Featured Post

NAMNA YA KUKOKOTOA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI

JINSI YA KUFAHAMU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI

Mfano leo umepata bleed tarehe 12/10/2019
Basi tarehe 12/10/2019 inakuwa siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi,
Na tarehe 13/10/2019 inakuwa siku yako ya pili ya mzunguko wa hedhi
Na teherhe 14/10/2019 inakuwa siku ya tatu kadhalika
tarehe 15/10//2019 ni siku ya 4
tarehe 16/10/2019 ni siku ya 5

Nakuendelea, utakoma kuhesabu mzunguko wako wa hedhi mara tu unapopata hedhi ingine.

Ikiwa Utapata bleed ingine tarehe 10/11/20179 Basi siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi inakuwa tarehe 09/11/2019. Na tarehe 10/11/2019 inakuwa ni siku yako ya kwanza ya mzunguko wa mwezi wa 11

 • [message]
  • ZINGATIA:
   •  mwezi unaweza kuwa na siku 31,28,29 au 30 - kwa hiyo kama hujui ukubwa mbalimbali wa miezi lazima utumie kalenda yako vizuri.

Mfano wa Asha 

Amepata bleed yake tarehe 02/10 ikaisha 05/10/19

KWANZA SIKU ZAKE ZA HEDHI 

kwa mwezi wa 10 au siku za kuwa mwezini ni 4 yaani
tarehe 02/10
tarehe 03/10
tarehe 04/10
tarehe 05/10

Mwezi huohuo wa kumi akipata bleed tena siku ya tarehe 28/10/017 na ikaisha tarehe 02/11.
2- Siku za hedhi kwa mwezi wa 11 ni 6 yaani kuanzia tarehe
tarehe 28/10
tarehe 29/10
tarehe 30/10
tarehe 31/10
na taerehe 01/11
na tarehe 12/12

JE ANAMZUNGUKO WA HEDHI WA SIKU NGAPI KWA MWEZI WA 10?


 • [message]
  • ZINGATIA:
   • HAKIKISHA UMEWEKA ALAMA kwenye kalenda tarehe zako za kuanza kwa bleed

Namna ya kufanya

1- aliingia mwezini kwanza tarehe 02/10
2 - akaimgia tena mwezi huo huo tarehe 28/10

A. Siku ya kwanza ya ku bleed ni tarehe 02/10 - hii ndio siku ya kwanza ya kuanza kuhesabu siku za mzunguko wako wa hedhi.
2. Siku ya mwisho ya mzunguko wa hedhi ni tarehe 27/10 na sio 28/10
Utahesabu mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi kuanzia siku ya tarehe 02/10 hadi tarehe 27/10.


 • [message]
  • KITU CHA KUFANYA:
   •  kila unapoanza kubleed unaweka alama nyekundu mfano tarehe 02/10 pia weka alama ya X kwenye tarehe 28/10


kisha hesabu siku zote zilizopo kati ya terehe 02/10 na tarehe 27/10. UKISHESABU SIKU HIZO UNAPATA SIKU 26.
Kwa hiyo Asha wa Makoroboi Mwanza anamzunguko wa siku 26.

BAADA YA KUJUA NAMNA YA KUKOKOTOA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI

Vitu ambazo unaweza kujua baada ya kufahamu mzunguko wako una chukua siku ngapi na ni waaina gani:

 1. - ujue namna ya kukokotoa siku zako za salama
 2. - ujue kukokotoa siku za uzazi
 3. - ujue kukokotoa siku ya kupata mimba
 4. - ujue kukotoa siku za hatari


Ili ufanikiwe kabisa katika zoezi hili basi huna budi kujua mizunguko yako ya hedhi ya zaidi ya miezi mitatu, na katika kuijua mizunguko hiyo pia inafaa utambue ya kwamba kunayo mizunguko ya hedhi ya aina mbalimbali na yote inaweza kufaa au kutokufaa ilimradi ipo kati ya siku 20 na 35. Nje na hapo mzunguko wako unakuwa siyo mzuri.

Labda utajiuliza kwa nini mzunguko wa siku chini ya 20 ni mbaya na mzunguko wa siku zaidi ya 35 ni mbaya?
- ni kwa sababu ili matukio muhimu ya uzazi yapate kufanyika kwa ufasaha ndani ya mwili wako basi angalau kwa wastani huchukua siku 28, au siku za chini kabisa ni siku 20 na angalua siku za juu kabisa ni 35. lasivyo kuna baadhi ya vitu vitakuwa havikamiliki au vinachukua muda mrefu isivyokawaida.
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni