MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 04 | BongoLife

$hide=mobile

MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 04

MTOTO WA MAAJABU: 4


Basi huyu mama alimkumbatia mtoto halafu akampakata vizuri na kumwambia,
“Mimi naenda, nitakukumbuka sana mjukuu wangu Ashura”
Baada ya kusema hayo alishangaa kumsikia mtoto huyu akimsonya.
Huyu mama aliogopa na kumuweka mtoto pembeni halafu aliwauliza wakina Mariam,
“Mmesikia jinsi alivyonisonya?”
Mariam akacheka na kusema,
“Hata hatujasikia, pole sana mama”
Juma alimuangalia mkewe na kumuuliza,
“Yani Mariam unacheka?”
“Jamani sijacheka kwa ubaya, kwani wewe umesikia mtoto akisonya?”
Juma nae akakataa kuwa hajasikia halafu Mariam akaongezea,
“Mtoto mdogo hivi na kusonya ni wapi na wapi jamani? Hakuna kitu kama hicho”
Mama mkwe hakuongea zaidi bali alibeba begi lake ikabidi wamsaidie tu kumsindikiza, wakati huo Juma ndio alimbeba mtoto wao, ila walipofika njiani tu, mama yao aliwataka warudi maana hakuona sababu ya mtoto kutembezwa barabarani ilihali akiwa mdogo bado.
Basi Juma na mkewe wakarudi nyumbani ambapo waliweka mtoto pembeni halafu Juma alianza kumsema mkewe,
“Unajua sijapenda kabisa, kilichokufanya kumcheka mama yangu sasa ni nini?”
“Sijamcheka kwa ubaya, ila huyo mama yako nilishamwambia kuwa mtoto huyu amelikataa hilo jina la Ashura ila alisema sina adabu hadi nikaja kumpigia magoti hapa kumuomba msamaha, yani siku ile ndio kacharusha mashetani yangu kabisa, muache tu asonywe”
“Mariam, chunga kauli zako. Kumbuka yule ni mama yangu, pia kumbuka umeteseka na hii mimba kwa miaka miwili ila yeye kahangaika kukutafutia dawa hadi wewe umeweza kujifungua salama, hivi kweli unaweza kumcheka?”
“Nisamehe mume wangu, haya tujadiliane huyu mtoto tumuite jina gani kwasasa?”
“Mmmmh tusimpe jina ila tumuite tu mtoto halafu hizo siku za mbeleni ndio tutampa jina”
“Jina gani unafikiri litamfaa?”
“Aaaah Mariam usiwe na haraka hivyo. Mambo yanaenda taratibu haya”
“Kwahiyo kwasasa tumuite mtoto tu!!”
“Ndio, tumuite mtoto”
Mariam aliitikia tu ili wasiendelee kujadili ile mada ya kuhusu mtoto ukizingatia kiukweli yeye alikuwa hamtaki kabisa huyu mtoto wake.

Leo mapema kabisa, Juma alimuaga Mariam kuwa anataka kutoka ila Mariam akang’aka na kusema,
“Kheeee unataka uniache na huyu mtoto peke yangu!!”
“Kwahiyo Mariam kwasasa sitatoka kwenda kutafuta hela wala nini, haya tutakula nini? Unataka niwe masikini unikimbie”
Mariam akacheka kidogo na kumuuliza Juma,
“Kwani hapo ulipo una utajiri gani jamani! Mbona sijakukimbia”
“Hivi Mariam, unaweza kuniweka mimi kwenye kundi la masikini? Ni kweli sina gari la kifahari wala gari la kawaida ila bado huwezi kuniweka kwenye kundi la umasikini, kumbuka hapa tunapoishi ni nyumba yangu mwenyewe kabisa, na hata kama ningekuwa nimepanga, ilimradi ningeweza kulipa kodi basi mimi sio masikini, hivi Mariam unavyopenda kula wewe na kuvaa vizuri, ningekuwa masikini ungekubali kuishi na mimi? Sina utajiri huo ila mimi huwezi kuniita masikini, hapo ulipo unakula unashiba tena chakula unachokitaka halafu upo kujichekelesha eti unaniuliza kuwa mimi nina utajiri gani!”
“Haya basi yamaisha Juma ila huwezi kutoka na kuniacha mimi na mtoto huyu peke yangu”
“Ngoja nikuulize sasa, unatakaje?”
“Labda atafutwe msichana wa kazi, yani hapa ndani tuwe tunaishi na msichana wa kazi ndio nitakuelewa”
“Sasa Mariam, swala la msichana wa kazi mapema hivyo itawezekanaje? Hayo ni maswala ya mchakato mke wangu”
Walianza kubishana tu pale kwani Mariam hakutaka kabisa mumewe kutoka pale nyumbani kwao, yani hiko kitu hakukitaka kabisa. Kisha Juma akamuuliza tena mke wake,
“Haya basi, sema tufanye nini kipindi hiki ambacho bado hatujapata msichana wa kazi?”
“Labda mdogo wangu Zayana aje hapa”
“Mmmh, ngoja tumpigie simu”
Moja kwa moja Juma alimpigia simu mdogo wake Mariam huku akimuahidi vitu vingi ili aweze kuja hapo kukaa na dada yake,
“Mmmmh sawa shemeji, mwambieni kabisa mama basi nitakuja kesho”
“Sawa, asante sana Zayana”
Basi moja kwa moja Juma alimpigia mama mkwe wake kumwambia kuhusu hilo ambapo mama yake Mariam alikubali kuhusu jambo hilo kuwa Zayana afike hapo kumsaidia dada yake.

Ilbidi leo Juma asitoke maana Mariam alisema hawezi kubaki hapo peke yake na mtoto basi Juma hakuona tatizo zaidi ya kuendelea pia kubaki hapo hapo ila akiwepo mdogo wake Mariam ndio aweze kuendelea na shughuli zake.
Basi Juma alipika pale na siku ile walikula huku akiongea na mke wake,
“Ila mke wangu wewe ni mvivu sana ndiomana unahitaji mdada wa kazi”
“Sio sababu ya uvivu tu ila mdada wa kazi namuhitaji sana sababu hata nikiwa nimeanza shughuli zangu basi apatikane mtu wa kumuachia mtoto”
“Mmmh haya bhana”
“Ila unajitahidi kupika mume wangu”
Juma alitabasamu tu na kuendelea kula, ila leo hakuna kituko chochote kilichofanywa na mtoto wao na waliishi nae vizuri tu hata usiku uliingia na walienda kulala na hakuna lolote baya ambalo lilitokea kati yao au kwa mtoto.
Kama kawaida usiku ule ni Juma ndio alilala na mtoto maana Mariam alishakataa kabisa jambo la yeye kulala na mtoto huyu.

Kulipokucha mapema kabisa, wote waliamka na kuanza kufanya shughuli chache za pale, huku nguo za mtoto zikiwa kwenye dishi, Juma akamwambia mke wake,
“Mariam, si ufue tu hizo nguo za mtoto”
“Mmmmh hivi Juma huna huruma wewe! Mimi nina mda gani toka nitoke kujifungua? Unawezaje kuniambia nifue nguo kweli!”
“Khaaaa Mariam, ila kweli sema mimi kidole kinaniuma sana”
“Atakuja kufua Zayana, unateseka na nini sasa”
Basi wakaacha zile nguo na kuendelea na mambo mengine.
Muda wakiwa wanakula leo, ndio muda ambao Zayana alifika na kuwasalimia, kisha walimkaribisha kile chakula na yeye aliungana nao kula kile chakula, ambapo Mariam akamwambia Zayana,
“Unaona mdogo wangu shemeji yako anavyoweza kukorofisha mambo, yani anajua kupika balaa”
Zayana akasema kwa aibu aibu,
“Naona, chakula ni kitamu sana”
Juma nae akasema,
“Yani dada yako badala apike yeye ili mimi nisifie, anabaki kila siku kusifia tu nikipika mimi”
Mariam akadakia,
“Na wewe Juma jamani! Ndio mahaba hayo”
Wakaendelea tu kula ambapo Juma aliinuka na kwenda kujiandaa kwani alifurahi sana kwa leo mdogo wake Mariam kufika ili na yeye aweze kwenda kwenye shughuli zake.

Zayana alikaa na dada yake na kuanza kuongea nae maana hata yeye hakupendezewa na ile kauli ya dada yake na ile ya shemeji yake,
“Dada jamani hadi leo unamuachia tu shemeji apike mwenyewe!”
“Tatizo liko wapi kwani? Anapenda kupika yule”
“Anapenda kupika ndio ila hadi analalamika kuwa hajala chakula chako dada! Nilijua kipindi kile cha mimba tu, yani hadi hapa umejifungua!”
“Hebu nitoleeni balaa na nyie, sijui sababu nimejifungua toto kubwa hilo ndiomana mnaona nipo sawa tu, sijui mnahisi toto limeshakuwa maana lina meno yote mdomoni, mimi bado nipo kwenye uzazi. Mdogo wangu wewe hujazaa bado kwahiyo mambo ya uzazi huyajui, kwa kawaida mwanamke anatakiwa kukaa miezi mitatu bila kufanya chochote”
“Mmmmh dada!”
“Unaguana nini sasa? Huko makazini kwenyewe huwa mwanamke akijifungua anapewa miezi mitatu ya kukaa nyumbani kwani uzazi unajulikana bhana, sasa mimi hata sina muda mrefu mnataka nianze kuhangaika jikoni kweli!! Hebu muwe na huruma basi, nimebeba mimba kwa miaka miwili jamani, halafu nianze kuhangaika na majiko kweli!!”
“Dada, sina maana hiyo. Ila ngoja nikurekebishe, unajua kwanini kazini huwa wanatoa miezi mitatu?”
“Kwanini?”
“Sababu mtoto anatakiwa kupata maziwa ya mama kwa muda wote kwa miezi hii mitatu, haya kuhusu kumpikia shemeji sina maana kuwa ndio uanze kukukuruka na majungu kwasasa, ila dada wewe ni mvivu jamani yani sijui kama ulikuwa ukimpikia shemeji kabisa”
“Weeee nilikuwa nikimpikia zamani, hebu achana na hizo habari kwanza. Kuna nguo za mtoto kwenye dishi pale nenda kazifue”
Basi Zayana akainuka na kwenda kufua zile nguo za mtoto wa dada yake.

Usiku wa leo, chakula kilipikwa na Zayana na kumfanya Juma afurahie kula kile chakula huku akisifia kuwa ni kizuri sana, basi waliongea mengi pale na moja kwa moja kwenda kulala.
Kama kawaida huyu mtoto alilala na Juma, ila Mariam alimuangalia sana mtoto wake na kuona kuwa kama siku hizi ameanza kubadilika vile, kwa kiasi Fulani aliacha kumuogopa yule mtoto wake.
Kulivyokucha asubuhi tu, Juma alifanya mambo yake na kuondoka zake, basi Mariam alibaki na mdogo wake wakisaidiana zile kazi ndogo ndogo za pale nyumbani kwao.
Basi muda huu walikuwa wamekaa huku wakiongea ambapo Zayana alimuuliza dada yake,
“Unajua dada, sijawahi kuona mtoto mdogo mwenye meno, huyu wa kwako ni vipi dada?”
“Umeanza sasa Zayana, huyo mtoto ana meno ya plastiki huwa wanaita hivyo, yatapotea yenyewe tu hayo”
“Duh!! Halafu dada, huyu mtoto mkubwa hivi hukujifungua kwa kisu kweli?”
“Mmmmh Zayana naomba usinikumbushe mambo ya uzazi wa huyu mtoto, nimeshaanza kusahau mimi haya mambo, tafadhari nakuomba usinikumbushe Zayana”
“Mmmh haya dada”
Waliendelea tu na maongezi mengine, kwakweli kwa kipinndi hiki kulikuwa na amani maana hakuna jambo baya ambalo limetokea hata Juma alikuwa akifurahi sana kila aliporudi na kukuta kuna amani mahali hapo.

Siku hii Juma alipokuwa anaenda kwenye shughuli zake akakutana na yule binti njiani ambapo yule binti alimsalimia Juma na kumuuliza,
“Hivi huhitaji msichana wa kazi nyumbani kwako?”
“Mmmmh wewe unataka nini kwani?”
“Hapana sitaki kitu ila hata mimi nafaa kuwa msichana wako wa kazi”
“Yani mimi nikuajiri mtu mwenye mambo ya ajabu kama wewe!! Siwezi kufanya huo upuuzi”
“Mambo yangu ya ajabu ni yapi?”
“Hapana, siwezi kukuajiri tu”
“Kwanini usiweze kuniajiri?”
“Hayakuhusu”
“Sawa hakuna shida, mkataa pema pabaya panamuita”
“Una maana gani?”
“Sina maana yoyote ila leo ukirudi nyumbani kwako utaona kuna tukio la ajabu limetendeka”
“Kivipi?”
“Hayanihusu”
Kisha huyu binti akaondoka zake na kumuacha Juma akiwa amesimama huku akimuangalia hadi alipoelekea halafu Juma alienda kwenye shughuli zake.

Mariam na mdogo wake wakiwa wamekaa wakamsikia mtoto akilia ambapo alikuwa kwenye kiti tu pale pale sebleni, basi Mariam akamwambia mdogo wake,
“Hebu muangalie hapo ana tatizo gani?”
“Atakuwa amekunya dada maana nasikia harufu hatari”
“Kheeee umenikumbusha kitu, hivi unajua kuwa huyu mtoto hajawahi kutoa haja kubwa kabisa!”
“Kheeee unamaanisha hajawahi kunya dada?”
“Mmmh na wewe, hebu kuwa na tafsida basi, najitahidi kuficha ukali wa neno hapa ila wewe hata hujali unaniambia tu ujinga ujinga, mimi na mume wangu humu ndani huwa hatutamki maneno ya hovyo kama hayo”
“Mmmh dada, haya bhana”
“Haya nenda kamuangalie basi umtoe hiyo haja”
Basi Zayana akainuka na kwenda kumuangalia mtoto ambapo aliamua kumuangalia kwanza kwa kumtoa ile nguo, Zayana alipomtoa alishangaa sana na kumwambia dada yake,
“Dada, njoo uone”
“Nione nini tena? Umenishtua loh!”
“Hapana, sina nia ya kukushtua ila njoo uone tu”
Mariam aliinuka na kusogea pale ambapo na yeye alishangaa sana halafu Zayana akasema,
“Dada inawezekana vipi kwa mtoto kunya mavi kama ya mbuzi!”
“Nimekwambia na wewe tumia tafsida basi jamani khaaa!! Hapa unajua nashangaa pia, sijawahi kuona kitu kama hiki, au sababu hajawahi kupata haja tangu amezaliwa?”
“Mmmmh inawezekana, ila dada uliwezaje kukaa na mtoto siku zote hizi bila kupata haja na bila kumpeleka hospitali?”
“Mmmh mdogo wangu acha tu, huyu mtoto hakuna hata huduma moja ya hospitali aliyoipata maana wote walimkataa”
“Mmmmh nadhani ndiomana sababu mtoto akizaliwa tu huwa wanamuangalia hivi vitu lazima anye na kukojoa ila mtoto akae siku zote hizo bila kunya jamani!”
“Hivi wewe Zayana una matatizo gani? Hebu acha maneno yako machafu hayo, kamnawishe basi huyo mtoto”
“Yananuka sana dada”
“Ndio hata mimi nasikia harufu, ila tutafanyaje sasa zaidi ya kumnawisha tu!”
Basi Zayana ilibidi tu amchukue yule mtoto na kwenda kumnawisha vile vile huku akiona kinyaa sana ila alimnawisha na kurudi kumvalisha.

Juma aliporudi tu ule ujumbe ndio ulikuwa wa kwanza kabisa kupewa kuhusu kujisaidia haja kubwa kwa mtoto basi alibaki kushangaa tu,
“Kama ya mbuzi!!”
Zayana akadakia,
“Ndio, yale kama karanga karanga”
“Yani Zayana khaaaa mambo yako mdogo wangu hadi unakera”
Juma alikuwa kimya tu ila alielewa maneno ya yule binti kuwa kuna jambo la ajabu litatokea ila kwake hili jambo hata halikuwa la ajabu sana kwani alihisi labda kutokana na mtoto wake kutokujisaidia toka siku amezaliwa ndio imepelekea kujisaidia kinyesi cha aina ile.
Usiku ule walilala tu kama kawaida, na hata asubuhi na mapema kabisa Juma aliamka na kujiandaa kwenda katika shughuli zake kama kawaida.

Basi muda huu Mariam alikaa na mdogo wake wakiongea ambapo mdogo wake aliamuuliza swali dada yake,
“Hivi dada, shemeji kasemaje jana kuhusu mwanae kutoa kinyesi kama cha mbuzi?”
“Kasema kuwa ni sababu mtoto hajapata choo toka azaliwe ndiomana imekuwa hivi”
“Ila dada kwa hizi siku chache tu nilizoishi hapa, namuona kama huyu mtoto hayupo sawa vile”
“Kivipi mdogo wangu?”
“Mmmmh namuona kama sio mtoto wa kawaida”
“Tatizo hujawahi kuzaa wewe mdogo wangu”
“Sio kutokuwahi kuzaa dada, ila nimewahi kuona watoto kadhaa dada ila mtoto huyu naona kama ni mtoto wa maajabu”
Mara mtoto alianza kullia kama ambavyo alikuwa akilia jana, ikabidi Zayana aende kumuangalia na kumkuta kajisaidia tena kama alivyojisaidia jana yake, basi Zayana akamwambia dada yake,
“Dada, mtoto wako kafanya tena mambo huku. Katoa kinyesi cha mbuzi”
“Mmmmh nenda kamnawishe tu Zayana”
Basi Zayana akambeba ili akamnawishe, alivyotaka kumuweka wenye dishi alishangaa yule mtoto akimwambia Zayana,
“Mimi sitaki kunawishwa na wewe, nataka kunawishwa na mama”
Yani Zayana aliogopa na kujikuta akitetemeka na kuwa kama ameganda vile alimuacha yule mtoto kwenye dishi na kumuita dada yake, Mariam alitoka hadi pale bila kujua kuwa kuna nini. Zayana akamwambia dada yake,
“Mtoto wako huyo, mnawishe mwenyewe”
Zayana akaondoka zake, na moja kwa moja alienda ndani kuchukua begi lake maana hakuona kama angeweza kuendelea kukaa pale na yule mtoto.

Mariam na yeye aliogopa alimuangalia yule mtoto aliyekalishwa kwenye dishi huku akimuangalia mdogo wake, akashangaa yule mtoto akimwambia,
“Unashangaa nini mama? Njoo uninawishe”
Mariam alitetemeka kwa uoga, na vile alivyomuona mdogo wake akitoka hata hakuuliza mara mbili bali na yeye aliunganisha nyuma kwa mdogo wake na wala hakubeba kitu.

Walipofika njiani ndipo walipoongea ambapo Zayana alimuuliza dada yake,
“Dada, mbona umeondoka pia?”
“Siwezikkuishi na mtoto wa ajabu kiasi kile”
“Ila ni mtoto wako dada, mimi ndio siwezi kabisa. Kitoto kidogo vile kinanisemesha, ila dada umemuacha mule mule kwenye dishi, si ataanguka kwenye maji yule? Atakufa dada”
“Aaaah siwezi, muache tu, yani hata nguo sichukui tutaenda tu wote nyumbani”
“Kwahiyo na kwako hujafunga wala nini?”
“Sijafunga ndio, siwezi kwakweli, mimi mwenyewe nimepatwa na uoga wa hali ya juu”
Walitembea hadi stendi, walikaa na kusubiria gari ila pale stendi wote wawili walianza kusinzia.
Waliposhtuka walijikuta wakiwa ndani sebleni huku mtoto akiwa kwenye kochi akiwaangalia.

Itaendelea…..!!!
By, Atuganile Mwakalile.
Leo nitaituma na MWANAUME WA DAR.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 04
MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 04
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-04.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-04.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content