MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 06

MWAJUMA UTAMU

              SEHEMU YA 6

               WHATSAPP 0655585220

                        ZANZIBAR 

Hakukuwa kuna kitu nilichokuwa nikikitamani kama kuwa na maisha mazuri. Niliutamani sana utajiri, nilipokuwa nikimsikia mtu akipiga stori za pesa nilihisi kusisimka mwili.
Kipindi hicho biashara niliyoambiwa kuwa ingeweza kunipa utajiri wa haraka ilikuwa ni ya uchangudoa, yaani nilitakiwa kujiuza kwa wanaume ambao wangenilipa na mwisho wa siku maisha yangu yangeweza kubadilika.
Mwanzoni biashara hiyo ya uchangudoa haikuniingia akilini, niliogopa kuifanya lakini Savela aliendelea kunishawishi.
Siku moja majira ya usiku alinipeleka Sinza kwenye klabu moja maarufu sana, Ambiance. Ilikuwa ni sehemu maarufu kwa wasichana kufanya biashara hiyo ya uchangudoa.
Macho yangu hayakutulia sehemu moja, nilikuwa nikiyashangaa mazingira niliyokutana nayo mahali hapo, wakati huo tulikuwa tumekaa nje ya baa hiyo upande ambao niliweza kuiona barabara ya Shekilango.
“Unashangaa nini?” aliniuliza Savela, wakati huo alikuwa ameagiza pombe kwa muhudumu aliyekuja kutusikiliza.
“Hakuna kitu,” nilimjibu huku nikijiweka sawa.
Muhudumu huyo akanigeukia na kuniuliza kuwa nilihitaji nini kwa muda huo, sikuwa ni mtumiaji wa kilevi chochote, nilimuagiza soda.
Jibu hilo likamshangaza sana Savela, akazidi kuniona nilikuwa mshamba sana.
“Hutumii pombe?” aliniuliza, muda huo yule muhudumu alikuwa tayari ameenda kuleta vinywaji.
“Ndiyo,” nilimjibu.
“Kwanini?”
“Sijazoea.”
“Mmh!”
Baada ya dakika kama tatu hivi yule muhudumu aliweza kurudi na vinywaji, alipomaliza kutuhudumia nikashangaa akimsogelea Savela, akamnong’oneza kitu, nikamuona Savela akitabasamu. Sikufahamu kwa muda huo ni nini kilichokuwa kikiendelea. Nilianza kuinywa soda yangu taratibu huku nikiendelea kuyashangaa mazingira ya sehemu hiyo. Kwa mbali niliwaona wasichana watatu waliyokuwa wamevalia mavazi yaliyowaacha sehemu kubwa za mwili wao kuwa wazi, walikuwa wakiikimbilia gari iliyokuja na kupaki eneo hilo la baa, walikuwa wakigombaniana, kila mmoja alihitaji kuwa karibu na kioo ambacho kilifungiliwa na dereva wa gari hilo. Baada ya sekunde chache wasichana wawili wakaondoka na kubaki msichana mmoja, mazingira niliyoyaona yalitafsiri wazi kulikuwa kuna biashara ya uchangudoa iliyokuwa inafanyika, kuna muda yule msichana nilimuona akiwa anajigeuza sehemu za nyuma ya maumbile yake. Haikuchukua muda, msichana yule akaingia ndani ya gari kisha likawashwa na kuondoka.
“Mwajuma,” aliniita Savela baada ya yule muhudumu kuondoka.
“Abee,” nilimuitikia.
“Umemuona huyu muhudumu?”
“Ndiyo nimemuona kwani amefanya nini?”
“Kuna mtu amemuagiza aje kuniambia kuwa ananiita.”
“Mtu gani?”
“Ni mwanaume.”
“Mmh!”
“Subiri nikaongee naye,” aliniambia kisha akainuka na kwenda kwenye meza iliyokuwa jirani kidogo na sisi.
Katika meza hiyo alikuwa amekaa mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa na mwili wa miraba minne, pembeni yake alikuwa amekaa msichana mmoja ambaye alionekana kuwa katika mavazi yaliyomuweka nusu uchi.
Savela alipofika katika meza hiyo nikamuona akikumbatiana na yule mwanaume, walionekana kama ni watu wanaofahamiana muda mrefu hivyo sikutaka kujaji sana, niliendelea kunywa soda yangu huku nikiwa sina wasiwasi wowote.
Bado niliendelea kuwashuhudia wasichana wakifanya biashara ya uchangudoa, biashara ilikuwa ikifanyika waziwazi wala hakukuwa na mtu aliyeonekana kuogopa au kushangaa, ilionekana kuwa ni biashara ya kawaida ambayo watu walizoea kuiona.
Nilibaki peke yangu katika meza hiyo mpaka pale ambapo Savela alirudi, aliniambia kuwa nilitakiwa kwenda kukaa naye meza moja na yule mwanaume aliyekuwa akizungumza naye, nilimkubalia kisha nikaenda kukaa naye katika meza ya mwanaume huyo, tulihamisha na vinywaji vyetu.
Yule msichana niliyemuona mwanzo akiwa amekaa na mwanaume huyo akainuka na kutupisha halafu nikamuona akimpa ishara fulani Savela ambayo nilishindwa kuielewa maana yake.
“Mwajuma huyu anaitwa Ibra, the big boss. Ibra huyu anaitwa Mwajuma ni msichana wangu na yeye ndiyo anainza hii kazi,” alinitambulisha kwa mwanaume huyo ambaye nilishikana naye mikono.
“Okay..anaonekana kuwa mrembo sana aisee nahisi hata yale mambo yetu yatakuwa mazuri,” alisema Ibra huku akitabasamu.
“Ndiyo hapo ni wewe tu sema kingine,” alisema Savela kisha Ibra akanitazama, Savela akaniambia nisimame, nikafanya kama alivyoniambia.
Unajua huwa sipendi kujisifia sana lakini kwenye ukweli acha niwaambie, nilikuwa nina chura, nadhani ninaposema nilikuwa nina chura mmeshanielewa nini ninachokimaanisha, nilikuwa nina kila sifa zinazoweza kumteka mwanaume rijali.
Ibra aliponiona alizidi kupagawa, alikosa neno la kuzungumza kwa wakati huo, muda wote huo macho yake yalikuwa yakiangalia chura yangu.
“Mimi nilikwambia chombo si cha nchi hii,” alisema Savela huku akitabasamu, aliimimina pombe kwenye glas kisha akanywa.
“Duh! Hiki chombo si mchezo ni balaa,” alisema Ibra, wakati huo tayari nilirudi kukaa.
Mazungumzo yaliyokuwa yakizungumzwa mahali hapo yalikuwa ni ya kibiashara, Ibra muda wote alikuwa akanitazama.
Nilitakiwa kufanya biashara ya uchangudoa na nilikubali kuifanya hivyo kila kitu kilichokuwa kikiendelea nilikubaliana nacho bila wasiwasi wowote, niliamini ilikuwa ni biashara ambayo ingeweza kunipa utajiri wa haraka.
“Kwahiyo mnakula nini?” aliuliza Ibra wakati huo alimuita muhudumu akawa anasubiria oda yetu.
“Mimi niletee mchemsho wa ndizi nyama,” alisema Savela.
“Mimi niletee chochote tu,” nilijibu jibu lililowafanya wote wakacheka.
“Hakuna chakula hicho, wewe sema unataka chakula gani?” aliniuliza Ibra.
“Basi niletee Chips,” nilisema.
“Chips nini, kuna mayai, kuku, mishikaki au kavu unataka?” aliniuliza yule muhudumu, alikuwa ni wa kiume.
“Chips mayai,” nilimjibu kisha akamgeukia Ibra na kumuuliza huduma ya chakula ambacho alihitaji.
“Hapana nipo sawa aisee, wewe wahudumie hawa warembo tu usijali,” alijibu kisha yule muhudumu akaondoka, baada ya dakika kadhaa alirudi na vyakula tulivyomuagiza.
Tulianza kula huku stori za hapa na pale zikiendelea, Savela aliniambia siku hiyo nilitakiwa kwenda kulala na Ibra.
Kiukweli kila nilipokuwa nikimuangalia Ibra jinsi alivyokuwa akionekana halafu nilipokumbuka kuwa usiku huo nilitakiwa kwenda kulala naye nilihisi kuingiwa na uwoga.
“Hutakiwi kuogopa kitu Mwajuma halafu tafadhali naomba usiniangushe,” aliniambia Savela.
“Sawa dada siwezi kukuangusha,” nilimwambia kisha tukaendelea kula mpaka pale ambapo tulimaliza, Ibra akalipa bili ya chakula.
“Kwahiyo nini kinachofuata?” aliuliza Ibra huku akimtazama Savela, hapohapo nikamuona Savela akinipa ishara ya kuniambia niondoke na Ibra.
“Nitamrudisha asubuhi,” alisema Ibra kisha akanishika mkono tukaanza kuondoka.
“Sawa hakuna shida,” alisema Savela.
Tulifika mpaka alipokuwa amelipaki gari lake, tukapanda kisha tukaondoka.

Je, nini kitaendelea?

By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni
close