Featured Post

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 08

MWAJUMA UTAMU

                    SEHEMU YA 8

                WHATSAPP 0655585220

                         ZANZIBAR 

Lengo la kuyaandika haya yote sina maana kwamba wasichana wenzangu wanaopitia maisha magumu, waamue kujiingiza kwenye biashara ya uchangudoa kwasababu tu inalipa la, isipokuwa nataka kuwaonyesha jinsi biashara hii ilivyokuwa na madhara makubwa na mwisho wake unavyokuwa mbaya.
Nilikuwa tayari nimefanikiwa kupanga nyumba maeneo ya Sinza kwa Remi, maisha yalikuwa mazuri tu, kipindi hicho nilikuwa nimeshafungua akaunti benki na pesa nilizokuwa nikizipata nilikwenda kuzihifadhi huko.
Nilikuwa katika mipango ya kununua kiwanja ambapo ningeanza ujenzi haraka iwezekanavyo hivyo nilihitaji kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa.
Hitaji langu kubwa lilikuwa ni kufanya biashara nyingi ambazo zingezidi kuniingizia pesa nyingi tofauti na biashara ya uchangudoa hivyo muda mwingi nilikuwa nikifikiria ni biashara gani ambayo nilitakiwa kuifanya katika kipindi hicho.
Pesa ilizidi kuchukua nafasi kubwa sana kwani hata nilipokuwa nikiwaza biashara ambayo nilitakiwa kuifanya bado pesa ilihitajika.
Unajua unaweza ukamkuta mtu ana wazo zuri la kufanya biashara lakini unakuta hana pesa, anashindwa kutimiza lengo lake, anaona ugumu, anakata tamaa na mwisho wa siku anaamua kujiingiza kwenye mambo yasiyompendeza Mungu.
Kila kitu kinachotokea katika maisha kina sababu yake, wakati mwingine Mungu anaamua kukupitisha katika wakati mgumu wa maisha ili kusudi akupime, aone utawezaje kuyastahimili.
Ni Binadamu wachache sana ambao wanapopata matatizo kitu cha kwanza wanachokikumbuka ni Mungu pekee, wanasali na kumuomba huku wakiamini hicho ni kipindi cha mpito na muda wowote maisha yanaweza kubadilika.
Sikuwa ni miongoni kati ya binadanu hao wenye imani thabiti, imani yangu ilikuwa ndogo mno. Kitu nilichokiamini katika maisha yangu ni pesa na ndiyo niliyoamini ingeweza kuyabadilisha maisha yangu, kama iliweza kusababisha nikapanga nyumba, nikaishi maisha mazuri basi niliamini pia ingeweza kunitimizia mahitaji yangu yote.
Siku zilizidi kukatika huku nikiendelea kufanya biashara ya uchangudoa bila mtu yoyote kufahamu hilo, ilikuwa ni siri yangu na sikutaka mtu yoyote afahamu.
Katika kipindi hicho nilipokuwa Sinza wanaume wengi walianza kunifukuzia, nilipata usumbufu mara kwa mara, kila mwanaume alihitaji kuwa na mimi.
“Nakupenda Mwajuma,” aliniambia mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Samir.
“Asante nashukuru kwa upendo,” nilimjibu, akaonekana kuchukizwa na jibu langu lenye madharau.
Samiri hakuwa ndiye mwanaume wa kwanza kumkataa, hapo kabla nilikuwa tayari nimeshawakataa wanaume kama watano hivi, sikutaka kuwa nao kimapenzi, niliwaambia wanipe pesa kisha nikaweza kulala nao kila mmoja kwa nafasi yake.
“Kwahiyo?” aliniuliza.
“Kuhusu nini?”
“Nakupenda, nahitaji kuwa na wewe.”
“Una pesa?”
“Ndiyo ila nikubalie kwanza niwe wako.”
“Sasa sikia hatutakiwi kuwa wapenzi, wewe nipe pesa nikupe mapenzi uondoke zako sitaki stress,” nilimwambia kisha akaonekana kunishangaa.
“Nini?” nilimuuliza.
“Unajiuza?”
“Ndiyo kama umeupenda mzigo ulipie ukalale nao usiku mzima,” nilimjibu kisha nikageuka na kumtishia sehemu za nyuma ya maumbile yangu, nilifahamu nilijaaliwa chura hivyo nilifanya makusudi.
Samir akazidi kuchanganyikiwa, kwa jinsi alivyokuwa akinitazama kwa macho, alionekana kuwa na hamu ya kuuona uhodari wangu kitandani.
“Kwani ni bei gani?” Aliniuliza, jinsi alivyokuwa akionekana, alionekana kuwa ni mtu mwenye pesa zake.
“Nipe laki mbili tukalale baby wangu,” nilimjibu.
“Hakuna shida,” aliniambia kisha tukaenda kulala kwenye lodge moja, huko hakukuwa na maongezi mengi zaidi ya kufanya mapenzi tu.
Nilikuwa nikijua kufanya mapenzi kuliko kitu chochote hapa duniani, nilijua kucheza mpira dakika zote tisini, mwanaume niliyelala naye nilihakikisha nafanya naye kila aina ya staili, nilijitoa ufahamu wakati wa kufanya mapenzi. Kama ni kukata viuno basi nilikata sana siku hiyo, yaani kila nilichokuwa nikikifanya kilikuwa ni cha tofauti.
Hapa ndipo wanawake wengi wanapofeli, unakuta umeolewa na mwanaume na umeishi naye kwenye ndoa zaidi ya miaka kadhaa na tayari mmefanikiwa kupata watoto. Maisha yanazoeleka, unafika wakati hata tendo la ndoa unafanya kwa mazoea kwasababu umeshamzalia watoto mumeo basi unaamini hawezi kuchepuka, ataendelea kuwa wako.
Maisha hayo mwanaume hawezi kuyavumilia, mwisho wa siku kisirikisiri atatafuta mchepuko wake au kwa wale wasiopenda kuwa na michepuko wanaangukia mikononi mwa Malaya, wanayofanyiwa wakati wa tendo la ndoa yanawashangaza na taratibu anajikuta akimsahau mke wake.
Usiku wa siku hiyo nilihakikisha nimempagawisha Samir vya kutosha, ingawa kuna imani ipo kuwa wanaume ndiyo waliyozoeleka kuwa hatari zaidi wakati wa kufanya mapenzi na kuwaridhisha wanawake lakini kwangu ilikuwa ni kinyume chake, nilijua kufanya mapenzi na kumtoa jasho mwanaume, kukurukakara na purukushani zote za kitandani nilizijua.
Siku iliyofuata Samir alinilipa pesa kama tulivyokuwa tumekubaliana na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa biashara yetu.
Japokuwa niliendelea kupata pesa lakini akili yangu ilikuwa ikifikiria kununua kiwanja kisha kuanza ujenzi wa nyumba yangu, nilikuwa nikifikiria pia kufungua biashara zangu mwenyewe.
“Fungua akaunti Facebook kisha Create page uanze kujitangaza, utapiga hela ndefu,” alinishauri Savela nilipomuelezea mipango yangu.
“Hiyo imekaa vipi?” Nilimuuliza.
“Ukifungua utakuwa ukipost picha na video za ngono halafu utakuwa ukitangaza biashara, lazima utapata wateja ila katika hizo picha utakazokuwa ukipost jaribu kuzikata kichwa usionekane,” alinijibu kwa ufafanuzi kisha akaendelea kuzungumza.
“Biashara sasa hivi imebadilika, kuna wateja wengi sana mitandaoni, wapo baadhi ya wanaume wanaogopa kwenda Sinza kutafuta Malaya, wengine wanaogopa kuonekana, kwa kutumia njia hii ya mtandao ni lazima utawapata wateja wote hao tena wengine wapo nje ya nchi kama vile Kenya, Uganda na nchi nyingine,” aliniambia.
“Na hao wateja wa nje ya nchi nitawafikiaje?”
“Wengine pesa ipo, wanakufuata au wanakutumia kila kitu, kazi yako ni kwenda kuwapa mapenzi tu.”

Je, nini kitaendelea?

By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni