MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 02 | BongoLife

$hide=mobile

MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 02

MTOTO WA MAAJABU 2:

Kitu ambacho kilimshangaza Mariam, hakujifungua mapacha bali alijifungua mtoto mmoja, kitu kilichowashangaza pale leba wote ni kuwa mtoto wa Mariam baada ya kuzaliwa alikaa mwenyewe pale kitandani.
Walizidi kushangaa zaidi kwa kitendo cha yule mtoto kushika kitovu na kukikata mwenyewe, yani pale wodini hakuna aliyebaki kwani wote walikimbia, alibaki tu Mariam na mtoto wake kwani kila Mariam alipojitahidi kuinuka alishindwa, alibaki akipiga kelele tu.
Yule mtoto alimsogelea Mariam na kumuuliza,
“Sasa kelele za nini mama?”
Kisha akajiweka vizuri kwenye mikono ya Mariam na kuanza kunyonya ziwa la Mariam, kwakweli Mariam hakuweza kuvumilia hali ile na kujikuta akizimia pale pale kwa muda ule maana hata nguvu ya kukimbia hakuwa nayo.

Daktari alienda moja kwa moja kumuita mume wa Mariam ambapo mume wa Mariam aliambatana na mama yake kwenda kumsikiliza daktari kuwa ana hoja gani kwa muda huo kwao,
“Jamani, kuna jambo sio la kawaida limetokea huko leba”
“Jambo gani tena?”
Dokta aliwaambia tu kifupi halafu akasema,
“Msishangae tumekimbia, katika hali ya kibinadamu lazima tuogope mambo kama haya, ni kweli madaktari tunakutana na vitu vya ajabu sana ila mambo mengine tunaingiwa na uoga”
Basi akaongozana na mume wa Mariam na mama yake hadi kile chumba ambacho Mariam alijifungulia maana aliwekwa kwenye chumba cha peke yake, walimkuta Mariam kazimia ila kale katoto kapo pembeni kakinyonya na wala hakakuwa na wasiwasi wowote ule, dokta aliwaambia,
“Mtoto mwenyewe ndio yule pale, hapa hata nafikiria namna ya kumchukua ili tumfanyie vipimo kujua kazaliwa na kilo ngapi hata kumpatia chacho ya kwanza”
Mume wa Mariam akamwambia daktari,
“Sasa dokta, kama wewe unaogopa unataka sisi tufanyeje? Nenda kamchukue maana hiyo ni kazi yako”
Basi dokta akataka kwenda kumchukua mtoto ila huyu mtoto alimpiga jicho hilo dokta na kumfanya dokta aogope maradufu ila Juma yani mume wa Mariam alijikuta akijivika ujasiri na kumwambia mama yake,
“Hivi mama, niogope nini sasa wakati yule aliyelala pale ni mke wangu na yule ni mtoto wangu! Niogope nini sasa?”
Juma akasogea karibu na kumchukua mtoto akamfunga vizuri, kisha akamuomba yule daktari kumshughulikia mke wake ili waweze kwenda nae nyumbani.
Na kweli Juma alipombeba yule mtoto ni muda ule ule yule mtoto alilala kwenye mikono ya Juma ila hakuna hata mtu mmoja aliyetaka kumshika yule mtoto kabisa.

Walirudi nyumbani sasa, kiukweli Mariam tangu ameshtuka hakutaka hata kuulizia habari za mtoto wala nini ila Juma anamchukua mtoto na kumweka kitandani karibu na Mariam, hapo Mariam akauliza,
“Hivi mimi ndio nimezaa kiumbe cha ajabu hivi!!”
Mama mkwe wake akamfokea Mariam,
“Weee hebu tema mate chini, kiumbe cha ajabu kivipi? Ngoja nikuuliza, huyo mtoto hana miguu?”
“Anayo”
“Hana macho, pua, mdomo na masikio?”
“Anayo”
“Hana mikono huyo mtoto? Hana ngozi au hana nywele”
“Vyote anavyo”
“Sasa unawezaje kumuita mtoto wako mwenyewe kuwa kiumbe cha ajabu? Tema mate chini Mariam, hebu angalia jinsi wewe na mumeo mlivyohangaika kupata hiyo mimba, hebu angalia mlivyohangaika kumpata huyo mtoto halafu muda huu unasema ni kiumbe cha ajabu?”
Mtoto aliamka na kuanza kulia, hapa Mariam alimshangaa zaidi mtoto wake,
“Khaaaa sikumuona jamani, kumbe huyu mtoto ana meno”
Mariam akaanza kuogopa, basi mama mkwe wake akaanza kumsema,
“Hebu acha ujinga Mariam, hivi unadhani ni masikhara kwa mtoto kukaa tumboni miaka miwili? Lazima mtoto atoke meno hapo, mambo ya dunia tu yalikuzunguka usiweze kuzaa, sasa umepata kitoto chako badala ukifurahie unaanza kuhaha na kasoro za mtoto, sijui ana meno sijui vitu gani, hebu acha ujinga”
Mariam alikaa kimya na huyu mama mkwe wake alimtaka Mariam ale chakula ilia toe maziwa mengi na apate kumnyonyesha mtoto wake, kwahiyo muda huu mama mkwe ndio alimchukua mtoto kumbembeleza.

Juma akawapigia simu ndugu zake na ndugu wa Mariam kuwa Mariam ameshajifungua na hiyo ilikuwa ni furaha kubwa sana hasa kwa mama yake Mariam ambaye alikuwa akimuonea huruma sana binti yake kwa kukawia bila kujifungua, alimuhurumia kwa kukaa na mimba kwa muda mrefu.
“Kheee Mungu ni mwema, kwahiyo kaniletea madume yangu maana aliniambia kuwa ana mapacha wa kiume”
“Hapana mama, ni mtoto mmoja wa kike”
“Kheeee, si mlisema mmepima hospitali nyie na kujua jinsia ya mtoto!”
“Ndio mama, ila mara nyingine vipimo navyo vinakosewa, wale nao ni binadamu wale”
“Mimi nilikuwa nawasikiliza tu na hoja zenu khaaaa, nitakuja kesho asubuhi huko kumuona mwanangu na mke mwenzangu, nimefurahi sana. Hongereni wanangu”
“Asante mama”
Basi kwa muda huu Juma aliamua kwenda mjini ili kumnunulia vizawadi kidogo mtoto wake ingawa vitu vingi vya mtoto vilikuwepo ndani ukizingatia walikuwa wakijiandaa kabisa bila ya mafanikio yoyote.

Yani usiku wa leo ni Juma tu ndiye aliyeweza kulala na mtoto pembeni maana Mariam alijikuta akimuogopa mtoto wake kupita maelezo ya kawaida, ilikuwa mtoto akiamka na kuanza kulia ndipo Juma alikuwa akimuamsha mkewe aweze kumnyonyesha mtoto wao huyu, yani Mariam hakumtaka kabisa huyu mtoto.
Kesho yake asubuhi na mapema kabisa, alifika pale mama mzazi wa Mariam na mdogo wake Mariam aliyejulikana kwa jina la Zayana.
Hata na wao walishangaa kumuona mtoto vile ila mama mzazi wa Mariam ilibidi tu ajiweke kwenye nafasi ya umama na kumfundisha mtoto wake namna ya kumkubali yule mtoto,
“Mariam mwanangu, sijaona tatizo la huyu mtoto”
“Mama, mtoto gani ana meno jamani!”
“Mbona wapo watoto wanaozaliwa na meno mwanangu?”
“Huwa wanaita meno ya plastiki ila huyu sio meno ya Plastiki ni meno kabisa ya kikubwa, halafu ungemuona jana sasa hizo kucha loh! Juma ndio alimkata”
“Ila mwanangu hiko kitu sio cha kushangaa sana, mtoto amekaa tumboni kwa miaka miwili! Ulitaka atoke vile vile akiwa mtoto!”
“Ila mama, laiti na wewe ungekuwepo hospitali na kuona kituko cha huyu mtoto sijui kama ungemtaka, unajua kuwa huyu mtoto alijikata kitovu mwenyewe halafu aliniongelesha!”
“Acha masikhara bhana Mariam, unajua mara nyingine wazazi tunakumbwa na mambo mengi, mimi bado sioni tatizo kwa huyu mtoto, leo mwanao Mariam na umlee kwa furaha tu”
Mama yake aliongea nae kwa muda sana ingawa kiukweli Mariam hakuwa na raha kabisa maana kuna matendo mengine ya mtoto yule, hawa wengine hawayajui ila Mariam pekee anayajua na kuyatambua matendo hayo.

Basi muda huu Mariam alienda uwani, akamsikia mdogo wake Zayana akiongea na simu yani kama alikuwa akimuelezea mtu kuhusu mtoto wa Mariam,
“Kheeee hicho kitoto cha dada sasa huwezi hata kukishika kwanza unaweza kuhisi kuwa utaota usiku, mtoto kazaliwa na sura ya utu uzima nakwambia, akicheka meno yote yamemjaa mdomoni, halafu halii ng’aaaa ng’aaaa kama watoto wengine yani analia kama toto kubwa kabisa”
Mariam akamfata mdogo wake na kumfokea pale,
“Hivi wewe Zayana una akili kweli?”
“Nisamehe dada”
“Usimcheke mamba kabla hujavuka mto, hapo ulipo hujaolewa, hujazaa bado halafu upo kunicheka mimi. Yani na wewe huwezi kutambua jinsi dada yako nilivyohangaika na hii mimba? Ni haki yangu kuzaa mtoto mkubwa, sasa mtoto kaka miaka miwili tumboni unategemea akitoka atakuwaje? Tembo ndio huwa wanabeba mimba miaka miwili ila sio binadamu, kwahiyo kilichotokea kwangu inamaana mtoto alikuwa akikulia tumboni”
“Ndio miaka miwili jamani dada!”
“Haya, wewe utabeba miezi mitatu, tusisumbuane akili halafu utaangalia mtoto wangu aliyezaliwa kwa miaka miwili na wako wa miezi mitatu yupi ni mtoto”
“Dada!!”
Mariam akaenda zake kwani hakupenda kabisa jinsi mdogo wake alivyokuwa akimwambia aliyekuwa anaongea nae kwenye simu, ingawa kiukweli hata yeye mwenyewe hakuupenda muonekano wa mtoto wake.

Basi leo mamake Mariam na mama mkwe wake wanaongea kuhusu jina la kumpa mtoto, basi mama mkwe wa Mariam akasema,
“Kikawaida jina la mtoto linatoka baada ya siku saba, kwahiyo baada ya siku saba tutamtajia mtoto jina lake”
“Sawa hakuna tatizo, ila hivi unavyoona huyu mtoto yupo sawa kweli?”
“Kwanini umeuliza hivyo wakati nilikusikia ukiongea na mtoto wako na ulimshauri vizuri tu!”
“Nimefanya vile kwaajili ya kucheza nafasi yangu ya umama kwa mtoto maana sisi wa nje tukimvunja moyo Mariam basi tunaweza fanya Mariam akamchukia huyu mwanae kupita maelezo ila kiukweli hata mimi nimejivika moyo wa chuma tu, ndiomana nakuuliza mwenzangu unaonaje?”
“Hata na mimi nimejivika moyo wa chuma hivyo hivyo, kwanza uzazi wa huyu mtoto ni waajabu sijapata kuona, hao wakina Mariam wameshaangaika kama kwa waganga wamemaliza, mahospitali ndio usiseme hadi mara ya mwisho kapatana na hoja kuwa ana mapacha wa kiume tupu, khaaaa madokta nao waongo jamani kumbe mtoto mmoja tena ni wa kike. Halafu hivi unajua kuwa mtoto huyu katangulia miguu kuzaliwa baada ya kichwa?”
“Kheeee, ilikuwaje sasa?”
“Ndio hivyo hivyo, madaktari walivyoangalia wakasema kuwa ni operesheni tu pale, ila sasa kabla ya hiyo operesheni alijifungua muda huo huo na hivyo hivyo mtoto katangulia miguu, halafu kilichoshangaza zaidi mtoto akakaa na kukata kitovu mwenyewe”
Mama Mariam kama alishtuka yani na kusema,
“Naogopa, sijui ningezaa mtoto wa hivyo ningekuwaje tunampa moyo tu Mariam ila kiukweli jambo hilo linaogopesha sana”
“Yani mimi mtoto nimekuja kumshika tukiwa hapa nyumbani, yani kutoka hospitali ni Juma ndio kamshika halafu Juma anamuona mwanae ni wa kawaida kabisa na hata kukesha usiku anakesha yeye na sio Mariam yani mwanao ndio nahisi alitamani hata angeambiwa kuwa mtoto wake amekufa”
“Mmmmh hapo pagumu, mimi kesho kutwa nitarudi nyumbani kwangu, yani hata sijui babake Mariam nitamueleza nini juu ya huyu mtoto jamani khaaaa!”
“Utamueleza tu, yani tuamini tu kuwa ni mtoto wa kawaida ili tusiishi kwa mashaka maana hali ya huyu mtoto inaogopesha kwakweli. Inatakiwa ujasiri”
Walijadiliana sana kuhusu mtoto wa Mariam.

Yani Juma ndio alikuwa pekee wa kumuangalia mtoto, kumbadilisha nguo, kusema kuwa apewe maziwa na kila kitu yani Mariam hata hakujisikia kumnyonyesha huyu mtoto.
Leo Mariam aliamka tu na kuanza kulia, ikabidi mumewe amuulize kitu kinachomliza,
“Matiti yananiuma”
“Kheeee kwanini sasa?”
“Yametoka viodonda, inaonyesha huyu mtoto usiku kaning’ata sana hata sijui kaning’ata kwa muda gani jamani!”
Basi Juma aliamua kumbembeleza mke wake ni kweli alikuwa na vidonda vikubwa sana, ikabidi kulivyokucha, Juma aende kutafuta maziwa ya ng’ombe kwaajili ya kumpa mtoto maana Mariam ndio alikataa ramsi kumnyonyesha mtoto wake kutokana na kutokwa na vidonda vingi kwenye maziwa yake.
Juma alipomletea huyu mtoto maziwa ya ng’ombe aligoma kuyanywa kabisa na alikuwa akilia sana hadi ilibidi wale bibi zake wamkorogee uji na kumpa ambapo alikunywa kidogo tu, basi Juma akajihimu kwa siku hii kwenda zake mjini ili kumtafutia mtoto maziwa ya kopo aliona pengine anaweza akayanywa maziwa hayo.

Juma akiwa mjini, kuna binti alikutana nae mjini ambapo binti huyu alimsalimia Juma na baada ya salamu akamwambia Juma,
“Hongera sana kwa kupata mtoto wa kike”
Juma hakuitikia kwanza ila alimuuliza,
“Kwani unanijua?”
“Ndio nakujua vizuri sana, naweza kukueleza historia ya maisha yako hadi na wewe ukashangaa”
“Mmmmh mbona mimi sikujui”
“Sio hunijui ila tu umenisahau maana ni kitambo sana, mimi najua kuwa wewe na mkeo hadi mlihama mtaa sababu ya mkeo kubeba mimba bila kujifungua, sikia Juma nikwambie, unajua mkeo ana kiherehere sana, kaambiwa zile dawa ni aoge siku tatu ila yeye alioga siku mbili kisa tu alitaka kujifungua ndio avumilie na kulea”
“Sikuelewi ujue”
“Tuachane na hayo, mwanao anaitwa nani?”
“Bado hatujampa jina”
“Nikutajie jina la kumpa?”
“Hapana, sisi wenyewe tuna majina mengi tu kwahiyo siwezi kukubali jina la mwanangu nitajiwe na mtu nisiyemjua”
“Sasa mimi unanijua ila umejisahaulisha tu, ila ngoja nisiongee sana. Ngoja nikwambie cha kufanya na maziwa hayo, yani hayo maziwa ya unga uwe unachanganya na yale ya ng’ombe unampa mtoto”
“Kheeee ndio mambo ya wapi hayo? Yani haya maziwa ya unga yakorogwe kwenye maziwa ya ng’ombe?”
“Ndio, unatakiwa kufanya hivyo”
Halafu huyu binti akaondoka na kumuacha Juma akimuangalia tu.

Juma alirudi nyumbani kwake akiwa na makopo mawili ya maziwa kwaajili ya mtoto na alipofika tu walimkorogea yle mtoto na kumpa, alikunywa kama maji mpaka Mariam akashangaa huku akiuliza,
“Jamani hii ni kawaida kweli?”
Mamake Mariam akasema,
“Kwa mtindo huu haya makopo mawili hayawezi kumaliza hata wiki!”
Mama mkwe wa Mariam akasema,
“Ila jamani tukumbuke huyu mtoto amekaa miaka miwili tumboni kwahiyo tuache kumuhesabie kitoto kama tunavyofanya, ndiomana tunapigwa na butwaa kila muda sababu huyu mtoto tunamuhesabia kitoto sana”
Basi wakaitikia tu.

Ilifika siku ambayo mamake Mariam alikuwa anaondoka, ila yule mtoto alikuwa ameshamaliza yale makopo mawili ya maziwa na alikuwa akilia njaa, hapo waliangaliana na kukosa jibu kabisa ikabidi Juma aanze kumbembeleza mwenyewe mtoto na alipolala alienda kumlaza chumbani na kurudi sebleni, basi mamake Mariam akashauri,
“Jamani, mimi sioni sababu ya kusubiria siku saba kwa mtoto mkubwa hivi, kwahiyo nashauri tumpe jina tu”
Hata mama mkwe wa Mariam naye alikubali hilo na kumuuliza Juma,
“Eeeeh mwanangu, unataka jina gani kumpa mtoto wako?”
“Aaaah mama, jina lolote tu mtakaloamua kumpa kwangu ni sawa, sina tatizo juu ya hilo kabisa. Ngoja niwahi mjini nikamnunulie maziwa mengine”
Basi Juma akajiandaa haraka na kuondoka zake, kule nyumbani walibaki wakiongea tu ambapo mamake Mariam akasema,
“Yani mimi napenda nijue jina la mtoto kabla sijaondoka”
Basi mamake Juma akasema,
“Sababu huyu mtoto ni wa kike basi aitwe jina langu”
“Aaaaah, hivi jina lako ni nani vile?”
“Mimi naitwa Ashura, kwahiyo huyu mtoto tumuite Ashura”
Yani mtoto alikuwa chumbani ila alilia sauti hiyo hadi wote ikawashtua na kumfanya Mariam aende kumuangalia kuwa ana tatizo gani.
Mariam alipofika tu akamsikia mtoto wake akisema,
“Mama, sitaki hilo jina”

Iatendelea…..!!!
By, Atuganile Mwakalile.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 02
MTOTO WA MAAJABU SEHEMU YA 02
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-02.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/mtoto-wa-maajabu-sehemu-ya-02.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content