Featured Post

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 07

MWAJUMA UTAMU

                SEHEMU YA 7

         SEHEMU YA 0655585220

              ZANZIBAR 

Safari yetu iliishia nje ya hoteli moja ya kifahari iliyokuwepo maeneo ya Sinza Makaburini. Hatukutembea umbali mrefu sana kutokea Sinza Afrika sana, ulikuwa ni mwendo kama wa dakika kumi na tano hivi tukawa tayari tumeshafika katika hoteli hiyo.
Ibra hakutaka kupoteza muda, alichukua chumba na baada ya muda mfupi tukaingia ndani ya chumba hicho. Kila nilipokuwa nikimtazama Ibra nilikuwa nikiogopa, niliingiwa na wasiwasi, sikuwa huru kabisa, nilitamani masaa yakimbie ili niondoke mahali hapo.
Tulipokuwa ndani ya chumba cha hoteli hiyo hakukuwa na stori nyingine alizoziongea Ibra zaidi ya mapenzi, umbo langu lilionekana kumchanganya kupita kawaida, muda wote alikuwa akinisifia.
“Umewahi kulala na wanaume wangapi?” aliniuliza.
“Wawili tu,” nilimjibu.
“Kumbe mtoto bado mbichi kabisa?” aliniuliza.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Leo nataka uniliwaze, nataka unipe mapenzi mpaka nimsahau mke wangu huko alipo,” aliniambia huku akitabasamu.
“Kumbe una mke?” nilimuuliza kwa mshangao.
“Ndiyo nina mke lakini naishi kama sina mke.”
“Kivipi?”
“Amepooza hivyo naishi naye kama sanamu tu, siwezi kufanya lolote lile,” aliniambia huku akiniomba tusiyazungumzie hayo.
Ibra hakutaka kupoteza muda, alianza kunipapasa huku akijaribu kunionyesha fundi aliyokuwa nao wa kucheza na hesabu za 2x+3y.
Nilisisimka mwili, hata hivyo sikutaka kubaki nyuma ya mchezo, sikutaka kuendelea kuwa shabiki wakati jezi nilikuwa nayo na mchezo niliufahamu.
Nilikuwa nikifahamu mbinu na michezo yote ya kitandani. Hakukuwa na kitu kigeni kwangu, siku hiyo haikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kufanya mapenzi.
Kila kitu nilichokuwa nikikifanya kilimshangaza sana Ibra, hakutaka kuamini kama nilifahamu mambo yote yale.
Nisingependa kusimulia kila kitu nilichokifanya usiku huo kwasababu ya kuheshimu sheria za kimitandao ila nataka mfahamu kuwa nilifanikiwa kufanya mapenzi na Ibra tena kwa kiwango cha juu kabisa.
Asubuhi ya siku iliyofuata tuliamka kisha tukaenda kuoga kwa pamoja, tulipomaliza tulijiandaa tayari kwa kuondoka.
“Umenifurahisha sana mrembo, umenipa mapenzi ambayo sijawahi kupewa hapo kabla, hivi nani aliyekufundisha?” Aliniuliza.
“Hakuna mtu aliyenifundisha,” nilimjibu kwa kujiamini.
Nilishangaa akitoa kiasi cha pesa kama laki mbili na nusu hivi kisha akanipa, nilipokea na kumshukuru.
“Hutakiwi kusema asante, hiyo ni haki yako,” aliniambia huku akikenua.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kulala na wanaume tofauti tofauti, kila siku nilikuwa nikifanya nao mapenzi na walikuwa wakinilipa vizuri.
Katika kipindi hicho biashara ya uchangudoa ilionekana kuwa nzuri kwa kiasi fulani, ilikuwa ikinipa faida kubwa na lilikuwa ni jambo gumu kuiacha biashara hiyo kwani tayari ilikuwa ni sehemu moja ya maisha yangu. Kila kitu nilichokuwa nikikifanya, kuanzia kula yangu, kuvaa kwangu ilitokana na biashara hiyo.
Kipindi hicho bado nilikuwa nikiishi nyumba moja na Savela, tangu alipoweza kunisaidia na kuniingiza katika biashara ya uchangudoa.
Nilikuwa nikifanya mapenzi na wanaume wanne na wakati mwingine nilikuwa nikifanya mapenzi na wanaume sita kwa siku. Walikuwa wakinilipa vizuri.
Kwa siku nilikuwa sikosi si chini ya laki moja na nusu, biashara ya siku hiyo ikiwa nzuri zaidi nilikuwa naingiza laki mbili.
Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kwa wakati huo, sikujali nililala na mwanaume wa aina gani, mwenye umri upi, yeyote aliyejitokeza na pesa nilienda kulala naye.
Nilitengeneza kiasi kikubwa cha pesa tena ndani ya muda mfupi.
Savela alionekana kukubuhu katika biashara ya uchangudoa, kipindi ambacho nilikuwa nikienda Sinza kujiuza yeye alibaki nyumbani, wanaume walikuwa wakimfuata.
Sikutaka kuendelea kuishi nyumba moja na Savela, kwa kuwa nilifanikiwa kutengeneza kiasi kizuri cha pesa nilipanga kupanga nyumba yangu ili niweze kuwa huru zaidi.
Nilipomwambia Savela kuhusu mipango hiyo alionekana kufurahi, alinipongeza kwa hatua nzuri ambayo nilikuwa nimefikia.
“Kwahiyo umepanga kuishi wapi?”
“Sinza.”
“Sawa.”
Baada ya siku kadhaa kupita, nilitafuta dalali ya nyumba ambaye nilimuelezea nyumba niliyokuwa nikiihitaji.
Dalali alionekana kuifahamu Sinza kiundani, baada ya kunisikiliza kwa muda mfupi akaniambia nyumba ilikuwepo tena kama ningezembea kuna mtu mwingine alikuwa akiihiitaji.
“Iko wapi?”
“Sinza kwa Remi.”
“Ni nzuri?”
“Ndiyo tena itaendana na hadhi yako,” aliniambia dalali.
Sikutaka kupoteza muda, nilienda naye mpaka kwenye nyumba hiyo ili nione kama kweli yale aliyokuwa akinieleza kuhusu nyumba hiyo yalifanana.
Kweli bana nilipofika nilikuta kila kitu nilichokuwa nikikihitaji katika nyumba, ilikuwa ni nyumba ya vyumba vitatu, sebule, chumba, jiko pamoja na choo.
“Umeipenda?” Aliniuliza dalali.
“Ndiyo nimeipenda, ni nyumba nzuri,” nilimjibu huku nikiendelea kuishangaa nyumba hiyo.
Baada ya makubaliano na dalali alinikutanisha na Mama mwenye nyumba hiyo, aliyejulikana kwa jina la Bi Latifa. Nilipokutana naye alinieleza kila kitu kuhusu nyumba yake, haikuwa na tatizo lolote na aliniambia angenipangishia kwa shilingi laki mbili na nusu kila mwezi.
“Laki mbili na nusu?” Nilimuuliza.
“Ndiyo tena nimekupunguzia baada ya kukuona, nilikuwa naipangisha kwa laki tatu au Jafari hujamwambia?” Aliniambia huku akimuuliza yule dalali.
Kwa kuwa nilikuwa nina shida na uhitaji mkubwa wa nyumba kwa wakati huo sikutaka kubisha wala kuweka longolongo nyingi, nilichoamua kukifanya ni kuingia mkataba na Bi Latifa.
Nilimlipa kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano, kodi ya miezi sita kama mkataba alivyokuwa ukisema. Bi Latifa alifurahi sana baada ya kumpatia kiasi hicho cha pesa.
Hatimaye niliyaanza maisha mpya katika nyumba hiyo, nilinunua kila kitu kilichokuwa kikihitajika ndani ya nyumba.
Kwa maisha niliyokuwa nikiishi ilikuwa ni vigumu mtu kuamini kama nilikuwa ni changudoa ambaye nilivizia usiku ndipo niende kufanya biashara hiyo.
Je, nini kitaendelea?

By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni