MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 03 | BongoLife

$hide=mobile

MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 03

MWAJUMA UTAMU 

             SEHEMU YA 3

       WHATSAPP 0655585220

                     ZANZIBAR 

Nilifukuzwa kama mbwa usiku huo. Nililipwa pesa yangu ya mshahara wa mwezi uliyopita niliyokuwa nikidai pamoja na mwezi huo ambao nililipwa nusu yake.
Hakukuwa na mtu ambaye alinisaidia siku hiyo, nilionekana kuwa mbaya kupita kawaida, niligeuka kuwa adui. Kuna muda nikatamani nimwambie kila kitu kuhusu mume wake lakini nilikosa muda huo, tayari nilishafukuzwa na sikuhitajika tena kuwemo katika familia hiyo.
Sikujua nilitakiwa kwenda wapi usiku huo, nilipolifikiria hilo nikazidi kuchanganyikiwa. Nilijutia mambo mengi mno lakini kubwa nililolijutia ni hili la kutembea na mume wa mtu, tamaa yangu ya pesa iliniponza na kuniweka katika wakati mgumu wa maisha ambao sikutegemea kuupitia.
Machozi yalikuwa yakinidondoka muda wote, njiani nilipishana na watu ambao walionekana kuwa bize na mambo yao, baadhi yao walinishangaa kutokana na muonekano niliyokuwa nao, ulitosha kabisa kunielezea kuwa nilifukuzwa na muda huo nilikuwa katika safari nisiyoifahamu mwisho wake.
Nilitembea umbali mrefu sana na mwisho nilichoka, sikuwa nikifahamu sehemu hiyo au mtaa huo niliyokuwepo uliitwaje. Kwa mbali niliwaona wanaume wawili wakinifuata, mwanzo sikutaka kuogopa kitu kwani kulikuwepo na watu wengi niliyopishana nao hivyo niliamini kuwa salama lakini nilipofika eneo hilo nilishangaa nikiwa peke yangu, hakukuwa na mtu niliyepishana naye zaidi yangu na hao wanaume wawili waliyokuwa wakinifuata.
Nilianza kuingiwa na wasiwasi, wanaume hao wakazidi kukazana kunifikia, moyo wangu ukalipuka paaa…. hofu ikazidi kunitawala, mapigo ya moyo wangu yakaanza kunienda mbio.
“Habari yako binti,” alinisalimia mwanaume mmoja huku yule mwingine nikimuona akiangalia huku na kule.
“Nzuri,” nilijibu huku nikitetemeka kwa uwoga.
“Mbona unaogopa usiogope sisi ni watu wazuri unaitwa nani?” aliniuliza yule mwanaume mwingine.
“Naitwa Mwajuma,”nilimjibu kwa sauti ya uwoga.
Walitazamana kisha wakapeana ishara fulani, sikujua walimaanisha nini katika ishara hiyo ila nikashangaa wakinisogelea, ghafla! yule mwanaume wa kwanza akanirukia na kunikaba, nilishtukia nikipigwa na ubapa wa panga kwenye paja na kuambiwa nisipige kelele na endapo kama ningekiuka agizo hilo wangeweza kuniua.
Niliogopa mno, nilibaki nikiugulia maumivu ya ubapa wa panga pamoja na kabali niliyokuwa nimepigwa. Yule mwanaume mwingine alianza kunisachi, akachukua simu, pesa pamoja na lile begi langu la nguo.
Alipojiridhisha kuwa alifanikiwa kuchukua kila kitu changu alimpa ishara mwenzake na ndipo hapo alipoweza kuniachia.
“Sasa sikia wewe fala ukipiga kelele tunakuua, kaa kimya hivyohivyo,” aliniambia kisha akanitukana tusi la nguoni.
Nikabaki kimya huku nikiendelea kuugulia maumivu niliyoyapata. Wale wanaume wakakimbia eneo hilo. Wakati nikiendelea kuugulia maumivu huku nikiwa sijui nini nifanye mara akatokea mwanaume mmoja ambapo aliponiona alinifuata na kuniuliza nilikuwa na tatizo gani?
“Nimeibiwa kaka yangu, wameniibia,” nilimwambia huku nikionekana kuchanganyikiwa.
“Embu subiri kwanza akina nani hao wamekuibia?” aliniuliza huku akijaribu kunituliza.
“Siwajui, siwajui kaka angu wameniibia,” nilimjibu huku nikianza kulia kwa sauti kubwa.
“Usilie sasa, niambie kwanza unatokea wapi na unaitwa nani?” aliniuliza.
“Naitwa Mwajuma nimetokea huko nilipokuwa nafanya kazi za ndani,” nilimjibu.
“Wapi huko?”
“Kijitonyama.”
“Sasa huku umekuja kufanyaje?”
“Wapi?”
“Kwani unajua hapa upo wapi?”
“Hapana sijui kaka angu mimi ni mgeni kwani hapa ni wapi?
“Tandale,” alinijibu kisha akaanza kunionea huruma, hakuishia hapo, aliendelea kunihoji.
“Umesema umetokea Kijitonyama?”
“Ndiyo.”
“Kwanini sasa wamekuruhusu kuja sehemu kama hii tena usiku?”
“Hapana nimefukuzwa,” nilimjibu kisha akaonekana kunihurumia zaidi.
Mpaka kufikia muda huo nilikuwa bado sijalifahamu jina lake, alinitazama kama niliumia lakini hakukuwa na majeraha niliyoyapata zaidi ya kuugulia maumivu ya ndani kwa ndani.
Hakutaka kuona nikiendelea kubaki eneo hilo kwani aliniambia mtaa huo palikuwa na vibaka wengi sana, hakuishia hapo alizidi kunipa sifa mbaya za mtaa huo hivyo kitendo cha mimi kuendelea kuwepo mahali hapo kingeweza kunihatarishia maisha yangu.
Baada ya kusikia kuwa nilifukuzwa na sikuwa na mahali pa kwenda usiku huo, alihitaji kunisaidia. Aliniambia alikuwa akiishi peke yake hivyo kama nisinge jali anichuke na kwenda naye kwake usiku huo.
Kiukweli sikuweza kumkubalia kirahisi, nilihofia mambo mengi mabaya ambayo angeweza kunifanyia lakini baada ya kunihakikishia kuwa ningekuwa salama na kuniondoa hofu ilibidi nimkubalie. Akanichukua na kunipeleka mpaka kwake.
Kilikuwa ni chumba kimoja, nilipofika nilifikiria ni jinsi gani ambavyo ningeweza kulala humo lakini hilo halikuwa tatizo. Yule mwanaume aliniambia kuwa nilitakiwa kulala kitandani na yeye angelala chini na maisha yangeendelea hivyo.
Ngoja nikuambie kitu msichana mwenzangu, kijana mwenzangu unayeisoma simulizi hii. Unajua kwenye haya maisha unaweza ukakutana na vikwazo vingi lakini baadhi ya watu wanaokutazama wakakuchukulia kuwa hayo yote unayopitia ni haki yako, wengine wanaweza kwenda mbali zaidi na kukutukana na kukulaumu kwa ujinga uliyoufanya.
Yote haya yanaweza yakatokea katika maisha na kitu unachotakiwa kukifanya ni kujua ni jinsi gani ambavyo unatakiwa kupambana nayo na si muda wa kujilaumu na kuona kama wewe ni mkosaji mbele za Mungu wako na hutakiwi kusamehewa.
Kwanini nakwambia haya ni kwasababu ya makosa niliyoyafanya katika maisha yangu, ujinga niliyoufanya, sitaki urudie makosa yangu sitaki urudie kufanya ujinga wangu, nataka ujifunze kitu kupitia simulizi hii ya maisha yangu.
Angalia kwa muda ambao niliweza kukutana na mwanaume huyo ambaye hata sikuwa nikilifahamu jina lake tayari nilimuamini, niliukubali msaada wake, bila kufuata taratibu zozote za kisheria nikajikuta nikiingia ndani kwake na maisha yakaanzia hapo.
itaendelea…

     by Ahmad Mdowe

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 03
MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 03
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mwajuma-utamu-sehemu-ya-03.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mwajuma-utamu-sehemu-ya-03.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content