurugu lakini Polisi wale walimuwahi na kumtwanga ngumi kadhaa papo hapo akaenda chini na kupoteza fahamu. Muda huo ndio Alie aliutumia kutoka mwilini mwa mwalimu yule na mtu pekee aliyeweza kumuona alikuwa ni Lutfia. Walibaki wakitazamana kwa macho ya shari hata baada ya muda aliamua kuondoka zake Alie.
Wale askari walimuangalia yule mwalimu na kupata kufahamu kuwa amepoteza fahamu hivyo walimuweka sehemu kwanza apate kutulia. Waliweza kuwaruhusu Lutfia pamoja na mama yake huku wakiwataka muda wowote endapo watawahitaji waweze kufika kituoni hapo maana kesi hiyo bado ipo kwenye upelelezi.

Waliongoza njia na kuanza safari ya kurudi nyumbani baada ya kupewa ruhusa hiyo. Mama mtu alikuwa akimtazama tu mwanaye aliyekuwa pembeni yake.
"Hivi ulikuwa na maana gani mwanangu kuongea mbele ya Polisi kwamba yule sio mwalimu wako?"aliuliza mama mtu akiwa anaendesha gari.
"Tangu tunaingia pale kituoni nilipomuona tu nilipata kutambua kuwa si yeye. Yule alikuwa kiumbe ambaye ndio wamesababisha mauaji ya wenzangu shuleni na hata kule hospitali. Ndio maana hata alikuwa haelewi kama uliwahi kwenda naye kule hospitali kuniangalia kipindi nimelazwa."
"Haa kumbe!.. Sasa ah..! Sasa walitaka nini kutoka kwako tena hadi wanakuweka katika matatizo haya?"
"Hawa walikuwa wananifuatilia kwa muda mrefu sana. Wacha tufike nyumbani nitakueleza ukweli wote utapata kuufahamu mama yangu, maana kwasasa tayari washanijua mimi ni nani."alisema Lutfia na kugeuka pembeni akawa anaangalia magorofa nje wakiyapita gari likiwa kwenye mwendo. Mama mtu alipatwa na mashaka kwa kile alichoambiwa na mwanaye, ilibidi azidi kukanyaga mafuta wafike nyumbani ili apate kuambiwa ukweli wa mambo yanavyokwenda.

Alie alifika mahala ambapo walikuwepo wenzake wakimsubiri. Walionesha kuhangaika kutafuta kitabu kile cha LUTKAS kila kona bila mafanikio.
"Hatimaye leo nimepata kufahamu jambo ambalo nadhani litatusaidia kupata kile tunachokitaka kama sio kufanikiwa kabisa. Yule niliyekuwa nadhania kuwa ana nguvu na uwezo mkubwa wa kutumia kile kitabu nimeweza kumpata. Na ninaamini kwa asilimia zote yeye ndiye mwenye kitabu cha LUTKAS maana hakuna mtu ambaye angeweza kukaa na kitabu hicho bila ya kuwa na maono, uwezo na upeo wa kukitumia. Yule binti ni wa kumfuata kwa hali na mali, kwa uwezo wetu wote tuhakikishe LUTKAS kinarudi mikononi mwetu haraka sana maana kuna kundi la wengine wanakitafuta pia."alisema Alie akiwaeleza wenzake, waliposikia habari hizo walipata tumaini jipya tena la kufanikiwa jambo lao. Walianza kupanga mikakati ya kuanza kufanikiwa kile walichokipanga. Kitabu hicho kinamaana kubwa sana kwao na ndio maana wanafanya juu chini waweze kukipata kabla ya watu wa Malkia Kasma kuweza kukitia mikononi.

Wakati wanapanga hayo ili wafanikiwe upande wa pili wale watu wa Kasma walikosa wapi watapata kitabu kile kama walivyoagizwa. Maana hata uwezo walionao haukuweza kusaidia kutambua wapi kilipo kitabu hicho jambo ambalo si kawaida. Ilibidi waamue kurudi tena katika jamii yao kuyoa taarifa ya kutopata muelekeo wowote na hawajui watafanikiwa kwa namna gani. Hata walipofika moja kwa moja wakaelekea kwa malkia wao Kasma na kuweza kumueleza hali halisi ilivyokuwa tangu wanaanza kazi hiyo. Ilikuwa na swala geni kwa Malkia huyo mdogo kuambia hawajapata kuona wala kujua wapi kilipo kitabu hicho. Hakutegemea kama jambo hilo litakuwa na uzito wa kiasi hicho, ilibidi awaite wale wazee na kuwaeleza hali halisi kama alivyoelezwa na watu wake waliokwenda duniani kutafuta kitabu cha LUTKAS bila mafanikio. Walijadiliana kwa muda kila mtu akitoa wazo lake ili wapate muafaka wa pamoja. Lakini wazo la mmoja wao lilikuwa ni kimshirilisha mtabiri wa mambo yajayo ili kama ataweza kujua kama ataweza kuona wapi kilipo kitabu hicho kwasasa na nani mwenye kukimiliki kwa muda huu huenda ikawa ni rahisi kwao kutambua wapi waanze.
Ilibidi wamuite mtabiri huyo na kumualika kwenye kikao hicho cha muda na kumueleza jambo hilo na hali halisi ilivyotokea pindi walipotuma vijana wao kwenda kutafuta lakini hawakufanikiwa.
Yule mtabiri baada ya kuambiwa hayo alitoka na kwenda kuchukua vifaa vyake vya kazi ili kuangalia mambo yanavyokwenda. Malkia alikaa na wazee wakuu wakiangalia kile anachokifanya yule mtabiri.
Alichanganya madawa yake na kuzungusha sehemu fulani kama duara huku akiwagia unga mwekundu katikati akiongea maneno ambayo hayakuweza kueleweka kwa wepesi. Mwisho wa siku alitoa kioo chake kikuukuu na kuanza kutemea temea mate huku akikifuta kwa usinga. Kasma alibaki kutazama tu mambo ya mtabiti huyo pale na kushuhudia kile kioo kikiachiwa mikononi na kudondoka kwenye jiwe lililopo chini ajabu hakikuweza kupasuka wala kutokwa na ufa wowote, hata mtabiri yule alishtuka kuona tukio hilo. Ilibidi ainame kuokota kile kio na kuanza kukisomea maneno fulani kisha akakitemea tena mate na kukifuta na usinga akakiachia tena kikadondoka hadi kwenye jiwe lile lakini hakikuweza kuvunjika. Aligeuka kumtazama Malkia pale alipokaa akiwa naye anamuangalia mtabiri huyo.
"Inamaana gani hiyo?"aliuliza Kasma akiwa amezungukwa na wale wazee wote wakiangalia kinachoendelea.
"Malkia wangu, inaonesha kitu mnachokitafuta kipo kwa mtu ambaye anauwezo mkubwa sana, ana nguvu za asili tena zenye uwezo mkubwa sana. Sidhani kama anaweza kuachia kitu ambacho mnakitaka na nyie pia."alisema yule mtabiri na kuwafanya hata wale wazee watazamane.
"Inamaana hakuna uwezekano wowote ule wa sisi kuweza kukipata?"aliuliza Kasma Malkia wa jamii hiyo.
"Kama kioo chepesi kimeshindwa jupasuka kwenye jiwe gumu hili mara mbili ni wazi kwamba swala hilo ni zito mno. Kama itakuwa na ulazima wa kupata kitu hicho basi inatakiwa nguvu kubwa sana itumike na sio watu watatu au wanne kama ulivyowaagiza watu wako."alisema yule mtabiri.
"Inamaana mtu mmoja tu huyo waende watu zaidi ya kumi kweli?"aliuliza mzee mmoja alionesha kushangzwa na jambo hilo.
"Ndio ninavyoona hapa, anaonekana ana nguvu sana."alisema mtabiri na kuwafanya wote pale wabaki kutafakari wanafanyaje.

Huku duniani Lutfia alikaa na mama yake chumbani kwake akimueleza yale yote ambayo awali aliyaficha na hakutaka mtu yeyote atambue. Lakini kwakuwa tayari ameshajulikana na Alie kule Polisi hakuona haja ya kumficha tena hata mamake.
"Yule aliyemuingilia mwalimu kumtumia kituoni ndio alitumia njama kuweza kumuingiza kwenye matatizo mwalimu wangu ambaye ndiye amenikabidhi hichi kitabu cha LUTKAS."alisema Lutfia na kumfanya mama yake ashangae.
"Haa, kwani yule si ndio aliyekupatia hichi kitabu na ukasema alikuwa anakufundisha?"aliuliza mama mtu huku akiwa amekishika kitabu hicho.
"Hapana, aliyenipa kitabu hicho ni ndugu yake wa damu kabisa na huyu ambaye alijifanya ni mwalimu. Yule alikuwa na upendo sana kwangu na alikuwa rafiki wa dhati kwangu. Aliniambia kwamba nimepata bahati ya kuwa na kitu kwenye akili yangu, na kweli nilijikuta namfahamu na kujua kuwa hakuwa mtu kama sisi bali alikuwa tofauti kabisa. Hata alipojibadilisha na kujionesha kuwa yeye ni nani siweza kumuogopa. Japo alikuwa anatisha sana, alikuwa mfu aliyeweza kuishi tena. Na nilipotaka kufahamu kwanini yumzima angali alikufa ndipo akanipa kitabu hichi na kunitaka nikisome kila siku kwa utaratibu maana kina maana kubwa sana. Nilipokiangalia tu sikuweza kujua kilichoandikwa mule ndani lakini akanipa moyo na kuniambia atanisaidia hadi niweze kujua kusoma. Alikuja hata usiku humu ndani na kuniamsha tukawa tunasoma wakati wewe umelala. Tulikuwa tunaonana kwa hivyo hadi shule akawa anakuja kunifundisha na nikajikuta namuona kama mwalimu wa pale maana alikuwa dujakinifundisha kupitia ubao uleule wa shule. Siku ya mwisho kuonana naye alikuja akiwa amebadilika na kuwa na sura ya huzuni sana na kuniomba niwe makini sana na hata akaamua kuniachia kila kitu alichonacho kwake na kuniwekea mimi na yeye akaamua kutoweka kabisa asiwepo kusudi ampe wakati mgumu ndugu yake huyu wa kutafuta kitu anachokitaka. Na tangu alipotokomea alimwacha kweli Alie katika wakati mgumu wa kutafuta kitabu hichi kilipo. Alinambia kuwa yeye na Alie walikufa muda wakiwa na nguvu fulani walizopewa na baba yao ambaye alimwachia kitabu cha Uhai ambacho kinaweza kuwarudisha watu waliokufa na kuwa watu tena wa kawaida, na Alie alitaka kurudi tena duniani na kutaka awe na roho tena ya binadamu kitu ambacho hakutaka abadani arudi maana alikuwa ana mipango mibaya hapo mbele na ni yeye ndiye aliweza kumuua baba yao ili aweze kurithi utajiri wake. Mwalimu wangu hakuweza kuvumilia hili walipambana na Alie na ndio sababu ya kupelekea wachinjane bila huruma na ndio ikawa siku ya mwisho kuishi duniani kama watu wa kawaida. Lakini kwa mwenzake alitaka kupata kitabu hicho ili arudi kama zamani, na ndio maana hadi leo hii Alie yupo duniani kutafuta hichi kitabu akishirikiana na wenzake wakijua endapo wakikipata basi wanarudi kuwa watu wa kawaida. Na endapo wakifanikiwa hilo basi kuna mengi atayafanya na huenda damu hizi za watoto zikawa maradufu kitu ambacho mimi Lutfia sitakubali itokee. Na muda mfupi tu mama yangu huenda nikawa mbali na wewe kama nilivyokwambia awali."alisema Luftia akimuelewesha mama yake yote hadi kufika hapo.
"Mh mwanangu Lutfia, wapi tena unaenda?"aliuliza mama mtu na kumfanya binti yake achukie kitabu kile kufunua ile kurasa aliyosoma ikionekana mtu anayeitwa Lutfia akiwa amekumbatiwa na yule mtu aliyepigwa mishale na watu wa Mfalme.
Walianza kumsogelea Lutfia akiwa pale, punde tu macho yake yakabadilika na kuwa makali yenye kuwaka sana. Hata wale watu wakahamaki kuona vile, alipiga ukelele wa nguvu na kufanya kutokee upepo mkali sana ulioanza kukusanya kila kitu kilichopo eneo nile na muda huohuo naye akapotea eneo lile na kuacha upepo ukivuma sana.

"Mama... nakwenda kwenye falme ya Maskoof. Sijawahi kufika huko, sipajui na hata sijui nitaenda kukutana na nani huko awe mwenyeji wangu ila naamini nitakuwa salama mama yangu."alisema Lutfia kwa kujiamini akimwambia mama yake.

Huku upande wa pili Kasma alimuamuru yule mtabiri ajaribu kumtazama huyo mtu ambaye ananguvu hizo ambazo hadi wao hawawezi kumgusa.
Yule mtabiri alifanya kazi yake hiyo na kuangalia mtu huyo mwenye nguvu hizo. Alipotazama kwenye kioo alishtuka kumuona mtu huyo, ilibidi anyanyue uso kumtazama malkia wake ambaye macho yake yalikuwa yakimtazama mtabiri huyo.
"Vipi umemuona?"aliuliza Malkia huku wale wazee wakimuangalia mtabiri yule. Ilibidi asogee na kumpatia kile kioo malkia Kasma atazame mtu huyo mwenye uwezo mkubwa.
Wale wazee wote walishtuka baada ya kuona kwenye kioo sura ya mtu huyo na kubaki kutazamana kwa mshangao. Malkia Kasma alibaki ameduwaa baada ya kuona sura yake ikiwa kwenye kioo kile kuonesha ndiye yeye mtu mwenye nguvu anayesadikika kuwa na kitabu hicho wanachokihiji.

LUTKAS SEHEMU YA 09


ILIPOISHIA
Malkia Kasma alibaki ameduwaa baada ya kuona sura yake ikiwa kwenye kioo kile kuonesha ndiye yeye mtu mwenye nguvu anayesadikika kuwa na kitabu hicho wanachokihiji.

TUENDELEE
"Imekuwaje naonekana mimi tena hapa?"aliuliza Kasma akiwa ameshikilia kile kioo. Hata wazee wenyewe walibaki njia panda hawaelewi. Iliwabidi watazame viziri tena kioo kile na kuweza kuona ni sura ya Malkia wao kabisa,Kasma. Hata yeye alijaribu kurudia kutazama zaidi na zaidi kama anaweza kuona utafauti baina ya yule anayeonekana kwenye kioo kile pamoja na yeye mwenyewe lakini hakukuwa na tofauti yeyote.
"Hicho ndicho kinachoonekana kwenye utabiri wangu na hata mimi sifahamu hili swala linakuwake. Kama mhusika tunayemuangalia anakuja sura yako basi ni wazi wewe ndiye mwenye hicho kitabu kinachotafutwa."alisema yule mtabiri.
"Unaongea ujinga gani wewe? Yaani ninawezaje kutafuta kitu ambacho ninacho mwenyewe? Huu ni ujinga kama imeshindikana kutambua mtu huyu basi hili zoezi tukubali limekuwa gumu kwetu tuangalie mambo mengine ya kufanya."aliongea Kasma kuonesha kukasirishwa sana kile kinachoendelea.
"Malkia wangu, naomba nisamehe kwa lolote ambalo nimekukwaza, sikuwa na maana mbaya kusema hivyo ila nimeongea kile ambacho nakiona katika utabiri wangu. Samahani sana kwa hilo."alijishusha yule mtabiri kwa kuona huenda amemkwaza malikia wake.
"Hili swala ni la kufanyia kazi mjue inakuwaje maana haiwezekani nipate kuonekana kwenye kitu ambacho sina."alisema Malkia na kunyanyuka kutembea tembea sehemu zengine. Aliwaacha pale wale wazee na yule mtabiri wamekaa tu kila mtu akisema la kwake.
"Hili swala linawezekanaje mbona tunachanganyikiwa?"
"Huenda labda ni maono tu hapo mbele akaja kuwa anauwezo huo bila yeye kujitambua."
"Au wapo wawili hawa ndio maana tunaona hivi?"yalikiwa ni maswali wakijatibu kuyachambua wao kwa wo. Lakini swali la mwisho lilizua mjadala wa papo kwa hapo na kumfanya hata yule mtabiri aingie tena kazini kuangalia kama hawa watu wapo wawili au laa.
Alifanya kila njia kuangalia ili wapate kuujua ukweli. Kasma pamoja wa jopo la wazee wale walikuwa wakimtazama tu mtabiri apate kuongea kile ambacho anakiona. Muda mchache yule mtabiri akaanza kutabasamu baada ya kutazama kioo chake na kuona maelfu ya watu wakishangilia sana kwenye uwanja mkubwa sana. Ilibidi asogee na kumpatia tena Malkia Kasma aweze kutazama na wale wazee. Alipotazama kwenye kioo kile alipata kujiona akiwa juu ya jukwaa kubwa huku mkononi akiwa ameshika kitabu. Alijikuta akianza kutabasamu Kasma baada ya kuona kuna kila dalili za yeye kuweza kufanikiwa kukipata kile kitabu hali iliyofanya hata wazee wale wapatwe na wimbi la furaha.
"Hili swala linatakiwa lifanywe haraka iwezekano kitabu kipatikane mapema. Tunavyoendelea kutazama tu kwa macho jinsi mambo unavyoendelea bila kufanya lolote."alisema Kasma aakitazama kile kioo kinachozidi kumpa hamasa ya kujiona ipo siku atakuja ashangiliwe na umati wa watu zaidi ya hawa anaowaongoza. Alijiona huenda hapo mbele akafanikiwa zaidi baada ya kupata kitabu kile ambacho amekuwa akihitaji kiweze kuwa mikononi mwake.

Huku nyumbani kwa Mama Lutfia alikuwa akimtazama mwanaye akiwa anajiandaa. Safari ambayo amekuwa akiitaja kuweza kwenda ndio imefika muda wake hivyo alihakikisha anaweka mambo yake sawa.
"Sasa huko unapokwenda mwanangu unapanda gari gani hadi kufika huko?"aliuliza mama mtu kutaka kufahamu maana haelewi.
Lutfia aliachia tabasamu tu na kugeuka kumtazama mama yake.
"Hapa utanisindikiza hadi karibu na kwenye Green Forest. Nadhani ukiniacha pale nitajua wapi naelekea."alisema Lutfia akionesha kutokuwa wa hofu.
"Lakini mwanangu hayo unayoyafanya kwako unaona ni kawaida? Hivi kuna mama ambaye ataridhia amkose mwanaye kwa kufanya mambo ambayo anajua ni hatari.?"aliongea mama mtu kwa uchungu na hisia za upendo kwa binti yake.
"Mama, tambua kwamba mimi ni tofauti na binafamu wa kawaida hivyo hayo mambo unayohisi ni hatari kwangu haipo hivyo. Na sio kwamba kuna kipya kitakwenda kutokea, ninafanya mambo nafuata hichi kitabu kama kilivyoandikwa hivyo usijali kuhusu mimi mama yangu."alisema Lutfia akimpa moto mama yake aliyeonekana kuwa na mashaka juu ya mwanaye. Waliongea mengi hasa kwa mama mtu aliona jambo hilo kama la utani lakini ni wazi na ukweli kwamba binti yake anaondoka na kuelekea sehemu ambayo ilipatwa kuandikwa kwenye kitabu kile cha LUTKAS hivyo anafuata kama ilivyoandikwa humo.
Muda ulipofika alijiandaa na mama mtu akaandaa usafiri wa kumpeleka mwanaye sehemu husika. Alijikuta anaamini tu kile kilichopo kwenye kitabu kile hivyo hata jambo la binti yake kuondoka halikumfanya atie kipingamizi juu ya hilo. Alikiamini kitabu kile ambacho kwake aliona ni kama msaada kwa binti yake hasa akifikiria kipindi alichokuwa anaumwa Lutfia nacho kikaweza kumtuliza maumivu yake.
Njiani waliongea mambo mengi sana huku akiamini safari ya mwanaye itakuwa yenye amani na kuweza kurejea akiwa salama.

Wakati hilo likiendelea kule kwa Kasma alipata kuangaliziwa na yule mtabiri na kuweza kufahamu kwamba mtu wanayemuona anayemiliki kitabu hicho ana muda mchache wa kuondoka duniani. Kauli hiyo ilimfanya Kasma ashtuke baada ya kujiaminisha kwamba mtu huyo ni yeye kama alivyoweza kujiona kwenye kioo.
"Inaonesha kwamba kuna mahala mtu huyu anakwenda, na ni sehemu ya kifalme ndipo anafikia. Sasa sijajua kama Malkia wetu nawe ulipanga kwenda sehemu yeyote kwa kipindi hiki?"aliuliza yule mtabiri na kumfanya Kasma atafakari kama aliwaza kutoka nje ya taifa lake. Hakuwahi kufikiria hata siku moja kama ataweza kutoka nje ya taifa lake analoongoza jambo ambalo nikafanya kuwashangaza hata wale wazee.
"Basi kama ni hivyo huenda huyo mtu akawa anaufanano na wewe kwa kila kitu, maana kila ninachokiona hapa kwake basi kipo kwako. Lakini sidhani kama kwa uwezo alionao mtakuwa sawa. Na huyu anaonekana ndiye mwenye uwezo mkubwa sana kuliko yeyote yule. Kama nilivyosema awali huyu mtu si wa kufuatwa na mtu mmoja, na kama kuna umuhimu wa kumpata basi yakipasa hata wewe Malkia uwepo na watu wako ili msaidie kama mnahitaji kupata hicho kitabu."alisema yule mtabiri kumfahamisha Kasma.
Hakutaka kusubiri tena muda huohuo alinyanyuka kwenye kiti chake na kuelekea kwenye chumba fulani. Wazee wakabaki kujadiliana kwa sauti ya chini pale walipo huku yule mtabiri akitazama utabiri wake unavyoonekana.
Muda mfupi tu alirejea Kasma akiwa amevalia mavazi ya vita, alikuwa tayari kufanya lolote kwaajili ya taifa lake. Alitoa amri waandaliwe jeshi la watu 50 apate kuongozana nao haraka. Zoezi hilo lilikuwa la dakika chache tu wakawa tayari kumsikiliza Malkia wao.
"Tunakwenda duniani na dhamira yetu ni moja tu, kupata kitabu cha LUTKAS. Tutazunguka maeneo yote yale na kama utapata kumuona mtu anayefanana na mimi basi haraka toa taarifa kwa wengine ili mpate kusaidiana. Kuna mtu anafanana nami, na ndio anayesadikika kuwa na kitabu hicho. Inasadikika ana uwezo mkubwa wa kututambua na hata kujilinda mwenyewe hivyo yatupasa tuwe makini naye. Matumaini yangu kwa umoja huu hili zoezi litakwenda kama tulivyopanga."alisema Malkia Kasma na jeshi lake likatii kukubali kile alichosema. Malkia Kasma aligeuka kuwatazama wale wazee akiagana nao kuwaachia waiongoze falme hiyo pindi yeye na jeshi lake wakijaribu kumtafuta mwenye kitabu wanachokihitaji.
Baada ya muda alipata kuonekana kubadilika gafla Kasma huku upepo mkali ukianza kuvuma na kuja kimbunga kabisa kikizunguka pale walipo wote na sekunde chache tu kukatulia. Wazee wale walionesha kutabasamu kuona tayari wameshaondoka hivyo jukumu la kuilinda falme ipo mikononi mwao.

Huku upande wa pili Alie alipata kuona gari la mama Lutfia njiani akiwa anaendesha. Alikitazama lile gari na kutafakari mahala lilipotokea. Ilibidi asogee hadi pale barabarani huku magali mengi yakizidi kupita tu na hayakuweza kumgonga maana ni kiumbe kilichokufa muda tu. Aliinama na kushika ile barabara papohapo ubongo wake ukashika mawasiliano na mkono ule ukaanza kuonesha njia zote alizopita mama Lutfia kwa gari lake hadi sehemu aliyotokea. Alishangaa kuona gari lile likitokea maeneo ya msituni. Alisimama huku akiwa mwenye kujiuliza mama huyo amefuata nini huko msituni alipotoka. Alianza kuwa na wasiwasi juu ya safari hiyo ikabidi apotee haraka pale barabarani kuelekea gari likipotokea.

Lutfia akiwa anaangaza macho yake huku na kule pale msituni akiangalia mahala pa kuanzia bila mafanikio huku akiwa na begi lake la nguo mgongoni na kitabu chake mkono wa kulia. Hakujua afanye nini maana alisoma tu mwenye kitabu na kuona mahala pa yeye kufika katika falme ya Maskoof ni kwenye msitu huo aliowasili yeye baada ya kusindikizwa na mama yake. Alipata kutokea mbele yake mtu mmoja na haraka aakamsogelea Lutfia pale aliposimama.
"Mwalimu!"alihamaki Lutfia baada ya kumuona mtu anayemfahamu.
"Hakuna muda wa kuendelea kusubiri tena. Tuondoke haraka.!"alisema yule mtu akionesha kutokuwa na imani na mahala pale, alimshika mkono Lutfia na kutaka kuanza kukimbia sehemu ile.
"Sitaweza kukimbia na begi hili Mwalimu, na imekuwa umerudi tena angali uliniambia unakwenda kuishi mbali baada kutoweka duniani?"alisema Lutfia huku akiwa anakimbizwa bila kupenda. Yule mtu aligeuka na kumtazama Lutfia, akitazama begi lile alilovaa binti yule kwa macho makali na kufanya mikanda ya begi kukatika na kuweza kudondoka chini. Alichukua kile kitabu cha Lutfia na kukihifadhi ndani ya koti lake kubwa alilovaa. Ikawa ni rahisi kwa wawili hao kuweza kukimbia sasa huku wakiongea baada ya kuliacha begi pale.
"Nimerudi kwaajili yako, hautaweza kufika huko unakopaswa kwenda na ndio maana nimekuja kukusaidia."alisema yule mtu na gafla akapata kutokea Alie mbele yao kuwafanya wasimame kukimbia mbele.
Wakabaki wanatazamana yule mtu pamoja na Alie kwa macho ya kutisha sana. Alipotazama kwenye koti la yule mtu alipata kuona kuna kitu kinatoa mwanga mkali sana kwa ndani. Akafahamu ni kile kitabu ambacho wamekuwa wakikifuatilia duniani na wenzake, hatimaye leo kipo mbele yake.
"Miaka mingi hatukuonana ndugu yangu Kasam. Hatimaye leo tumekutana tena katika mazingira tofauti."alisema Alie akionesha tabadamu la kutengeneza akimtazama ndugu yake. Ni yule mtu aliyemsaidia Lutfia kipindi chote na kumkabidhi binti huyo nguvu zake zote baada ya kuona ndugu yake Alie amekuwa adui namba moja wa kutaka kitabu kile cha LUTKAS ili akitumie kuweza kurudi kuwa mtu wa kawaida pamoja na wenzake. Jambo ambalo Kasam hakutaka abadani litokee akifahamu kufanya hivyo kutaleta matatizo kwenye dunia.
"Naona bado unashikilia msimamo wako wa kurudi duniani, sijui umepatwa na tamaa ya aina gani Alie ndugu yangu. Kwanini lakini hukubali kushindwa? Nani sasa atakaye ridhia kuwa karibu nawe karibu, nani atakayeridhia kuwa na ukaribu na mtu aliyemuua mzazi wake kwa tamaa ya.."
"Inatosha Kasam! Yote ulitaka wewe na mama yako ambaye alikupendelea kwa kila kitu, akamfanya baba amchukie mama yangu ili azidi kupendwa yeye pamoja nawe. Kipindi alipouawa mama yangu mbele ya baba niliumia sana na nikaweka dhamira ya kufanya kitu kama alichofanyiwa mama yangu. Ndio ni mimi nilimuua baba tena kwa mikono yangu miwili, na nilifanya hivyo baada ya kuona amekupa nguvu zaidi na kukuzawadia na kitabu cha Uhai wewe wakati mtu aliyepaswa kupewa nilikuwa mimi mtoto wake wa kwanza. LUTKAS ni mali yangu mimi na sio wewe! Na hadi narudi tena duniani lengo langu ni moja tu, nahitaji LUTKAS."alisema Alie na kumfanya nduguye atabasamu.
"Unachekesha ndugu yangu, nadhani ulikuwa ufahamu maana halisi ya neno LUTKAS ndio maana hadi sasa wahangaika kufuatilia."alisema Kasam na kumtazama Lutfia.
"Huyu ndiye mtu wa anayepaswa kumiliki kitabu hiki, LUTFIA ndio jona lake. Jina lenye herufi tatu kwenye kitabu cha LUTKAS, nadhani jina langu unalifahamu hivyo utapata jibu kamili juu ya kitabu hicho unachosema chako angali majina yanajionesha. Nilipaswa kuwa wa kwanza kumiliki milele kitabu hiki lakini baada ya sisi wawili kutoweka duniani basi zawadi hii imefika kwa binti huyu. Na sidhani kama utaweza kumpindua hadi kupata unachokitaka, maana kuna mwenzake pia atafuata nahisi ndiye atanisaidia kukamilisha jina halisi la LUTKAS pindi nitakapoenda kupumzika milele. Hivyo huna vita na mimi tena, una vita na wenye kitabu hiki."alisema Kasam na kwa maneno yake yakampandisha hasira Alie akatoka kama umeme pale aliposimama kutaka kumvamia ndugu yake lakini hakufanikiwa, kwani Kasam alikuwa mwepesi zaidi ya maelezo akiwa amemshika Lutfia walipotea eneo lile wakamuacha Alie peke yake.
Alipoona atapata kazi kubwa sana ikabdi aite wadu wenzake hata dakika haikupita wakagika eneno lile wakiwa wengi sana na kuwapa majukumu ya kuzunguka msitu mzima maana kiyu wanachokitafuta kipo mikononi mwa watu waliopo ndani ya msitu huo.

LUTKAS SEHEMU YA 10


ILIPOISHIA
Alipoona atapata kazi kubwa sana ikabidi aite wenzake hata dakika haikupita wakafika eneno lile wakiwa wengi sana na kuwapa majukumu ya kuzunguka msitu mzima maana kitu wanachokitafuta kipo mikononi mwa watu waliopo ndani ya msitu huo.

TUENDELEE.
Walisambaa kila eneo kuwatafuta wahusika na lengo hasa ni kupata kitabu. Muda huo Kasam na Lutfia walitokea upande wa pili ambapo ndipo kunasadikika ni sehemu maalumu ya kuanza safari hiyo ya kuelekea kwenye falme ya Maskoof. Kasam aligeuka na kumtazama Lutfia aliyeonekana kuwa mkimya sana.
"Nadhani ndio muda pekee wa wewe kuelekea mahala unapostahili. Nakuomba sana ufikapo huko fuata kile ambacho kimeandikwa katika kitabu maana ndio kila kitu. Tambua kwamba kitabu hiki ndio kila kitu kwako, ndio mwongozo wa maisha yako hivyo ukae ukikilinda pasitokee mtu yeyote akashika wala kukupokonya kitabu hiki. Kama hawa washafahamu kwamba unacho basi lazima watakuandama. Na ndio maana nikataka uende katika falme ya Maskoof nikijua fika hawa hawataweza kufika huko wanavita kubwa sana na falme ya utawala wa taifa hilo."alisema Kasam na maneno yale yakamfanya Lutfia akumbuke kwenye kitabu aliwahi kusoma siku ile akiona Lutfia anaongea na mtu msituni akimshauri aelekee kwenue falme ya ya Maskoof. Alihisi ndio tukio lile linajitokeza tena siku hiyo. Wakati wanatafakari hayo kundi la Alie lilifika eneo hilo wakionekana kila mtu kushika mishale na taratibu wakaanza kiwasonhelea wahusika. Hali ile ikamfanya hata Lutfia aamini sasa kile kilichoandikwa kwenye kitabu kile ndio ile siku wanashambuliwa kwa mishale.
"Usihofie kuhusu hilo Lutfia ukiwa na mimi amini upo kwenye amani tele. Mimi nipo nyuma yako na lazima utafika tu."alisema Kasam na muda huohuo akaanza kubadilika macho yake na kumkumbatia Lutfia pia naye hali hiyo ikawa hivyo. Wakina Alie walipoona vile wakajua wanaachwa, haraka wakaanza kirusha mishale kuelekeza kule walipo wawili hao na kwa bahati mishale ile ikatua mwilini mwa Kasam ambaye alipiga ukelele wa maumivu anayoyasikia. Lutfia alis
htuka kusikia vile na kutazama mwilini mwa mwalimu wake huyo kukijaa mishale mirefu iliyozama. Picha ikamjia ndio siku ile akisoma kile kitanu hili tukio lililipata kutokea. Mishale ilizidi kitushwa lakini Kasam alimkumbatia kwa nguvu zote Lutfia kuzuia asije dhurika na mshale wowote.
"Lakini kwanini unajitolea vyote hivi hadi kuhatarisha maisha yako Kasam?"aliuliza Lutfia akiwa mwenye majonzi ya kumuonea huruma Kasam. Alijenga tu tabasamu japo maumivu makali anayasikilizia Kasam. Alitazama pembeni na kuona kikosi cha wakina Alie wakiwa wanakuja haraka wawawahi pale walipo.
"Lutfia, wewe ni bora kwangu, usijali kuhusu mimi ipo siku tutaonana tena ila kwasasa nenda kwenye taifa la Maskoof japo yataka utumie akili za ziada na ushawishi mjubwa ili waweze kukuamini na kukupokea. Waeleze ukweli wa mambo wala usiwe muongo kwenye maelezo yako kwani Mfalme wao ana uadui mkubwa sana na mtu yeyote muongo, naomba nikuage na kamwe usikae mbali na kitabu hicho." alisema Kasam huku akimtazama Lutfia. Maneno hayo yalimfanya binti huyo akumbuke kwenye kitabu kile alichosoma aliambiwa hivyo na yule mtu aliyemsaidia kule msituni na kumpa ushauri wa kukimbia kwenda falme ya Maskoof. Hakuamini kile anachosikia ndio vile vile alivyopata kusoma.
"Hapana, sitaki kuamini kile nilichosoma! Inamaana.. Ah!
"Amini kile ulichosoma ndio kitakavyokuwa, LUTKAS hakidanganyi kila kitu kilichomo mule basi kitakamilika kama imepangwa. Naomba ufanye kile unachoona kinafaa katika maamuzi yako Lutfia wala usiyumbishwe na mtu. Mimi naamini kila kitu kitakwenda sawa."alisema Kasam huku akimpatia Lutfia kile kitabu chake tena. Muda huohuo akaanza kuonekana kupuputika kama unga na mwishowe kupotea kabisa. Akabaki amekishikilia tu kile kitabu na papo hapo herufi zinazowakilisha jina lake katika kitabu kile zikapata kuonekana kun'gara sana huku mwanga ukianza kuonekana. Mwanga uliwafanya wakina Alie waliokuwa wakimkaribia waamini huenda watamkosa. Alijaribu kuongeza spidi akitumia nguvu zake lakini haikusaidia. Lutfia alipotea gafla pale alipo na kumfanya Alie apige ukelele wa nguvu uliofanya baadhi ya miti iliyo pembeni kukatika.
Hakika alikasirika sana na hakutegemea kama angekosa kupata kile alichohitaji muda mrefu. Aligeuka na kuwatazama wenzake wakiwa wameinama chini kuona zoezi hilo limeshindikana japo wamelipigania kwa muda mrefu hadi hapo.

Muda huohuo Kasma pamoja na jopo lake nao baada ya kufanya tafiti zao walipata kuhisi mahala ambapo angeliweza kuwepo mhusika wanaomhitaji. Walifika nao kwenye msitu ule na kuanza kutembea huku na kule kupata kuona kama wataweza kuona lolote.
Hisia za viumbe tofauti kifika eneo hilo zilitanda kwa Alie pamoja na wenzake wote wakageuka nyuma huku wakinusa harufu, walifahamu kuna viumbe wengine wameingia sehemu hiyo hivyo iliwafanya haraka wapotee eneo hilo kujificha.

Kasma na wenzake walizidi kuzunguka kila sehemu kuweza kupata uhakika wa kile walichofuata. Hata walipofika mbele alipata kuona begi la nguo likiwa chini ikamlazimu kuinama huku akilitazama. Alifungua zipu na kutoka baadhi ya nguo zilizopo mule akaweza kuona zinalingana kabisa na umbo lake. Yote hayo yakiwa yanaendelea Alie alikuwa sehemu akichungulia huku akiwa amepewa mgongo na Kasma hivyo aliachwa kwenye sintofahamu hakuweza kumtambua mapema.
Kasma alishangaa kuona vile na hapo ndipo akaamini kweli huenda kuna mtu anaendana na kufanana naye. Aligeuka akiwa ameshika nguo ile kuwaonesha wenzake. Kitendo cha kugeuka tu Alie alishtuka baada ya kumuona kwa sura, alihisi kama haoni vizuri ilimbidi atazame kwa macho makali ili apate kuona vizuri.
Ni wazi kwamba alichofikiri ni kumuona Lutfia tena kwa mara nyengine wakati mhusika alionekana kupotea.
"Mbona sielewi hapa, huyu ni nani tena?alibaki kujiuliza mwenyewe huku akiendelea kushuhudia sura ya Kasma ambayo ni vilevile na alivyo Lutfia.

"Inaonekana huyu mtu kweli alikuwa eneo hili hadi nguo zake hizi tunaziona hapa. Hivyo tusichoke kutafuta huenda tukafanikiwa jambo letu."alisema Kasma kuwaambia watu wake wakamuelewa. Iliwabidi waendelee kuzunguka tena kutafuta kama watafanikiwa kumpata mhusika. Yote hayo alikuwa akiyasikiliza Alie na kubaki njia panda maana wanaonekana pia kumfuatilia Lutfia, je huyu anayefanana naye ni nani. Au kuna mchezo unachezeka ili asielewe kinachoendelea?. Ni maswali ambayo yalibaki akilini mwake bila kuyapatia jibu kamili. Naye hakutaka kuendelea kuwachungulia, alizidi kuwafuatilia kujua mwisho wao.

Ilipata kusikika kengele yenye mlio mkubwa ikilia mfululizo. Watu wa mji huo wakaanza kukimbia kwa haraka kuweza kusogea panapo mlio huo wa kengele unapotokea. Ikawa ni vurumai ndani ya mji kila mtu akikimbia kwa haraka sana huenda ni kama sheria kwao.
Katikati ya soko Lutfia alijikuta akitokea eneo hilo na kubaki tu kushangaa. Aliona umati wa watu wakikimbia uelekeo mmoja si mkubwa wala watoto wote walifanya hivyo. Japo alikuwa na mawenge haelewi mahala alipofikia ni sehemu gani lakini naye akajiongeza na kuamua kukimbia na wenzake huku akiwa ameshika kitabu chake kwa makini. Alipata kumuona mtoto mwenye rika kama lake akionekana kuchafuka nguo zake zikiwa zenye kuchakaa. Ilimbidi aongeze kasi hadi kumfikia wakawa wanakimbia pamoja.
"Watu wanaenda wapi mbona wote wanakimbia kuelekea sehemu moja?"aliuliza Lutfia huku akimtazama yule binti mdogo. Aligeuka naye kumtazama anayemuuliza kuanzia juu hadi kwenye chini viatu. Kwa muonekao ule akajua huenda ni mgeni wa eneo hilo.
"Wewe ni mgeni hapa Maskoof?"aliuliza binti yule na kumfanya Lutfia atambue kuwa tayari yupo kwenye jamii ya Maskoof kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Hakuwa na uharaka wa kumjibu binti yule akihofia huenda akakubali alichoulizwa kikamletea shida hapo baadae.
"Hapana, ila nilikuwa nje ya mji kwa muda kidogo na leo ndio nimerejea hivyo sielewi utaratibu wa hapa unaendaje."alisema Lutfia wakiwa wanakimbia.
"Ahaa sawa, utakapofika kwenye uwanja utapata kufahamu tunachoitiwa."alisema yule binti na kuongeza kasi kuwahi mbele. Alimwacha Lutfia akiwa njia panda haelewi wanakimbia kwaajili gani. Ilimbidi naye aongeze spidi kwenda kushuhudia huko mbele.

Umati wa watu wote uliingia kwenye uwanja mkubwa sana ambao ulitengenezwa kama uwanja wa mpira wa miguu. Ulikuwa na mahala pa watu kuweza kukaa hivyo kila mmoja alikwenda kutafuta sehemu yake akae. Lutfia alibaki kushangaa baada ya kuona uwanja huo mkubwa ukianza kujaa watu kila sehemu. Alitazama kaikati ya uwanja akaona kuna sehemu maalumu imejengwa kama jukwaa. Alipotazama viziri pale chini alishyuka kuona damu zikiwa zimetapakaa pale chini ya jukwaa lile. Walikuja vijana watatu wakiwa na mandoo ya maji kila mtu wakaanza kumimina pale chini kuweza kuiondoa ile damu ili pakae safi.
Alijikuta akiwa na wasiwasi juu ya tukio lile Lutfia, ilimbidi naye atafute mahala aweze kukaa ili kusubiri kinachoendelea. Kelele za watu zilisikika baada ya kuonekana askari wanaosadikika ni wa mfalme wakiwa wanakuja huku wameshika silaha mbalimbali za chuma. Mapanga, mashoka, sululu na hata misumeno ya kukatia miti mikubwa iliweza kuletwa pale na kiwekwa kwenye meza maalum. Makelele yalipozidi ndani ya uwanja ule yakafanya Lutfia azidi kuchanganyikiwa asijue kuna kitu gani kinaendelea pale. Alijikuta akiziba masikio yake asipate kusikia kelele zile ambazo kwake hazikuwa na maana yeyote.
Muda mfupi baadae walionekana askari wengine wa Mfalme wakiwasili huku wamewashika baadhi ya watu waliokuwa wamefungwa minyororo mikononi pamoja na miguuni huku miili yao ikiwa uchi wa mnyama. Watu walishangilia kwa kupiga kelele za mfululizo huku wakiwatazsma wale watu walioonekana kama watumwa.
Lutfia alipowatazama tu moyo wake ulipata kwenda mbio sana na kuwa mwenye hofu kubwa asielewe kwanini. Hakika alijionea udhalilishaji ule kwa binadamu wale walioomekana hata kukauka midomo yao huki damu kwenye miili yao zikiwa zimekauka kabisa.
Ilisikika sauti ya askari akitangaza kwa sauti kuwa Mfalme na Malkia wanaingia kwenye kiwanja hivyo hivyo kila mtu alinyamaza kimya huku wakisimama kwa heshima yao. Lutfia alinyanyuka pia kufuata wenzake wanachofanya lakini macho yake yakiwa yanapekua kutaka kuwaona hao viongozi wa jamii hiyo ambayo ni ngeni kwake.


LUTKAS SEHEMU YA 11


ILIPOISHIA
Lutfia alinyanyuka pia kufuata wenzake wanachofanya lakini macho yake yakiwa yanapekua kutaka kuwaona hao viongozi wa jamii hiyo ambayo ni ngeni kwake.

TUENDELEE.
Ulinzi ulionekana mkubwa sana wa kuwalinda viongozi hao wawili hadi walipofika kwenye jukwaa lile lililoandaliwa imara. Lutfia alipata kuwaona viongozi hao wakiwa pamoja , walivaa mavazi ya kifalme yenye thamani kubwa sana huku yakipambwa na vitufe vya dhahabu. Hakuwahi kuona mavazi hayo kwa macho yake zaidi ya kuona kwenye televisheni.

Walisogezwa wale watu waliokuwa uchi na kuanza kufunguliwa mmoja na kushikwa na askari wawili wakamsogeza hadi kwenye meza iliyo na silaha zile. Alionekana kufurukuta akijaribu kujinasua kwa askari hao lakini haikuwa rahisi. Mfalme alisimama muda huo na kusogea mbele huku akiwatazama raia wake waliofurika kwenye uwanja huo huku wote wakiwa kimya.
"Siku zote amani ndio kitu tunachojivunia ndani ya Maskoof. Upendo baina yetu ndio kitupekee kinatutofautisha na mataifa mengine. Na haya yote yametokana na kuweka mikakati na sheria ili zifuatwe na watu wote ili twende mbele zaidi. Sasa panapotokea mtu anakwenda kinyume basi uongozi hautakuwa na huruma naye kuendelelea kumchekea angali amekosea. Ni sheria halali kabisa kwa mtu kama huyo aweze kunyongwa mpaka kufa,kukatwa baadhi ya viungo hadi kufa au laa upewe sumu kali upate kunywa. Sasa hawa wenzetu.. "alisogea Mfalme hadi kwa wale watu waliokua uchi wa mnyama.
"Hawa walikamatwa na askari wangu wakijaribu kuingia ndani ya falme kujaribu kuiba dhahabu. Na nilipowahoji walikanusha swala hilo kuwa hawakufanya, jambo ambalo hakuna asiyefahamu kuwa sipendi uongi. Na hili la wizi ni kosa na ni wizi ambao umekithiri hadi kuamua kuingia kwenye falme yangu inamaana umejipanga kufanya hivyo. Kuna wengine wameingia katika taifa langu bila idhini yeyote, wamekuja kubadilisha amani yetu, wamekuja kuwabadilisha hata watu wa taifa hili na ndio hawahawa wamekuwa wezi hadi kudiriki kuingia kutaka kuiba. Sasa hawa wanakuwa mfano kwenu ili kusudi kama kuna anayeanza kuiga ajifunze kutokana na hili."alisema Mfalme na kuamuru mmoja wa wale watu akasogezwa vizuri pale kwenye meza ile na kulazwa. Mfalme alikamata upanga mkali wenye kun'gaa. Baadhi ya watu waliokaa mule uwanjani waliwaziba macho watoto wao wakijua kitakachoendelea.
Mfalme bila huruma alimchinja yule mtu kwa kupitisha upanga wake kwenye shingo bila huruma kabisa. Wengi walifumba macho kwa kuogopa kuona adhabu ile ya unyama. Hata baada ya kumaliza hilo alirejea kukaa sehemu yake na kushuhudia mateka wengine kuuawa na askari wake mbele ya wananchi hadi wote walipoisha. Lutfia alibaki kushuhudia matukio hayo na kupata picha uhalisia wa Mfalme huyo huwa haruhusu watu wageni kuingia kwenye taifa lake. Aliwaza itakuwaje kama atajulikana kuwa naye amezamia kwenye taifa hilo la Maskoof.
Alibaki kushuhudia tu hukumu ile ikitolewa kwa wale watu wote hadi walipomalizika huku wananchi wakishangilia kuonesha wanakubaliana na jambo analofanya Mfalme wao la kuwadhibiti wahamiaje ambao wanakuja kuichafua Maskoof. Lutfia alibaki kutazama tu umati ule wa watu na kuona kweli wanaumoja wa kuhakikisha taifa lao haliambukizwi tabia za ajabu na wageni wanaozamia kutoka mataifa tofauti. Alitazama mbele na kumuona Malkia wa taifa hilo Rayuu akinyanyuka pale alipo na kuanza kushuka kwenye lile jukwaa akiwa na wasichana wanne nyuma yake wakimsindikiza. Mfalme naye baada ya kumaliza kile kilichomfanya awakusanye wananchi wake aliongea maneno kadhaa na watu wake kisha akawaruhusu wakaendelee na kazi zao katika jamii.
Alimuita mkuu wa majeshi na kumpa kazi ya kuzunguka mji mzima kuwasaka watu wote waliohamia ndani ya taifa la Maskoof bila ruhusa yake. Alitaka kufuta mwenendo wa uzamiaji wa kiholela wa watu wanaotoka katika mataifa ya mbali.

Maskoof ni taifa la watu ambao walikuwa wakiishi kwa amani, upendo na ukaribu baina ya viongozi na raia wao. Karne na karne zilipita na mfumo huo uliendelea na kuwa na kawaida kwao. Ilifika hata wakati baadhi ya mataifa tofauti walitamani kuwa wakazi wa Maskoof, walitamani kuhama kutoka mataifa yao na kuhamia katika taifa hilo lenye amani.
Mfalme wa kipindi hicho ambaye ndiye mwenye jina la taifa hilo Maskoof hakuwa na hiyana juu ya hilo aliwakarimu watu wote wanaokuja katika taifa lake. Yeye alikuwa anaakili moja tu kuwa ujio wa wageni hao unaitengeneza taifa lake kuwa na heshima kwa ukarimu na hata bidhaa mbalimbali zitapatikana kutoka kwa wageni. Na kweli ujio wa wageni hao uliweza kuinua utajiri wa taifa hilo kwa kupatikana kwa mali mbalimbali, wageni walijikuta wanapeleka dhahabu, madini na hata pesa kwa Mfalme ikiwa ni kama shukrani tu ya kuwapokea watu kwa ukarimu wake huku jina lake likizidi kujulikana kwa mataifa mbalimbali hadi siku anaamua kulitangaza taifa lake liitwe jina la Maskoof na watu wakiridhia hivyo.
Lakini mambo yalikuja kubadilika hapo mbele baada ya Mfalme huyo kuanza kuwaamini wageni wanaokuja katika taifa lake. Wageni wenye tamaa na waliokosa shukrani ya kukaribishwa, walifanya njama waweze kummaliza Mfalme huyo wakiwa na lengo la kumiliki Taifa hilo wao hapo baadae. Zoezi hilo halikuwa la mara muda mfupi, ilipita miaka kadhaa wakimuandaa mhusika na kusoma mazingira kusudi isije kutokea tatizo likawa ni kikwazo kwao.
Siku hiyo Mfalme Maskoof alikuwa na wanae wawili wa kiume wakiwa juu ya farasi wao wanazunguka katika makazi ya watu. Na ndio siku hiyo ambayo wale wageni walipanga kumaliza familia hiyo yote kabisa ili pasiwe na mtu wa kurithi uongozi huo pindi watakapomuua Maskoof. Hakika siku hiyo ilikuwa ni kama vita watu wote walijifungia kwenye majumba yako na ile dhamira ya wageni wale ilifanikiwa, waliweza kummaliza Mfalme Maskoof pamoja na mwanaye mmoja. Shuhuli ikawa kwa mwanaye wa mwisho ambaye aliwasumbua sana, alitumia majeshi ya baba yake na kuweza kuishinda vita hivyo ya tamaa. Aliumia sana kumpoteza baba yake ambaye ni Mfalme pamoja na ndugu yake na kwasababu ya ukarimu wa kuwaruhusu wageni kuishi nao katika taifa moja. Tangu siku hiyo hakukuwa na ruhusa ya mgeni yeyote kuingia ndani ya Taifa la Maskoof bila kibali maalumu na chenye kumridhisha mtoto huyo wa Mfalme ambaye kwasasa ndiye Mfalme wa taifa hilo.

Askari walizagaa kila eneo huku wakishirikiana na wananchi kuwafichua wahamiaji wote wanaoishi humo. Zoezi hilo lilimshtua sana Lutfia na kuona kama ameletwa makusudi ili adhabu ile ya upanga imkute. Hakuwa na mahala pa kwenda hivyo akawa anacheza na vile askari wanavyokwenda mbele basi yeye anaenda pengine akitafuta tu sehemu ya kuweza kupumzika kwa muda.
Alifika kwenye kibanda kimoja kilichoonekana kususwa na mwenye nacho maana hakukuwa na dalili ya mtu kuishi hapo. Alisogea hadi pale lengo ni kupata kivuli apumzike kwa muda. Alitazama huku na kule akiona watu wakiendelea na shuhuli zao za kijamii, upande wa mbele yake alipata kuona watoto wakike na wakiume wakicheza mchezo wa mpira wa miguu kwa pamoja. Walionekana kufurahia sana mchezo hali iliyomfanya Lutfia pale alipo atabasamu, hata yeye alipendelea kucheza mchezo huo.
Alinyoosha miguu yake na kuweka kitabu cha LUTKAS juu ya mapaja yake anawa anafungua kurasa kadhaa hadi pale alipoishia kusoma.

Ndani ya Falme Malkia Rayuu aliweza kuwasili na moja kwa moja akawa anaelekea zake ndani huku akisindikizwa na wapambe wake. Alipofika ndani alipata kutabasamu baada ya kumuona binti yake mdogo akiwa amekaa kwenye kitu cha umalkia. Alipomuona tu mama yake alinyanyuka na kumkimbilia hadi alipokumbatiwa.
"Umeamka mama yangu! Umeshakula?" alisema Malkia akijenga tabasamu usoni mwake.
"Sijala hadi sasa, Mlienda wapi hadi mkaniacha wakati tulikuwa wote hapa ndani?"aliuliza binti yule.
"Ulikuwa umelala mwanangu, nimetoka huku kuwaangalia wananchi, nilikuwa pamona na baba yako."
"Sitaki! Baba gani huyo? Baba Saadie hawezi kuwa yule. Baba yangu mimi ni mpole na hamwagi damu za watu hovyo."alisema binti huyo akimkataa katakata baba yake ambaye ndiye Mfalme.
"Saadie, baba yako alishaacha mambo hayo mara tu baada ya kumwambia vile. Sasa hivi ni mwema anapenda na watu wote huko na ndio maana tumetoka kuwatembelea watu."
"Kama mlitaka kwenda huko kwanini msiniamshe mimi ili nikashuhudie kama kweli nlienda kuwatembelea watu?"aliongea binti huyo akionekana kukasirika kwa jambo hilo. Hakuwa anampenda baba yake na hii ni kutokana na kushuhudia matukio kadhaa ya watu wakiuawa kwa mikono ya Mfalme huyo.
Malkia alikosa jibu la kuongea wakabaki wanatazamana tu na binti yake ambaye hakuona haja ya kuendelea kuwa pale. Aligeuka na kuelekea zake chumbani kwake akiwa hana furaha. Malkia Rayuu alibaki kumtazama tu binti yake, alijisikia vibaya hata yeye kuona mtoto mdogo tayari ameshuhudia kwa macho mauaji ya watu. Aligeuka nyuma na kumtazama msichana wake mmoja wa kazi.
"Hakikisha Saadie anakula na anapata furaha, sitapenda nimuone akiwa vile."alitoa amri Malkia na msichana yule akakubali kufanya kile alichoagizwa na Malkia wake. Haraka akatoka na kwenda kuandaa chakula kwaajili ya binti wa kifalme.

Tukirudi duniani, Kasma na watu wake walibaki palepale msituni wakijadili namna ya kumpata huyo mtu anayesadikika kufanana naye. Na ndiye mtu anayeonekana kuwa na nguvu zaidi yake, jambo ambalo limekuwa likimtia katika mashaka sana akihisi kupata upinzani siku moja. Aliwatazama watu wake wakiwa wanajadiliana wenyewe kwa wenyewe.
"Vipi kuna wazo ambalo mmepata katika mijadala yenu?"aliuliza Malkia huyo huku akiwatazama watu wake.
Wakabaki wanatazamana tu huku wengine wakitazama chini, japo kwa udogo alionao lakini walimheshimu sana kama Malkia wa taifa lao.
Mmoja alisimama na kumsogelea Kasma pale alipo.
"Malkia mtukufu, kuna jambo nahisi linahitajika kufanyika haraka ili swala hili tuone muafaka wake. Kama tulikuja huku kwa kile alichokiona mtabiri basi hatuna budi kumfanyisha kazi mtabiri yuleyule aweze kujua tutatumia njia gani ili tumpate huyu mtu. Hili swala sio kubwa sana ila sisi tunapita njia ndefu ndio maana tunaliona lina uzito. Kama utaridhia ninachokisema basi naamini tutapata kujua njia mbadala ya kumpata huyu mtu maana kama amejulikana kuwa ataondoka duniani na kweli hata kwa uwezo wetu hatumuoni mtu huyo dunia nzima ni wazi kwamba kuna mahala kapelekwa, basi mtabiri atafute njia ya kutujuza. Hili tatizo litakuwa limekwisha haraka."alisema yule kijana na kuinama chini kwa heshima.
Maelezo yake yakamuingia Kasma na kuona ni kweli njia pekee ni kurudi ili wampe kazi hiyo yule mtabiri wajue alipo Lutfia.

Maskoof, Usingizi ulimchukua Lutfia pale alipoweka kambi kwa muda. Upepo mzuri ulipepea na kuzidi kuuongezea usingizi wake mtamu. Alionekana yule mtoto aliyekuwa akikimbia sambamba na Lutfia wakielekea Uwanjani muda ule, alisogea hadi pale alipolala Lutfia akimtazama kwa makini. Akamkumbuka kuwa ndio yule aliyemuuliza kuhusu kinachokwenda kutokea uwanjani. Kwa swali lile aliloulizwa na jinsi anavyomuona pale akiwa amejilaza katika banda bovu akahisi huenda na huyu ni kati ya walewale wahamiaji wanaotafutwa na Askari wa kifalme ndani ya mji mzima. Alishapata kusimuliwa historia za watu wageni hivyo hakuona sababu ya kukaa kimya. Alitoka nduki pale na kwenda kuwajuza askari kuhusu mtoto yule aliyemuona amejilaza pale bandani. Askari walipopewa taarifa hiyo walikusanyana haraka wakaongozana na binti yule hadi walipokaribia eneno lile wakamruhusu arudi yule binti baada ya kumuona mhusika akiwa amelala pale huku akiwa amekumbatia kitabu.
Walisogea hadi pale wakimtazama kwanza na kuona huenda ni kweli mtoto huyo ni mgeni kutokana na mavazi yake na hata staili yake ya nyweli. Hakukuwa na mtoto wa jamii yao anayevaa vizuri na kuwa msafi kama binti ambaye wanamuona mbele yao. Ilizoeleka ni binti mmoja tu mwenye muonekano mzuri na wa kuvutia na mavazi ni binti wa Mfalme pekee, Saadie.
Askari mmoja alitoa upanga wake mrefu na kuanza kumpiga piga Lutfia mgongoni ili aamke. Kurupu alishtuka baada ya kuhisi anaguswa na kitu, alishangaa kuona askari zaidi ya watano wakimtazama akiwa pale chini. Alitaka kunyanyuka lakini akasukumwa kumaanisha akae chini. Hawakuwa na sura za kutabasamu askari hao hali iliyomfanya Lutfia ahisi hayupo kwenye mikono salama.

LUTKAS SEHEMU YA 12


ILIPOISHIA
Alitaka kunyanyuka lakini akasukumwa kumaanisha akae chini. Hawakuwa na sura za kutabasamu askari hao hali iliyomfanya Lutfia ahisi hayupo kwenye mikono salama.

TUENDELEE.
"Wewe ni mtoto wa nani? Na kwanini upo hapa?"ni maswali aliyouliza askati yule huku wakimtazama Lutfia aliyeonekana kuwa na wasiwasi.
Aliwatazama wale askari huku akifikiria jibu la kuwapa ili wamuelewe.
"Wewe ni bubu? Mbona hujibu kile unachoulizwa?"aliongea askari mwengine akionesha kuchoshwa na ukimya wa binti yule.
"Mungu wangu, niwajibu nini hawa watu?"alijisemea moyoni Lutfia akitafuta jibu la kuwapa. Alipigwa teke la nguvu kwenye kichwa chake na kumfanya adondokee pembeni hata kitabu chake kuanguka upande mwengine. Alipata maumivu makali sana kwa pigo lile ambalo hakutegemea. Alipeleka mkono wake mdomoni na kushuhudia damu ikimtoka hali iliyomfanya ashangae kuona vile. Hakuwahi kupigwa hadi kutoka damu kiasi hicho, alishikwa na hasira za gafla hadi macho yake yakabadilika na kuwaka akiwa anatazama chini. Hali ile hata yeye alishangaa kuona mabadiliko yale.
"Hapana, hii hali isinitokee muda huu. Naomba ipotee haraka."alisema Lutfia kwa sauti ya chini baada ya kujiona amebadilika. Hakutaka ajulikane yeye nani kwa askari hao na kweli hali ile ikatoweka na macho yake yakawa kama awali.
Muda huohuo walisogea askari wawili pale na kumnyanyua pale chini.
"Nyie ndio tuliokuwa tunawatafuta hebu twende huku utajieleza vizuri."walisema wale askari na kumbeba Lutfia kama mzigo.
"Subiri basi jamani nijieleze.. naniliu.. kitabu changu jamani!"walimbeba na kuanza kuondoka naye bila kujali chochote. Askari mmoja aligeuka na kukifuata kile kitabu, alikiinua na kukitazama kwa ndani lakini alishangaa kuona kichwa kinakuwa kizito huku macho yake yakionekana kama kutokwa machozi kama kuna vitunguu vinakatwa karibu na macho yake. Hakutaka kuendelea kukifunua, alifunika na kufuta machozi kugeuka kuondoka nacho kuwafuata wenzake waliotangulia na Lutfia.

Zoezi hilo la kuwatoa watu wote wahamiaji ilizidi kasi, watu wengi walifichuliwa na kuweza kukamatwa wakafungwa kwenye mnyororo mmoja mrefu safari ikielekea kwenye magereza yaliyo ndani ya jengo la kifalme. Raia wa taifa hilo waliwatazama watu hao wakionekana kama mateka wakipeleka sehemu husika. Wapo waliwaonea huruma kwa kuona wanadhalilishwa na kuonewa, ila wengine ndio walishangilia wakiona ni bora taifa lao wabaki wenyewe hasa wakikumbuka yaliyomtokea Mfalme wao Maskoof.

Ndani ya falme Malkia alikuwa chumbani kwa binti yake anampa dawa apate kumeza. Alikuwa akiugua kwa muda mrefu maradhi ambayo hayakuweza kitibika moja kwa moja yakapotea. Binti Saadie baada ya kumeza dawa alirejea zake kitandani na kulala huku mama yake akikunjua shuka kumfunika. Aliingia Mfalme Yazid na kusogea hadi kwenye kitanda cha mwanaye pale wakabaki kutazamana.
"Unajisikiaje sasahivi?"aliuliza Mfalme akiweka shuka vizuri.
"Baridi kwa mbali."alijibu Saadie huku akimtazama baba yake.
"Usijali binti yangu utapona tu muhimu dawa za kutumia kwa wakati."alisema Mfalme na kusogea karibu na mwanaye akakaa. Aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa hereni pamoja na bangili za dhahabu.
"Inuka kidogo nikuvishe mikufu yako, nimekununulia binti yangu kama zawadi."alisema Mfalme na bila kuchelewa binti yule alinyanyuka kumtii baba yake. Malkia alishuhudia binti yake akivishwa urembo huo huku akiwa mwenye tabasamu.
"Nashkuru sana kwa zawadi hii."alisema Saadie na kunyanyuka pale kitandani kuelekea kujitazama kwenye kioo jinsi alivyopendeza. Walibaki wakimwangalia binti yao, hakika walimpenda kwa kila kitu maana ndiye mtoto pekee wamejaaliwa kupata.
"Nilikwambia hapo awali, hakika baba yako anakupenda sana na ndio maana anakuletea zawadi nzuri kama hizo."alisema Malkia akijatibu kumuweka binti yake karibu na baba yake. Saadie aligeuka nyuma kumtazama Mfalme na taratibu akamsogelea.
"Eti ni kweli baba unanipenda?"aliuliza Saadie swali ambalo lilimfanya Mfalme atabasamu. Alimshika mkono binti yake na kumnyanyua kumbeba.
"Wewe ndio mama yangu, wewe ndio kila kitu kwangu ndio maana unapokasirika basi nakuwa sipati raha. Amini kile anachosema mama yako, hakika nakupenda sana mwanangu."alisema Mfalme huku akijenga tabasamu bashasha lililoanza kumuaminisha binti yake.
"Mama alinambia umeacha kuwatesa watu, na mlitoka kwenda kuwaangalia watu huko mtaani. Napenda hali hiyo iendelee, watu waishi nasisi kwa upendo. Nachukia kuona damu za watu huku wengine wakilia.."alisema Saadie maneno mazito yaliyomfanya Mfalme ageuke kumtazama mkewe aliyeinamia chini. Alirudisha tabadamu tena kwa binti yake.
"Nimekuelewa mama yangu, hutakuja kuona trna nikifanya hivyo vibaya. Mawapenda watu wa Maskoof na wao wamekiri kunipenda pia."alisema Mfalme na kuyafanya mawazo mabaya kwa binti yake dhidi yake yaanze kuyeyuka taratibu. Alimkumbatia baba yake kuonesha kweli amemuamini kwa maneno aliyoongea. Malkia alifurahi sana kuona hali ile baina ya wawili hao mtu na mwanaye.

Muda huohuo ilisikika kengele yenye mlio mkubwa nje. Kengele iliyowafanya watu wote wajue kuna jambo linaloendelea. Haraka wakaacha kazi zao na kuanza kuelekea kule kwenye uwanja kwa mara nyengine tena.
Nje ya mlango palisikia sauti ya askari akihitaji kuonana na Mfalme apate kumpasha habari. Ilibidi Mfalme amruhusu kuweza kuingia mule ndani. Alisogea hadi pale na kuinama kama kutoa heshima kwa viongozi hao huku binti Saadie akiangalia.
"Mfalme, hatimaye tumeweza kuwapata wahamiaji ishirini na watatu . Tumejaribu kuwahoji waseme walipotokea hawakuwa na sababu za msingi. Hivyo nimeleta taarifa hiyo utoe tamko lako tuweze kutekeleza."alisema yule askari akiwa makini kumsikiliza.
Mfalme Yazid alimkodolea macho Malkia ashindwe cha kujibu maana ni muda mfupi tu ametoka kumuaminisha mwanaye kuhusu wema wake dhidi ya raia. Ilimbidi amshushe binti yake kwanza kisha naye akashuka chini kuchuchumaa wakawa wanatazamana.
"Saadie, kuna mahala naelekea mara moja kuongea na watu sitakaa sana nitarudi."alisema Mfalme akiwa amemsika mkono mwanaye.
"Nahitaji safari hii nami niongozane na wewe, niweze kushuhudia jinsi watu wanavyokupenda kwa wema wako."alisema Saadie bila mashaka.
"Hapana sio kwa safari hii nitaongozana nawe, na naomba uape kwamba hutanifuata tena huko ninapoenda. Siku inayofuata nitatembea nawe kila sehemu utakayo ila kwasasa wacha niwahi. Naomba tuweke kiapo."alisema Mfalme na kunyanyua kidole cha mwisho kutaka kuwekeana kiapo na binti yake asiweze kumfuata, maana binti huyo aliwahi kutoka ndani kumfuata baba yake na ndipo aliposhuhudia Mfalme akifanya mauaji ya watu ikiwa kama adhabu na sheria ya taifa hilo. Saadie kwa maelezo aliyosikia kwa baba yake alipata kuwa na mashaka juu ya safari hiyo. Alitazama kidole kile cha baba yake na mwishowe naye akanyoosha kidole chake wakaweka kiapo kuwa hatamfuata huko anapoenda.
Alifurahi baada ya kiapo hicho alinyanyuka mfalme na kuanza safari ya kuondoka na askari yule. Saadie pale aliposimama alibaki kumtazama tu baba yake akitokomea. Wakati wakifanya kiapo hicho yeye aliweka nyuma mkono mwengine na kukunja vidole viwili kumaanisha kiapo hicho ni batili hakukubaliana nacho. Alidhamiria kwenda kupata uhakika tena kama baba yake ameacha mabaya yake kama alivyoongea mwenyewe.
Alirudi zake kitandani na kuweza kupumzika. Malkia alivyoona vile akajiaminisha binti yake anapumzika. Naye taratibu akaanza asafari yakuelekea naye kupata kupumzika.
Alikuwa makini kuhakikisha mama yake hamuoni, taratubu akashuka pale kitandani na kuanza kupiga hatua kutoka nje huku kelele na shwange zikiendelea.

Kama ilivyo awali watu walifurika kwenye uwanja ule wakitegemea kushuhudia adhabu zitolewazo kwa watu ambao wameshikwa na kubainika kuwa ni wahamiaji. Lutfia alikuwa miongoni mwa watu hao ambao walifungwa minyororo na kuwa kama mateka huku wakiwa kama walivyozaliwa. Aliwatazama wenzake na kuona karibia wote wana rika la juu kushinda yeye huku nyuso zao zikionesha kuwa na huzuni kana kwamba wanajua kinachokwenda kutokea. Alimtazama yule askari ambaye muda wote alikuwa ameshikilia kile kitabu alichookota muda ule.
"Nipatie kitabu changu.!"alisema kwa sauti Lutfia na huenda askari yuke hakuweza kusikia kutokana na kekele za watu ndani ya uwanja ule.
"Wewe askari nipe kitabu changu si mmeshanikamata!"aliongeza sauti kuyasema hayo na kuwafanya hata wenzake wakaribu wageuke kumtazama. Waliangalia pembeni alipo yule askari na kuona akiwa ameshikilia kile kitabu huku akitabasamu baada ya kumsikia binti huyo. Taratibu alimsogelea kwa dharau huku akimtazama.
"Unataka kitabu ili ukakisome ukiwa kuzimu? Au unadhani utapona hapa. Hakujawahi kupatikana mtu mwenye bahati kama hiyo ya kufungwa mnyororo huo halafu akaachiwa hai."alisema yule askari kwa msisitizo na kumtupia Lutfia kitabu kile usoni kikadondoka chini. Alirejea mahala alipokuwa huku akitazamwa na binti huyo mdogo kwa jicho la hasira sana. Hakuwa na ujanja alishuka taratibu na kukichukua kitabu chake kwa tabu huku mikono yake yote ikiwa ndani ya pingu.

Muda mfupi aliwasili Mfalme na watu wote walisimama baada ya askari mmoja kutangaza ujio huo wa kiongozi wao. Alikwenda kukaa sehemu yake na watu nao wakakaa kusubiri kinachokwenda kutokea. Aliwatazama wale wahamiaji waliokuwa kwenye mnyororo ule huku akionekana mwenye hasira sana. Hata alipomuona binti mdogo akiwa miongoni mwao huku ameshikilia kitabu kwenye mikono yake iliyofungwa pingu hakuwa na huruma naye hata kidogo. Aliona wote ndio walewale tu wamekuja kuiharibu Maskoof yake hivyo hakuwa na huruma dhidi yao. Zililetwa silaha kama ilivyo kawaida na kuwekwa sehemu maalumu. Mfalme alisimama na kusogea mbele kuongea tena na watu wake.
"Naamini kwa mwenendo huu tutaifanya Maskoof iwe ya kwetu na sio kuruhusu wageni hawa waanze kuzoea kuishi humu. Hakuna asiyefahamu ubaya wa hawa watu na ndio maana tumeweka sheria pasitokee mgeni yeyote kuweza kufika katika ardhi hii."alisema Mfalme Yazid na kukamata upanga mrefu wenye ku'gaa. Walimfungulia mtu mmoja na kumkamata barabara hadi sehemu ya hukumu kisha wakamlaza. Mfalme alisogea pale akiwa amebadilika suta na kujenga ukatili rohoni.
Lutfia akawa anashuhudia tu kile kinachokwenda kutokea. Palepale akanyanyua kile kitabu chake chenyewe kikajifungua kurasa kana kwamba kinatafuta maelezo katika kurasa husika. Kilitulia baada ya kufika ukurasi fulani na papo hapo binti huyo akaanza kusoma sehemu fulani. Alitulia kwa makini kusoma kitabu kila bila kujali kinachokwenda kutokea. Alishtuka baada ya kufika sehemu kuona hali halisi.
Ni tukio ambalo lipo muda huo linaendelea likionesha Mfalme akiwa ameshikilia upanda huku askari wake wakiwa wamemshika mtu wakimsogeza karibu ya Mfalme kisha wakamlaza kwenye sehemu iliyooneka kiwa na damu iloganda. Bila huruma yule Mfalme alishusha upanga wake ukatua shingoni mwa mtu yule na kukata kabisa kichwa chake. Watu wengi walificha macho yao na hata wengine kufumba midomo kwa kile ambacho wanakiona. Baada ya kumalizwa mtu huyo alifuata binti mdogo naye akisogezwa pale.

Lutfia alishtuka baada ya kusoma kitabu kile na haraka akageuka kutazama kwenye mnyororo ule kama kuna myu wa rika lake lakini hapakuwa na yeyite zaidi yake. Alitazsma mbele alipo Mfalme na kushuhudia lilelile tukio alilosoma kwenye kitabu likiendelea. Mfalme alinyanyua upanga wake juu na bila huruma aliushusha kwa kasi na kukata kichwa caha mtu yule huku kelele za watu zikisikika kuonesha kweli hawawataki wahamiaji.
Mfalme aliamuru aletwe binti huyo mdogo ili afanye hukumu yake.
Alimeza mate Lutfia baada ya kuona askari wawili wakisogea pale alipo na kumfungulia mikono yake iliyofungwa minyororo. Walimsogeza pale mbele huku akishuhudia kiwiliwili cha yule mtu aliyekatwa kichwa kikiondolewa sehemu ile ya hukumu kisha akapokonywa tena kile kitabu chake kikatupwa chini kukionekana kuna damu nyingi zikitapakaa eneo lile. Aliwekwa sehemu husika huku Mfalme Yazid akichukua kishoka chenye mpini mrefu kidogo na kusogea hadi pale alipo Lutfia. Watu walipiga mayowe ya kutaka wote wauawe bila kujali rika lao. Lutfia aligeuka na kutazama kile kitabu kilichopo pale chini kikitapakaa damu za watu.
"Hapana Lutfia siwezi kufa kifo hiki, wacha nijioneshe mimi nani maana sitaweza kuruhusu mauaji haya yaendelee."alisema Lutfia na taratibu macho yake yakaanza kubadilika na kuwa tofauti na binafamu wa kawaida.

Mfalme alinyanyua kishoka kile kikali na bila huruma akaanza kushuka kwenda chini.
"Baba....!"ilisikika sauti ya binti iliyowafanya askari pamoja Mfalme aliyesitisha zoezi hilo kugeuka nyuma.
Lutfia kusikia vile hakutaka kujionesha tena haraka akarudi hali yake ya kawaida. Mfalme alishangaa kumuona binti yake Saadie akiwa kaachama mdomo baada ya kuona tukio lile. Alitazama pembeni na kuona mwili wa binadamu ukiwa utupu tena bila kichwa huku damu zikitapakaa mahala pale. Hata alipotazama sehemu ile ya mauaji alimuona binti mdogo wa umri wake kabisa akiwa ndio anatakiwa kuhukumiwa na baba yake.

Mfalme hakuamini kile anachokiona, kwa mara nyengine binti yake anashuhudia akifanya ukatili huo. Taratibu akashusha silaha ile na kujikuta akikosa nguvu kabisa ya kuendelea na zoezi hilo.
"Saadie..!"alijikuta akimuita binti yake kwa sauti ya upole kabisa.
Kwa huruma aliyonayo Saadie alipiga hatua na kuchukua mtandio aliovaa na kumsogelea Lutfia pale alipolazwa akamsitiri kwanza kwa jinsi alivyo kisha akamgeukia baba yake akionekana kuwa mwenye hasira sana.
"Nilijua tu kuwa huwezi kubadilika mapema tabia yako. Siwezi kuwa na baba kama wewe, usiyekuwa na huruma hata kwa watoto wadogo kama mimi. Huyu si kama Saadie tu amekukosea nini?"aliongea Saadie kwa uchungu na kijikuta hata machozi yakimtoka. Lutfia alimtazama yule binti kwa kauli zake na hisia alizonazo za huruma kwa watu aliamini huyu anaweza kuwa mwema kwake. Na ndivyo ilivyokuwa baada ya kuyasema hayo Saadie alimshika mkono Lutfia kwa ujasiri bila kuogoa yeyote pale jukwaani.
"Anaenda kuingia chumbani kwangu na nitakuwa naishi naye miaka yote mule ndani. Kama uliamua kumuua basi nitaanza kufa mimi kisha yeye atafuata."alisema Saadie maneno mazito yaliyowashtua watu wote pale jukwaani hata Lutfia mwenyewe. Mfalme alishangaa baada ya kuambiwa maneno hayo na binti yake anayempenda kwa dhati. Binti alianza kupiga hatua kutaka kuondoka na Luftia ambaye hakutaka kukiacha kitabu chake, alikiokota kutoka kwenye sakafu ya damu na kuanza safari ya kuongozana na Saadie kwenda kwenye falme kama alivyoamua binti huyo wa kifalme kuishi na Lutfia kuanzia siku hiyo.
Watu wote pale uwanjani walibaki kushangaa kuona jambo lile likiendelea, walipata kushuhudia mabinti hao wawili wakishuka kwenye jukwaa lile na kutoka kabisa kwenye uwanja huo. Kila mtu alibaki kuongea lake pale uwanjani,hata Mfalme alirudi kukaa kwanza haamini kile ambacho kimetokea.

Saadie alimpeleka moja kwa moja Lutfia hadi ndani ya falme na kuamrisha wafanyakazi wamsafishe vizuri kuondoa damu na uchufu kisha wamshuke zile nywele zake ndefu zilizojiachia. Haraka wakaanza kufanya kazi hiyo huku Malkia akishangaa kumuona yule binti.
"Wewe ulikuwa wapi? Na huyu binti umemtoa wapi?"aliuliza Malkia Rayuu akimshangaa Lutfia akipelekwa bafuni.
Saadie alinyanyua kile kitabu cha Lutfia kilicholoa damu na kumuonesha mama yake.
"Mnayofanya wewe na baba ipo siku hizi nafsi na damu zitakuja kuongea na kulia mbele ya haki. Wakati huo na nyie mnalia kutaka msaada kwa hawahawa mliowadhulumu uhai wao. Ni wewe ndio uliniaminisha kuwa baba amekuwa mtu mzuri sasa na ameshaacha dhambi. Hata dakika kadhaa hazijafika ametoka kurudi kumwaga damu, na huyu binti ndio alikuwa anafuata nahisi kifo chake kingekuwa cha kikatili sana kama nisingelitoroka humu ndani kwenda kujionea kwa macho. Nakupenda sana yangu, ila kwa haya unayoweka ukaribu na baba kuyafanya utanifanya hata na wewe nikuchukie."alisema Saadie akiongea kile anachokiona ni sahihi. Hakutaka kuendelea kuwa mbele ya mama yake aliondoka zake kwenda chumbani akiwa na kitabu kile akimwacha mama yake katika gharika zito la mawazo. Maneno mazito yalimuingia na kuona kweli wanadhurumu nafsi za watu.

Watu walirudi kwenye shuhuli zao baada ya zoezi la kuwahukumu wale wahamiaji kusitishwaa baada ya kile kilichotokea na haikuwa bahati kwa yule mtu wa kwanza kuweza kuuawa kikatikili na Mfalme Yazid.

Jioni ya siku hiyo baada ya Lutfia kutengenezwa na hata muonekano wake kuweza kubadilika akavalishwa mavazi ya kawada yenye kuficha baadhi ya viungo vengine ikiwa kama heshima kwa binti wa kile kujisitiri kuanzia kichwani hadi chini. Walimwacha kwenye chumba kimoja baada ya kumuweka sawa akabaki anajitazama kwenye kioo na kujiona jinsi alivyobadilika tofauti na Lutfia yule wa awali.

LUTKAS SEHEMU YA 13


ILIPOISHIA
Walimwacha kwenye chumba kimoja baada ya kumuweka sawa akabaki anajitazama kwenye kioo na kujiona jinsi alivyobadilika tofauti na Lutfia yule wa awali.

TUENDELEE LEO.
Alijikuta hata yeye akitabasamu tu baada ya kujiona vile alivyo. Muda mfupi walikuja wasichana wawili ambao ni wafanyakazi na kutaka waongozane naye kumpeleka kwa mwenyeji wake. Hakuwa na kipingamizi alinyanyuka na safari ikaanza kuelekea kwa Saadie.

Upande wa pili Kasma aliweza kurejea katika falme yake. Hakutaka kupoteza muda aliamuru yule mtabiri aitwe tena. Watu wake walifanya hivyo na baada ya muda yule mtabiri aliwasili tena mbele ya Malkia na kumpa heshima yake. Alimweleza kila kitu baada ya kufika duniani na kukuta vitu tofauti na walivyotegemea. Ilimbidi yule mtabiri aingie tena kazini upya ili kuweza kujaribu kutambua alipo mtu huyo wanayemdhania kufanana na Malkia Kasma. Wote walinyamaza kimya wakitazama mtabiri akifanya mambo yake mbele ya malkia wao. Alinyanyua tena kioo na kuzungushia usinga huku akiongea maneno yake kwa kunon'gona na mwishowe akatazama pale kwenye kioo. Alishangaa kuona mtu huyo yupo mahala amekaa na binti mwengine ambaye kwa muonekano wake huenda ni binti ya kifalme maana mavazi yake ni tofauti na ya mtu wa kawaida. Aligeuka kimtazama Kasma.
"Naona kitu kigeni kabisa hapa."alisema yule mtabiri na kumsogezea Kasma kile kioo apate kutazama yaliyomo.
Hata yeye alishangaa kuwaona wawili hao tena wakiwa mahala penye muonekano mzuri.
Ilibidi mtabiri afanye kazi kupata kujua ni mahala gani wanapopatikana kwasasa. Malkia Kasma alikuwa mwenye shauku kubwa kujua kinachoendelea.

Huku upande wa pili Lutfia alikuwa chumbani kwa Saadie wakiongea mawili matatu wakijaribu kiulizana.
"Hebu niambie mwenzangu umetokea wapi? Na wazazi wako wapo wapi?"aluliza Saadie akiwa anamtazama mhusika ajibu.
"Nimetoka mbali sana. Hata nikikuelekeza sidhani kama utaweza kunielewa. Ila tambua kwamba nimetoka mahala tofauti na hapa tulivyo, na huko nimetoka kuna watu walikuwa wananitafuta wapate hicho kitabu."alisema Lutfia na kumfanya Saadie ashtuke kusikia hivyo.
"Unamaana gani kusema hivyo?"aliuliza Saadie baada ya kusikia kuhusu kufuatiliwa mwenzake.
"Kuna kikundi kinahitaji kitabu hichi kwa nguvu zote. Hawa si binadamu wa kawaida ni kama wafu wenye nguvu za ajabu, na hili swala limeshika kasi kwa muda mrefu sana."alisema Lutfia na kumfanya ageuke kutazama kile kitabu cha LUTKAS, hakuweza kuelewa maana yake.
"Kwani kina jambo gani hasa hiki kitabu ndani yake?"aliuliza Saadie huku akiwa makini kumsikiliza Lutfia.
"Kinamaana kubwa sana tena sana, hiki ni kitabu cha uhai nadhani kama utakijua maana yake utafahamu nini namaanisha."alisema Lutfia akikifunua kitabu kile. Ilibidi Saadie asogee karibu yake naye kutazama kitabu kile, alishangaa kuona macho yake hayaoni vizuri maandishi yaliyopo mule kwenye kitabu. Hata kujikuta akianza kulengwa na machozi kabisa ikabidi asogee pembeni.
"Mbona naomba maluweluwe siwezi kuona kilichopo kwenye kitabu?"aliongea Saadie huku akijifuta machozi. Ilimlazimu Lutfia kuweza kutabasamu baada ya kuambiwa hivyo.
"Hichi kitabu kina mambo mengi ambayo ni tofauti na maisha halisi ya binadamu wa kawaida. Hiki ni kitabu cha uhai, ambacho kinaweza kutumika kuwarudisha wafu ambao wametangulia kwa miaka mingi. Ni zaidi ya miujiza iliyopo humu ndani yake. Na hadi unavyoniona nipo katika taifa hili basi ilitumika miujiza kunifikisha hapa, na ndio maana sikuweza kupata jibu la kujitetea kwa askari hadi kupelekea mimi kukamatwa."alisema Lutfia akimuelewesha Saadie.
"Inamaana... na wewe pia ni mfu?"aliuliza Saadie akimtazama Lutfia machoni.
"Hapana, mimi Lutfia ni mtu kabisa. Ila ninao uwezo wa kuwatambua wafu ambao wanaishi na kujifanya ni binadamu na viumbe wengine. Uwezo huo ninao na ndio maana hata kitabu hiki ambacho kinasomwa na watu maalum wenye uwezo na nguvu hizi za miujiza huwezi kusoma wala kuyaona maandishi yaliyomo humu. Mtu wa kawaida hawezi kufahamu kilichoandikwa humu labda niamue kukupa walau uwezo wa mara moja kusoma."alisema Lutfia akiwa hana hofu yeyote. Saadie alimeza mate baada ya kufahamu kwamba mtu aliyenaye si wa kawaida.
"Sasa.. huku Maskoof umefuata nini?"aliuliza Saadie na kumfanya Lutfia ashushe pumzi kidogo na kuendelea.
"Kuna wafu ambao wanataka kurudi kuwa watu kama sisi, sasa wameshafahamu kuwa njia pekee ya wao kurudi kuwa watu ni kukipata hiki kitabu. Hivyo hapa nina kazi ya kuwadhibiti wasiweze kukipata. Hapa nimewatoroka huko tulipokuwa tunaishi na ndio sababu ya kufika hapa."aliongea Lutfia na kuzidi kumuelewesha binti wa Mfalme ambaye taratibu alianza kumzoea Lutfia na kumfahamu kwa undani zaidi kuwa ni mtu wa aina gani.
Hata ilifika muda aliweza kumuonesha mabadiliko yake pindi akiwa tofauti na binadamu, alibadilika macho na hata sura hali iliyomfanya Saadie aogope sana lakini alisisitizwa azoee na iwe siri baina ya wawili hao.

Wakati hayo yakiendelea huku upande wa pili Kasma alikuwa amekaa pamoja na wazee wakijaribu kuyaweka mambo sawa. Hii ni baada ya kupata kufahamu wapi anapopatikana mtu mwenye kile kitabu wanachokihitaji.
Kwa Kasma aliona ni mzunguko mkubwa sana na alijikuta akikata tamaa ya kuendelea kufuatilia mambo hayo. Lakini wazee walimhimiza na kumtaka afuatikie hilo swala ili aweze kufanikiwa kukipata kitabu hicho maana kina umuhimi sana kwa upande wao. Walimjaza shauku ya kuendelea na moyo wa kutafuta kitabu cha LUTKAS na waliweza kufanikiwa.
"Ninawezaje sasa kufika huko Maskoof?"aliuliza Malkia Kasma huku akiwatazama wazee wale.
"Unaweza kufika huko japo kuna kazi sana ili uweze kuipata nafasi hiyo."alisema Mzee mmoja na kumfanya Kasma amsikilize kwa makini.
"Ni siku ya tarehe 7 au 14 ya kila mwezi ndio kuna nafasi ya kuweza kufika huko. Hivyo yatupasa tusubiri mwezi ujao hadi tarehe hizi zitakapofika."alisema yule mzee na Malkia akawaelewa. Wakapanga wasubiri mwanzoni mwa mwezi tarehe saba ili wapange mpango wa kuelekea Maskoof.

Ilikuwa ni mapema sana kuzoeana mabinti wawili Saadie pamoja na Lutfia. Ukaribu wao ulimshangaza hata Mfalme mwenyewe ambaye hadi muda huu hakuweza kuonana na mwanaye tokea pale uwanjani na kuweza kushuhudia ukatili ule. Baada ya muda Malkia alimuhitaji Lutfia aweze kufika alipo wapate kuongea mawili matatu maana sura yabinti huyo haikuweza kuonekana mahala popote ndani ya Maskoof.
Ilimbidi Saadie amuandae kuweza kuwa safi maana anakwenda kuonana na mkuuu wa taifa.
"Mama na baba yangu hawapendi kitu uongo katika maisha yako. Hivyo atakapokuulizwa lolote kuhusiana na undani wako wewe mueleze ukweli wanaweza kukuua ukibainika. Hivyo usifiche mambo ambayo ni ya ukweli. Kuwa makini lakini."alisema Saadie akimuelewesha Lutfia.
"Hilo usijali nafahamu, nitasema tu ukweli pale inapohitajika kusema."alisema Lutfia na maongezi mengine yakaendelea.

Alie hajuwa mwenye kukubali kushindwa kirahisi mara baada ya kumkosa Lutfia kwa sekunde chache tu kule msituni. Alianza kuunda mbinu tofauti na awali ili afahamu ataanzake kumfuatilia hadi kumnyaka binti huyo. Wakati wanaendelea kutafakari na wenzake walipata kuhisi harufu tofauti na waliyo uzoea. Alie alisimama na kuanza kutembea tembea kila sehemu sehemu pale walipofikia. Alikuwa makini sana kwa kila hatua ambayo anapiga ili kupata kutambua kinachoendelea. Mwisho wa siku akapata kutambua kuwa kuna watu walikuwa wakielekea kule msituni walipoachwa na Lutfia. Haraka palepale akapotea kimiujiza bila kuwaambia wenzake ambao walimshuhudia akitoweka. Baadhi walitaka kumuona kiongozi wao alipokwenda ila walipotaka kumfuata walizuiwa na wenzao kwamba wamuache anajua anachokifanya.

Kasma aliweza kufika eneo ambalo linasadikika litatumika siku ambayo atapaswa kwenda Maskoof huko kufuata kitabu cha LUTKAS. Walisimama na kutembea huku na kule wakizidi kuongea na kupanga mikakati yao. Yote hayo Alie alikuwa akitazama na kupata kuwaona sura zao. Alishtuka sana baada ya kuona sura ya Kasma pale miongoni mwa wale waliofika eneo lile. Alipatwa na mshangao mkubwa sana ikambidi atafute sehemu apate kuwatazama vizuri. Hakika alishuhudia kuona sura ya yule mtu ambaye amekuwa akimfuatilia mara kwa mara na kutambua ndiye mwenye kitabu ambacho anakihitaji, Lutfia.
"Imekuwaje huyu arudi tena hapahapa? Na hawa mbona ni askari wa...! Ah mbona sielewi hapa?"alishindwa kutambua kinachoendelea na kitu pekee kinacho mchanganya ni baada ya kufahamu Lutfia ameshatokomea huko alipokwenda, iweje amuone tena anarudi maeneo yaleyale tena anaonekana kuwa na baadhi ya askari wa kifalme. Ilimbidi tu kuzidi kufuatilia kwa makini ajue hatma ya yote hayo.

Kasma alikuwa akitazama eneno lile akiwa sambamba na askari wa kifalme. Walikuja kuangalia mazingira kwanza wapate kufahamu sehemu ambayo watapaswa kupita siku ikifika. Walizunguka kila mahala kuangalia na usalama uliopo pale wakajitidhisha na kuamua kurudi zao hadi siku hiyo ikifika.
Alie alikuwa akiwasindikiza tu macho hadi walitokomea. Jambo pekee alilolipata ni kuhisi walikuja kukagua mazingira ya pale lakini hakuwa anafahamu lengo lao hasa ni nini. Kwa akili za haraka haraka akaona huenda kuna jambo linaweza kutokea hivyo njia pekee wao ni kuwepo maeneo hayo kila siku ili wapate uhakika wa jambo wanalolihisi. Alirudi kwa wenzake na kuwapa taarifa kamili juu ya ujio ule alioweza kuuona pale. Nao baada ya kuambiwa hibyo wakakubaliana na kiongozi wao huyo na mara moja wakasogea maeneo ya msiyuni kule kuweka doria.

Maskoof, Mfalme alionekana akiwa na Malkia wakiwa wanaongea mambo yao.
"Sidhani kama ataweza kunielewa tena maana safari hii ni mbele ya watu wakishuhudia kinachoendelea. Na sijui imekuwaje hadi ukamruhusu kuweza kutoka humu ndani."aliongea Mfalme akijadili na mkewe baada ya kuweza kuonekana na binto yake akifanya mauaji.
"Mimi nilimwacha amelala sasa sielewi imekuwaje hadi akatoka ndano, akapita kwa walinzi wote waliokuwa kila sehemu hadi kuweza kufoka uwanjani."aliongea Malkia na maneno yake yakamfanya hata Mfalme atafakari mara mbilimbili maana ulinzi aliouweka kila sehemu lakini binti yake ameweza kupita.
"Inamaana hawakumuona au imekuwaje?"alijiuliza Mfalme na kuamua kugeuka nyuma. Hakutaka kusubiri alitoka pale alipo na kwenda kwa walinzi wake wote waliosimama kuweka ulinzi kila sehemu.


LUTKAS SEHEMU YA 14


ILIPOISHIA
Hakutaka kusubiri alitoka pale alipo na kwenda kwa walinzi wake wote waliosimama kuweka ulinzi kila sehemu.

TUENDELEE.
Muda huohuo Lutfia pamoja na Saadie ndio walikuwa wakitoka chumbani na kuelekea sebuleni kuweza kupata chakula ili baadae Lutfia apate kukutana na viongozi wa taifa hilo wamhoji. Mfalme aliweza kukumbana nao na kubaki kusimama akiwatazama tu. Lutfia kwa heshima ya Mfalme akainamisha kichwa chini baada ya kutambua ndio desturi ya ardhi hiyo ya Maskoof ikimaanisha heshima kwa kiongozi. Saadie alimtazama baba yake kwa muda na kuamua kuendelea na safari yake huku akiwa amemshika kabisa mkono Lutfia. Alipata kufahamu Lutfia kwamba watu hao wawili mtu na mwanaye hawana uhusiano mzuri mule ndani. Hakutaka kujadili sana swala hilo alifuata kule anakopelekwa na Saadie.

Upande wa pili Alie hakuwa nyuma katika swala zima la kumfuatilia Kasma pamoja na jeshi lake.
Aliwafuata kila hatua wanayopiga na mwishowe akapata kutambua yule si Lutfia anayedhania yeye kutokana na ufanano wa sura hadi umbo. Uchunguzi wake ulifana baada ya kutambua hasa lengo la kundi hilo linaloongozwa na bintimdogo ni kutaka kutoka hapo walipo kwenda huko alipowasili Lutfia. Akaona hii ndio fursa ya yeye pamoja na watu wake kuweza kupata kile wanachokihitaji. Aliapata akili ya haraka na maamuzi magumu ambayo aliona ndio njia pekee ya wao kuweza kufanikiwa zoezi lao. Haraka akarudi kule ambapo wapo wenzake waliokuwa na sura halisi za binafamu angali ni wafu.
"Kuna njia nimeipata ya kutumia huenda ikawa salama kwetu. Mnafahamu Maskoof hatuwezi kusogea katika ardhi yake kwa hali hii. Hivyo nimepata wazo ambalo limekuja gafla tu baada ya wenzetu upande wa pili wanahitaji waelekee Maskoof. Na kwa maelezo yao pale nimesikia kuwa ndio hawahawa ambao wanakifuatilia kitabu cha LUTKAS kwa yule binti tuliyemkosa kule msituni. Na leo nimepata kuona kitu cha tofauti, kumbe hawa mabinti wapo wawili wanafanana sana. Hivyo naamini safari yao hawa itakuwa tu ya kupata kitabu na sisi ndio nafasi tutakayoitumia kuweza kuchujua kitabu kile."alisema Alie akiongea na wenzake.
"Sasa kama uwezo wa kukanyaga Maskoof hatuma itakuwaje ?"aliuliza mmoja wapo.
"Hapa nimepanga tujishushe kwa binti huyu, na tumueleze ukweli kuwa tunatafuta kitabu na yeye kama anakitafuta basi tukiwa pamoja atakubali tu yule. Akifanya hivyo hapo mbele mambo yatakuwa mazuri."alisema Alie na wenzake wakamuelewa asemacho. Aliona ni bora ajishushe chini na kuwa kama mfanyakazi, kibaraka cha binti Kasma ili awe karibu na vingozi wenye mbinu za kuweza kufika Maskoof.
Zoezi hilo halikuwa lenye kuchelewa haraka walianza taratibu za kutafuta wanapopatikana wakina Kasma lengo ni kutaka waungane kutafuta kitabu hicho.

Muda ulizidi kuyoyoma na baadae Lutfia alipata kukaa mbele ya Mfalme pamoja na Malkia waliwa wamekaa kwenye viti vyao vya uongozi wakimtazama binti huyo aliyesimama kuwatazama.
"Jina lako unaitwa nani?"aliuliza Mfalme huku akimtazama binti huyo.
"Lutfia.. Naitwa Lutfia ndilo jina langu. Nimetoka mbali sana na hapa Maskoof na ninakiri kwamba sina ndugu wala mtu wa karibu katika ardhi hii, huenda ni kwasababu ya kuja bila kutambua wapi nitafikia na kupokelewa. Ila sikuja kwakuwa sina pa kukaa huko nilipotoka, nimekuja kwa kuwakimbia watu waliokuwa wakitaka kitu kutoka kwangu. Na nimeelekezwa nikimbilie huku huenda kukawa ni salama kwangu."alisema Lutfia akijieleza yote ili kukatisha maswali ambayo alihisi angeulizwa. Mfalme alimgeukia Malkia wakawa wanatazamana baada ya kusikia maelezo hayo.
"Watu gani hao wanaokufuata? Na ni kitu gani hicho wanachokitaka kutoka kwako.?"aliuliza Mfalme na muda huohuo akaingia Saadie akiwa amekishika kile kitabu cha LUTKAS na kusogea hadi pale aliposimama Lutfia akamkabidhi kisha akarudi zake alipotoka. Hali hiyo ikawafanya hata wazazi wake watambue wawili hao wameanza kuzoeana japo ni kwa
"Kitabu hiki ndio kitu pekee wanakitafuta. Kinaitwa LUTKAS, ni kitabu chenye maono ya mbele, na kina miujiza mingi sana ndani yake. Wanakiita ni kitabu cha uhai maana hata wafu waliozikwa muda mrefu wanaweza hata kufufuliwa kwa kutumia kitabu hiki."alisema Lutfia na kuwafanya mtu na mkewe washangae kusikia hivyo. Malkia alijikuta akisimama kumtazama Lutfia pale mbele akiwa amekishika kile kitabu.
"Wewe umejuaje hayo yote? Na unauhakika wa hicho unachokisema?"
"Ujio wangu hapa sikuja kwa kupanda gari wala farasi kusema ndio amenifikisha hapa Maskoof. Nimekuja kimiujiza na kwa nguvu za kipekee na ndio maana sikuweza kupata jibu la kuwapa askari pindi walipotaka ninieleze nikipotokea."alisema Lutfia akizidi kuwashangaza viongozi hao.
"Inamaana unatumia nguvu za kichawi?"aliuliza Mfalme na kumfanya Lutfia atazame chini.
"Sio uchawi mbaya ambao anao huyu Lutfia. Kwa masaa tu niliyokaa naye nimepata kumfahamu mambo mengi sana ambayo ni tofauti na wale ambao tumekuwa tukiwahisi wenye nguvu hizi."alipata kusikika Saadie akisogea tena pale aliposimama mwenzake. "Lutfia anaonekana yupo kwaajili ya kuwatetea watu na sio kuwadhuru. Lutfia amekuja Maskoof kuiweka iwe tofauti na nahisi ataibafilisha sana na kuwa mtu anayependwa na watu. Namuona Lutfia wa baadae akiwa anatetea wanyonge na hata kubadilisha matukio na desturi mbaya zinazoendeshwa na viongozi wa Maskoof. Mimi nitakuwa naye sambamba kwa kila anachokifanya na mbele yenu nasema hivyo."alisema Saadie akiwa mwenye kujiamini sana. Alionesha jinsi alivyompokea Lutfia kwa mikono miwili na kuwafanya wazazi wake wabaki kuangaliana tu hawana la kusema mbele ya binti yao kwa uamuzi alioamua.
"Na ulisema kuna aliyekushauri uweze kufika hapa Maskoof, ni nano huyo angali umesema huna ndugu wala jamaa hapa."aliuliza Mfalme Yazid.
"Anaitwa Kasam."
"Kasam!"
"He! Nani Kasam!"walijikuta wote wakishangaa baada ya kusikia jina hilo likilotajwa na binti Lutfia.
"Ndio, yeye ndiye aliyeniambia niweze kufika Maskoof kwamaana ndio mahala ambapo si rahisi kwa hao wanaonifuatilia kuweza kufika."
"Ulionana naye wapi Kasam?"aliuliza Mfalme akionekana kuwa na shauku ya kutaka kujua habari za huyo mtu.
"Huko nilipotokea. Yeye ndio kanieleza hali halisi ya huku na kuniambia hata habari kuhusu undani wa uongozi wenu."alisema Lutfia akiwatazama viongozi hao usoni wakionekana kuna kitu kimewashtua.
"Unamaana gani kusema hivyo, kuna kitu gani amekwambia Kasam kuhusu sisi?"aliuliza Malkia na kumfanya Lutfia ageuke kumtazama.
"Nawaomba kwa leo niweze kuishoa hapo. Kesho tukutanapo nitazidi kuwaeleza mengi tu, na yote haya yapp kwenye kitabu hiki hivyo nahitaji muda mwingi pia wa kukisoma hichi kitabu."alisema Lutfia na kutoa tena heshima kisha akageuka kurudi zake chumbani.
Mfalme na Malkia walibaki kumtazama hadi alipotokomea eneo lile na kubaki wenye maswali mengi kichwani.
"Mh huyu mtoto anaonekana sio wa kawaida kabisa!"aliongea Malkia akiwa anatazama kule alielekea Lutfia.
"Na anaonekana mwenye kujiamini sana kama Saadie vilevile."
"Ah huu mtihani tena sasa sijui anajua nini kuhusu sisi. Kwani kuna kitu kibaya gani tumekifanya?"alisema Malkia akigeuka kumtazama mumewe aliyeonekana kutafakari mambo bila kupata muafaka.
"Ila bado sina imani naye huyu binti, moyo wangu nahisi kujawa na wasiwasi sana dhidi yake."alisema Mfalme akiongea na mkewe.
"Mh sidhani kama ni mbaya kwetu, halafu amemtaja Kasam na kuonekana kuwa yeye ndiye amempa maelekezo ya yeye kuweza kujisitiri. Inamaana anamfahamu?"aliuliza Malkia na wote wakabaki njia panda hawaelewi imekuwaje.

Kwa Saadie alifurahishwa sana na yale yote ambayo ameyaongea Lutfia mbele ya Mfalme na Malkia. Hakutaka kuongopa aliyasema yote ambayo yanamhusu yeye hadi kuweza kufika katika falme ya Maskoof. Taratibu akaanza kumtembeza mule ndani kila sehemu hali iliyomfanya Lutfia ashuhudie wafanyakazi wengi ndani ya jengo lile la kifalme kila sehemu wapitayo wakitoa heshima kwa binti wa Mfalme.
Waliweza kupanda juu kabisa ya jengo hilo na hapo ndipo Lutfia akapata kushuhudia jinsi Maskoof ilivyokuwa kubwa.
"Mara nyingi huwa napenda kuja huku juu na kutazama makazi ya watu kama hivi. Nakuwa nafikiria mambo mengi sana pindi ninapoona hali zao na maisha ambayo wanaishi."alisema Saadie wakiwa wamesimama huku wakiangalia mji huo. Aligeuka na kumtazama Lutfia akiwa bize kuangalia mbele.
"Hivi haiwezekani watu wakaishi maisha mazuri kama ambavyo humu ndani tunaishi?"aliuliza Saadie na maneno yake yakageuza Lutfia amtazame.
"Napenda sana pawe na usawa na wala kusitokee matabaka baina ya watu na watu. Hebu tazama tu hapa ndani, watu wamenizidi umri na wengine wazee kabisa lakini nipitapo mimi wao wanainama chini kunipa heshima hali ya kuwa ni mdogo. Hili swala huwa silipendi ila baba amekuwa mstari wa mbele kunikataza na kusema ndio heshima."
"Ni viongozi wachache sana ambao watakuja kuwa na moyo kama wako Saadie. Sifa pekee ya kiongozi popote pale lazima aheshimike kwa watu wake.
Unachosema kipo sawa kuwa unahitaji usawa kwa watu wote ila kiongozi naye anapaswa kuheshimiwa na watu. Huenda alichosema Mfalme kilikuwa na maana ya kutofautisha kati ya kiongozi na watu. Ukaribu wako na watu ndio utakufanya wengi wakuzoee na kuona upo kawaida tu na huenda hata wale watu wabaya wakajua nyendo zako ikawa rahisi kukufelisha. Tangu nilipokuona wewe nikaiona kabisa kesho yako. Una moyo wa huruma sana kwa watu tofauti na Mfalme, ila naamini utakuwa kiongozi wa taifa hili na utaliongoza kwa amani sana watu watakupenda."alisema Lutfia na maneno yale yakampa faraja Saadie akayapokea.
Waliongea mambo mengi sana wakiwa pamoja hadi muda ulipokwenda wakarudi chini.

Upande wa pili Alie aliweza kufika hadi kwenye mji ambao Kasma na watu wake wanapatikana humo. Alijigeuka na kuwa na mavazi ya raia wa kawaida kusha akaanza kuingia mitaani kwanza kupekuwa mazingira yalivyo na jinsi wanavyoishi. Hakuna aliyeweza kumtilia shaka kwani hakuonekana tofauti na raia wengine. Alifika mahala akaona kina askari wamewakamata raia watatu wakiwapeleka kwenye falme, Alie alihisi tu huenda watu wale wamefanya makosa hivyo wanapelekwa sehemu yenye sheria. Naye alianza kuwafuata taratibu bila wao kujua hadi walipofika kwenye falme akapata kuona jengo hilo. Alishuhudia watu wale wakiingizwa na askari ndani huku yeye akiwa amesimama kutafakari ataanzaje kuingia lengo hasa ni kwenda kuonana na yule binti Kasma aliyemuona amefanana na Lutfia ili akubali kuungana naye katika swala zima la kutafuta kile kitabu.

LUTKAS SEHEMU YA 15


ILIPOISHIA

Alishuhudia watu wale wakiingizwa na askari ndani huku yeye akiwa amesimama kutafakari ataanzaje kuingia lengo hasa ni kwenda kuonana na yule binti Kasma aliyemuona amefanana na Lutfia ili akubali kuungana naye katika swala zima la kutafuta kile kitabu.

TUENDELEE
Alichokifanya ni kujibadili muonekano na kuwa askari wa kifalme akifanana na wenzake kila kitu kwenye suala zima la mavazi na hata kutembea. Taratibu akaanza kuingia ndani ya falme kuanza kumtafuta kiongozi wa hapo.
Mambo yalikuwa katika hatua za mwisho kwa Kasma pamoja na wale walezi kwa namna ya kuweza kulifanikisha swala lililo mbele yao. Wahudumu walianza kuwaandalia vyakula na vinywaji askari ambao wataweza kuondoka na Malkia huko wanakopaswa kwenda. Ilikuwa ni siri ndani ya falme tu hakuna raia anayefahamu kwamba kuna kitu nikaendelea,kila mtu alikuwa katika shuhuli zake.
Alie alifika hadi mule ndani akiwa mwenye kutambulika kama askari. Alijichanganya na wenzake wakawa wanafanya maandalizi ya safari. Hata ikafika muda ilibidi askari wote wakusanywe wapate kuchaguliwa baadhi yao ambao wataweza kuongozana ba Malkia Kasma kuelekea Maskoof . Walikuwa askari wengi sana lakini iliwalazimu waondoke wachache sana maana wanapokwenda ni kwenye falme tofauti hivyo wanakuwa kama wakimbizi.
Malkia alianza kupita kwenye mistari ya askari kuanza kuwagusa wale ambao anaona watamfaa siku ya kwenda Maskoof. Kila aliyeguswa alitoa heshima na kusogea mbele kuunda mstari wao, muda wote Alie alikuwa miongoni mwa askari hao akionesha ukakamavu wa kweli. Kasma aliposogea kwenye mstari aliokuwa Alie alisimama na kuanza kuangaza macho yake huku na kule, taratibu alisogea na kukaribiana na hata alipogeuka kumtazama askari huyo alitumia muda wa sekunde kadhaa kumtathmini na mwishowe akaachia tabasamu kisha akamshika mkono na kuanza kwenda naye mbele walipo askati wengine aliowachagua, Alie alishukuru kuona amefanikiwa kuwa miongoni mwa watakaokwenda Maskoof. Alimsimamisha pale na wenzake kisha akageuka nyuma kuwatazama askari waliobaki.
"Lengo letu ni moja, tutakapofanikiwa basi tumefanikiwa wote, na endapo tukafeli basi wote tumeshindwa japo sitegemei kushindwa katika hili. Hawa walipo mbele yenu sio bora sana kushinda nyie mliobaki, hawa wanawawakilisha huko tuendapo na endapo tukafanikiwa basi tutegemee mambo mazuri hapo mbele yetu.
Hatuna muda wa kupoteza jiandaeni nyie niliowachagua muwe tayari muda wowote ule tunaweza kuanza safari."alisema Kasma na kuondoka zake huku akifuatwa na walinzi wake pembeni.
Wale askari waliochaguliwa walifuatwa na wenzao wakipongezwa na pia kupewa moyo wa kujituma huko waendako. Alie alikuwa miongoni mwao wakipewa hamasa huku akiwa na sura tofauti na yake bila yeyote kumtambua kuwa yeye ni nani.
Zoezi la kuwaanda askari watakaoongozana na Malkia Kasma lilishamiri kila mtu alifahamu safari hiyo ya Malkia. Alie alitazama maeneo mengi na kupata kufahamu mambo mengi ambayo yanaendelea katika arshi hiyo. Alipata kujua endapo akiondoka Malkia kwenda huko basi Falme itakuwa inaongozwa na wale wazee ambao kwa upande wake hakuona ambaye anaweza kumzuia kufabya lolote. Alichokifanya muda huohuo alitokomea haraka kurudi ambako wenzake wapo wameweka kambi lengo ni kuwaeleza hali halisi.

Upande wa pili ukaribu wa Saadie pamoja na Lutfia ulizidi kushamiri kila siku maana ikawa kila mahala ambapo Saadie akitaka kwenda basi Lutfia ni pacha kwake lazima awepo. Siku hiyo walitoka kwenye matembezi yao wakapata kuingia ndani kwenda kupumzika. Mfalme alikuwa na ugeni kutoka taifa la jirani kwake wakija kutembeleana. Mgeni huyo ambaye pia ni Mfalme alipata kuwaona mabinti hao wawili wakipita pale walipokuwa wamekaa kuongea.
"Kwani unamabinti wawili au?"aliuliza Mfalme yule akiwaangalia wakina Saadie hadi walipoingia chumbani.
"Hapana, yule wa mbele ndio binti yangu. Huyu ni binti tu rafiki yake."alisema Mfalme akikosa neno hata la kuongea.
"Maana nilitaka kushangaa mbona imekuwa hivyo!"alisema Mfalme huyo na kuendelea na mambo yao
Kwa Saadie mara baada ya kuingia chumbani kwake alionekana kuchoka sana hadi kuamua kujitupa kitandani.
"Najihisi kichwa kinauma sana hata sielewi."alisema Saadie akiwa amejilaza.
"Pole sana, basi wewe pumzika kwanza mimi wacha nifanye usafi wa mwili tutaongea baadae."alisema Lutfia na kubafilisha nguo kisha akaelekea bafuni huku akimwacha Saadie katika hali ile ambayo ilianza kumtesa taratibu.
Muda mfupi alijikuta akipiga ukelele wa maumivu hadi kule alipo Lutfia akapata kushtuka. Ilibidi atoke haraka kwenda kujua kipi kimempata mwenzake

Kelele zile za Saadie ziliwashtua hata baadhi ya watu mule ndani akiwemo mama na baba yake. Haraka wakaanza kuharakisha kwenda kupata kujua nini kimetoa. Hata walipoingia Malkia alipomtazama mwanayr yu akapata kutambua ni ule ugonjwa wake ambao unamtesa sana hivyo swala hilo ni kawaida katika maisha ya Saadie. Lutfia alipofika pale alipata kuona baadhi ya watu wakiwa wamesimama pale alipojilaza Saadie. Alishtuka kumuona mwenzake alivyolala ni ishara kwamba amepatwa na tatizo. Haraka akasogea pale waliposimama watu na kushuhudia baadhi ya wazee wakiwa wamemzingira Saadie wakimpaka dawa kumsaidia. Povu jeupe lilimtoka binti huyo akiomesha kuzidiwa kimarafhi hali iliyowafanya hata wazazi wake wapate mashaka juu ya swala hilo.
Hali ile ikamfanya hata Lutfia ashanga maana hakuwahi kifahamu kama mwenzake anaumwa ugongwa huo. Ilimbidi anyanyue uso wake kuwatazama watu waliokuwa pale lakini idadi yao ikamzuia kufanya jambo akabaki amesimama pia lakini moyoni anaumia. Alijitahidi kujizuia huku akiwatazama wale wazee ambao kwake hakuona kama wanafanya jambo la kutoa msaada pale mbele ya Saaidie. Aliamua kujitoa na kuamua kusogea hadi pale walipo kisha akawatazama wale wazee ambao walipomwona yeye wakabaki kumtazama tu.
"Nipisheni?"alisema Lutfia akihitaji pale alipolala Saaide akiwa amezingirwa aachwe huru. Wale wazee walimshangaa akiwemo hata Mfalme na Malkia
Alipomtambua kuwa ni Lutfia na kukumbuka kile alichowaambia wakajua hueda kumsaada anaweza kuutoa. Wale wazee walitii maneno ya binti huyo wakampisha afanye yake. Ilibidi ageuke na kwenda kuchukua kile kitabu cha LUTKAS kisha akasimama pale Mfalme na Malkia wakiwa wanamtazama. Alikifunua kile kitabu katikati kisha akakiweka kichwani kwa Saadie ambaye alikuwa akitokwa na jasho jingi sana, akaanza kumfuta yale mapovu yali. Wale wazee wakabaki kushangaa tu kile kinachoendelea pale wakishuhudia binti yule anachokifanya.
Lutfia alishika kile kitabu huku akitamka maneno fulani ambayo hakuna mtu aliyeweza kuyasikia kwa ufasaha. Mwisho wa yote wakapata kumuona Saadie akikohoa kwa mkupuo hali iliyofanya anyanyuke pale alipolala huki akizidi kukohoa. Haraka Lutfia akaagiza maji yaletwe na likatekelezwa hilo akampatia Saadie apate kunywa.
Mfalme na Malkia baada ya kumuona binti yao akiwa ana hali ile muda huo walipata faraja na kuona kweli Lutfia ameweza kumsaidia binti yao siku hiyo. Malkia alisogea pale alipo mwanaye na kumkumbatia maana alikuwa mwenye kuumwa sana na ugonjwa wake huo umekuwa ukijirudia mara kwa mara na haukuwa wenye kutibika kwa simu moja. Ajabu leo haukupita ameweza kunyanyuka tena hata kunuwa maji kabisa. Alibaki kiwatazama watu walimzunguka pale alipo na kuhisi huenda hakuwa salama ndio sababu ya mkusanyikio huo. Alipomtazama Lutfia alipata faraja kuona mwenzake huyo yupo.
"Unajisikiaje na hali kwasasa?"aliuliza Lutfia akiwa anamtazama Saadie. Alishika kichwa chake kusikilizia maumivu lakini hapakuwa na sehemu yenye kumuuma.
"Siumwi sasahivi najiona mzima kabisa. Ilaa... mbona kumbukumbu zangu bado zipo! Nakumbuka nilijilaza baada ya kuhisi kichwa kuuma."alisema Saadie akiwa anashangaa. Malkia kusikia hivyo hata yeye alijihisi furaha na kuona kweli Lutfia ameweza kumsaidia binti yake.
Ilizoeleka pindi atakapokumbwa na matatizo hayo basi si leo wala kesho kuweza kupona, na hata akipata nafuu basi kumbukumbu zake zote hupotea na inachukua muda mrefu kuweza kurudi taratibu.
Watu wote waliokuwa pale baada ya kushuhudia tukio hilo walibaki kustaajabu huki wakimtazama Lutfia ambaye alikuwa mwenye kutabasamu tu huku akimtazama Saadie. Ilikuwa ni furaha kwa wote hasa Mfalme Yazid aliyeanza taratibu kumuamini Lutfia kuwa kweli nguvu zile anazitumia kwaajili ya kusaidia watu na si kudhuru. Alijikuta akipata heshima kubwa Lutfia kwa kile alichokifanya pale mbele ya Mfalme. Ilibidi watu watoke nje kumuacha binti wa kifalme apate kupumzika kwanza, muda huohuo Mfalme alihitaji kuongea na Lutfia wakiwa wawili.

Safari ya kuelekea katika falme ya Maskoof iliwadia, askari walikusanyika akiwemo Alie ambaye alikuwa na shauku ya kufika huko lengo lake lipate kutimia. Alikumbuka muda ule aliporudi kwa wenzake baada ya kupata kufahamu falme itakuwa chini ya mikono ya wazee pindi Malkia Kasma atakapoondoka kuelekea Maskoof.
"Nahisi hii pia ni nafasi nzuri ya sisi kuweza hata kuichukua falme ile. Mtu ambaye anauwezo wa kutuzidi ni yule Malkia wao mdogo ambaye tutaondoka naye pamoja. Hivyo pindi tukiondoka tu basi nanyi ndio muda wa kuivamia falme ile muweze muipindua na naamini tutaipata iwe mikononi mwetu. Mimi naimani huko tuendako tutafanikiwa tu kupata kile kitabu na itakuwa vyema tukapata ushindi huu kwa pamoja ili tutakaporudi wakute kila kitu kimebadilika."aliongea Alie kuwaambia wenzake ambao walimuelewa kwa kile alichokisema.
Yote hayo alikuwa akiyakumbuka akiwa pamoja na wenzake wakijiandaa kwa safari.
Malkia Kasma alisimama akiwa amevalia mavazi maalumu huku akiwatazama askari ambao ataongozana nao kuelekea huko. Alitabasamu kuona watu wake wapo imara na muda huohuo safari ikaanza kuelekea kule msituni kusubiri mahala ambapo ndio njia ya kuweza kufika Maskoof.

Kwa Mfalme Yazid alikuwa na Lutfia juu kabisa ya jengo la kifalme wakiwa wanaongea.
"Nashkuru kwanza kwa kuweza kuonesha huruma yako kwa kumsaidia binti yangu. Tumekuwa hatuna raha kabisa pindi hali ile itakapomtokea na imekuwa tunamtibia kwa muda mrefu sana hadi kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida. Leo imekuwa kama bahati hata yeye kuweza kushangaa kuona ni mapema mno. Nashkuru sana Lutfia kwa kuweza kuwa karibu na binti yangu sijui nikulipe nini."alisema Mfalme kwa upole akimpa shukrani Lutfia.
"Usijali Mfalme wangu, nimemsaidia Saadie kama ndugu yangu na wala sikuwa nahitaji malipo yeyote. Yeye kama asingenitetea siku ya kwanza basi ni wewe ndio ulikuwa unayakatisha maisha yangu mbele ya umati wa watu bila kutaka kujua undani wa mtu. Si kila watu wanaokuja ndani ya Maskoof wanakuja kwa ubaya Mfalme tambua hilo. Wengi wao wanakimbia mataifa yao kwa kuona hakuna amani, hakuna uhuru baina ya watu na viongozi. Hivyo hii ni sifa pekee unapaswa ujivunie kuona Taifa lako ndio kimbilio la wanyonge kutoka mataifa tofauti. Yakupasa uwakarimu na kuwaweka sehemu salama naamini kwa wema utakaowapatia hawawezi kukulipa ubaya kwa pamoja. Unapaswa ubadilike sasa hata Mungu atakubariki na sio kila mgeni unamdhulumu uhai wake. Huenda hata ugonjwa wa binti yako wewe ndio ukawa chanzo maana Mungu anakuhukumu kupitia yeye, hivyo pindi utakapoacha basi na Saadie atakuwa salama katika maisha yake yote."alisema Lutfia na maneno yake yakamjenga imani upya Mfalme dhidi ya wageni. Taratibu akaanza kuhisi kweli amekuwa mkosaji kwa kuua watu nila hatia. Alijikuta akimsogelea Lutfia na kupiga magoti mbele yake huku machozi yakimlenga.
"Nakiri kufanya makosa, ulichokisema huenda ikawa ni kweli huenda ni mimi ndiye niliyekuwa namuadhibu mwanangu kwa maradhi bila kujijua. Naweka kiapo kuanzia sasa sitaweza kumwaga damu na kuua watu kama ikivyo zamani. Na ninaombi moja kwako Lutfia nitafurahi sana ukilikubali."alisema Mfalme na kumeza funda moja la mate kisha akaendelea.
"Nahitaji uwe mlinzi wa mwanangu kuanzia sasa, popote alipo nawe uwepo naamini kwa uwezo ulionao Saadie atakuwa salama siku zote. Tafadhari naomba ukubali ombi langu."alisema Mfalme kwa sauti ya unyenyekevu hali iliyomfanya hata Lutfia apate furaha kuona kweli Mfalme ametubu madhambi yake ya kuua watu. Hakuona sababu ya kupinga ombi lile maana Saadie ndiye mtu pekee aliyemkarimu tangu kufika kwake Maskoof.
"Usijali kuhusu hilo Mfalme, nipo tayari kumlinda Saadie, nitakuwa naye muda wote."aliongea Lutfia na maneno yake yakafanya Mfalme ajihisi furaha, alimsogelea na wakakumbatiana kuonesha wamekubaliana.


LUTKAS SEHEMU YA 16


ILIPOISHIA

"Usijali kuhusu hilo Mfalme, nipo tayari kumlinda Saadie, nitakuwa naye muda wote."aliongea Lutfia na maneno yake yakafanya Mfalme ajihisi furaha, alimsogelea na wakakumbatiana kuonesha wamekubaliana.

TUENDELEE.
Siku hiyo kila mtu ndani ya jengo la kifalme alimtambua Lutfia ni nani na anauwezo wa aina gani, hivyo hawakumwona tena ni mtu wa kawaida bali walimpa heshima yake hasa wale wazee ambao walitegemewa katika masuala ya nguvu hizo. Walipata kutambua uwezo alionao binti huyo ni wa aina yake hivyo wapo waliomkubali nao moja kwa moja.

Wakina Kasma waliweza kutokea katika msitu huo mkubwa ambao ndio pekee ambao watu hupita hapo kuelekea katika mataifa mbalimbali. Walitawanyika askari kuweka ulinzi kusudi Malkia asipate tatizo. Alitazama huku na kule kwenye eneo lile bila kuona mtu wala kitu chochote pale, ilibidi atafute mahala apate kutulia kwanza wakisubiri huo muda wa kuona njia ya kuweza kupita kuelekea Maskoof. Alie alikuwa anatazama tu kinachoendelea akiwa kama askari wa Malkia Kasma. Muda wote alikuwa akimtazama Malkia na kumfananisha kabisa na binti Lutfia ambaye amekuwa akimfuatilia tangu awali lakini mwishowe alimkosa hapohapo kwenye msitu huo.

Muda huo Lutfia alikuwa zake chumbani kwa Saadie aliyekuwa ameegamia ukuta akiwa kitandani. Alishika bakuli la supu na kumsogelea binti huyo wa Mfalme na kuanza kumywesha taratibu. Walijikuta wote wakitabasamu maana wamekuwa ni zaidi ya marafiki tangu wafahamiane.
"Nashkuru sana kwa kuonesha upendo wako kwangu Lutfia, nimekuwa nasumbuliwa na ugonjwa huu tangu niko mdogo na nimewafanya wazazi wangu wahangaike kila mahala na kutumia dawa za kila aina lakini sikuwa mwenye kupona kabisa zaidi ya kunipa nafuu kidogo tena inachukua muda mrefu kuwa hivyo. Leo hata mimi nimeshangaa kuona nimerudi kama awali, imekuwa ni mapema sana sikutegemea. Hakika umenisaidia sana."alisema Saadie akiwa anamtazama Lutfia aliyekuwa mwenye kutabasamu tu.
"Usijali Saadie mimi nipo kwaajili ya kusaidia watu wenye matatizo. Hivyo ni wajibu wangu kufanya hivyo hasa kwako wewe ambaye ndiye uliyenipokea hadi kuwa hapa."alisema Lutfia na maneno yake yakampa faraja Saadie, walisogeleana na kukumbatiana wawili hao kisha wakaendelea kunyweshana supu. Lakini Lutfia alianza kuhisi tofauti na kujawa na wasiwasi wa ghafla moyoni mwake. Alijikuta akiachana na Saadie wakiwa wamekumbatia na kuanza kuangaza macho yake huku na kule akiwa kama mwenye hofu.
"Vipi tena?"aliuliza Saadie akiwa anamshangaa Lutfia.
"Mh nahisi tofauti, huenda kuna kitu kibaya kitatokea."alisema Lutfia na maneno yake yakamshtua Saadie pale alipo.

Kule msituni baada ya muda palionekana hali ya hewa ikianza kubadilika eneo lile. Upepo ulivuma na kukusanyika kujenga kimbunga kikali sana na kuwafanya askari wa Malkia watudi nyuma maana upeoo ulikuwa mkali sana hata Kadma mwenyewe alibaki kukinga macho yake yasipatwe na vumbi kali.
"Malkia, nadhani hii ndio njia pekee ya sisi kuweza kuingia ili tufike huko tunapokwenda. Yatupasa tuingie ndani ya kimbunga kile."alisema askari mmoja aliyesogea pale alipo Malkia, alikuwa ni Alie aliyefuata Malkia ambaye alishangaa baada ya kuambiwa vile ikabidi ageuke kumtazama askari yule.
"Inamaana hii ndio njia ya kuelekea Maskoof?"aliuliza Kasma na kumfanya Alie ajibu lile swali.
Hapakuwa na njia nyengine kweli ikabidi awataarifu askari wake kuhusu njia husika ya kufika Maskoof kama walivyopanga pamoja. Kauli ile iliwashtua baadhi ya askari ambao hawakutegemea kuona njia hiyo, wote wakabaki kutazama kimbunga kile kikizidi kukusanya majani na hata vimbi la ardhini. Hapakuwa na jinsi Malkia Kasma aliamua kuanza mwenyewe bila kihofia alikimbia na kujiingiza ndani ya kimbunga kile. Alie kuona vile akaamua kufuata akajitosa pia na kuwafanya watu wengine waamini na wao wakafuata kila mmoja hafi wote walipomalizika na kimbunga kile taratibu kikaanza kupungua kasi na mwishowe kutokomea kabisa na kuacha baadhi ya takataka tu zikiwa zimejikusanga.

Upande wa pili Lutfia ile hali ilizidi kumtia wasiwasi na kuamua kutoka kabisa mule kwa Saadie akaenda kuchukua kitabu chake apate kusoma huenda akaona jambo jipya.
Alipokishika tu kitabu hicho karatasi zikaanza kujifungua na kufika sehemu ikabidi aitazame kurasa hiyo iliyofunguka na kuanza kusoma kwa makini. Alibaki kushangaa sana kwa maelezo ambayo ameweza kuyaona ndani ya kitabu cha LUTKAS. Mikono ikaanza kutetemeka na woga ukaanza kumjaa hadi akatupa kile kitabu akihisi kuchanganyikiwa. Alibaki kushika tu kichwa chake akihisi maumivu yanaanza kumjia, haraka akalala chini na kukinyanyua kitabu kile akakiweka kwenye paji la uso huku akionekana kuhema sana. Machozi yakaanza kumtiriri pale chini na kushudia yakishuka masikioni hadi kupenya kwenye madikio yake. Alijiona mwenye kazi kubwa ya kufanya hapo mbele maana kuna matukio amepata kuyaona ndani ya LUTKAS.

Mtaani huko kile kikosi cha askari wa Malkia Kasma kilianza kutembele kila mtu kivyake wakiwa wamebadili mavazi yako kusudi wasijulikane kabisa. Walitembelea kila sehemu na kushuhudia askari wa falme ya Maskoof wakiwa wameimarika kwa ulinzi kila kona wakihakikisha usalama wa raia. Waliwasiliana wao kwa wao kwa hisia na uwezo walionao bila ya mtu yeyote kuweza kusikia.
Maongezi yao yaliweza kumshtua Lutfia pale chini alipolala na kujikuta akikurupuka haraka akanyanyuka. Haraka akatoka mbio na kuelekea juu kabisa ya jengo hilo la kifalme hali iliyomfanya hata Malkia aliyekuwa ametulia mahali na kumwona binti huyo akipita kwa kasi.
Lutfia alisogea mbele kabisa akiwa juu ya jengo na kuanza kutazama makazi ya watu. Aliona watu wengi wakienda kwenye shuhuli zao muda huo kila myu akiwa katika pilika pilika za kutafuta riziki. Ilimbidi atege masikio yake vizuri kusikiliza tena sauti zile ambazo alifahamu ni wazi kwamba hakuna binadamu wa kawaida ambaye ataweza kuongea kwa hisia namna hiyo. Ni wazi kwamba kuna watu tofauti na binadamu wa kawaida wapo ndani ya Maskoof wamechanganyika na raia wa kawaida.

Huku Malkia Kasma alikuwa naye ametulia sehemu akiwa na askari wawili akiwemo Alie ambaye hakutaka kuwa mbali na Malkia huyo.
"Nadhani hakuna muda wa kupoteza tena hapa, tunapaswa kuelekea kunapo falme maana yule binti nilipata kumwona akiwa na binti wa Mfalme hivyo lazima atakuwa amekaribishwa kuishi humo."alisema Kasma akiwa anatazama mazingira ya pale walipo.
"Na itakuwaje kama watu wakikufuata wakijua kuwa ndio huyo mtu ambaye unafanana naye. Na hatujui huyu mtu alipokelewa kwa wema au kwa ubaya hivyo yatupasa tuwe makini sana."alisema Alie akiwa kwenye muonekano wa askari wa Malkia.
Aligeuka Kasma na kumtazama Alie, alitikisa kichwa na kutabasamu kisha akageuka kuangalia makazi ya watu.
"Unachosema ni sahihi, huyu mtu tunayemfuata sio wa kawaida kwanza. Pia ufanano wetu hata mimi ndio umenishawishi kuja huku kuona kama ni kweli kile nilichokiona au laa. Inabidi nijizuie kutoonekana uso wangu wote ili watu wasiweze kuniona wakanifananisha. Ila huyu mtu ni lazima apatikane leo na tupate hicho kitabu."alisema Kasma akitilia mkazo. Maneno yake yalimfurahisha Alie kuona kumtumia Kasma atafanikisha malengo yake. Wakaanza safari ya kuelekea katika falme lengo ni kumtafuta Lutfia. Kasma alitembea mtaani akiwa amejifunika nusu uso wake ili asipate kuonekana mapema na watu, huku Alie akiwa makini kuangalia huku na kule kuona kama ataweza kupata kitu kitakachomsaidia.

Ndani ya falme Lutfia aliongoza njia kwenda kwa Mfalme kumpa taarifa mapema kuhusu kile alichokiona na kuhisi huenda kuna tatizo linaweza kutokea. Alipofika karibu na mlango wa Mfalme alipata kusikia maongezi mule ndani wakiongea Mfalme pamoja na wazee wa falme ya Maskoof ikabidi asogee kusikiliza.
"Lakini huo sio utaratibu Mfalme, huyu amekuja tu ni kama amesaidiwa na binti yako aweze kuishi naye tu. Lakini swala uliloamua la kumpa kabisa uhuru wa kumlinda Saadie sio sawa kabisa. Hatujui ametokea wapi, hatujui amekuja hapa kwa lengo gani, unawezaje kumpa idhini ya kumlinda binti yako angali hata muda wa kumchunguza hujapata. Hebu jaribu kulifikiria hilo usije kumuweka binti yako mwenyewe kwenye mikono hatarishi. Tunampenda sana Saadie na ndiye ambaye atakuja kurithi ufalme wako hapo baadae hivyo kama wazee wa falme hii tunaomba utusikilize Mfalme wetu."alisema Mzee mmoja na wenzake wakamuunga mkono kwa kile ambacho amesema. Mfalme aliwatazama na kujikuta akishusha pumzi yake taratibu.
"Mimi na binti yangu hatuna ukaribu kama wa baba na mwanaye, binti yangu ananiona mimi ni kama Mfalme nisiye na huruma kwa watu. Hana upendo na mimi hata kidogo hali inayofanya nijione si lolote kwake. Nitakuwa baba gani nisipopendwa na mwanangu? Furaha yake ndio baraka kwangu, tangu Lutfia afike katika ardhi hii mtu pekee aliyempokea na kujenga naye urafiki ni binti yang na ndicho nilichofanya hadi kuchukua uamuzi wa kumpa Lutfia wazfa wa kuwa mlinzi wa mwanangu. Muda wote wapo pamoja na ndicho ninachotaka mwanangu awe mwenye furaha, licha ya urafiki wao mkumbuke binti huyu anauwezo wa kipekee na ndio umemsaidia Saadie hadi sasa yupo salama. Asingelikuwepo Lutfia basi tungelisubiri siku isiyo na uhakika kusubiri Saadie apate kuinuka. Acheni uamuzi wangu uwe ni sheria kwa hili, Lutfia atabaki kuwa mlinzi wa mwanangu na siwezi kulisitisha hilo."alisema Mfalme Yazid akiweka msisitizo wa maneno aliyosema. Aliyokea kumkubalia Lutfia kwa machache tu aliyofanya kwa binti yake, wale wazee wakabaki kutazama tu na kuona hata wakiendelea kumuelewesha Mfalme hawatambadili maamuzi yake abadani.
Lutfia alikuwa amesimama pale mlangoni akiyasikia maongezi yao. Aliona jinsi Mfalme anavyomuamini kwasasa lakini si kwa wazee wale, hivyo hakutaka kuingia kuongea na Mfalme angali wazee wale wapo. Aliamua kugeuka na kurudi zake alipotoka, lakini moyo wake unakuwa mgumu sana kuondoka akiliacha swala hili. Aliona aelekee kwa Saadie kwenda kumpa taarifa hiyo ambayo amepata kuona na kusikia sauti za watu ambao anahisi si wema katika taifa hilo.

Muda huo ndio Kasma pamoja na askari wake kadhaa akiwemo Alie waliweza kufika nje ya jengo la kifalme. Wakabaki kulitazama tu hata Alie ilikuwa ndio mara yake ya kwanza kuweza kuona falme ya Maskoof. Hapo ndipo inaaminika Lutfia anaishi, aliona ndio muda muafaka wa kufanya kile kilichomleta aweze kupata kitabu ambacho muda mrwfu amekuwa akikifuatilia.


LUTKAS SEHEMU YA 17


ILIPOISHIA

Hapo ndipo inaaminika Lutfia anaishi, aliona ndio muda muafaka wa kufanya kile kilichomleta aweze kupata kitabu ambacho muda mrefu amekuwa akikifuatilia.

TUENDELEE SASA...
"Unauhakika wa hicho unachosema Lutfia?" Ilisikika sauti ya binti wa Mfalme akiongea huku akimtazama Lutfia. Ni baada ya kuambiwa kila kitu kuhusu ujio wa watu ambao Lutfia anahisi si wema katika taifa hilo.
"Amini hivyo, moyo wangu umekuwa hauna amani kabisa Saadie siwezi hata kukaaa nitulie angali naona kuna tatizo mbele yangu."alisema Lutfia akionesha kujali kile asemacho.
Saadie alikuwa amejipumzisha kitandani akiwa ameegemea ukuta, kwa maelezo aliyopata kutoka kwa Lutfia yalimshtua sana na kubaki kutafakari kwa muda hasa swala la hao watu wageni ambao wanasadikika si wema katika taifa hilo. Alitamani kwenda kutoa taarifa kwa baba yake lakini ni yeye ndiye aliyemtaka baba yake aache kuua raia wageni wanaokuja kutoka mataifa tofauti. Hivyo zoezi la wageni kuvamia pindi akisikia Mfalme itamfanya arudi katika tabia yake ya awali ya kuwahumu watu hao.
"Unachokifikira wewe ndio hata mimi nafikiri hivyo, sidhani kama akijua hilo atakuwa na huruma tena kwa raia wa kigeni hata kama ni wema."
"Sasa tunafanyaje ndugu yangu?" aliuliza Saadie akiwa anamtazama Lutfia.

Huku chini Kasma alikuwa katibu na geti kuu la kifalme ambalo pale nje palikuwa na askari walishamiri kulinda amani mahala hapo. Aliwatazama wote na kutambua idadi yao ili afahamu namna ya kufanya muda huo. Kwa uwezo alionao Kasma alijibadili na kuwa kama askari wa kifalme, hali hiyo hata Alie aliweza kumuona na kujua kinachoendele. Moja kwa moja aliongoza njia kuelekea ndani bila kufahamika kirahisi, ilimbidi Alie naye afanye hivyo ili kuwa sambamba na Malkia huyo kila hatua anayokwenda.

Lutfia alionekana akimfunga zipu ya gauni binti wa Mfalme aliyeonekana karibu na kioo akijitazama jinsi alivyopendeza. Lakini macho yake yalikuwa ni ya kutisha sana kiasi cha kumfanya hata yeye aheme kwa hofu akiwa amesimama.
"Tafadhari Saadie, jitahidi kuzuia hiyo hali usiweze kuonekana kama ni mwoga kiasi hicho. Hebu kuwa imara fanya kama huna kigeni kilochopo mwilini mwako naamini wakikuona hata wao wataogopa."alisema Lutfia akiwa anamuweka gauni sawa Saadie karibu na kioo kikubwa sana kilichopo ndani ya chumba hicho.
"Najitahidi lakini naogopa sana Lutfia. Hivi ni kweli mimi ndio natisha kiasi hiki?"alijitazama Saadie akionekana kwenye hali ile, macho yaliwaka na kuwa makali kama paka aangaliapo usiku wenye kiza kinene. Ilimbidi Lutfia naye ajisoheze na kutazama kioo kile huku akijibadilisha na kuwa kama Saadie.
"Hii hali ni ya muda tu na ndio maana nikasema jifunze kutuliza hofu yako na hali hiyo itapotea. Uwapo na hasira pamoja na hofu basi lazima itokee hii hali hivyo hawa watu usiwafikirie sana. Tambua nilichokupatia ni kitu kikubwa sana na kila kitu ambacho nafanya mimi basi hata wewe unaweza. Tukifanikiwa kuwadhibiti hawa watu nakuahidi uwezo huo utakuwa kwako daima. Hiyo ni silaha tosha ya kuwadhibiti hawa watu, tunailinda Falme, tunalinda Maskoof bila kusaidiwa na jeshi la Mfalme kama tulivyopanga."alisema Lutfia akimpa ujasiri mwenzake. Manano hayo yalimuinua Saadie na kianza kuoma kweli anapaswa kulifanimisha hilo kwaajili ya taifa lake. Aligeuka kutazamana na Lutfia wakiwa wote wenye macho ya kutisha. Punde tu alishusha pumzi Saadie na papo hapo hali ile ikapotea na kujiona wa kawaida, alipoona hivyo Lutfia naye akarudi kama awali. Saadie alikubaliana na mwenzangu wakaamua kufanya kazi hiyo wawili. Alinyanyuka pale kuanza njia kutoka mule chumbani kisha akafuata Lutfia safari ikiwa ni kuzunguka jengo zima kwanza kuhakikisha usalama.
Malkia alipata kumwona binti yake Saadie akiwa mwenye haraka kwa kutembea kwake huku akiwa anawatazama sana watu wa mule ndani hususan askari wa mule ndani ya jengo hilo. Malkia alipatwa na wasiwasi baada ya kumwona tena Lutfia akiwa mwenye kutembea kama ilivyo kwa Saadie. Ilimpa mashaka kidogo lakini hakutaka kuumiza kichwa chake akaendelea na mambo yake.

Ulikuwa ni msako wa kuhakikisha Falme nzima hakuna mabadiliko yeyote katika sehemu mbalimbali . Usalama pia maana taarifa ya kuwepo kwa hao watu wanaohisiwa kuwa si wema kwao. Saadie alihakikisha kila askari wao anawatazama kwa jicho la tatu na uwezo alipatiwa na Lutfia ambaye muda huo naye alifika eneo hili akimuona Saadie amesimama huku macho yake yakitalii kila upande. Ilibidi wakubaliane kugawana sehemu za kufanya doria hiyo fupi kwa muda kadhaa. Hakuna yeyote aliyefahamu kama kuna jambo linaendelea ndani ya falme kila mtu alikuwa katika shuhuli zake.

Upande wa pili Kasma alifika nje ya chumba kimoja akiwa kama askari wa kifalme. Aliwakuta askari wanne wamesimama nje ya chumba hicho hivyo alihisi huenda ni chumba cha Mfalme sababu ya ulinzi huo. Aliamua kupita huku akipeana heshima na askari wale waliofahamu ni mwenzao. Alizidi kupiga hatua kupitia vyumba vengine lengo ni kutambua alipo Lutfia. Hata alipofika mbele alipata kuona chumba kimoja mlango ukiwa wazi. Aligeuka nyuma kutazama kama kuna ambaye anayemuona lakini hapakuwa na yeyote eneo hilo. Haraka akaingia humo na kuanza kuangaza macho yake yaliyobadilika gafla akiwa anatafuta kile kitabu.

Huku upande mwengine Alie kila anapopita anakutana na idadi kubwa na askari wakiweka ulinzi kila sehemu. Katika harakati hizo alipata kumwona binti wa Mfalme mbele kabisa akiwa anaangalia huku na kule kana kwamba anatafuta kitu. Alimtazama jinsi alivyo na kuona huenda akimtumia huyu ataweza kumpata Lutfia kwa urahisi, hakutaka kuchelewa muda huohuo akawa anayasema maneno fulani na kuonekana moshi ukijitokeza kuelekea kule alipo Saadie ambaye hakuwa analojua yeye alikuwa anakuja tu hadi moshi ule ukamkuta na kuanza kumzunguka pale ndipo alipokuja kushtuka kukutana na hali ile. Alibadilika gafla baada ya kuona kuna kitu ametupiwa cha kumdhuru, aligeuka kuangalia kule moshi ulipotoka na kukumbana na sura ya Alie ambaye naye alibaki kushangaa kuona kile alichokitaka hakikufanikiwa.

Ilimbidi yeye apite njia tofauti asipate kukutana na binti huyo wa Mfalme. Alitoka mbio eneo lile huku Saadie naye akaanza kukimbia kumfuata baada ya kuiona sura ya msichana huyo ambaye.
Alifika mahala Alie akajificha kwanza huku akihema maana haamini kile alichokiona.
"Inamaana hata huyu anauwezo wa kututambua?"alijiuliza mwenyewe Alie akiwa anahema. Alijitazama vizuri na kujiona kabisa yupo katika umbo la kiume tena askari wa kifalme lakini kwa kile alichokiona pale ni wazi kwamba mtoto wa Mfalme ameweza kumtambua. Ilimbidi ampe taarifa hiyo Kasma aliyekuwa kule chumbani akiendelea kutafuta kitavu cha LUTKAS.
"Mtoto wa Mfalme pia anauwezo mkubwa wa kututambua tulivyo, hili ni tatizo ni wazi kwamba sasa wamejua kuwa yumeingia humu."aliongea Alie na maneno yake yakamfikia Kasma kule alipo, alishangaa kusikia hivyo. Aliona uwepo wake mule chumbani huenda kukawa ni hatari haraka akaanza kuweka vitu sana apate kuondoka.
"Unatafuta nini humu chumbani?"ilisikika sauti hiyo iliyomshtua Kasma mule ndani akishindwa kuelewa ajibu nini. Taratibu akageuka nyuma sauti inapotokea.

Upande wa pili wale askari waliokuja na Kasma nao waliweza kuwasili katika falme kila mtu akiwa amekuja kwa namna yake walitazamana na kupeana ishara kwamba wanapaswa kuingia ndani kwa namna yeyote ile. Na kwakuwa walikuja kwaajili ya kufanya kazi hivyo hawakuwa na huruma kwa mtu yeyote waliamua kuingia kwa mabavu kuweza kuwapunguza askari wote wa kifalme ili wapate uhuru wa kuingia ndani zaidi. Walianza kusogea kwenye lango kuu na walipolikaribia tu wakaanza kutoa silaha zao mapanga marefu yenye kun'gaa hali iliyowafanya askari wa kifalme washangae nao wakajiweka sawa baada ya kuona hakuna amani tena eneo hilo. Zililia kelele za panga na makelele ya watu wakijeruhiwa vibaya hali iliyowafanya askari wengine watambue hakuna usalama. Haraka kamanda wa majeshi ya kifalme alikimbia kwenda kutoa taarifa kwa Mfalme kuhusu falme kuvamiwa. Alie alipata kusikia kelele zile na kutambua wenzao wameshaanza kupambana vikali ili wapate kuingia ndani. Hakutaka kusibiri gafla alipotea pale alipo na kutokea kwenye vita hiyo ya mapanga. Hakhitaji silaha yeyote uwezo alionao ulimtosha kuwadhibiti askari wengi kwa mkupuo. Alikuwa mwenye uwezo mkubwa sana wa kuwadhibiti watu na kila anapootewa kukatwa na mapanga alibaki kutazama sehemu hiyo iliyokatwa na kutabadamu yu maana hakuna damu ambayo inatoka mwilini mwake, ni mfu ambaye bado anaishi na ndio sababu ya kukitafuta kitabu cha LUTKAS ili apate kubadilika kabisa kurudi kuwa binafamu wa kawaida.
Makundi ya askari yalizidi kujitokeza wakijatibu kwazuia watu wachache waliovamia falme hiyo tukufu lakini haikuwa rahisi kama ilivyodhaniwa. Askari wa Kasma walikuwa na spidi pamoja na uwezo wa kipekee wa kupambana na watu wengi japo kwa uchache wao hawakujali.

Taarifa za kuvamiwa kwa Falme ilifika mahala husika ikamshangaza sana Mfalme aliyejikuta akinyanyuka kusimama kwa hasira sana.
"Ni nani ambao wamevamia katika nyumba yangu?"
"Hawa watu hatufahamu walipotokea na ni wachache sana ila baadhi yao wanaonekana si watu wa kawaida. Wana nguvu kama ambazo binti Lutfia anazitumia. Sasa tuna mashaka na hili swala huenda hata huyu binti walimtanguliza kusudi ili tumuone mwema na wenzake ndio hawa sasa wanakuja kuliharibu taifa letu."alisema Kamanda mkuu akiwa anatazamana na Mfalme. Maneno yale Mfalme yalimuingia moja kwa moja na kuhisi huenda ikawa kweli maana hawafahamu wapi alipotokea Lutfia, hivyo kama waliovamia falme yake wanauwezo kama alionao binti huyo ni wazi kwamba wapo pamoja kuipindua Falme yake.
Alicheka kwa dharau sana na kumtazama kamanda mkuu aliyekuwa akisubiri kauli kutoka kwa Mfalme.
"Hakuna kumuonea yeyote huruma hao watu hata wawe na uwezo gani lazima wauawe. Huyu binti pia sitaki kumuona katika dunia hii maana nilianza kumuamini kumbe si mwema kwetu. Na haraka mtafuteni mwanangu mumuwekee ulinzi wa kutosha asije kudhurika na huyo mbwa mtoto.. HARAKAA!"alitoa amri hiyo Mfalme alionekana kuchukizwa na jambo hilo. Muda huohuo kamanda alitoka na kuwapa kazi majeshi yake yakaungane na wenzao kuwazuia wale watu wasizidi kuingia ndani. Huku yeye pamoja na askari kadhaa wakielekea kumtafuta binti wa Mfalme awe katika mikono salama.

Mule chumbani alipo Kasma alijikuta akishikwa na butwaa baada ya kutazama na yule mtu aliyemgeukia. Alikuwa ni Lutfia ambaye hata yeye alipata kushangaa baada ya kumuona Kasma akiwa katika umbo, sura na hata muonekano kama wake. Hakika walifanana kila kitu wote ikabidi wasogeleane karibu kila mtu akamshika mwenzake sura maana haamini kabisa ufanano huo.
"Wewe ni nani?"
"Wewe ni nani?"
Ni swali ambalo kila mmoja wapo alikuwa akimuuliza mwenzake maana walikuwa wakipata tu habari ya ufanano huo lakini leo wameonana kabisa uso kwa uso.
Muda huohuo Saadie naye akapata kuingia kwenye chumba kile na kusimama sambamba na Lutfia huku akimtazama Kasma aliyekuwa mbele yao. Alijikuta akishangaa kuona aliyembele ni yeule anayemfahamu Lutfia. Ilibidi ageuke kumtazama aliyesimama naye pale, alibaki ameshukwa na bumbuwazi kuona sura ileile. Ikambidi asogee pembeni kuwatazama kwa pamoja kujaribu kuwatofautisha lakini hakukuwa na tofauti yeyote kati yao.


LUTKAS SEHEMU YA 18


#ILIPOISHIA
Ilibidi ageuke kumtazama aliyesimama naye pale, alibaki ameshikwa na bumbuwazi kuona sura ileile. Ikambidi asogee pembeni kuwatazama kwa pamoja kujaribu kuwatofautisha lakini hakukuwa na tofauti yeyote kati yao.

#TUENDELEE.
"Wewe ni nani?"aliuliza Lutfia akiwa anamtazama Kasma.
"Nikuulize wewe, mbona upo sawa na mimi kila kitu, ni nani wewe?"aliuliza Kasma kila mtu akitaka kujua kuhusu mwenzake. Maswali hayo yalimchanganya hata Saadie ashindwe kutambua mapema Lutfia halali ni yupi. Lakini alipotazama nguo zao tu akatambua kuwa yule aliye karibu na mlango ndiye.
"Najua kilichowaleta huku Maskoof, ila kwa hiki kinachoendelea hapa mbele yetu ni jambo kubwa sana na tusipoangalia mmoja kati yetu atajuta kama hatutosikilizana."alisema Lutfia na kufunua nguo yake akatoa kitabu cha LUTKAS akakikamata kwa mikono miwili.
"Hiki ndicho kilichowaleta huku Maskoof na hakuna lengine, nimekuwa na hiki kitabu kwa muda mrefu sana hadi sasa kimenizoea. Nilitamani kujua mengi zaidi na hata maana halisi ya neno LUTKAS. Nikafanikiwa kujulishwa maana yake kuwa ni majina ya watu wawili ndio imefanya kutokee jina hili. Lutfia na Kasma ndiyo majina pekee yanayounda neno moja. Na bila shaka wewe ndiye Kasma mwenyewe, naitwa Lutfia, na nilitamani siku moja niweze kukuona kwa macho yangu maana nimepata habari zako hapo nyuma."alisema Lutfia akionekana mwenye tabasamu usoni.
Kasma baada ya kusikiliza maneno hayo aliyafananisha na yale aliyoambiwa na yule mtabiri wao aliyemuonesha Lutfia akiwa na binti wa Mfalme. Ilibidi ageuke kumtazama na Saadie ambaye muda wote alikuwa akiwatazama tu.
Hapo ndipo akaamini kile alichokiona awali baada ya kuwaona kwa macho wawili hao. Alibaki kushusha pumzi tu maana haelewi nini afanye.
"Hebu niambie kwanini jina langu lihusike katika kitabu hicho? Na imekuaje sisi tuwe hivi angali si ndugu na hatujuani?"aliuliza Kasma akiwa anamtazama Lutfia.
"Hilo swali lako ni gumu kwa upande wangu maana hata mimi sielewi kwanini inakuwa hivi. Ila nakuomba sana uamuzi uliokuja nao ubadilishe, hiki kitabu kinawindwa na wafu ambao lengo lao hasa pindi wakikipata kiwasaidie kubadilika na kuwa binadamu tena, na mabadiliko hayo hayatakuwa na amani wataleta matatizo makinwa sana ulimwenguni. Ndio maana nimekimbilia huku walikuwa wakinitafuta kila sehemu. Maskoof ndio kimbilio langu sehemu ambayo wao hawawezi kufika huku, na huenda ujio wako ndani ya watu uliokuja nao basi na wao wakawepo maana wasingeweza kufika hapa."alisema Lutfia na kumfanya Kasma atafakari kama kuna mtu ambaye anahisi si askari wake.

Huku nje askari walizidi kuweka ulinzi kila kona huku wengine wakijaribu kuwazuia askari hao waliovamia ndani ya falme. Malkia alichukuliwa na baadhi ya askari wakimsindikiza hadi alipo mumewe na kuwaweka pamoja huki wakiimarisha ulinzi nje. Walizidi kumtafuta sasa Saadie ambaye hakuweza kufahamika wapi alipo. Ilimfanya mama yake ahofie juu ya maisha ya binti yake ambaye muda mwingi amekuwa naye.
Kasma alikuwa anapekua baadhi ya vyumba kwa ndani akizidi kukitafuta kitabu wanachokiandama kukipata. Hakujali lolote lile lengo hasa ni kufanikiwa kile kilichowaleta. Gafla walitokea kundi la askari wakimtaka anyanyuke pale alipo huku mikono yake ikiangalia juu. Hakuwa na hiyana alifanya kama alivyoagizwa, alinyanyuka na kuweka mikono juu huku taratibu na kuanza kuwahesabu watu wote waliomzunguka wakiwa na majamvua.
Taratibu wakaanza kumsogele ili wapate kumtia mikononi mwao haraka lakini kwa Kasma haikuwa rahisi hivyo. Alijidhihirisha kwamba yeye ni nani na ndio sababu ya kufika hapo maana kwa muda mchache tu aliweza kuwamudu watu wote pale na kuwaacha vilema na wengine kupoteza maisha kabisa kwa kipigo cha muda mfupi na kwa uwezo alionao. Aliona tayari majeshi ya kifalme yanashamiri na bado lengo lale hakijakamilika. Alitoka pale upesi na kuelekea vyumba vyengine akiendelea kutafuta kitabu.

Upande wa pili Mfalme na Malkia walikuwa sehemu maalum kwa ajili ya usalama zaidi. Muda wote Mfalme alionekana mwenye jazba sana baada ya kuona Falme yake ikivamiwa. Akili na mawazo aliyonayo kwasasa ni kuwa Lutfia ndiye mtu aliyesababisha haya. Alijikuta akipatwa na hasira dhidi yake hata kuvunja baadhi ya vitu kwa hasira alizonazo. Malkia alibaki kumtazama tu huku akionekana kuwa na hofu juu ya tukio linaloendelea. Muda mfupi walifika askari wa kifalme na kutoa heshima kwa viongozi hao.
"Tunahitaji kuwatoa hapa kuwapeleka sehemu ya usalama zaidi, hawa watu wamezidi kuingia ndani zaidi."alisema askari mmoja na kumfanya Mfalme Yazidi akubaliane naye. Alimsogelea mkewe na kumshika mkono wakaanza kuongozwa na askari wale kwenda sehemu yenye usalama maana vita imezidi kuwa kubwa zaidi.

Kwa Lutfia kule alipo hakuwa mwenye pupa pindi alipokutana na Kasma. Lengo hasa ni kumbadilisha kimawazo ambayo anaonekana amekuja kwa shari hivyo alihakikisha anamuweka upande wake. Swala ambalo lilikuwa si jepesi kama alivyodhani maana Kasma hadi muda huo haelewi nini afanye baada ya kujidhihirishia kwa macho yake kumuona Lutfia. Muda huohuo Alie alifika eneo hilo na kukutana na mazungumzo ya watu hao wawili yakiendelea, ikambidi asikilize kabla ya kkufanya kile alivhokipanga.
"Kama kweli hufahamu asili ya ufanano wetu basi yatupasa kulifuatilia hili tujue imekuwaje. Hilo swala sio dogo kama tunavyofikiri linauzito wake, kiukweli nakosa hata nguvu ya kuendelea kufanya kile kilichonileta, nafsi imekuwa nzito kuendelea na nilipanga kweli nikusambaratishe moja kwa moja ili niweze kupata hicho kitabu."
Maneno yao yakamfanya Alie astaajabu kuona sasa Kasma anaelekea kutekwa kiakili na kimawazo ili apate kurudi kama awali. Na huenda akapata kuungana na Lutfia na jambo hilo likawa kubwa haswa. Hakutaka kuendelea kukaa tena pale alichokifanaya ni kuondoka zake pale kwenda kuwajuza wale askari wa Kasma waliochaguliwa kuhakikisha wanapata kile kilichowaleta huku Maskood.
"Jamani Malkia huenda kwa muda mfupi kuanzia sasa akawa si mwenzetu tena, tayari nimemuona akiwa mweye hali ya kuwasikiliza wale mabinti hasa huyu mlengwa Lutfia."alisema Kasma akiwa kwenye umbo la kiaskari na sura tofauti."
"Hapana tulikuja na Malkia huku lengo ni kupata kule ambacho kimetuleta hapa.. sasa iweje tumuache huku hata kama ameshikiliwa na hawa watu ndio muda sahihi wa kumsaidia."alisema askari mmoja aliyeonekana ni jasiri na wenzake wakamuunga mkono huku wakimtazama Alie.
"Au wewe unachoogopa ni nini? Unakuwa kama sio mwanaume, hapa ni kuhakikisha tunarudi tukiwa na ushindi kama nguvu tunazo."walizidi kujitapa pale huku Alie akiwatazama. Alibaki kunyamaza kimya na wanaume wale wakaongoza njia kuzidi kwuingi andani tu. Alie aliwatazama wakiwa mbele na kuona ndio muda wale wa kuzidi kuwadidimiza tu. Aliyaongea maneno fulani ambayo hayakuweza kusikika kwa urahisi, kisha akageuka na kutafuta njia ya kurudi kule alipotokea.

"Inamaana hawa askari niliokuja nao kuna ambao wananisaliti?"ilisikika sauti ya Kasma kule chumbani walipo. Lutfia alitabasamu huku akimsogelea kabisa na kusimama pamoja.
"Tangu awali nilikwambia hivyo, watu uliotembea nao kutoka huko mlipotokea hadi kufika hapa lazima kutakuwa na watu ambao wanakugeuka tu. Na kwa ninavyodhani ni mtu mmoja uliyekua naye, huyu sio kama mlivyo ninyi, huyu ni mfu ambaye anaishi hivyo toka awali alikuwa akitafuta njia ya kufika huku, na njia ndio hiyo kapitia migongo yenu naameweza kufanikisha zoezi lake alilokusudia."alisema Lutfia na kuzodi kumpa wakati mgumu Kasma, alijikuta akisogeza kiti na kukalia maana anayoelezwa ni mengi ambayo hayafahamu.
"Lutfia, huu sio muda wa kuanza kubembelezana au kukaa sehemu kama hii, tupo kwenye wakati mgumu hatuna haja ya kuendelea kuyaongelea hayo angali watu wanazidi kuangamia huko nje. Kama huyu ni muelewa wa haya machache tu uliyoyaongea basi atajua wapi ni sehemu sahihi kwake na kuweza kuyoa idhini ya kuwasimamisha askari wake."alisema Saadie na kumfanya Lutfia amshike mkono Kasma.
"Hakuna haja ya kuendelea kujadili haya, ni vyema ukafanya uamuzi ulio sahihi kwako."alisema Lutfia na kugeuka kuondoka zake, Saadie alibaki kumtazama tu Kasma akionekana kuwa kwenye sintofahamu. Hakutaka kuendelea kukaa pale naye akatoka kumfuata Lutfia alipoelekea.

Ilimbidi Kasma akae atulize akili kutafakari ni mtu gani ambaye amekuja naye na si mwema kwake. Alikumbuka kila hatua ambayo wameanza kupanga mikakati ya kuja huku Maskoof hadi walipofika. Ni askari mmoja tu ambaye amekuwa akitoa mawazo ambayo wao waliyaona ni sahihi. Alikumbuka muda ule ambao walikuwa kule msituni kukatokea kimbunga kikali sana na adkati mmoja ndiye aliyehisi ndio njia pekee ya wao kufika Maskoof. Hata walipowasili katika ardhi hiyo ya ufalme wa Yazid ni askari huyohuyo aliyemshauri Kasma kuhusu ufanano wake na Lutfia hivyo akataka ajifunike kusudi watu wasiweze kumwona pindi wakitembea,. Alijuaje hayo yote angali hakuwa anaelewa kuhusu kile kimbunga wala kufanana kwa Lutfia na Kasma. Taratibu akaanza kuhisi huenda yule ndiye akawa mbaya kwa upande wake na ndio ambaye Lutfia anamsema muda ule.
Aliona kuna haja ya kumtafuta yule askari aweze kumbana aseme ukweli kuwa yeye ni nani. Alijikuta akipatwa na hasira na ghadhabu akanyanyuka pale aliposimama na kuanza kuongoza njia kutoka mule chumbani. Punde tu wakatokea askari zaidi ya 10 wakiongozwa na kamanda mkuu wa jeshi hilo la kifalme wakiwa na silaha mbalimbali. Walizinyanyua na kumuonesha Kasma aliyebaki kushangaa.
"Tumejua njama zako zote na hao wenzako waliovamia leo kuangusha ufalme wa Mfalme Yazid. Hamtaweza hata kidogo tumeapa kulitumikia taifa hili, upo kwenye mikono yetu kuanzia sasa."aliongea Kamanda mkuu akiwa ameshikilia panga lenye kun'gaa sana akimuonesha Kasma ambaye hakuwa anaelewa lolote hapo awali, ila kwa maelezo hayo akapata kutambua huenda wanamdhania ni Lutfia. Lakini hata angejitetea vipi asingeweza kueleweka, ilimbidi afanye ujanja wa kuweza kuwatoka kundi hilo la askari.

LUTKAS SEHEMU YA 19


# ILIPOISHIA
Ilibidi ageuke kumtazama aliyesimama naye pale, alibaki ameshikwa na bumbuwazi kuona sura ileile. Ikambidi asogee pembeni kuwatazama kwa pamoja kujaribu kuwatofautisha lakini hakukuwa na tofauti yeyote kati yao.

# TUENDELEE.

Taratibu bila kujulikana akaanza kuzipandisha nguvu zake ili aweze kuchoropoka mikononi mwa askari wale lakini haikuwa rahisi. Walimuwahi askari kadhaa wakamtupia unga wa rangi ya kijani uliomwingia machoni na hata vumbi lake likiaanza kumdhuru muda huohuo akadondoka chini na kupotoza fahamu. Alisogea kamanda mkuu na kumtazama Kasma pale chini kisha akaamuru abebwe kupelekwa alipo Mfalme Yazid.

Upande mengine wale askari wa Kasma waliokuwa na shauku ya kwenda kufuata Malkia wao aliyesadikika kuanza kutekwa akili na Lutfia. Hata wao nao akaanza kuingiwa na sintofahamu ya kuendelea mbele. Miili yao haikuweza kutamani kuendelea tena kumfata Malkia wao hivyo ikawabidi wageuke nyuma walipotokea na kuanza kumfuata sasa yule aliyewapa taarifa hizo kuhusu Kasma.
Mfalme na Malkia ndio walikuwa wanafika nje ya jengo la kifalme ambapo walipatwa kuambiwa na askari wanaowalinda kuwa ndio sehemu salama kwao. Wale askari walisogea mbele kuangaza huku na kule kujua kama atatokea mahala hapo, walibaki wakitabasamu tu na gafla miili yao ilaanza kubadiki na kuwa na maumbile yale ya kwao. Mfalme na Malkia walipowatazama wale watu walishangaa baada ya kuona wanageuka kuwa viumbe wa ajabu. Ni wazi kwamba wamechukuliwa na askari ambao sio wa falme yao hivyo wapo kwenye mikono hatarishi.
Muda huohuo alifika Alie akiwa mwenye tabasamu na kusogea hadi walipowekwa Mfalme pamoja na Malkia wake ambao walipomuona Alie walishangaa na kushikwa na butwaa.
"Alie!!"Mfalme alishangaa huju sura ya Alie ikiwa yenye kutabasamu.
"Ndio mimi, nilijua umenisahau nilitaka kukukumbusha kwa kile ulichokifanya."alisema Alie na kusogeza kiti akapata kukaa huku akiwatazama viongozi hao.
Malkia alibaki kushika tu mdomo maana hakutegemea kama angemuona msichana huyo mbele yao.
"Hata mimi sikutegemea kama nitaweza kukutana na wabaya wangu kwa mara nyengine, ila kwakuwa nafasi hii nimeipata basi napaswa kufanya kile ambacho kitakuwa ni haki kwetu wote sio eti wenzangu?"alisema Alie akiwa anawatazama viongozi hao ambao waligeukiana wakatazamana kwa muda maana kumuona mtu huo mbele yao imekuwa ni kama kitu cha kushangaza sana. Mfalme aligeuka na kumtazama Alie huku akishuka chini kupiga magoti.
"Naomba tusamehe sana Alie kwa kile tulichokifanya, ni muda mrefu umepita na sada tumejisafisha na kiwa na moyo wa upendo. Tusamehe sana kwakweli na tunaomba usifanye baya kwetu."aliongea Mfalme Yazid na kumshawishi hata Malkia naye ashuke chini kupiga magoti.
Alie aliwatazama tu huku akitabasamu japo moyoni ana maumivu dhidi ya watu hao. Alibadilika gafla na kuonekana mwenye hasira sana huku akisimama.
"Siwezi kuwaacha watu ambao mmedhurumu maisha yangu kirahisi, leo nahakikisha wote nawamaliza kwa mikono yangu iwe ni malipizo kama vile mlivyoua kwa ukatili."alisema Alie na kunyanyuka akanyoosha mkono wake pembeni kukatokea upanga mrefu wenye kun'gaa na kuwafanya hata viongozi hao waliopiga magoti pale chini washangae kuona miujiza hiyo. Aliunyanyua upanga wake na kuuweka shingoni mwa Malkia na kuwafanya wote waanze kuomba samahani mfululizo huku wakianza kutoa machozi.
"Tusamehe sana Alie, tumekosa kweli na ndio maana tunaomba samahani kwasasa, tunaomba utusamehe."alisema Malkia huku akitetemeka kwa woga.
"Alie naomba tusamehe kwakweli tuamini tumebadilika sio kama zamani. Tutakupa chochote unachotaka lakini usitudhuru wala kutukatia uhai."aliomba Mfalme huku akionesha huruma.
"Kama unaogopa na kuthamini uhai wako kwanini uliniua bila huruma, bila kujali utu wangu, kwa umri nilionao na hamkuwa na sura ya huruma hata kidogo na mlichokita kikatimia. Hadi nipo hapa nimetumia akili yangu kufika huku, mnajua ninachotaka kukifanya sasa!.."aliongea Alie na bila huruma alipitisha upanga mkali kwenye shingo ya Malkia na kufanya papo hapo adondoke chini kama zigo. Mfalme alishangaa kuona tukio lile kwa macho yake akashikwa butwaa. Haraka akaanza kutambaa kwa magoti pale chini kumsogelea mkewe aliyekuwa anatapatapa pale chini huku damu zikitapakaa pale chini. Alijikuta akidondosha machozi huku akishuhudia mkewe taratibu akianza kukata roho na muda mfupi tu hakuwa tena na uhai wa kuendelea kuishi duniani.
Alie alinyanya upanga kwake na kumuwekea Mfalme kwenye shingo yake kuonesha anayefuata ni yeye. Mfalme alishtuka sana kuona hivyo, uoga ulimjaa akifikiria muda mfupi tu ameshuhudia kifo cha mkewe akiuawa bila huruma na msichana huyo.
"Tafadhari Alie naomba sana usiniue, naomba usifanye hivyo nitakupa chochote utakacho nipo radhi kwa lolote lile niachhhhie... niache roho yangu naomba sana..!"aliongea kwa woga Mfalme huku panga kali likiwa shingoni mwake. Alie alimtazama Mfalme akionekana mwenye hasira sana.
"Nitakuacha kama utaniahidi kufanya hiki ninachokitaka hapa."alisema Alie huku akimtazama Mfalme aliyekuwa mpole akimsikiliza kwa makini.
"Nahitaji kitabu cha Lutfia hapa nikipate, endapo ukafanikiwa kukipata na kuniletea basi nitakuacha ukiwa hai ila.. kama litaingia giza siku hii ya leo basi tambua utamfuata mkeo huku alipokwenda maana bado ninahasira nanyi. Ni masaa mawili tu yamesalia kuzama kwa jua."alisema Alie na kumfanya Mfalme aitikie kwa haraka na kumhakikishia kwamba kazi hiyo ataifanya kabla ya jua kuzama.
Alie alitoa upanga wake kwenye shingo ya Mfalme na kumuacha huru kwa muda akafanye kile ambacho anakihitaji. Aliondoka pale Mfalme huku akiuangalia mwili wa Malkia ukiwa pale chini huku damu zikitapakaa. Hakutaka kuchelewa haraka akaanza kuondoka kurudi kwenye falme kwanza kujua kinachoendelea maana mara ya mwisho alitoa amri kwa kamanda mkuu amkamate Lutfia na aliamini wanaweza kumpata na ndio akajiaminisha kwa Alie kuwa kazi hiyo ataifanya. Hakujua kinachoendelea ndani ya kitabu kile ambacho kaagizwa akichukue mikononi mwa Lutfia.

Huku upande wa pili Lutfia pamoja na Saadie walifika eneo la mashambulio baina ya askari wa Mfalme pamoja na wale askari waliokuja na Malkia Kasma wakionekana kuwa na uwezo mkubwa japo kwa uchache wao walifanikiwa kuwaua askari wengi sana wa Mfalme Yazid. Hakutaka kuchelewa Lutfia kwa uwezo alionao alisogea katikati yao na kukumbana na askari mmoja wa Kasma, alinyanyua mikono yake iliyoonekana kujinjenga kama moto asili ya duara na kuachia nguvu hizo kuelekea kwa askari huyo ambaye alirushwa umbali mrefu sana na kupoteza maisha. Watu walioshuhudia pigo hulo walishikwa na butwaa huku wengine wakiacha hata kupambana wakimtazama Lutfua kwa kile alichokifanya. Haikuwa rahisi kwa binti mdogo kama huyo kuweza kufanya kitu kikubwa kiasi hicho. Shambulio hilo likawapa nguvu mpya askari wa Mfalme Yazid wakaanza upya kupambana na askari wale wachache. Saadie naye hakuwa nyuma alitumia nguvu zile alizopewa na Lutfia kuwapunguza wale askari ambao wamefanikiwa kuua askari wa taifa la Maskoof. Askari hao walipoona wanazidiwa upande wao wakapeana tu ishara ya kurudi nyuma maana ujio wa Lutfia pamoja na mtoto wa Mfalme umewafanya washindwe kuendelea kuwaangusha chini askari wa Maskoof.

Mfalme Yazidi alifika katika falme yake na kushudia watu wengi wakiwa wamepoteza maisha huku kwa mbali akisikia sauti za mapanga zikisikika kumaanisha vita bado inaendelea. Aliona kitu cha muhimu ni kupita nyuma aweze kuingia ndani ya jengo hilo bila ya kupitia kwa mbele ambapo vita hiyo ikikuwa ikipamba moto. Kamanda mkuu aliweza kufika kwenye chumba cha Mfalme akiwa na vijana wake waliomdhibiti Kasma aliyefungwa kila sehemu hadi mdomo wake kwa kamba iliyomzuia kuweza kuongea kabisa maana ni muda mfupi ametoka kurudisha fahamu zake baada ya kupuliziwa unga ule uliomlewesha kwa muda. Walifika na kuona chumba kikiwa cheupe kabisa hali iliyomfanya Kamanda ashangae maana ndio Mfalme na Malkia walihifadhiwa humo ili vita iishe kwanza ndio viongozi hao wapate kuwa salama. Ilibidi sasa atoke yeye mwenye kuanza kupekuwa kila chumba kujua wapi wamekimbilia viongozi wake. Hata alipotoka tubalipata kuonana uso kwa uso na Mfalme akiwa anakuja. Haraka akamkimbilia hadi alipomfikia na kutoa heshima.
"Nimekuwa nakuangalia huku sikuweza kuwaona mlienda wapi na Malkia wakati niliwaambia msitoke popote?aliongea Kamanda huyo huku akimtazama Mfalme aliyeonekana kuhema.
"Vipi mmempata Lutfia?"ni swali la kwanza ambalo Mfalme aliuliza bila kutaka lolote. Kamanda alisimama vizuri na kumuaminisha Mfalme kuwa wamemkamata Lutfia na yupo chumbani kwa Mfalme. Maelezo hayo yalimfanya Mfalme kidogo apate kutulia maana amefanikisha nusu ya kile alichoagizwa. Haraka akaanza kupiga hatua kueleke kule kwake akitaka kumuona mhusika mwenyewe.

Hata walipofika alisogezwa Kasma pale mbele ya Mfalme aliyeonekana kitabasamu tu wakidhani wote mtu yule ni Lutfia kwa jinsi walivyofanana. Taratibu akamsogelea hadi pale alipo Kasma aliyewekwa kwenye kiti kidogo naye akasogeza kiti na kukaa.
"Nina muda mchache usiokuwa na huruma ya kukusubiri wewe. Kwasasa siangalii jinsi ulivyonidanganya kuwa wewe ni mwema na kuweka ukaribu na binti yangu, sitajali umewatuma na wenzako sasa wamekuja kuiharibu Maskoof yangu na kuua askari wangu wengi ambayo ilikuwa ya amani. Nahitaji unambie jambo moja tu kwasasa... kile kitabu ulichokishika muda wote kipo wapi?"aliuliza Mfalme huku akimtazama Kasma akiwa amefungwa kamba mdomoni akijitahidi kuongea bila kusikika. Ilibidi atoe amri afunguliwe mdomo tu maana wanajua fika ni Lutfia hivyo ana nguvu za kipekee. Walimtoa ile kamba na kumacha huru aweze kujibu maswali anayoulizwa.
"Sio mimi, mimi sio Lutfia mnayemdh..."alipigwa kofi zito hadi akadondoka chini na kiti alichokalia. Askari wawili walisogea na kumnyanyua kumkalisha tena sawiya huku safari hii akivuja damu mdomoni kwa uzito wa kofi lile.
"Sina matani mimi nina muda mchache wa kukuuliza unijibu. Kipo wapi kile kitabu!!?"alifoka kwa hasira Mfalme bila kujua anayemuuliza siye.
"Nieleweni jamani mimi sio Lutfia, mimi naitwa Kasma tumefanana tu jamani na sijui kitabu kipo wapi."aliongea Kasma na kumfanya Mfalme amtazame Kasma usoni. Baadhi ya askari walipatwa na hasira akiwemo Kamanda mkuu kwa kile asemacho Kasma wakidhani anawatania bado.
Mfalme alinyanyuka akiwa mwenye jazma na hasira ndani yake, akaomba upanga kwa Kamanda naye akampatia. Aliona bora afanye kile ambacho anaona ni sahihi maana binti huyo kama anamchezea wakati amepewa muda mchache wa kukamilisha kile ambacho anatakiwa amkabidhi Alie ili apate kunusuru uhai wake.

LUTKAS SEHEMU YA 20


# ILIPOISHIA

Aliona bora afanye kile ambacho anaona ni sahihi maana binti huyo kama anamchezea wakati amepewa muda mchache wa kukamilisha kile ambacho anatakiwa amkabidhi Alie ili apate kunusuru uhai wake.

# TUENDELEE
Kasma alishuhudia tu panga lile likiwa mikononi mwa Mfalme likiwekwa sawa ili litue sehemu moja katika mwili wake. Alianza kufurukuta pale kujinusuru kwa askari wale waliomshika barabara lakini haikuwa rahisi maana walihakikisha hadi Mfalme amalize jambo lake.
Mfalme alinyanyua upanga ule ulio mkali huku Kasma akiutazama kwa makini naye akijiandaa kufanya jambo asije kupoteza maisha kweli japo hayupo sawa maana unga ule aliomwagiwa ulimdhuru. Punde tu akatokea Saadie na kushuhudia baba yake akitaka kufanya mauaji hayo. Alipiga ukelele wa nguvu kumuita baba yake ambaye alishusha upanga ule kuelekea kwa Kasma lakini haukumfikia baada ya kusikia sauti ya binti yake huyo. Aligeuka nyuma haraka baada ya kumsikia Saadie ambaye walikuwa wakimsubiri na kupatwa na hofu juu ya binti yao huo. Alijiwa na moyo wa ubinafamu na kugeuka kabisa kumtazama binti yake kule alipo. Lakini akikumbuka kile alichoagizwa na Alie aliirudisha ile roho ya kufanya mauaji kwa Kasma akijua ndiye Lutfia ambaye anahitajika auawe endapo hataeleza ukweli wapi alipokiweka kitabu hicho.
"Unataka kufanya nini baba yangu? Kwani bado tu unadhambi hii unayoifanya kila siku na hubadiliki?"alionhea Saadie kwa uchungu huku akimtazama baba yake.
"Huwezi kunipangia maaamuzi yangu Saadie? Huyu sio mtu mwema kwako, yupo na wenzake ndio aliyeungana nao kuivunja falme yetu. Siwezi kumuacha akiwa hai huyu ni kifo tu kitakachofuata endapo hutoniambia ukweli wapi kilipo kile kitabu."alisema Mfalme akionekana kuwa na hasira. Saadie alipata kutambua kile ambacho kinaendelea hapo. Ilibidi amueleze hali halisi kuhusiana na kile ambacho kinaendelea baina ya Kasma pamoja na Lutfia.
"Huyo aliyeko karibu yako sio Lutfia unayemdhani wewe, huyo hajui hata kinachoendelea dhidi yetu. Huyu ndiye mtu aliyekuja na hawa watu wengine ambao wametuvamia."alisema Saadie na kumfanya baba'ke akumbuke ni muda mfupi Kasma amekuwa akijitetea ili asiuawe.
"Unataka kuniambia huyu sio Lutfia?"aliuliza Mfalme akiwa anashangaa baada ya kusikia maneno ya mwanaye.
"Huo ndio ukweli, huyu siye, Lutfia yupo nje anajaribu kuwazuia maadui waliovamia falme yetu."alisema Saadie akizidi kumchanganya Mfalme ambaye hakutaka kuamini maneno hayo kwa haraka. Alipiga hatua hadi dirishani kuangalia kule nje na kuona mapambano yakiendelea baina na askari wake na askari wa Malkia Kasma. Na hapo ndipo aliweza kumuona Lutfia akiwa anatumia nguvu zake kuwashambulia adui zake. Alibaki kushangaa kuona hivyo maana haamini anachokiona. Alirudisha macho yake kumtazama Kasma akiwa pale ameshikiliwa na askari wake na kuona ni vilevile alivyo Lutfia. Alishusha pumzi baada ya kujiridhisha kiwa watu hawa wapo wawili na taratibu akarejea pale alipo Kasma.
"Sasa wewe ni nani na mmefuata nini katika ufalme wangu?"aliuliza Mfalme akiwa anamtazama Kasma pale chini.
Alinyanyua uso wake Kasma kumtazama Mfalme akiwa anamkodolea macho muda wote.
"Nimefuata kitabu tu na sina kingine nilichofuata, hicho tu ndiyo nilichokifuata."alisema Kasma akiwa mwenye kujiamini sana.
"Kitabu..! Kitabu gani hicho?"
"Lutkas.... Nimefuata kitabu hicho, kitabu cha Uhai na ndio maana nimethubutu kuingia hadi humu kwaajili hiyo."alisema Kasma akiwa anamtazama Mfalme kwa macho makavu. Ilibidi Mfalme amsogelee kwanza na kushuka chini kuwa sawa na Kasma.
"Hebu niambie, hicho kitabu kina umuhimu gani hasa hadi udiriki kuja hadi huku na hawa wenzako."
"Mimi natokea taifa la mbali sana, tena mbali na hapa Maskoof. Mimi ndiye Malkia wa Taifa letu, hivyo kitu muhimu ambacho lazima tukimiliki katika taifa letu basi ni wajibu wangu nami kushiriki nitoe jashi langu hadi kukipata. Hivyo suala la kuja huku ni wajibu wangu na ndio maana nipo hapa baada ya kufahamu kuwa Lutfia ndio mwenye kitabu hicho. Ni zaidi ya zawadi yeyote hapa duniani. Lutkas kina mambo mengu sana ndani yake ambayo ni wachache tu ambao wanaweza kukimiliki na kukielewa wakafaidika nacho. Ila moja ya kitu pekee ambacho kila mmoja wa viongozi angependa kuwa na Lutkas ni vile kilovyo na uwezo wa kuwarudisha watu waliokwisha kufa muda mrefu. Na pindi wakirudi basi huwa chini yako na kufuata kila kitu ambacho unaamua nini kifanyike. Hii ni zaidi ya silaha kubwa sana kwa kila kiongozi ambaye anahitaji kuwa na jeshi kibwa la watu."alisema Kasma na kuongea mambo mengi sana ambayo Mfalme hakuweza kuyafahamu hapo awali. Saadie alibaki kusikiliza tu yanayozungumzwa na kuona ndio yaleyale ambayo ameweza kuelezwa na Lutfia.

Kwa maelezo hayo Mfalme akafahamu sasa umuhimu wa kitabu kile ambacho muda wote Lutfia amekuwa akitembea nacho. Alisimama na kugeuka nyuma kisha akarudi tena pale dirishani kumuangalia Lutfia kile nje akizidi kuwalunguza wale watu waliovamia Falme hiyo. Alijikuta akitabasamu tu baada ya kujua kumbe kitabu kile kina umuhimu sana. Alitambua kuwa ndio sababu ya Alie kumtuma yeye akakichukue kitabu kile kwa Lutfia amkabidhi.
"Kama Alie alikufa na amerejea, na sasa anahitaji hiki kitabu anamaana gani? Au anataka naye kuwa na jeshi lake? Ili iweje sasa? Au anataka kutumia njia hii kuuangusha utawala wangu hapa Maskoof? Mmh hapana hapa nahisi najichochelea kuni endapo nikipeleka kitabu hicho kwake. Alie hawezi kuwa mwema kwangu hata kama nikimpatia kitabu, kama ameweza kumuua mkewangu si rahisi akaniacha mimi hai."alijikuta Mfalme akiyafikiria hayo moyoni mwake huku macho yake yakiangalia jinsi Lutfia kule nje anavyomwaga damu. Taratibu chozi likaanza kumdondoka baada ya kukumbuka kuwa amemppteza mke wake kipenzi lakini alijikaza na kujifuta. Saadie alipata kuliona hilo lakini hakujua sababu za baba yake kutokwa na machozi hivyo. Alihisi huenda baba yake akawa anamfikiria vibaya tena Lutfia.
Hakutaka kuendelea kukaa ndani tena naye akatoka nje kuelekea kwenye uwanja wa vita kuungana na mwenzake. Hata alipoingia tu alitumia ule uwezo alionao kupambana na adui zake. Kitendo kile kilimfanya hata Mfalme Yazid astaajabu pale dirishani kumuona binti yake akitumia nyuvu za kichawi kuwadhibiti adui zake. Hata baadhi ya askari wa kifalme walishangaa kuona tukio hilo ambalo hawakutegemea kabisa kama binti wa kifalme angeweza kupambana kwa nguvu zile za ajabu. Lutfia alimshangaa Saadie kwa kile anachokifanya maana hakutaka binti huyo aonekane mapema kama anauwezo huo.

Wakati yote hayo yakiendelea Alie alikuwa sehemu anatazama tu na kujidhihirishia kwa macho yake mawili kila kitu kinachoendelea.
"Huyu mpumbavu ameshashikwa akili tena, sidhani kama atalekileta kitabu kwangu."aliongea Alie akimtazama Mfalme akiwa ndani ya falme anachungulia tu nje kumtazama binti yake katikati ya uwanja wa vita. Hakutaka kuendelea kukaa pale Alie aliamua kuondoka zake kabisa baada ya kuona hakuna dalili za Mfalme kuweza kuleta kile kitabu tena.

Baada ya muda mchache wale maadui waliovamia falme walisambaratishwa wote bila huruma. Hali iliyofanya askari wa kifalme wafurahi baada ya kumaliza vita hiyo na kupata ushindi kwa kuwadhibiti adui zao wote. Saadie alimsogelea Lutfia hadi pale alipo.
"Kasma amekamatwa yupo mikononi mwa baba, nahisi hatakuwa katika mikono salama maana ndiye mtu ambaye amekuja na hawa watu waliovamia falme. Tunamsaidiaje sasa?"aliongea Saadie akiwa anatokwa na jasho kwa kazi waliyoifanya.
Lutfia baada ya kuambiwa hivyo hakutaka kusimama tena alianza kupiga hatua kuelekea ndani huku Saadie naye akimfuata.

Alie alifika sehemu akapumzika kwanza ili atafute namna ya kuendeleza vita hii. Lengo lake hasa ni kuhakikisha anaondoka Maskoof akiwa na kitabu cha Lutkas. Alikumbuka aliwatuma wenzake kule katika falme ya Malkia Kasma waende kuvamia ili huku wao wakirudi wakute mambo yamebadilika. Ilibidi awasiliane na wenzake kwa hisia za nguvu walizonazo huko kujua kinachoendelea.
"Imekuwaje huko mlipo nini kinaendelea?"aluiliza Alie akiwa amefumba macho yake akiweka umakini wa kusikiliza.
"Tumefanikiwa kuingia kwenye falme na kupambania na majeshi yao. Hapa tunapoongea baadhi ya askari wameshusha silaha zao chini kukubali kushindwa, hivyo wamekuwa ni mateka kwetu."alisikika mmoja wa watu wa Alie waliokuwa kule kwenye falme. Kauli ile ilimpa faraja sana Alie kusikia wenzake wamelifanikisha zoezi hilo hivyo kazi imebaki kwake huku alipo kukamilisha kuipata Lutkas.
"Sawa hakikisheni kila kitu kimekuwa chini ya mikono yetu, huku kuna kazi moja nataka kuifanya naamini nitafanikiwa kabla ya jioni ya leo."alisema Alie akimueleza kijana wake aliyekuwa aliongea naye na mwishowe wakakata mawasilianao hayo baada ya kuelewana. Alijikuta akipata hata nguvu ya kuendelea na kazi yake mara baada ya kujua wenzake wamefaulu kile alichowaagiza wafanye.
Alinyanyuka pale alipokaa huku akiachia tabasamu.
"Hapa ni kuwachanganya tu tena sitakuwa na huruma na yeyote aliye mbele yangu. Lutkas itatua tu mikononi mwangu."alisema Alie na papo hapo akapotea

Baada ya muda kupita askari kadhaa walionekana kutembea taratibu huku wakiwa wameubeba mwili wa mtu kuuingiza ndani ya falme. Lutfia muda huo alikuwa na kazi moja tu ya kumfariji Saadie ambaye alikuwa akilia sana. Hii ni baada ya Mfalme kuwaeleza ukweli kuwa Malkia ameuawa katika harakati za kukimbia kuyanusuru maisha yao. Askari wote na baadi ya raia walikuwa kwenye wakati mgumu kila mtu akihuzunika kwa kile kilichotokea. Ulikiwa ni msiba wa taifa zima hakuna mtu ambaye aliweza kubaki ndani siku hiyo kila mtu alitoka na kuelekea kwenye uwanja wa makutano kama ilivyo ada. Watu walifurika uwanjani kila mtu akiwa analia kwa majonzi. Iliandaliwa sehemu maalumu ya kuupumzisha mwili wa Malkia mulemule kwenye uwanja ule, askari walikuwa washapu sana hata dakika kadhaa zilipotimia kazi hiyo ilikamilika. Mfalme alikuwa tu ndani karibu na jeneza ambalo mkewe amehifadhiwa humo. Alibaki kumtazama tu akionekana kufumbwa macho yake huku mashada na maua yakitanda kwenye jeneza hilo. Muda mfupi waliingia askari kadhaa wakiongozwa na kamanda mkuu wakimtaka Mfalme anyanyuke kusdi wautoe mwili wa Malkia ukapate kupumzika. Ilikuwa ngumu kwa Mfalme lakini hakuwa na jinsi, ilimbidi Kamanda mkuu amsogelee na kumsaidia Mfalme kunyanyuka pale kisha askari wake wakasogea kulinyanyua jeneza hilo na kuanza kutoka nalo nje kwenda moja kwa moja kwenye uwanja. Saadie na Lutfia walikuwa wamekaa sehemu maalumu ya wanafamilia na kushuhudia askari wakiwa wameubeba mwili wa Malkia kuusogeza hadi kwenye sehemu iliyoandaliwa. Alifika Mfalme naye na kukaa karinu na mwanaye.
Taratibu zote zikaendelea na muda wa kwenda kuuaga mwili ulipofika familia ilisogea hadi pale kwenye uwanja na kutoa heshima ya mwisho. Saadie alilia sana pale alipofahamu kuwa ndio mara ya mwisho kumwona mama yake, ilikuwa kazi kwa Lutfia kuweza kumzuia mwenzake aliyeonekana kuumia zaidi ya wote. Raia wote walibaki kulia tu hakuna aliyeweza kuzuia hisia zake.
Baada ya zoezi hilo kwisha taratibu askari waliushusha mwili wa Malkia ndani ya kaburi na kuanza kufikia.
Kitendo cha kufukia tu jeneza hilo Lutfia akapata kusikia kicheko cha mtu akicheka kwa sauti sana. Sauti ambayo Saadie pamoja na Kasma aliyefungwa kwenye gereza ndani ya falme hiyo ashtuke akiwa zake amejilaza. Ilibidi anyanyuke na kusogea hadi kwenye nondo akapata kumuona askari akiwa amesimama kumlinda. Saadie na Lutfia pale uwanjani waligeuka huku na kule kupata kujua sauti ile inapotokea. Katika kutafuta huko Lutfia alipata kumuona Alie akiwa amejichanganya na raia wakiwa wamesimama kama heshima ya kumuaga Malkia. Ni yeye ndio alikuwa akitoa kicheko hiko chenye dharau na kebehi ndani yake. Hakuna myu yeyote aliyeweza kusikia zaidi yao. Saadie naye aliweza kumuona mtu huyo na kufahamu huenda ndiye aliyesababisha kifo cha mama yake. Alipandwa na hasira hata macho yake kuweza kubadilika na kutaka kumfuata kulekule alipo lakini Lutfia akamshika mkono.
"Si muda wake wa kufanya hivi, hebu mpe heshima mama yako tumuache apumzike salama kwanza na haya mengine yatafuata."alisema Lutfia na maneno yake yakamfanya Saadie taratibu arudi katika hali yake ya kawaida. Waligeuka na kutoa heshima ya mwisho kwa Malkia ili apate kupumzika salama.
Kule alipo Kasma alishikwa na hasira sana baada ya kufahamu huyo mtu ndiye aliyejichanganya nao hadi kuja huku Maskoof kumbe alikuja kwa manufaa yake binafsi. Alitamani atoke mule ndani akakutane naye ana kwa ana huenda akamaliza hasira zake.

LUTKAS SEHEMU YA 21


#ILIPOISHIA

Kule alipo Kasma alishikwa na hasira sana baada ya kufahamu huyo mtu ndiye aliyejichanganya nao hadi kuja huku Maskoof kumbe alikuja kwa manufaa yake binafsi. Alitamani atoke mule ndani akakutane naye ana kwa ana huenda akamaliza hasira zake.

#TUENDELEE
Taratibu za mazishi zilienda kama ilivyopangwa hadi kukamilika na kila mtu akarudi kwake japo majonzi yalitawala kwa kila mtu. Baada ya muda kupita uwanja ulikuwa mweupe kabisa kila mtu aliondoka zake usiku ule. Lakini Mfalme alikuwa amesimama tu pembeni ya kaburi lile la mkewe akilitazama. Hakika alikuwa anampenda sana na hata kifo chake hicho hakuweza kuamini kama na kuhisi huenda ni kama mchezo wa kuigiza tu hivyo alisimama kusubiri kama Malkia ataweza kunyanyuka tena.
Alikumbuka jinsi Alie alivyopitisha upanga wake mkali kwenye shingo ya Malkia na kumsababishia hadi kupoteza uhai wake. Alijikuta akienda chini taratibu na kupiga magoti kabisa, nafsi ikaanza kumsuta pale alipokumbuka matukio ya nyuma aliyofanya. Hakika alikuwa hana huruma Mfale hata kidogo. Kwake kuua ilikuwa ni kama kunywa maji hakuona ugumu wowote wa kufanya hivyo. Siku zote damu ya mtu inadai na ndivyo ilivyotokea kwa upande wake. Kifo cha Malkia aliona kama yeye ndio sababu japo hadi muda huo haamini kile anachokiona. Alikaa na kutafakari lakini jibu la mwisho katika kufikiri kwake ni hawa watu waliovamia falme ndio sababu. Alijikuta akipandwa na hasira juu ya binti Kasma na kuona ndiye mtu aliyesababisha haya kutokea.
Alitoka hapo na kuanza safari ya kuelekea kule alipohifadhiwa binti huyo.

Lutfia alikuwa huko akijaribu kuongea na Kasma aliyekuwa ndani ya gereza dogo lenye nondo kuukuu. Huku miguu yake ikifungwa minyororo ambayo iliacha hatua za yeye kitembea tu na hata akiachiwa huru asiweze kukimbia vizuri.
"Umeamua kipi hadi sasa, maana hakuna mtu wako yeyote aliyeweza kuwa hai mpaka dakika hii. Ni wewe tu ndio uliyebaki na sidhani kama Mfalme kwa msiba alioupata ataweza kukuacha salama."alisema Lutfia akiwa anamtazama Kasma aliyeshikilia nondo.
"Na vipi kuhusu huyo mtu aliyejichanganya nasi ili aje huku Maskoof.?"aliuliza Kasma.
"Anaitwa Alie, ni msichana wa makamo na alishakufa zamani, ila amepata uwezo wa kurudi tena kuwa hai lengo ni kukipata hichi kitabu."alisema Lutfia na kukitoa kitabu kile. Alijiamini na kuamua kumpatia Kasma aweze kukishika. Alikipokea kwa mikono miwili na kujikuta akibadilika hata macho yake huku nuru ikitanda kwenye kile kitabu kuashiria ni myu sahihi mwenye uwezo wa kukitumia kitabu kile. Hata yeye alijihisi faraja sana pindi alipoona hali hiyo, zikaanza kufunguka kurasa za kitabu kile na zilipotulia, Kasma alitazama sehemu iliyofunguka na kuona maelezo ndani ya kitabu kile akaweza kuyasoma. Alishtuka baada ya kutambua jambo haraka akamtazama Lutfia.
"Nilichokiona ni kweli au! Yaani... Hapana kwakweli haiwezi kuwa hivyo kirahisi."alijikuta akipagawa Kasma baada ya kusoma maelezo yaliyo kwenye kitabu kile.
"Huo ndio ukweli Kasma, Lutkas hata siku moja haidanganyi, hata mimi nimepata kusoma hiyo habari, ni ukweli kuwa ufalme wako kwasasa haupo tena. Ni huyu Alie ndio aliyefanya haya yote, kipindi mnapanga safari ya kuja huku yeye aliwaandaa wafu wenzake waweze kuvamia taifa lako, na ndio walichokifanya na wamefanikiwa. Kwasasa wao ndio wanatawala falme yako hivyo kuna kazi ya kurudisha heshima yako kama Malkia."alisema Lutfia na maelezo yake yalimfanya Kasma aamini kweli huyu ni mtu sahihi asiye na shaka ndani yake. Alishusha pumzi kidogo kisha akakirudisha kitabu kile kwa Lutfia.
"Kiukweli sijielewi hadi sasa Lutfia, mimi si wa kufungwa minyororo hii halafu nishindwe kujitetea. Wamenitupia unga ambao umenimaliza kabisa nguvu zangu na sielewi hapa natokaje, naomba nisaidie niweze kutoka hapa nikaitete ardhi yangu. Watu wangu wapo kwenye hali mbaya."alisema Kasma akiomba msaada kwa Lutfia.
Walibaki kutazama kwa muda kila mtu akimtazama mwenzake na kuona hawana utofauti wowote.
"Naomba nihakikishie kama utakuwa nami muda wote, huyu Alie ni wa kumdhibiti ili haya yote anayotaka yasifanimiwe."aliongea Lutfia na kunyoosha mkono wake kumpa Kasma ambaye alibaki kumtazama Lutfia. Aliukamata mkono huo na kukubaliana naye.
"Hakika sitaruhusu kupoteza taifa langu kwa huyu shetani mmoja,nipo pamoja nawewe, na nisamehe kwa kuwa awali sikujua ukweli wa haya yote."alisema Kasma na maneno yake yakamfanya Lutfia akubaliane naye.
Alielekeza mbele kitabu kile na wote wakakishika kwa mikono yote,nuru ilianza kuangaza kutoka kwenye kitabu kile na kuanza kuingia kwenye mwili wa Kasma. Muda huohuo Mfalme ndio alikuwa akifika eneo hilo na kukutana na tukio lililo mbele yake. Alishindwa kuelewa mapema kinachoendelea, alibaki kutazama kile aonacho mbele yake akishuhudia wawili hao wakifanya jambo kwa pamoja. Jambo lile lilimchanganya Mfalme ashindwe kuelewa nini afanye.
"Lutfia.. nini unafanya?"aliongea Mfalme kwa sauti isiyo na nguvu sana. Lutfia aligeuka kumtazama Mfalme akiwa mwenye kutisha macho yake, safari hii hakutaka kuficha lolote mbele ya Mfalme ambaye baada ya kumuona binti hiyo akiwa kwenye hali ile hata upanga aliyoushika ulimdondoka kwa woga maana macho yake yalitisha sana.
"Usiogope Mfalme wangu. Hakuna kibaya chochote ambacho kinaendelea hapa."alisema Lutfia huku Mfalme alimtazama Kasma naye akiwa kama vile alivyo mwenzake. Alibaki kumeza mate tu haamini kile anachokiona.
Waliendelea na zoezi lao hadi hapo walipomaliza na kurudi katika hali zao za kawaida kama binadamu. Lutfia aligeuka na kumsogelea Mfalme aliyekuwa mwenye woga.
"Wewe utabaki kuwa Mfalme tu na mmiliki halali wa falme hii. Kitu pekee ambacho sasa wapaswa uwe nacho ni ujasiri, maamuzi na wema kwa raia wako naamini kila mmoja atakupenda katika hili taifa."aliongea Lutfia na punde tu Kasma akapata kuonekana akitoka kwenye lile gereza huku mikono na miguu yake ikiwa huru kabisa hapakuonekana mnyororo wowote jambo ambalo lilimshangaza hata Mfalme. Alisogea hadi pale walipo na kumfuata Mfalme wakawa wanatazamana.
"Nadhani utakuwa na hasira dhidi yangu kwa maana ndiye mtu pekee niliyetoa jeshi kuja huku kuvamia, kusababisha watu wako wapoteze maisha akiwemo Malkia na kikubwa ni kuja na mbaya ambaye hakupaswa kukanyaga ardhi hii. Awali sikuwa na uwezo wa kumtambua mbaya ndio maana akaweza kuchanganyika nasi hadi huku. Ila kwasasa tuna nia moja ya kumdhibiti. Tutamtafuta popote alipo kumdhibiti arudi alipotoka. Ila nisamehe sana kwa upande wangu."alisema Kasma na maneno yake pamoja na umri alio nao Mfalme alijikuta hata zile hasira zake zinapotea hewani. Aliwatazama mabinti wale wenye kufanana kila kitu na kuona jinsi walivyo wema kweli.
"Ulinipa kazi ya kumlinda Saadie na kuhakikisha hapotezi furaha yake. Nami ndio nalifanya hilo japo kuna tukio ambalo limemuumiza sana moyo hata wewe, kifo cha Malkia wa Maskoof."alisema Lutfia huku akimtazama Mfalme, taratibu akakitoa kile kitabu cha Lutkas na kumsogelea Mfalme akamshika mkono.
"Naanza kufanya kazi kupitia kitabu hiki ndani ya ardhi hii ya Maskoof. Malkia hakupaswa kufa kifo kama kile tena na mtu asiyestahili. Nakwenda kumpa furaha tena Saadie na hata taifa zima japo wanapaswa kutoogopa."alisema Lutfia na maneno yake yakamuacha njia panda kiongozi huyo.
"U... una.. unamaana gani kusema hivyo.?"alijikuta kupatwa na kigugumizi lakini hakuweza kujibiwa tena. Alishuhudia kumuona Lutfia akiondoka zake kwenda nje jioni ile kiza kikianza kuchukua nafasi yake. Kasma naye alifuata kuelekea nje wakimwacha Mfalme pale asielewe maana yao. Hakutaka kupitwa na kitu naye akageuka kuanza kuwafuata wawili hao na kuona wakielekea kule uwanjani kabisa. Askari wengi walikuwa wakikusanya wenzao ambao wamejetuhiwa na vita ile na wengine kupoteza kabisa maisha.

Askari waliokuwa wakilinda eneo hiko walipowaona tu Lutfia na Kasma walitaka kuweka ulinzi zaidi lakini alifika Mfalme na kuamuru mabinti hao walite bila kuguswa. Walipata nafasi hiyo hadi kuelekea karibu kabisa na kaburi la Malkia na Lutfia akaweza kukifunua kile kitabu na kukuweka juu ya kaburi. Saadie kule chumbani alipo alishtuka na kuhisi tofauti. Alitazama pembeni yake bila kuona mtu yeyote, taratibu akaanza kushuka kutoka chumbani kwake na kuanza kutafuta kujua kinachoendelea.
Mfalme alikua akitazama tu bila kuelewa, alikuwa makini kumtazama Lutfia akiwa pale karibu na kaburi la Malkia. Taratibu akaanza kubadilika sura hata macho yake na kuonekana mwenye kutisha sana huku akisema maneno ambayo hayakuweza kueleweka kwa lugha ya kawaida. Saadie alifika kule uwanjani na kukutana na tukio hilo likiendelea, awali hakujua kunachoendelea lakini aliposogea karibu alipata kuelewa kile ambacho Lutfia anakifanya muda huo. Aligeuka kumtazama baba yake ambaye alikuwa makini kuangalia kinachofanywa na binti Lutfia.
Punde tu lile kaburi likaanza kutokwa na nyufa ambazo kila sekunde ziliongezeka na kujenga uwazi mkubwa sana. Kwa pamoja walipata kushuhudia mwili wa Malkia ukinyanyuka kutoka pale kaburini tena bila kuchafuka udongo wala mchanga utokao pale. Mfalme Yazid alitoa macho kishangaa kile ambacho anakiona mbele yake, akabami kufumba mdomo tu haamini tukio lile ambalo amelishuhudia kwa macho yake. Saadie alibaki kushangaa kuweza kumwona mama yake tena, alijikuta akitokwa machozi ya furaha maana hakutegemea kama ingelitokea hilo.
Ilimbidi Lutfia akamate kitabu kile na kumsogelea Malkia ambaye hakuonesha dalili zozote za kutambua wapi alipo muda huo. Aliikamata mikono ya Malkia na kumshikisha kwenye kitabu cha LUTKAS huku akiendelea kuomba. Muda huo Kasma aliutumia kumsogelea Mfalme pale aliposimama.
"Hupaswi kuonesha dalili zozote za kutokea kwa msiba wa Malkia, tambua kwamba bado yupo hai hivyo jaribu kusahau kuhusu msiba wake."alisema Kasma akijaribu kumuweka kwanza sawa Mfalme ili aioneshe woga kwa Malkia hapo baadae. Ilibidi akubaliane nao na kuona hali ile ni ya kawaida. Alifanya hivyo hata kwa Saadie kumueleza swala hilo naye hakuwa na shaka juu ya hilo.
Muda mfupi tu Lutfia alikitoa kitabu kile mikononi mwa Malkia na papohapo Malkia akashtuka na kujiona yupo pale usiku ule. Alitazama sehemu ile na kuona ni uwanjani ambao ni sehemu ambayo huja watu kwa matukio maalumu. Aliwatazama watu waliopo pale na kuona ni walewale muhimu kwake, alipomtazama mumewe alijikuta akimsogelea hadi pale na kumshika mikono miwili. Mfalme akajitahidi kutoleta tofauti yeyote ili tu mkewe asielewe kinachoendelea.
"Imekuwaje mbona mpo hapa usiku huu kuna tatizo?"aliuliza Malkia akiwa anamtazama Mfalme. Haraka Lutfia akasambaratisha lile kaburi na sehemu ile ikarudi kama mwanzo ili kufuta ushahidi wa kifo chake.
"Aam. Eeh, nanihii. Tupoo..."
"Mfalme ametupa adhabu ya kukaa hapa uwanjani na baridi hili hadi asubuhi kwakuwa nimemleta na ndugu yangu katika falme yake hivyo nilikosea maana hatukumjulisha kwamba ndugu yangu atakuja leo."alidakia Lutfia baada ya kuona Mfalme hana la kusema akajenga uongo wa hapohapo. Malkia aligeuka kumtazama Kasma na kuona jinsi alivyofanana kweli na Lutfia akapata kuamini ni kweli.
"Ninyi ni mapacha?"aliuliza Malkia akimsogelea Kasma na kumshika.
"Ndio.."alijibu Kasma na kufanya Malkia aamini kwa sura zao kufanana. Saadie kuona vile naye akajisogeza karibu na Lutfia ili kuwrka uzito wa uongo wao.
"Mama naomba utuombee kwa baba kwakuwa hatukumshirikisha kwa hili na atusamehe."aliongea Saadie huku akionesha kulia. Kilio cha furaha kwa kumuona tena mama yake ambaye alionekana hajui lolote ambalo limetokea katika falme hata vita iliyosababisha kifo chake.
Maneno yale yakamfanya Malkia amtazame binti yake kisha akageuka kumwangalia Mfalme.
"Hakuna haja ya kuendelea kuwatesa watoto usiku huu, kama tumempokea Lutfia kwa wema si vibaya hata ndugu yake akaishi hapa. Naomba mruhusu wawe naye pamoja."aliongea Malkia huku akimtazama Mfalme. Alibaki kumwangalia tu mkewe na kujikuta akitabasamu baada ya kuamini kweli mkewe amerudi kuwa mzima. Alikubaliana naye ili tu amridhishe akijua ni mbinu tu ya Lutfia, aligeuka na kurudi zake kwenye falme na Malkia akamshika mkono Saadie wakiongozana kwenda ndani. Kasma aligeuka kumtazama Lutfia akishusha pumzi kwa kile kilichofanyika maana si kazi ndogo kumrudisha Malkia tena duniani na kufuta kabisa matukio mabaya yalimsababishia kifo chake na hata kumuaminisha kwa uongo ule walioutumia.

LUTKAS SEHEMU YA 22


# ILIPOISHIA

Kasma aligeuka kumtazama Lutfia akishusha pumzi kwa kile kilichofanyika maana si kazi ndogo kumrudisha Malkia tena duniani na kufuta kabisa matukio mabaya yalimsababishia kifo chake na hata kumuaminisha kwa uongo ule walioutumia.

# TUENDELEE

Lutfia alijikuta anashusha pumzi kwanza na kukaa chini akifikiria kile kilichotokea muda mfupi. Alisogea Kasma hadi pale alipo mwenza.
"Nadhani hili tumelimaliza salama, nahitaji nirudi kuwahi taifa langu maana lipo katika hali mbaya. Na nahisi huyu Alie atakuwa kashafika tena huko akiona huku kashindwa kupata kile anachokitaka."alisema Kasma akimwelezea Lutfia.
"Hata mimi nilikuwa nafikiria swala hilo lakini hatupaswi kufanya kitu kwa kukurupuka. Alie ana mbinu nyingi za kutafuta kufanikiwa. Huenda akawa humuhumu Maskoof hivyo tukasema tuondoke kumbe tunamuachia Saadie na familia yake wakati mgumu."alise Lutfia.
"Halafu.. imekuwaje ukamuamini sana huyu binti hadi naye kuwa na uwezo ka alionao wewe.?"aliuliza Kasma.
"Yupo tofauti na mioyo ya wazazi wake na hata watu wa Maskoof. Yeye ndio alinitetea na kuniokoa nisiadhibiwe kifo mbele ya mikono ya baba yake. Nilipokaa naye na kuniambia hali halisi na hata mimi nikamtazama tu nikajiaminisha kile nilochokidhani kutoka kwake. Saadie ni mtu mwenye roho ya upendo sana kwa wenzake. Hapendi kuona mtu anadhurumu mtu haki yake na maanini atakuja kuwa kiongozi anayependwa na watu sana."alisema Lutfia akitoa sifa za Saadie kwa uchache aliokaa naye ameweza kumtambua. Waliongea mengi usiku huo lakini swala ambalo bado hawakulipatia jibu ni kuhusu uamuzi sahihi wa kuondoka au wabaki kwaajili ya mtu mmoja tu, Alie.

Kwa Alie alikuwa juu ya mlima mmoja akitazama mji wa Maskoof ukiwa unaonekana taa zikiwaka kwenye nyumba za raia. Jumba la kifalme likionekana kushamiri mwanga wa taa nyingi ndani ya vyumba. Alikuwa akipanga namna ya kurudi tena mule ndani kwa njia nyengine lengo likiwa ni kupata kitabu cha Lutkas. Alifunua nguo yake kutazama mkono wake wa kushoto na kuona ukianza kuharibika kuonekana kuoza. Alivuta pumzi na kuishusha baada ya kuona anaanza kupoteza uhalisia wake wa kuwa binadamu wa kawaida. Hali hiyo ilimfanya azidi kuongeza shauku ya kukitafuta kitabu hicho ili apate kurudi kuwa binadamu kamili.
"Nadhani Mfalme ameshindwa kutekeleza kile alichoniahidi kufanya. Ni muda wa kufanya kweli ili niweze kupata kile ninachokitaka."alisema Alie na kuamka pale aliposimama huku akitazama jengo la kifalme likiwa mbali na pale alipo, gafla tu akapotea.

Kwenye falme, baada ya Malkia kurejea na hakuweza kufahamu lolote lile linaloendelea, Mfalme Yazid alimuamuru kamanda mkuu akawaite Saadie,Lutfia pamoja na Kasma kuna mambo anahitaji kuongea nao. Haraka jambo hilo likafanyika wakaenda kuitwa mabinti hao na kupelekwa kwenye chumba kimoja ambacho walipata kumwona Mfalme akiwa amesimama kuwasubiri.
"Baba..!"aliita Saadie baada ya kumwona Mfalme akionekana kutokuwa na furaha usoni mwake. Walisogea hadi pale na kuwataka wakae kwenye viti vilivyoizunguka meza moja naye akasogea na kukaa. Mfalme alimtaka kamanda atoke nje awaache wao wenyewe, naye akafanya hivyo kisha akaufunga mlango kuwaacha waongee wenyewe.
"Nina jambo moja tu nahitaji kuwaeleza ili mpate kufahamu, huenda ndio sababu ya matatizo yote haya yanayotokea. Bila shaka mshapata kumsikia au kumwona mtu anayeitwa Alie. Huyu si mara ya kwanza kuweza kufika hapa katika ardhi ya Maskoof. Ni muda mrefu umepita aliingia hapa na familia yaje akiwepo ndugu yake pamoja na baba yao mzazi ambaye nilipata kufahamu hapo mbele kuwa alikuwa anauwezo mkubwa sana wa kutumia nguvu za ajabu japo hakutaka kujionesha abadani. Walikuja kama wahamiaji ambao lengo lao ni kuhitaji makazi ya kukaa maana taifa lao walipotokea kulikuwa na vita kali hivyo baba yao aliwahamisha ndugu hao ili kunusuru maisha yao. Sokuwa na pingamizi nikawakaribusha wakPata sehemu ya kukaa maisha yakawa yanaenda. Sasa kadiri miezi inavyozidi kuyoyoma baba yao hakuwa na afya njema, ikapelekea kuanza kuwapa watoto wake nguvu za ajabu alizonazo maana alihisi hataweza kupona kweli.
Nikapata kuambiwa tu baada ya muda kupita kwamba baba yao alifariki na kuwaacha watoto wake angali bado wadogo. Sikuona haja ya wao kuendelea kuteseka angali wapo wawili hivyo nikawatafutia mfanyakazi akawa anawahudumia kulekule nyumbabi kwake. Miaka kadhaa kupita na wao wameshazoea maisha ya hapa Maskoof taratibu Alie akaanza kubadilika. Na baada ya kuanza kujua umuhimu wa nguvu alizinazo kufanya mambo ambayo ni tofauti, alikuwa ni mtu wa kujionesha kwa watu kwa kile alichonacho, hali hiyo iliwapelekea hata watu wabaya wanaotamani kunipindua wamtumie yeye kuweza kuniangusha. Kwakuwa alikuwa bafo mdogo alofanya kile anachoambia huku akiahidiwa vitu vya thamani. Ndugu yake Kasam alikuwa mwelevu na mwenye huruma sana kwa watu na ilifanya hadi kupendwa sana na baba yao. Alie alianza kuua askari wangu kwa siti na ikawa kila siki lazima vifo vya askari watano ndani ya Maskoof tupate hivyo kazi ikawa ni kuzika tu. Hali ilizidi kwenda huku tukiwa tunatafuta nani mhusika wa mauaji hayo bila mafanikio. Ilifika muda hata baadhi ya ndugu wa askari wangu wakawa wanawasihi ndugu zao waachane na kazi hiyo ambayo muda wowote kifo kipo kilikuwa mbele yako. Ushawishi huo ulikuwa mkubwa sana na kushuhidia kweli askari wangu wanapungua kwa kuhofia kifo ambacho muda wowote kinatokea. Niliumia sana bila kujua mhusika wa yote. Lakini kadiri siku zinavyoenda nikawa nahisi jambo ikabidi nimshirikishe na ndugu wa Alie nikijaribu kumuuliza kuhusu ndugu yake ambaye hata yeye alianza kumuona yupo tofauti na kuniambia ndio sababu hata marehemu baba yao aliweza kumpatia Kasam mambo mengi sana yenye kumsaidia akijua fika Alie ameanza kuonekana hashikiki.
Hadi mwisho wa siku nakuja kumuweka mikononi mwangu nilikuwa na hasira zote hasa kikubwa ni kufahamu kwamba ni yeye ndiye aliyehusika na mauaji ya askari wangu wengi sana. Binafsi sikuwa na huruma naye, alikamatwa haraka sana na kuletwa uwanjani na watu walishamiri. Hali ile ilimfanya hata ndugu yake baada ya kufahamu kuhusu Alie kuweza kuchukizwa na taarifa hizo. Alipojaribu kuongea naye hakuwa mwenye kusikilizwa, kitu pekee alochoona Kasam ni kumzuia Alie kwa namna yeyote ile. Ilifika hatua hata wao kwa wao kuweza kupigana maana Alie tayari alishakuwa na roho tofauti na ya kibinadamu, hakuwa muelewa, alikuwa tayari kufanya kazi na watu fulani kwa manufaa yake. Sikuwa na chaguo jengine zaidi ya kuamua kutoa uhai wake. Siku hiyo niliondoka na Malkia pamoja na askari wangu kwenda kumfuata Alie lengo ni kumuua, lakini tulipofika eneo anakopatika tuliona vitu vingi kuvurugika kana kwamba kuna vurumai limetokea muda mfupi. Tulipojaribu kusogea mbele zaidi ndipo tukashuhudia kuona Kasam na Alie wakiwa chini wote wakivuja damu. Walionekana kupambana sana wenyewe kwa wenyewe. Tulisogea hadi pale na kushuhudia Kasam akipoteza maisha muda huo, Alie alikuwa akihema kwa tabu sana lakini hakuna mtu aliyekuwa na hamu naye.
Mungu anisamehe tu mimi ndiye niliyemuua Alie kwa upanga wangu kwakuwa ndiye mtu aliyesababisha mauaji ya askari wangu na alikiwa kama anatusaliti. Sikuona umuhimu wa yeye kumsaidia pale chini nilifanya hivyo kuliweka taifa langu katika usalama zaidi. Nahisi ndio sababu ya yeye kuwa na hasira nasisi baada kurejea japo tumeshangaa sana kumuona akiwa hai tena."aliongea Mfalme akiwa anawasimulia mabinti hao watatu waliokuwa makini kumsikiliza. Kasma alishusha pumzi baada ya kusikia mambo ya Alie ya huko nyuma.
"Huyu mtu anachokitaka kwasasa ni hiki kitabu, anataka kurudi kuwa binadamu tena ili aishi tena duniani. Hapa anatumia uwezo alionao ambao muda wowote ukiisha lazima atarudi kuwa mfu tena na wenzake waliokuja duniani. Hivyo wanafanya kila jitihada wakipate hicho kitabu ili wabadili maisha yao, na ndio kitu ambacho kamwe hatupaswi kuruhusu wakipate hichi kitabu. Sio wema hata kidogo hivyo tutakaporuhusu hili litokee sidhani kama tutaweza kuwazuia maana atafufua watu wengi sana ambao watamsikiliza yeye, na hakuna uwezo wa kupambana na wafu wengi kwa pamoja. Hivyo kitu pekee kwasasa ni kuzuia kitabu hiki kisifike mikononi mwa Alie na ikiwezekana kuwamaliza kabisa yeye na wenzake ambao kwasasa wameshaiteka ufalme unaoongozea na huyu Kasma."alisema Lutfia akimtazama Mfalme aliyebaki kushangaa tu. Aligeuka kumtazama Kasma baadaa ya kujua kumbe ni Malkia anaongoza taifa lake mwenyewe.
"Kwahiyo Kasma ni mkubwa kwako ndio maana kapeea aongoze taifa lenu?"aliuliza Mfalme akimgeukia Lutfia kumtazama.
"Ndio, huyu ni mkubwa kwangu na huenda sababu ya pekee iliyomfanya apewe uongozi na baba ni kwasababu amekuwa karibu sana na wazazi. Niliondoka kwenye taifa letu na kwenda kuishi mbali na hapo hivyo ikapelekea mwenzangu aaminike na kupewa uongozi."alisema Lutfia akiuweka undugu wake na Kasma kuaminika kuwa ni kweli. Hata Kasma mwenyewe alimshangaa kwa kujiamini kuongea vile mbele ya Mfalme. Hakutaka kuonesha kwamba hawajuani baina yake na Kasma.
Mfalme alimuelewa na kumuamini kile anachosema, yote hayo yalikuwa yakiendelea bila ya Malkia kuweza kufahamu lolote hawakutaka ajue kuwa kuna vita ilitokea huenda ikapelelea akakumbuka tukio la mwisho walilokutana na Alie na ikapelekea kifo chake.

Upande wa pili Alie alifika tena nje ya jengo la kifalme. Alibaki kulitazama tu kwa hamu akijua safari hii huenda wakaweka ulinzi zaidi baada ya hapo awali kuvamiwa. Safari hii alijipanga kuingia ndani mwenyewe usiku ule na alihakikisha lazima LUTKAS inakiwa mikononi mwake aweze kurudi nayo kule kwenye falme ambapo wenzake wapo kwasasa. Muda huohuo alipata kuona kundi la wasichana wa kazi wakitoka ndani ya falme kwenda kutupa mabaki ya vyakula na takataka zilizosalia. Akaona ndio nafasi pekee yeye kujichanganya nao ili apate kuingia kwenye falme asionekane kwa sura yake. Alipopiga hatua kuelekea mbele alihisi maumivu kwenye mkono wake, aliutazama na kuona ukianza kubadilika na kuzidi kuoza, alifahamu ni dalili mbaya za yeye kurudi tena kuwa mfu. Hakutaka jambo hilo litokee tena alihakikisha usiku huo hapotezi nafasi yeyote ili kujihakikishia uhai wa kuendelea kuishi tena.

LUTKAS SEHEMU YA 23


# ILIPOISHIA
...alifahamu ni dalili mbaya za yeye kurudi tena kuwa mfu. Hakutaka jambo hilo litokee tena alihakikisha usiku huo nafasi yeyote ili kujihakikishia uhai wa kuendelea kuishi tena.

# TUENDELEE_NAYO

Mfalme alirejea chumbani kwake na kumkuta Malkia akiwa tayari amelala. Taratibu naye akajisogeza na kupanda zake kitandani huku akiwa na mawazo mengi kichwani. Alimtazama mkewe na kukumbuka kile ambacho kilimtokea, alishuhudia kwa macho yake upanga mkali wa Alie ukipita shingoni kwa Malkia na kumfanya adondoke chini na punde tu akapoteza maisha. Alimsogelea mkewe na kuupitisha mkono wake shingoni, hakuweza kuona kovu wala jeraha lolote lile hali iliyomfanya ashangae. Haikuwa jambo rahisi kuamini lakini kwa kile alichokiona akaanza kuamini kweli kitabu cha Lutkas ni uhai kwa wafu. Alifurahi kuona hivyo na hakusita kumsogelea mkewe na kumbusu kuonesha anampenda na kushukuru kirudi kuwa mzima. Alivuta shuka na kujifunika kuanza kuutafuta usingizi usiku huo.

Baada ya muda wale wafanyakazi walipata kuonekana wakirejea kutoka kumwaga taka. Walitembea kwa mstari mmoja kila mtu akionekana kubeba tenga. Kasma alikuwa miongoni mwao akiwa na sura ya binti mmoja ambaye ni mfanyakazi akiwa na wenzake. Muda ule aliweza kuwafuata kule kwenye dampo na kufanikiwa kumnasa binti mmoja akampeleka pembeni na kumuua ili chukue kila kitu chake na muonekano wa msichana huyo kabisa. Hiyo ndio ikawa tiketi yake kuweza kuingia tena kwenye falme pamoja na wasichana wale. Alifuata kila ambacho wenzake wanafanya kazi zote ili tu asipate kuonekana kuwa tofauti.

Muda huo Saadie alikuwa chumbani kwa wenzake Kasma pamoja na Lutfia wakiwa wamekaa wote kitandani wakijadili yale ambayo wamepata kuambiwa na Mfalme.
"Ukimya huu sio wa heri kwa mtu ambaye amekuja kwa ubaya, huyu lazima anaanda mbunu za kurudi tena baada ya kuona watu aliokuja nao wameuawa. Na hawezi kutoka humu Maskoof mwenyewe labda akipate hiki kitabu. Hivyo Alie lazima atakuwa Maskoof anafanya njama za kurudi tena humu. Hivyo hatupaswi kukaa kulinda LUTKAS isichukuliwe bali tunapaswa kumtafuta mtu ambaye anataka kuichukua LUTKAS. Kama kweli Saadie unataka Maskoof ibaki salama pigania ardhi hii huyu mtu asiichafue. Kama kweli Kasma unataka taifa lako lirudi mikononi mwako basi huyu mtu popote pale lazima atafutwe asambaratishwe hatuna huruma wala urafiki naye."alisema Lutfia akiwajaza wenzake mori ya kumpata Alie popote pale. Maneno yake yalijaza hasira na shauku kwenye mioyo ya wenzake, walikubaliana naye na kuona kweli hakuna haja ya kukaa wakati wao ndio wanawindwa. Hawakuwa na haja ya kulala usiku huo kazi ilianza siku hiyohiyo wakaanza kutafuta namna ya kutoka nje ya falme pasi na yeyote kujua kinachoendelea.

Baada ya kumaliza kazi zao za usafi kila mtu alielekea zake kupumzika mahala pake kama ilivyo kawaida. Alie aliongozana na msichana mmoja kwenda kupumzika baada ya kudadisi na kujua ndiye mtu aliyepangwa naye kulala mahala pamoja. Hats walipofika walijipumzisha usiku ule huku Alie akiwa na shauku ya kufanya kazi lake. Alisubiri hadi msichana yule aliposinzia naye akatoka sasa kuanza kutafuta wapi alipo Lutfia. Aliingia kila chumba kuangalia kama atapata kile alichokisudia. Hata alipofika kwenye chumba kimoja ambapo aliona askari wawili wamesimama karibu na mlango wakiweka ulinzi. Alihisi ni ndani kwa Mfalme lazima ulinzi ule uwepo. Alianza kusogea pale ili apate kuingia ndani akafanyr mile alichoahidi, kumuua Mfalme kwakuwa hakutimiza mile ambacho amemuagiza kufanya. Alianza kutoa moshi mikononi mwake huku akitembea kwa mafaha kuwafuata wale askari ambao walipomuona Alie akionekana kutoa moshi mikononi wakajua mtu huyo si mwema. Haraka wakatoa mapanga yao kuyaweka sana lengo ni kutaka kumzuia msichana huyo. Moshi huo haukuwa wa kawaida, haukuwa mzuri kwa afya ya binadamu, uliwafanya askari hao wajikute wanadondoka chini na kuanza kutokwa na damu puani huku wakitetereka miili yao. Alie alisogea pale huku akiwatazama wale askari ambao punde tu walipoteza maisha. Alishika kitasa kile cha mlango na kuufungua kuingia ndani.
Saadie na wenzake walihisi kitu tofauti gafla wakiwa katika kumtafuta Alie, waligeuka kutazamana.
"Huyu mtu yupo humuhumu tayari ameingia."alisema Kasma baada ya kupata hisia juu ya kitu kibaya.
"Hapa ni kujigawa huyu dada hastahili kutoka humu akiwa hai."alisema Lutfia na wenzake wakaliafiki swala hilo. Haraka bila kuchelewa wakatawanyika kila mtu akaelekea mahala pake.

Alie baada ya kufika mule ndani macho yake yalinyooka moja kwa moja kitandani ambapo alipata kuona watu wawili wakiwa wamelala, alistabu kuona hivyo alitegemea kumwona Mfalme peke yake, ilibidi awashe taa kutazama vizuri ili apate kuwaangalia watu hao. Aliposogea karibu kuwatazama alistaajabu sana kumwona Malkia akiwa amesinzia.
Alibaki ameduwaa akifikiria siku ile alimchinja Malkia kwa upanga mkali na kuhakikisha amepoteza maisha lakini ajabu leo anamuona akiwa pale kitandani. Hakutaka kuamini alisogea hadi pale na kumshika upande wa kushoto kifuani mwake na kishuhudia mapigo ya moyo yakidunda kama ilivyo kawaida na kumdhihirishia kwamba mtu huyo yumzima. Alifikiria imekuwaje swala kama hilo kutokea, lakini alipokumbuka kuhusu kile kitabu cha LUTKAS akapata kufahamu huenda wamekitumia kwaajili ya kumrudisha Malkia kuwa hai tena. Alipolitambua hilo akapata hamasa ya kuamini kumbe swala hilo linawezekana. Alitoa kisu chake na kukishika mkononi akitaka kurudia tena kuua tena safari hii awamailize wote kabisa. Alinyanyua kisu chake kutaka kumuanza Malkia alisimama kwanza na kutafakari endapo atakapowaua hawatakuwa wafu lazima watarudishwa tena kuwa hai maana LUTKAS ipo mikononi mwa Lutfia. Hivyo kama akihitaji watu hao wauawe lazima kitabu hicho kiwe mikononi mwake ndipo hayo mengine yafuate. Taratibu alikishusha kile kisu baada ya kuona hakuna haja ya kufanya mauaji hayo, alibaki kuwatazama tu japo ana hasira nao maana ni wabaya kwake. Hakutaka kuendelea kukaa tena mule ndani aligeuka na kuanza safari ya kwenda vyumba vengine kutafuta.

Kasma katika harakati za kutembea mule ndani aliweza kuonwa na askari waliokuwa wakilinda baadhi ya sehemu ndani ya falme. Ilibidi wamfuate kumhoji maana usiku ulikuwa mkubwa sana,ilibidi Kasma atumie ujanja ili kuwakwepa askari hao wasijue kinachoendelea.
"Unafanya nini usiku huu wakati watu wote wamelala?"aliuliza askari mmoja huku wenzake watatu wakiwa wameshika mapanga yao kama silaha. Kasma aliwasogelea na kumshika mmoja mkono huku akijenga tabasamu.
"Sikuwa najisikia vizuri ndio maana nimeamua kutoka nje mara moja nitembee."alisema Kasma na kuwafanya askari wale wamuelewe. Hawakutaka hata kuuliza lolote walimuacha na kuendelea na ulinzi wao. Alibaki kutabasamu tu Kasma baada ya kuona amefanikiwa kuwasahaulisha kile ambacho wamekuwa wakiuliza. Alizidi kwenda mbele zaidi huku akiangalia huku na kule kumtafuta Alie aliyesadikika kuwepo ndani ya falme.
Katika kurakati za kutafutana huko Saadie alipata kumwona Alie akiwa ndani ya chumba kilekile ambacho awali alimuona Kasma amekutwa na Lutfia na kubaki kuwashangaa. Bila kuchelewa naye aliingia mule ndani na kumfanya Alie ashtuke baada ya kuona mtu ameingia mule ndani. Alipomtazama kwa sura akapata kumtambua kuwa ni Malkia Kasma, mtu ambaye aliweza kuja naye Maskoof wakiwa na baadhi ya askari lengo ni kukipata kitabu cha LUTKAS.
Walibaki wametazama tu kwa muda kila mtu akimtazama mwenzake kwa namna yake.
"Naona umekuwa mfanyakazi wa kifalme sasa badala ya kuwa askari wangu."aliongea Kasma akiwa anamtazama Alie akiwa kwenye mavazi na umbo la yule msichana wa kazi aliyemuua. Alie aliposikia hivyo akafahamu Kasma amemjua kuwa awali alijifanya ni askari wake hadi kuweza kuongozana naye kuja huku Maskoof.
"Shida yangu ni kupata kitabu cha LUTKAS, nafahamu mwenye nacho kwasasa ni Lutfia nawe ni mmoja wapo ambao unastahili kupata kitabu hicho. Itakuwa vyema kama ukaniambia alipo Lutfia nijue namalizana naye vipi."aliongea Alie huku akipiga hatua kumsogelea Kasma pale aliposimama. Naye hakutaka kuwa nyuma akaanza kupiga hatua kumsogelea Alie.
"Nashukuru nimeanza kukuona mimi kabla ya wenzangu, shida yangu kubwa kwako ni kutaka kujua kwanini umetutumia sisi kama njia ya kuja huku, tumeanzisha vita dhidi ya askari wa Maskoof lakini wewe hukuwa mwenye kushiriki, ulikuwa tofauti na sisi kabisa wala hukuonekana ukiwa pamoja nasi, wewe ndio uliyesababisha askari wangu wauawe. Sasa, unachokitaka abadani huwezi kukipata kirahisi hivyo kama unavyodhani."alisema Kasma akimkingia kifua Alie. Maneno yake yalimfanya Alie apandwe na hasira akijua hatapata chochote kwake. Alibadilika macho yake na kuanza kumshambulia Kasma kwa mateke na ngumi mziyo ambazo hazikuweza kumfikia mlengwa kwani alikuwa makini sana japo umbo umbo lake dogo likimfanya Alie anammudu. Walirurushiana nguvu za kichawi mule ndani kila mtu akitaka kumdhuru mwenzake lakini walikuwa makini kukwepa. Vita hiyo iliwafanya Saadie na Lutfia huko walipo wafahamu wapi kulipo na tafarani hiyo, haraka wakapotea kuwahi kufika eneo husika.

Baadhi ya askariwa kifalme waliokiwa wakizunguka kuwrka ulinzi humu walikuwa wakiendelea na operesheni hiyo kuhakikisha usalama. Lakini walipofika eneo ambalo wenzao husimama nje ya chumba cha Mfalme na Malkia kuweka ulinzi walishangaa kuona wenzao wapo chini. Ilibidi wasogee hadi pale na kushuhudia wenzao damu zikiwatoka puani na kusambaa pale chini. Hali ile iliwashtua sana na kuamua hata kuingia ndani ya chumba cha Mfalme wakihisi huenda kuna tatizo limewakuta viongozi hao. Walipowasha taa walipata kuona Mfalme na Malkia wakiwa wamelala bila tatizo, ikawafanya watambue huenda kuna mtu ameingia ndani ya falme kwa ubaya. Walitoka mule ndani na kumwacha adkati mmoja pale kuweka ulinzi huku wengine wakienda kutoa taarifa kwa wenzako hasa kamanda mkuu.

Purukushani ziliendelea ndani ya chumba kile baina ya Kasma pamoja na Alie ambaye alionekana kuwa moto na mwingi wa hasira. Wote walirudi nyuma kwanza kila mtu akihema na kutokwa na jasho jingi mwilini, walitazamana kwa hasira huku macho yao yakiwaka kama paka aangaliapo usiku. Alie akaanza kuhisi maumivu kwenye mkono wake wa kushoto, aliuficha kwa nyuma baada ya kitambua anazidi kuoza hivyo ni lazima kupata LUTKAS. Alisimama imara huku akiandaa kombora la aina yake akijua litakapofika kwa Kasma basi asambaratike kabisa. Alipandisha kwa spidi ya ajabu na kuachia shabulio hilo kielekea kwa Kasma na muda huohuo Lutfia alifika hapo na kushuhudia kama kimbunga kikielekea kwa Kasma, kwa spifi ya ajabu na kusimama mbele ya Kasma na kombora lile likapiga mwilini mwake. Saadie naye ndio alikuwa akifika sehemu hiyo na kukutana tukio hilo. Kila mtu akashikwa na butwaa baada ya kuona hali ile, hata Alie mwenyewe alishangaa kuona Lutfia akitokea gafla mbele ya Kasma. Alidondosha kitabu kile cha LUTKAS chini baada ya kukosa nguvu, lilikuwa ni pigo la aina yake lililopenya moja kwa moja mwilini mwa Lutfia aliyeonekana kukosa nguvu hata ya kusimama, taratibu akaanza kwenda chini lakini Kasma akamshika kwa nyuma asidondoke.
"Lutfia..!! Lutfiaaaa!"aliita Kasma huku akionekana kustaajabu.
"Lutfiaaa!"Saadie alikimbia kumfuata Lutfia pale alipodondoka wote wakionekana kupagawa kabisa baada ya kumwona mwenzao akikosa nguvu hata ya kusimama. Lutfia alibaki kumtazama Alie mbele alipo akionekana kuhema, aliishia kumnyooshea tu kidole ambacho hakikusimama kwa muda mrefu mkono wake ukashuka chini kama mzigo na papo hapo akazima na kuwaacha wenzale latika sintofahamu.
Alie alishuhudia tukio hilo ambalo hakulipanga kulifanya lakini imetokea kama bahati kwake maana mhusika aliyekuwa akimtaka ndio amedhurika na shambulio hilo alilorusha. Alipoangaza macho yake vizuri akapata kuona kitabu kile pale chini huku Saadie na Kasma wakiwa hawaamini kile alichofanyiwa mwenzake. Akaona ndio njia na muda sahihi kwake kuondoka na kitabu hicho, alivuta pumzi yake ili apate kukimbia kwa kasi kukiokota kitabu kile pale chini.

LUTKAS SEHEMU YA 24


# ILIPOISHIA

Akaona ndio njia na muda sahihi kwake kuondoka na kitabu hicho, alivuta pumzi yake ili apate kukimbia kwa kasi kukiokota kitabu kile pale chini.

# TUENDELEE.
Kwa wepesi wa hali ya juu Alie alichomoka pale alipo kukifuata kile kitabu huku Saadie na Kasma walijaribu kumuamsha Lutfia.
"Lutfia...Lutfiaa... wewe..!"sauti hiyo ilipenya masikioni mwa Lutfia aliyeanza kufumbua macho yake taratibu na kugonganisha macho yake na mtu aliyekuwa akimuamsha. Ilibidi ageuke kwa unyonge kutazama mahala pale. Aliona yupo kwenye chumba ambacho alihisi anakifahamu, alipapasa pale alipolala na kujikuta akilishika shuka zito. Hapo ndipo akafumbua vizuri macho yake yote kuangaza ili afahamu yuko wapi. Kitanda kizuri, kabati la nguo, televisheni huku kiyoyozi kikisaidia kuleta hali nzuri ndani ya chumba kile ilimfanya Lutfia ashangae bila kupata jibu kamili. Alimtazama yule mtu na kubaki kushangaa kumuona mama yake mzazi akiwa ameshika glasi ya maji pamoja na dawa zilizokuwa kwenye kikopo.
"Hebu kunywa kwanza hizi unaonekana umepata nafuu eh!"alisema Mama Lutfia akimpatia mwanaye dawa.
"Alah!, hii inamaana gani?"alishindwa kuelewa swala hilo linaendaje. Amefikaje tena nyumbani kwao angali alikuwa kwenye taifa la Maskoof. Alitazama zile dawa na yale maji huku akili ikiwa mbali sana ikifikiria matukio ambayo yanaendelea kwenye taifa la Maskoof.
"Wewe unanini jamani! hebu kunywa kwanza.!"aliongea Mama mtu na kumfanya Lutfia apokee chupa ya maji na dawa zile za maumivu na kuzinywa kwanza akihisi kama kuvurugwa akili.
Hata alipomaliza ilibidi atazame mahala ambapo yupo kwasasa. Aliona ni ndani ya chumba chake cha awali huku mama yake mzazi akimtazama kushuhudia mwanaye akionekana kutokuwa sawa.
"Mama... ni muda gani tangu nifike hapa ndani? Na nimekujaje kujaje humu?"aliongea Lutfia akiwa ameshikilia chupa ya maji aliyopewa kumezea dawa.
"Jamani... inamaana bado hujapata nafuu?"aliuliza mama huku akimtazama mwanaye.
"Nafuu?"alishangaa Lutfia bada ya kusikia hivyo kwa mama yake. Ilibidi akumbuke mara ya mwisho alipata kushuhudia Kasma akielekea kupigwa kombora kutoka kwa Alie aliyekuwa amesimama kumtazama Kasma. Na ndio muda ule ambao Lutfia alitokea na kushuhudia tukio hili kiliendelea. Alivyokuwa mwepesi wa hali ya juu alichomoka pale alipo na kujitokeza mbele ya Kasma naye akapigwa na shambulio hilo ambalo hakutemegemea.
Alishangaa kuona kwasasa yupo tena nyumbani kwao ilihali muda mfupi alikuwa kwenye taifa la Maskoof.
"Mama hebu niambie ukweli mbona kama sielewi! Muda mfupi tu nilikuwa Maskoof imekuwaje najikuta huku tena?"aliuliza Lutfia huku akimtazama mama yake ambaye alibaki kumshangaa mwanaye. Ilibidi aachie tu tabadamu huku akipandisha pumzi na kuishusha kwa nguvu.
"Yaani naona unaongea tofauti na ambavyo nimekuzoea. Yapata wiki tatu sasa upo hapa baada ya kutoka huko unapopasema kuwa Mfalme wa huko Maskoof anakutafuta umesingiziwa kumuua binti yake. Tangu umekuja hapa tunakula na kunywa pamoja, ni mimi ndiye ninayekupeleka shuleni kila siku leo iweje useme muda mfupi ulikuwa Maskoof au mwenzako ulirudi tena huko ulipokuwa watafutwa?"aliuongea mama mtu na maneno yale yakawa mapya kwenye ngoma za masikio ya Lutfia.
"Ati nini? Mimi nimuue Saadie? Kwa kosa gani hada?"ni maswali yaliyoongozana kwa pamoja aliyoyatoa Lutfia huku akimtazama mama yake.
"Jamani mwanangu, yote hayo ulinambia kipindi unarejea kutoka huko na nikakupokea kwa mikono miwili."alisema Mama Lutfia na maelezo yake yakamfanya binti yake aamini huenda ikawa ni kweli. Aligeuka kutazama kulia na kushoto kwake kama anatafuta kitu. Aliangalia kwa muda bila mafanikio.
"LUTKAS iko wapi?"aliuliza Lutfia huku akiendelea kutafuta hadi mama yake akashangaa kuona mambo hayo yanavyokwenda. Haraka akanyanyuka pale kitandani alipo.
"Mama kitabu kipo wapi? Kile kitabu changu kipo wapi?"aliongea Lutfia akionesha kupagawa. Mama yake ikabidi asimame nayeye kuanza kutafuta hicho kitabu.
Iliwachukua muda mrefu kulifanya zoezi hilo ambalo halikuwa na maana ndani yake, hadi walichoka na kuamua kukaa kupumzika.
"Lakini una uhakika ulikuja nacho siku ile maana tangu uje sijawahi kukuona na kitabu humu ndani, au upumzike kwanza huenda ukakumbuka."aliongea Mama na maneno yake yakamfanya Lutfia apoe kwanza. Alivuta kumbukumbu na kuamua kurudi tena kitandani kujilaza kwanza huku mama yake akishuhudia. Alifumba macho yake kisha akaanza kukumbuka nyuma mara ya mwisho katika tukio lile ambao aliweza kupigwa kombora na kumfanya adondoshe kitabu kile. Alibaki kumtazama Alie akiwa amesimama huku mkono wake ukielekea kwa Lutfia aliyemrushia vile. Taratibu akaenda chini na kushuhudia Alie akiwa anatabasamu tu huku akikitazama kitabu kile chini. Lutfia aliishia kumnyooshea kidole Alie akitamani anyanyue ngumi nzito amrukie Alie aliyeonekana kutaka kufanya jambo hilo. Alijitahidi kuamka lakini hakuweza, mwili ulitawaliwa na baridi akihisi nguvu zake kushuka huku kwa mbali akishuhudia Alie akitoka spidi kuweza kukimbilia kitabu kile. Alijitahidi kurudisha nguvu zake kuweza kumzuia Alie.

Alifumbua macho yake gafla na kukutana na tukio lilelile likiendelea akimuona Alie akikikaribia kitabu kile, kitendo cha yeye kufumbua macho yake kwa haraka kiasi hicho Saadie na Kasma walipata kuona tukio hilo na kupatwa na machale. Walihisi kitu kibaya nyuma yao haraka waligeuka kwa pamoja na kuona Alie kwa spidi ya ajabu akikikamata kitabu kile. Walinyoosha mikono yao kama kumzuia asije huku ikitoa miale ya mwanga iliyomchapa Alie kifuani kujikuta akirushwa mbali na kukitupa kitabu kile. Alidondokea kwenye meza ya thamani ya vioo na kusababisha kuvunjika hata kutoa makelele ambayo yaliwafanya baadhi ya askari mule ndani ya jengo la kifalme washtuke. Haraka wakaanza kukimbia kufuata kelele hizo zilipotokea. Hata Alie alishangaa kuona umoja ule wenye nguvu ukimuadhibu hata yeye mwenyewe hakutegemea kama lingetokea hilo. Ilisikika filimbi ikilia kuashiria kuna tatizo limetokea hivyo askari walihitaji msaada kwa wenzao ambao haraka wakaanza kusogea. Alie kuona hivyo hakuona haja ya kuendelea kukaa pale japo alipatwa na hasira sana huku akiwatazama mabinti hao, alipotea gafla na kuwafanya Kasma na Saadie wamgeukie Lutfia aliyeonesha kufumbua macho yake.
"Lutfia.. vipi upo salama?"aliuliza Kasma akiwa amemshika kichwani Lutfia, taratibu walimnyanyua pale chini alipo akionekana kuugulia maumivu tumboni. Ilimbidi Saadie achukue kile kitabu na kumuwekea mwenzao tumboni. Taratibu maumivu hayo yakaanza kupotea kabisa na hali ya Lutfia ikarejea kuwa sawiya.
Punde tu wakatokea kundi la maaskari wakiongozwa na Kamanda mkuu kuwakuta mabinti hao watatu wakiwa wamesimama.
"Vipi kuna nini kimetokea humu?"aliuliza Kamanda mkuu akimtazama Saadie.
"Kuna mtu alikuja kutuvamia ndio Lutfia alikuwa akijaribu kumzuia, ameweza kutoweka japo mwenzetu hayupo sawa kidogo."alisema Saadie akiwa amemshika mkono Lutfia.
Kamanda mkuu alimuelewa na kuwaruhusu askari wake watawanyike kuangalia usalama zaidi. Alimpa pole Lutfia na kuwaacha kisha akatoka mule chumbani.
"Bado ninamashaka na huyu Alie anaweza kurudi tena hapa mjue!"aliongea Saadie akiwa na hofu juu ya ujio wa Alie tena.
"Alie hatachoka kurudi humu, lazima atakuja maana anataka ahakikishe anakipata kitabu hiki. Yaani sasahivi hatuna muda wa kusubiri atufuate inatakiwa sisi ndio tumtafute yeye tuhakikishe tunammaliza. Tukifanikiwa hilo basi wale wenzake hawatakuwa na ujanja tena wa kufanya lolote. Alie ndio mzizi wa hawa wote."alisema Lutfia akiwaeleza wenzake.
"Hatupaswi tena kusubiri muda uende huyu atafutwe muda huu."aliongea Saadie akionekana kuchukizwa na Alie.
"Hapana kwasasa hataweza kurudi humu wala kufanya lolote sasa, nasi tunapaswa kupumzika itakuwa vyema kesho tukalifanyia kazi hilo."alisema Lutfia na wenzake wakakubaliana naye.

Alie alionekana kubadilika kabisa sura yake kwa hasira alizonazo. Ni baada ya kushindwa kukichukua kitabu kile mbele ya mabinti watatu. Alikaa kujiuliza wapi anapofeli hadi sasa hafanikiwi jambo lolote, akijitazama hali yake inazidi kubadilika.
"Bila ya kufanya kitu cha ziada sitaweza kufanikiwa kwakweli."aliongea Alie na kutafuta mahala pazuri akakaa. Alitazama chini ya ardhi na kuweka chini mkono wake huku akiyaandika majina ya mabinti watatu. Kila amalizapo jina moja basi hutokea sura ya mhusika hadi wote kumalizika.
Lutfia, Saadie pamoja na Kasma waliweza kuonekana pale chini ya ardhi huku Alie aliwatazama, alichukua muda mrefu kuwachambua kila mmoja akiangalia uwezo wa mhusika binafsi. Mtu pekee aliyeonekana hana uzoefu wa nguvu za kujilinda ni Saadie ambaye ndio hata Alie aliona anafaa kumtumia kwasasa. Alipolipanga zoezi hilo alishusha pumzi kwanza na kuweza kupumzika maana kabla jua kuzama alikuwa akihangainga bila mafanikio. Alisubiri kukuche apate kuweka uzito kwa Saadie lengo ni kumuingia apate kumtumia atakavyo.

Lutfia alikuwa zake kitandani amejilaza huku akitazama jii ya paa la chumba hicho akiwa na Kasma aliyekuwa anakoroma muda huo. Alitafakari mambo mengi sana namna ya kumdhibiti Alie. Alikumbuka muda ule baada ya kupigwa pigo lenye nguvu na Alie alipata maumivu makali sana hadi kupelekea kutojitambua kabisa. Alikumbuka kuwa alitokea nyumbani kwao na kujiona akiwa kitandani huku akionekana kama kuugua maradhi hadi kupewa dawa na mama yake apate kuwa sawa.
"Inamaana nilifika nyumbani kweli au?mbona sijui ilikuwaje hadi nionekane nipo na mama na gafla nikatoweka tena."alijisemea Lutfia moyoni akishindwa kuelewa imekuwaje hadi yeye kuweza kurudi kwao gafla. Alijikuta akitabasamu lakini baada ya kumwona mama yake akiwa salama kabisa.
Akiwa kwenye tafakari hizo aliona chumba kikianza kuwaka nuru, mwanga mweupe ulianza kutaka kumulika mule ndani. Ilimbidi Lutfia anyanyuke pale alipolala na kukaa kitako huku akizuia mwanga mkali uliokiwa ukipiga machoni mwake, punde akatokea mtu na mwanga ule ukafifia. Alipomtazama kwa makini alipata kuachia tabasamu baada ya kumwona Kasam, mtu ambaye amemkabidhi kitabu cha Lutfia na ndio ndugu wa damu wa Alie.
"Ni muda hatukuweza kukutana walau kusalimiana tu, nimekuja kukujulia hali baada ya kupatwa na mtihani pindi ulipokuwa unamzuia Alie, pole sana. Ila kuna jambo moja nahitaji ulifahamu muda na wakati wowote, katika maisha yako sio kila kitu utafanikiwa, kuna mambo ambayo yanakuwa ni changamoto yakupasa wewe kama wewe ujisaidie mwenyewe huenda ikawa ni mtihani. Wewe ndio mwenye kuwaongoza wenzako muda wote na wewe ndio mwenye uwezo zaidi ya kupambana na Alie. Kuwa karibu na wenzako, kuwa mlinzi wa wenzako na kwa umoja wenu naamini mtafanikiwa kuondoa kizazi cha wafu kinachoanza taratibu kirejea duniani. Namsikitikia Kasma maana taifa lake lote linaelekea kuwa wafu maana kila siku wanawaua watu zaidi ya kumi na kuwageuza kuwa kama wao. Hivyo mnakqzi kunwa hapo mbele ya kumsaidia mwenzenu. Nakuomba sana LUTKAS iwe mikononi mwenu asishike mfu yeyote yule maana kitakapokuwa mikononi mwao kwa siku moja tu basi kuna uwezekano mkubwa hata ninyi pia mkabadilika na kuwa wao. Kazi ni kwenu muhimu kuwa na ujasiri na moyo wa pamoja, naona nikutakie usiku ulio mwema na nahakika mtashinda."aliongea kwa upana Kasam akiwa amekaa kwenye kitanda akiongea na Lutfia,
"Na imekuwaje nikarudi tena nyumbani nikiwa kitandani na nimeweza kumwona mama yangu?aliuliza Lutfia lakini swali lake halikupatiwa jibu, Kasma alinyanyuka na kufanya chumba kile kitawale tena mwanga mkali sana kumfanya Lutfia ajikinge hadi ulipotokomea na Kasam akapotea. Alishusha pumzi binti mwenye dhamani ya kuwalinda wenzake na kulinda kitabu cha LUTKAS.
Muda wote wakiwa wanaongea Kasma alikuwa macho akisikiliza kila kitu kinachozungumzwa baina ya Kasam na Lutfia. Alijikuta akitokwa na machozi baada ya kusikia taifa lake linafanyiwa ukatili, raia wanauliwa na kugeuzwa wafu ambao wanaongozwa na Alie ambaye hata wao anawasumbua. Hasira na uchungu ulichanganyika na kuzidi kumchukia adui yao, Alie.

LUTKAS SEHEMU YA 25


#ILIPOISHIA

Alijikuta akitokwa na machozi baada ya kusikia taifa lake linafanyiwa ukatili, raia wanauliwa na kugeuzwa wafu ambao wanaongozwa na Alie ambaye hata wao anawasumbua. Hasira na uchungu ulichanganyika na kuzidi kumchukia adui yao, Alie.

#TUENDELEE

Kulipo pambazuka taarifa za kuvamiwa tena ndani ya falme ilimfikia kiongozi wa taifa hilo ambaye alistaajabu kusikia hivyo. Alibaki kutafakari tu mwenyewe swala hilo linaendaje. Hayo yote yakiwa wanaendelea hakuna hata moja ambalo Malkia anafahamu na hawakutaka kumjulisha maana hawataki afahamu kwamba alikufa tayari. Ilibidi Mfalme awaite mabinti zake kwanza ili apate kujua namna ya mambo yanavyokwenda maana anazidi kuona mitihani inamuandama katika taifa lake . Saadie na wenzake walielekea kwenye chumba cha kukutana na Mfalme kupanga mambo yao. Wote walipofika swala lililoongelewa ni namna ya kumdhibiti Alie kwa namna yeyote ile.
"Hili swala baba tumeshakaa na kupanga tutamdhibiti vipi huyu, nilikuwa namuhofia zamani lakini kwasasa sina hata chembe ya woga dhidi yake."alisema Saadie kwa ujasiri ya hali ya juu. Hata baba yake alistaajabu kuona kwasasa haogopi lolote kutoka kwa Alie. Ilibidi hata Lutfia atumie maneno ya busara kuongea na Mfalme aone jinsi watatu hao walivyopanga kuhusu Alie.
Baada ya kujiridhisha hayo Mfalme hakutaka tena kusubiri alinyanyuka na kuondoka zake akiwaacha mabinti hao wamekaa. Walinyanyuka baadae na shuhuli zengine zikaendelea kila sehemu ya ardhi ya Maskoof.
Kwa Alie hakuwa mwenye kukata tamaa na safari hii aliamua kuwa lolote litakalotokea atakabiliana nalo.
"Siwezi kushindwa na vitoto ambavyo nimekuwa nikiwaona awali. Safari hii sitokubali kwa namna yeyote ile na hata ikiwezekana nitoe uhai wa watu ili tu nifanikiwe."alijisemea mwenyewe Alie akionesha kukasirishwa na kutopata kile anachokihitaji. Aliamua kufanya lolote safari hii kuonesha amechoshwa na vizuwizi kwa mabinti watatu wanaomuwinda pia. Safari ya kurudi tena kwenye falme ikaanza na lengo hasa kwasasa alilopanga ni kuhakikisha anamuweka Saadie katika mikono yake kwa namna yeyote ile. Wakati anawazo hilo kuna jambo moja likamjia kichwani na kubaki kulitafakari kwa muda na mwishowe akapata jibu kamili.

Siku hiyo Malkia alikuwa zake chumbani amepumzika mwenyewe na muda mfupi akapata kuingia mfanyakazi mmoja akiwa anamhudumia kumuandalia matunda na vinywaji. Aliyatenga juu ya meza moja ndogo iliyopo karibu na Malkia kisha akaweka na visu kadhaa pale, hata alipomaliza alinyanyua uso wake kwa kutoa heshima kwa Malkoa kisha akaanza kuondoka.
"Hebu subiri kwanza.!"alisema Malkoa huki akiyatazama yale mayunda mezani. Yule mfanyakazi ilimbidi asimame kutii sheria.
"Haya tangu lini kumekuwa na tabia ya kuandaa matunda kisha unaondoka? Unategemea nani ayakate?"aliongea Malkia huku akimtazama.
"Oh samahani Malkia wangu niwie radhi kwa hilo."aliongea hivyo na haraka yule mfanyazi akasogea pale mezani kukamata visu na kuanza kuvinoa visu hivyo kwa kuvigusanisha kila muda huku visu vikosikika kama kunolewa na chuma.
Kelele zile sasa za visu kugusana na kutoa kelele hizo zilimfanya hata Malkia ahisi kichwa kuuma sana. Hali hiyo yule mfanayakazi alipata kuona na kuzidi kufanya vile kusudi.
Malkia alianza kuhiisi mambo tofauti, alijikuta alianza kukumbuka matukio ya nyuma, sauti ile ya visu ilimfanya akumbuke tukio la yeye kukatwa shingoni na upanga mkali na ikaelekea kudondoka chini asijue kilitokea nini baada ya hapo. Alishtuka baada ya kukumbuka hayo na haraka akajishika shingo yake akijaribu kuangalia kama kuna jelaha au kovu lolote lile kutokana na kuchinjwa kikatili siku ile na Alie. Ajabu hakuweza kuona utofauti wowote ule kwenye shingo yake hali iliyopelekea kushikwa na butwaa, alimtazama yule mfanyakazi akiendelea kugusanisha visu vile na taratibu akabadilika kabisa na kuonekana uhalisia wake. Ni Alie akiwa ameshika visu viwili huku akiwa mwenye kutabasamu akimtazama Malkia akionekana mwenye woga.
"Usishangae kuniona nipo hapa muda huu, sina muda wa kukaa tena hapa nimekuja kurudisha akili yako na kuwa kama zamani. Nimewekeana makunaliano na mumeo Mfalme Yazid uweze kuwa hai tena nami niweze kumchukua binti yako Saadie. Na ndio maana unajiona huna hata alama ya jeraha shingoni angali nilikuchinja kwa upanga mkali. Hivyo nimekurudisha kuwa hai na akili zako nami sina budi kuondoka na binti yako, anakuwa mali yangu sasa na ndivyo alivyoona mumeo ni bora awe nawewe. Niwatakie siku njema."alisema Alie akimwacha Malkia akiwa ameshikwa na butwaa baada ya kusikia maneno hayo ambayo hakutegemea kama yangelitokea. Ilimbidi ahakikishe tena kuupeleka mkono wake shingoni bila kuona tofauti yeyote, alishindwa aseme nini akabaki kunyamaza tu. Alie alipotea gafla akimuacha Malkia akiwa katika hali ile ya kuamini Mfalme Yazid amekubaliana na Alie amchukue Saadie na kuurudisha uhai wa mkewe Malkia.
Machozi yakaanza kumtoka Malkia akijua tayari amempoteza mwanaye kwaajili yake yeye. Hakutaka kuendelea kuumiza moyo wake alitoka mule ndani kumtafuta Mfalme ili amueleze kwa kina zaidi juu ya taarifa hizo.

Muda huo Mfalme Yazid alikuwa juu ya farasi akitembea kwenye makazo ya wananchi wake akiwajulia hali na kuangalia maendeleo yao. Watu walimpa heshima yake kama Mfalme kila sehemu apitayo akizidi kuwahamasisha kufanya kazi. Alie alikuwa miongoni mwa raia wa kawaida akiwa amejichanganya nao. Alitafuta sehemu na muda muafaka wa kuweza kuonana na Mfalme Yazid kabla hajarudi katika falme.
Kule kwenye falme Saadie na Kasma walitoka nje wakianza msako mkali wa kumpata Alie popote pale alipo, huku wakimuacha Lutfia ndani ya falme akizunguka kila sehemu kama ataweza kumuona Alie huenda akawa yumo humo. Katika tembea yake alipata kumwona Malkia akiwaa anatembea kwa hasira na haraka sana. Alistaajabu kuona hali ile ikabidi amfuate ili kujua tatizo linalomkabili.
"Vipi kuna tatizo Malkoa wangu?"aliuliza Lutfia akisimama kwa mbele kumzuia Malkia kutembea. Alibaki kumtazama tu Lutfia akiwa pale mbele huku uso wake ukijaa na chuki za wazi.
"Inamaana hata ninyi mlikuwa mnafahamu kwamba niliuawa na Alie lakini mkanyamaza kimya?"aliuliza Malkia kwa hasira, swali lake likawa gumu kujibiwa kutokana na hali aliyonayo. Lutfia alinyamaza tu asiongee lolote mbele ya Malkiia.

Mfalme alikuwa kwenye mawazo makubwa juu ya taifa lake linapoelekea. Muda mfupi alitokea Alie akiwa anamtazama Mfalme Yazid huku akijenga tabasamu la kutengeneza. Mfalme alishtuka kumwona tena Alie akiwa mule ndani.
"Imekuwa ni gafla tu kuonana nawe uso kwa uso tena. Mara ya mwisho nakumbuka tuliachana kwa makubaliano baina yangu mimi na wewe na hafi sasa hakuna na sijasikia kuhusu wewe kunijuza kuwa umefikia wapi. Ilaaa..... kimya kingi pia ni jibu kwamba umeshindwa kuwapata. Sisi tutamtafuta mwenyewe ila tutakapompata basi safari yako ya kuendelea kuishi itakuwa imefika tamati. Hebu nambie kazi imekushinda?"aliuliza Alie huku akimtazama Mfalme.
Alibaki kutazama tu chini Mfalme asijue amjibu nini msichana huyo. Alie alimtazama Mfalme kwa jicho kali na kuonekana kiongozi huyo akijishika shingo yake kana kwamba anakabwa na mtu tena kwa nguvu.
"Ukimya wako ni jibu tosha kwangu,na nikwambie jambo ambalo hukuwa walifahamu hapo awali, Saadie muda wowote atakuwa mfu anayemilikiwa na Lutfia kwani naye yupo kama mimi. Tumekuja katika taifa lako kwaajili ya kuchukua watu ambao watatufaa katika mambo yetu, nadhani mwenzangu amefanikiwa kumpata binti yako muda na saa yeyote tegemea kupata msiba huo."alisema Alie akimjaza imani mbaya Mfalme Yazid, maneno yale yalimshtua sana kiongozi huyo huku akishuhudia Alie akigeuka na kuondoka zake.
"Lutfia..! Inamaana ndio anataka kumgeuza binti yangu mimi?"alishindwa kuelewa mapema juu ya jambo hilo. Maelezo ya Alie yalimchanganya kabisa na kuanza kweli kumtilia mashaka Lutfia kwa kile alichoambiwa muda mfupi. Punde wakatokea askari kadhaa wakiwa wanaongozwa na kamanda mkuu aliyesogea hadi pale alipo Mfalme.
"Upo salama Mfalme?"aliuliza Kamanda akimtazama kiongozi huyo.
"Hakikisheni ndani ya muda mchache mnampata binti yangu Saadie akiwa salama."alitoa amri hiyo Mfalme Yazid akionesha kuwa makinj na kauli yake.
"Bila shaka atakuwa na wenzake maana mara ya mwisho nilipata kuwaona pamoja wakionekana kushirikiana kumtaf..."
"Nimesema namujitaji Saadie wangu hapa akiwa mzima, hao wengine achana nao mimi namuhitaji binti yangu hapa.!"alisema Mfalme akionesha kuwa na jazba. Ilimbidi Kamanda atii amri kutoka kwa Mfalme, aligeuka na kuwataka askari aliokuja nao aongozane nao kwenda kumtafuta Saadie popote pale alipo.

Huku Lutfia alikuwa makini katika harakati za kumtafuta Alie popote pale alipo maana ameleta tafarani kubwa kwao. Katika harakati za kutafuta uso kwa uso alipata kuonana na Alie na wote wakabaki kutazama takribani dakika nzima kila mtu akimtathimini mwenzake kwa aina yake. Pamoja na udogo wa kimo Lutfia hakuweza kuhofia lolote, wote wawili walianza kupiga hatua kusogeleana kila mtu akiwa na kinyongo chake moyoni. Hadi walipokaribiana wakasimama na kubaki kutazama tu.
"Bila shaka nimekuwa nikisubiriwa kwa hamu kubwa sana, basi mimi ndiye yule ambaye mmemuona kwenye sehemu nyingi na kwenye matukio tofauti, naitwa Alie."alijitambulisha mbele ya Lutfia aliyeachia tu tabasamu tu. Hakuhitaji hata kutambulishwa alimfahamu sana.
"Sitegemei kama leo nitaweza kukuacha hapa ukiwa unaendelea kuvuta pumzi. Matendo, visa na matukio yote nategemea leo utaweza kuvilipa. Mengi unajua umefanya, umeua watu wengi sana ambao hawana hatia. Na sasa unadiriki kutafuta kitabu ili upate kurudi kuwa hai, nakusikitikia sana na sahau kabisa kupata LUTKAS dada yangu, wewe ni kurudi tu ulipotoka na muda ndio huu.."aliongea Lutfia na kumsukuma Alie kwa nguvu za ajabu itokayo mikononi mwake. Alie alirushwa kurudi nyuma na kubaki kushika ukuta ulio pembeni. Hata yeye mwenyewe alishangaa kuona tukio hilo. Aliachia tu tabasamu baada ya kuona anayepambana naye yupo imara hivyo hakupaswa kumdharau. Alisimama imara wote wakabaki kutazama huku macho yao yakibadilika kabisa kuwa ya kutisha.
"Kuna kazi muhimu sana naimalizia kwanza ndipo nikutane na wewe tumalize hili swala vizuri, tutakutana siku nyengine."alisema Alie akiwa amesimama imara. Gafla akapotea eneo lile akimwacha Lutfia akiwa amesimama pale. Naye hakutaka kumwacha amkimbie alipotea kumfuata hukohuko alipoenda. Alikuja kutokea kwenye uwanja mkubwa ambapo alitegemea kukutana tena na Alie lakini haikuwa hivyo kama alivyotegemea. Aliangaza macho yake huku na kule lakini hakupata kuona chochote hali iliyomfanya hata yeye mwenyewe ashikwe na hasira kuona amempoteza mbaya wake.

Upande wa pili Saadie alikuwa katika harakati za kumtafuta Alie. Alitokea kumchukia sana baada ya kutambua kuwa dada huyo si binadamu aliye hai na unyama anaoufanya kwa watu ili awabadilishe kuwa jamii yake ambao watamfuata yeye. Alitembea ndani ya jengo la kifalme kila sehemu akiwa amejiandaa kukabiliana na Alie, muda mfupi alipata kumwona Lutfia alitokea mbele yake naye akionekana kutafuta.
"Lutfia.. vipi umefanikiwa kutambua alipo Alie?"
"Nilimwona na tukawa tunapambana lakini akanipotea na sijui alipoelekea. Ila naamini atakuwa tu humu bado."aliongea Lutfia akionekana kutazama huku na kule kuonesha anashauku ya kumpata Alie.
"Huyu leo tunaye lazima apatikane kwa namna yeyote ile. Hapa tujigawe tu wewe pitia hivi nami niendelee kwenda mbele utakapomwona tujulishe haraka tutafika."alisema Saadie.
"Sawa nanyi mkimwona mniambie mapema."aliongea Lutfia wakaelewana, Saadie aliongoza njia yake kuendelea na msako wa kumpata Alie.
Lutfia akabaki kumtazama tu Saadie akipiga hatua, alitabasamu pale alipo na gafla akabadilika.
Sura na muonekano wa Alie ukapata kuonekana huku macho yake yakibadilika, taratibu akaanza kumsogelea Saadie ambaye hakuwa ametilia maanani kuhusu Lutfia ambaye sekunde chache wametoka kupeana majukumu. Alie alinyoosha vidole vyake na kuonekana vikianza kurefuka zaidi hasa kidole chake cha shahada kikiwa kama sindano kwa mbele. Alipiga hatua kumsogelea Saadie, na hata alipomfikia akanyoosha kidole chake na kukisogeza karibu na shingo ya Saadie ambaye alihisi kama kuna utofauti eneo lile. Alipatwa na msisimko wa ghafla ikabidi ageuke nyuma kuangalia. Papo hapo Alie alibadilika tena na kuwa sura ya Lutfia, bila huruma alisokomeza kidole chake chenye ncha kali shingoni kwa Saadie ambaye alipata kushuhudia Lutfia akifanya tukio hilo, na baada ya sekunde chache kikatolewa kidole kile na kuacha damu ikianza kumiminika kutoka shingoni mwa binti wa Mfalme. Saadie alishangaa sana na kubaki kuziba sehemu ile kwa mkono wake.

LUTKAS SEHEMU YA 26


# ILIPOISHIA
...na baada ya sekunde chache kikatolewa kidole kile na kuacha damu ikianza kumiminika kutoka shingoni mwa binti wa Mfalme. Saadie alishangaa sana na kubaki kuziba sehemu ile kwa mkono wake.

#TUNAUGANISHA
"Lut..fiaa.. umenigeuka?"aliongea Saadie huku akionekana taratibu akiishiwa nguvu hata ya kusimama vyema. Alie alimsogelea karibu kabisa huku akiwa na umbo la Lutfia.
"Hiki ndicho nilikisubiri kwa muda mrefu, nimeanza nawewe nakuja kumalizia na wenzako hadi nipate kile ninachokohitaji."aliongea Alie na maneno yake yakamfanya Saadie atambue kwamba si Lutfia ambaye anamfahamu, Alie alipeleka mkono wake shingoni mwa Saadie kumkaba akizidi kumpa maumivu makali, Saadie hakuwa na uwezo tena wa kumzuia kwa nguvu ambazo anatumia adui yake. Muda huohuo Kamanda mkuu pamoja na baadhi ya askari walikuwa wanafika eneo hilo. Wote walishanga kumwona Lutfia akiwa anammaliza Saadie pale, walitoka mbio na mapanga yao kumkabili Lutfia aliyeonekana kabisa kuwa na niya ya kumuua binti wa Mfalme. Hata walipomkaribia kutaka kumshambulia alipotea gafla na kuwaacha wakishangaa. Haraka Kamanda mkuu alimsogelea Saadie aliyekuwa anatokwa na damu nyingi shingoni huku akihema kwa tabu sana. Kila mtu alifumba mdomo wake kwa huruma kumwona binti wa Mfalme akiwa meshambuliwa sehemu mbaya sana.
"Saadie... usijali utapona tu na Lutfia lazima tumkamate apate afhabu kwa hiki alichokofanya."aliongea Kamanda mkuu akitamani hata kulia. Alitoa nguo yake kujaribu kumfunga Saadie shingoni maana damu nyingi zilikuwa zikichuruzika. Saadie alitamani kusema ukweli lakini hakuweza hata kuongea, alibaki kuunyanyua tu mkono wake na kubaki kutikisa tu kidole lakini hakuna aliyeelewa alikuwa anamaana gani.

"Sidhani kama wazazi wangu watakuelewa Lutfia kwa hichi kilichotokea."ilisikika sauti masikioni mwa Lutfia akiwa anahaha kumsaka Alie. Ilibidi asimame baada ya kutambua kuwa ni sauti ya Saadie.
"Unamaana gani kusema hivyo.?"aliuliza Lutfia akiwa haelewi kinachoendelea.
"Muda mfupi sitakuwa tena nanyi, Alie amenidhuru sehemu mbaya sana, alichukua uhalisia wako na kuuvaa yeye akaonekana ni wewe Lutfia. Ameniumiza sehemu mbaya na kibaya hata kamanda na askari wengine wamekuona wewe ndiye mhusika uliyenifanyia haya. Hivyo huwezi kukwepa hii kesi. Nakusihi uondoke tu kabisa Maskoof kwa usalama wako, nafahamu maamuzi ya Mfalme pindi akipewa taarifa hizi mbaya. Nakuomba ondokeni na Kasma haraka kabla taarifa hizi hazijasambaa mji mzima."alisikika Saadie akiongea hayo, Lutfia akijikuta akibaki ameduwaa tu asielewe hata amjibu nini Saadie. Alijikuta akienda chini na kupiga magoti, aliishiwa na nguvu baada ya kusikia kuwa Alie amemdhuru rafiki yake kipenzi Saadie. Chozi lilimtoka na kujikuta akilia sana kwa uchungu, mwishowe alipiga kelele za hasira huku akilitaja jina la A L I E kwa sauti ya juu. Sauti iliyofanya upepo na radi za gafla kuanza kufuatana kwa pamoja, Kasma huko alipo alisikia kelele zile na kujua ni Lutfia huenda kuna kitu kimemkwaza ndio sababu ya kufanya hivyo.
Alie alisikia sauti ile akiitwa kwa hasira, alibaki akicheka sana na kuona ndio kitu ambacho alitegemea kitokee.
"Ushidi unakaribia kunisogelea, tutakutana tu tuongee vizuri Lutfia."alisema Alie akiwa mwenye kujiamini sana kwa kile alichokofanya.

Alionekana Kamanda mkuu akimnyanyua Saadie pale chini akiwa amelegea kila kiungo kuonesha tayari mwili wake umeshatengana na roho muda mfupi tu. Aliongoza njia huku chozi likimtoka kisha askari wengine wakiweka mapanga yao na kwenda chini kutoa heshima ya mwisho kwa binti wa Mfalme baada ya kutambua Saadie amekufa kikatili.

Huku upande wa pili Malkia alifika kwenye chumba ambacho Mfalme alikuwepo. Alipoingia tu macho yake yakagongana na macho ya Mfalme wakabaki kutazama. Hakuonekana mwenye furaha Malkia hasa uso wake ulioonesha kutokuwa na furaha hata kidogo. Alimsogelea Mfalme hadi pale alipo akizidi kumtazama.
"Hivi una roho ya kinyama kiasi gani wewe mwanaume? Hivi ni kweli unaamua kuonesha ushetani wako hata kwa binti yako, nilitegemea uwe baba mzuri kwa binti yetu lakini mwishowe umekuwa ndio adui namba moja kwake. Aah siamini kwakweli.!"aliongea Malkia huku machozi yakimbubujika kwa uchungu baada ya kuambia maneno na Alie muda ule.
"Unaongea kuhusu nini mkewangu mbona sikuelewi?"aliongea Mfalme na kumsogelea mkewe kutaka kumshika.
"Ushinishike.. siwezi kuvumilia ukatili wako mpaka kwenye familia yako. Na imekuwaje ukanyamaza kimya bila kunambia kilichotokea siku ile Alie alipotaka kutuua, kumbe nilishauliwa muda mrefu lakini kwa ujinga wako ukaona mimi ni bora kuliko binti yetu. Kwanini usingeniacha mimi nipumzike kwa amani ili binti yetu apate kuwa kiongozi bora kwa taifa hili, kwanini lakini umemkatisha ndoto zake angali bado mdogo.?!"aliongea Malkia kwa huruma sana lakini maneno yake yote yalikuwa mapya na yenye kumchanganya akili Mfalme baada ya kuambiwa kuwa yeye ndiye mhusika wa yote. Alimkamata kwa nguvu Malkia kwenye mabega yake.
"Unaongea kuhusu nini wewe mbona sikuelewi. Nimtoe Saadie nimpeleke wapi? Mwanangu ni mzima hadi leo. Na kuhusu swala lako ilikuwa ni bahati mbaya tu na hatukutaka watu wajue maana kila mtu anafahamu kwamba wewe ulikufa sasa isingekuwa rahisi kuwaaminisha watu kwamba bado umzima."aliongea Mfalme alijaribu kumwelewesha mkewe lakini hawakuwa wenye kuelewana. Muda huohuo Mlango uligonjwa na kuwafanya wawili hao watazame mlangoni, aliingia Kamanda mkuu akiwa amelowa damu huku akiwa amembeba Saadie kwa mikono miwili. Askari wengine walikuwa nyuma yake wakisogea taratibu kuwafuata viongozi wa taifa hilo. Mfalme na Malkia walishikwa na butwaa baada ya kumuwona binti yao akionekana kulegea juu ya mikono ya Kamanda huku damu zikitiririka kutoka shingoni mwake. Malkia alishindwa kuvumilia hali ile akajikuta akidondoka chini na kupoteza fahamu. Askari wawili walikimbiakwenda kumpa msaada huku Mfalme akiwa amesimama tu hajielewi, haamini kilr ambacho anakiona mbele ya macho yake.
Kamanda alisogea karibu kabisa na Mfalme kisha akapiga magoti kwa heshima akiwa amemshika Saadie na taratibu akamuweka chini binti huyo.
Taratibu Mfalme akapiga magoti na kuanza kunyanyua mikono yake ikionekana kutetemeka, haamini kile aonacho mbele yake.
"Sa....Saad...iee.!! Binti yaa...ngu!"alijikuta anashindwa hata kuongea kwa ufasaha. Aliushika mwili wa binti yake na kumsogeza kabisa kwenye miguu yake. Chozi lilimtoka Mfalme na kushindwa hata kujizuia kulia kwa sauti. Alimkumbatia binti yake huku akizidi kulia kwa uchungu sana. Kilio ambacho kila askari aliyeko mule ndani aliguswa na wao wakaanza kutokwa na machozi.

Lutfia alikuwa bado amekaa tu chini haelewi ataanzia wapi. Muda huohuo mwanga mkali ulipata kumulika pale alipo na punde akatoke Kasam pale alipokaa Lutfia. Alipomtazama akabaki kusikitika tu, alisogea hadi pale na kumsikia mkono Lutfia.
"Hupaswi kukaa tena hapa tuondoke."alisema Kasam akitaka kumnyanyua Lutfia ambaye hakutaka kwenda popote, aliutoa mkono wake kuonesha hataki kwenda huko anakopelekwa.
"Naomba niache, siwezi kuondoka popote pale."aliongea Lutfia akionesha kuchukia sana. Kasam alimtazama na kutambua jinsi gani binti huyo alivyoumia na kifo cha mwenzake.
"Alichosema Saadie yupo sahihi, tambua kwamba kwasasa adui mkubwa wa Maskoof ni wewe Lutfia.

Huku kwa Mfalme alipata kuelezwa kila kitu na Kamanda mkuu kuhusiana na kifo cha binti yake. Alibaki kucheka sana baada ya kufahamu kuwa Lutfia ndiye aliyemuua Saadie. Kicheko ambacho mwishowe kilimtoa machozi ya hasira.
"NAMUHITAJI AKIWA MZIMA AU AMEKUFA, KAMA MTAONA NI KAZI KUMBEBA NILETEENI HATA KICHWA CHAKE NIAMINI KWAMBA MLIMPATA LUTFIA MKAMUUA." alitoa amri hiyo Mfalme akiwa ametapakaa damu nguoni kwa kumkumbatia binti yake. Kamanda mkuu alipokea amri hiyo, akanyanyua na kugeuka nyuma kuwapanga askari wake namna ya kuanza kazi.
Huku Mfalme alifikiria sana kuhusu mwanaye na jinsi alivyokuwa akisemwa na mkewe kuhusu kumtoa Saadie ili Malkia apate kuwa hai tena. Alikumbuka kuwa aliyemfufua Makia ni Lutfia hivyo huenda alifanya kusudi Malkia awe hai ili Saadie apate kuwa mfu. Alipolitambua hilo hakuona umuhimu wa yeye kukaa kusubiri aletewe mwili wa mbaya wake. Taratibu alimuweka binti yake pembeni na kumbusu kwenye paji la uso kisha akasimama akionekana kuwa mwenye hasira usoni.
Alinyoosha mkono pembeni kuonesha anahitaji kitu, askari mmoja alipoona hivyo akatambua nini anataka Mfalme, haraka akasogea sehemu ambayo kuna mapanga ya thamani akaenda kuchukua panga moja na kumkabidhi Mfalme. Alilishika sawiya kisha yeye akawa wa kwanza kutoka nje na kumfanya hata kamanda mkuu ashangae. Hakuwa na jinsi naye akamfuata huku askati wengine wakafuata. Kila mtu alipanda kwenye farasi wake huku majeshi mengine yakibeba mikuki na mishale wakiwa wanatembea. Ilitolewa amri moja tu atafutwe LUTFIA popote pale alipo auawe. Mfalme alianzisha msafari huo akiwa juu ya farasi kumsaka Lutfia wakijua ndiye aliyesababisha kifo cha binti wa Mfalme, Saadie.

LUTKAS SEHEMU YA 27


# ILIPOISHIA
Mfalme alianzisha msafari huo akiwa juu ya farasi kumsaka Lutfia wakijua ndiye aliyesababisha kifo cha binti wa Mfalme, Saadie.

# TUENDELEE
Haikuwa rahisi kwa Lutfia kuweza kukubali kirahisi kuweza kuondoka Maskoof. Alijua endapo akiondoka atawaacha watu katika wakati mgumu. Alichokihitaji yeye ni kubaki ili amalizane na Alie katika ardhi hiyo ambayo ameweza kumwaga damu za watu humo. Kasam alipoona ubishi wa binti huyo unazidi kuwa mkubwa alichukua uamuzi wake yeye mwenyewe, alimkamata mkono Lutfia na punde tu wakapotea eneo lile na muda huohuo Mfalme Yazid na askari wake ndio walikuwa wakipita eneo lile bila kuona chochote. Waligawana maeneo kila mtu akipita sehemu yake ikiwa ni njia ya kumtafuta Lutfia kwa kile kilichotokea.

Huku nyuma Malkia alipata kurudisha fahamu na kujikuta yupo kitandani. Akajitahidi kunyanyuka pale kitandani huku akiangaza macho yake huku na kule asijue amefikaje pale kitandani. Alikumbuka mara ya mwisho walikuwa wakijibizana na Mfalme juu ya swala lake baada ya kutambua kwamba alikufa lakini anashangaa kusikia amerudishwa tena kuwa hai. Na kitu pekee cha mwisho kuona ni mwili wa binti yake Saadie ukiwa umebebwa na Kamanda huku ukiwa umelowa damu na hakufahamu kiliendelea kitu gani.
Alipolifahamu hilo haraka akakurupuka pale kitandani na kutaka kwenda kumtazama binti yake ili apate kujiridhisha kile ambacho alipata kukiona mara ya mwisho. Mwili wake ulitetemeka akiwa anatembea hadi alipofika sehemu ambapo mwili wa Saadie hadi ulipopatwa kuhifadhiwa. Hapo ndipo akaamini kweli binti yake ameiaga ardhi ya Maskoof angali bado mdogo sana. Alienda chini kwa kukosa nguvu na kupaki kupiga tu magoti huku akishuhudia askari kadhaa wakiwa wanaweka vichwa vyao chini kama kutoa heshima ya mwisho kwa binti huyo wa kifalme. Taratibu taarifa za kufariki kwa Saadie zikaanza kusambaa ndani ya falme nzima hadi ikaanza kutoka na nje baadhi ya watu wakapata kusikia taarifa hiyo ambayo kila mmoja wao ilimshangaza sana na hata wengine ambao walipata kumwona binti huyo kwa umbo na maneno yake kwa watu wa kawaida.

Kifo hicho hakikuwa cha kawaida kwa Malkia ambaye akili na mawazo yake ni kwamba Mfalme Yazid ndiye aliyeyafanya haya kama alivyoambiwa na Alie muda ule kuhusu swala la yeye kurudi kuwa hai ili Saadie apate kufa.
Hata alipowasili Mfalme katika chumba kile alichopumzishwa Saadie mtu wa kwanza kunyanyuka pale alikuwa ni Malkia ambaye alimsogelea Mfalme akiwa anatembea na kuanza kumtwanga makofi Mfalme huku akiyasema yale yote yaliyo moyoni mwake. Maneno yake yakawa mapya na mshangao kwa baadhi ya watu ambao hawakuelewa hayo yote hususani askari walioongozwa na Kamanda mkuu ambao siku hiyo walimshuhudia Lutfia ndiye aliyemuua binti wa Mfalme.
Kamanda Mkuu alipoona hali ile aliwahi kwenda kumzuia Malkia ambaye alionekana kuchukia sana.
"Unachokisema hapa mbele za watu humu ndani sio kweli. Mfalme alituagiza sisi twenda kumtafuta Saadie ili apate kuwa salama maana amekuwa akihisi hata Lutfia si mwema tena. Na kitendo cha sisi kuendelea kumtafuta Saadie ndipo tulipata kushuhudia kwa macho yetu Lutfia akijaribu kummaliza Saadie maana tayati alishamdhuru sehemu mbaya sana shingoni. Tulipotaka kumuwahi kumdhibiti alitupotea. Na ndio maana muda ule mliona tumeingia na mwili wa Saadie pale akiwa tayari kafariki, ikapelekea hata wewe kupoteza fahamu maana ni tukio ambalo hakuna asiyeumizwa nalo. Tumeumia kwakweli naomba uelewe sio Mfalme aliyehusika na hili."alisema Kamanda akijaribu kumueleza Malkia aliyekuwa hana analofahamu. Maelezo hayo ndio yakamfanya atambue chanzo cha kifo cha binti yake. Jina la Lutfia likamfanya ashangae kuona ndiye mhusika wa hayo, hakuweza kuamink mapema maana amekuwa akimuamini binti huyo na hata ukaribu wake na Saadie ulikuwa wa aina yake.
"Hapana kwakweli Lutfia hawezi kufanya unyama wa aina hii kwa binti yangu, hilo nakataa."
"Huo ndio ukweli Malkia wangu. Siwezi nikadanganya angali kila kitu kimeonekana na watu wengi. Lutfia ndiye aliyemuua binti yako."alisema Kamanda mkuu kwa kujiamini hasa. Taratibu Malkia akaanza kupoa na kuamini huenda ikawa kweli. Alipolifahamu hilo ikawa ni kama kasikia upya kwamba binti yake ameuawa, alilia sana kiasi cha kumfanya Mfalme azidi kumchukia Lutfia kwa kuona ndiye aliyeleta majonzi hayo katika falme.

Haikuwa tena siri ndani ya Maskoof kwamba binti wa kifalme amefariki lakini habari mpya ni kwamba Malkia yupo hai. Taarifa hizo mbili ziliwashangaza sana watu na hata wengine wakibaki njia panda wasielewe swala hilo linaendaje. Ilibidi wazee wa taifa hilo wakae kikao cha muda pamoja na Mfalme kumueleza hali halisi huko mitaani inavyoendelea baadhi ya watu wakihisi vibaya huenda kuna njia za kichawi zilifanyika kumuua binti huyo mdogo ili Malkia apate kurudi upya. Walikaa kusubiri maelezo ya kina kutoka kwa Mfalme juu ya swala hilo na mwisho hakusita kuwaeleza ukweli wote hadi binti yake kuweza kupata umauti ili kuwatoa hofu dhidi yake.
"Adui wa familia yangu kwasasa ni huyu binti Lutfia, sitakuwa na huruma naye wala kumsikiliza pindi nikimuona. Saadie wangu hakuwa na ubaya na mtu hata kidogo, alimuonesha upendo muda wote na ni yeye Saadie ndiye aliniaminisha mimi kuwa Lutfia ni mtu mzuri kumbe ndio anamtetea adui yake. Naweka nadhiri mbele yenu endapo nikimpata huyu binti, kichwa chake ni halali kwangu."aliongea Mfalme kwa uchungu kuonesha kweli amechukia. Wazee walitazama baada ya kufahamu kwamba kweli Mfalme swala lile limemgusa kutoka moyoni. Walimpa moyo tu na kumliwaza kutokana na msiba huo wa binti yake.

Kasma akiwa katika harakati za kuendelea kumsaka Alie bila kujua lolote linaloendelea alijikuta akishikwa mkono na kupotea gafla bila hata yeye kufahamu. Muda mfupi tu akaja kutokea ndani ya msitu mmoja tena akiwa pekeake. Alibaki kushangaa tu huku na kule bila kumwona mtu yeyote yule.
"Nani amenileta huku? Hapa ni wapi?"ni maswali ambayo yalitawala akilini mwake bila kupata jibu kamili. Alizidi kuangalia eneo lile alio na alipolitazama vizuri akafahamu kwamba hapo ni pale ambapo yeye pamoja na askari wake kwa mara ya kwanza walikuwa wakisubiri njia ya kuelekea Maskoof na kikatokea kimbunga kilichowaaminisha kuwa ndio njia pekee ya kufika huko. Alipatazama vizuri na kweli akapata kuona kuna baadhi ya vitu ikiwemo chakula walivyovibeba kutoka kwao ambavyo waliviacha pale na kuingia ndani ya kimbunga. Alishangaa sana baada ya kufahamu hilo maana ni muda mchache tu alikuwa ndani ya Maskoof. Alisogea taratibu hadi kwenye vyakula vile na kufunua , havikuweza kuharibika kabisa japo ni siku kadhaa zimepita tangu waviache hapo. Hakuwa mwenye kuhofia alianza kula bila wasi huku swali lililobaki akilini mwake ni nani aliyemleta hapo.

Huku upande wa pili kwenye msitu huohuo Kasam aliweza kuonekana akiwa na Lutfia wakiwa wamesimama.
"Sikia nikwambie Lutfia, swala la wewe kurudi Maskoof sasahivi hebu lifute kabisa. Hakuna ambaye hafahamu kwamba wewe ndiye umehusika na mauaji hayo, wewe ni adui wa Maskoof nzima kwasasa usifirie kuna ambaye atakuelewa kwa hili tukio."alisema Kasam akimuelewesha Lutfia.
"Lakini sikufanya mauaji mimi iweje nihofie kitu ambacho sijahusika?"
"Lutfia, wenzako hawaelewi hilo, Alie ametumia sura na mwili wako kumuua Saadie na askari wengi wameona tukio hilo wakajua ni wewe. Sasa Malkia pamoja na Mfalme wote wanajua kiwa wewe ni adui na wala hawana mawazo tena na Alie. Na ndio maana nakwambia huu sio muda wa kuifikiria Maskoof tena."alisema Kasam na kumfanya Lutfia ajisikie vibaya. Alie amempa kesi kubwa sana ambayo kweli hawezi kuizuia. Alimfikiria Saadie ambaye kwake aliona ni kama ndugu kwa ukarimu wake na ukaribu waliokuwa nao. Alijikuta akitafuta sehemu na kukaa kwanza kutuliza akili. Alikumbuka kipindi akiwa kwao aliwahi kusoma kitabu cha LUTKAS na kuona alipata kesi ya kumdhuru mtoto wa Mfalme hivyo anatafutwa kwa hamu. Na ni Kasam ndiye aliyeonekana akimshauri akimbilie katika mji wa Maskoof maana una amani, leo imekuwa kinyume tena anaikimbia Maskoof. Jina la Alie lilitawala katika kichwa chake akijua ndiye aliyetengeneza mambo yote hayo ya kuonekana yeye ndiye mbaya katika familia na taifa zima la Maskoof. Hasira zilimpanda na kujikita alipiga kelele kumuita Alie adui namba moja kwake, kelele zilisikika ndani ya msitu wote na kufanya hata wanyama washangae na wengine kujificha katika makazi yao. Alie alipata kusikia sauti ile akiwa ndani ya Madkoof, alifurahi sana kuona tayari amemchoma Lutfia na ndicho kitu ambacho alikuwa akihitaji ili mambo mengine yaendelee.
Kelele zile zilimfanya Kasma pale alipo ageuke kusikiliza zinapotokea.
"Lutfia!"alishangaa Kasma baada ya kufahamu kuwa ni sauti ya mwenzake. Haraka akapotea pale alipo kufuata sauti ile ilipo.

Maskoof ilijawa na majonzi, kila mtu aliyemfahamu binti wa Mfalme alikuwa mwenye majonzi hasa kwa umri alionao. Taratibu za kufanya mazishi zilifuata huku hali ya Malkia ikiwa si nzuri, hakuwa mwenye nguvu za kusimama imara, muda wote alikuwa anashikwa na wafanyakazi waliokuwa wakimfariji. Taratibu zilienda kama ilivyopangwana muda ulipofika ratiba za mazishi zikaendelea.

Lutfia baada ya kutafakari kwa muda mrefu na kuhakikisha hasira alizonazo zimeshuka alinyanyuka pale alipo na kumsogelea Kasam aliyekuwa anamtazama muda wote.
"Tunafanyaje sasa?"aliuliza Lutfia akiwa anamtazama Kasam. Muda huohuo Kasma naye alitokea mbele yao na kuwaona wawili hao wakiwa wanatazamana.
"Nini kimetokea? Mbona sielewi.?"aliuliza Kasma akiwa hana lolote analojua.
"Ni mimi ndiye niliyekuleta huku upate kuwa salama, Maskoof imeingia doa hasa kwenu ninyi na ni kwadababu ya mtu mmoja tu. Alie amejibadilisha kuwa kama Lutfia kisha amemuua Saadie na ameonekana na askari wa kifalme. Hivyo kila mtu anajua kuwa Saadie ameliwa na Lutfia."alisema Kasam akiwa anamueleza Kasma.
"Ati nini? Saadie ameuawa?"hakuamini Kasma kile ambacho anaambiwa na Kasam. Alihuzunika sana kusikia taarifa hiyo ambayo ni mbaya kwa wote.
"Kasam, naomba niambie kitu gani tufanye."aliongea Lutfia akionekana kuwa makini na kile anachozungumza.
"Lutfia.. mimi sina chochote ambacho naweza kufanya kwasasa. Wewe na mwenzako Kasma ndio mnatakiwa mlimalize hili jambo. Kwasasa kuna kazi ya kusaidia taifa la Kasma, kuwadhibiti wafu wote ambao wameteka falme hiyo na kuanza kuwaua watu wazidi kuwa upande wao."alisema Kasam akiwaeleza mabinti hao wawili wakiwa makini kumsikiliza.
"Na vipi kuhusu Saadie maana ni mwenzetu pia.?"aliuliza Kasma.
"Nahisi baada ya muda ndio atazikwa, watu wengi watafurika kumzika. Mnapaswa kwenda kumchukua mapema kabla ya kufukiwa mwili wake na msionekane na mtu yeyote yule, mnafahamu jinsi mlivyofanana hivyo hata ukikamatwa Kasma basi utaonekana ni Lutfia tu. Naamini kwa ushirikiano wenu mtamaliza jamii yote ya Alie na hata amani itarejea tena, naomba niwaache mlifanyie kazi jili swala kama tutaonana tena sawa."alisema Kasam na kuwaaga mabinyi hao kisha akapotea. Waligeuka kutazamana baada ya kufahamu wanakazi ya kufanya tena zote ni muhimu.
Hakutaka kupoteza muda Lutfia alikitoa kitabu cha LUTKAS kukishika mkononi, Kasma naye alijisogeza kisha akakamata kitabu kile papo hapo wakapotea ndani ya msitu ule safari ikielekea Maskoof kumchukua mwenzao.

LUTKAS SEHEMU YA 28


#ILIPOISHIA
Hakutaka kupoteza muda Lutfia alikitoa kitabu cha LUTKAS kukishika mkononi, Kasma naye alijisogeza kisha akakamata kitabu kile papo hapo wakapotea ndani ya msitu ule safari ikielekea Maskoof kumchukua mwenzao.

#TUENDELEE.
Watu walifurika uwanjani kwaajili ya kusubiri kuuaga mwili wa Saadie kwa mara ya mwisho. Mfalme na Malkia waliwasili kwenye uwanja huo na kukaa sehemu maalumu wakisubiri askari kuuleta mwili wa binti yao ambaye hadi muda huo Malkia hakuwa mwenye kuamini wazi kwamba Saadie amefariki. Kwake ilikuwa kama utani tu unaoendelea lakini ni ukweli usiopingika. Muda huohuo Lutfia pamoja na Kasma waliwasili kwenye mjengo wa kifalme na bila kuchelewa wakawa wanaelekea mahala ambapo miili ya marehemu huwekwa humo kabla ya kuelekea kwenye mazishi.
Ndani ya uwanja Alie alikuwa miongoni mwao kushuhudia kwamba kile alichokifanya kimeenda kama alivyopanga yawe. Na muda mfupi askari walikuwa wanawasili katika uwanja huo ulioongozwa na Kamanda mkuu wote wakionesha sura za huzuni usoni mwao huku jeneza lililokuwa na mwili wa Saadie likiwa mabegani mwao wakisogeza katikati ya uwanja. Malkia alijikuta akianza upya kuangusha machozi lakini Mfalme akawa na kazi ya kumfariji huku kelele za baadhi ya watu zikisikika wakilia pia. Alie alibaki kuangalia tu huku furaha ikitawala moyoni mwake.

Askari hao walifika na kuuweka mwili ule sehemu husika kisha eakatoa heshima na kurudi nyuma. Iliwabidi Mfalme na Malkia wasogee eneo lile wapate kuuaga mwili wa binti yao. Kila mtu aliwaonea huruma kwa pigo lile maana ni mtoto pekee kwenye familia hiyo. Haikuwa na jinsi Malkia alipata kumwona binti yake akiwa kwenye amelazwa kwenye jeneza tayari kwa kuweza kupumzishwa. Alilia sana kumpoteza binti yake huku Mfalme akizidi kumfariji. Hata walipomaliza walitejea sehemu zao na kuwaruhusu wazee na wafanyakazi wa falme wauage mwili wa marehemu. Baada ya kila kitu mwenda sawa walisogea askari kadhaa na kunyanyua jeneza lile kusogeza sehemu iliyochimbwa ili upate kuhifadhiwa mwili. Mfalme na Malkia walibaki kushuhudia tukio lile likitaka kufanyika.
"Mama....!"ilisikika sauti masikioni mwa Malkia na kumfanya ashtuke. Aligeuka kutazama kama kuna mtu nyuma anamuongelesha lakini hakupata kuona yeyote, hata Alie pale aliposimama alipata kusikia sauti ile kwa uwezo alionao. Akabaki kutafuta sauti ile inapotokea.
"Mama ni mimi mwanao... Saadie."ilisikika tena sauti ile na kuzidi kumchanganya Malkia, Mfalme alimshangaa mkewe kumwona gafla amekuwa kama anawasiwasi.
Alie alisimama pale alipokaa baada ya kusikia jina la Saadie binti aliyemuua kwa mikono yake. Alijikuta akibadilika macho na kuanza kuangaza uwanja mzima kwa umakini, alihisi kupagawa baada ya kusikia sauti ya binti huyo akionesha kuwa bado yuhai.
Malkia pale alipo akasimama huku akigeuka kila pande kutazama.
"Wewe ni nani?"aliuliza Malkia akitaka kujua sauti ile inapotokea hata kumfanya Mfalme anyanyuke.
"Kuna nini kwani mbona sikuelewi?"aliuliza Mfalme bila kupata jibu.
"Mama mimi ni mwanao Saadie, nakuomba sana mama yangu usioneshe utofauti wowote mbele za watu wakahisi unaongea na mimi, na naomba wasishuhudie hicho kinachokwenda kufanyika hapo maana watazidi kuwa na wasiwasi juu yangu hapo mbele. Mimi ni mzima mama na Lutfia ndiye amenisaidia, hana kosa lolote na hajaniua yeye kama mlivyodhani."ilisikika sauti ya Saadie na kumfanya Alie kule alipo ashtuke baada ya kusikia kuwa binti huyo yupo hai tena na mtu pekee aliyemrudisha ni Lutfia.
"Mwanangu... uko wapi?"aliuliza Malkia na kauli yake hiyo ikamfanya hata Mfalme ashangae. Alimtazama mkewe na kuhisi huenda kuna jambo linaloendelea. Haraka akawasimamisha wale askari wasishushe jeneza lile kwenye kaburi, nao wakatii.
"Tuna kazi ya kwenda kufanya sehenu ila nitakaporejea ndio nitaongea kila kitu. Hapo hakuna aliyekufa mama tumeweka mfano wa mwili wangu ili watu waamini hivyo lakini mimi nipo mama pamoja na wenzangu tunaenda sehemu. Yote haya ameyafanya Alie kutuweka tuwe tofauti lakini mimi ndiye nafahamu kila kitu. Msimchukie Lutfia hausiki na lolote, yeye ndio msaada kwangu, mueleze na baba hivyo wacha sisi tuwahi kuna mahala tunaenda."alisema Saadie na kule alipo wenzake walikaa kimya amalizane na wazazi wake. Walisimama imara mabinti hao watatu wakiwa wanatazama umati uliofurika kwenye uwanja huo kwaajili ya kumuaga Saadie aliyesadikika kufariki.
"Huyu mpumbavu maamini atakuwa humu uwanjani naye akishuhudia kinachoendelea."alisema Kasma akihisi Alie atakuwepo miongoni mwa watu waliofika uwanjani.
"Hakuna haja ya kumfuatilia kwasasa, tuna kazi ya kulitetea taifa lako kwanza naamini hata Maskoof tutaiacha salama endapo akisikia kuwa tupo kule naye atakuja tu."alisema Lutfia akiwaeleza wenzake huku akiwa ameshika LUTKAS, kitabu ambacho kimetumika kumrudisha Saadie tena kuwa hai. Walikubaliana naye na kuona hakuna haja ya kumfuatilia Alie tena. Walishikana na punde tu wakapotea safari ikielekea kwenye ufalme uliokuwa unaongozwa na Kasma akiwa kama Malkia wa taifa lao.

Alie baada ya kutambua hilo alinyanyuka haraka pale alipo na kuanza kuondoka kwenye umati ule wa watu asijulikane kama yeye ni nani. Alipofika mbele alibadilika na kuwa na sira ya kazi. Aliangaza macho yake huku na kule kujaribu kama ataweza kujua Saadie yupo wapi lakini haikuwa rahisi. Alishikwa na hasira sana na kujikuta akiupiga ukuta ngumi yenye uzito hadi kuweza kuweka ufa kwenye kuta. Hakutaka kubaki tena pale alipotea haraka kujua wapi atampata Saadie tena.

Malkia pale alipo alimgeukia Mfalme akionekana kuwa na shauku ya kitu.
"Nimesikia sauti na mwanangu, inamaana hakufa?"aliyasema hayo Malkia na kumfanya Mfalme ashangae.
"Unasemaje?"alistaajabu Mfalme baada ya kuambiwa hivyo. Wote kwa pamoja walipiga hatua kusogea hadi lilipo jeneza ambalo lilikuwa na mwili wa Saadie huku askari kadhaa wakiwa pembeni. Hata walipofika kulitazama waliona dhahiri mwili wa Saadie ukiwa mule ndani. Waligeuka kutazamana wote wawili na kuanza kuamini huenda ikawa kweli kile kilichosema na sauti ile ya Saadie kwamba yupo hai. Ilibidi Mfalme amuite Kamanda mkuu na kumpa maelekezo kisha viongozi hao wakaanza safari ya kurudi kwenye falme, watu wakabaki kushangaa tu.
"Wananchi wa Maskoof, kuna mambo yamejitokeza hapa muda huu hivyo Mfalme ameniagiza niwataarifu wote kwamba kwasasa kila mtu arudi kwake aendelee na shuhuli za kila siku. Kuhusu mazishi na taratibu za msiba mtapewa taarifa muda wowote, hivyo kila mtu arudi kwake kuanzia sasa."alisema Kamanda mkuu kwa sauti ya ushababi iliyosikika na mamia ya watu. Walistaajabu kuambiwa hivyo huku kila mtu akijawa na maswali kwenye kichwa chake wasipate jibu kamili. Kila mtu aliongea lake huku wakianza kutoka ndani ya uwanja taratibu. Hata Kamanda mkuu mwenyewe hakuweza kuelewa kwa kina zaidi sababu ya kukatisha mazishi yale.
Hata walipofika ndani Mfalme alikuwa wa kwanza kumhoji mkewe juu ya swala zima la bonti yao.
"Umeongea na Saadie! Anasemaje? Na yupo wapi?"
"Amesema yupo na wenzake kuna mahali wanaenda, ila ameniambia tu kwamba swala hili Lutfia hausiki kabisa."
"Hausiki? Kivipi wakati ameonekana kwamba ndiye?"
"Hiyo ni njama tu ya Alie."alisema kwa ufupi Malkia na Mfalme aliposikia jina la Alie hata yeye alitulia maana anamjua, na huenda ikawa kweli.
Walishindwa kuelewa nini wafanye na wote wakabaki kutafakari namna ya kufanya.

Taifa la Kasma lilikuwa katika hali mbaya. Wafu walizidi kuua watu na kuwafanya kuwa upande wao ili wazidi kuongeza nguvu ya jeshi lao. Hii ni amri ambayo Alie aliwaamuru kufanya hivyo ili kuweza kulitawala taifa na wamefanikiwa kwa asilimia kubwa. Hata baadhi ya wananchi waliobaki waliogopa hata kutoka ndani ya makazi yao na wengine kuamua kuhama kabisa makazi ili kuwaepuka wafu hao wanaozidi kuua kila kukicha.
Mama mmoja alipata kuonekana kukimbia haraka huku mara kwa mara akiangalia nyuma alipotokea. Ni wazi kwamba alikuwa akifuatwa na mmoja wa wafu ambao wanahitaji kuwachukua wananchi hao kuwa jamii yao. Alipoona mama yule anazidi kutokomea kwa mbio haraka akapotea na kuja kutokea mbele ya mama yule aliyepiga mweleka kwenda chini baada ya kushtushwa na kiumbe ambaye alionekana kuoza kwenye baadhi ya sehemu zake za mwili.
Taratibu akaanza kumsogelea mama yule ambaye alikosa hata nguvu ya kusimama kwa woga na wasiwasi, alibaki kujiburuza tu kurudi nyuma huku macho yake yakimtazama kiumbe huyo aliyeonekana mfu aliyefufuka.
Mama alibaki kuomba aachiwe huku akijitahidi kuuburuza mwili wake kurudi nyuma.
Kuua kwao ilikuwa ni amri hakukuwa na huruma wala msamaha kwa binadamu au raia yeyote ndani ya falme ile inayotawaliwa na wafu kwasasa. Aliongeza mwendo wa kumsogelelea mama yule hadi alipomfikia, taratibu akaanza kunyoosha mikono yake lengo ni kumkamata mama yule apate kumnyonya damu shingoni. Mama alipiga kelele nyingi sana za kuomba asaidiwe lakini hapakuwa na mtu wa kumsikiliza, mji mzima ulitawala wafu. Alibaki kufumba macho yake kwa woga huku akinyoosha mikono yake amzuie yule mfu huyo.
Sekunde, dakika zikapita hakuona mwili wake kuguswa na mfu huyo. Ikibidi tayari afumbue jicho lake moja kichungulia nini kimejiri. Ajabu aliona mfu yule ameganda tu pale huku mikono yake ikionesha dhahiri alikuwa anataka kumkaba mama yule. Kwa tukio lile likikuwa la ajabu kwa yule mama ikabidi afumbue jicho la pili na kuishusha kabisa mikono yake akapata kumwona vizuri yule mfu akiwa ameganda pale.
Gafla akatokea Kasma na kujisogeza hadi pale alipo mama yule.
"Malkia...!"alishtuka mama yule baada ya kumwona kiongozi wa taifa lao Malkia Kasma akionesha kuwa na tabasamu usoni. Mama yule alishuka kupiga goti moja chini kumpa heshima binti huyo ambaye alimshika mabega kumtaka anyanyuke.
"Malkia... mji umevamiwa, watu wamehama makazi yao na wengine kujifungia ndani yapata muda mrefu sasa. Hapa nimetoka kwangu baada ya watoto wangu kuuawa nikaona sina haja ya kubaki tena ndani nami ndio nilikuwa nahama niende kutafuta mji mwengine wa kuishi ili nipate kuwa na amani."alisema mama yule kwa uchungu hadi Kasma akajisikia vibaya.
"Pole sana mama yangu, nahisi ni makosa yangu na kutokuwa makini na uongozi wangu imepelekea wananchi wangu kupatwa na matatizo haya. Wala hupaswi kwenda popote, wewe ni mzaliwa wa taifa hili, si vyema kuondoka maana Malkia wako amerejea tena kuwatoa hawa walioharibu na kuleta huzuni ndani ya taifa hili."aliongea Kasma akiwa amemshika mkono mwananchi wake.
"Malkia wangu, hawa wafu ni wengi sana na kila siku wanaua watu na kuwafanya kuwa jamii yao hivyo kila siku wanazidi."aliongea mama yule na muda huohuo Lutfia na Saadie wakapata kutokea na kusogea hadi pale waliposimama Kasma na mama yule ambaye alishangaa kuwaona mabinti hao walipotokea. Alipomtazama Lutfia alishangaa na kustaajabu, ikabidi ageuke kumtazama Malkia Kasma na kuona ndio vilevile ufanano wao.
"Inamaana una ndugu yako Malkia?"aliuliza Mama yule
"Hapa unapotuona wote wa tatu ni ndugu. Nguvu nilizonazo mimi na hawa wanazo pia. Na tumekuja lengo ni moja tu, kuirudisha falme iwe mikononi mwetu, tuwamalize hawa wafu wote waliosababisha vifo kwa wenzetu na mwisho ni kuwarudisha ndugu zetu ambao wamekimbia taifa hili kwenda kujistiri kwengine."alisema Kasma akimuaminisha mama yule. Alipowatazama mabinti hao watatu akapata amani moyoni na kuhisi huenda kweli wakaifanya kazi hiyo kama alivyosema Malkia Kasma. Alikubaliana naye kwa kile alichokisema na muda huohuo Lutfia akasogea hadi alipo yule mfu aliyegandishwa, alimshika tumboni na kushudia moto ukiwa na kuanza kumuunguza yule mfu huku kelele zake zikisikika kwa nguvu akiugulia kuchomwa moto. Mwili ulionekana kubadilika badilika, sura za watu zaidi ya watano tofauti wakibadilika tu huku wakilia wote kwa kuchomwa moto huo. Yule mama akabaki kushangaa akijionea maajabu hayo kwa macho yake.
"Huyo alikuwa anatembea na watu watano kwenye mwili wake , hivyo hata wenzake huko walipo wameshajua kuwa kuna wenzao watano wameuawa. Hakuna dawa nyengine ya kuwapunguza zaidi ya kuwachoma tu."aliongea Lutfia na kumsogelea mama yule pale aliposimama.
"Mama wewe kuwa na amani tu, ongozana nasisi hadi utuoneshe unapokaa tukakupumzishe maana tuna kazi kubwa ya kuwamaliza hawa na hatakimbia hata mmoja, usikimbie taifa lako na tegemea amani muda mfupi."alisema Lutfia akimjaza imani mama yule ambaye hakuwa na wazo tena la kuondoka. Mabinti watatu wakaanza kuongozana na mama huyo kumpa ulinzi hadi kwake. Na walipohakikisha ameingia ndani wakaufunga mlango na muda huohuo macho yao yakabadilika kuwa makali yenye kutisha, wakageuka kutazamana kila mtu akionekana kuwa tayari kuingia kazini.

LUTKAS SEHEMU YA 29


#ILIPOISHIA
Na walipohakikisha ameingia ndani wakaufunga mlango na muda huohuo macho yao yakabadilika kuwa makali yenye kutisha, wakageuka kutazamana kila mtu akionekana kuwa tayari kuingia kazini.

#SONGA_NAYO
Falme ya taifa hilo lilijawa na wafu waliokuwa wakizunguka kila sehemu kana kwamba makazi yao ya kudumu. Baadhi yao walikuwa wakikilinda kiti cha kifalme wakitegemea Alie ndiye atakuja kukaa hapo kuwaongoza kama Malkia wao. Hakika walitanda kila sehemu ya jumba hilo wakiweka ulinzi kuhakikisha hakuna kiumbe aitwae binadamu aliye hai anaingia tena ndani ya falme hiyo.

Kasma pamoja na wenzake walipata kutokea mbele kabisa ya lango kuu la kuingilia na kubaki kutazama falme hiyo. Aliangalia jinsi nyumba hiyo ilivyokuwa chafu kimazingira tu na hata muonekano wake. Alikumbuka kipindi yupo kama Malkia muda wote alikuwa akiwatazama raia wake wakifanya kazi na biashara zao mbalimbali kwa amani, lakini sasa imekuwa ni tofauti mji mzima umekuwa kimya hakuna hata raia mmoja mwenye ubavu wa kutoka nje. Alijikuta chozi likimtoka na kuona ameshindwa kulinda yltaifa lake hadi viumbe visivyo na uhai kuweza kuitawala falme. Moyo wake ulipatwa na jazba ya haraka, hasira zikamjaa hali iliyopelekea apige kelele za hasira.
Kelele zilizotetemesha jengo la kifalme hiyo kwa sekunde kadhaa, raia ambao walisalia kwenye makazi yao waliposikia kelele hizo walishtuka wote na kusogea madirishani kuangalia kelele hizo zinapotokea.
Wafu wote walishtuka baada ya kuona tetemeko hilo lililoongozana na kelele kali. Haraka wakaanza kutoka nje kuangalia ni nani aliyefanya hilo jambo.
Wananchi waliokuwa madirishani walipata kushuhudia wafu hao wakitoka nje kwa wingi huku wakiangalia huku na kule kutafuta sauti ile ilipotokea bila mafanikio.
Mule ndani ya falme walibaki wachache waliokuwa wamesimama kulinda sehemu ya kukaa Mfalme. Gafla wakatokea mabinti watatu wakiwa kwenye muonekano wa kutisha huku macho yao yakiwa yenye kutisha na makali. Wafu wale baada ya kuona hivyo wakawa wakali nao wakawa tayari kwa kupambana maana waliona mabinti hao wamekuja kwa shari. Walinyanyua mikono yao juu na kutokea mapanga ya moto wakakata vyema na kuanza kuwasogelea mabinti hao ambao hawakuonesha dalili zozote za woga. Hata walipokakatibia wakantoosha mapanga yao kuwakata mabinti hao ambao kwa wepesi wa hali ya juu walipotea pale walipo na kutokea nyuma yao wakiacha wafu hao wakipitisha mapanga yao hewani bila kuwakata wahusika. Hata walipotaka kugeuka kwa nyuma mabinti walitoa nguvu zao na kila mmoja wao akapiga ngumi iliyo na uzito wa aina kuelekea tumboni mwa wafu hao ambao walirushwa kama upepo na kudondokea mbali. Sekunde chache tu wakaanza kuona miili yao ikiwaka moto na kuanza kutekekea kabisa na ndio ukawa mwisho wao. Hawakuwa na muda wa kupoteza wakina Lutfia walisonga mbele kuwadhibiti adui zao wengine.

Kule nje wale wafu baada ya kutoweza kuona lolote wakawa na mashaka juu ya sauti ile waliyoisikia. Iliwalazimu wageuze kurejea tena ndani ya falme baada ya kutoona chochote nje, lakini rejea yao haikuwa salama kama walivyotoka. Wale wafu wa mbele walipata kushuhudia vivuli vitatu vikipita katikati yao kwa kasi ya ajabu na kupotea. Punde tu wakaanza kudondoka vipande viwili kila mmoja kuonesha kama kuna kitu kimepita kuwakata, hali iliyowafanya hata wenzao waliosalia washangae kuona tukio hilo. Walishuhudia wenzao wakianza kuwaka moto na mwishowe kupotea kabisa, iliwalazimu wawe makini sasa kila mtu akiangaza machi yake huku na kule kama ataweza kuona kitu kinachosababisha mauaji hayo ya kutisha kwao.

Lutfia, Saadie pamoja na Malkia wa ardhi hiyo Kasma aliyeonekana kuwa na hasira dhidi ya wafu hao, walikuwa wakiwatazama tu wanavyohaha kutafuta wahusika. Hawakuwa na huruma nao hata kidogo walipotea gafla kuwafuta tena wale wafu kwa njia uleile, na safari hii walipita na kuwakata wafu wengi sana hali iliyowafanya wenzao wachanganyikiwe maana hawaoni kitu ambacho kinawamaliza taratibu. Pamoja na nguvu walizonazo lakini haikuweza kuwasaidia, walichoamua kila mtu ni kwenda njia yake kutafuta mwenyewe suluhisho la jambo hilo. Kiongozi wao ilibidi atafute mahala pa usalama kwanza apate kuongea na mkuu wao, Alie.
"Hali si shwari huku wenzetu wanazidi kupungua kila muda hatujui ni nini kimetokea. Kunaonekana kuna kitu tena si kimoja kinafanya mauaji haya, ni zaidi ya nguvu tulizonazo maana hatuelewi hata wanapotokea."alitoa taarifa hiyo yule mfu akiongea na Alie ambaye muda huo alikuwa akihaha kule Maskoof kuwatafuta mabinti watatu. Aliposikia taarifa hiyo akafahamu anaowasaka muda wote ndio hao anapata kuambiwa.
"Hao ni watu, wapo mabinti watatu, wametoka huku na mmoja kati yao ndiye Malkia wa taifa hilo. Nakuja haraka najua namna ya kuwadhibiti ila hakikisha mnawaepuka kwa namna yeyote ile na kama wakionekana pambaneni nao mimi nakuja."alisema Alie na kuanza kukimbia kwa kasi mwishowe akapotea.

Kasma alikuwa na hasira nao wafu wale, alikuwa anawaadhibu kisawasawa na kuhakikisha wanapotea kabisa. Walikuwa na umoja kuhakikisha siku hiyo falme inakuwa mikononi mwao maana hadi muda huo asilimia kubwa ya wafu waliwamaliza kabisa. Yule kiongozi aliyeyoka kuongea na Alie alipoona wenzake wanazidi kumalizwa ikambidi atumie njia mbadala ya kuongeza jeshi zaidi. Aliwachukua wenzake watano na kutoka nje ya taifa hilo kutafuta mji ambao hauelewi kinachoendelea. Hawakuwa na huruma walianza kuwanyonya damu na hata wengine kuwaua kwa namna yeyote, zoeizi hilo lilifanyika kwa muda mfupi tu na kufanikiwa kumaliza kijiji kizima bila kuchagua rika lolote. Walipohakikisha kazi hiyo kufanikiwa wakaanza kuwanyunyizia moshi utokao kwenye vinywa vyao. Ni kama uhai wenye asili yao, watu wote waliokufa wakaanza kunyanyuka tena wakiwa tofauti na kubaki kuwatazama wale wafu waliowafanya kuwa tena hai. Yule kiongozi na wenzake wakageuka na kuanza kutembea sasa kurudi kwenye taifa ambalo tayari washaingiliwa na Kasma mwenye taifa lake.

Iliwachukua muda hadi kuwamaliza wafu wengi ndani ya falme ile. Walibaki wakuhesabika tu ambao hawakuwa na shida, ilibidi wapambane nao hivihivi wakionana. Nguvu za ajabu zilitumika baina ya wafu pamoja na mabinti hao ambao walikuwa makini kuhakikisha kile kilichowaleta kinatimia. Wananchi walikuwa madirishani wakisikia tu sauti za watu wakilia kwa uchungu na maumivu. Iliwafanya wasielewe kabisa kitu gani kinaendelea ndani ya falme na hawakutaka kutoka nje kabisa maana hawana imani na wafu hao. Na baada ya muda kidogo walipata kusikia ukimya ukitawala, mji mzima hapakuwa na kelele yeyite zaidi ya ndege warukai angani. Hali ile ikawafanya wazidi kukodoa macho kutazama tu lango la kifalme likiwa imara limefungwa. Taratibu wakaona mlango unafunguliwa, akaanza kutoka Saadie huku akiwa anatazama mazingira yale ya nje akiwa kama mtu wa kawaida. Akafuata Kasma kutoka hali iliyowafanya wale wananchi waliokuwa wakichungulia washangae, mioyo yao ikaanza kupata amani na furaha baada ya kumwona kiongozi wao. Walitamani kutoka nje lakini nafsi haikuwa tayari kuamini kwa asilimia zote. Furaha yao iliishia madirishani tu wakimtazama Malkia wao, muda huohuo akapata kutoka Lutfia na kukamilisha jeshi lao la mabinti wa tatu. Ujio wake uliwashangaza watu wale maana alivyo ni vilevile kama Malkia Kasma. Kila mtu akawa na kazi sasa ya kushangaa wawili hao wakijaribu kuwatofautisha lakini hakukuwa na tofauti yeyote zaidi ya nguo walizovaa. Taratibu Kasma akasogea hatua kadhaa mbele na kuangalia juu ya mbigu, alimshukuru Mungu kwa kuweza kusaidia hadi kuwamaliza wafu wote waliokuwa ndani ya Falme yake na wenzake wakiwa salama kabisa. Aliangaza macho yake kwenye nyumba za wananchi wake.
"Hatimaye nimetejea tena Malkia wenu, amani ambayo mmeupoteza kipindi ambacho sipo hapa naamini imerejea tena. Hivi mnavyotuona ndivyo tumekuja kupambana na hawa viumbe ambao wamekuwa ni hatari kwa maisha yenu."alisikika Kasma akizidi kuongea kuwapata imani watu ambao wamesalia kwenye taifa lake. Na kweli taratibu baadhi yao wakamtambua kwa sauti na hata ukarimu wake.

Wakati hayo yakiendelea Alie alikuwa amewasili katika taifa huo. Alipata kutokea mbele ya wale wenzake ambao walitoka kwenye ule mji pamoja na watu waliowageuza kuwa wafu kama wao. Aliwatazama na kuona wingi wao hali iliyompa nguvu Alie kuona wanauwezo wa kuwadhibiti mabinti watatu. Aligeuka na kuanza safari ya kwenda sasa kwenye falme kukutana na watu anaowataka.

Kule walipo wakina Saadie walihisi utofauti katika eneo lile. Hisia ziliwastua na kuonekana kama kuna jambo baya mbele yao. Hata Kasma aliyekuwa akiongea kuwapa moyo watu wake ilimbidi anyamaze baada ya kuhisi tofauti. Kwa pamoja wakageuka kutazama kwenye njia kubwa ambayo watu hutumia kutembea kuja kwenye jengo hilo la kifalme. Kwa mbali walisikia vishindo vya watu wengi sana kama wanatembea kwa haraka kuja walipo wao. Iliwabidi watazame mabinti hao, Lutfia na Saadie walisogea mbele alipo Kasma na kusimama wote sawa macho yao wote yakiwa yanatazama njia ile kushuhudia ni nini.
Wa kwanza kuonekana kuwa mbele alikuwa ni Alie ambaye alionekana kuwa na hasira ya hali ya juu.
"Huyu mfu amekuja huku!"alishangaa Saadie kumwona Alie akiwa mbele ya kundi lile.
"Nahisi ndio muda muafaka wa kuhakikisha leo ndio mwisho wake huyu dada."alisema Lutfia akiwa anatazama kundi lile.
"Sitakubali kuwaacha waondoke kwenye taifa langu wakiwa hai."alisema Kasma akiweka nadhiri ya kumdhibiti Alie na kundi lake.
Wananchi baada ya kuona tukio hilo wakaanza kufunga madirisha yote wasitazame kinachoendelea, amani iliyokuja kwa sekunde kadhaa imetoweka tena na kuwaacha na hofu. Kila mtu alijificha kabisa asipate kutazama kinachoendelea.

Alie na wenzake walipokaribu eneo lile wakaanza kusambaratika kuwazunguka mabinti watatu ambao na wao kila mtu aligeuka upande wake kuwatazama wafu hao ambao walionesha dhahiri kuwa tayari kuwavamia. Kasma alipowatazama kwa makini baadhi ya wale wafu alishtuka kuona anawafahamu hata kwa sura japo hazikuwa zikitamanika kwa kuharibika, damu zilitawala kwenye miili yao.
"Jamani, hawa ni watu wa mji wa jirani na hapa nilipo. Inamaana hawa wafu wameenda kuwaua ili waungane nao?"alistaajabu Kasma baada ya kulitambua hilo.
Saadie na Lutfia kusikia hivyo nao walishangaa maana si kawaida. Inamaana watapambana na miili ya watu ambao hawakuwa tayari kuwa wafu wanaomfuata Alie.
"Hakuna jinsi ni kuwamaliza wote bila kuangalia nani unamjua. Usiangalie sura ya mtu aliyeko mbele yako ni adui kwako."alisema Lutfia kauli ya kishujaa iliyowafanya wenzake wakubaliane naye na kupata nguvu ya kuwadhibiti wafu.


LUTKAS SEHEMU YA 30


ILIPOISHIA
"Hakuna jinsi ni kuwamaliza wote bila kuangalia nani unamjua. Usiangalie sura ya mtu aliyeko mbele yako ni adui kwako."alisema Lutfia kauli ya kishujaa iliyowafanya wenzake wakubaliane naye na kupata nguvu ya kuwadhibiti wafu.

SONGA NAYO.
Hawakuchelewa hata dakika moja wakaanza kuwasogelea wale wafu ambao kila wanavyopiga hatua mbele ndio wanazidi kubadilika kimwili na kuwa wa kutisha sana huku macho yao yakibadilika gafla. Saadie alipotea ili kuweza kuwazunguka kwa nyuma huku akiwaacha wenzake wakiendelea na kupambana nao kwa mbele.
Kasma pamoja na Lutfia walinyoosha mikomo yao juu kama wanapokea kitu na punde tu kukatokea mapanga yaliyotua mikononi mwao. Wakaanza kuwakata kata wale wote walioanza kutangulia mbele. Ajabu hata wao walishangaa bada ya kuona kila mtu anayekatwa na upanga ule basi anatokomea kabisa na kuacha kivuli tu kikififia kabia na kupotea huku wafu wengine wakibaki pale chini. Hali ile ikamfanya Alie ataharuki baada ya kuona kile kinachoendelea na hakutegemea kama itakuja kuwa hivyo.
Aligeuka kumtazama binti wa Mfalme, Saadie akiwa anatumia uwezo wake kwenye kupambana. Akaamini kweli zoezi lake la kumuua Saadie limefeli kabida. Ikabidi arudi nyuma kwanza hatua kadhaa huku watu wake wakizidi kwenda mbele na kukumbana na kipigo kutoka kwa mabinti watatu waliokamilika kwenye kuwadhibiti. Akili za haraka na aliona huenda ikawa ndio sababu ya Saadie kuwa mzima tena na kile kitabu cha LUTKAS kimesaidia hadi kuweza kuwa hai kwa mara nyengine. Hakuona haja ya kuendelea kuzubaa tena mtu pekee aliyefahamu kwamba ndiye mwenye kile kitabu ni Lutfia hivyo aliondoka moja kwa moja kumfuata binti huyo. Hakutaka kutumia njia ndefu namna ya kupata kitabu hicho, alitembea kwa kujiamini huku macho yake yakimtazama Lutfia tu akiwa anatumia nguvu zake kuwamaliza wale wafu. Hata alipomkaribia alinyoosha vidole vya mkono wake wa kulia chini vikapata kuonekana vikiwaka moto na mwishowe kuonekana Mapanga makubwa yenye moto na bila kuchelewa akayanyanyua na kutaka kumkata nauo Lutfia aliyekuwa hajui kinachoendelea. Wenzake katika harakati za kuwapunguza wafu hao walipata kumwona Alie akiwa tayari kumdhuru Lutfia, ilibidi wote wawili Saadie pamoja na Kasma wapotee haraka walipo ili kuwahi. Alie alishusha upanga ule ilion'gaa lengo ni kumkata kabisa kichwa Lutfia, alishuhudia Lutfia akipelekwa chini na wenzake wawili wote wakadondoka chini na upanga ule ukipita hewani jila kumdhuru yeyote. Alishangaa Alie kuona bile na kusababisha hasira maradufu baada ya kumkosa mtu aliyelenga kummaliza siku hiyo.
Lutfia alishangaa kuona amesikumwa na wenzake hadi chini, alipotazama mbele akapata kumwona Alie akiwa na upanga wake mrefu na mkali na hapo ndipo akafahamu kumbe alikuwa ameandaliwa kifo hicho cha upanga. Kwa pamoja wakanyanyuka huku wakimtazama Alie aliyesimama imara huku nyuma kundi la wenzake wakianza kusogea taratibu na kusimama nyuma yake akionekana dhahiri kwamba yeye ndiye kiongozi wao mkuu.
Lutfia naye akasogea mbele na kubaki wakitazamana pamoja na Alie.
"Bila shaka umekuwa na shauku ya kukutana na mimi kwa namna ya tofauti, na lengo ni hiki kitabu."alisema Alie huku akikitoa kitabu na kumuonesha Alie ambaye alizidi kupagawa baada ya kukiona kitabu halisi. Wenzake macho yaliwatoka kutazama kitu ambacho wamekuwa wakikisaka kwa muda mrefu sana.
"Sasa niwaambieni mjue ukweli, hata siku moja msitegemee ninyi kuja kurudi kuwa binadamu wa kawaida tena. Nani ataruhusu mje kuiharibu hii dunia iliyo tulivu kwa amani. Hivi mmesahau mauaji mliyofanya kwenye mahospitali na hata shule za watoto wadogo sana na wala hamkujali hilo. Yaani msitegemee kabisa huo ujinga kuja kutokea, na leo nahisi ndio mwisho wa kusumbua ardhi hii, mnarudi mlipotoka wote."alisema Lutfia akiwa mwenye kujiamini sana.
Alie alibaki kumtazama tu na kujikuta akicheka sana. Kicheko kilichobeba mengi ndani yake ikiwemo chuki na hasira kwa mabinti hao wanaoongozwa na Lutfia.
"Si rahisi kama unavyofikiri mdogo wangu. Na nadhani unapata kiburi cha kusema hayo kwakuwa unaongozwa na Kasam. Yeye na wewe wote ni wajinga tu na hamuwezi kunizuia kufanya kile nitakacho. Tazama kwanza, jeshi jili nuuma yangu unaona kuna sura za zamani sana hapa? Hawa ni watu wa taifa hili na wengine jirani tu, hii inamaana ninauwezo wa kuongezo wengine zaidi ya hawa. Mtaua wangapi na kwa muda gani, safari hii ninyi ndio hamtoki hapa nahakikisha nawamaliza na mnakuwa chini yangu."aliongea Alie kwa kujiamini sana huku akigeuka kuwatazama watu wake lukuki.
Kasma alipiga hatua mbili mbele huku akimtazama Alie aliyekuwa anajiamini sana.
"Kama wewe umezaliwa hapa na hizo maiti zilizopo nyuma yako basi utaweza kutuondoka duniani, ila kama mimi ndiye Malkia wa hii ardhi... aisee utajuta leo kuingia hapa bila ruhusa yangu. Una deni kubwa sana la kuwaua watu wangu na kuichafua falme yangu."aliongea Kasma akiwa mwenye hasira dhidi ya Alie. Saadie na Lutfia hawakutaka kubaki nyuma, walimsogelea mwenzao na kushikana mikono.
"Wewe ndio tatizo katika falme ya Maskoof, umelichafua taifa la baba yangu hadi watu hawaelewani. Hupaswi kuendelea kuishi we mwanamke."alisema Saadie huku mikono yao ikishikana kwa nguvu zote.
Kukaanza kutoka moshi mikononi mwao hali iliyomfanya Alie atabasamu tu, naye akabadilika gafla kuwafanya hata watu wake nao waanze kupandisha mzuka wa kuingia vitani.
Mabinti watatu pale walipo walionekana kupotea gafla hali ilimfanya Alie awe makini kwa hilo, hata hakutaka kupoteza muda naye akapotea akiwaacha watu wake wakianza kukimbia wakionekana kama wanamuona kiongozi wao anapoelekea.
Saadie na wenzake walipata kutokea nyuma yao wakiwa hawana habari, walijenga shambulio moja kubwa sana wakiunganisha nguvu zao na kutengeneza radi yenye nguvu kama umeme ambayo waliiachia kwa pamoja na kusambaratisha asilimia kubwa ya wafu wale kwa pamoja. Alie alijitokesha alistaajabu kuona shambulio lile la ajabu ambalo hakutegemea kabisa. Aliwatazama mabinti wale wakionekana kusimama pamoja huku wakiwa wanahema maana nguvu walizotoa hapo hazikuwa za kawaida. Hakutaka kuwaacha wapumzike aliamuru wayu wake wageuke kuwafuata mabinti hao kupambana nao huku naye akitoka spidi kuwafuata. Lutfia alipoona hili ikambidi awagawe wenzake waweze kuwadhibiti wale wafu huku yeye akijiaminisha kumdhibiti Alie ambaye naye ndio aliona mtu pekee wa kupambana naue ni Lutfia ili akimdhibiti apate kitabu anachotaka.
Saadie na Kasma wakafanya hivyo kuwadhibiti wafu wale huku Lutgia akimsogelea Alie ambaye pia alikuwa akitembea kumfuata binti huyo mdogo. Hata walipokaribiana hakuna aliyeweza kuwa mnyonge kwa mwenzie kwan waliziachia nguvu zao kitoka mikononi mwao na kusababisha kitu kama shoti ikiomesha kama nguvu zao zimegongana angani. Kila mtu alijaribu kuelekeza kwa mwenzake lakini uwezo wao ulikuwa mkubwa sana hakukua na yeyote ambaye angeliweza kuchemka kwa kilichotokea. Kila mtu alitumia njia mbadala ya kumdhuru mwenzake lakini haikuwa kazi rahisi kwako kwani walikuwa makini kila mtu alijionesha kwamba ana kipi cha kujitamba mbele ya mwenzake. Kuna muda Alie alithubutu hata kutumia silaha kali zenye ncha ili kufanikisha zoezi lake lakini Lutfia alikuwa makini sana katika kuangalia namna adui yake. Hakika ilikuwa ni mpambano wa aina yake na hakuna mtu aliyekubali kushindwa kwa urahisi.

Wafu walizidi kuwaandama Saadie na Malkia wa taifa hilo Kasma ambaye alikuwa akipambana kwa uchungu wa kutetea ardhi yake na wananchi wake ambao idadi kubwa yao tayari wameshauawa na kuwekwa kama wafuasi wa Alie wakitii na kufuata kile ambacho wanaambiwa. Yeye pamoja na mwenzake walionesha ujuzi wao lakini jeshi la wafu halikuwa na uelewa wa kufahamu kitu tofauti ma walivyoagizwa kufanya. Wao walizidi kusonga tu mbele na lengo lao ni kuwamaliza mabinti hao wawili. Ilifika muda Saadie akamtaka Kasma waondoke kwanza ili wapate kuvuta pumzi lakini kwa Kasma haikuwa rahisi kukubaliana naye akifikiria ni ardhi yake ndio inafanywa machafu haya yote. Badala ya kupumzika yeye ndio kwanza alizidi kuongeza mashambulizi kwa wafu hao ambao taratibu wakaanza kupungua kila wakati. Hali hiyo alipoiona Saadie akapata hata nguvu ya kuendelea kumsaidia mwenzake.
Haikuwa kazi rahisi kama alivyofikira Alie pindi alipoliona umbo dogo la Lutfia. Pamoja na udogo huo lakini alihakikisha anammaliza kabisa Alie na kuweza kumrudisha Kasma katika haki yake. Lutfia alikuwa mwepesi katika mashambulizi ya Alie aliyeonekana kama kupandisha hasira na hata ikabidi yeye mwenyewe ajiongeze. Alie alipojaribu kugeuka nyuma kuwatazama wenzake ni wachache hali iliyomfanya kichwa kuweza kujaa mambo mengi.

Muda wote wakati hayo yakiendelea watu walikuwa kwenye makazi yao wakichungulia dirishani kujua kinachondelea. Walijionea kila kitu kinachoendelea, mabinti hao watatu walikuwa wakitumia uwezo wao kuwamaliza wafu ambao wamekuwa wakiitawala falme hiyo kwa muda sasa. Saadie na wenzake hawakuwa hawakuwa na huruma nao walihakikisha siku hiyo wanawamaliza wote ili amani ipate kurejea tena kwenye taifa hilo. Alie alipoona Lutfia anazidi kuwa moto ikabidi arudi nyuma kwanza kujipanga tena. Alimtazama binti huyo akiwa kama chui mwenye kutisha, macho makali yaliwaka huku meno yake kama jini yakichomoza kwa nje hali iliuomfanya Alie atambue binti huyo amekuwa na hasira sana. Muda huohuo akapata kuhisi maumivu mikononi mwake, alipofunua nguo yake kuutazama mkono wake akishuhudia tayari nyama za mkono zimelika na kuonekana kuoza kabisa. Hali ile ilimpa hofu akijua ana muda mchache wa kukamilisha zoezi lake analotaka bila hivyo atapotea yeye bila kufanya chochote. Alimtazama Lutfia kwa umakini kila sehemu lakini ajabu hakupata kuona kile kitabu ambacho anakitaka ili aweze kukifanyia kazi. Akajikuta anajawa na maswali kujaribu kujijibu lakini hakupata jibu sahihi.
Lutfia alikuwa anamtazama tu Alie akiwa anahema maana mpambano uliokuwa unaendelea haukuwa wa kawaida.
"Usimruhusu apumzike, endelea kumshambulia."ilisikika sauti masikioni mwa Lutfia ilimfanya atambue kwamba ni sauti ya Kasam. Aliposikia hivyo naye akafanya kama alivyoambiwa. Alitoka kwa kasi kumfuata Alie na kumkamata kwenye mkono uleule ulianza kuharibika huku akiuminya bila kujua kwamba ni mbovu. Maumivu aliyosikia Alie yalimfanya apige kelele kwa sauti huku akimsukuma Lutfia akadondokea mbali. Alipoona ameumizwa sana haraka akapotea eneo lile akimwacha Lutfia akiugulia maumivu mahala alipodondokea, alitazama mbele yake na kuona Alie ametoweka na asijue wapi alipoenda. Haraka akanyanyuka kutazama huku na kule kujaribu kujua wapi alipotokomea, alikasirika kumkosa kwa muda ule na kubaki kukunja ngumi kwa hasira.

Kitendo cha kukunja vidole vyake akapata kuhisi vidole vikiwa baridi sana, ilimbidi avikunjue kujua ni nini na hapo ndipo akashangaa kuona vidole vyake vimetapakaa damu iliyo na rangi tofauti kabisa. Damu ya kijani ikiwa imegandia kwenye mikono yake, na hapo ndipo alipotambua huenda muda ule akipomkamata mkono Alie na kumminya ndipo akiposhika damu hiyo. Hivyo Alie atakuwa ana jeraha mkononi na ndio maana amekimbia.
Kwa kujua hilo akaamini kwasasa Akie hana uwezo mkubwa wa kuoambana maana mkoni wake mmoja ni mbovu. Alitazama chini ya sakafu na kuona matone ya damu ya kijani yalipoelekea hadi kufika kwenye ukuta na kuishia hapo. Lutfia alipoona hivyo akaamini Alie alitokea kwenye ukuta ule hivyo hapaswi kumwacha hata kidogo.
"Saadie.. vipi huko kwenu?"aliongea Lutfia na maneno yake yakasikikaa kwa mhusika akiwa anaachia pigo la mwisho kwa mfu mmija aliyesalia.
"Ndio nimemaliza hapa, upande wangu wamekwisha."alisema Saadie akimhakikishia Lutfia.
"Kasma unahitaji msaada kwako?"aliuliza Lutfia na muda huohuo Kasma ndio alikuwa akimnyofoa mikono yote miwili mfu aliyekuwa akipambana naye, hakutaka abaki kabisa kwa hasira alizonazo akamkata kabisa kichwa na kumakiza kikosi chote cha wafu waliokuwa wakipambana naye.
"Nimemaliza kila kitu huku."alirudisha majibu hayo Kasma.
"Safi, Saadie itabidi tuonhozane wote haraka kumfuata Alie maana amenikimbia huku, ila anaonekana kutokuwa sawa ameumia mkono mmoja. Kasma itakubidi ubaki katika taifa lako uanze kuwapa imani watu wako waliojificha kwenye makazi yako. Taifa lako sasa lipo salama kabisa."aliongea Lutfia na kupotea gafla akatokea walipo wenzake wakabaki kutazamana.
"Lakini kuna raia wangu ambao wameuawa na hawa wafu, ndugu zao waliobaki watajisikia vibaya sana kutoweka kwa wenzao"aliongea Kasma akiwa anahitaji msaada huo. Lutfia alimtazama Kasma kwa muda kisha akageuka kumuangalia Saadie na kumruhusu kitu.
Kasma alipata kushuhudia Saadie akitoa kitabu kile cha LUTKAS na kumpa mikononi mwake.
"Wacha sisi tukamakizane na Alie wewe tumia kitabu hiki kuwarudisha watu wake wote waliokufa. Tutawasiliana na wewe baada ya kazi hii kuisha."aliongea Lutfia na kumfanya Kasma aelewe. Alikubaliana nao na kukipokea kile kitabu kisha akawaruhusu. Lutfia na Saadie waligeuka na kushikana kisha wakaanza kukimbia na punde tu wakapotea.
Kasma aligeuka na kutazama mbele yake, wafu wengi sana walio wamaliza walikuwa pale chini tu. Alikamata kitabu kile na kushusha pumzi kwanza ili apate kuanza kazi yake ya kuwarudisha watu wake wote.

LUTKAS SEHEMU YA 31


# ILIPOISHIA
Kasma aligeuka na kutazama mbele yake, wafu wengi sana walio wamaliza walikuwa pale chini tu. Alikamata kitabu kile na kushusha pumzi kwanza ili apate kuanza kazi yake ya kuwarudisha watu wake wote.

#TUENDELEE
Alichofanya kwanza alisimama katikati ya uwanja ambao ndi o sehemu maalum yeye kusimama na wananchi wake wakiwa wanamsikiliza enzi za utawala wake kabla ya matatizo yoye kutokea.
Akaanza kuongea maneno mengi sana ambao yaliwalenga wananchi wake ambao muda huo walikuwa zao ndani wamejificha kuhofia vita hiyo. Kwa maelezo ambayo walikuwa wakiyasikia kila mtu akawa na mashaka juu ya kile kinachoongelewa maana bado walikuwa wanaimani kwamba wafu wale kutoka katika taifa lao ni kazi kubwa sana, na hii ni kwasababu ya mamna walivyo wakiwa ni wafu wa tofauti sana wenye kuambukiza pindi wakikukamata na kukuua nawe huwa kama wao.
"Niliahidi kurudisha amani na sasa amani imerejea tena kwenye taifa letu. Mimi pamoja na wenzangu tumeweza kulifanikisha hili na kitu pekee ambacho nahitaji kuwahakikishia ni kuhusu ndugu zetu wote ambao wameuawa na wafu hawa. Leo nawarudisha wenzetu na tuendelee kuishi kama tulivyokuwa zamani, ondoeni hofu kwenye mioyo yenu na tuwe na umoja juu ya hili. Nawaombeni msijifiche tena ndani japo kwa uchache tulionao basi tuwe huru tena katika ardhi yetu."alisema Kasma akitazama kila kona bila kuona yeyote ambaye aliguswa na maneno yake. Alishusha pumzi baada ya kuona ameongea sana bila kueleweka. Punde akatoka bibi mmoja kutoka kwenye nyumba yake na kubaki kumtazama Kasma aliyekuwa mbali naye kwa muda kidogo. Taratibu akaanza kumsogelea hadi alipomfikia na kufanya hata watu wengine nao waanze kutoka kwenye makazi yao tena na kusogea alipo bibi yule wakasimama pamoja huku wakimtazama Malkia wao.
"Kwa maneno yako ya ukarimu ambayo nimeyakariri hasa sauti yako yamenifanya niamini hiki usemacho, uliposema kuwarudisha ndugu zetu ambao tunafahamu kwamba wameuliwa na hawa wafu basi imenishtua na kujiuliza umepata wapi ujasiri wa kuyasema hayo! maana kitu pekee kinachoweza kumrudisha mtu aliyedhurumiwa uhai wake ni kutumia kitabu kimoja tu, LUTKAS. Na ndio maana nilipotoka ndani kwangu cha kwanza kuangalia ni kuona umekishika hicho kitabu. Kwa hilo sina wasiwasi na karibu tena kiongozi wetu."alisema yule bibi na kumpa heshima Kasma kama ishara ya kukubaliana naye.
Malkia Kadma alilipokea hilo na kushuhudia hata wenzake wakimpongeza kwa kazi aliyoifanya na wenzake. Alitazama idadi ya wafu wale waliokuwa pale chini kisha akapiga hatua kadhaa kusogea hadi walipo na kushuka chini. Alimtazama mmoja wa wafu wale shingoni mwake na hata kwenye bega kisha akamuacha na kwenda kwa mwengine. Alifanya hivyo mara kadhaa na mwishowe akapata kile ambacho alikuwa akikitafuta. Watu wote wa taifa lake huwa wana alama zao kwenye miili hivyo ilimfanya atambue yupi ni mfu anayepaswa kumrudisha tena kuwa hai. Zoezi hilo lilikuwa zito kwake kuweza kumpitia kila mmoja hadi wamalizike wote.
Aliwaacha watu midomo wazi baada ya kushuhudia kila ambaye anawekewa kitabu kile kifuani huku Malkia Kasma akiongea maneno fulani yaliwafanya kila mfu aanze kurudi hali yake ya awali kuwa mzima kabisa huku wakishangaa kinachoendelea. Kila mtu alistaajabu kumwona ndugu yake ambaye alishafahamu kwamba hawezi kumwona tena.

Upande wa pili Lutfia pamoja na Saadie walifikia eneo moja ambao lipo nje ya Maskoof. Kitendo kile hata Lutfia kilimshangaza kuona wamerudi tena nyumbani,Maskoof.
"Inamaana huyu mtu amekuja huku tena? Si inafamika kwamba hana uwezo wa kufika huku peke yake.?"alishangaa Saadie baada ya kuhisi Alie huenda akawa amerejea ndani ya Maskoof. Bila kupoteza muda walianza kùfuata njia kuelekea huko kujua kinachoendelea. Kitendo cha kuingia tu kwenye mji mkuu walipata kuomba utofauti kabisa, hata wao hawakuamini kile ambacho wanakiona mbele yao. Mji mzima ulikuwa umeungua kwa moto tena ukionekana kumalizikia baadhi ya vitu vilivyosalia.
Saadie hakuamini kile ambacho anakiona mbele yake na kubaki kushangaa tu.
"Nini kimetokea? Eti Lutfia?"alijkuta akijaribu kupata majibu ya kumridhisha lakini hata mwenzake naye alibaki kushangaa asielewe nini kimetokea. Wtu wengi waliuawa kwa dhoruba hilo ambalo palionekana kama kumetokea mlipuko usio wa kawaida na kusamabaratisha watu,makazi ya watu na hata mali za watu ambazo zilipata kuonekana zikiteketea kwa moto. Hakutaka kuamini kile alichokiona mbele yake Saadie moja kwa moja akaongoza njia kwenda hadi kwenye falme ambapo baba na mama yake aliwaacha humo.
Alipofika eneo husika cha kwanza kilichomfanya akose hata nguvu za kusimama imara, alijikuta akipiga magoti chini huku akishuhudia jengo la kifalme likiteketea kwa moto.
"Mama...!"alitamka Saadie kwa sauti ya upole, sauti iliyoashiria kuumizwa na kile kinachoendelea akihisi hata mama amedhurika. Lutfia alifika eneo hilo na kushuhudia falme ukiteketea kwa moto ulio mkali sana
"Jamani Jamani huyu mtu anatutafuta nini hasa? Hapana sasa imetosha, imetosha kumchekea sasa amezidi ."aliongea Lutfia kwa uchungu baada ya kuona jambo lililotokea. Alitoka haraka bila woga kuingia ndani ya falme huku moto ukizidi kushika kasi. Saadie alibaki pale chini akilitazama tu jengo hilo na kujua hakuna usalama hata kwa familia yake.

Lutfia aliingia humo na kushuhudia vitu vya samani vikiteketea kwa moto, alijitahidi kuziba pua yake asipate kuvuta moshi mwingi uliotanda mule ndani. Akawa na kazi ya kuita mule ndani kama ataweza kumpata mtu ambaye bado yupo hai anahitaji msaada. Alifanya hivyo kwa muda kadhaa ajabu hakukuwa na mtu yeyote aliyemsikia wala mwili wowote alio uona ukiwa chini kwa kuuawa. Hali hiyo ikamfanya ashangae na kuacha maswali mengi kichwani.
Alifuata njia ya kuelekea chumbani kwa Mfalme na kutazama chumba kizima bila kuona mtu, ikambidi amtaarifu mwenzake kwa kile anachokiona ndani.
"Saadie, sioni mtu yeyote humu ndani na sijui wamekwenda wapi."aliongea Lutfia na sauti yake ikamfikia Saadie akiwa pale nje. Kauli iliyomshtua na kujkuta akipata hata nguvu ya kunyanyuka kutoka pale chini.
"Hakuna hata mtu aliyejeruhiwa?"
"Yaani hata aliyekufa haonekani."aliongea Lutfia na kumfanya Saadie pale aliposimama ahisi kusisimka asijue wapi aanzie.

Punde tu kukapita kiumbe ambaye kwa kasi aliyopita nayo haikumfanya Saadie atambue ni kiumbe gani. Aligeuka kutazana kilipotokomea na kutega umakini wa hali ya juu, sekunde chache kile kiumbe kikapita na kumchana Saadie mkononi. Alikasirika sana hata kubadilika macho yake kuchukia kile akichofanyiwa kukatwa na kitu kama kisu chenye makali.
"Lutfia.. Alie yupo karibu nami ananichenga."aliongea Saadie na kauli ile ikamfanya Lutfia kule ndani atoke haraka kwenda kumsaidia mwenzake.
Saadie akibaki kusimama tu pale nje huku akiendelea kupatwa na maswahibu hayo ya kuviziwa na kiumbe ambacho hakuweza kukifahamu huku akizidi kuwa mwenye hasira sana.
"Kama wewe ni jasiri na si muoga jitokeze basi unajificha nini?"aliongea Saadie kwa hasira sana huku mkono wake ukichirizika damu. Aligeuka huku na kule akihema kwa hasira na kuzidi kuyaongea maneno hayo ili anayemfanyia hivyo apate kujitokeza.
Bila kujua lolote nyuma yake kulionekana kitu kama upepo ukimfuata kwa kasi sana na ilipomkaribia tu akapata kuonekana mtu akiwa ameushika upanga refu kwa mbele akielekeza alipo Saadie ambaye hakujua kinachoendelea.
Upanga ule ulipotaka kuingia mwilini mwa Saadie kilirushwa kisu kirefu na Lutfia aliyejitokeza haraka kumsaidia mwenzake na kikapata kukita mwilini mwa yule mtu na kufanya ashindwe kummaliza Saadie ambaye muda huo naye alikuwa akigeuka kutazama nyuma na kukutana na mtu huyo akienda chini huku panga lake akiwa amelishika mkononi. Alishtuka Saadie baada ya kumtazama usoni mtu huyo na kutambua kuwa ni mama yake, Malkia wa Maskoof.
"Mama...!"alistaajabu Saadie baada ya kushuhudia mama yake akitokwa na damu nyingi akiwa pale chini.
Haraka Lutfia akaanza kukimbia hadi pale alipo Saadie akionekana kuvhanganyikiwa akimnyanyua mama yake. Alimtazama Lutfia na kujua ndiye aliyefanya hayo.
"Hili linakuwaje tena mbon..."
"Hapanaaaaaa.!!"alifoka kwa hasira Saadie na kuelekeza nguvu zake kwa Lutfia aliyerushwa mbali na pale aliposimama akadondokea kwenye kibanda cha mbao kilichokuwa kinaanza kushika moto , aliumia sana na kubaki kuugulia tu maumivu huku moto ukianza kushika kwenye nguo zake. Alijitahidi kunyanyuka pale alipo japo maumivu yalikuwa makali sana huku akijikun'guta kuzima moto kwenye nguo zake.

Saadie alibaki kumnyanyua mama yake aliyekuwa akitokwa na damu mdomoni huku kisu kile kilichorushwa na Lutfia kikiwa nyuma kimeingia mgongoni mwake.
"Mama.. pole sana naomba nisamehe mimi, nimeshindwa kukulinda mama yangu."aliongea Saadie akionesha kuwa na huzuni kwa kile kikichotokea muda huo. Malkia alishindwa kabisa hata kuongea na kubaki kumuoneshea Saadie mkono kumaanisha asogeze sikio lake kutaka kumwambia kitu.

Lutfia pale aliporushwa baada ya kusimama na kuwatazama Saadie na Malkia aliyeonekana kulala chini, alishtuka baada ya kumuona Malkia akiwa tofauti kabisa. Aliposimama sawiya kumtazama alishtuka baada ya kutambua ni Alie ndiye aliyelala pale bila ya Saadie kutambua, alianza kusogeza sikio lake kumsikiliza mama yake.
"SAADIE MUACHE!!!. Ni Alie huyo na wala sio Malkia!"alisema kwa sauti Lutfia na kumfanya Saadie pale alipo ashtuke baada ya kusikia hivyo. Malkia baada ya kusikia vile naye akamkamata kichwa Saadie na kumn'gata shingoni huku Saadie akijitetea kutoka mikononi mwa mama yake lakini tayari alishajeruhiwa shingoni. Alijikuta akimkandamiza mama yake chini na kisu kile kikapata kuingia zaidi ndani papo hapo Alie akajitoa mwilini mwa Malkia huku akicheka kwa dharau sanaa. Lutfia akabaki kushangaa kile anachokiona pale. Saadie alisimama huku akishika shingoni pale alipon'gatwa, alianza kujihisi kupoteza ngubu kabisa. Alimtazama mama yake pale alipo chini na kuona akikaribia kuaga dunia. Kwa kile kilichotokea hakutaka tena kumjali mama yake na kuhisi ni Alie tu.
Lutfia akamsogelea pale alipo na kumtazama Malkia pale chini akikata kauli.
"Huyu sasa ndio mama yako halali, Malkia, ni Alie ndiye alimtumia akijifanya yeye ni Malkia ili akudhuru."aliongea Lutfia akiwa anamtazama Malkia. Aligeuka kumtazama Saadie ajabu naye kumwona amedondoka chini huku sura yake ikianza kubadilika kabisa. Lutfia alishangaa kuona maajabu hayo kwa mwenzake, alipotaka kumsogelea alishangaa kumwona Saadie akibadilika dhahiri na kuwa na sura tofauti kabisa. Macho yalikuwa makali sana hadi Lutfia akaanza kuogopa na kuanza kurudi nyuma taratibu. Saadie alisimama pale alipo huku akitazama huku na kule kisha akageuka kumuangalia Lutfia aliyekuwa mbele yake. Hakuwa Saadie tena yule wa mwanzo, alikuwa kama mfu ambaye alikuwa anatafuta mtu. Muda huohuo Alie alijitokeza na kusogea aliposimama Saadie wakawa pamoja wamesimama. Lutfia alishangaa kuona jambo hilo ambalo hakutegemea kukutana nalo, muda huohuo vishindo vya watu kutembea vilisikika na kufanya Lutfia ageuke nyuma yake kutazama ni nini, hammadi.....
Mfalme, kamanda mkuu wa kifalme pamoja na watu wote ndani ya falme walikuwa tayari wameshabadilika kabisa na kuwa kama wafu, na wote sasa wanafuata kile ambacho Alie anataka kiwe.

LUTKAS SEHEMU YA 32


ILIPOISHIA
Mfalme, kamanda mkuu wa kifalme pamoja na watu wote ndani ya falme walikuwa tayari wameshabadilika kabisa na kuwa kama wafu, na wote sasa wanafuata kile ambacho Alie anataka kiwe.

TUENDELEE LEO
Alie alisogea hatua kadhaa mbele huku akimtazama Lutfia aliyekuwa akiangalia watu wale wote walikuwa eneo hilo wakimtazama yeye kutaka kumvamia muda wowote.
"Haya leo kuna kipi ambacho utaweza kujivunia nacho hapa Lutfia? Nakwambiaga siku zote Alie hashindwi na kitu hasa kama ameamua kukipata kitu hicho."aliongea Alie huku Lutgia akimtazama. Gafla kamanda mkuu na askari kadhaa walifika pale alipo Lutfia na kumkamata mikono yake wakamlaza chini. Waliongezeka askari wengine wanne wakambana Lutfia kisawasawa asiweze hata kufurukuta.
Alie alijisogeza pale akiamini Lutfia hawezi kuwazidi ujanja watu zaidi ya kumi waliomkamata. Binti huyo alikasirika sana kukamatwa hivyo, hasira zake zilimfanya abadilike kabisa na kuanza kufurukuta kuwasukuma watu hao lakini walikuwa wenye nguvu sana hadi yeye mwenyewe alishangaa. Alibaki kupiga kelele za hasira kwa kukamatwa na watu wengi. Alie aliachia pigo moja likamwingia Lutfia ipasavyo hadi damu zikamtoka mdomoni.
"Shhhhhhhh! Acha kelele zako bwana , huoni unatupigia kelele hapa! Kelele hizo hazitakusaidia kokote kule hata upige kutwa nzima. Leo nawe unakuwa chini ya mikono yangu baada ya kupata kile nilichokihitaji siku zote."alisema Alie na kumgeukia Saadie aliyesimama naye akimuamuru asogee pale alipo Lutfia. Bila pingamizi alisogea hadi pale huku Lutfia akimtazama Saadie ambaye hakuonekana kuelewa lolote linaloendelea wala kumtambua Lutfia kwa muda huo.
"Saadie hebu shtuka unafanya kazi na huyo mfu na wewe unakubali, hebu amka Saadie."alilalama Lutgia pale chini akiwa ameshikwa kila sehemu hakuwa na ujanja wowote ule wa kjjitetea. Saadie bila kuelewa kitu alimsogelea Lutfia pale alipo na kuanza kumpekuwa Lutfia pale chini, kila sehemu alimpapasa kujaribu kuangalia kama anakile kitabu ambacho Alie amekuwa akitegemea Lutfia ndio mwenye nacho muda wote. Alinyanyuka na kumgeukia Alie hukubakitinhisha kichwa kumaanisha hakuna kitu. Maelezo hayo yalimshtua Alie na kuamua kusogea mwenyewe hadi pale alipo Lutfia na kuanza kumpapasa kila sehemu bila mafanikio.
Naye baada ya kutambua kile wanachokitafuta alitulia kimya na kukubaliana nao kukamatwa vile.
Ilimbidi Alie atumie nguvu za ziada kupata kitabu hicho baada ya kutambua hakipo kwa Lutfia kwa muda huo. Alianza kuangaza macho yake huku na kule akinusa kutaka kujua kama wapi kilipowekwa kitabu hicho baada ya kushindwa kupata kutoka kwa mtu aliyetegemea kuwa nacho.
"Usijihangaishe tu kutafuta, kama kitabu kila siku nakuwa nacho mimi iweje leo sipo nacho? Sahau kukipata na hautafanikiwa hilo unalolitaka kufanya."aliongea Lutfia pale chini akiwa ameshikwa kila upande. Kwa maneno yake Alie alikasirika sana na kujikuta akimsogelea Lutfia akamkwida nguo yake na kumnyanyua juujuu.
"Wewe ukinifanyia ujinga wapo leo nakumaliza bila huruma. Siwezi nihangaike kila kona lakini sioni maendeleo yoyote. Niambie kitabu kipo wapi?"aliongea Alie kwa hasira akiwa amemkwida Lutfia ambaye hakuonesha hata hali yeyote ya kuogoa.
"Ukweli upo palepale, hili swala halitageuka nyuma, sahau kuhusu kitabu cha uhai. Wewe utarudi ulipotoka na wale uliowadhurumu nafsi zao watarudi tena kuishi hadi hapo watakapokufa kwa halali ya Mungu alivyopanga. Wewe sio mtoa roho za watu, huna mamlaka hayo abadani."aliongea Lutfia akizidi kumkasirisha Alie. Alijikuta akitupwa kwa nguvu zote na Alie hadi kudondokea kwenye ukuta uliomuumiza pindi alipofika chini. Damu zilimtoka mdomoni huku akiomesha kulegea mwili. Alikuwa mwenye kuhema kwa kasi kama ametoka kukimbia.
Hakuwa na huruma Alie alimsogelea tena na kumkamata Lutfia kwa nguvu zote.
"Niambie kitabu kipo wapi??" Safari hii alionyesha kutokuwa na masihara kabisa Alie. Alishuhudia tabasamu likitawala usoni mwa Lutfia huku damu zikimtoka.
"Sijawahi kuona mfu aliyekuwa kin'gan'ganizi kama wewe dada yangu. Labda niseme na unisikie kwa herufi kubwa kwamba HUWEZI KUKIPATA KITABU CHA LUTKAS. Hata ufanye nini hautafanikiwa, kubali tu kurudi mavumbini."alisema Lutfia kwa dharau akizidi kumchoma Alie kwa maneno yake. Na kweli maneno hayo yalimfanya Alie azidi kuchanganyikiwa. Aliamua ammalize kabisa Lutfia pale aliposimama akiwa hajiwezi kiafya, aliandaa shambulio la aina yake kusudi atakaporuhusu kuelekea kwa mhusika basi lisambaratishe kila kitu. Alirudi nyuma hatua kadhaa kwanza na kuwa karibu na Saadie, Mfalme Yazid pamoja na askari wengi wa kifalme waliogeuka kuwa kma wafu wakiongozwa na msichana Alie ambaye alipotaka kuruhusu pigo lake gafla tu kikapata kutokea kimbunga kikali sana kilichowafanya pale wote warudi nyuma na kuziba uso wao kwa vumbi.
Lutfia aliinama chini naye akizuia macho yake yasipate kudhurika na vumbi. Hali ile ilikuwa endelevu hafi baada ya muda kadhaa kimbunga kile kikapaga kutulia kabisa na wote wakageuka kutazama kukikoni.
Wote walibaki kuduwaa hawaanini kwa kile ambacho wanakiona mbele yao. Ni Malkia Kasma akiwa amekamata kitabu huku nyuma yake akiwa na watu wote ambao walipata kuonja kifo kutoka kwa Alie pamoja na jamii yake. Tena nao walikuwa zaidi ya wafu wenye kuonesha dhahiri nguvu zao.

Alie alishangaa kuona Kasma naye anamili watu waliokufa pia, tena amewabeba wote ni umati mzima hivyo kuna kazi nzito ya kupambana nao. Kasma alimsogelea Lutfia kwanza na kumjulia hali, hakika aliumia sana mwilini. Kasma akikitoka kitabu cha LUTKAS na kumkabidhi Lutfia palepale alipo naye akapokea. Alie alipata kushudia tukio hilo na kufahamu sasa kwamba kitabu anachokitafuta kila siku kilikuwa kwa Kasma siku zote.
"Huwezi kumudhuru mwenzetu angali bado tupo hai, siku ya leo nyote mtarudi mlipotoka hutaamini."aliongea Kasma kwa kujiamini na bila kuchelewa aliachia pigo moja nyuma ya Alie likasambaratisha baadhi ya wafu waliokuwa nyuma kabisa ya Alie. Hapo ndipo varangati likaanza baada ya wafu wale kuona wanapungua.
Kasma aliwaandaa watu wake waliokuwa nao wamebadilika kutoka umbo la kawaida. Walimsikiliza mtu mmoja tu Kasma ambaye ndiye ameja nao hadi katika ardhibya Maskoof tena. Haraka Kasma akasogea kwa Lutfia aliyekuwa akijihisi vibaya, alimchukua na kumuweka sehemu salama kisha akamlaza chini huku vurumai ndani ya ardhi ya Maskoof ikiendelea. Watu wa Kasma walikuwa nguvu zaidi ya kujua mambo mengi wanayopanga wapinzani waobhivuo ikawasaidia kuwamudu vyema. Alie alikuwa anatumia nguvu zake kuwamaliza watu hao waliongozana na Kasma japo akili yake ilikuwa kwenye kukutana na Kasma baada kufahamu ndiye mtu anayemuhitaji kwasasa ili apate kile kitabu.
Kasma alimsaidia Lutfia kusogea sehemu ikiyo salama kisha akampatia kile kitabu na kukikamata kwa mikono miwili. Alimshika kichwani na kuanza kuyatamka maneno kadhaa ambayo yalifanya mwili wa Lutfia kuweza kutokwa na moshi hasa kwenye mikono yake. Muda mfupi Lutfia alitulia na kuanza kushusha pumzi kwa kasi baada ya kufanyiwa jambo hilo na mwenzake. Alie alipata kukiona hilo na haraka akawahi ili aweze kupambana na Kasma akijua muda mfupi Lutfia atakuwa vizuri na huenda akaleta kizuwizi. Alimvamia Kasma na kumtupia mbali hali ilifanya binti huyo augulie maumivu, aligeuka kutazama aliyefanya hivyo na kukutana na Alie akiwa amesimama anamtazama huku akiwa na hasira hadi kubadilika macho yake. Kasma alinyanyuka kusimama imara bila kuhofia, walitazamana kila mtu akimtamani mwenzake kummakiza. Kwa pamoja wakapotea kama upepo na kuvamiana, ngumi na vurumai zilitawala kwa wawili hao ambao kila mmoja alionesha uwezo wake alionao.
Alie alikuwa mwepesi sana na amezoea katika kumkabili adui yake hivyo alimpa wakati mgumu malkia Kasma mara kadhaa. Alikuwa na uwezo hata kufanya Alie wawe wawili hali iliyomshangaza Kasma kuona mbele yake kuna adui zake wawili wenye kufanana. Alirudi nyuma kwanza hatua kadhaa huku akishuhudia Alie wawili wakimsogelea huku wakiwa wanajiamini. Hawakutaka kumsubiri avute nguvu hata sekunde, walitoka spidi pale walipo na kumkamata Kasma aliyekuwa anajitetea kwa adui zake ambao walionekana kummaliza kweli. Alijitahidi kuweza kujitetea lakini kwa umoja wa wawili hao hakuwa na uwezo wa kuwamudi wote, alijikuta anateswa sana hadi kuumizwa. Damu zilimtoka huku akiwa anahema sana baada ya kupigwa pigo moja lililopelekea kudondoka chini.
Alinyanyua uso wake kuwatazama na kuwaona wanakuja tena pale alipodondoka. Alijikuta akishusha pumzi na kuona anapaswa kujitahidi tu kunyanyuka maana akiendelea kuzembea watamuua. Alijitahidi kunyanyuka kwa mbinde mwili wake ukionekana kuwa dhaifu kabisa huku damu zikimtoka. Aliwatazama wale Alie na kuona wanamkaribia lakini gafla tu wakasimama kwa pamoja huku wakimtazama Kasma ambaye alibaki kuwashangaa tu asijue ni kipi kimewasimamisha angali walikuwa wanamfuata.
Alijitokeza Lutfia nyuma yake na kusimama sambamba na Kasma aliyekuwa hoi. Aligeuka kumtazama na kubaki kutabasamu.
"Pumzika kidogo nikusaidie."aliongea Lutfia akiwa mwenye kujiamini sana.
"Yakupasa kuwa makini nao."aliongea Kasma akiwa ameshika tumbo lake.
Lutfia alimtazama huku akiachia tabasamu hafifu. Aligeuka kuwatazama wale Alie wawili wakiwa wapo sawiya kabisa. Alikitoa kile kitabu cha LUTKAS kisha akafunua karatasi kadhaa na kuzichana, kisha kile kitabu akampatia Kasma akishike.
"Unafanya nini Lutfia?"alishangaa Kasma huku akipokea kile kitabu. Punde tu akajikuta anapata nguvu hata ya kunyanyuka tena. Alie na mwenzake wakabaki kushangaa na kuona nao wamekuwa wawili tena. Kasma alionekana kushika kile kitabu huku Lutfia akikamata zile karatasi.
"Nadhani unachokitaka ni hiki hapa, kama unauwezo wa kuchukua basi sogea uchukue."aliongea Lutfia kwa kujiamini huku akimtazama Alie ambaye maneno hayo yakamfanya amtazame mwenzake na kumruhusu afuate kile kitabu.
Alitoka spidi ya hali ya juu kwenda kumpora Kasma kile kitabu alichoshika na kuziacha zile karatasi alizokamata Lutfia. Akipokishika tu kile kitabu alishangaa kuona mkono ulioshikilia kitabu hicho ukiwaka moto. Lutfia alitoka mbio na kumkamata mkono mwengine na kuuminya haswa. Ilisikika sauti ya mtu akiugulia tu mumivu. Maumivu ambayo hata Alie pale aliposimama aliyasikia na kujikuta akipata ufahamu kwamba kila atakachofanyiwa mwenzake basi na yeye lazima atasikia maumivu. Alipolitambua hilo akashtuka sana, ilibidi mwenyewe ajiongeze akihofia kutokea makubwa kwa mwenzake. Alikimbia kwa kasi hadi pale alipo mwenzake, kikatokea kisu mkononi mwake ambacho alikipeka moja kwa moja kifuani kwa mwenzake pale alikoamatwa na Lutfia. Papo hapo akapata kuonekana akipuputika kama udongo na mwishowe kapotea kabia akimwacha Lutfia pale aliposimama akamate hewa. Alie alisimama sehemu na kubaki kumtazama Lutfia ambaye anaonekana safari hii amekuja kivingine.

LUTKAS SEHEMU YA 33


ILIPOISHIA
Alie alisimama sehemu na kubaki kumtazama Lutfia ambaye anaonekana safari hii amekuja kivingine.

TUMALIZIE
Alijiandaa naye barabara kusudi amvamie binti huyo aliyekuwa amesimama tu huku kitabu chake kikiwa mkononi. Punde tu alichoropoka pale alipo na kutokea karibu na Lutfia kisha akakamata kile kitabu kutaka kumpora mwenye nacho.
Ilikuw ni zaidi ya umeme uliomrusha Alie kutoka pale alipo hadi kudondoka mbali na japo. Hata yeye alishangaa na kujikuta akinyanyuka pale alipo kumtazama Lutgia aliyekuwa amesimama tu hana wasi.
"Mbona umeshtuka hivyo? Si ulitaka kitabu hiki hapa chukua."aliongea Lutfia akinyoosha kitabu cha LUTKAS kumpatia Alie. Alibaki kukodoa macho tu.
"Kile kitabu kina nini mbona imekuwa hivi?"alibaki kujiuliza mwenyewe baada ya kujaribu kumpokonya Lutfia lakini ajabu alipokigusa kilimrusha hadi hapo na kumfanya ashangae tukio hilo ambalo kwake ni geni na hakutegemea. Lutfia alizidi kumsisitiza asogee kuchukua alichokuwa anakitaka siku zote. Alimfanya Alie atafakari kwa kina sana nini afanye ili alitatue tatizo jilo. Alangalia wenzake ambao amekuwa akiwatuma nao washateketea. Ilimbidi Lutfia ageuke na kusogea kumchukua mwenzake Kasma ambaye alipata kupumzika baada ya Malkia huyo kupata dhoruba kutoka kwa Alie. Alimkamata mkono na kumnyanyua huku akionekana kutokuwa sawa. Mbele ya Alie alitumia kitabu cha LUTKAS kumsaidia mwenzake na punde hali yake ikawa sawa kama zamani. Hali ile ilizidi kumtia hasira Alie ambaye hadi kuda hio jambo humu kwake ni kupata LUTKAS ambayo awali alitegemea kuipata kwa urahisi pindi atakapomdhibiti Lutfia na kuichukua yeye, lakini siku hiyo anaona mambo tofauti, LUTKAS haitaki kuguswa na mtu yeyote ambaye hatambuliki. Akili za haraka haraka zikamtuma amtumie Kasma pale alipo aweze kumuingia huenda akafanikiwa na kuweza kuipata LUTKAS kwa njia tofauti. Alijiandaa kamili kuweza kulifanikisha hilo na alipoanza kutoka spidi pale alipo alishangaa anashikwa mkono na mtu. Haraka akageuka kumtazama mtu alikuta uso kwa uso na sura sura ya Lutfia hali iliyomfanya ageuke kutazam kule alipokuwa anataka kwenda na kukutana na hao Lutfia na Kasma wakiwa eneo lile. Tukio hilo akatambua kwamba Lutfia naye ametumia nguvu kama alivyofanya yeye hapo awali za kutokea wawili.
Mkono ule uliminywa na kujikuta akipiga kelele za maumivu na kuutoa mkono wake haraka. Hakutaka kusimama tena eneo hilo alipotea hataka kwenda kuugulia maumivu ya mkono aliyopata kutoka kwa Lutfia aliyebaki kutazama tu hadi alipotokomea.

Huku upande wa pili jeshi ambalo Alie amekuwa akiliongoza halikonekana tena kuwa na nguvu hata za kuendelea na kupambana. Ni wachache akiwemo Saadie, Mfalme pamoja na jeshi lao walikuwa wanafuata kile mkunwa wao akisema.
"Huyu leo hawezi kutoka kwenda taifa lolote."aliongea Lutfia akiwa anamwambia Kasma.
"Unamaana gani kusema hivyo?"aliukiza Kasm huku akimtazama mwenzake.
"Kila sehemu nimeweka kizuwizi cha kutoka kwenda sehemu yoyote, huyu leo anarudi kule alipotoka tena hakuna watu wa kuongozane naye."aliongea Lutfia wakidhamiria kummaliza siku hiyo Alie.
Baada ya muda kadhaa Kasma aliweza kuamka baada ya kujiridhisha kuwa sawiya. Lutfia alimpatia tena kitabu kile Kasma akiwa na maana.
"Yakupasa uwasaidie watu wa Maskoof ambao wameuawa na kuwa chini ya Alie. Hivyo leo tumalizane na kila kitu hapa tukiiacha ardhi hii ikiwa na amani kabisa. Saadie naye bado yupo kwenye mtihani hivyo msaidie ili muweze kusaidiana kuwamaliza watu wote waliouawa na Alie. Mimi huyu dada leo nipo naye hadi nijue hatma yake."aliongea Lutfia akimueleza Kasma naye akapata kuelewa. Waligawana majukumu hayo Kasma akaelekea kule alipowaacha wale watu wake aliokuja nao wakipambana na wafu wa Alie ambao miongoni mwao yuponpia Mgalme Yazid pamoja na askari wake wote. Kasma alichokifanya nibkumtafuta kwanza Saadie aweze kumuweka chini kwanza amrudishe kuwa mtu kama alivyo awali ili apate kusaidiana na wenzake. Hata alipomuona alikuwa katikati ya kundi la watu wakiendeleza mapambano. Alisogelea karibu yake kabisa na kubaki kusikitika tu lakini haikuwa na jinsi, alichomoa panga lake kuukuu na kujifunika moyo wa huruma. Alimkita nalo panga la mgongo papohapo Saadie akaenda chini huku akionekana kuchafuka sana kama chokoraa. Japo alipatwa na hofu kubwa kwa kile alichokifanya lakini aliamini anafanya hivyo kwa lengo la kumsaidia mwenzake. Alishuhudia Saadie akitapatapa pale chini na mwishowe akapoteza maisha kabisa. Na huo ndio ukawa muda sahihi wa Kasma kwenda kufanya kile alichotegemea kukifanya . Alichukua kile kitabu cha LUTKAS na kumuwekea Saadie kifuani mwake huku akiyanena maneno fulani. Alianza kubadilika Kasma na kuwa na macho makali sana huku akikitazama kitabu kile kilichopo juu ya kifua. Muda mfupi tu Saadie alitapika tonge la damu iliyoanza hata kubadilika rangi na kuwa nyeusi kabisa. Alipoliona hilo haraka Kasma akatoa nguo yake na kumfuta damu iliyokuwa mdomoni mwa Saadie. Alifurahi sana baada ya kuona mwenza wao amerudi tena kama alivyo awali. Saadie alinyanyuka taratibu huku akisaidiwa na Kasma, aliyatazama mazingira ambayo yupo kwa muda huo na kujikuta akishangaa mahala alipo. Alimtazama Kasma na kumwona akiwa mwenye furaha kiasi usoni mwake.
"Kasma, nini kimetokea?"aliuliza Saadie akiwa haelewi kinachoendelea. Alitazama watu wengi wakiwa chini wameuawa. Alikumbuka mara ya mwisho alikuwa wapi hadi muda huo anajiona yupo nje tena akionekana mchafu sana. Alijikuta ananyanyuka haraka na kuanza kujitazama kwa mara nyengine, hata yeye haamini kwa vile alivyo. Ikambidi aulize tena ili apate jibu kamili. Hawakuwa na hiyana ikibidi aelezwe ukweki hali halisi hadi kwa muda huo waliokuwa wamesimama. Saadie alistaajabu sana baada ya kufahamu kila kitu tangu alipokuwa mikononi mwa Alie hadi muda huo. Hawakuwa na muda tena wa kuendelea kuongea kazi ikawa ni kuwarudisha watu wote muhumu akianza Mfalme pamoja na mkewe kisha askari wengine wakiongozwa na Kamanda nao waliweza kupata msaada huo.

Huku upande wa pili Lutfia alikuwa sambamba na adui yake. Alishafahamu udhaifu wa Alie ni mkono wake mmoja imezidi kuharibika kila muda unavyozidi kwenda, hivyo alihakikisha anamsumbua kupitia udhaifu huo.
Lakini kwa Alie hakutaka kukubali kushindwa kirahisi, aliona siku hiyo ndiyo ya mwisho kwake kusubiri kupata kile ambacho anakihitaji. Alikuwa mwenye kujiamini sana japo aliona binti Lutfia akizidi kumuandama.
Alionesha ubora wake na nguvu alizonazo kumdhibiti Lutfia lakini kwa safari hii hata yeye alishangaa kumwona binti huyo akiwa mwenye nguvu zaidi ya bile alivyo mwanzo. Hali iliyopelekea hata kurudi nyuma kwanza amtazame vizuri.
"Mbona amebadilika gafla hivi wakati hakuwa akinisumbua siku zote?"alibaki kujiuliza Alie huku akiwa anahema kwa mapambano. Lutfia alimtazama tu adui yake na kujiwa na hali ya hasira pindi amuangaliapo Alie, alitoka kama umeme pale aliposimama na kwenda kumkamata mkono uleule mbovu wa Alie aliyebaki kupiga kelele za maumivu huju akijitoa mikononi mwa Lutfia. Safari hii alifanikiwa hata kuondoka na kipande cha nyama ya mkono wa Alie ambaye alibaki kuutazama mkono wake ukiwa umeoza na hata kuumizwa na Lutfia.
Hasira zikampanda na kujikuta anapata hata nguvu ya kuendelea kupambana naye akiwa na sera ya kutokushindwa na mtu. Ikikuwa ni zaidi ya dakika kumi na tano wakioneshana uwezo kila mtu.
"Pole sana dada yangu maana nakusikitikia umerudi duniani kupata mateso tu ni heri ungeendelea kupumzika katika nyumba yako ya kila siku. Tamaa za kuwa juu zaidi ya wenzako ndio zinakufanya leo ukubali kurudishwa kwenye nyumba yako ya milele."aliongea Lutfia akiwa anajiamini sana.
"Nani kakwambia kuwa umefaulu kwa hicho inachokisema. Yaani umekaa ukifikiri mimi niweze kufeli katika hili? Sahau kuhusu hilo maana napambana kurudisha heshima."
"Sasa unachokitafuta huwezi kukipata kamwe. Nakuonea huruma sana maana dada yangu."aliongea Lutfia na maneno yake yakazidi kumfanya Alie ahisi anadhaurika. Alisogea mbele kwa hatua kadhaa na kushusha pumzi kwanza akijua kitu anachokwenda kukifanya kitamfanya Lutfia asiweze kujitetea tena. Aliandaa pigo la mwisho kabisa na kuziruhusu nguvu zake zote ili aweze kukamikisha zoezi lake. Alipojihakikishia hilo aliachia nguvu hizo za kichawi na kuzipeleka kwa kasi kuelekea kwa Lutfia pale aliposimama na gafla tu mbele ya Lutfia akapata kutokea ndugu yake Alie, Kasam aliyejaribu kuzuia uchawi huo uliopaswa kuingia kwa binti mdogo huku akimtupia kisu cha mbao kilichochongwa kikiwa na rangi ya kijani kabisa. Lutfia alipoona hivyo haraka akachukua kisu kile mikononi mwa Kasam na kupotea gafla. Alie akiwa kwenye hali ya kushangaa baada ya kuona shambulio alilolituma kwenda kwa Lutfia limeweza kuzuiwa na ndugu yake Kasam, Lutfia aliweza kutokea nyuma yake aliposimama na kunyanyua kile kisu, bila kupepesa macho alikikita upande wa moyo na kuzama kabisa. Zilisikika kelele za Alie akilia kwa maumivu makali sana anayosikia. Walimshuhudia akizunguka pale katikati yao huku akipeleka mikono yake nyuma kujaribu kutoa kisu hicho bila mafanikio. Alianza kubadilika, mwili wake ulianza kutuna huku sura mbalimbali za watu zikionekana zililia kwa uchungu sana kiasi cha kumfanya hata Lutfia ashangae kuona hali ile.
Kasma alitokea muda huo akiwa na kile kitabu cha LUTKAS.
"Unapaswa ukitumie kitabu hicho na kusoma yale yaliyomo humo ili nafsi za watu wote aliowaua zipate kuwa huru zitoke mwilini mwake maana alizishika na ndio maana akawa anafuatwa na wote anaowamaliza."aliongea Kasam akimweleza hali halisi Kasma.
Kasam aligeuka na kumtazama Alie akiwa pale kati akizidi kufutuka kuwa mnene sana huku nafsi za watu zikitokea mwilini mwake. Muda huohuo LUTKAS ikaanza kufunguka kurasa zenyewe hadi kufika mahala kikatulia. Kasma alitazama na kujionea kurasa hiyo ikiwa imechorwa kiumbe cha ajabu kama jini lililofutuka sana huku sura mbalimbali zikitokea mwilini mwake. Chini kukawa na maneno ambayo yalikuwa tofauti na lugha ambayo Kasma anaifahamu na hayo ndio yanasadikika yasomwe ili nafsi zote zikizokuwa zikiamrishwa na Alie ziwe huru.
Alishindwa kuelewa aanzie wapi maana lugha ile ni ngeni kwake. Alie akaanza kurudi polepole mwili wake hali iliyomfanya Kasam amtazame Kasma.
"HARAKA FANYA HIVYO!!" aliongea Kasam kwa sauti baada ya kuona Alie anapata nguvu ya kurudi kama alivyo mwanzo. Lutfia alivyoona hali inataka kubadilika alitoka mbio hadi pale alipo mwenzake Kasma kisha akamkamata mkono, gafla macho yake yakabadilika na kuwa makali sana. Aliongea maneno fulani polepole na punde tu mwiki wake ukazama ndani ya mwiki wa Kasma pale aliposimama. Macho ya Kasma yakabalika huku akikitazama kile kitabu alichokishia.
"Wanneer elke ziel terugkeert naar een plaats van vrede, beveelt LUTKAS een zelfopgelegde ziel om haar onafhankelijkheid vandaag te claimen.. KOM TERUG BIJ JOU ALIE!.(wakati kila roho inarudi mahali pa amani, LUTKAS inaamuru roho inayojiweka sawa kudai uhuru wake leo. RUDI ULIPOTOKA ALIE!)."aliyasema hayo Kasma kwa hisia kali na kwa sauti. Walishuhudia kumwona Alie akianza tena kubadilika na kuwa mnene sana. Akaanza kunyofoka ile mkono wake ulioanza kuharibika na kuruhusu moshi mweusi ukianza kutoka kwa kasi kupanda juu angani. Ukafuata mkono wa pili nao hali ikawa vivyo hivyo ikiwaacha kwenye mshangao Kasma na Lutfia aliyeko ndani yake. Kile kisu kilichokita mwikini mwa Alie kikaanza kumbadikisha kabisa rangi dada huyo na kuwa wa kijani kabisa na mwishowe akapasuka kama puto lililojazwa sana, na huo ndio ukawa mwisho wa Alie katika ardhi ya Mfalme Yazid.
Muda huo Saadie naye ndio alikuwa akifika eneo hilo na kushuhudia mabaki yakielea juu angani. Alimtazama Kasma pale aliposimama na kushuhudia Lutfia akijitoa mwilini mwa Kasma na kusimama kutazama jinsi Alie alivyo sambaratika. Alifahamu kuwa tayari wamemmaliza Alie, mwanadada ambaye ameua watu wengi sana. Lutfia aligeuka kumtazama mwenzake na kujikuta wakifurahi kwa pamoja baada ya kufanikiwa kummaliza mtu ambaye amekuwa akileta tafarani kila siku katika maisha yao.

Waligeuka kumuangalia Kasam wakamwona akiondoka zake baada ya zoezi hilo kumalizika.
"Tungependa tubaki na wewe siku zote Kasam."aliongea Kasma wakiwa wanamtazama aliyewasaidia.
"Nimetimiza kile nilichostahi kuwasaidia. Alie amerudi sehemu yake anayostahili. Wacha na mimi nirudi sasa kupumzika kwa amani, umoja wenu umefanikisha hili. Nawapongeza wote watatu kwa kuwa pamoja katika shida na raha. LUTKAS ni zawadi kwenu. Milele kitabaki kutetea uhai uliodhurumika."aliongea Kasam akiwa mwenye tabasamu murua. Aliwapungia mkono na kugeuka kutembea hatua kadhaa akapoteabkama upepo.

Mabinti watatu wakabaki kutabasamu kwa pamoja baada maneno ya kupewa moyo kutoka kwa Kasam. Saadie aliwashukuru sana wenzake kwa umoja walio uonesha katika kipindi chote cha matatizo yaliyotokea katika ardhi ya Maskoof.
Baada ya muda wakarudi uraiani kuanza kuweka mambo sawa kwa watu ambao waliuawa akiwemo Malkia pamoja na Mfalme Yazid. Mambo yote yalipokaa sawa Kasma pamoja na watu wake wote akiokuja nao walipata kuwaaga wenyeji wao ili nao warejee kwenye taifa lao kinaloongozwa na Malkia mdogo Kasma. Kilichowaacha watu hali ya mshangao ni kule kufanana kwa Lutfia pamoja na Kasma ambao hata wao hawakupata ukweli wa ufanano wao. Walichotambua ni kwamba majina yao ya kwanza ndio yametumika kuunda jina la kitabu cha uhai, LUTKAS.

Jioni ya siku hiyo Lutfia aliitwa na Mfalme Yazid, ilimbidi atii wito huo akaanza kuelekea kwa Mfalme. Hata alipofika kwenye ukumbi ambao Mfalme huwa anakutana na watu mbalimbali. Aliingia humo na kuwakuta viongozi wa taifa hilo Mfalme na Malkia wakiwa wamekaa kwenye viti vyao huku nyuso zao zikijawa na tabasamu. Alisogea hadi mbele yao na kuinama kuwapa heshima nao wakaipokea.
"Nimefika kuitika wito wako Mfalme."aliongea Lutfia kwa unyenyekevu. Mfalme Yazid alisimama na kusogea pale alipo Lutfia.
"Kwanza nikushuru sana kwa yote uliyotenda ndani ya taifa langu, umesaidia watu wengi sana. Awali sikutambua umuhimu wako na hata muda mwengine nikihisi wewe ndio sababu ya matatizo mbalimbali hapa Maskoof. Hivyo nimekuita hapa kukuomba samahani kwa upande wangu na hata kwa Malkia pia kwa lolote lile ambalo amekukwaza. Alie alituchanganya sana ndio maana hatukuwa upande wako kukuamini kwa asilimia zote. Tusamehe sana."aliongea Mfalme Yazid na kumfanya hata Malkia pale alipo asimame kama kuonesha kweli kuhitaji msamaha.
"Mimi nishawasamehe kwa kila kitu wazazi wangu. Nilijua tu kuwa Alie ndio kayafanya haya hivyo hampaswi kuwa na wasi. Mimi ni binti yenu kama alivyo Saadie, msijali kuhusu hilo."aliongea Lutfia kwa upole.
Muda huohuo Saadie alitokea na kusogea hadi pale alipo Lutfia naye akasimama.
"Nimewaita wote leo nahitaji kuwapa zawadi ambayo mimi na Malkia tumekaa na kuona itawafaa. Nashukuru Lutfia kwa kumfanya binti yangu awe ni wakipekee na mwenye uwezo wa kupambana na watu wenye nguvu za ajabu. Hivyo tumeamua kuwapa uongozi wa kuitawala Maskoof hii, namaanisha kwamba mtakuwa badala yetu sisi. Tunahitaji kupumzika hivyo jukumu la kuiongoza Maskoof lipo mikononi mwenu. Saadie utachukua nafasi ya mama yako kuwa Malkia mpya wa taifa hili ilihali Lutfia atakuwa badala yangu. Naamini kwa umoja wenu Maskoof itakuwa salama siku zote."alisema Mfalme maneno hayo na kumfanya binti yake Saadie afurahi kusikia hivyo. Lutfia hakuamini uamuzi walio uchukua Mfalme na Malkia kuutoa uongozi wao na kuwapa mabinti hao wawili. Bila kizuwizi chochote Mfalme alichukua mkataba waraka wa zamani unaomtambua yeye na mkewe kuwa viongozi kisha akauchoma mbele ya wazee wa taifa hilo wakiwa kama mashahidi. Uliletwa waraka mpya ambao kwa mikono yake akaandika uongozi mpya wa mabinti hao wawili.

Asubuhi kulipo pambazuka sherehe ya kuwatawaza viongozi hao wapya ikaandaliwa. Ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa taifa hilo. Kwa mara ya kwanza Maskoof inaongozwa na mabinti wawili angali Mfalme na Malkia bado wapo hai.
Walivalishwa kofia za Mfalme na Malkia wapya wa Maskoof. Kasma naye aliweza kufika kwenye sherehe hizo kuwashuhudia wenzake nao wanatawazwa kuwa Mfalme na Malkia mpya wa taifa hilo. Aliwapa pongezi kwa nafasi waliyopewa na siku hiyo Saadie aliitumia kuwalisha watu wote wa taifa lake kuonesha upendo kwako. Watu walikula na kunywa wakiupokea uongozi mpya kwa baraka ya chakula.
Baada ya muda Lutfia aliwachukua wenzake na kuelekea msituni wasijue ana maana gani. Hata walipofika walibaki kumtazama nini anataka kufanya. Alionekana kuwa na furaha usoni mwake.
"Nadhani ni jambo moja tu limebaki kati ya yote tuliyofanya."alisema Lutfia wakiwa wameshikana mikono na kuwafanya wenzake watazamane wasijue maana yake.
"Unamaana gani?"walisema kwa pamoja. Lutfia alibadilika macho na kuyanena maneno fulani, punde tu wote wakapotea.
Sekunde kadhaa walikuja kutokea kwenye chumba kimoja tena wote wakiwa kitandani. Saadie na Kasma walitazama kila kona ya chumba kile na kupata kuona vitu mbalimbali. Kitu pekee walichokitambua ni kuona picha za Lutfia zikiwa ukutani akionesha tabasamu. Waligeuka kumtazama wakamwoma akiwa mwenye tabasamu . Aliwaeleza ukweli kwamba amewaleta nyumbani kwao ambapo ndipo alipotokea kabla ya kuingia katika mji wa Maskoof. Ilibidi anyanyuke na kuwataka wenzake wamfuate kwenda kumwona mama yake.
Saadie na Kasma wakafanya na kuanza kumfuata Lutfia kwa nyuma. Walifika sebuleni na kumkuta mama akiwa anatazama televisheni hana analojua.
"Mama...!"aliita Lutfia na sauyi yake ilimshtua mama yake baada ya kugeuka kutazama. Alistaajabu baada ya kumwona binti yake mbele ya macho yake.
"Mwanangu....!"alinyanyuka kwa furaha mama na kushuhudia Lutfia akimkimbilia na kumkumbatia kwa mahaba yote. Kadma na Saadie walibaki kutabasamu tu baada ya mwenzao kuweza kuonana tena na mzazi wake. Ilikuwa ni siku ya furaha siku kwa mtu na binti maana ni muda mrefu hawakuweza kuonana. Mama alipowatazama mabinti walioonhozana na mwanaye alishangaa kumwona Kasma akiwa vilevile na alivyo binti yake, ilibidi amgeukie Lutfia kujaribu kuwatofautisha lakini kwake aliweza kuwatambua tofauti zao kama mzazi.
Walikaa pamoja na hapo ndipo Lutfia akaanza kumweleza mama yake yale yote ambayo alikutana nayo tangu siku ya kwanza anaondoka hadi kipindi anarudi kwa muda mchache siku ile. Alimweleza pia na uongozi ambao ameweza kupatiwa huko Maskoof akiwa sambamba na Saadie.
Kwa maelezo yake ya kina yalimuingia mama na kujikuta akiwapa pole kwa matatizo waliyokutana nayo dhidi ya wafu waliokuwa walingozwa na Alie. Walikaa na kuongea mambo mengi sana siku hiyo hadi kiza kilipoanza ambapo Saadie pamoja na Kasma wakataka kuondoka. Kauli ambayo mama Lutfia hakutaka kuikubali na kuwataka walale ili kesho asubuhi waondoke. Nao walitii kile alichosema mama huyo wakimheshimu kama mama wa rafiki yao.

Kesho yake asubuhi baada ya kila kitu kumalizika ikafika muda wa safari waliaga tena. Lutfia alijiandaa kuweza kuondoka na wenzake maana naye ni kiongozi wa Maskoof hivyo yampasa kuwa karibu na watu wake. Mama aliwatuliza kwanza kisha akaingia ndani. Ikabidi wamsubiri wakijua anawabebea zawadi waweze kuondoka nayo. Punde tu alirejea akiwa amebeba begi la nguo hali iliyowafanya mabinti hao watatu washangae.
"Mama... haya kulikoni!"aliuliza Lutfia akimshangaa mama yake aliyekuwa akivaa viatu vizuri.
"Mnaniambia Maskoof Maskoof mimi napajua?. Sasa leo tunaenda wote huko nikapaone."aliongea mama Lutfia na kuwafanya mabinti hao waangue kicheko. Hata yeye mwenyewe alifurahi maana anachokisema kina ukweli na kiafurahisha. Hawakuwa na kipingamizi walisogeleana karibu na kushikana mikono akiwepo mama mtu, punde tu wakapotea kueleke Maskoof.

MWISHO

Nawashkuru kwa kuweza kuwa nami sambamba toka 1 hadi leo tunahitimisha. Changamoto za kuchelewa kuituma SIMULIZI hii zilikuwa ndio kubwa na yote ni sababu ya mambo kuingiliana.
Panapo uzima tukutane kwenye SIMULIZI zengine.COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : LUTKAS (Kitabu CHA Uhai)
LUTKAS (Kitabu CHA Uhai)
https://1.bp.blogspot.com/-Bar6x6MD8oo/XXYXIXfaOMI/AAAAAAAACyU/Bvri-tvcY6Qvs0fgcQLftmiFx1vpfvwYwCLcBGAs/s1600/LUTKAS%2B%2528Kitabu%2BCHA%2BUhai%2529.jpeg
https://1.bp.blogspot.com/-Bar6x6MD8oo/XXYXIXfaOMI/AAAAAAAACyU/Bvri-tvcY6Qvs0fgcQLftmiFx1vpfvwYwCLcBGAs/s72-c/LUTKAS%2B%2528Kitabu%2BCHA%2BUhai%2529.jpeg
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/09/lutkas-kitabu-cha-uhai.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/09/lutkas-kitabu-cha-uhai.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content