Featured Post

I WILL BE BACK SEHEMU YA 13

I WILL BE BACK 13

Maelezo ya Joel yaliniacha kinywa wazi, kila kitu kilichokua kimefanyika kilifanyika kisomi, mipango yote ilifuata intelejensia kubwa sana haikua rahisi mtu wa kawaida kugundua chochote. Baada ya Joel kumaliza kuongea alimpisha James ambaye ndiye alikua kiongozi wa ile timu na mission nzima.                         
Kwa mara ya kwanza nilimuona James katika sura mpya, alikua makini sana hakucheka hata kidogo kama nilivyozoea kumuona siku zote. Zile smart tv zilifanya kazi, James alibofya kifute zikawaka zote zilizokuwemo mle ndani, maneno FBI yakaonekana kwenye kila tv.

“Our mission is to take down this son of bitch Abraham Odhiambo dead or alive”(mission yetu ni kumkamata Abraham Odhiambo akiwa mzima au amekufa) 

James aliongea kwa msisitizo, hakua na masihara hata kidogo, sauti yake ilipenya ngoma za masikio yetu mle ndani na kutuingia kisawasawa, wote tulimuelewa alichokua anakimaanisha.                                           

“It’s dangerous mission than we think he own more than 500 soldiers and we are only just 41”(ni mission hatari kuliko tunavyofikiria anamiliki wanajeshi zaidi ya 500 na sisi tupo 41 pekee)

James alizidi kutuambia lakini hadi muda huo mle ndani tulikuwepo watu 40 tu, Kama kiongozi mkuu James alitupa semina kidogo kuhusu ile mission itakavyokua, kupitia video games kwenye zile smart tukaona kila kitu kinavyotakiwa kufanyika kuanzia mwanzo hadi mwisho. Baada ya semina hiyo kumalizika, alisema tutakuwepo pale msituni Nakuru kwa muda wa wiki 2 kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na kuchukua mafunzo ya mwisho kwenda kuitekeleza ile mission ambayo kutokana na maelezo ya James ilikua mission ngumu na hatari sana. 

Sikua na undugu wala connection yoyote na nchi ya Marekani lakini kama ilivyokua imepangwa na mimi nilibaki msituni Nakuru kwa muda wa wiki 3. Tulifanya na kumaliza mazoezi ya oparesheni nzima pamoja na mafunzo ya kulenga shabaha kutoka kwa best snipers kwa ajili ya kufanya back-up pindi tutakapokua kwenye uwanja wa mapambano. Sikujua kwanini nilihusishwa kwenye ile mission lakini muda uliokua umebaki haukutosha kuuliza maswali ya kipuuzi, zaidi ya kusubiri na kujionea kila kitu kwa macho yangu.         
                                                                    
 Maandalizi na kila kitu kilikamilika kilichobaki ilikua ni kwenda kumkabili yule mwanaharamu Motemapembe. 
  
Ilikua siku ya Jumatano tulivu iliyojaa ukimya mkubwa, majira ya saa 12 na nusu jioni muda tulioianza safari yetu kwenda kuitekeleza mission nzito ya kumtafuta mwanaharamu Abraham Odhiambo, kirusi kilichocheza patapotea na kuingia choo cha kike kwa kulikorofisha na kulikasirisha taifa la Marekani, taifa lenye nguvu kuliko taifa lolote juu ya uso wa dunia hii.  

Tulitoka msituni Nakuru mpaka Mombasa kwa kutumia magari ya jeshi. Mombasa tuliweka kambi ya siku mbili kwenye uwanja wa ndege wa jeshi wakati tukisubiri ndege binafsi kutoka Marekani ije kutuchukua ilikua mission ya siri sana hivyo hatukutakiwa kutumia usafiri wowote wa public.
Kitu kikubwa nilichojifunza wenzetu wanafanya kila kitu kwa mipango, hawakurupuki hata kidogo, likipangwa kufanyika jambo fulani kwa njia moja mbili tatu hata liwe jambo dogo kiasi gani watafuata hivyo.       

 Pia wenzetu walijali sana muda mkikubaliana kitu fulani ni saa moja kamili basi kweli ni saa moja kamili hakuna samahani au bahati mbaya za kipumbavu kwa wenzetu.  
Ndani siku mbili ndege ya abiria Air bus C283 ilitua Mombasa. Bendera ya Marekani na chapa zote za ndege zilitoka zimefutwa hukohuko Marekani ili kuficha utambulisho wa ndege hio. Jambo lingine lililofanya tutumie ndege binafsi ilikua kukwepa usumbufu wa kukaguliwa mizigo uwanjani.  
Bila kupoteza muda tulipakia mizigo yetu, silaha, ma begi pamoja nyenzo zote zilizohitajika kwenye ile mission.  
 Air bus C283 ilikua na uwezo wa kubeba abiria 290 lakini umuhimu wa ile mission ulifanya watu 40 pekee tujiachie ndani yake tena bure kabisa. 
Air bus C283 iliiacha ardhi ya Mombasa ikakata mawingu kwa masaa kadhaa kisha tukaenda kutua uwanja wa ndege wa kijeshi uliopo Ukonga banana jijiji Dar es salaam.

Tulivyotua tu James alienda ofisi za jeshi uwanjani hapo, aka saini nyaraka kadhaa kisha akatumia simu ya ofisi hiyo kuongea na balozi wa Marekani nchini Tanzania. Haikupita muda magari kumi aina ya V8 yalikuja pale uwanjani yakatubeba sisi na mizigo yetu yote mpaka ofisi za balozi wa Marekani nchini Tanzania.   
                                              
Ubalozini tulipewa chumba kilichokua na kila kitu kama ilivyokua ile nyumba ya maajabu kule msituni Nakuru.
Hatukua na muda wa kupumzika tulivyoingia ndani ya kile chumba balozi wa Marekani aliingia kuongea na sisi, alitusisitiza sana kufanya juu chini kuhakikisha Abrahamu Odhiambo anakamatwa akiwa hai au amekufa.   
Baada ya maongezi alipiga video call kwa boss wake, raisi wa Marekani ambaye aliongea uso kwa uso na James huku na sisi tukishuhudia live.

“James you and your team you are doing this on behalf of American people if possible take him alive otherwise shoot him down” (James wewe na timu yako mnafanya hivi kwa niaba ya watu wa Marekani kama ikiwezekana mkamateni akiwa hai ikishindikana mmue) rais alisikika kupitia video call.

“Yes Mr. President I promise we will bring him alive” (Ndio Mr. President naahidi tutamleta akiwa hai)

“Thanks for your service. God bless you all God America” (Asante kwa huduma yenu. Mungu awabariki wote Mungu aibariki Marekani) Raisi alisema akapiga saluti nasi tukampigia kisha video call ikakata.

Kila kilichofanyika kiliniongezea motisha, kwangu kupigiwa na kumpigia saluti raisi wa Marekani au raisi wa dunia kwa uhalisia uliofichika lilikua jambo muhimu sana kwangu, nilijisikia fahari kuna kitu fulani kisichoelezeka kiliuvaa mwili wangu nikajiona nimekua mwepesi.    
Simu ilivyokatika balozi alirudi ofisini kwake bila kupoteza muda James alisogea mbele zaidi.

“1:00 am today we will start our mission we will go to Mr. Davis house and catch all bastard they will help us to find Abraham Odhiambo” (Saa 7 kamili usiku wa leo tutaanza mission yetu tutaenda nyumbani kwa Mr. Davis na kuwakamata wanaharamu wote watakao tusaidia kumpata Abraham Odhiambo) 

James alituambia kisha afungua ramani ya nyumba yangu kwenye ile smart tv tuliyoitumia kuongea na raisi muda mfupi uliopita. Nikiwa katika kujiuliza mahali alipoitoa hio ramani James akaanza kutuelekeza jinsi tutakavyoingia ndani ya nyumba yangu, tutakavyowatia nguvuni wafanyakazi na jinsi ya kutoka nje.                                             
Alipomaliza alifungua ramani nyingine ya msitu wa Magopande. Safari hii aliomba tumsikilize kwa makini zaidi alisisitiza lazima kila mtu aelewe kile alichokua anaenda kukiongea.

James alituonyesha ile ramani kwa kutumia pointer ya rimoti.
 Ulikua msitu wa Magopande mahali aliposadikika kuwepo Abraham Odhiambo pamoja na kundi lake lote la uhalifu.     
Kupitia ile ramani James alituelekeza jinsi ya kuingis ndani ya ule msitu, jinsi tutakavyo wakabiri wapiganaji wa Odhiambo. James alitusisitiza kua makini kuhakikisha tunamkamata Odhiambo akiwa mzima huku akituonya kua uzembe wowote unaweza kuyagharimu maisha yetu.
Kila tukio lilipangwa namna ya kufanyika kwa jinsi mambo yalivyopangiliwa hata kabla ya mapigano mtu ulikua ushaanza kusikia harufu ya ushindi.                                             
Baada ya maelezo yote, James aliniita pembeni mimi Joel na Slyvester, alitupa maelekezo yetu binafsi kua tutakapoivamia nyumba yangu sisi hatutaingia ndani kwangu bali tutamvamia Mzee Ambrosi na kumzimisha kwa dawa ya usingizi ili tutumie nyumba yake kupata shabaha nzuri za ki sniper wakati tukifanya back up.

Baada ya maelekezo yote kumalizika yule mzungu wa kike niliedhani ni mpenzi wake na Joel hapo awali alifungua mabegi na kumkabidhi kila mtu nguo za kuvaa wakati wa mission, alitupa dakika 20 kila mtu awe amezivaa ili aturuhusu kwenda kwenye chumba cha silaha.   
Dakika kumi na tano zilimtosha kila mmoja kuvaa zile nguo bila kupoteza muda tukaenda chumba cha silaha tulichokikuta humo hakielezeki kulikua na bunduki za kila aina, bastola, smg, sniper guns, mabomu ya machozi na ya kutupa kwa mkono, makombora tu ndio sikuyaona nadhani waliogopa kuwatisha Watanzania.

Saa saba kamili usiku ilifika. Tukiwa ndani ya mavazi maalumu ya kazi timu yetu nzima ya watu arobaini tuliianza mission yetu, tulitumia yale yake magari kwenda nyumbani kwangu maeneo ya mbezi beach.
Tulipokaribia kufika tulishuka tukapaki magari mbali mbali kwenye giza ili kuogopa kushtukiwa.     

James aliiongoza timu nzima alitugawanyisha makundi matatu, kundi langu nilikua mimi, Joel na Slyvester kazi yetu ilikua kuvamia nyumba ya jirani yangu Mzee Ambrosi na kumzimisha ili tuweze kuitumia nyumba yake kupata shabaha nzuri. 
Kwa kua tulikua watu w kutoa back up (msaada) kundi letu lilianza kutekeleza majukumu wengine waliizingira nyumba yangu lakini hawakufanya kitu walisubiri mpaka tukamilishe kazi yetu.                                                                                   

Kwa umakini mkubwa na kunyata kwa kujificha, mimi, Joel na Slyvester tulilifikia geti la Mzee Ambrosi. Ilikua usiku sana kupiga hodi kungewashtua wale wahalifu na Mzee Ambrosi mwenyewe, ili kuepusha kelele nilimpigia simu Mzee Ambrosi baada ya dakika kadhaa alipokea, nilimuomba radhi na kumuomba aje anifungulie geti maana nilikua nje.   
                 
Wema wake ulimponza Mzee Ambrosu alipofungua geti Joel alimziba pua zake na kitambaa chenye dawa ya usingizi bila ubishi Mzee Ambrosi alilala, tuliingia ndani tulifunga geti tukamkokota Mzee Ambrosi na kwenda kumlaza chumbani kwake. Msako mdogo ulifanyika tukawapata watu wanne, dada wa kazi na wanaume watatu nao bila kupoteza muda Joel akawazimisha na ile dawa ya usingizi.
Tulienda chumba kikubwa cha ghorofa ya juu, Joel alitumia kifaa maalumu kukata pazia na kioo cha dirisha usawa wa mdomo wa bunduki, alifunga silencer ili kuzuia mlio wa risasi kisha akautoa mdomo wa bunduki kwenye lile tundu dirishani. Kazi yetu ilikua tayari, Joel alimpa ishara Sylvester bila kuchelewa microphone ndogo sikioni kwa Slyvester ilifanya kazi yake.

“We are in position” (Tupo eneo husika) alimwambia James.          

          .…..ITAENDELEA…..
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni