MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 03 | BongoLife

$hide=mobile

MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 03

MTOTO WA MAAJABU: 3

Yani mtoto alikuwa chumbani ila alilia sauti hiyo hadi wote ikawashtua na kumfanya Mariam aende kumuangalia kuwa ana tatizo gani.
Mariam alipofika tu akamsikia mtoto wake akisema,
“Mama, sitaki hilo jina”
Mariam alijikuta yupo kama kaganda vile, yani alihisi kupigwa na ganzi mwili mzima kwakweli, alikodoa macho kumuangalia yule mtoto kwa muda kidogo halafu ndio akaanza kuogopa na kukimbilia sebleni,
“Jamani mama, huyu mtoto anaongea”
“Mariam, mtoto mdogo huyo anaongea kivipi?”
“Ila mkumbuke amekaa miaka miwili tumboni, mbona mengine mnayakubali halafu hili la kuongea mnalikataa?”
“Haya tumekubali, amesemaje? Amesema anataka maziwa au?”
“Hapana, ila kasema hataki hilo jina la Ashura”
Mama mkwe wa Mariam akacheka sana na kumuangalia Mariam kisha akamwambia,
“Hivi Mariam, unajua kama Ashura ni jina langu au hujui? Kama hujui basi ngoja nikujuze, hili ni jina langu na mimi nilirithi toka kwa bibi yangu”
Kisha yule mama mkwe wa Mariam alimgeukia mama yake Mariam na kumuuliza,
“Hivi mwenzangu, huyu mtoto ulimfunda akafundika kweli?”
Kiukweli mama Mariam alihisi aibu na kumfanya ainuke na kumvuta mkono Mariam hadi nje na kuanza kumsema,
“Mariam, unajua sio adabu hiyo yani kabisa unakataa jina la mama mkwe wako?”
“Hapana mama, mimi sijakataa ila mtoto ndio kakataa”
“Huyo mtoto akatae kwako wewe kwa ufahamu upi alionao? Mariam acha kunitia fedheha jamani, sijui naondokaje na kukuacha mtoto usiyekuwa na adabu hivi! Si unaweza kumjibu kitu kibaya mama mkwe wako wewe!”
“Hapana mama, nisamehe”
Mama Mariam alitumia muda kumkanya sana Mariam kwani hakupenda kabisa, aliona kama Mariam amemdhalilisha kwakweli.

Kisha walirudi ndani, ambapo Mariam alipiga magoti kwa mama mkwe wake kumuomba msamaha maana hata hakuna aliyemuamini pale kuwa mtoto kakataa jina, ilionekana ni yeye ndio halitaki lile jina,
“Naomba unisamehe mama, hii kitu haitajirudia tena mama yangu”
“Mariam, nione mimi kama mama yako na usithubutu kunivunjia heshima”
“Nimekuelewa mama, nisamehe mama yangu”
Kisha wakapatana pale halafu mama Mariam ndio akawaaga vizuri sasa halafu mama mkwe wa Mariam aliinuka kumsindikiza mama Mariam.
Kiukweli Mariam hata hakupenda kubakia peke yake na mtoto ila afanye nini ilihali yule ni mtoto wake? Yule ni damu yake? Yani Mariam hakuwa na raha kabisa.
Muda huu alijikuta tu kainuka na kwenda chumbani ambapo alimkuta yule mtoto kama yupo tu kucheza cheza kitoto kitandani, akawaza kuwa muda wote huyu mtoto angekuwa hivi basi kwake ingekuwa afadhari ila huyu mtoto alikuwa akimtisha tu.
Mariam alienda kukaa pale kitandani akimtazama huyu mtoto ila gafla huyu mtoto alianza kuongea yani Mariam alikuwa kama kapigwa na butwaa tena, huyu mtoto alisema,
“Mama, mkiniletea yale maziwa ya kopo mnichanganyie na ya ng’ombe ila msipofanya hivyo kwa hakika mtaingia umasikini maana mimi nakunywa sana maziwa”
Mariam alikuwa kama kapigwa gundi maana hakuweza kuinuka pale kitandani wala nini, ila moyo wake ulikuwa unaenda mbio sana hadi akaanguka pale kitandani na kuzimia.

Juma alipokuwa anatoka mjini, akakutana na yule binti ambaye jana yake alimpongeza kwa kupata mtoto, huyu binti alimsalimia Juma,
“Habari yako baba Ashura!”
Juma alishtuka na kumuangalia huyu binti kwa muda bila kusema chochote ambapo huyu binti akamwambia Juma,
“Hujui kama mwanao kapewa jina la Ashura?”
Juma akamuuliza,
“Unajua sikuelewi? Unaongelea nini?”
“Inamaana hujui jina la Ashura ni la nani?”
“Ni la mama yangu”
“Basi mama yako kampa jina hili mtoto wako, je umependa?”
Juma alimuangalia huyu binti na kumuuliza pia,
“Kwanini nisipende wakati ni jina la mama yangu?”
Huyu binti akamwambia Juma,
“Ni jina la mama yako ndio ila halimfai mtoto wako”
“Kwahiyo jina gani ndio linamfaa mwanangu?”
“Hapo sawa ulivyouliza, muite mwanao Mishi”
Juma akashtuka sana na kumuangalia huyu binti kisha akamwambia,
“Yani mimi nimuite mtoto wangu Mishi!! Hapana kwakweli”
“Kataa hilo jina ila jina atakalolitaka huyo mtoto wenu nadhani ndio utalipenda. Kwaheri”
Yule binti akaondoka, yani Juma alimuangalia bila ya kummaliza kisha yeye akarudi zake nyumbani kwake.

Juma alimkuta mama yake akiwa na harakati za kupika kwa muda huu, basi alimsalimia na kumuuliza mama mzazi wa Mariam,
“Khaaa kashaondoka yule”
“Yani nilikuwa nimechanganyikiwa hata sijamuaga vizuri masikini jamani, ila nishaleta maziwa. Safari hii nimeleta makopo manne”
“Yani hayo hesabu wiki tu yatakuwa yameisha”
“Jamani mama!!”
“Mimi nawaambia jamani, watoto kama hawa huwa tunawapa uji, ukijifanya unapenda kumpa maziwa sana basi utalia na kufilisika nakwambia mwanangu. Kwanza huyu mwanamke mwenyewe kakufilisi, halafu uzao wake nao unataka kukufilisi khaaa jamani!”
Juma akaenda moja kwa moja ndani ili amwambie mkewe amuandalie mtoto maziwa, ila alishangaa sana alipoingia chumbani kumkuta Mariam kalala hoi halafu yule mtoto yupo pembeni akinyonya ziwa la Mariam wakati Mariam alishamuachisha mtoto huyu.
Juma alisogea na kumuondoa yule mtoto huku akimuamsha Mariam maana aliona kanyonywa maziwa hadi yamelegea yani, alijikuta akimuonea huruma tu kwa muda huo.
Juma alijitahidi kumuamsha na hata kummwagia maji ndipo Mariam aliposhtuka ila alishindwa kunyanyuka maana alikuwa akihisi kizunguzungu, alikuwa akinyanyuka anaanguka.
“Khaaa Mariam, itabidi twende hospitali mke wangu”
Hata kujibu Mariam hakuweza kabisa, ikabidi Juma amuandae mke wake na kumuacha mtoto kwa mama yao kisha yeye kumpeleka Mariam hospitali.

Kule hospitali, Mariam alionekana kupungukiwa damu mwilini mwake, hivyo Juma mwenyewe ndio alijitolea kumuongezea damu mke wake huku akimuhurumia sana.
“Pole mke wangu, utapona kabisa”
Kwahiyo Mariam aliachwa kalazwa hapa, halafu Juma alirudi nyumbani maana kule alimuacha mama yake peke yake na mtoto.
Alipofika tu nyumbani, Juma akapewa ujumbe na mama yake,
“Hivi unaweza kuamini?”
“Kuamini nini mama?”
“Huyu mtoto kamaliza kopo lote la maziwa”
“Kheeee!! Huyu huyu mtoto?”
“Ndio, kwani tunamuongelea nani hapa?”
“Nimechoka mama kwa hilo, halafu Mariam amepungukiwa na damu nimetoka kumuongezea”
“Pole mwanangu, itakuwa sababu ya uzazi, wanawake huwa tunapoteza damu nyingi sana wakati wa kujifungua”
“Ndio hivyo mama ila swala la mtoto kumaliza maziwa kopo lote mbona limenitatiza zaidi!”
Juma aliongea sana na mama yake, ila leo usiku ilibidi Juma alale na mtoto maana Mariam alikuwa hospitali.

Leo Mariam alipewa ruhusa ya kurudi nyumbani, ila alimgomea mumewe kabisa kurudi nyumbani,
“Sasa Mariam unataka kuendelea kukaa hapa hospitali?”
“Hapana, ila nataka nirudi nyumbani kwetu”
“Khaaaa na mtoto wako je?”
“Huyo mtoto ndio simtaki kabisa, ataniua huyo mtoto Juma”
“Hapana hakuui ni wasiwasi wako tu”
“Mtoto gani mchanga anaongea?”
“Haongei bhana ila ni hisia zako tu Mariam”
“Basi nikirudi nyumbani naomba ufatane na sharti langu”
“Sawa nipo tayari ila sitaki uende pengine zaidi ya kule tunapoishi mimi na wewe”
“Sawa, ila sitaki kulala na huyo mtoto kabisa, utakuwa ukilala nae wewe”
Juma ilibidi tu akubali kwani yeye kama yeye hakuona kama kuna tatizo zaidi kwa yule mtoto ukizingatia huko kuongea hajawahi kumsikia yule mtoto akiongea.
Basi walikamilisha kila kitu pale hospitali kisha kupewa ruhusa ya kurudi nyumbani.

Mama mkwe wa Mariam alikuwa akilalamika tu pale waliporudi kuhusu maziwa maana yule mtoto alimaliza kopo lingine la maziwa,
“Jamani, kopo la pili la maziwa limeisha, khaaaa hili ni balaa”
Mariam akadakia na kusema,
“Jamani huyu sio mtoto nawaambia”
Mama mkwe wake akamfokea,
“Acha ujinga Mariam, kwahiyo umezaa kitu gani? Hebu kumbuka ni kipindi gani umetafuta mtoto, hebu kumbuka ni kiasi gani umehangaika na uzao wa mtoto hadi Mwenyezi Mungu kakusaidia kumpata mtoto huyu, unatakiwa uwe na shukrani sana”
Mariam alikaa kimya ila hakuwa na raha na huyu mtoto wake kabisa, kwa muda huu aliamua tu kwenda kupumzika maana alijihisi bado ana uchovu wa hospitali.
Mama Juma akaanza kuongea na Juma pale,
“Mwanangu bila maarifa yoyote jua kwamba itasumbua sana kumlea huyu mtoto!”
“Maarifa gani sasa mama?”
“Nakwambia huyu mtoto tumtengenezee uji tu hakuna namna, aanze kunywa uji vilivyo, sio kwa ulaji huu jamani”
Muda huo huo Mariam alitoka ndani na kuwaambia,
“Nimekumbuka kitu, huyu mtoto aliniambia kuwa tukitaka ashibe basi tumchanganyie maziwa ya unga na maziwa ya ng’ombe”
Mama mkwe wa Mariam alishangaa sana,
“Weee Mariam, umeanza sasa ndoto zako? Huyu mtoto kakwambia saa ngapi? Halafu hayo mambo ya kuchanganya maziwa ya unga na maziwa ya ng’ombe kumpa mtoto ndio mambo ya wapi?”
“Hata mimi sijui ila huyu mtoto aliniambia kweli”
“Mariam, Mariam unajua mambo mengine uwe unafikiria kabla ya kuyasema, haya tumekubalia ila je anapewa kwanza maziwa ya ng’ombe halafu yanakuja ya unga au anaanza kwa kukorogewa kwanza ya unga halafu anakuja kunywa ya ng’ombe?”
“Kwa uelewa wangu ni kuwa yale maziwa ya ng’ombe tukiyachukua tumkorogee na maziwa ya unga, yani kwenye maziwa ya unga badala ya kukoroga maji tumkorogee kwa maziwa ya ng’ombe kwahiyo kiwango cha maji kiwe ndio kiwango cha maziwa ya ng’ombe”
“Kheeee makubwa hayo, kwahiyo huyu mtoto itakuwa maji yake ni maziwa eeeh!! Makubwa haya, sijapata kuyafikiria”
Juma aliyekuwa kimya kwa muda mrefu alikuwa akitafakari ujumbe ule na maneno ambayo aliwahi kuambiw ana yule binti waliyekutana nae kuwa huyu mtoto akimfanyia hivyo ndio atafurahi, basi mama mkwe wa Mariam akamshtrua Juma pale kwa kumuuliza,
“Haya, na wewe unasemaje juu ya kauli ya mkeo kuwa mtoto akorogewe maziwa ya ng’ombe na ya unga pamoja!”
“Mama sikia, tusianze kujadili sana kuwa Mariam kaongea muda gani na huyu mtoto, kwanza tukumbuke kuwa Mariam ni mama wa huyu mtoto kwahiyo ni mengi anayaelewa ya mwanae, mengine tunageleshwa tu sisi hapa. Sikia tufanye hivyo hivyo alivyosema yeye, huwezi jua uleaji alioupanga juu ya huyu mtoto”
Mariam alimuangalia mumewe, ila hakupenda ile kauli ya mumewe kabisa, akainuka na kwenda chumbani ila muda wote wanaongea hayo mtoto alikuwa amelala kwenye kochi pale sebleni.

Usiku wakiwa wamelala, ilikuwa kama walivyopanga kuwa Juma ndio awe analala na mtoto halafu Mariam asiwe analala na mtoto kabisa ila Juma alimvizia Mariam akiwa amelala kabisa kisha akaenda kumuweka mtoto pembeni ya Mariam ambapo Mariam alilala usingizi mzito sana yani alikuja kushtuka wakati tayari pameshakucha kabisa anashangaa tu kumuona mtoto pmbeni, akamuangalia huyu mtoto akamuona akitabasamu, kiukweli Mariam kila tendo la huyu mtoto alijikuta tu kutokulipenda kabisa, kwahiyo kitendo cha huyu mtoto kutabasamu wala Mariam hakukipenda wala nini.
Akakaa kama kuogopa hivi ila huyu mtoto kama alitaka kuongea ila hakuongea kitu chochote zaidi zaidi Mariam aliona kama muonekano wa mtoto wake umebadilika yani akawa kama mtoto aliyetoka kuzaliwa mwenye wiki moja hivi tofauti na ambavyo huwa anamuona, pale Mariam alishtuka tena na kuinuka kwenda kumuita mumewe aliyekuwa akijiandaa kwaajili ya kwenda kwenye shughuli zake chache,
“Juma, njoo umuone huyu mtoto kabadilika leo”
“Kivipi yani, kabadilikaje?”
“Kawa kama mtoto mchanga”
Juma akamuangalia mkewe kwa makini kisha akaenda chumbani ambapo walimkuta mtoto akiwa vile vile kama siku zote, Juma alimuangalia mkewe na kutikisa kichwa huku akisema,
“Ila Mariam una matatizo sana tena sana”
Halafu Juma akatoka na kuondoka zake, Mariam alijisemea,
“Hivi mimi nitaweza kweli kumlea huyu mtoto!!”
Mara akamsikia huyu mtoto akisema,
“Utaweza tu mama”
Hapa Mariam aliogopa na kutoka nje ila hakuongea chochote na mama mkwe wake ukizingatia alikuwa haaminiki kabisa kwenye swala la kusema kuwa mtoto anaongea.

Mama mkwe wa Mariam aliona Mariam amekaa muda mrefu sana nje ikabidi aende kumuuliza maana hata ile kumaliza vizuri kuhusu uzazi alikuwa hajamaliza wala nini,
“Unajua Mariam huwa sikuelewi kabisa mwanangu, kwani huyu mtoto ilikuwaje kwanza?”
“Kivipi mama?”
“Kwanini unamkimbia? Unajua hujamaliza siku nyingi tangu ujifungue ila ushaanza tabia ya kukaa muda wote nje na kumuacha mtoto ndani peke yake, unajua sikuelewi”
“Mama, sidhani kama mnaweza kunielewa hata nikisema nini bado kunielewa itakuwa ngumu. Hapa nangoja mwezi ufike tu nianze kufanya shughuli zangu zingine”
“Mmmmh hivi unafikiri kuwa mimi nitakuwa hapa siku zote? Hapana, mimi nitaondoka”
“Hamna shida, nitatafuta msichana wa kazi”
“Mmmmh sijapata kuona binti mvivu kama wewe hata sijui mwanangu alikupendea nini”
“Mama, usitake nikujibu vibaya kabisa. Huyo mwanao hebu muulize vizuri, alinibembeleza kunioa balaa na wala nilikuwa simtaki halafu kuhusu swala la uvivu huyo mwanao anatambua fika kuwa mimi ni mvivu namba moja, kiasi kwamba hata nguo zake huwa anajifulia mwenyewe”
“Mmmmmh!! Sijui kama wazazi wako walitambua wajibu wao kwako jamani loh!! Mimi kesho au kesho kutwa naondoka, nitakuacha wewe na mumeo hapa mfurahi”
“Haya hakuna tatizo”
Yani Mariam alimjibu tu mama mkwe wake bila hata ya kujali, na wala hakuwa anawaza kuwa mama huyu ndio kamsaidia dawa hadi ya kuweza kujifungua mimba iliyompeteza kwa miaka miwili ila muda huu alikuwa akimjibu kwa kujisikia yeye.
Mama mkwe aliondoka zake na kurudi zake ndani maana hakupenda kubishana kwa muda huo na Mariam.

Usiku ule, mama mkwe wa Mariam aliamua kuongea na mwanae Juma maana hapo alishakata shauri la kuondoka kesho yake maana alihisi kuendelea kuishi hapo angegombana tu na huyu mkwe wake Mariam,
“Mwanangu, mimi naondoka kesho”
“Kheee mama, mbona mapema hivyo?”
“Ndio nimeshaamua hivyo, nitaondoka kesho”
“Kwani kuna tatizo lolote mama yangu?”
“Hamna ila kumbuka na mimi nina mji wangu, na mimi nina majukumu yangu, kama mkeo nimeshamuhudumia tayari imetosha”
“Mama, hata wiki mbili hazijapita?”
“Sio tatizo, ilimradi kaonekana kuweza kujihudumia mwenyewe, nibaki nifanye nini mimi? Kesho naondoka zangu, nielewe tu mwanangu”
“Sawa mama, ila tutakukumbuka sana mama”
“Ila nakuonea huruma maana najua nepi zote utafua wewe, chakula utapika wewe, na nyumba utasafisha wewe, huyu mwanamke ni kama umeoa doli tu ndani ya nyumba”
Juma alicheka kidogo na kutikisa kichwa kisha akamwambia mama yake,
“Yani mama, huyu Mariam nisingekuwa nampenda kwa hakika nisingemuoa, sijapata kuona mwanamke mvivu kiasi hiki”
“Na mimi sijapata kuona wakina Mariam wavivu kama huyo mke wako!”
“Mama, kuna historia ndefu sana ya huyu mtu ila tu ni sababu nampenda sana na siwezi kumuacha”
“Ila wewe, kama ni kurogwa basi umerogwa na kupitiliza. Haya mimi naenda na ninakutakia kazi njema za humu ndani maana najua zote zitakuangukia wewe mwenyewe”
Huyu mama alionekana kuongea kwa simanzi sana kwani toka mwanzoni wakati Juma anaoa alikuwa ni kinyume kabisa na ndoa hii.

Kesho yake mapema kabisa, mama mkwe wa Mariam alishajiandaa kwaajili ya safari aliwaita wote kwaajili ya kuwaaga ambapo Juma alimpa mamake mtoto wake ili yule mama aweze kumuaga mjukuu wake.
Basi huyu mama alimkumbatia mtoto halafu akampakata vizuri na kumwambia,
“Mimi naenda, nitakukumbuka sana mjukuu wangu Ashura”
Baada ya kusema hayo alishangaa kumsikia mtoto huyu akimsonya.

Itaendelea…..!!!
By, Atuganile Mwakalile.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 03
MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 03
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-03.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-03.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content