MAMBO 5 YENYE ATHARI MBAYA KWENYE NDOA YAKO

Kama unataka ndoa yako idumu, kuna tabia na mazoea kadhaa ambayo unatakiwa kuyaacha. Mazoea hayo hayatakuwa na manufaa kwa ndoa na uhusiano wako.

Yafuatayo ni mambo 5 ambayo unapoyafanya huiathiri vibaya ndoa yako:

1. KUTOKUWA MSIKILIZAJI

Wengi wetu huwa tunasikia, lakini huwa hatusikilizi. Kuna tofauti kati ya KUSIKIA na KUSIKILIZA. Mwenza wako anataka kusikika na unapokuwa humsikilizi, inaweza kumkasirisha. Jifunze kumpa umakini mwenza wako na uepuke kutokuwa msikilizaji. Wakati fulani hataki utatue tatizo lake, bali anataka umsikilize tu.

2. AHADI HEWA

Wazikumbuka ahadi zile ulizompatia mwenza wako mlipoanza uhusiano wenu? Watu wengi hupendelea kuzipuuza ahadi walizoziweka wanapokuwa wameshapata walichokitafuta na hilo linaweza kuwa na taathira mbaya kwenye ndoa au uhusiano wako.

3. MAWASILIANO DHAIFU

Mawasiliano yanapokuwa dhaifu katika ndoa yako, ndoa hiyo huathirika vibaya. Mlipoanza uhusiano wenu ulikuwa ukimpigia simu mara kwa mara, lakini siku hizi unapuuza simu ya mwenza wako. Tabia yako ya kutowasiliana na mwenza wako huathiri ndoa yako.

4. KUWA ‘BIZE’ KUPITA KIASI

Ukishindwa kutenga muda kwa ajili ya mwenza wako, ndoa yako itaathirika. Unapokuwa na muda wa kufanya kila kitu lakini ukakosa muda kwa ajili ya mwenza wako, unakuwa unaiharibu ndoa yako.

5. KUKOSA UKARIBU WA KIMAHABBA

Ukosefu wa ukaribu wa kimahabba huwa na taathira mbaya kwenye ndoa na uhusiano wako. Ninaposema ukaribu wa kimahabba, simaanishi tendo la ndoa tu. Unapokuwa huna utaratibu wa kumkumbatia, kumbusu, kumsifu, kumgusa na kumpapasa mwenza wako, ndoa yako inakuwa inaathirika na kudorora.🍫🍫🍫🍫🍫🍅🍅🍅🍅🍅🍅🍅🍅


DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni