MWAJUMA UTAMU SEHEMU YA 02

MWAJUMA UTAMU

                      SEHEMU YA 2

                WHATSAPP 0655585220

                        ZANZIBAR 

Mzee Gidion alipagawa, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, moyo wake ulimuuma mno, aliponitazama alionekana kuwa mwenye hasira, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.
Nilishindwa kuamua la kufanya kwani mpaka kufikia muda huo nilikuwa tayari nimeshafanya makosa. Kwanza nilikuwa nikitembea na mume wa mtu kwa kujua, pili niliwachanganya kimapenzi baba na mtoto. Haya yalikuwa ni makosa ambayo kiukweli sikuwahi kukaa na kuwaza kwamba kuna siku yangeweza kunigharimu maisha yangu.
Nilishindwa kuvumilia kumuona Mzee Gidion akiendelea kulia mbele yangu kama mtoto mdogo, ilibidi nimsimulie kila kitu kilichotokea kwa Daniel mpaka nikajikuta nikimkubalia na kuwa wapenzi, sikuacha kumuomba msamaha kwa kosa nililokuwa nimelifanya, nilikiri kukosea na kumuahidi kutorudia tena makosa.
Baada ya kumueleza hayo pamoja na kumuomba samahani Mzee Gidion hakutaka kunielewa kabisa, alinichukia, alinifananisha na kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima.
Hilo lilizidi kuniumiza mno, kitendo cha kuniita kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima hakika kiliniumiza sana, moyo wangu ulikuwa kwenye maumivu makali mno.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuishi maisha ya visasi kila siku, Mzee Gidion alikuwa ni mtu wa kunitishia maisha, alinikosesha amani ya moyo niliyoishi nayo kwa muda mrefu, sikuwa huru tena, muda wote nilikuwa nikimfikiria pamoja na vitisho alivyokuwa akinipa.
Kuna kipindi nilitamani kumueleza mke wake ukweli wote wa kile kilichokuwa kikiendelea kati yangu na mume wake lakini unafikiri ningeanzia wapi? Ningeupatia wapi ujasiri huo wa kumueleza kila kitu na wakati hapohapo tayari nilishamkosea kwa kitendo cha kutembea na mume wake.
Hiyo iliendelea kubaki siri ya moyo wangu, siri iliyokuwa ikinitesa mno. Mzee Gidion hakuacha kushiriki kufanya mapenzi na mimi, aliendelea kunitumia kimwili lakini safari hii haikuwa kama hapo awali, alibadilika na alikuwa akifanya mapenzi na mimi kama sehemu moja wapo ya starehe, yaani alinifanya kuwa kama kahaba ambaye alinitumia wakati alipohitaji kufanya mapenzi tu. Hilo liliniumiza sana, siwezi kusema ni maumivu kiasi gani niliyokuwa nayo katika moyo wangu lakini naweza kusema tamaa zangu za pesa ndizo zilizonipelekea nipitie katika wakati huu mgumu.
Daniel alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuigundua tofauti yangu japo Mama yake alianza kuniuliza kuhusu mabadiliko yangu lakini nilimficha, sikutaka kumueleza ukweli.
“Niambie nini kinachokusumbua mpenzi, malaika, mke, malkia wa maisha yangu,” aliniuliza Daniel.
“Hakuna kitu,” nilimjibu.
“Usiniambie hakuna kitu wakati nikikuangalia nakuona kabisa kuna kitu unanificha,” aliniambia.
“Kweli hakuna kitu.”
“Usinifiche tafadhali.”
“Naogopa kukuambia Daniel.”
“Unaogopa nini wewe niambie au mimba imengia?”
“Hapana bora ingekuwa mimba ningejua baba yake yupo.”
“Ni nini sasa?”
“Ni kuhusu baba yako.”
“Amefanyaje?” aliniuliza Daniel kisha nikaanza kumsimulia kila kitu. Nilipomaliza kumsimulia nikamuona akivuta pumzi ndefu na kuziachia kwa pupa, kama ilivyokuwa kwa Baba yake na yeye pia hakutaka kuamini, kitendo cha kuwachanganya kimapenzi na Baba yake kilimuumiza mno.
Nilishangazwa na maamuzi aliyoyachukua Daniel, hakutaka kuendelea kuushuhudia uchafu kama huo ukiendelea mbele yake, alichoamua kukifanya ni kuniambia kuwa siku hiyo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa mapenzi yetu, hakutaka kusikia nikimuita mpenzi tena.
Niliumia sana baada ya Daniel kuchukua maamuzi hayo, mtu ambaye niliamini ndiye angeweza kuwa msaada wangu kwa wakati huo hakutaka kunisikia hata mara moja.
Maisha yalibadilika ndani ya nyumba, kila siku nilikuwa ni mtu wa kumuomba Mungu aninusuru na mabaya ambayo yangeweza kunitokea. Nilifahamu hapakuwa na amani tena, kuanzia Baba na Mtoto wote walikuwa na visasi juu yangu, hawakunitazama kwa macho ya wema tena, nilionekana kuwa mbaya tena adui mkubwa ambaye walitakiwa kuniepuka.
Vitisho havikuishia hapo, Mzee Gidion aliendelea kunitishia kuniua kila kukicha, wakati mwingine alikuwa akiniambia ni lazima niondoke katika nyumba yake nikiwa maiti ndani ya jeneza.
Wakati yote haya yakiendelea mke wake alikuwa hafahamu lolote, iliendelea kubaki siri katika moyo wangu mpaka pale nilipoanza kukosa uvumilivu, nilitishiwa sana, sikuwa na amani tena katika moyo wangu, uhuru wangu wote ulipotea, nilikuwa nikiishi maisha kama ya mfungwa aliyetoroka gerezani.
Wazo la kutoroka likanijia kichwani, nilichokuwa nikikiwaza kwa wakati huo ni kutoroka na kwenda mbali. Sikuwa mwenyeji wa jiji la Daresalaam, tangu nilipoweza kufika kwa mara ya kwanza maisha yangu yote yalikuwa ni ya kukaa ndani, labda siku moja moja za wikiendi niliweza kupata bahati ya kupelekwa katika fukwe za Coco ambapo hata njia ya kufikia huko nilikuwa siifahamu.
Nadhani unaweza ukaona ni kwa jinsi gani nilivyokuwa mgeni katika jiji hili. Wakati ambapo nilikuwa sifahamu mtaa hata mmoja tayari nilikuwa nimejiwa na wazo la kutoroka. Unafikiri nilifanikiwa katika mpango huu? Jibu ni hapana, niliendelea kujiuliza maswali ambayo yalizidi kuniumiza kichwa.
Ni katika kipindi hicho ambapo kumbukumbu za nyumbani kwetu zikaanza kunijia, nilipakumbuka mno, nilitamani kuambiwa kuwa nilitakiwa kurudi nyumbani kwetu lakini jambo hilo halikuweza kutokea hata mara moja.
Nitaishi maisha ya vitisho mpaka lini? Hili lilikuwa ni swali lililoniumiza usiku na mchana, nilikosa wa kumsimulia maisha niliyokuwa nikiyapitia kwa wakati huo.
Baada ya kupita mwezi mmoja huku nikiendelea kuishi maisha ya vitisho, siku moja majira ya usiku Mama Daniel aliniita na kuniambia kuwa alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, aligundua kuwa nilikuwa nikitembea na mume wake jambo ambalo lilimuumiza mno.
“Mwajuma msaada wangu wote niliyokusaidia katika maisha yako leo umeamua kunilipa kwa kutembea na mume wangu kweli?” aliniuliza, wakati huo machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni mwake.
“Hapana Mama nili….” kabla sijamaliza kuzungumza alinikata kauli, nilishtukia nikipigwa kofi moja zito lililoniyumbisha, wakati nikiendelea kuugulia maumivu ya kofi, hakuishia hapo, alianza kunipiga kila sehemu ya mwili wangu huku akinilaani kwa kitendo nilichomfanyia. Nilipata maumivu makali mno, siwezi kuyaelezea maumivu niliyokuwa nikiyapa, nililia sana, nilimuomba kila aina ya msamaha lakini sikuweza kuambulia jibu lolote zaidi ya kipigo kikali kama cha mbwa koko na mwisho wa siku aliweza kunifukuza.
Je, nini kitaendelea?
Nini hatma ya Mwajuma. 

 Usipitwe na Huu Utamu
 
   by Ahmad Mdowe
DONATE VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Your donation helps the Admin to be even more active in sharing quality blog templates. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni