Featured Post

LOVE BITE SEHEMU YA 10

LOVE BITE
SEHEMU YA 10
WHATSAPP 0655585220
ZANZIBAR
MWISHO
Safari ilianza huku kila mtu akiwa amenyamaza bila kuongea chochote. Jothan alishangaa kuona gari linaelekea mtaa aliokuwa anakaa yeye zamani kabla ya nyumba yake kuuzwa. Gari lilipiga honi kwenye geti la nyumba yake Jothan. Mlinzi alifungua mlango na Jothan hakuamini kuwa mmiliki wanyumba yake ni Prisca.
“siamini Prisca kama ni wewe ndio umeinunua nyumba hii?” aliongea Jothan baada ya kuingia kwenye nyumba ile ambayo haikubadilishwa kitu chochote zaidi ya rangi tu.
“siku zote huwa napenda kukuona ukiwa mwenye furaha. Ndio maana niliposikia nyumba hii inauzwa ndipo niliamua kuinunua kwa sababu sikupenda ipotee kwenye upeo wa macho yako. Sio nyumba tu, na kila kilichukuwa ndani pia nimevinunua. Hata gari lako pia ukilihitaji nitakupatia kwa sababu kwa sasa halipo hapa. Nimevinunua vitu vyote hivi kwa ajili yako Jothan.” Aliongea Prisca huku machozi yanamtoka. Jothan naye hakuweza kuyazuia machozi yake na kumfuata Prisca na kumkumbatia.
“moyo wa mtu ni kichaka Prisca, sikuweza kufikiria kama ipo siku Shani angeweza kuyabadili maisha yangu na kunifanya niwe hivi… nashukuru sana kwa yote uliyoyafanya kwa ajili yangu Prisca.”
Aliongea Jothan maneno yale na kumfanya Prisca azidi kulia.
“kesho nitachukua begi langu na kuondoka. Maana kazi yangu ya kukutafuta wewe nimeshaimaliza Jothan.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan ambaye wote walikuwa wanalia wakati huo.
“hapana, hutakiwi kuondoka Prisca. Na kama utaondoka basi hii numba na kila kitu kilichomo humu ndani bado vitakuwa havitoshi kutimiza furaha yangu bila ya wewe kuwa karibu yangu.” Aliongea Jothan huku analia.
“mimi sio chaguo lako Jothan, siwezi kukaa karibu na wewe. Nitakuwa naumia roho tu na sitaweza kuvumilia kukuona ukiwa na msichana mwengine mbele yangu.” Aliongea Prisca huku analia kwa uchungu.
“nilikosea kuchagua kwakua sikujua upi ni mchele ni zipi ni pumba. Niliacha mchele kwakua pumba zilinivutia angi yake. Leo najuta kwakua pumba zimenilaza njaa. Wewe ndio mchele wa kunifanya nishibe na kunitoa njaa hii ya kufa inayonikabili. Nakupenda sana Prisca.” Aliongea Jothan na kujikuta ameeanguka kwa magoti mbele ya Prisca ambaye wakati huo na yeye alikuwa haoni vizuri kutokana na ukungu wa machozi ulikuwa kwenye macho yake.
“toka siku uliyonikana Jothan kule Peacock hotel kuwa mimi sio chaguo lako. Moyo wangu uliingia ganzi na kuamua kuishi single Jothan. Sihitaji tena kupenda kwakua nina bahati mbaya ya kupenda nisipopendwa. Sipendi kuumizwa tena kwakua maumivu yake siwezi kuyastahimili. Nikuache tu na maisha yako na mimi naiche na maisha yangu” aliongea Prisca kwa uchungu maneno yalimchoma sana Jothan ambaye bado alikuwa analowanisha viatu vya Prisca kwa machozi yake pale chini.
“nisamehe mimi, nimeshajifunza Prisca,” aliendelea kuomba Jothan huku sauti iliyojaa uchungu ikiendelea kumtoka mtoto wa kiume.
Nguvu ya mapenzi inaweza kuhamisha milima, wahenga walisema hayo na mimi nawaunga mkono kwa kusadiki maneno hayo.
Prisca alijikuta anamnyanyua Jothan na kumkumbatia. Wote walilia sana na kila mmoja kwa muda wake alimbembeleza mwenzake kwa mumfariji.
Ukurasa mpya wa mapenzi kwa wapendanao hao walioanza mapenzi toka walipokuwa shuleni yalianza kwa kasi kubwa.
Hakukua na sababu ya kuchunguzana wala kupeana muda. Walikubaliana kupima ukimwi kabla ya kufanya mapenzi.
Zoezi hilo lilifanikiwa kwa asilimia mia moja. Wote walikuwa wazima na mipango ya ndoa ilifanyika haraka.
Vitu vyote vilivyokuwa kabatini alivikuta vile vile. Kasoro hati ya nyumba tu ambayo alirudishiwa na mpenzi wake Prisca.
Alifurahi sana na kwenda kupeleka cv zake kwenye kampuni ya Fast jet. Alipata kazi haraka na kuungana na rafiki yake kipenzi John.
Ndoa ya aina yake ilifungwa kati ya Jothan na Prisca. Wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walihudhuria harusi ile.
Kwenye Hight table walikwepo John na mkewe, Bahati na mumewe Saimon pamoja na mama yake.
Hakika furaha ambayo ilipotea kwa muda mrefu kwa Jothan ilirudi alifurahia uwepo wa watu hao muhimu katika maisha yake kwa vipindi tofauti..
Miezi saba baadae, Jothan na mkewe Prisca walikuwa wanatoka kwenye matembezi yao usiku wa saa sita.
Wailpofika msasani. Walilakuta wasichana wengi walikuwa wamejiremba na kuvaa nusu uchi wakiashiria kuwa walikuwa wanauza miili yao.
Jothan hakuamini kumuona Shani akiwa amejiingiza kwenye kundi hilo. Alisikitika sana kumuona Shani akikimbilia magari na kuanza kujinadi kama wafanyavyo mada wengine wanaojiuza hapo.
Alisimamisha gari lake na kumuangalia mkewe ambaye alimpa ishara ya kuondoka na kumuacha mwanamke huyo na maisha yake.
Walirudi nyumbani na kumshukuru Mungu kwa kuwaunganisha tena na kuyahesabu yote yaliyotokea nyuma ni mitihani tu, na wao ndio couple iliyokubaliwa na Mungu.
Maisha ni sahani iliyojaa mazuri na mabaya. Kuna wakati unaweza kukubali kuwa maisha ni jinsi unavyoishi. Ila wapo wanaoishi nje ya malengo waliojiwekea. Hakuna anayependa kupata hasara, ila kama una muamini Mungu basi utaamini kuwa kupata hasara katika jambo Fulani ni moja ya mitihani na huenda mungu amekuEpushia kitu Fulani katika jambo hilo.
Kila hatua unayopitia ni moja ya changamoto katika mafanikio yako.
Ukianguka jikaze na jaribu kuruka tena hata kama utasikia maumivu. Tochi ya mungu hummulkika kila mtu isipokuwa kwa atakayekataa mwenyewe. Ridhiki ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe ndio maana huwezi kuizuia.
Mungu ametoa vitu vitatu vikubwa kuliko Mali.
Kwanza Mungu katoa akili za kipekee. Nikisema akili za kipekee namaanisha kuwa kila mtu Mungu kampa akili lakini hawa wenye akili za kipekee huweza kufanya mambo makubwa na ya kushangaza hali ambayo mtu uliyepewa akili ya kawaida huwezi kufanya hata kama una pesa.
Pili Mungu katoa vipaji. Mtu mwenye kipaji Fulani basi huweza kufanya mambo makubwa ikiwemo kufikisha ujumbe haraka kwa watu kutokana na kukubalika na watu wengi zaidi ya mtu wa kawaida.
Kimfano matangazo, tangazo hilo akipewa mtu Fulani atangaze basi muitikio utakuwa mdogo kuliko akipewa tangazo hilo Diamond, Mrisho Mpoto na wengne wengi.
Kipaji ni kitu cha pekee alichotoa mungu kama zawadi kwa mtu Fulani na kama kitathaminika na yeye kukiwekea mkazo basi hiyo ndio inaweza kuwa njia ya mafanikio yake kupitia kipaji hicho.
Tatu mungu katoa Moyo wa pekee. Moyo huu amewapa watu wachache. Na cha ajabu kuwa mtu mwenye moyo wa kutoa basi hutoa kitu kikubwa bila kujali kubakiwa na kidogo. Humshinda mwenye mali ambaye akitoa hata kitu kidogo huhisi anapungukiwa.
Mtu mwenye moyo wa pekee hupenda kutenda mambo yanayompendeza mwenzake hata kama yanaweza kuharibu furaha yake. Hapendi kumuona mtu akilia au akihuzunika wakati yeye anaweza kumfanya mtu huyo kuwa na furaha hata kwa kumuongopea. Hawezi kula yeye kabla ya kuangalia wenzake wenye njaa. Hayo na mengine mengi kajaaliwa mtu mwenye moyo wa pekee.
Na huwashinda wenye vipaji na akili za pekee. Watu hawa mungu huwajaalia kwa kuendelea kuwapa na kutia Baraka mali zao hata kama ni kidogo.
Nia na madhumuni ni kujifunza kupitia burudani hii iliyowaacha watu kwenye majonzi au kufurahia mwisha mzuri wa Jothan kuwa na mtu ampendaye.
Asanteni sana frend mulionisapot mwanzo mpk mwisho
Kuwa wa kwanza kupata Hadith kali za kusikiliza na zakusoma njoo whatsApp 0655585220 karib
MWISHO

By Ahmad Mdowe
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni