JAMBO USILO LIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA | BongoLife

JAMBO USILO LIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA

SIMULIZI FUPI:
   Katika kijiji cha Mtakuja kulikuwapo na wasichana watatu na wote walikuwa ni warembo kwani kwa uzuri waliokuwa nao ulitosha kabisa kuwatetemesha na kuwatoa udenda wakware wote watakao waona hao warembo wamepita mbele yao .Uzuri hao mabinti walikuwa marafiki wa chanda na Pete kwani walipendana kuliko kawaida mpaka wakawashangaza watu katika kijiji hicho,kwa majina yao binti wa kwanza aliitwa Aisha ,wa pili aliitwa Manka na wa tatu aliitwa Jasmini. Sasa katika tembea tembea zao hapo mtaani siku moja,walikutana na kijana mmoja mtanashati na mpole akiwa anapishana nao njiani, mmmmh usema ukweli yule kijana aliwapasua moyo hao mabinti kwani wote walimwangalia mno kwa hisia nzito ,waliendelea kumtazama yule kijana mpaka alipotoweka kwenye mboni za macho yao.Yule kijana pasipo kujua kwamba anatazamwa kwa hisia nzito aliendelea na safari yake kama kawaida, Binti mmoja aliyeonekana kuwa mrembo kuliko wote ,Jasmini, ndiye aliyeonekana kutekwa zaidi na hisia za mapenzi kwa huyo kijana pasipo kujua hisia za wenzake zipoje Kuhusu huyo kijana handsome, Jasmini alilemewa na hisia nzito sana akiwa amekaa ,amelala au anakula,alimfikiria sana huyo kijana ikafikia kipindi akaonekana kana kwamba alikuwa akiumwa,alinyong'onyea sana akatamani angarau siku moja aone hata picha ya huyo kijana moyo wake ufarijike.

  Siku moja hisia zilimlemea akaamua kuwatoroka wenzake bila hata kuwaaga na kwenda kumsaka yule kijana popote pale alipo,alizunguka kila sehemu pale mtaani kama chizi huku njemba zingine zikiendelea kumwangalia huku zikimmezea mate,watu wengine walianza kujiuliza,huyu siye Jasmini shogae na akina Aisha na Manka? Mbona yuko peke yake wakati Mara nyingi tumezoea kumwona akiwa na wenzake, kipi kimemsibu huyu binti? Mbona anaonekana kama amechanganyikiwa vile mmh!! Makubwa!!. Jasmini aliwasikia yote waliyokuwa wakiyaongea lakini hakuwajali,duuh! Mapenzi bwana daah! Noma sana ,watu wanasema mwanamke akipenda amependa kweli sasa nimeelewa kupitia kwa Jasmini. Akiwa anatembea huku akiwa amekalibia uwanja wa mpira wa miguu lahaura Jasmini akamwona yule kijana akiwa amekaa peke yake akiangalia mpira huku akiwa hajui hili wala lile,Jasmini alipomuona akaachia tabasamu la furaha la chini chini akajipiga konde na kuamua kusogea hadi sehemu aliyokuwa amekaa huyo kijana, akajisogeza na kuketi karibu nae,kijana akiwa anaangalia mpira,Ghafla aliamua kuangalia pembeni yake mh! Hakuamini macho yake kama amekaa na binti mrembo kiasi hicho,Alijikaza kimya kimya na kujifanya na yeye kama anaangalia mpira huku akiibia ibia kumwangalia Jasmini, mood ya huyo kijana kuendelea kuangalia mpira iliyeyuka mara moja kutokana na uwepo wa Jasmini pembeni yake ,Jasmini na yeye kimya kimya aliendelea kumwangalia huyo kijana kwa kuibia.Wakiwa wanaendelea kutizamana kwa kuibiana mmh! si ghafla wakakutanisha macho yao, Jasmini akawa wa kwanza kuyakwepesha macho yake kwa aibu.
Kijana akaamua kutumia uanaume wake kuvunja ukimya akaanza kama hivi; samahani Dada ninaweza kukufahamu? Jasmini akaitikia bila samahani ,kwa jina Mimi naitwa Jasmini nakaa mtaa wa pili kutoka hapa,alijibu huku akiachia tabasamu nono lililozidi kumchanganya huyo kijana, kijana nae akaamua kujitambulisha,Mimi naitwa Kelvin au kwa kifupi unaweza niita Kelv,nakaa mtaa wa kwanza kutoka hapa,Jasmini akamjibu unajina zurii nimelipenda sana sana,akaendelea; kama hutojali Kelv ningependa tupeane mawasiliano hehehee!! Alijichekesha huku akijaribu kujiinamisha kwa Kelvin, haina shida Jasmini, baada ya hapo wakapeana mawasiliano na kuagana kila mmoja baada ya kumaliza kuangalia mpira.
 Jasmini alirudi nyumbani kwao huku akiwa na furaha ya ushindi katika jambo lililokuwa likimnyima usingizi siku baada ya siku.Usiku wa siku hiyo Jasmini hakuweza kupata usingizi kabisa, hivyo akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Kelvin usiku huo huo na mazungumzo yakawa hivi;

Jasmini: Haloo! Darling? Uko poa!
Kelvin: Niko fresh kabisa Jasmini!, nambie.
Jasmini: Nimekumis!! Sana Kelvin ama hakika wewe ni mwanaume pekee niliyetokea kukupenda katika maisha yangu na siwezi kuishi bila wewe Kelvin, wewe ndiye chaguo sahihi la moyo wangu Leo nimeamua kukukabidhi moyo wangu usiniumize mwenzio nitakufa .
  Kelvin kusikia hivyo alihisi kama yuko paradiso maana hata ile sauti tu ya Jasmini ilitosha kabisa kumtoa nyoka pangoni,ilikuwa ni sauti nyororo na laini .Kelvin akamjibu Jasmini hata Mimi nakupenda sana Jasmini tokea tuonane kule uwanjani nimetokea kukupenda, Waooo!! Umenifurahisha sana Kelvin wangu nitakupenda daima, ukifa na Mimi nakufa.Waliongea mengi sana mwishowe wakatakiana usiku mwema .
Asubuhi na mapema Jasmini aliamka na kwenda kuwaeleza mashoga zake Kuhusu ujio wa mpenzi wake,nao bila kinyongo wakamkubalia huku wakiwa na hamu kubwa ya kumuona shemela wao mtarajiwa.*Laiti kama angejua kuwa huyo anayemwita mpenzie anawindwa pia na shoga zake hao asingedhubutu hata kuwaambia*.Baada ya masaa mawili Kelvin alifika hapo nyumbani alipokuwa ameelekezwa na Jasmini na kuwakuta Jasmini pamoja na shoga zake wawili, Waooo!! Baby ,Jasmini alimkimbilia Kelvin na kumkumbatia huku akimmiminia busu za nguvu, mashavuni na mdomoni. Wakati hayo yakiendelea Aisha na Manka hawakuamini macho yao wakabaki wameshangaa huku wakiwa wamepigwa na butwaa maana walimkumbuka vilivyo huyo kijana handsome. Jasmini pamoja na Kelvin waliendelea kubaki wamekumbatiana wakiwa hawajui hili wala lile.

 Mapenzi kati ya Jasmini na Kelvin yaliendelea kuchanua siku hadi siku huku wivu wa mashoga zake Aisha na Manka ukizidi kuongezeka siku baada ya siku .Siku moja Jasmini akiwa kwa Kelvin yaani sehemu walipoamua kuyaanzia maisha yao mara baada ya kuwa pamoja,Aisha na Manka walipanga kitu kibaya cha kumkomesha Jasmini kwa usaliti wake zidi yao.Siku zikapita Jasmini na Kelvin wakiishi kwa furaha kama mke na mume .Siku moja Aisha pamoja na Manka waliamua kuwatembelea Jasmini pamoja na Kelvin kwa lengo la kuwasalimia.Walipofika nyumbani kwao bahati mbaya au nzuri walimkuta Kelvin peke yake akiwa amejipumzisha sebuleni huku pembeni yake akiwa ameweka kinywaji chake kwenye bilauri na kinywaji hicho kilikuwa ni maji ,wakati huo Jasmini yeye alikuwa ametoka kidogo kwenda kidogo kwenda kufanya mahemezi ya hapa na pale sokoni ,Basi Aisha pamoja na Manka wakafika pale....Manka akachungulia dirishani akamuona Kelvin amelala peke yake sebuleni huku pembeni yake kukiwa kuwewekwa bilauri ya maji iliyokuwa juu ya meza maana yeye alikuwa amejilaza juu ya sofa .Manka bila kupoteza muda alinyata mpaka kwenye bilauri hiyo alipoifikia akatoa kijikaratasi kimoja haraka haraka akachukua dawa kutoka kwenye hicho kijimfuko yenye rangi nyeupe mithili ya glucose akaiweka kwenye hayo maji ya Kelvin kisha akatikisa pole pole alipomaliza akaondoka, punde si punde Kelvin akashtuka usingizini na kuhisi kama ana kiu,maskini wa Mungu ! Kelvin akachukua bilauri ya maji akaamua kunywa pasipo kujua kama kuna adui aliingia na kuweka sumu kwenye maji hayo ,alipomaliza tu kunywa ghafla akahisi maumivu ya tumbo kama vile kuna kisu tumboni kinakata ,,Kelvin alianguka chini na kugaa gaa kisha akatulia kimya.Jasmini alirudi akiwa mwenye furaha ya kwenda kumpikia mumewe chakula kile akipendacho ,Mume wangu Leo utakipenda chakula nitakacho kupitia, Jasmini aliongea bila kujua nini kimempata mmewe Ghafla alipoingia sebuleni na kumkuta mpenzi wake amedondoka chini alimkimbilia na kwenda kumwangalia huku akiwa analia,Mme wangu,Mme wanguuuu!! My husband, amkaa uone nilicho hemea ,amkaa ! Umekufa Mme wangu, amka babaaaaa!! Usiniache peke yangu amkaaa!! My Darling!!, Jasmini hakuwa na chochote cha kufanya au kusaidia maana Kelvin tayari alikuwa ameaga dunia ,Alilia sana mwishowe na yeye akaamua kujiua.

FUNZO:

 Usimwamini kila umdhaniye kuwa ni rafiki yako wa dhati maana hujui uadui alio nao moyoni mwake akikuona umefanikiwa.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,156,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,13,biashara mtandaoni,3,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,209,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,118,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,229,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : JAMBO USILO LIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA
JAMBO USILO LIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/08/jambo-usilo-lijua-ni-kama-usiku-wa-giza.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/08/jambo-usilo-lijua-ni-kama-usiku-wa-giza.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content