UPISHI WA MAYAI


UPISHI WA MAYAI

MAHITAJI YA KUPIKA MAYAI

  • Mayai 4
  • Hoho 1
  • Pipipili mtama
  • Karroti 1
  • Chumvi kiasi 
  • Mafuta kijiko 1
JINSI YA KUPIKA MAYAI:

  1. Unachukua vibakuli viwili kimoja unaweka ute kimoja kiini tia hoho,karroti,pilipili mtama na chumvi ktk vibakuli vyote viliwili,unaweka frampen jikoni ikipata moto unatia mafuta kidogo halafu unaaza kuwekaa ute nusu nusu unabakisha ukikauka unakunja humo humo kwenye frampen kwa urefu unabakisha ncha nyembamba,unaweka kiini chote kwa hivyo ncha ya kiini na ute zitashikana ukikauka unakunja tena hungeuzi unabakisha ncha ndogo unamimina ule nusu ya ute uliyobakisha ncha ya kiini na ute zitashikana unasubiri ukauke unakunja halafu unatoa unasubiri kipoe unakata shepu unayoitaka ukikata kiini cha njano kitakuwa Kati...andaa kwenye sahani yako pamba na saladi tayari kwa kula.
  2. Hakikisha hutoi unakunja humo humo kwenye frampen wala hungeuzi ili kishikane wakati wa kukunja na pia wakati ukiendelea nayo inaendelea kuiva.
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni
close