Featured Post

NGUVU YA KITANDA

Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5. Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha.
♦♦♦♦♦
Hiyo iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala. Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.
♦♦♦♦♦
Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu. Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugomvi? Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugomvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kumpapasa mwingine.
♦♦♦♦♦
Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremala avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.💞💞💞💞💞💞💞💞💞💞
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni