JINSI YA KUPIKA ACHARI YA EMBE


ACHARI YA EMBE

MAHITAJI YA KUPIKA ACHARI YA EMBE


  • Embe 5 ndogo
  • Sukari robo
  • Hiliki chembe 6
  • Pilipili mtama chembe 10
  • Rangi ya chakula kiasi
  • Mji kikombe kimoja
  • vanilla kifuniko kimoja
HATUA ZA KUPIKA ACHARI YA EMBE

  1. Katakata embe saizi unayotaka weka juani kwa muda wa siku mbili mpk ikauke ziwe kavu, chukua sufuria weka maji ,sukari,hiliiki,pilipili mtama,rangi n'a vanilla weka jikoni ichemke mpk iwe nzito inate vidoleni weka embe zako changanya na mwiko mpk ikauke epua tandaza ktk sahani subir upoe andaa kwa kula 
  2. Mm napenda usiwe mkavu uwe laini km picha y'a kwanza unavyoiona nimetumia rangi ya orange nilikosa nyekundu hizo picha mbili kwa hisani ya mtandao ni vizuri kutumia rangi ya manjano na nyekundu huwa zinavutia snaa
  3. Sio lazima embe kuzimenya ila mm napenda za kumenya.huu ubuyu mtamu snaaa.

Chapisha Maoni

0 Maoni