MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 07

MTOTO WA MAAJABU: 7

Mariam na Dora walijikuta wameganda kama vile wamechomwa sindano za kuwagandisha yani hawawezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.
Tukio hili lilikuwa la ajabu sana kwa Dora na lilimfanya aogope sana, cha kushangaza walipokimbilia chumbani waliweza ila kwenda nje ilishindikana, kwahiyo kila mmoja alikuwa chumbani kwake kwa muda huu, Dora aliwaza sana,
“Hivi ni nini hiki? Kazi zote zipo hivi au ni hii hii jamani! Mbona hii nyumba imeanza kunitisha? Nitaweza kweli kuendeles kuishi hapa? Natakiwa kufanya maamuzi kwakweli”
Akajikuta akikumbuka na maneno ya yule mdada aliyekutana nae njiani hivyo akaogopa sana na kuona kuwa hapo mahali hapafai kabisa ila mwisho wa siku alilala tu mule chumbani.

Juma alirudi na kukuta kimya kabisa, alijiuliza mno kuwa wameenda wapi? Ila akahisi tu lazima wamelala ila alishangaa kuona ni mapema mno! Akaamua kumuita Dora maana alikuwa amefika na mboga ambayo alitaka waichemshe kabisa,
“Dora”
Dora akatoka chumbani ila kitu cha kwanza kabla ya salamu alimwambia Juma,
“Shemeji, hii nyumba imenishinda, sidhani kama naweza kuendelea kuishi hapa”
“Kwanini?”
“Mtoto wako anaongea shemeji”
“Khaaaa hivi una kichaa au ni kitu gani wewe? Sasa ulitaka mtoto wangu awe bubu au ni kitu gani?”
“Kwahiyo shemeji ni kawaida hiyo?”
“Ndio ni kawaida, mtoto wangu lazima aongee maana kazaliwa mzima kabisa”
“Na kula chakula chote je?”
“Kula chakula chote kivipi?”
“Mtu ambaye anakula chakula kila dada akitenga mezani ni mtoto wako”
“Unajua wakati mwingine ukiwa unaongea unatakiwa uttambue kuwa unaongea na nani na unaongea nae kuhusu nini. Njoo uchukue hii mboga”
“Kiukweli shemeji mimi siwezi kuendelea kuishi hapa, naondoka mimi. Muite dada tu”
Dora alienda ndani kupakia nguo zake maana aliona watu wenyewe kwenye ile nyumba wanajifanya kama hawaelewi vile.
Juma alimfata mke wake ambaye alimuhadithia kitu kile kile cha mtoto kuongea na kula chote, kisha Juma alimuuliza mke wake,
“Hivi unaona hiko kitu kina maana yoyote?”
“Sijui ila ni mtoto mwenyewe ndio kasema”
Kidogo Dora akawaita, walipotoka akawaambia,
“Jamani mimi naondoka, kwaherini”
“Kheeee msahahara wako je?”
“Dada, sitaki mshahara wala nini”
Juma akatikisa kichwa na kisha akaingiza mkono mfukoni kwake na kutoa elfu thelathini akamkabidhi Dora na kumwambia,
“Chukua hiyo, najua hujamaliza mwezi ila chukua hiyo hela”
Dora alishukuru na kuchukua kisha akaondoka zake yani hakutaka hata wamsindikize wala nini, kwahiyo ndani alibaki Juma na Mariam ambapo Mariam na yeye alimwambia mumewe,
“Na mimi naondoka”
“Sasa uondoke uende wapi?”
“Naenda kwetu”
“Na mtoto unamuacha na nani?”
“Na wewe baba yake”
“Hebu acha uchizi wako Mariam, hapa huendi popote tutabaki wote kulea mtoto”
“Unadhani nipo tayari kubaki mwenyewe na huyu mtoto!!”
“Ngoja, usipaniki”
Juma akachukua simu yake na kumpigia mama yake kumuomba mdada wa kazi,
“Mama naomba utusaidie, unajua wazi kuwa mke wangu hawezi peke yake halafu na mimi natakiwa kwenye kazi zangu”
“Nimlete msichana wa kazi kwa huyo mtoto anayesonya?”
“Aaah mama, usiseme hivyo jamani! Nisikilize mtoto wako”
“Kesho, nitamuagiza mamako mdogo akuletee mdada wake maana na yeye alisema kuwa hataki tena msichana wa kazi”
“Dah!! Utakuwa umenisaidia sana mama”
Juma alifurahi sana kuongea vile na mama yake kwahiyo alimpa mke wake ujumbe huo wa kuhusu msichana wa kazi atakayeletwa.

Siku hii ni Juma mwenyewe ndio alipika na wakapata kula na kulala ila kiukweli Mariam alikuwa na mawazo sana na hata hakupenda kabisa mambo haya yanayoendelea wala nini.
Kulipokucha, Mariam alimgomea Juma kuondoka hadi hao ndugu zake wafike na kweli kwenye mida ya saa nne asubuhi hivi, walifika ndugu wa Juma yani mamamdogo wa Juma na huyo msichana wa kazi, basi waliwasalimia pale huku mamamdogo wa Juma akiwapa hongera kwa kupata mtoto,
“Hongereni sana, hebu mleteni mtoto nimshike kidogo”
Basi Juma akampatia mamake mdogo mtoto huku akitabasamu, yule mamake mdogo alimshika mtoto na kumuangalia huku akisema,
“Tuseme ndio sijaja siku nyingi mpaka mtoto amekuwa mkubwa jamani khaaa mimi mbaya loh!! Ila hongereni sana, mmepata katoto kazuri hadi raha, mmekapa jina gani?”
Mariam na Juma wakaangaliana kwani kiukweli mtoto huyu hakuwa na jina, basi mama mdogo akauliza tena,
“Kwani anaitwa nani mtoto”
“Aaaah mamdogo bado mtoto hajapewa jina”
“Jamani acheni masikhara, kinachowashinda kumpa jina mtoto ni kitu gani? Ndio mnatafuta majina ya kizungu? Si mmuite tu majina yetu ya Kiswahili? Mnaweza hata kumpa jina langu la Nasra”
Mariam akamuangalia yule mama na kumwambia,
“Hebu muite hilo jina uone kama litaendana nae”
Juma akaingilia kati kwani alihisi tu kitakachotokea, akamwambia mamake mdogo,
“Mama, mwanangu hawezi kuitwa Nasra lipo jina lake makini kabisa, subiri tu utalisikia”
“Mmmmh jina gani hilo? Kwani Nasra sio jina?”
“Ni jina mamdogo ila huyu ana jina lake, hatupendi kulitaja kwa watu kwasasa ila muda ukifika utalisikia tu”
“Mmmmh makubwa, haya jamani huyu nimekuja nae ndio mdada wa kazi ambaye mama yako Juma kaniagizia, huyu dada anaitwa Lulu”
“Aaaah Lulu, karibu sana”
“Asante”
“Jamani ila mimi sikai sana maana si unajua tena biashara zangu, alivyoniambia nikasema ngoja niende kuwaona pia, kwahiyo mimi naondoka muda sio mrefu”
Na kweli baada ya muda mfupi tu huyu mamdogo akawaaga na kuondoka zake.

Mariam kama kawaida alianza kumuelekeza huyu Lulu majukumu ya hapo nyumbani kwake, alimuonyesha nyumba nzima ilivyo na kazi za kufanya,
“Umeelewa kazi za humu?”
“Nimeelewa ndio, hizo kazi ni kila siku?”
“Ndio, kwani vyombo ni vya kuosha siku moja moja? Hizi kazi ni kila siku”
Basi na hapo akampa kazi ya kupika chakula cha siku hiyo, kwahiyo Lulu alipika na alivyomaliza kupika waliandaa na kuweza kula, wakati wanakula mtoto alilia ndipo Mariam alipomwambia Lulu,
“Mtoto yule chakula chake maziwa, kamtengenezee, ngoja nikuelekeze ukamtengenezee”
Juma akainuka akasema,
“Ngoja nikamtengenezee mwenyewe”
Basi Juma alienda kumtengenezea mtoto wao maziwa na kumpatia wakati wenyewe wakiendelea kula ila Lulu alimwambia Mariam,
“Ila dada sio vizuri, mkianza kula pamoja halafu mumeo akainuka kama hivyo unatakiwa kumsubiri ili muendelee kula pamoja”
“Kheee wewe, kwahiyo njaa nayo huwa inasubiri au ni nini unaongea? Haya mambo ya humu ndani yaache kama yalivyo, yatakushinda ukianza kuyapekenyua”
“Sawa dada, yameisha”
Basi walimalizia kula pale na kumuachia tu Juma chakula chake ambapo aliendelea kula baada ya kumaliza kumlisha mtoto wao.

Leo mapema kabisa, Juma aliondoka zake kwenda kwenye shughuli zake ukizingatia jana yake hakwenda popote pale, kwahiyo alibaki Mariam na Lulu ambapo Mariam alipoamka alimfata Lulu na kuanza kumwambia,
“Ukiamka asubuhi, cha kwanza kabisa unatakiwa kubandika chai maana mimi huwa naamka na njaa sana”
“Aaaah sawa dada”
Umeshachota maji?”
“Hapana, bado sijachota dada”
“Mmmmh mmh!”
Mariam alimuona Lulu ni mzembe zaidi ya Dora maana Dora ingawa alikuwa anabishana ila alikuwa sio mzembe kama Lulu.
Basi Mariam alikaa sebleni ambapo mtoto wake alianza kulia njaa, akamuita Lulu,
“Njoo nikuelekeze umkorogee maziwa umpe”
Lulu alienda na kuelekezwa vile namna ya kumkorogea huyu mtoto maziwa, alishangaa sana,
“Yani tunakoroga maziwa ndani ya maziwa?”
“Usishangae, ndio chakula nilichoamua kumpa mtoto wangu”
Basi Lulu alienda kukoroga na kumnywesha yule mtoto ambapo alikunywa yote aliyokorogewa, kisha Mariam akamwambia Lulu,
“Inabidi uanze kupika chakula cha mchana tule mapema maana hatujanywa chai”
“Ila dada bado namalizia kufagia nje”
“Acha, utamalizia badae. Kapike kwanza”
Lulu ilibidi aende kupika na baada ya kupika walikula halafu ndio akaenda kumalizia kazi zake za nje ila kiukweli alikuwa akichukia sana.

Jioni, Juma alirudi na mboga ambapo Mariam alimuita Lulu aikatekate na kuibandika, basi Lulu alienda kuandaa ile mboga vizuri tu huku Mariam akiongea na Juma,
“Vipi umeshindaje na huyu mdada?”
“Vizuri tu”
“Ila ndio usiwe unamuachia kazi zote mke wangu”
“Kheeee analipwa mshahara, asiachiwe kazi zote yeye kama nani?”
“Tutapoteza wasichana wa kazi sijui tutapata wapi mwingine?”
“Wapo watu wengi tu wanatafuta kazi, akiondoka huyu mmoja atakuja mwingine, sio kazi sana kumpata msichana wa kazi si unaona tukisema tu tunaletewa”
“Mmmmh kwa mtindo huu hata wanaotuletea watachoka nakwambia”
Juma aliamua kuingia ndani huku Mariam akimfata Lulu na kumwambia kuwa aandae chakula cha usiku.
“Ukimaliza hapa, andaa chakula cha usiku Lulu”
“Sawa dada”
Chkula kilipokuwa tayari, wote walikaa na kuanza kula huku wakiongea mambo mbalimbali na baada ya chakula walianza maongezi mbalimbali ambapo Lulu akawasimulia kitu,
“Nakumbuka bibi yangu aliwahi kunisimulia kuwa kijijini kwao alizaliwa mtoto wa ajabu, maana kuzaliwa tu akaanza kuongea”
Hapo Mariam alimkatisha Lulu kwa kumwambia,
“Humu ndani huwa hatusimuliani stori za kutisha, kwasasa ni muda wa kulala”
Ukweli ni kuwa sio stori za kutisha ila tu aliogopa pale mtoto wake angejibu kwahiyo aliamua kumkatisha Lulu kwa namna hiyo.
Na kweli kwa muda huo, wote walienda zao kulala.

Leo mapema kabisa, Lulu aliandaa chai kama ambavyo alipewa maagizo na mama mwenye nyumba, kisha baada ya hapo ndio alianza kufanya kazi zingine, na kweli Mariam alifurahi sana na kwenda kunywa chai huku akifurahia ila badae Lulu nae alienda kunywa chai ila Mariam akamwambia,
“Lulu ukimaliza hapo kunywa chai uende chumbani kwangu kusafisha”
Lulu aliitikia tu ila hakupenda kabisa, na kweli alipomaliza alienda kusafisha mule chumbani kwa Mariam na baaada ya hapo akaitwa kwaajili ya kuandaa chakula cha mtoto yani Lulu alikuwa akichukia sana na siku zote alikuwa akifanya tu zile kazi kimya kimya ila alijisemea kuwa kuna siku ataamua kuongea tu.

Siku hii baada ya Lulu kumaliza kazi zake aliamua kuongea na Mariam kwani aliona zile kazi anapewa kama kuonewa hivi,
“Ila dada, mambo mengine ungekuwa unafanya mwenyewe bhana”
“Unamaanisha nini?”
“Dada jamani, kweli wewe uamke uje kunywa chai halafu mimi nikakutandikie kitanda na kusafisha chumba ambacho unalala wewe na mumeo, unaona hiyo ni sawa kabisa?”
“Unaongelea nini kwani?”
“Nasema kuwa kazi zingine uwe unafanya mwenyewe, ni kweli mimi ni msichana wa kazi ila kuna wakati nachoka. Na mimi ni binadamu, sio mashine mimi, kazi zingine fanya mwenyewe”
“Kheeee usinisumbue, kama umechoka kazi unaweza kwenda, ni wapi msichana wa kazi anaambiwa kulipwa hela nzuri kama hapa? Mambo ya mimi kutandika mwenyewe kitanda changu ni pale nitakapojisikia lakini sio lazima kuwa kila siku ninapoamka nitandike kitanda changu wakati wewe msichana wa kazi upo! Haiwezekani hiyo”
“Mmmmh dada!!”
“Ndio hivyo, na ukimaliza kupumzika hapo kuna nguo za kufua pale chumbani, utazichukua na kwenda kuzifua”
“Duh!! Sijapata kuyona haya!!”
“Ndio uone sasa”
Lulu aliinuka na kwenda kuchukua hizo nguo na kuzifua.

Ila leo usiku Lulu aliamua kuongea na Juma maana aliona kamavile huyu Mariam hamuelewi, basi aliongea nae,
“Shemeji, ni kweli nina shida na kazi, ni kweli nimetafuta kazi hata nilipoambiwa kuwa naletwa huku nilifurahi sana kwani ni kweli nina uhitaji wa kazi sana. Ila shemeji kuna kazi zingine dada angekuwa anazifanya mwenyewe”
“Kama kazi gani?”
“Mimi sio wa kutandika kitanda chenu shemeji, mimi sio wa kusafisha chumba chenu shemeji. Bora nifanye kazi zote za huku ila hizo za chumbani basi mkeo angekuwa anafanya mwenyewe”
“Sawa nimekusikia”
Juma alipoenda kulala alimsema mke wake,
“Unajua Mariam nilikuwa najua tu wewe ni msumbufu kwenye kazi za nje, hata kutandika kitanda kweli kukushinde mke wangu?”
“Aaaaah na wewe usinitibue, kile kisichana ndio kimekwambia ujinga sio? Yani visichana vingine vya ajabu kweli, kufatilia maisha ya watu tu. Hivi nikiondoka na kukuacha na kile kisichana utajisikiaje?”
“Kwani mimi nimesema uondoke jamani Mariam? Ila nimesema ujirekesbishe”
“Haya, mfano naumwa unadhani huko chumbani atasafisha nani? Hiko kitanda atatandika nani?”
“Kuumwa ni swala lingine Mariam, hata mimi nafanya kazi hizo lakini sio kumpa mtu ambaye hahusiki, nishakwambia mke wangu, tutamfanya huyu dada akimbie hapa nyumbani kwakweli”
“Akikimbia yeye tutapata mdada mwingine”
“Na hilo ndio tatizo lako, haya siongei sana ila akikimbia usinisumbue kuwa nisiende kazini”
Mariam hakumjibu mume wake kwani kwa wakati huo alishachukia na akaanza kuwaza mambo mbalimbali ya kufanya ili na yeye aweze kupakimbia hapo nyumbani kwake.

Kulipokucha Mariam alishtuka na kuona mtoto wao kalala pembeni yake, yani alichukia sana, ambacho hapendi Mariam ni kusogelewa na huyu mtoto yani alikuwa hapendi kabisa kwahiyo siku hiyo alijikuta amechukia sana.
Basi alipoondoka Juma, Mariam nae alijiandaa na baadhi ya nguo zake akabeba kwenye rambo na kumwambia Lulu kuwa anaenda kupeleka nguo kwa fundi,
“Naenda hapo kwa fundi, nataka akaniwekee kiraka kidogo kwenye nguo zangu”
“Sawa dada”
Kwahiyo Mariam alimuacha pale Lulu na mtoto na kuondoka zake, akiwa njiani alijisemea,
“Ningemuaga yule mwanaume angekataa, ila kwasasa naondoka zangu, siwezi yani siwezi kuendelea kuishi na yule mtoto hata kama nimemzaa mwenyewe ila siwezi kuishi nae kwakweli”
Basi alienda hadi stendi ambapo hakukaa chini kwani aliogopa kusinzia kama siku ile, moja kwa moja alipanda gari ya kumpeleka nyumbani kwao.
Na kweli aliingia kwenye ile gari na hakulala kabisa, aliwashuhudia abiria wote waliokuwa wakipanda na kushuka kwenye lile gari.
Alifika hadi kwao na kushuka, alitembea huku akiangalia mazingira ya nyumbani kwao hadi kwenye nyumba yao na kugonga, kisha akafunguliwa mlango ila aliyemfungulia mlango alimshangaza sana kwani alikuwa ni Lulu.

Itaendelea……!!!

By, Atuganile Mwakalile.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 07
MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 07
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-07.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-07.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content