Featured Post

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 05

MWAJUMA UTAMU 

                  SEHEMU YA 5

               WHATSAPP 0655585220

                   ZANZIBAR 

Siku moja nilikutana na msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Savela, aliponiona alihitaji kunisaidia. Nilipojitambulisha Savela alianza kunisifia, nikashangazwa na sifa zake yaani iliwezekana vipi msichana mwenzangu kama yeye akaanza kunisifia kama mwanaume?
Hilo lilinifanya nianze kuogopa, nilihisi Savela hakuwa mtu mwema kwangu, nilipokuwa nikimuangalia nikatamani anipe pesa kisha niondoke zangu.
Baada ya Savela kunihoji na kugundua mengi yaliyokuwa yamenitokea, alihitaji kunisaidia.
Nilisita kuchukua maamuzi ya haraka lakini baada ya kujifikiria maisha ambayo tayari nilikuwa nikiishi nilijikuta nikikubali tena bila kipingamizi chochote.
Alinichukua na kunipeleka mpaka nyumbani kwake alipokuwa akiishi maeneo ya Tegeta. Kwa muonekano wa nyumba yake jinsi ilivyokuwa ikionekana ilikuwa ni vigumu kuamini kwamba Savela ndiye ambaye alikuwa mmiliki wa nyumba hiyo, hakufanania kabisa.
“Hapa ni kwako?” nilijikuta nikiropoka na kumuuliza.
“Ndiyo hii ni nyumba yangu,” alinijibu huku akionekana kuwa kawaida, hakujali lolote.
“Hongera ni nyumba nzuri sana,” nilimwambia huku macho yangu yakiendelea kutazama sehemu za nyumba hiyo.
“Unaishi na nani?” nilimuuliza.
“Peke yangu,” alinijibu.
Ilionekana kuwa ni nyumba kubwa iliyokuwa na vyumba vingi sana, kitendo cha Savela kuniambia kuwa aliishi peke yake kilinishangaza sana, sikutaka kuamini lakini huo ndiyo iliyokuwa ukweli.
Siku hiyo ikapita huku nikiwa nimeshapata bahati ya kufadhiliwa na Savela ambaye alionekana kuwa na moyo wa kipekee sana.
Hapa ngoja nikwambie kitu, nilikuwa mchafu sana, sikuwa na nguo zaidi ya niliyokuwa nimeivaa. Siku iliyofuata Savela aliamua kunipeleka kwenye duka la nguo maeneo ya Kinondoni, tulipofika huko alininunilia nguo, alinipeleka saluni ambapo huko nikazidi kupendezeshwa, ndani ya masaa kadhaa nilikuwa nimebadilika, sikuwa Mwajuma yule mchafu ambaye nilishindia nguo moja. “Kwanini unayafanya yote haya?” nilimuuliza.
Usijali Mwajuma nafanya haya kama masaada wangu kwako, najua umepitia magumu mangapi, sitaki kuona ukirudi kule wakati wewe bado ni msichana mrembo, unavutia, wasichana wenzako kama wewe mjini hawafi njaa, wanafanikiwa kiulaini,” aliniambia maneno ambayo aliniacha nayo njia panda.
“Unamaanisha nini?”
“Usijali muda ukifika utajua namaanisha nini au wewe hupendi kuona ukiwa na maisha mazuri, ukamiliki nyumba ya kifahari, ukamiliki gari la gharama, ukawa mfanyabiashara mkubwa sana hapa mjini yaani kila mtu akawa anakuzungumzia wewe tu?”
“Napenda ila…”
“Basi kila kitu kinawezekana, mimi binafsi nimewahi kuishi kama yako, niliteseka mno, hakukuwa na mtu wa kunisaidia yaani kama sio mimi mwenyewe kujitambua sijui leo hii ningekuwa wapi?” alisema Savela kisha akaendelea kuzunguza.
“Umeiona ile nyumba yangu ya Tegeta nimeinunua juzi tu, nafanya biashara inayoniingizia pesa nyingi mno, sijasoma lakini nimeweza kufanya vitu vikubwa ambavyo wasomi wameshindwa kuvifanya,” aliniambia Savela.
Kwa muda ambao Savela aliutumia kuzungumza na mimi tayari alikuwa ameipandikiza mbegu ya tamaa ya mafanikio ndani yangu, alijua kunishawishi, alijua kuzungumza yaani maneno yake yalitosha kunifanya nitamani kujua ni biashara gani hiyo ambayo alikuwa akiifanya.
Siku ziliendelea kukatika huku ujauzito nao ukiendelea kukua, mwanzoni nilimficha Savela hali niliyokuwa nayo lakini kama unavyojua mimba haiwezi kufichika mwisho wa siku alifahamu kila kitu.
Hakuonekana kuchukia baada ya kufahamu ukweli ambao nilimficha hapo awali, alinikumbusha kuhusu msaada ambao aliamua kunipa ulikuwa ni wa lengo la kufanya biashara. Ilibidi nimuulize ni biashara gani hiyo ambayo kila siku alikuwa akinidokeza na ndipo hapo ambapo aliniambia ukweli, aliniambia biashara hiyo ilikuwa ni ya uchangudoa yaani ilitakiwa nijiuze ili niweze kupata pesa, alienda mbali zaidi na kuniambia kuwa mafanikio yake yote yalisababishwa na biashara hiyo uchangudoa.
Nilihisi mwili wote ukipigwa na ganzi baada ya kuyasikia hayo, sikutaka kuamini hata kidogo, kuna muda nilidhani labda alinitania lakini hakukuwa na utani kati yangu na yake.
“Baba wa huo ujauzito ni nani?”
“Ni Oscar.”
“Anajua?”
“Ndiyo ila anifukuza, aliukataa.”
“Sawa, sasa kwenye kazi hii ya uchangudoa ujauzito hautakiwi, utakupotezea wateja,” aliniambia Savela.
Licha ya kuwa nilitokea katika maisha ya kimasikini pamoja na kukutana na changamoto zote mpaka kufikia hatua ya kukutana na Savela bado nilikuwa mwenye tamaa.
Tamaa ya utajiri ilishakwishaniingia, kila nilipokuwa nikimuangalia Savela pamoja na mafanikio aliyokuwa nao katika maisha yake sikutaka kuamini kama biashara hiyo ya uchangudoa ndiyo iliyomletea mafanikio yote hayo, kuna muda nilikataa lakini mwisho wa siku nilijikuta nikiamini.
Kwa kuwa nilikuwa tayari kufanya lolote Savela alinishauri niende hospitali nikautoe ujauzito niliyokuwa nao kwa madai kuwa ingeniharibia soko la biashara yangu ya uchangudoa.
Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, mipango ikaandaliwa kisha nikaenda kwenye hospitali moja ya kibinafsi maarufu sana hapa mjini, sitaweza kuitaja kwasababu za kibiashara.
Nilifanikiwa kuutoa ujauzito wa miezi mitatu, hilo lilimfurahisha Savela mno, aliniambia huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kutengeneza pesa na kuwa mwenye mafanikio kama aliyokuwa nayo yeye.
Kichwa changu kilikuwa kikifikiria mabilioni ya pesa, nyumba za kifahari, pamoja na biashara ambazo ningeweza kuzifungua kipindi ambacho ningefanikiwa katika biashara hiyo ya uchangudoa.
itaendelea..

  by Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni