MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 08

MTOTO WA MAAJABU: 8

Alifika hadi kwao na kushuka, alitembea huku akiangalia mazingira ya nyumbani kwao hadi kwenye nyumba yao na kugonga, kisha akafunguliwa mlango ila aliyemfungulia mlango alimshangaza sana kwani alikuwa ni Lulu.
Yani Mariam ilikuwa bado kidogo akimbie ila Lulu alimdaka na kumuuliza,
“Kwani dada kuna nini?”
Mariam aliangalia vizuti yale mazingira, na Lulu alimshika mkono na kuingia ndani, ni kweli ilikuwa ni ndani kwake na sio nyumbani kwao wala nini, alijikuta akimuuliza Lulu kwa uhakika zaidi,
“Tupo wapi kwani hapa Lulu?”
“Si tupo nyumbani dada?”
“Nyumbani kivipi? Nyumbani kwangu?”
“Ndio, ni nyumbani kwako dada”
Mariam alikaa kimya yani hakuelewa kabisa aliona kamavile anaota basi moja kwa moja aliongoza hadi chumbani kwake na kwenda kulala yani hakujielewa kabisa.
Lulu alibaki tu kumshangaa ila aliamua tu kuendelea na kazi zake ambapo aliandaa chakula ila alipoenda kumuita Mariam aligoma kwenda kwahiyo ilibidi Lulu ale mwenyewe na bila kuelewa ni kitu gani kimempata bosi wake.

Muda huu Lulu alipigiwa simu na mama yake, kwahiyo alipokea na kuanza kuongea nayo ile simu, alimsalimia kwanza na kuanza kuongea habari za hapo,
“Vipi Lulu maisha ya hapo?”
“Si nilikwambia eeeh mama kuwa sipo tena kwa yule dada, amenileta kwa ndugu yake kuja kumsaidia kazi”
“Aaaah sawa, ila vipi maisha huko?”
“Jamani mama, huyu dada ni mvivu sijapata kuona mama yangu. Yani hakuna kazi anayofanya, zote nafanya mwenyewe”
“Kwani si anafanya kazi?”
“Hapana, yupo yeye na mumewe na mtoto ila mumewe ndio anafanya kazi, yeye huwa anashinda nyumbani ila ni mvivu mama balaa. Hebu fikiria hadi kitanda anacholala na mumewe nikatandike mimi kweli! Chumbani kwao nisafishe mimi jamani, na zaidi ya yote unajua nguo za ndani zake na mumewe nafua mimi!”
“Kheeee mbona makubwa, yani huyo sio uvivu tu bali atakuwa ni mchafu pia maana kusipokuwa na msichana wa kazi kwake inamaana hizo kazi hatozifanya?”
“Sijui mama, yani ni mvivu hatari”
“Ndiomana wanawake wengine wanaibiwaga waume zao!”
“Umeona mama eeeh! Sema kanikuta mtu mwenyewe sina tabia hiyo ila nilimwambia mume wake kuhusu swala la kutandika kitanda chao na kufagia ndani kwao kuwa mkewe ajitahidi awe anafanya mwenyewe”
“Alisemaje sasa?”
“Mmmh hata hakusema kitu, nadhani kazoea ila sikumwambia kuhusu mimi kufua nguo zao za ndani kwani najua bado hawezi kusema chochote anampenda sana mke wake ila mwanamke mwenyewe ni mvivu sana sijapata kuona jamani!”
Mara mlango ulifunguliwa, aliyeingia alikuwa ni Juma, hapo Lulu alishusha simu na kukata haraka haraka huku akimsalimia kwa uoga,
“Shikamoo shemeji!”
“Marahaba”
Juma hakusema neno zaidi ya kuitikia hiyo salamu tu, na moja kwa moja alienda chumbani kwake na kumkuta mke wake kajilaza, basi akamuamsha na kuanza kuongea nae,
“Hivi Mariam kweli kabisa hadi nguo zetu za ndani za kumpa msichana wa kazi afue jamani?”
“Kwani na zenyewe si nguo! Anafua kama anavyofua nguo zingine”
“Hivi Mariam mke wangu una nini? Hivi unajua nguo za ndani zilivyo? Mtu anaweza kukutendea jambo baya kwa kutumia nguo za ndani”
“Kama mtu akiamua kukutendea jambo baya anakutendea tu, iwe kwa nguo za ndani au la! Mambo mengine inategemea tu na moyo wa mtu, vipi kwani umemkuta Lulu ndio anazifua muda huu? Nimemuachia asubuhi kabisa ujue!”
“Hebu acha ujinga Mariam na acha kujipumbaza, unafanya ujinga tena ujinga haswaa, kinachokushinda kufua nguo a ndani ni nini? Kheri nguo zingine ila hadi za ndani jamani Mariam mbona ni mambo ya ajabu hayo lakini? Aaaarrgh sikujua yote haya, kama huwezi uwe unaziweka pembeni halafu mimi nikipumzika niwe nazifua mwenyewe”
“Ila ujue Juma nakushangaa sana, yani umefika hakuna cha salama, hakuna cha kuniuliza nimeshindaje, hakuna chochote umefika tu na swala lako la kufuliwa nguo za ndani utafikiri ni kitu cha ajabu sana kutokea kwenye maisha, mbona ni kawaida tu na wengi sana wanaishi maisha ya namna hii? Kuna wanawake ndani kwao hawashiki kitu chochote kile, kila kitu kinafanywa na mdada wa kazi, kwanini kunishangaa mimi sasa? Kwani nimefanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa dunia nzima au ni kitu gani?”
“Hakuna siku ambayo nimewahi kukuelewesha ukaelewa Mariam hakuna kabisa, haya umeshindaje?”
“Sipo vizuri kiafya, kesho twende tu hospitali yani nina hali mbaya kwakweli”
“Sawa, tutaenda huko hospitali”
Kwahiyo ile mada ya uvivu tena ikaisha kwa namna hiyo maana hakuna kingine kilichoendelea kuzungumziwa zaidi ya Mariam kusema kuwa hana hali nzuri kumbe Mariam bado alikuwa na yale mawenge ya kwenda kwao na kujikuta akirudi hapo hapo.

Hata chakula cha usiku kwa siku hii Mariam hakula kama kawaida yake na kumfanya Juma ajue kuwa Mariam anaumwa kweli maana aliona amebadilika na wala hana furaha tena, basi akahisi huenda na swala la kumsema kwa uvivu limechangia hali ile na kumfanya Juma kuanza kumuomba msamaha kumbe Mariam alikuwa na swala lake lililomsumbua akili na kumtatiza zaidi ya hata swala la uvivu.
Usiku huu wakati wa kulala, Mariam alikataa kabisa kusogezewa mtoto wake karibu yake kwahiyo muda wote kama kawaida mtoto alibaki kulala na Juma tu hadi kulipokucha.
Basi Juma aliamua mwenyewe kwenda kuandaa kifungua kinywa ili wapate kwanza kifungua kinywa kabla ya kwenda hospitali na Mariam.
Ila hii chai Mariam alikunywa sana hadi alianza kuhisi usingizi ila bado alikazana kusisitiza swala la kwenda hospitali.
Baada ya kumaliza kunywa chai, Mariam aliinuka na kwenda kulala alisema kuwa atalala kidogo ila alivyoenda kulala ilibidi Juma pia ajiandae kwaajili ya kwenda kazini huku akimwambia Lulu,
“Iwapo akazidiwa basi utanipigia simu Lulu”
“Sawa shemeji, hakuna tatizo”
Basi Juma akamuachia Lulu namba zake halafu yeye aliondoka zake kwenda kwenye shughuli zake.

Kwenye mida ya saa nane mchana, Mariam alimka na kilichomuamsha ilikuwa ni njaa, basi alitoka chumbani kwake na kwenda sebleni ambapo alimkuta Lulu akiwa pale sebleni na kuanza kuongea nae kwa kumuuliza,
“Umeshapika Lulu?”
“Ndio dada”
“Nina njaa hapa hatari, weka hiko chakula tule maana nina njaa sana”
Basi Lulu aliandaa kile chakula na kuanza kula na Mariam huku akimwambia,
“Ila dada utanenepa sana ujue!”
“kwanini?”
“Yani asubuhi tu umekunywa chai na kwenda kulala yani tabia ya kula halafu kwenda kulala ndio tabia inayofanya wengi sana wanenepe hovyo”
“Sasa chakula kinavyolewesha vile haswa chai, kweli mtu unywe na uache kulala ufanye nini sasa?”
“Bora ufanye mambo mengine, halafu dada una eneo kubwa na zuri unaweza kuamua kulima lima huko na kupanda mboga”
“Khaaaa unaugua nini wewe, yani mimi nikalime lime na kupanda mboga kisa nini? Mume wangu kaishiwa hela au ni kitu gani? Mume wangu ana pesa, mambo mengine hajaamua tu, kama kununua gari ila mume wangu hela anayo, sina sababu mimi ya kuanza kulima lima wala nini”
“Kwani dada wote wanaolima lima waume zao hawana hela?”
“Ni umasikini tu huo, sasa mimi ukanishikishe jembe kweli!! Eti nalima mboga mboga, ili iweje sasa?”
“Ili usiwe unalala ukitoka kula tu, chakula kifanye kazi kwanza sio kukimbiziwa kwenda kulala”
“Nishazoea tayari, kwahiyo naona kama unanipigia kelele tu”
Lulu alinyamaza maana hakuona kama kuna kitu cha kumuelewesha huyu dada na akaelewa maana yeye huwa na kile anachokiamini yeye tu.
Kisha Mariam akamuuliza sasa,
“Halafu zile nguo nilikupa jana asubuhi, kuzifua jioni wakati shemeji yako anarudi ndio nini?”
“Nimezifua asubuhi dada”
“Haya huyo shemeji yako kajuaje kama nakupa ufue hadi nguo za ndani?”
Hapo Lulu alinyamaza kimya, kisha Mariam akamwmabia Lulu,
“Kama una mpango wa kuniroga mimi sababu eti nakupa nguo zangu za ndani, futa kabisa huo mpango wako maana mimi sirogeki mimi. Nione hivi hivi yani, mimi sirogeki na sitokuja kurogeka kamwe”
Lulu alimuangalia Mariam na kumuuliza,
“Kwani dada umenisikia muda gani kuwa nina mpango wa kukuroga?”
“Haijalishi nimekusikia au la ila mimi sirogeki kizembe namna hiyo”
Mtoto alianza kulia, ilibidi Lulu ainuke na kwenda kumpa maziwa maana hakuwa na mengi ya kuongea na Mariam.

Usiku wa leo, Mariam alifikiria jambo na jambo lenyewe ni swala la yeye kuondoka mahali hapo, yani alichokuwa akihisi yeye ni kuwa akiwa kwao kabisa atakuwa amefanikiwa kuondoka hapo ingawa hakujua ni kitu gani ambacho kimekuwa kikimrudisha hapo.
Basi muda huu alimpigia simu mama yake na kuongea nae,
“Mama, hivi mtu ukiwa unaenda mahali na kushangaa gafla umerudi kwako huwa ni kitu gani hicho?”
“Unaongelea nini Mariam?”
“Aaaah kuna tukio limenitokea hapa nyumbani kwangu”
“Tukio gani?”
“Mama sikia, nilipanga kuja huko nyumbani. Nimeenda hadi stendi na kupanda daladala halafu nimeshangaa badala ya kuja huko nyumbani eti nimerudi nyumbani kwangu”
“Mmmmh mmmh yani kama alivyonihadithia Zayana, mbona kuna maajabu huko kwako? Nimesahau tu kukuuliza, kwani huyo mtoto wako ana nini?”
“Hata mimi mwenyewe sielewi mama, huyu mtoto ana nini sijui”
“Zayana kaniambia kuwa huyo mtoto anatoa kinyesi kama cha mbuzi!”
“Ni kweli mama, halafu kuna muda anaongea”
“Duh!! Sasa Zayana aliniambia kuna siku mliamua kuondoka mkaenda hadi stendi na kujikuta mmerudi nyumbani sijui mlipitiwa na usingizi stendi”
“Ndio mama, kuna mambo ya ajabu sana. Haswa huyu mtoto mama huwa simuelewi kabisa. Ni kweli nimemzaa mwenyewe ila nashindwa kumuelewa, unajua huyu mtoto alimsonya mama yake Juma!”
“Kheeeee mbona makubwa”
“Ndio hivyo mama halafu Juma anaona kawaida tu, kila kinachotokea kwa huyu mtoto basi yeye anaona kawaida, sasa mimi nataka niondoke halafu huyu mtoto nimuachie yeye mwenyewe aendelee kumlea”
“Ila mwanangu mbona nahisi mtoto wako huyo atakuwa amerogwa! Maana unajua mtoto wako ni mzuri sana hata mambo unayoyasema ni yanashangaza sana, yani ni ngumu mtu kumjua kuwa ana mambo ya namna hiyo, mwanao ni mzuri sana mwanangu. Sasa sikia, njoo nyumbani ili tupange cha kufanya”
“Unadhani Juma anaweza kunipa ruhusa ya kuja? Hapa cha muhimu ni kutoroka tu, hebu niambie nitumie njia gani ili nisijikute nimerudi tena hapa nyumbani”
“Unajua hayo mambo ni kama mazingaombwe eeeh! Sikia Mariam, ukiondoka hapo kwako geuza viatu yani cha kulia vaa kushoto na cha kushoto vaa kulia maana naona hayo mambo kama mazingaombwe”
“Sawa mama yangu, ndiomana nimekupigia simu wewe ili unipe maujuzi”
Basi Mariam alifuirahi sana kupewa njia hii ya kufanya na mama yake, hapo sasa ndio aliweza kuendelea na mambo mengine huku mpango wake ukifanya kazi vilivyo kwenye akili yake.

Wakati wa kulala, Mariam alimsisitiza Juma kuwa anataka kesho waende hospitali maana hali yake sio nzuri ila alimwambia kuwa,
“Naomba tuondoke kabla hata ya kunywa chai”
“Duh!! Kwanini sasa?”
“Nimeamua, sitaki kulala kama leo maana huu ni ujinga, unapanga kwenda sehemu unakunywa chai unalala na huendi tena, sitaki huu ujinga kwakweli”
“Mmmmh!! Haya, nimekuelewa kwahiyo twende asubuhi kabisa?”
“Ndio, ni vizuri kwenda hospitali asubuhi”
Basi wakalala na kweli asubuhi na mapema, Juma alipoamka tu akamuamsha na mkewe kisha wakajiandaa na kumuachia mtoto Lulu, ila Juma hakuelewa kuwa mkewe alikuwa na mpango gani kwa siku hii ya leo.
Waliondoka pamoja hadi hospitali ambapo kabla ya kwenda kwa daktari, Juma alimuuliza kwanza mkewe,
“Hivi ni kitu gani kinachokuuma haswa?”
“Hata nikikwambia bado hutaelewa maana wewe si daktari”
“Ila mimi ni mume wako, napaswa kujua maana mimi na wewe ni mwili mmoja”
“Tungekuwa ni mwili mmoja hivyo basi kitu kinachonisumbua ungekuwa umeshakijua maana si mwili ni mmoja? Ila huo ni msemo tu, kila mtu na mwili wake Juma. Nikienda kwa daktari na kumueleza ndio nitakwambia ninachoumwa”
“Kwahiyo kwa daktari hatuendi wote?”
“Kwa leo hapana, itabidi unisubirie tu”
Yani kwa siku hii Mariam alikuwa ameshakamilisha vizuri kabisa mipango yake, wakati ndio anataka kwenda kwa daktari Juma alimuangalia miguuni na kumshangaa,
“Weeee Mariam mbona umegeuza viatu?”
Mariam alimuangalia mumewe bila ya kumjibu kisha akainuka na kwenda kwa daktari ila hakuingia kwa daktari yule bali alipitiliza halafu Juma hakuelewa kama Mariam hakuingia kwa daktari kwahiyo alikuwa akimngoja tu pale pale nje.

Juma alikaa sana pale nje na kuona kuwa kwasasa aende kuulizia kwa daktari, na alipoenda kuulizia kweli aliambiwa kuwa huyo mtu hakuingia pale kwa daktari, Juma alishangaa kuona kuwa mkewe kamchezea mchezo pale pale, wazo la haraka haraka lililomjia kichwani ni kuwa huenda Mariam kaenda kwao,
“Khaaaa mwanamke kichaa huyu, sasa angeniomba ruhusa angepungukiwa na nini? Si angeniambia tu na pengine ningemsindikiza na kurudi nae. Inabidi nikamfate tena jamani loh!!”
Kwanza Juma alitafuta tafuta pale hospitali, alipomkosa kabisa ikabidi tu aamue kwenda kumfata mke wake nyumbani kwao, hakumpigia simu sababu Mariam huwa hatembei na simu kwahiyo angejisumbua tu kumpigia.
Juma akiwa njiani kuelekea nyumbani kwakina Mariam, alikutana na yule binti ambaye alimsalimia Juma,
“Habari yako baba Mishi”
Juma alimuangalia yule binti na kumwambia,
“Una kichaa nini? Nishakwambia kuwa mwanangu hawezi kuitwa hilo jina”
“Haya yameisha, unaenda wapi?”
“Hayakuhusu”
Yule binti akacheka na kumwmabia Juma,
“Hata usihangaike kwenda kumfata mkeo nyumbani kwao, rudi tu nyumbani kwako utakutana nae njiani”
“Inamaana kaenda nyumbani!”
“Ndiomaana yake, mkeo kaamua arudi nyumbani sababu kaona hakuna anachoumwa ni kukusumbua tu”
“Khaaaa mwanamke ni kichaa sana huyu”
Juma aligeuza muda huo na kuondoka zake.

Mariam akiwa njiani, kwanza alikuwa na furaha sana kwani alikuwa amegeuza vile viatu bado ingawa watu walikuwa wakimshangaa ila yeye aliona ni sawa sawa tu kufanya vile huku akiwaza yale maneno ya mama yake kuwa hayo ni maswala ya mazingaombwe.
Ila aliposhuka kwenye gari kuelekea nyumbani kwao, alitokea mvuta bangi akiwa amebeba panga na kumwambia Mariam atoe kila alichokuwa nacho, yani Mariam alianza kulia tu na hakuwa na kitu cha kutoa kwakweli, yule mwizi akachukua nauli ya Mariam na viatu vya Mariam akaondoka navyo. Yani Mariam alihisi kuchanganyikiwa basi akaanza kukimbia kuelekea nyumbani kwao maana akili yake muda huo hadi imegoma kufanya kazi.
Ila wakati anakimbia, akashikwa bega, akaogopa sana kwani akajua ni kibaka mwingine, ila alipogeuka alimkuta ni Juma,
“Khaaaa mume wangu?”
“Mbona unakimbia jamani mke wangu, tena upo peku, umeanza kuchanganyikiwa?”
Mariam hakujibu ila alikuwa akiyaangalia yale mazingira sasa, alishangaa sana kwani yale mazingira yalikuwa ni mazingira ya kuelekea nyumbani kwake ambapo Juma alimshika tu mkono kumuongoza kuwa waende nyumbani.

Leo Lulu akiwa na yule mtoto ndipo akasikia harufu kali sana na kuhisi kuwa huenda yule mtoto amejisaidia haja kubwa, na kweli alipomtoa alikuta amejisaidia haja yenye muonekano ule ule wa kinyesi cha mbuzi, Lulu alishangaa sana na kuogopa hata kuendelea kumshika yule mtoto.
Ila badae alijipa ujasiri na kwenda kumnawisha kisha kumrudisha na kumvisha nguo vizuri halafu akajisemea sasa,
“Kwakweli hii nyumba itanishinda, mtoto anatoa kinyesi kinanuka hivi na kinafanana na kinyesi cha mbuzi halafu mama yake ni mvivu sijawahi ona dunia nzima. Mimi siwezi kuendelea kuishi hapa”
Mara yule mtoto akamwambia Lulu,
“Ulidhani kuwa utaweza?”
Lulu alijikuta akitetemeka mahali pale nakuanguka chini.

Itaendelea…..!!!

By, Atuganile Mwakalile.
Story ya MWANAUME WA DAR inaendelea 

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 08
MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 08
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-08.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-08.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content