Featured Post

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 10

MWAJUMA UTAMU

            SEHEMU YA 10

          WHATSAPP 0655585220

                  ZANZIBAR 

Tetesi za jini mweusi zilitufanya tukaanza kuishi maisha ya hofu, kila changudoa akaanza kuwa makini na usalama wa maisha yake, gari lolote lenye rangi nyeusi lililoonekana likiingia na kupaki eneo hilo la Afrika sana tulipoliona tulikimbia, tuliamini ndiyo jini huyo mweusi aliyekuwa akiwaua machangudoa.

Hali ya sintofahamu ilitukumba, jeshi la polisi liliingilia kati, msako dhidi ya muuaji huyo ukaanza kufanyika lakini haikuishia hapo tu, pia walianza kuwakamata machangudoa na kuwafikisha mbele ya sheria.

Vyombo vya habari navyo havikuwa mbali, viliendelea kuripoti taarifa za muuaji huyo ambaye alisumbua sana na mpaka kufikia wakati huo hakukuwa na dalili zozote za kupatikana.

Kipindi hicho ukurasa wangu ya Mwajuma Utamu ulikuwa umefikisha wafuatiliaji 500,000. Ulikuwa ni ukurasa ambao baadae niliutumia kwa kuwauza machangudoa wengine.

Suzie huyu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu lakini pia alikuwa ni changudoa, alikuwa akiishi hostel. Nilifahamiana naye kipindi ambapo tetesi za jini mweusi zilivuma.

Suzie alipofahamu nimepata mwanaume tajiri ambaye alininunulia gari pamoja na nyumba ya kifahari maeneo ya Msasani, hakutaka kuamini, alionekana kunishangaa kupita kawaida.

Kwa jinsi alivyokuwa akiniangalia usoni, macho yake yalionyesha kuniuliza kwanini niliendelea kufanya biashara ya uchangudoa wakati nilipata mwanaume ambaye alikuwa na pesa na tayari alinifanyia mambo makubwa katika maisha yangu.

“Kwanini usitulie tu na Martin, anaonekana kweli anakupenda?” aliniuliza Suzie.
“Hapana siwezi,” nilimjibu
“Kwanini au hujampenda?”
“Sijazoea kuwa na mwanaume mmoja katika maisha yangu, nisipofanya mapenzi na wanaume zaidi ya wawili najiona kama sijakamilika.”
“Jitahidi kwa Martin, anaonekana kuwa mtu mwema kwako.”
“Nitatulia lakini sio sasa, acha niendelee na uchangudoa wangu mpaka pale nitakaposema basi.”
“Sawa ila kuwa makini maana siku akigundua kuwa wewe ni changudoa nadhani huo ndiyo unaweza kuwa mwisho wa mahusiano yenu.”
“Hilo haliwezi kutokea na hata kama likitokea siogopi kitu kwanza nishamchuna sana,” nilimwambia.
Urafiki wangu na Suzie uliendelea kila siku, nilimshauri ajipige picha za utupu kisha nikamuweka katika ukurasa wangu, huko nilimtafutia wateja, nikamuunganisha nao, safari ya kupiga pesa mitandaoni ikaendelea.
Nilifanya mambo yote hayo lakini Martin Sepeku hakufahamu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia, alikuwa ni mtu wa kusafiri mara kwa mara. Safari zake nyingi zilikuwa ni za nje ya nchi hivyo ilikuwa ni vigumu kugundua lolote.
“Nataka kukuoa Mwajuma uwe mke wangu kabisa,” aliniambia Martin siku moja kabla ya safari yake ya kwenda Dubai.
“Unafikiri itawezekana?” nilimuuliza.
“Kwanini isiwezekane au ugumu uko wapi?”
“Dini.”
“Dini sio tatizo mpenzi wangu ninachokitaka ni kufunga ndoa na wewe, nakupenda sana Mwajuma.”
“Nakupenda pia Martin lakini….”
“Nipo tayari kubadilisha dini kwasababu yako, nikirudi kutoka Dubai nataka nihalalishe mahusiano yetu au hupendi kuona siku nakuwa baba wa watoto wako na wewe unakuwa mama wa wanangu?”
“Napenda.”
“Basi nikubalie hili litimie kwanza.”
“Sawa litatimia,” nilimjibu.
Kichwa kilianza kuniuma baada ya kumsikia Martin alihitaji kufunga ndoa na mimi kipindi atakaporudi kutoka safari yake ya Dubai. Kiukweli sikuwa nimejipanga katika hilo wala moyoni mwangu sikuwa nina mapenzi ya dhati na Martin.
Nilichokuwa nimekifuata kwake ni pesa pamoja na mali alizonimilikisha. Suala la kufunga ndoa nililiona kuwa gumu hasa kwa mtu kama Martin ambaye sikumpenda kutoka moyoni mwangu.
Nilipomueleza Suzie habari hizo alionekana kufurahi, aliniambia nisikubali nafasi hiyo ipotee, alienda mbali zaidi na kuniambia kama angekuwa ni yeye angekubali tena bila kipingamizi chochote.
“Ungekubali?” nilimuuliza.
“Ndiyo mimi ningekubali shoga yangu, embu angalia jinsi maisha yalivyokuwa magumu, angalia tunavyoteseka katika biashara hii, wakati mwingine tunakutana na wanaume wenye maumbile makubwa, kwasababu tunahitaji pesa tunakubali kufanya nao mapenzi, tunapata maumivu makali sana, hivi hii biashara tutaifanya mpaka lini?” aliniuliza Suzie kwa uchungu kisha akaendelea.
“Kama huyo mwanaume anakupenda na ana malengo na wewe naomba utulie naye, hii biashara ni bora ukaachana nayo tu,”aliniambia.
Maneno ya Suzie yalianza kuniingia, niliyatafakari na kuona kuwa yalikuwa na ukweli mtupu lakini tatizo lilikuja sehemu moja, sikumpenda Martin kutoka moyoni mwangu, kwake nilifuata pesa na maslahi mengine ambayo nilikuwa tayari nimeshayapata.
Nilipoona Suzie ananing’ang’aniza nikubali kuolewa na Martin ilibidi nilimueleze ukweli kuwa sikumpenda kama alivyokuwa akiamini, nilimpendea pesa zake na hiyo ndiyo ilikuwa tamaa yangu.

Je, nini kitaendelea?

By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni