MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 04 | BongoLife

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 04

MWAJUMA UTAMU 

              SEHEMU YA 4

              WHATSAPP 0655585220

                       ZANZIBAR 

Mwanzoni alionyesha moyo wa kunisaidia kweli, aliguswa na tukio langu la kufukuzwa.
Maisha yalianzia hapo huku kila siku mwanaume huyo akiniaga kwenda kwenye mihangaiko yake. Aligeuka kuwa msaada mkubwa sana kwangu, alinihudumia kwa kila kitu nilichokuwa nikikihitaji, aliyabadilisha maisha yangu.
Ama kwa hakika penzi ni kikohozi kama wasemavyo wahenga, baada ya kupita siku kadhaa nikajikuta nikiwa katika mahusiano na mwanaume huyo ambaye tayari nilifanikiwa kulifahamu jina lake. Nakumbuka alijitambusha kwa jina la Oscar, na ni katika penzi hilo ambalo lilienda kunipa funzo lingine jipya la maisha yangu. ****
Nilijikuta nikizama kwenye dimbwi la kimapenzi na Oscar, huyu alikuwa ni mpiga picha, alikuwa akimiliki studio yake ya picha iliyokuwepo Sinza Palestina.
Kimuonekano alikuwa ni kijana mtanashati, kiukweli nilitokea kumpenda kwa moyo wangu wote. Kipindi nipo katika mahusiano naye nilisahau shida na matatizo yote niliyokutana nayo katika maisha yangu, sikutaka kukumbuka kitu chochote kilichotokea nyuma.
Oscar alinipenda sana, ahadi zake za kunioa ndizo zilizonifanya nikazidi kumuamini mara dufu, bila kujali nikamkabidhi mwili wangu ambao aliutumia autakavyo.
Maisha yalibadilika kwa kiasi fulani, nilikuwa nikiishi maisha yenye furaha, Oscar aliendelea kunijali, alinipa matunzo pamoja na mapenzi moto moto.
Kiukweli wazo la kurudi nyumbani kichwani mwangu halikuwepo kabisa kwa wakati huo, niliona ni jambo gumu mno kurudi katika maisha ya kimasikini niliyozaliwa katika familia yetu.
Nilikuwa nikiishi maisha ya furaha yaliyogubikwa na amani tele, sasa kwanini nikumbuke maisha ya kimasikini ya nyumbani kwetu?
Hilo lilikuwa ni jambo gumu mno kutokea.
Siku ziliendelea kukatika huku penzi likizidi kupamba moto, Oscar aliendelea na kazi yake ya upiga picha, muda mwingi aliutumia katika kazi yake hiyo, mwanzoni sikuwa na wasiwasi wowote, niliamini katika mapenzi ya dhati pamoja kazi yake, sikutaka kumuwazia vibaya.
Baada ya kupitia mwezi mmoja nilianza kusikia maneno ya chinichini kutoka kwa majirani ambao tayari nilianza kuwazoea. Waliniambia kuwa Oscar alikuwa ni mume wa mtu na kipindi hicho mke wake alikuwa amesafiri.
Nilipoyasikia maneno hayo sikutaka kuamini hata kidogo, nilihisi walipanga kutugombanisha hivyo sikutaka kuyapa uzito maneno yao.
Maisha yaliendelea huku kila siku maneno yakiwa ni yaleyale. Mwanzoni nilionekana kuyapuuzia lakini nilipoona yamezidi ilibidi nimuulize Oscar.
“Nani kakuambia maneno hayo?” aliniuliza huku akionekana kukubwa na mshangao.
“Kuna watu wameniambia,” nilimjibu.
“Nilikwambia usipende kuamini kila unachoambiwa,” aliniambia.
Kiukweli ilikuwa ni vigumu kuamini kama Oscar alikuwa akinidanganya, alionekana kumaanisha kila kitu alichokuwa akikizungumza, hakutaka kuona nikiendelea kuyasikiliza maneno ya watu ambayo yangeweza kuvuruga amani ya mapenzi yetu.
Hilo lilizidi kunifanya nimuamini sana Oscar kupita maelezo hata pale nilipokuwa nikitahadharishwa na watu sikutaka kuwasikiliza, niliwaona ni binadamu wenye nia mbaya kwangu, hawakupenda mafanikio yangu.
“Binti utajiingiza katika matatizo huyo unayeishi naye ni mume wa mtu,” aliniambia Mama mmoja niliyemfahamu kwa jina la Mama Musa.
“Si kweli,” nilimwambia huku nikiamini hakukuwa na ukweli wowote.
“Shauri yako binti unachokitafuta utakipata tu,” aliniambia huku akionekana kunihurumia.
Bado sikutaka kuyaamini maneno yao, niliendelea kuwa katika mahusiano na Oscar. Miezi iliendelea kukatika hatimaye mwaka huo ukapita, ulipoingia mwaka 2011 mwezi wa kwanza ndipo nilipofanikiwa kubeba ujauzito wa Oscar.
Nilifurahi sana baada ya kuubeba ujauzito huo, niliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuyaanza maisha mapya ya familia lakini ilikuwa ni tofauti kabisa na mawazo yangu.
Oscar alibadilika ghafla! baada ya kumpa taarifa hizo za ujazito, hakuwa Oscar yule niliyekuwa nikimfahamu, hakutaka kuamini kama nilikuwa nimebeba ujauzito wake, hilo lilizidi kumchanganya sana.
Nilishindwa kuelewa ni nini kilichokuwa kikiendelea, nilishangazwa na mabadiliko yake na hata nilipomuuliza nilishangaa akinigombeza na kunitolea maneno makali.
Nilihisi kuchanganyikiwa, sikutaka kuamini kama Oscar aliukataa ujauzito wake, hilo lilizidi kuniumiza sana, nilishindwa kuvumilia machozi yakaanza kunidondoka mfululizo.
Wakati nilipokuwa katika maumivu ya kukataliwa ujauzito ndipo hapohapo ambapo nilipokea maumivu mengine nisiyoyatarajia katika moyo wangu, Oscar aliamua kunieleza ukweli wa maisha yake.
Aliniambia alikuwa ni mume wa mtu na kipindi hicho mke wake ndiyo alikuwa akikaribia kurudi kutoka safarini.
Nilihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia maneno hayo, niliyakumbuka yale maneno niliyowahi kuambiwa na baadhi ya majirani lakini kutokana na kiburi changu sikutaka kuwasikiliza.
Mapenzi hatimaye yakaniingiza katika dunia ya maumivu na machozi, sikujua nilitakiwa kulia na nani kwani kama kuonywa nilionywa sana lakini sikutaka kusikia la mwadhini wala la mnadi swala.
“Kwahiyo unaamuaje?” nilimuuliza.
“Kuhusu nini?” aliniuliza.
“Huu ujauzito wako?”
“Mwajuma wewe ni chizi, mpumbavu, mshenzi, fala, hujielewi kabisa hivi unahisi ninaweza kuwa baba wa huo ujauzito wako? nenda katafute Baba halali lakini siyo mimi,” aliniambia Oscar maneno yaliyonifanya nitokwe na machozi. Nilishindwa kuzungumza, niliendelea kulia.
Kama ni makosa tayari nilikuwa nimeshayafanya. Kitendo cha kuishi na mwanaume bila ndoa, nikamuamini pasipokutegemea kama mwisho wa siku ningeweza kuvuna maumivu, hakika lilikuwa ni kosa kubwa mno nililolifanya.
Hatimaye Oscar aliweza kunifukuza, nikaanza kuishi maisha ya kutangatanga mitaani. Sikuwa na ndugu wala rafiki kusema labda ningeenda kumuomba hifadhi kwa muda, nilikuwa ni mimi na ujauzito wangu pekee.
Maisha yangu yalikuwa ni ya kutangatanga mitaani huku nikiomba msaada wa pesa na wakati mwingine nilikuwa nikienda kwa Mama Ntilie kuomba chakula, usiku ulipoingia nilikuwa nikilala nje, kiufupi hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu tangu nilipoweza kufukuzwa na Oscar.
Mwanzoni niliona ugumu kuishi maisha hayo lakini kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele, nilijikuta nikizoea na kuona ni maisha ambayo ni ya kawaida kuishi.
itaendelea…

by Ahmad Mdowe

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,168,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,211,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 04
MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 04
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mwajuma-utamu-sehemu-ya-04.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mwajuma-utamu-sehemu-ya-04.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content