UTAMSHAURI NINI UYU MWANAMKE ALIYETOA SIRI ZA MUMEWE NA KISHA KUIBIWA MUME

Mimi ni Mama wa watoto watatu, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 10 sasa,mimi na rafiki zangu akina Mama hapa mtaani na mashoga zangu wengine tuna group letu la Whatsapp ambapo tunajadili mambo yetu. Kuna wakati wa kuchat mimi niliomba ushauri kuhusiana na maumbile ya mume wangu, yeye ana maumbile madogo hivyo niliwaeleza rafiki zangu, kwakua group ni la wanawake ta tulishaahidiana kuwa hakuna kotoa siri basi niliwaambia rafiki zangu namna ambavyo siridhiki na mume wangu ili wanipe maujuzi.

Mumue wangu mimi hana shida, ni wale wanaume wakujali, ananipenda mpaka basi, tatizo lake ni hilo tu maumbile yake ni madogo na si ridhiki. Niliomba ushauri wengi wakashauri lakini haikusaidia, walinishauri niwe na sehemu nyingine ya kupoozea lakini niliona haina maana mimi kumsaliti mume wangu. Hiyo ilikua ni mwaka jana na yaliisha. Tatizo nikwamba mwaka huu kuanzia mwezi wa pili mume wangu alibadilika, alianza kuwa mtu wa pombe, kuchelewa na kwa mara ya kwanza nilikuta meseji za wanawake katika simu yake.

Nilimuuliza aliomba msamaha yakaisha, lakini hakubadilika, alikua ni mtu wa kulala nnje nilishitaki mpaka kwao lakini aliomba msmahaa ila hakubadilika. Sasa mwezi uliopita mume wangu aliniambia kuwa hajisikii tena kuwa na mimi, aliniambia kuwa hawezi kuwa na mimi kwani hanipendi tena, nilimuuliza sababu lakini hakuniambia. Ila baada ya kama wiki moja alihapa chumba na akawa harudi tena nyumbani, nilifuatilia na kugundua kuwa anaishi na rafiki yangu, mmoja wa w atu ambao tupo kwneye group naye ambaye naye ni mke wa mtu lakini wamegombana na mume wake.

Mume wake alikua na matatizo mengine tu anampiga wakaachana mwaka huu mwanzoni sasa anaishi na mume wangu. Nilimuuliza mume wangu kwanini ndipo akanitumia screenshot ya zile meseji nilizotuma kwenye group na kuniambia kuwa mwenzakoa anatosheka wewe si uliamua kunidhalilisha. Naomba ushauri wako, nifanye nini kwani nimechanganyikiwa, nafanya kazi kweli lakini mume wangu nampenda, sikua na lengo la kumdhalilisha lakini kwanini rafiki yangu atoe matatizo ya mume wangu mbele ya watu.
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni 2

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment
  1. Pole sana mpendwa ndo mambo ssi wanawake hatuna urafiki mwema

    JibuFuta
  2. Dah pole sana usipende kuwqshirikisha mashoga na kuwamini mashoga c watu wazur dah pole inaumaa

    JibuFuta
close